UISLAMU NA ELIMU

UISLAMU NA ELIMU

UISLAMU NA ELIMU

Uislamu ni dini ya elimu na maarifa

Hapana shaka kuwa Njia ya Furaha hapana budi kupita katika njia za elimu na ustaarabu, haiwezekani kwa hali yoyote kupita katika mabonde ya ujinga, na haipatikani dini wala fikra ambayo imenyanyua hadhi ya wanazuoni na kuheshimu miamala yao na kuhimiza kutafuta elimu na kuitumia akili na kulingania katika mazingatio na kufikiria kama mfano wa dini ya Uislamu aliokuja nao Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ambae alijenga ustaarabu mkubwa ulioenea mashariki ya ardhi na magharibi yake.

Kwa hali hiyo kutumwa kwake Swala Llahu ‘alayhi wasallam kunahesabiwa kuwa ni mapinduzi ya kweli ya kielimu katika mazingira ambayo roho ya kielimu imeyazoea, Kwa hiyo Uislamu ukaja ili elimu ianze, na dunia ing’are kwa nuru ya uongofu wa Mwenyezi Mungu, Akasema Aliyetukuka: “Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” (5:50).

Hakuna nafasi ya ujinga kwenye dini hii au dhana au shaka, aya ya kwanza kushuka kwa Nabii Umiyyi (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.” (96:1-5).

Ikawa wazi kuwa maudhui ya kwanza ni ufunguo wa kufahamu dini hii, na ni ufunguo wa kufahamu dunia hii, bali kufahamu akhera ambayo ni marejeo ya watu wote.

Nafasi ya elimu katika Qur-aan na Sunna

$RobertJoseph.jpg*

Robert Pierre Joseph

Profesa wa Falsafa katika Vyuo Vikuu vya Ufaransa.
Soma… Huu Ndio Mwito wa Uislamu
“Hapana shaka kuwa Uislamu (ambayo ni dini ya elimu na maarifa) inawalingania wenye kuikumbatia katika kutafuta elimu na kuitumia, wala hakuna ajabu katika hilo. Kwani Ayah ya mwanzo katika Qur-aan Tukufu ni kauli yake Allah Ta’ala: “Soma kwa jina la Mola wako Aliyeumba.”

Atakayeangalia jinsi Qur-aan ilivyojali kadhia ya elimu haimdhihirikii katika mazingatio ya mwanzo kuteremshwa kwake tu, lakini ilikuwa tokea kuumbwa kwa mwanadamu mwenyewe, kama Qur-aan yenyewe ilivyolieleza hilo katika aya zake; Allah amemuumba Adam na kumfanya khalifa katika ardhi, akaamuru Malaika kumsujudia, akamkirimu na kumtukuza na kumnyanyua, kisha akatutajia sisi na Malaika sababu ya heshima, utukufu na kunyanyuliwa huku; akaainisha kuwa ni elimu Allah, Aliyetukuka amesema: “Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua. Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli. Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima. Akasema: Ewe Adam! Waambie majina yake. Basi alipo waambia majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani, na ninayajua mnayo yadhihirisha na mliyo kuwa mnayaficha?” (2:30-33).

Kinachoashiria umuhimu wa elimu na thamani yake katika Uislamu ni kuwa si tu kuwa tokea mwanzo katika Qur-aan imezungumzia masuala ya elimu katika kauli yake Allah “Soma”

$Stanly_Lane-Pool.jpg*

Stanley Lane-Poole

Mwanazuoni wa Uingereza.
Msikiti…Chuo Kikuu
“Ndivyo misikiti ilivyokuwa hapo kabla (hata leo hii baadhi yake) imekuwa ni vyuo vikuu vya Kiislamu: Ni mshangao mkubwa kwa wanafunzi waliojawa na hamu katika elimu. Wanafunzi ambao wamekuja kusikiliza mihadhara ya wanazuoni katika elimu za dini, sheria, falsafa, tiba na hesabu. Na kwa hakika wanazuoni wenyewe wamekuja kutoka pande zote za Ulimwengu ambao walikuwa wakizungumza lugha ya Kiarabu, nao walikuwa wakimkaribisha kila mwanafunzi bila kujali utaifa wake.”

