Ananijua Kuliko Ninavyoijua Nafsi Yangu

Ananijua Kuliko Ninavyoijua Nafsi Yangu

“Qur-aan, kitabu hiki kitukufu kimeniteka kwa nguvu na kumiliki moyo wangu na kunifanya nijisalimishe kwa Allah, na Qur-aan humsukuma msomaji wake kwenye upeo wa mbali ambapo humtanguliza (kujiona) anasimama peke yake mbele ya Muumba wake. Ukiichukulia Qur-aan kwa umakini zaidi basi huwezi kusoma kwa urahisi, kwani hukubeba kama kwamba ina haki juu yako! Nayo inajadiliana nawe, kukukosoa na kushindana nawe. Nilikuwa katika kipande cha mwisho ikadhihirika wazi kuwa aliyeshusha Qur-aan ananijua kuliko ninavyojijua mwenyewe. Kwa hakika Qur-aan siku zote inanitangulia katika kufikiri kwangu, ilikuwa inajibu maswali yangu na kila usiku nilikuwa ninaweka maswali yangu na pingamizi zangu, hata hivyo nilikuwa napata majibu siku inayofuatia. Nimekabiliana na nafsi yangu uso kwa uso katika kurasa za Qur-aan.”


Tags: