WIZI

WIZI

WIZI

(1)

Kakhi mimi nimejiandaa kwa safari..nataka ujue kuwa kadhia ni ya maadili na sio kadhia ya maslahi.

Vizuri ..lakini nina sharti!

Sharti ? sharti gani hilo?

Watumie barua idarani kuhusu kughairi kwako kuacha kazi, na kuwa upo tayari kwa safari?

Kwa nini?

Ili umalize zogo ulilolianzisha.

Vizuri, hakuna tatizo, lini safari?

Katika muda wa karibu zaidi na kwa kadiri tiketi itakavyopatikana, lakini kwenda wapi?

Tunakubaliana, nitasafiri kuelekea Misri.

Unavyoonesha bado unatafuta njia bora ya maisha! Muda sio mrefu atakuja mkurugenzi wa mahusiano na tiketi ya safari, ili uende kwa furaha yako.

Asante.

Joji aliondoka ofisini kwake, na hazikupita dakika kumi alifika mkurugenzi mkuu wa mahusiano…
Nimekukatia tiketi ya kuondoka kesho kutwa kwenda Misri, je ni sawa kwako?
Haraka yote ya nini?
Sijui, hayo ni matakwa ya Kakhi, kwa ujumla nimefurahishwa na taarifa, kwa vile wewe utaendelea kazi na sisi.

Na nani aliyesema kinyume na hayo?

Habari iliyoenea kwa nguvu kwa wafanyakazi ni kwamba Kakhi anataka kukuachisha kazi.

Niliogopa, ama kwa sasa sijui kama kuna mtu mwingine ataachishwa, basi mimi ndie nitakaye muachisha yeye, asante kwa hisia zako.

Na Kakhi akaniambia nikukumbuke kwa email.

Amekuwa ananiogopa mimi, nitamtumia email anayotaka baada ya muda mchache.

Utatumiwa kabrasha zote pamoja na maelezo kwa email yako leo, kwani hazijatayarishwa bado, kwani tumeshtukizwa na taarifa.

Nazisubiri… Nakushukuru.

Wasia wangu kwako kama rafiki: kuwa makini sana na Kakh ama kwa upande wa kazi yangu mimi nimekufikishia, naomba idhini.

Asante sana, niamini, kwamba misingi na maadili ya tabia zinashinda ujanja na hadaa.

Joji alishika simu yake na kuwasiliana na Adam ili kumjulisha safari yake..

Hallo, nimeshakata tiketi ya kwenda nchini kwenu ewe Mmisri.

Hongera sana, hii ni habari ya kufurahisha, nitamweleza Sheikh Baasim ili amwambie kaka yake akupokee, na ndugu yake anaongea Kiingereza na sio kama kaka yangu, lini safari?

Kesho kutwa, inaonekana maudhui ni ya haraka zaidi kuliko nilivyotarajia.

Je unaweza kuja kwangu leo, na mimi nipo peke yangu hospitalini.

Ikiwa ni sawa kwako nitakuja baada ya muda mfupi ujao, naondoka sasa hivi.

Sawa ….nakusubiri.

Joji alifika hospitalini na kuonana na Adam akiwa kitandani huku akisoma..

Karibu, unaonekana umezama katika kusoma, unasoma nini?

Nasoma kitabu cha Allah, “Qur’an”.

Kwani hukuwahi kukisoma?

Hapana, bali nimekisoma sana, ila napenda kukisoma kila siku.

Kila siku? kwani hamchoki?

Ndio, sisi tunakisoma kila siku, tunapendezwa nacho, kama ambavyo miujiza wa Issa juu yake amani ilikuwa ni ya kuponyesha vipofu na mbaranga na ukoma kwa idhini ya Allah, basi miujiza wa Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ni hii Qur’an ya kudumu.

Una maana gani kusema ya kudumu?

Kwamba Allah ameahidi kuilinda, je hukusoma tafsiri yake: “Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.” (15:19) kwa kusoma tafsiri yake kweli unahisi muujiza wake?

Kweli…natamani wakati nikisoma tafsiri yake kuwa ningekuwa nasoma asili yake na sio tafsiri yake, ijapokuwa mimi nasoma tafsiri yake ila najihisi inaniongelea mimi katika maudhui nyingi.

Mimi najua maudhui nyingi zinazo kuongelea wewe.

Umejuaje?

