Muujiza wa Milele

Muujiza wa Milele
“Kwa hakika miujiza ya Manabii waliomtangulia Muhammad katika uhalisia ilikuwa ni miujiza ya wakati maalumu. Ambapo tunaweza kuiita Qur-aan muujiza wa milele: kwani taathiria yake ni yenye kudumu na kuendelea. Ni rahisi kwa muumini katika zama na mahali popote kuona muujiza huu kwa kusoma tu katika kitabu cha Mwenyezi Mungu. Katika muujiza huu tunapata sababu ya kuenea kwa kasi kwa Uislamu. Kuenea ambako sababu yake wazungu hawaifahamu; kwa sababu hawajui Qur-aan, au ni kwa sababu hawaifahamu ila kupitia kwenye tafsiri ambazo hazinufaishi kwenye maisha achilia mbali kuwa si sahihi."


Tags: