VILINZI VYA NJIA YA FURAHA

VILINZI VYA NJIA YA FURAHA

VILINZI VYA NJIA YA FURAHA

Misingi ya Ustaarabu

Ustaarabu wa Kiislamu una vidhibiti bainifu na wasifu uliokuwa wazi ambao unatengeneza haiba ya mtu mkamilifu vidhibiti vyenye alama zenye kujitegemea na nyinginezo kwa misingi ya ustaarabu, malengo yake na misingi yake pamoja na kuwepo kiasi cha ushirikiano kati yake na tamaduni nyingine.

Misingi ya ustaarabu wa Kiislamu sio tu kutukuza akili kama ilivyokuwa kwa Wagiriki, wala kutukuza nguvu na utawala kama ilivyokuwa kwa Waroma, au kuupa umuhimu matamanio ya kiwiliwili na nguvu za kijeshi na siasa kama ilivyokuwa kwa wafursi au kujenga nguvu za kiroho kama walivyofanya Wahindu na baadhi ya Wachina au nguvu na utawala wa ‘watu wa dini’ pamoja na upotofu ambao ulipelekea kwenye kiza katika karne ya kati huko Ulaya.

Kadhalika sio kama ilivyo hivi sasa ambapo fitna ya sayansi na elimu na maada na kiasi binadamu kufaidika na silaha na hazina zilizokuwepo ulimwenguni kwa maada yenye kuangamiza kama tunavyoona leo hii katika mfumo wa ustaarabu huu uliorithiwa kutoka kwa Wagiriki na Warumi.

Ama misingi ya Ustaarabu wa Kiislamu una Tawhidi, kufikiri, elimu, matendo, roho, kujenga, kuheshimu akili na kuheshimu mwanadamu, yaani kwa vile inavyokusanya sehemu zote za maisha ya mwanadamu, na hili ndilo lililofanya Ustaarabu huu wa Kiislamu uwe unajitegemea kwa ukamilifu yenye desturi pana maalumu inatofautiana kwa tofauti kubwa na misingi ya staarabu nyinginezo.

Ustaarabu wa Kiislamu upo juu ya staarabu nyingine kwa kuwa na nguvu ya kiroho, kijihadi, kujitahidi, usawa, uadilifu, msamaha pamoja na wenye kutofautiana nao, na kadhalika kupenda kheri na kueneza sayansi ulimwenguni kote, na kwa hilo basi ustaarabu huu unapendekezwa kwa mara nyingine tena kuwaongoza wanadamu kwa hoja ya kumiliki vidhibiti hivi.

Uislamu unajipambanua kwa vipambanuzi vingi katika hivyo ni:

Ustaarabu wa imani na Tawhidi

$Gustaf_Lubon.jpg*

Gustaf Lubon

Mwanahistoria wa Kifaransa.
Karne ya Kati
“Lau Musa bin Nasir angewafikisha kuichangua Ulaya; Basi angeifanya Ulaya nzima kuwa ni ya Kiislamu, na angeiokoa Ulaya (bila ya shaka) katika duru ya karne ya Kati ambayo Uhispania haikuweza kujua na kusimama ila kwa fadhila za Waarabu.”

Imani inahesabiwa kuwa ni kiini cha njia ya furaha na linganio kubwa kwenye kutafuta elimu na kujenga ustaarabu, na kila ustaarabu ambao hautosimama katika imani ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na tawhidi yake ni ustaarabu wenye mgogoro ndani yake, wenye kupigana vita kati ya sehemu zake, baadhi yake kuangamiza zingine, ambapo huwafanya asiyekuwa Allah kwa miungu mingine kwa kutofautiana majina, ambayo hupelekea kwenye ufisadi wa maisha ya mwanadamu na uovu wake!! Allah amesema: “Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. Subahana ‘Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu, Bwana wa A’rshi (Kiti cha Enzi), na hayo wanayo yazua.” (21:22),

$Arnold_Toynbee.jpg*

Arnold J. Toynbee

Mwanahistoria Mwingereza.
Ushindi wa Mateka.
“Uislamu uliziteka nchi zilizoishinda katika vita vya msalaba na hivyo kuingiza fani mbali mbali na ustaarabu katika maisha ya ulimwengu wa Wakristo. Maisha ya walatini yalikuwa na kutu katika baadhi ya makonde ya harakati ya mwanadamu, kwa mfano kama vile uhandisi wa ujenzi. Athari za Uislamu ziliingia katika ulimwengu wa Kikristo muda wote wa karne ya kati. Ama Sicily na Andalusia (Hispania) athari ya ufalme mpya wa Waarabu ulidhihirika zaidi na kupanuka.”

Na akasema Aliyetukuka: “Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu.” (23:91)

Na Akasema tena Aliyetukuka, “Sema: Lau kuwa wangeli kuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi wangeli tafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi.” (17:42)

$K._LalGaba.jpg*

K. Lal Gaba

Mwanasiasa na Mwanahabari wa India.
Unaingia katika Maisha
“Uislam ndio dini bora kwa mwanadamu: Uislamu ndio ambao unaingia ndani ya maisha ya Muislamu katika vipengele vyake vyote, bali ndio kipambanuzi cha mwisho katika kila shughuli anayofanya Muislamu. Hakuna dini nyingine zaidi ya Uislamu ambayo ina uwezo wa kutatua matatizo yote ya watu katika Ulimwengu huu leo hii. Na huu ndio ubora pekee wa Uislamu.”

Na kinachoakisi haya ni kile kilichotokea na kinachoendelea kutokea sana katika tamaduni nyingine, na hivyo kupoteza malengo yake, na kupotoka kilichoelekezwa kwake; na hivyo kumpa mwanadamu uovu hata kama ilikusudia kumpa kheri, Allah amesema: “Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipo kuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo” (9:31).

Ustaarabu wa Ulimwengu

Uislamu ni dini ya ulimwengu, imekuja iwe ni kwa zama na mahali pote na kwa kila lugha na watu wote, kwa kila rangi na taifa, Allah Aliyetukuka amesema: “Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui.” (34:28),

$William_Montgomery_Watt.jpg*

W. Montgomery Watt

Mustashrik wa Uingereza.
Yuko wapi Kiongozi Afaae?
“Akipatikana kiongozi anayefaa ambaye atazungumza maneno yanayofaa kuhusu Uislamu. Basi kuna uwezekano wa dini hii kuibuka tena kama ni moja ya nguvu kubwa za msingi za kisiasa ulimwenguni kwa mara nyingine.”

Na Allah akasema: “Ametukuka aliye teremsha Furqani kwa mja wake, ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote.” (25:1),

Na akasema tena: “Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi….” (7:158)

Na akasema tena Aliyetukuka, “Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” (21:107).

Hivyo basi Uislamu ukaja na itikadi thabiti ambayo haibadiliki kwa kubadilika hali, na sheria iliyosimama kwa misingi ya uadilifu, haki na kheri inayowiana na tabia ya mwanadamu katika kila zama na mahali na sababu yake ni kuwa inatoka kwa Allah ambae hufahamu yenye kufaa viumbe vyake, Allah amesema: “Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari? ” (67:14),

Kama ambavyo Uislamu sio dini mahususi kwa kundi au rangi au taifa maalumu la watu, Uislamu ni kwa ajili ya weupe, weusi, watu wa manjano, wekundu, nayo ni kwa ajili ya zama zilizopita na zama zilizopo na zama zijazo, wala mtafiti vyovyote atakavyopewa uwezo mkubwa wa kielimu hataona aliyokuja nayo Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) hisia yoyote ya kimajimbo, au ya kikundi au kitabaka, na hiyo ni alama ya wazi kuwa Da’wah yake ni ya Kilimwengu haitegemei kwa kundi maalumu au taifa maalumu; kwani ibada za Kiislamu, sheria zake, hukumu zake, tabia zake zote zinafaa kwa watu wote katika zama zote;

$The_Gospel_of_arnabas.jpg*

Injili ya Mathayo

“Akajibu, akasema, “Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea katika nyumba ya Israeli.” Na alipowachaguwa watu kumi na wawili ili wakawalinganie mayahudi aliwausia: “Hao Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, katika njia ya mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Na katika kuenda kwenu, hubirini mkisema, Ufalme wa mbingu umekaribia.”

hivyo basi haiwezekani kusema kuwa uadilifu au tabia njema haifai watu fulani au zama fulani, na hili ni maalumu kwa Uislamu.

Ama katika baadhi ya dini zile hisia za kimajimbo au za kitaifa au za kujuana zipo wazi sana; kwa mfano Mayahudi wanapoamiliana na wasio katika dini yao Mwenyezi Mungu anawaelezea: “Na miongoni mwa Watu wa Kitabu yupo ambaye ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurudishia, na miongoni mwao yupo ambaye ukimpa amana ya dinari moja hakurudishii isipo kuwa ukimsimamia kumdai. Haya ni kwa kuwa wakisema: Hatuna lawama kwa ajili ya hawa wasio jua kusoma. Na wanamzulia uwongo Mwenyezi Mungu, hali nao wanajua.” (3:75).

Ustaarabu wa elimu na kujenga

$Sir_Charles_Edward_Archibald.jpg*

Sir Charles Edward Archibald.

Mwanasiasa wa Uingereza.
Kujenga na Kuimarisha
“Uislamu unatambua kuimarisha vipaji; uzamifu na upembuzi binafsi: ni dini ya kujenga na kuimarisha na sio dini ya kubomoa. Kama kwa mfano mtu anamiliki ardhi na yeye kwa upande mwingine ana utajiri ambao hataki kulima ardhi ile na akaiacha tupu, baada ya muda fulani ardhi ile itahamia katika ardhi za Ummah katika hali ya kawaida. Sheria ya Kiislamu inathibitisha kuwa miliki ya ardhi hiyo itahamia katika mkono wa mtu wa kwanza ambae atalima ardhi ile.”

Mtazamo wa Uislamu kwa mwanadamu ni kuwa Allah amemuumba kwa ajili ya Ukhalifa na kuimarisha Ulimwengu, Allah amesema: “…Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo….” (11:61),

Na akasema Aliyetukuka: “Yeye ndiye aliye kufanyeni manaibu katika ardhi. Na anaye kufuru, basi kufuru yake ni juu yake; na kufuru za makafiri haziwazidishii kwa Mola wao Mlezi ila kuchukiwa. Wala kufuru za makafiri haziwazidishii ila khasara.” (35:39),

$Gustaf_Lubon.jpg*

Gustof Lubon

Mwanahistoria Mfaransa.
Kunyoosha Nafsi
“Uislamu ni dini ambayo ina afikiana na ugunduzi wa elimu, na kubwa katika hayo ni kuzinyoosha kuzipeleka kwenye Uadilifu, wema na kusameheana.”

Hivyo ndani ya dini ya Kiislamu watu hupata dhambi watakapoacha elimu yoyote inayomfaidisha mwanadamu na kuimarisha ulimwengu, wakati ambapo Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ametumwa wakati watu wakiishi katika shimo la ujima wa ustaarabu na elimu, na watu kushughulishwa na falsafa, majadiliano kinyume na kujenga, kutenda na kuimarisha ardhi; hivyo Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) akawanyanyua wanadamu kwa dini ya Uislamu, dini ya Ustaarabu na dini ya kujenga bila ya kuwepo mgongano kati yake na kuimarisha ardhi, na kati yake na kunawirisha roho, hivyo hamna migongano ndani ya nafsi ya Muislamu baina ya ibada na matendo, na kuimarisha ardhi na kati yake na maisha ya kiroho na kutenda katika kumridhisha Mola wake, yote hayo ni kwa ajili ya Allah na katika njia yake, Allah Aliyetukuka amesema: “Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.” (6:162).

Ustaarabu wa Kimaadili

$Abdullah_Herilal_Gandhi.jpg*

Abdullah Harlal Ghandi,

Mtoto wa Mahatma Ghandi
Juu ya Vichwa vya Mashahidi.
“Nyote mnafahamu kuwa mimi ni “Heral” mtoto wa kiongozi mkubwa wa Kipagani, “Ghandi”. Mimi natangaza mbele ya vichwa vya mashahidi na katikati ya kundi kubwa hili la Waislamu kuwa mimi nimeupenda Uislamu, nimeipenda Qur-aan na nimemuamini Allah Peke Yake na Mtume wake mtukufu Sayidina Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na kuwa yeye ni Mtume wa mwisho na kuwa hakuna nabii baada yake na Qur-aan ilichokileta ni haki na vitabu vyote viliyoteremshwa ni haki. Mitume na manabii wote ni haki. Na kwa Uislamu na Qur-aan nitaishi na kufa kwa ajili yake na nitautetea na kupigana kwa ajili yake na nitakuwa moja ya nguzo yake imara na nitaulingania kati ya jamaa na ndugu zangu. Dini hii tukufu ni dini ya elimu, utamaduni, uadilifu, uaminifu, rehama na usawa.”

Tabia njema katika Uislamu ni ibada, bali Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ametujulisha kuwa lengo la kutumwa kwake ni kukamilisha Matukufu ya maadili; amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Nimetumwa kukamilisha matukufu ya tabia.” (Imepokewa na Malik), hivyo basi njia ya ustaarabu na furaha ni njia ya kimaadili inahimiza matukufu ya tabia na matendo mema, na maadili katika Uislamu ni mpana katika nyanya zote za maisha, mfano wa mtu kuamiliana na nafsi yake pamoja na Allah na wengine, kama inavyokusanya muamala wa Muislamu pamoja na kafiri na pamoja na mdogo na mkubwa na mwanamume na mwanamke na mtu na mtesi wake.

Hivyo basi Uislamu ukaamrisha ukarimu, ushujaa, na uadilifu, rehema na huruma, kutojikweza, adabu njema katika miamala na watu, ukweli, haya, uvumilivu, amani ya moyo na kupenda kheri na yasiyokuwa hayo, Allah Aliyetukuka ameelezea umuhimu na wajibu wa kufanya uadilifu hata ikiwa ni mtu na mtesi wake: “Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” (5:8),

Na akasema kuhusu ujumbe wa Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na kubainisha kuwa yeye ni rehema kwa walimwengu wote na sio mahsusi kwa waliomuamini peke yake tu, Allah aliyetukuka amesema: “Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” (21:107),

Tabia hizi ni sehemu muhimu katika ustaarabu wa Kiislamu na nguzo yake ya asili, ndani yake, wala haiwezekani kupotea tabia njema kwa Muislamu kwa sababu yoyote ile kwa ajili ya kujenga ulimwengu huu au kwa ajili ya maslahi yoyote au yasiokuwa hayo, Allah amemtengeneza Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na kumpa adabu ili awe mfano katika adabu na maadili na kigezo chema katika kila kitu, Allah amesema: “Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana” (33:21),

Na Allah akaelezea sehemu ya rehema yake na pupa yake katika kuwaongoza watu kwenye uongofu katika njia ya furaha, Allah Aliyetukuka amesema: “Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma.” (9:128).

Ustaarabu wa akili na tafakuri

Katika dini ya Uislamu hakuna ukahanuti (siri zinazotawaliwa na makuhani na watu wa dini) ambao huwezi kuuliza au siri ambayo hauwezi kuzingatia, bali Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ameamrisha kufikiria katika aya zake, katika viumbe na katika Ummah mbali mbali, Allah Aliyetukuka amesema: “Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma.” (3:191),

Na Allah Aliyetukuka akasema tena: “…Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri.” (10:24),

Na Allah Aliyetukuka akasema: “Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri.” (16:44),

Na akasema Aliyetukuka: “ Je! Hawajifikirii nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake ila kwa Haki na kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukataa kuwa watakutana na Mola wao Mlezi.” (30:8)

Na akasema tena Aliyetukuka, “…Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri.” (59:21),

Bali Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ametufundisha kuwa elimu sio dhana peke yake bali hapana budi elimu hiyo iwe na dalili inayosimamia, Allah Aliyetukuka amesema: “…Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli” (2:111)

Hivyo hakuna siri anayoifahamu mtu au kuhani au kiongozi wa dini ambaye hatoi siri hiyo kwa mtu.

Ustaarabu wa amani ndani ya mtu na nje yake

$Harun_Mustafa_Lyon.jpg*

Profesa Haroon Mustapha Lion

Mwanazuoni wa Mambo ya Lugha huko Uingereza.
Akili na Mantiki
“Katika vivutio vya Uislamu ni kuwa kwake dini inayosimama kwa kutumia akili. Haumtaki kamwe mfuasi wake kufuta kipaji hiki alichopewa na Mungu. Kama ambavyo Uislamu unapenda utafiti na kuulizia mambo. Kadhalika inalingania wafuasi wake katika kusoma na kufanya utafiti, uchunguzi na kuangalia kabla ya imani. Uislamu unaunga mkono hekima isemayo: Thibitisha ukweli wa kila jambo kisha shikamana na kheri. Hili si jambo geni: Kwani hekima ni jambo lililompotea muumini popote alipatapo basi ni mwenye haki nayo zaidi. Uislamu ni dini ya matumizi ya akili na mantiki: Hivyo basi tunakuta kuwa neno la kwanza lililoshuka kwa Nabii Muhammad ni: “Soma”, kama ambavyo tunaiona kauli mbiu ya Uislamu ni kulingania katika kuangalia na kutafakari kabla ya kuamini: Kwani Uislamu ni haki na silaha yake ni elimu, na adui yake mkubwa ni ujinga.”

Amani ya ndani ina maanisha furaha ya ndani ya mwanadamu na kuokoka kwake na migongano ya ndani ambayo huwakumba watu wengi katika ustaarabu wa kisasa; kiasi cha kuwa dunia na akhera zikaishi katika fikra ya amani ya mwanadamu na hivyo ibada na matendo na ujenzi wa ardhi kuishi pamoja, roho na mada, elimu na dini, hakika amani ya ndani katika ustaarabu wa Uislamu ni alama ya wazi inayotokana na tawhidi ambayo inakusanya yote yaliyotangulia katika nafsi ya muumini kwa wepesi na urahisi.

Katika Uislamu dunia si lengo katika dhati yake, bali ni shamba la akhera, mapito na kivuko cha kuelekea huko, na hili lipo wazi katika kauli yake Allah Aliyetukuka: “Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.” (28:77);

$William_Montgomery_Watt.jpg*

W. Montgomery Watt

Mustashrik wa Kiingereza.
Suluhisho la Kiakili
“Qur-aan imeleta suluhisho la kiakili la matatizo ya zama hizi za Kiuchumi, kijamii na kimaadili: Kwa hili haiwezikani kutia shaka katika ile hekima ya Qur-aan kwa kuangalia mafanikio ya Muhammad katika kufikisha ujumbe ambao Mungu amemuarisha kuufikisha. Hivyo yapasa kwetu (kwa mtazamo wangu) kadiri ya misimamo yetu ya dini ilivyo kuzingatia ujumbe wa Qur-aan tangu kuchimbuka kwake huko Makkah.”

Na, “Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa” (62:10);

Yaani utakapomaliza Swala basi uende kwenye kazi zako za kidunia madamu ni halali na utafute kwenye kazi hizo ikhilasi, ukitarajia radhi za Allah; kama Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alivyomwambia mmoja wa sahaba zake: “Na wewe hutotoa matumizi yoyote ukitarajia nayo radhi za Allah isipokuwa utalipwa ujira hata kile ambacho utakiingiza katika mdomo wa mke wako.” (Imepokewa na Malik); Yaani katika mdomo wa mke wako unapata ujira, katika dini yetu hakuna kutenganisha kati ya dunia na akhera lakini kwa sharti ya kutoshughulishwa na dunia na kuacha akhera, kama alivyosema Allah Aliyetukuka: “Enyi mlio amini! Yasikusahaulisheni mali yenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio walio khasiri” (63:9)

Na akasema vile vile: “Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe….” (28:77),

Hivyo basi mapenzi ya matendo, mapenzi ya mke, kucheza na watoto na kuwajali, na mengine katika mipaka ya kisheria katika dini ni miongoni mwa uongofu wa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) iwapo kutakusudiwa radhi za Allah, Allah amesema: “Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.” (6:162),

Kwa hiyo maisha yote ni kwa ajili ya Allah, hata kile ambacho ndani yake kuna hadhi ya nafsi basi hicho ni kwa ajili ya kumtii Allah Aliyetakasika na kutukuka madamu nia imenyooka.

$Ignaz Goldziher.jpg*

Ignaz Goldziher

Mustashrik wa Kiyahudi.
Maisha Mazuri
“Ikiwa tunataka kuwa waadilifu kuhusu Uislamu ni juu yetu kukubali kuwa katika mafundisho yake kunapatikana nguvu hii ambayo inawezekana ikawa maisha mazuri na haswa katika upande wa kimaadili. Mafundisho haya yanatakia rehema kwa viumbe vyote vya Mungu, na uaminifu katika mahusiano ya watu wenyewe kwa wenyewe, kadhalika mapenzi na ikhlasi na kuzuia silika zenye kuipelekea kwenye matamanio kama ambayo inavyowatakia mambo mengine mazuri. Matokeo ya mambo yote haya ni kuwa Muislamu mwema anaishi maisha yenye uzalishaji mwingi kwa kadiri maadili yanavyohitajia.”

Amani ya nje pamoja na watu wa karibu na wa mbali, mwenye kuafikiana nae na mwenye kutofautiana nae, bali salamu ya kwanza anayomsalimia mtu nduguye ni kauli yake kwa nduguye; Amani juu yenu na rehema za Allah na baraka zake, watu hawakufurahi na kuhifadhika kwenye dini zote kama walivyofurahi katika utawala wa Uislamu; ni kiasi gani ulimwengu ulivyopata hasara kwa kuanguka kwa baadhi yaWaislamu, Allah amesema: “…Wala kuwachukia watu kwa kuwa wali-kuzuilieni kufika Msikiti mtakatifu kusikupelekeeni kuwafanyia uadui. Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu..” (5:2).

Ustaarabu safi na mapenzi

Ustaarabu wa Kiislamu unawajibisha Waislamu kuwa watu wenye nyoyo zilizosalimika na nafsi zilizo safi, amesema Allah Aliyetukuka kuhusu kisa cha dua ya Waumini: “Na walio kuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu.” (59:10)

$Will_Durant.jpg*

Will Durant

Mwandishi wa Kimarekani.
Maadili ya Watu
“Kwa hakika Waislamu kama wanavyojulikana ni watu waliokamilika zaidi kuliko Wakristo: Walikuwa ni watu wenye kulinda ahadi zaidi, wenye kuwahurumia zaidi wanaowashinda. Na makosa machache sana waliyofanya katika historia yao kuliko unyama waliofanya Wakristo walipotawala Qudsi mwaka 1099.

Na, “Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana. Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi.” (26:88-89),

Na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) akasema: “Msibughudhiane wala msihusudiane na kuweni waja wa Allah ni ndugu, haiwi halali Muislamu kumuhama nduguye zaidi ya siku tatu, hukutana huyu akampa mgongo huyu na mbora wao ni yule anayeanza kutoa salamu.” (Imepokewa na Muslim).

Na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) akasema huku akihimiza mapenzi na kuzoeana: “Naapa kwa ambae nafsi yangu ipo mikononi mwake, hamtoingia peponi hadi muamini, na hamtoamini hadi mpendane, Je, nikujulisheni kitakachothibitisha hilo kwa ajili yenu? Enezeni salamu.” (Imepokewa na Tirmidhi).

Wakati fulani Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) aliulizwa: ni mtu yupi bora? Akasema: Kila mwenye moyo Makhmum, mkweli wa ulimi, wakasema: Mkweli wa ulimi tunamjua, basi ni nani Makhmumul-Qalbi? Akasema: “Huyo ni mcha-Mungu msafi, hakuna dhambi, wala uovu, wala kuvuka mipaka, wala husuda.” (Imepokewa na Ibn Majah).

Ustaarabu wa kiroho na maada

Ustaarabu wa Kiislamu umekuja kung’arisha roho za watu, na wakati huo huo haujasahau mada wala kuipuuuza, Allah amemuumba mwanadamu katika mada na roho, na kumpa sababu zote za maisha katika pande zake za kimada na kiroho; akatayarishia mwili mazingira yenye kufaa kuishi nayo katika uso wa ardhi, kadhalika Allah Aliyetukuka akaitayarishia chakula cha roho kutokana na wahyi wa mbinguni ambao Allah amemteremshia mwanadamu kupitia Mitume yake, Allah Aliyetukuka amesema: “Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia.” (15:28-29),

$Dale_Carnegie.jpg*

Dale Carnegie

Mwandishi wa Kimarekani
Starehe ya Kiroho.
“Kinachonishughulisha mimi sasa hivi ni ninachokipata katika neema za dini. Kama vile ambavyo ninajali neema tunayopata kutokana na umeme, chakula bora na maji safi. Haya yote hutusaidia kuishi maisha mazuri yenye neema. Ama dini hunipa mengi zaidi ya haya. Hunipa raha starehe ya kiroho, au hunipa (kama aliyozungumza William James) msukumo wa nguvu wenye kuunganisha maisha. Maisha yenye nafasi, yenye furaha maridhawa, kwa hakika inanipa imani, matarajio na ujasiri na huniondolea khofu, sononeko na wasiwasi. Vile vile hunielekeza kwenye malengo katika maisha na hukunjua mbele yangu upeo wa furaha na kunisaidia katika kujenga chemchem ya maji na rutuba katikati ya jangwa la maisha yetu.”

Hivyo basi roho na kiwiliwili ni vitu viwili vyenye kulazimiana kimoja hakitoki kwa mwenzake ila kwa mauti ya mtu.

Roho na kiwiliwili kila kimoja kina mahitaji na matakwa yake; kiwiliwili kinaishi kwa kula, kunywa na kuvaa hata kama kutakuwa na mapungufu upande mmoja utaona athari ya upande mwingine, kama mtu atakuwa amefanya mapungufu katika chakula chake utamkuta kuwa ni dhaifu anayeangamia hawezi kuishi maisha yenye utulivu na mazuri, vivyo hivyo kwenye kunywa na kuvaa.

$NassrySalhab.jpg*

Nassry Salhab

Mwanafasihi wa Kilebanoni
Ukubwa wa Uislamu
“Uislamu hauhitaji kalamu zetu kwa ufasaha wowote ule kalamu zetu zitakaoufikia. Lakini kalamu zetu zinauhitajia Uislamu, kwa yale ambayo Uislamu unayo kama vile utajiri wa kiroho na kimaadili kutoka kwenye Qur-aan yake nzuri ambayo kwake tunaweza kujifunza mengi.”