Inabaki kumpwekesha Allah na majina yake, sifa zake, utukufu wake, na uzuri wake ni kubwa zaidi katika mambo yanayomtikisa binadamu yeyote, wala sihitaji kujua yasiyoonekana.

Oh, ndio umesema kweli, kama ambavyo ukamilifu katika Uislamu upo katika kuchanganya baina ya dunia na akhera pamoja na kuwa mambo ya kiroho ni ya kipekee kabisa na ni katika vitu ambavyo nashangazwa navyo sana.

Uislamu unayafanya maisha ya mwanadamu yawe kamili, hakuna utawa wala kujiweka mbali na Allah, bali uhai wote ni kwa ajili ya ibada pale utakapo kuwa na nia nzuri.

La msingi ni kuwa mimi kesho nasafiri kwenda Cairo, unaniusia nini?

Haahaa kunywa maji ya mto Nile.

Je katika Uislamu kunywa maji ya Mto Nile ni ibada?

Haa haa, nilikuwa nakutania tu, katika imani zetu Wamisri ni kwamba mwenye kunywa maji hayo ni lazima arudi tena; ni kwa ajili ya uzuri wa nchi na watu wake pia.

Inavyoonekana Misri ni nchi unayoipenda zaidi!

Bila shaka, mimi naipenda Misri sana tu, na mara ngapi napenda kurudi huko, ila napenda Makkah na Madina zaidi.

Jambo la kushangaza zaidi! kwa nini?

Ni miji ya kipenzi changu Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam)

Je mnamuhesabu Mtume wenu kuwa ni mkombozi wenu, kama sisi tunavyomuhesabu Issa?

Fikra ya uokovu haiendani na wazo la Uislamu katu, Issa ni Nabii na Mtume Muhammad ni Nabii na Mtume, na wote hao katika imani ni sawa bila kutofautisha yeyote, na sisi tunaamini Mitume wote, na mwenye kuwatia makosa au kuwapunguza katika shani yao kwetu, atakuwa amekufuru.

Hata kama ataukashifu utu wa Musa Nabii wa Mayahudi au Issa Nabii wa Manaswara?

Ndio, je hukusoma katika Quran tamko lake Allah katika Surat Baqarah Aya.

“…hatutafautishi baina ya yeyote katika hao,...” (2:136)

Nimesoma… na hiki ndicho kitu kilichonivuta katika Qur’an, nyinyi mnawaheshimu sana Mitume: Musa, Issa, Luti na Adam kuliko wafuasi wao, umenikumbusha mambo mawili: Kitabu ambacho alipewa Katarina na Mmisri. “Mapenzi yangu makubwa kwa Issa ndio yaliyoniingiza katika Uislamu.” cha mwandishi Mvenezuela, na umenikumbusha Mitume katika Agano la Kale.

Mitume wote walikuja kumpwekesha Allah na kumwabudu yeye pekee, lakini wachafuzi wameingiza ushirikina katika dini.

Samahani, huwezi kutufundisha kuhusu dini yetu, na huwezi kuwa mjuzi wakujua Uyahudi kuliko Wayahudi wenyewe wala Ukristo kuliko Wakristo.

Umesema kweli huenda Wayahudi wanaijua dini yao kuliko mimi kwa sasa na Wakristo ni hivyo hivyo, lakini ni kitu kisichowezekana kiakili na kisheria kuwepo Mungu mwingine!

Kivipi?

Ama kiakili: Allah ametaja kwa ushahidi wa kiakili katika Surat Ambiyai Aya ya 22 “Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. Subahana ‘Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu, Bwana wa A’rshi (Kiti cha Enzi), na hayo wanayo yazua.” (21:22). Na kungekuwa na waendesha dunia wawili au waungu wawili au zaidi ya hivyo, basi kungekuwa na dosari katika kuratibu na hivyo kuharibu misingi yake. Wangekuwa wanapingana, kwa mfano mmoja angetaka kupanga kitu, mwingine akakataa na akataka kinyume chake, kwa hiyo haiwezekani wote kuwa kitu kimoja, na pia haiwezekani mmoja kutaka kufanya jambo bila ya ridhaa ya mwingine na itakuwa ni kushindwa kwa mwingine na kutoweza, pia haitowezekana kwa wao wawili kuafikiana katika jambo, kwa hivyo mwenye nguvu ya kutaka kufanya mambo pekee bila kizuizi ni Allah pekee mwenye nguvu. Na Allah ameliweka wazi katika Surat AlMuuminuuna aya 91: “Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu.” (23:91)

Falsafa ya kimantiki nzuri! Ijapokuwa inatofautiana na Ukristo na kupingana nayo kwa ujumla!

Sio falsafa bali ni katika uchaji mungu, wala haipingani na Ukristo bali inapingana na ushirikina na upagani, kwani Nabii Issa alikuja kumpwekesha Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), acha nikuulize kama alivyouliza Nabii Yusuph kuwauliza wale rafiki zake wawili pale walipo kuwa jela, kama alivyosema Allah katika Surat Yusuf ayah No. 3940, “…Je, mabwana wengi wanao farikiana wao kwa wao ni bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu? Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo nyooka. Lakini watu wengi hawajui.” (12:3940) kipi bora kati ya waungu wengi au mungu mmoja?

Lakini vipi unasema, Allah hajalitolea dalili? Na katika Agano Jipya imejaa kutaja Uungu wa Issa!

Ijapokuwa swali lako limesimamia upande mmoja, ila tukamilishe mjadala wetu, wewe unafahamu sana kuliko mimi, ni kwamba Agano Jipya limejaa upotoshaji na unafahamu baadhi ya nakala za Agano Jipya zimetaja kumpwekesha Allah na wala sijui ni kwa nini kuwe na Waungu wawili, hata kiakili tu, na huenda wakazozana au kuhitalifiana na kusababisha kuharibika kwa mbingu na ardhi. Kama anavyosema Allah katika Qur’an Surat Anbiyaa: “Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. Subahana ‘Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu, Bwana wa A’rshi (Kiti cha Enzi), na hayo wanayo yazua.” (19:22) au tofauti zao kama alivyobainisha katika Surat ya Muuminuuna aya 91: “Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu.” (23:91)

Haya ni maudhui marefu sana, ni mara ngapi nachukia masanamu na picha ndani ya kanisa Katoliki, na nadhani hiyo ni aina ya ibada ya vitu ambavyo umenitajia kwa wale wanaoabudu masanamu, lakini sijaja kwa mjadala huu!

Hakuna kitu kizuri chenye kupendwa ndani ya Uislamu kama kumpwekesha Allah, utulivu wake na wema wake pamoja na amani.

Wema wake! Utulivu! Na Amani!

Ndio, ushirikina unaufanya moyo kuwa na dhiki na kuparaganyika, hivi hukusoma tafsiri katika kauli ya Allah katika Suurat At An’ami aya ya 82, “Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka.”

Na katika Surat ArRa’ad aya ya 28;

“Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!” (13:28)

Na katika Surat Twaha aya ya 124:

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” (20:124). Najua kwamba wewe hukuja kwa hili! Kwa hiyo nisamehe, na huenda nimerefusha maongezi, lakini wewe ndio uliyeniuliza.

Kabla haujafunga maudhui haya naomba kukuuliza swali ambalo lipo kichwani mwangu sana na wakati nasoma Qur’an, imetaja mwishoni mwa aya katika Qur’an kitisho cha Allah cha kuwafufua baadhi ya watu wakiwa vipofu! Je hii siyo mapenzi ya kuadhibu kutoka kwa Allah?

Ametakasika Allah na yote hayo, Qur’an imejaa sifa nzuri za Allah (mwenye kutakasika na kutukuka). Allah ni mkarimu, mwenye huruma na rehema, msamehevu, mtoaji na mwenye shukrani…mpaka mwisho wa uzuri wa majina yake, kama ambavyo anasifa za nguvu na uwezo, na katika Surat Rahmaan aya ya 78: “Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.” (55:78)

Huenda hayo yamekuja katika mawazo yangu ni kwa sababu ya kukuta katika Agano la Kale wasia wa kuuwa, kupora na kutumia nguvu.

Ndio, hiyo ndio sababu, ninaongoza sababu zingine, kwani Wakristo wamezoea fikra ya utakaso, ya kwamba hakuna moto utakaokuwepo siku ya kiyama, ila kwa fukara au maskini asiyeweza kulipa kiasi fulani kwa ajili ya ukombozi au usamehevu.

Umeanza hujuma; hatuna sisi Waprotestanti mkataba wa kusamehe, kama walivyo Wakatoliki na Waorthodoksi, ijapokuwa wazo la kutakaswa lipo kwetu sote.

Kama ulivyosema.. wazo la imani ya utakaso katika utekelezaji wake inapelekea kuwa watu wote watapona kwa uokovu na utakaso wa Masiya juu yake amani; kitu ambacho kinafanya Siku ya kiyama kutokuwa na faida wala maana, kama ambavyo matendo ya ibada ni sawa kwa mwenye kufanya na asiyefanya kwa sababu wote hao wametakaswa na Masiya. Je huoni hicho ni kichocheo na kihamasishi cha kutomtii Mungu na kutenda matendo yasiyokuwa na tija?

Huenda, na kwa mnasaba wa maadili, umenikumbusha Kakhi na mambo ya kazini, kesho kutwa ni safari kwenda kwenu Cairo, je kuna mipango gani iliyopendekezwa?

Nataraji atawasili sasa hivi Sheikh Baasim kwani nimewasiliana nae baada yako na kumuelezea na amesema atakuja baada ya saa moja hivi na nadhani yupo karibu kufika, ndugu yake ndio atakuwa mwenyeji wako huko, na anataka akusikie wewe kwa kile unachohitaji huko kabla ya kusafiri kwako, tupo tayari kukuhudumia kwa hilo.

Haa…haa, kwa nini?

Sijakufahamu!

Kwa nini mnitumikie mimi? Nini mnapata kwa huduma yenu kwangu?! Samahani kwa swali hilo lakini linanijia mara nyingi.

Wewe ni rafiki yangu ndio maana nakutumikia na Sheikh Baasim anakutumikia kwa niaba yangu, kwani wewe ni rafiki yangu, na pia kuna sababu nyingine napenda kuificha.

Samahani, unaweza kunitajia sababu nyingine?

Kwa kweli…mimi na yeye tuna matarajio kwamba huenda wewe ukasilimu, na katika dini yetu ukimfikisha mtu katika imani ya kweli ya Allah ni katika bora ya kujikurubisha kwake.

Samahani Adam, japo una juhudi kubwa, nadhani sitasilimu katu, kwa hivyo nashauri msipate tabu sana ya nafsi zenu, na katika kunifahamisha juu ya Uislamu au kunitumikia mimi

Usituhofie sana sisi, ujira au malipo tunayapata kwa zile juhudi tu hata kama hujasilimu na utumishi ninaoutoa kwako ni sadaka na una ujira kwa Allah pia, na kuwatumikia watu na kuwasaidia ni katika mambo bora ya kujikurubisha kwa Allah, na mimi nina imani ya kwamba pamoja na hayo mwenye kutakiwa kheri na Allah basi humkunjulia kifua chake katika Uislamu na mimi nina matumaini makubwa utasilimu kwani wewe ni mtu mwenye akili na kutumia mantiki.

Huenda, lakini sidhani, naomba lisikukere hilo, lakini kwa nini umebadilika lahaja yako na ya mwanzo?

Unakusudia nini?

Hukuwahi kuniambia chochote kuhusu dini yako wala Qur’an, na kwa sasa muda wako mwingi unaongelea hivyo, je ulikuwa una nidhihaki na kunitania?

Nilikuwa na imani ya kwamba utakuja katika Uislamu na utaacha dini zote, na wewe umepita katika njia inayokuongoza katika Uislamu, kwa nini nikukatishe njia hiyo? Na sijabadili fikra yangu ila katika kipindi kimoja!

Lini?

Pale ulipokuwa mgonjwa kabla huja fanyiwa operesheni.

Kwa nini?

Nilihofia utakufa kwa kweli, kwani mimi napenda rafiki yangu awe na mimi peponi…huyu Sheikh Baasim amefika, karibu Sheikh.

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakaatuh.

Waalaykum Salamu Warahmatullah Wabarakaatuh.

Joji kwa mshangao!

Karibu, nini unakusudia kwa maneno yenu?

Hiyo ni salamu yetu sisi Waislamu, pia ni dua akhera, una muomba Allah amsalimishe na mabalaa yasiyoonekana na yanayoonekana, na usalama wa hisia ni usalama wa mwili, utu na mali, na usalama wa ndani (wa kimaana) ni usalama wa dini dhidi ya maangamizo, kisha ni dua ya rehema na baraka, kwani dini yetu ni dini ya amani na rehema.

