Gustaf Lubon

quotes:
  • Hakuna tofauti kati ya Muarabu na Muajeni.
  • “Waislamu, hawaonani wageni vyovyote vile watakavyotofautiana mataifa yao, vivyo hivyo katika miji ya Waislamu (Daarul Islam) hakuna tofauti kati ya Mchina Muislamu na Muarabu Muislamu katika kufaidi haki zao. Kwa sababu haki za Kiislamu zinatofautiana na haki za wazungu (Ulaya) na hii ni tofauti ya msingi kabisa.”


  • Uislamu ni Mwepesi.
  • “Hakika wepesi mkubwa wa Uislamu unatokana na tawhidi halisi. Katika wepesi huu ndio kuna siri ya nguvu ya Uislamu. Uislamu na ufahamu wake ni mwepesi umeepukana na yale tunayo yaona katika dini nyingine na akili iliyosalimika inakataa migongano na utata. Hakuna kitu kilicho wazi zaidi kuliko misingi ya Uislamu inayoeleza uwepo wa Mungu mmoja na usawa wa wanadamu wote mbele ya Allah.”


  • Ustaarabu wa Elimu
  • “Kila tunapoangalia kwa kina ustaarabu wa Waarabu, vitabu vyao vya kielimu. Uvumbuzi wao, fani zao, inadhihiri kwetu ukweli mpya na upeo mpana. Na kwa haraka tumewaona Waarabu kuwa ndio watu bora katika karne za kati (Middle age) kuwa na maarifa kwa ajili ya elimu za waliotangulia. Kwa muda wa karne tano vyuo vikuu vya Magharibi (Ulaya) vilitegemea vyanzo vya elimu na machapisho ya Waarabu. Nao ndio ambao waliiendeleza Ulaya kwa akili na tabia njema. Historia haijawahi kufahamu Ummah uliozalisha kama walivyozalisha Waarabu (Waislamu) kwa muda mfupi na hakuna watu wengine waliowafikia katika uvumbuzi na fani zingine.”


  • Karne ya Kati
  • “Lau Musa bin Nasir angewafikisha kuichangua Ulaya; Basi angeifanya Ulaya nzima kuwa ni ya Kiislamu, na angeiokoa Ulaya (bila ya shaka) katika duru ya karne ya Kati ambayo Uhispania haikuweza kujua na kusimama ila kwa fadhila za Waarabu.”


  • Kunyoosha Nafsi
  • “Uislamu ni dini ambayo ina afikia na ugunduzi wa elimu, na kubwa katika hayo ni kuzinyoosha kuzipeleka kwenye Uadilifu, wema na kusameheana.”


  • Misingi ya Kimaadili
  • “Kwa hakika misingi ya kimaadili katika Uislamu ni ya juu kabisa, na kuwa maadili ya Ummah zingine, zilizofuata dini ile zilibadilika baada ya muda mfano wa mabadiliko yale ya wale waliofuata dini ya Issa.