Kwa hakika upungufu wa matakwa yoyote katika kiwiliwili hiki kinaakisi yote katika maisha yake, hawezi kuishi vizuri wala kusaidia upande wake wa pili (kiroho) katika maisha ya utulivu.

Hali kadhalika roho ina matakwa yake, roho haiishi bila mapenzi kutoa, wala kujitolea basi vipi roho itaishi bila mola inayemuabudu, kumpenda, kumtarajia, kumuogopa na kumkimbilia? Vipi roho itaishi ikiwa kifua kitupu haipati inayomtegemea na kutulia kwake, au haipati amani, kutoa na kusalimika moyo na mahaba baina ya watu?!

Ama kwa hakika mwanadamu akifanya mapungufu katika kuipa roho haja zake basi yeye ni kama aliyefanya mapungufu katika chakula chake na kinywaji chake, mwanadamu atatulia vipi, vipi hali yake itakuwa na utulivu na nusu yake ya pili hulalama na jeraha?! Kwa bahati mbaya ustaarabu wa Kimagharibi umesahau furaha ya roho na ndio maana ikawa na huzuni katika maisha haya ya dunia wakati ambapo yeye yupo katika kilele cha maisha mazuri, Ustaarabu wa kisasa ni ustaarabu uliopambazuka kwa kuhudumia kiwiliwili na Mada lakini umesahau au kujisahaulisha kiwiliwili bila ya roho ambayo haina furaha wala mafanikio wala utulivu, bali sio ustaarabu wa kweli.

Ustaarabu unaomjali mwanadamu na haki zake

Limekuwa ni jambo maarufu kuwa utekelezaji wa haki za mwanadamu kuhesabiwa kuwa ni kigezo cha kujua kiasi ambacho nchi husika inazingatia misingi ya uadilifu, usawa, kulinda haki za wananchi wake na uhuru wao.

$Leopold_Weiss.jpg*

Leopold Weiss

Mwanafikra wa Austria.
Aibu ipo Ndani Yetu
“Yapasa kuwa wazi kwetu kuwa Waislamu kupuuzia mambo (na sio upungufu katika mafundisho ya Uislamu) Hiyo ndio ambalo limesababisha matatizo tuliyonayo leo hii.”

Kama ambavyo huzingatiwa kuwa ni kipimo cha ufahamu na mwamko wa wananchi kuneemeka na haki na uhuru wao, bali ni kipengele muhimu sana katika mifumo ya Kidemokrasia ambayo ni kulinda haki za wanadamu.

Katika Ustaarabu wa Kiislamu imejaa mifano mingi na ya kipekee katika uhalisia kuhusu haki za binadamu, nayo ndio ukubwa na utukufu wa ustaarabu huu wa Kiislamu, na kuwa sio maneno matupu tu au alama au kauli mbiu tu.

Mambo yenye kupambanua haki za binadamu katika Uislamu ni haya yafuatayo:

1-Chanzo cha haki hizi zimejengwa katika msingi kuwa ubwana na utawala ni wa Allah Aliyetukuka, Allah Ta’ala amesema: “…Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu. Yeye anasimulia yaliyo kweli; naye ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote.” (6:57).

Hivyo basi sheria ya Kiislamu kuhusu haki huangaliwa kwa mtazamo wa kiiungu kwa kiumbe huyu, na yale yenye kumfaa.

2-Kuthibiti: Haibadiliki kwa kubadilika wakati na kubadilika mazingira na hali.

3-Kuchunga haki kulingana na msimamo wa hisani: Haki katika Uislamu zinaibuka kutokana na kisimamo ambacho ndani yake mja anakuwa chini ya kumuogopa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), nacho ni kisimamo cha hisani (wema) ambacho Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ameielezea: “Kumuabudu Allah kana kwamba unamuona, na kama humuoni yeye anakuona.” (Muslim).

$Cat_Stevens.jpg*

Cat Stevens

Mwimbaji wa Uingereza.
Amani ya Ulimwengu.
“Taarifa ya Qur-aan kuhusu Muumba wa Ulimwengu ilinitingisha: Nimeufahamu Uislamu kupitia Qur-aan, na sio katika matendo ya Waislamu. Enyi Waislamu kuweni Waislamu wa kweli ili Uislamu uweze kuenea ulimwengu. Kwani huo ni amani kwa ulimwengu wote.”

4-Kuchanganyika na ukamilifu kati ya haki za binadamu na tabia ya dini hii:

Kwa hiyo Uislamu haukuacha haki hivi hivi tu, bali imezitengenezea mazingira ya hukumu za kisheria na katika mtazamo wa makusudio ya kisheria, na ikazilinganisha na adabu na maadili yake, na ikafanya kuharibu adabu zile ni kuharibu haki hizi, na mwishowe ni kuziunganisha na dini, na kuzingatia vyanzo vyake vya kiungu, na hivyo basi huhesabiwa kuwa ni majukumu ya Muislamu binafsi, na sio haki hivi hivi tu, hivyo basi kujenga haki katika Uislamu ni kujenga kwa ukamilifu wenye kulandana na tabia ya kiungu ya dini hii.

5-Utawala wa mtu binafsi katika jamii ya kiislamu ndio msingi wa haki za binadamu katika Uislamu, na sio kinyume chake kama hali ilivyo katika sheria za wanadamu, Allah Aliyetukuka amesema: “Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.” (5:32).

5-Uislamu kutangulia katika haki za binadamu kabla ya wengine.

Kwa hiyo haki hizi ambazo Uislamu umedhamini kwa mwanadamu hazikuja katika mapambano ya kifikra au ya kimapinduzi na matakwa yake kama ilivyo katika historia ya haki za binadamu katika mfumo wa kidemokrasia na sababu za kuanza kwake, kama vile ilivyokuwa hali ya Ufaransa na Marekani na kwingineko, bali (haki hizi ambazo Uislamu umezidhamini) misingi yake imetulia na hukumu zake kwa Wahyi kutoka kwa Allah Aliyetukuka bila kuwepo mazungumzo yake kabla ya hapo au kuyafuatilia au mapambano ya kufikia njia yake.

6-Kuwa inafuata hali halisi na inaungana na maisha, hugusa haja ya mwanadamu; kinyume na haki katika sheria za kigeni –ambazo zimewekwa na kupambwa katika hali ya kifalsafa zaidi.

7-Kuna sheria ambazo ni za Uislamu peke yake, miongoni mwa haki hizo muhimu ni: haki za wazazi wawili, haki za ndugu kwa watoto, haki za jamaa wenye ndugu, haki ya kichanga tumboni, haki ya mtu kupata malezi ya kidini na ya kidunia, haki ya chumo halali, makatazo ya riba, haki ya kulingania katika kheri, kuamrisha mema na kukataza maovu.

8-Suluhisho la Uislamu kuhusu kadhia za haki za binadamu inasimama katika asili ya utu wa mwanadamu na kuchochea hisia ya imani kwa Allah Aliyetukuka, kinyume na sheria zingine. Haki hizi zinaegemea katika ufahamu wa kuwa ulimwengu huu umedhalilishwa na Allah Aliyetukuka kwa maslahi ya binadamu kulingana na kanuni za kimaumbile. Historia ya mwanadamu haikuwa kushuhudia ustaarabu ambao umetekeleza haki za mwanadamu pasipo maslahi (ya watawala), vinginevyo tunaona kwa wepesi nembo zinazotolewa na wito mwingi na kunyanyuliwa kwa mabango, lakini ni ugumu ulioje kugundua hakika zilizojificha nyuma yake na nia zilizo funikwa nyuma yake pindi wale viongozi wake wanapokuwa chini ya viwango vya utata….

$MarmadukePickthall.jpg*

Marmaduke Pickthal

Mwandishi wa Uingereza.
Ulimwengu Mtupu
“Inawezekana Waislamu wakasambaza ustaarabu wao katika ulimwengu kwa haraka ile ile ambayo walioisambaza hapo kabla: Kwani ulimwengu huu mtupu hauwezi kuthubutu mbele ya Roho ya Ustaarabu wao.”

Pamoja na ustaarabu huu kuwaenea wanadamu kwa kutumwa kwake, ila ni kuwa baadhi ya watu wanaweza kujiuliza-kuhusu sababu za kurudi nyuma Waislamu na kuwa kwao katika hali waliyonayo leo hii pamoja na maendeleo haya ya Ustaarabu wa Kiislamu?!

Hata hivyo kushangazwa huku kunaondoka tukifahamu hali ya Waislamu leo hii haiwakilishi ukweli wa dini yao, wengi wao wamerudi nyuma pindi walipoacha misingi ya dini yao na yaliyokuja kwenye kitabu chao na katika Sunnah ya Mtume wao (Swala Llahu ‘alayhi wasallam), vinginevyo dunia isingefahamu ustaarabu uliofurahisha walimwengu wote kuliko ustaarabu wa Kiislamu, inatosha kusoma historia na kusikiliza kauli za waadilifu hata wasiokuwa Waislamu ili tuone ni kwanini ulimwengu umepata hasara kwa kuparaganyika Waislamu?!