bali huu ndio mfumo uliothibiti katika katiba hii ya milele, hivyo hakuna sura yoyote miongoni mwa sura zake zenye kuzungumzia elimu, iwe ni kwa njia ya moja kwa moja au isiwe ya moja kwa moja, Allah ameamrisha elimu katika jambo kubwa lenye kushuhudiwa nalo ni kumpwekesha Allah Aliyetukuka; katika kauli yake Allah Ta’ala: “Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa.” (47:19),

Kwa hiyo ikaonyesha juu ya ukubwa wa ubora wa elimu na watu wake, imekana kulinganisha kati ya mwenye kujua na asiye jua: “…Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili.”(39:9).

Bali Allah amewanyanyua ambao wamepewa elimu daraja la juu duniani, mbali na thawabu huko akhera. Allah amesema: “…Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” (58:11),

Ikutoshe kuwa haipatikani katika Qur-aan kusisitizwa juu ya kuomba ziada ya kitu chochote isipokuwa katika elimu, Allah amesema: “…Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu.” (20:114),

Wala haikuwa amri ni kwenye mlango wa kuzidisha pindi Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) aliposema: “Atakayefuata njia ya kutafuta elimu Mwenyezi Mungu atamrahisishia njia ya peponi, na kuwa Malaika wanaweka mbawa zao kwa kuridhia mtafuta elimu, na kuwa mtafuta elimu wanamuombea msamaha waliomo mbinguni na ardhini, hata nyangumi baharini, na kuwa ubora wa mwanazuoni juu ya mshika ibada (mwenye kuabudu) ni kama ubora wa mwezi kwa sayari nyinginezo, kwa hakika wanazuoni ni warithi wa Mitume, kwani Mitume hawarithiwi dinari wala dirhamu bali hurithiwa elimu, kwa hiyo atakayeichukua amechukue hadhi kubwa.” (Muslim). Na hivyo basi baada ya kutumilizwa kwake misikiti ikawa ndio kasri ya elimu na wanazuoni.

$Maurice_Bucaille.jpg*

Maurice Buccaile

Mwanazuoni na tabibu wa Kifaransa.
Qur-aan na Sayansi
“Qur-aan imekusanya ndani aya bainifu katika elimu ya mazingira (sayansi) zilizotolewa na Pro Yusuf Marwa katika kitabu chake, “Sayansi katika Qur-aan.” Na ikafikia aya mia saba na sabini na nne. Na maelezo yake ni kama ifuatavyo: Hesabu aya sitini na moja, Fizikia aya mia mbili na sitini na nne, atom aya tano, Kemia aya ishirini na tisa, Vipimo vya mwendo aya sitini na mbili. Hali ya hewa aya ishirini, maji aya kumi na nne, elimu ya anga aya kumi na moja, elimu ya wanyama aya kumi na mbili, kilimo aya ishirini na moja, elimu ya viumbe hai aya thelathini na sita, Jiografia aya sabini na tatu, elimu ya nasaba za watu aya kumi, elimu ya tabaka za ardhi aya ishirini na elimu kuhusu ulimwengu na historia ya matukio yake aya thelathini na sita.”

Jambo kubwa la kushtua ni pale utakapohesabu idadi ya neno “Elimu-‘Ilmu” na vitoheo vyake tofauti vilivyokuja kwenye kitabu cha Allah; unapata idadi yake kufikia mara mia saba na sabini na tisa (779); kwa wastani wa mara saba kwa kila sura ya Qur-aan! Hii ni kuhusu neno elimu, hata hivyo kuna maneno mengi yenye kuashiria maana ya elimu lakini hayakutajwa kwa tamko lenyewe; mfano: Yakini, uongofu, akili, kufikiri, kuangalia, hekima, fiqhi (kujua), Burhani, dalili, hoja, aya (alama) ubainifu na mengineyo yasiyokuwa hayo katika maana yanayotokana na elimu na kuhimiza elimu yenyewe, ama sunnah ya Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kuhesabu neno hili ni vigumu kwa wingi wa ilivyoelezwa.