Kwa mara nyingine mtanirudisha katika mjadala juu ya dini! Mimi kesho kutwa nasafari, je ni zipi taratibu zinazotakiwa?

Unachokitaka, ndugu yangu yupo huko, anaweza kukuandalia kile unachotaka.

Sijajua kinachotakiwa kufanywa huko mpaka muda huu, nataraji atanitumia email, lakini mimi baada ya kufikiri, natamani kutembelea na kuona vitu mimi mwenyewe ukiacha kazi, mnaweza kuniandalia sehemu na mambo mengine.

Unataka kutembelea nini?

Nataka kutembelea pyramids, kanisa la Waorthodox, kukutana na makasisi wao, pia nataka kuonana na baadhi ya wanachuoni wa Kiislamu.

Yote uliyoyataja ni rahisi sana, na atakuandalia kaka yangu, tayari nimeshamwambia na ameshakuandalia baadhi ya mapendekezo, lakini muamuzi ni wewe, ishi na watu wa kawaida na uwasikilizie wao.

Vizuri na ni muhimu, lakini mizunguko yote hii ya kitalii itanigharimu kiasi gani?

Sisi sio shirika la kitalii, wewe mwenyewe utalipa gharama za utalii, ama kuhusu ndugu yangu hiyo ni takrima kwa mgeni na ni katika ibada alizoamrishwa Muislamu.

Waislamu wote wako hivi?

Haa haa, hapana.

Adamu alijinyoosha na kukaa sawa sawa na kusema kwa mzaha:

Kuwa muangalifu na wezi na vibaka, wana mazingaombwe na wadanganyifu, na wengineo katika jamii, hutapata jamii yenye kufanana katika maisha haya, mji mwema na wenye watu wazuri pekee.

Je Uislamu hauwaiti watu kunako tabia nzuri?

Bali Mtume aliletwa kwa ajili ya kuendeleza hizo tabia nzuri kama anavyosema (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) “Hakika nimeletwa ili kukamilisha na kuendeleza tabia nzuri.” Na kwa kadiri Waislamu wanavyoshikamana na Uislamu ndivyo wanavyoshikamana na tabia nzuri, na tabia nzuri zilikuwepo hata kabla ya Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na yeye kuja kuzikamilisha, la muhimu kuwa makini, na kwa bahati mbaya miji yetu ni dhaifu kiuchumi na kimfumo

Baasimu alimpa kitambulisho…

Chukua kitambulisho hiki chenye maelezo ya kaka yangu kwa ukamilifu na atakusubiria airport pale tu utakapo mtumia email au kumpigia na kumpatia muda maalum, usiogope kitu, ndugu yangu anaongea Kiingereza.

Niliongea na ndugu yangu muda sio mrefu pia, ili akukaribishe nyumbani kwetu, ila yeye haongei Kiingereza, kwa hivyo hatafaa kuwa mwenyeji wako.

Nawashukuru sana na nalazimika kuondoka kwa sababu nimechelewa na nategemea kwa kesho muda mwingi nitakuwa kwenye shirika ili kukamilisha baadhi ya maandalizi ya safari na kuna baadhi ya mambo lazima niyakamilishe kwa leo hii, na tutawasiliana nanyi nikiwa Misri, nawashukuru sana.

Misri inakusubiri, kwa heri ya amani.

Nanyi kuweni katika amani ya Allah.

(2)

Joji alifungua email yake kuona kama ametumiwa utaratibu wa kina wa kazi akiwa Misri au bado, alikuta barua mbili ya kwanza imetoka kwa John Luke,

“Mpendwa Joji:

Mimi nastarehe sana Libya kuliko nilivyotarajia… ila kuna tatizo la usalama katika masiku haya, tatizo lingine ni hali ya hewa, lakini najisikia ni safari nzuri ya kitalii ijapokuwa kuna ukame wa jangwa.

Nitakupa habari hatua kwa hatua, ninatarajia utanipa habari zako pia mpaka tupate njia bora ya maisha. Angalizo: Laiti ungenijulisha kuwa utakwenda Misri basi ningeifanya safari yangu kwenda huko badala ya Libya. Ni mimi John Luke.”

Joji alimjibu:

“Mpendwa John Luke, Samahani kwa kutokujulisha kuhusu safari yangu ya Misri, sikuwa natarajia bali haikuthibitishwa ila leo, nitakufahamisha juu ya safari yangu. Angalizo: Sijakuelewa unakusudia nini unaposema ni safari nzuri ya kinafsi na roho?! Lakini mimi nahisi ina ukame wa kiroho. Ni mimi Joji.”

