NJIA YA USTAARABU

NJIA YA USTAARABU

NJIA YA USTAARABU

Tofauti kati ya Thaqafa na Ustaarabu

$H._G._Wells.jpg*

H. G. Wells

Mwandishi
Mfumo Bora
“Uislamu ulifanikiwa: Kwa sababu ulikuwa ni mfumo bora wa Kijamii na kisiasa ambao siku ziliweza kuutanguliza (mbele). Nao ulisambaa. Kwa sababu kila ulipokwenda ulikumbana na mataifa yaliyokuwa nyuma kisiasa. Mataifa ambayo yalikuwa yakinyang’anya raia zake, yakidhulumu na yakiwahofisha wala hayakusoma wala kuwa na utaratibu wowote, vile vile ulikuta serikali hizo zina ubinafsi na ugonjwa hazina uhusiano baina yake na watu wake. Hivyo Uislamu ukabaki ndio fikra safi zaidi ya kisiasa na utendaji mzuri ulimwenguni hadi muda ule ulikuwa ukiwatumikia watu kwa mfumo bora kuliko nidhamu yoyote nyingine. Ama mfumo wa Kibepari ulikuwa ukiwafanya watu kuwa ni watumwa katika ufalme wa Roma. Elimu, fasihi na taratibu na ada na kijamii huko Ulaya zilikwisha anguka kabla ya Uislamu kuibuka.”

Hakuna umma, kundi, taifa iwe ni la kijima au la kisasa, ambalo litakuwa na utamaduni ambao unawaunganisha na kuwapa tabia pambanuzi, utamaduni ni njia katika kuishi, ni sehemu ya maisha na uwepo, ni mfumo wa maadili na kijamii ambayo yanahukumu mandhari ya maisha na vipengele vyake vyote, hili linaakisiwa katika mambo ya nguvu na tabia zote na kuipa jamii kitambulisho chake na kuhifadhi mshikamano wake.

Ustaarabu wa Uislamu kumkirimu mwanadamu

Ama ustaarabu huu ni wasifu wa ziada wa uwepo kwa utamaduni wa kijamii ambao unabeba maana ya maendeleo, na kupanda (kuendelea) kwa pande zote mbili ya aina na idadi, na hivyo kupata mafanikio katika uhalisia wa mambo, ni hatua inayoonekana katika athari ya mazingira katika historia yenye uwezo wa kutengeneza matukio yake na kuyaelekeza, harakati zinaweza kufikia kiasi cha kutengeneza bonde linatotenganisha zama na mahali.

Na hivi ndivyo ambavyo ustaarabu unavyowakilisha hakuna mfano wake katika tabia na mazingira, siasa na dini, utamaduni na sayansi na Akhlaqi, vipengele vyote hivi tunaviona vikitoka katika chombo kimoja nacho ni ustaarabu wa watu hawa au wale kwa tabia zao za kipekee.

Uislamu umefanikiwa kubadilisha nafsi za kundi la mwanzo lililoamini kutoka katika maisha ya kibedui ambayo ilikuwa yakitawaliwa na kasumba na kuwa nyuma na kuwafanya kupambika kwa tabia tukufu na kwa muda mfupi maendeleo na ustaarabu ukasambaa duniani na watu wengi wakaitikia kwenye ustaarabu huu wakati ule kwa wepesi wa dini aliyobashiriwa nayo Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam), uadilifu, udugu na usawa, ustaarabu huu ulikuja wakati ambapo binadamu alikuwa amekwisha choshwa na mfumo wa zamani uliosimamishwa kutokana na utumwa na udikteta, kwa hiyo wakaukumbatia mfumo mpya ambao ndani yake waliona utukufu na utu wao baada ya kuonja dhulma na ukandamizaji chini ya wafalme, makuhani na utawala wa kidikteta wa mtu mmoja.

$William_Montgomery_Watt.jpg*

W. Montgomery Watt

Mustashrik wa Uingereza.
Miongoni mwa Alama za Kughurika.
“Hakika ni wakati muafaka kufanya utafiti kuhusu athari za Kiislamu juu ya Ulaya kwa wakati huu ambapo uhusiano kati ya Waislamu na Wakristo Waarabu pamoja na Wazungu wa Ulaya unaongezeka katika ulimwengu huu mmoja. Kwani imewahi kuonekana wakati fulani kabla katika karne za kati waandishi Wakristo wa Ulaya walitengeneza sura chafu kuhusu Uislamu katika maeneo mengi: Hata hivyo kwa fadhila za jaribio la watafiti katika karne iliyopita sura sahihi zaidi ya kuangalia mambo kwa mtazamo usio na upendeleo imeanza kutengenezwa katika akili za watu wa Magharibi: Na kwa sababu ya kuwepo mahusiano mzuri na Waarabu na Waislamu basi ni juu yetu kutambua fadhila zote tulizofanyiwa na Waislamu. Ama jaribio letu la kukana hayo ni alama miongoni mwa alama za uongo za kudanganyika.”

Kwa hiyo Uislamu ukawa ndio fursa yao ya dhahabu, kwani Uislamu huo ulitengeneza mambo yao mengi na ndani yake wakaona maisha matukufu ambayo walikuwa wakiyatamani, na wakati huo huo ikawaondoshea dhuluma, ujinga na ujima.

Ustaarabu wa Kiislamu umeheshimu mtazamo wa binadamu; haukuwahi kumtofautisha hata siku moja kati ya mtu na nduguye, kwa misingi ya ubaguzi wa rangi au lugha, bali umewapa wote muamala mmoja na haki sawa kwa wote, na hivyo Ustaarabu ukachangia maendeleo ya wanadamu baada ya kubadilisha mfumo wa kikabila ambao unasimama katika uhusiano wa damu na nasaba kuelekea katika mfumo wa kundi unaoshirikiana katika itikadi na fikra ambayo inasimama katika mashirikiano ya kijamii kwa misingi ya udugu na usawa.

$MarmadukePickthall.jpg*

Marmaduke Picthall

Mwanafasihi na Mwanafikra Mwingereza
Kuanguka kwa Ulimwengu.
“Magharibi kwa sasa wana haja ya Uislamu kuliko muda wowote uliopita ili kuyapa maisha maana na historia makusudio yake, hadi Wamagharibi waweze kubadili tabia yao ya kutenganisha kati ya elimu na imani. Uislamu hauweki kizuizi kati ya elimu na imani, bali kinyume chake unaunganisha baina yake kwa kuzingatia kuwa hicho ni kitu kimoja kisichowezakugawanyika. Kama ambavyo inawezekana kwa Uislamu kurejesha uhai wa matarajio ya jamii yetu mpya iliyoathirika na upweke (ubinafsi) wa njia ambayo inaupeleka ulimwengu kwa ujumla wake kuanguka.”

Lengo la kwanza la Ustaarabu kwa mtazamo wa Uislamu ni kufanikisha utulivu, usalama na amani na kusimamisha jamii bora na kuwafurahisha wanadamu katika yaliyokuwa ya kheri, kadhalika kupiga vita matendo yote ya shari; ambapo maendeleo yote, ustaarabu na tamaduni zote lengo lake sio ustaarabu wenyewe kwani malengo halisi ya ustaarabu sahihi ni kufikia katika furaha ndani ya nafsi ya mwanadamu na utulivu katika moyo wake na kwenda pamoja katika kufikia amani na maendeleo ya jamii pamoja na mataifa, na hilo kupitia kufikia katika yaliyokuwa ya kheri na yenye manufaa na kuwa mbali na kila yaliyokuwa ya shari na yenye kudhuru

$Prince_Charles.jpg*

Prince Charles

Mwanamfalme wa Uingereza
Mafanikio ya Kielimu
“Uislamu umepata mafanikio makubwa ya kielimu zaidi ya karne nane: Hivyo basi ni makosa kudhania kuwa Uislamu ni kunakili Ustaarabu tu. Au kuwa ustaarabu mpya ni wa Magharibi kwa vile umekamilika. Uislamu una fadhila kubwa katika kuweka kanuni za awali ambazo zimepelekea mafanikio hayo.”

ambayo ni kinyume na ustaarabu wa kisasa ambayo umemuongezea mwanadamu khofu na wasi wasi na kumswaga mwanadamu katika upotofu wa kimaada unaoangamiza na kuwa mbali na tabia njema, fadhila na dini na mfano wake katika thamani za utu wa mwanadamu, hali ambayo (kwa ustaarabu mambo leo) umemfanya mwadamu kuwa ni chombo (mashine) kisichokuwa na roho ambayo mwenye nguvu humsaga mnyonge.