Wanadamu kuendelea kwa ajili ya Uislamu

Qur-aan sio kitabu cha Physics, Chemistry, Biology au hesabu, bali ni kitabu cha Uongofu pamoja na hayo haukusaza chochote kulichothibitishwa na sayansi ya kisasa.

Hayo yalikuwa na athari kubwa katika dola ya Kiislamu baada ya hapo; kwani kulikuwepo na harakati kubwa kabisa za kielimu katika nyanja zote za elimu na mataifa, harakati na nguvu ambazo hazijawahi kuwepo mfano wake katika historia; jambo ambalo lilifanya ustaarabu na maendeleo makubwa kufikiwa katika mikono ya wanazuoni wa Kiislamu, na kumpa urithi binadamu kwa silaha nzuri za elimu ambayo dunia nzima inadaiwa na Uislamu.

MarxMarhaaf anasema: “Maendeleo ya Chemistry Ulaya yanarejewa kwa Jabir bin Hayyan moja kwa moja, na dalili kubwa ya hilo ni kuwa Istilahi nyingi alizozigundua bado hutumika katika lugha mbali mbali za Ulaya.”

Ama Aldo Mieli anasema: “Na tukihamia katika elimu ya sayari (astronomy), tokea mwanzo tutawaona wanazuoni wa sampuli ya kwanza, na miongoni mwa wanazuoni hao maarufu ni Abu Abdullah Muhammad bin Musa Al-Khawarizmy.

$Stanly_Lane-Pool.jpg*

Stanley Lane-Poole

Mustashrik wa Uingereza.
Mapenzi ya kuelimika.
“Haikuwahi kutokea katika Historia ya maendeleo Ulimwenguni harakati yenye kufurahisha kuliko mapenzi ya ghafla ya utamaduni. Kama ilivyotokea katika sehemu zote za ulimwengu wa Kiislamu: Ikawa kila Muislamu kwa khalifa kuwa ni msanii (mtengenezaji) kama kwamba ghafla tu amekumbwa na shauku ya elimu na kiu ya safari (kutafuta elimu). Haya yakawa ni mambo ya kheri Uislamu ulioyaleta kutoka pande zote. Wanafunzi walisongamana katika vituo kama vile Baghdad. Na baada ya hapo katika vituo vingine ambavyo vilikuwa ni mbeleko ya adabu na elimu, mfano wake ni harakati mpya za wanazuoni wa ulaya ambao walifurika katika vyuo vikuu kuchukua elimu mpya. Bali kwa hakika lilikuwa ni jambo zuri.”

Al- Khawarizmy alikuwa ndie mfunguzi wa mnyororo wa wanazuoni wakubwa wa mahesabu, na vitabu vyake viliendelea kusomeshwa katika vyuo vikuu vya Ulaya hadi karne ya kumi na sita.”

Zaghrid Honka amesema katika juzuu maalumu kuhusu operesheni katika kitabu: “Ubainifu kwa aliyeshindwa kutunga.” Cha mwandishi: Az-Zahrawy; (sehemu ya tatu ya kitabu hiki kimekuwa na nafasi muhimu sana Ulaya ambapo paliwekwa misingi ya operesheni Ulaya, tawi hili la tiba likawa lipo kileleni, hivyo masuala ya operesheniyakawa yanajitegemea katika misingi yake katika elimu za upasuaji.”

Kitabu cha Az-Zahrawy kilikuwa na athari kubwa katika kuinyanyua Ulaya kwa muda wa karne tano, ambapo kilikuwa kikifundishiwa katika vyuo vikuu vya Ulaya, kama ambavyo wapasuaji wengi wa Ulaya wakidondoa humo na kuchukua.

Bado wanazuoni wa Kiislamu waliendelea kutoa michango yao kwa wanadamu wote; Ahmad Zuwayl anasema: katika kitabu chake, Zama za Elimu: (kazi yangu kubwa ilikuwa ikiangukia kwenye sehemu maalum katika moyo wa atoms, ambapo kuna kukutana na kuna kuachana kwa vitu katika milango ya fahamu, kama ambavyo muda ulivyo ndani ya sekunde; ambapo sekunde huwa ni muda mkubwa.”

$Gustaf_Lubon.jpg*

Gustaf Lubon

Mwanahistoria wa Ufaransa
Ustaarabu wa Elimu
“Kila tunapoangalia kwa kina ustaarabu wa Waarabu, vitabu vyao vya kielimu. Uvumbuzi wao, fani zao, inadhihiri kwetu ukweli mpya na upeo mpana. Na kwa haraka tumewaona Waarabu kuwa ndio watu bora katika karne za kati (Middle age) kuwa na maarifa kwa ajili ya elimu za waliotangulia. Kwa muda wa karne tano vyuo vikuu vya Magharibi (Ulaya) vilitegemea vyanzo vya elimu na machapisho ya Waarabu. Nao ndio ambao waliiendeleza Ulaya kwa akili na tabia njema. Historia haijawahi kufahamu Ummah uliozalisha kama walivyozalisha Waarabu (Waislamu) kwa muda mfupi na hakuna watu wengine waliowafikia katika uvumbuzi na fani zingine.”

Wala hakuna ubishi kuwa elimu hii, uongofu, na nuru aliyokuja nayo Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) imemtoa mwanadamu kutoka katika makutano ya maji ya Asina (yaliyobadilika rangi), hivyo akainyanyua kwa elimu, ustaarabu na utamaduni kwa muda wote wa historia.

Njia ya Uislamu ni njia ya elimu

Uislamu ukaja kwa mfumo wa kielimu na kisayansi, kwa mfano Uislamu unahadharisha kuiga kibubusa bila kutumia akili; anasema Subhaanahu kuhusu washirikina: “…wao husema: Bali tutafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka?” (2:170),

Na kufuata dhana bila kufuata mfumo wa kielimu; Allah Aliyetukuka amesema: “…Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu.” (6:116)

Na kuhusu matamanio ambayo yanakwenda kinyume na elimu, mantiki, akili na utafiti; Allah amesema: “…Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao bila ya kuwa na ilimu….” (6:119),

Na kuhusu bughudha na chuki ambayo inamuweka mtu mbali na uadilifu amesema: “…Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” (5:8),

$Rene_Guenon.jpg*

Rene Guenon

Mwanafalsafa wa Kifaransa.
Qur-aan ni Miujiza
“Kwa hakika nimefuatilia aya zote za Qur-aan ambazo zina uhusiano na sayansi na mazingira nikazikuta kwamba aya hizi zinakubaliana na elimu zetu mpya. Nimeyakinisha kuwa Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi Wasallam) amekuja na ukweli ulio wazi kabla ya miaka elfu moja, na kabla ya kuwepo mwalimu yoyote miongoni mwa wanadamu. Lau kila mwenye elimu au fani angelinganisha vizuri aya zote za Qur-aan zinazohusiana na alichokisoma, kama nilivyolinganisha bila shaka angetii Qur-aan, ikiwa ana akili ameepukana na hisia za chuki.”

Na kuhusu uwazi wa usio na upendeleo kuhusu elimu; Allah Ta’ala amesema kuhusu Mayahudi: “Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake, na husema: Tumesikia na tumeasi…” (4:46)

Na kuhusu kutofanya dhuluma na uharibifu amesema Aliyetukuka: “Bali lawama ipo kwa wale wanao wadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika nchi bila ya haki. Hao watapata adhabu iliyo chungu.” (42:42)

Na kuhusu amana ya kielimu pamoja na uadilifu baina ya watu; amesema: “…Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu….” (4:58),

Na uadilifu, unyoofu na kushuhudia haki; Amesema: “Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu…” (4:135),

Ama kuhusu umuhimu wa utafiti wa dalili na hoja amesema: “Sema Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli.” (27:64):

Na mengi yasiyokuwa hayo yenye kujenga na kutengeneza mfumo wa kisomi kwa njia ya sayansi na ustaarabu.