Halafu Joji alifungua barua ya Mkurugenzi Mkuu wa Mahusiano, na alisoma vipengele vinavyotakiwa huko Misri kwa mazingatio makubwa, kwa hiyo kazi ni ngumu sana, kwani amemtaka kufungua ofisi ya utaalamu wa ufundi na biashara huko Cairo ili iwe ni kituo cha uwakala katika mashariki ya kati yote. Ilibainika wazi kwamba Kakhi hakutaka arudi haraka na kwa hivyo akafanya haraka kumpangia kazi iliyokuwa ngumu isiyowezekana, na hivyo basi kuamua afanye jitahada ya leo na kesho kwa ajili tu ya kujiandaa kwa safari hii iliyokuwa ngumu ili afanikishe jukumu lake gumu kama ni changamoto kwa Kakhi.
Joji alianza kuwasiliana na mashirika ya kitaalumu ya kiufundi Misri na kuwajulisha kwamba atawasili baada ya siku mbili na anawahitaji baadhi ya wafanya kazi wawe tayari kumpokea kwa muda muwafaka, na kwa kupitia intaneti akaweka kabisa nafasi katika hoteli ya kifahari siku ya kwanza atakapofika, kisha ataangalia nyumba ya kuishi kwa msaada wa Jamali ambae ni ndugu wa Sheikh Baasim aliyekutana nae hospitalini wakati wa kumtembelea Adamu. Na alianza kutafiti katika mitandao ya kimataifa juu ya maelekezo na taarifa zitakazomsaidia kufanikisha safari yake kwa ufanisi, na kuandaa dondoo na vipengele mnasaba kwa ajili ya mkataba na kutafuta fursa za ufanisi.
Katarina aliingia na kumkuta Joji akiwa amezama katika kupitia vipengele vya kazi na majukumu yake, huku akijua yupo katika changamoto kubwa kutoka kwa Kakhi, na yeye Kakhi hatamwachia kuhusiana na jambo lake, lazima ajiandae vizuri kwa yatakayo kuja mbeleni.

Ilikuwa ni siku ngumu, haya nipe habari njema, je unalo jipya?

Nitasafiri kesho kutwa kwenda Misri.

Kesho kutwa! haraka ya nini hiyo?

Ni kwa ajili ya jukumu refu na gumu sana, huenda nilikosea nilipochagua kwenda Misri, au Kakhi alitaka kuniadhibu mimi kwa hili na kuharibu sifa yangu mbele ya bodi.

Mimi nina imani utafaulu katika jukumu lako, japokuwa anakufanyia hivyo, Mungu yupo pamoja nawe.

Katarina nakupenda sana, na nahofia safari yangu hii ikachukua zaidi ya mwezi, na katika nchi ya ugenini tofauti na nchi yetu au ulimwengu wetu na lugha tofauti, dini tofauti, utamaduni tofauti na mfumo ulio tofauti pia.

Huenda, ila nina imani kuwa utastarehe katika safari yako hiyo.

Natamani hivyo, na Adam amenihakikishia kwamba nchi ni nzuri, inaonesha Adam anaipenda nchi yake sana.

Kila watu wanapenda nchi zao!

Sawa, lakini cha ajabu, yeye anapenda Makkah zaidi kuliko anavyoipenda Misri, kwa sababu Mtume wao anaipenda Makkah zaidi, ni utii gani na mapenzi gani haya? Je haikukumbushi mapenzi ya Ukristo kwa watawa?

Kamwe, inanikumbusha mapenzi yetu juu ya Yesu, hata kama kuna tofauti.

Tofauti katika nini?

Sisi tuna muona Yesu katika nafasi ya Uungu, na wao wanamuona ni Mtume aliyetumwa, sisi mapenzi yetu kwa Yesu yanazingatiwa kwa kuwa yeye aliitoa nafsi yake kutukomboa, na wao wana mzingatia kama ni Mtume kutoka kwa Mungu na amewafundisha mambo mengi ya kheri.

Kheri gani!

Uislamu, wanaona kuwa ndio kila kheri ndani yake.

Kila kheri!

Wao wanaona hivyo, na wanatanguliza mtazamo wa Kiislamu katika kila nyanja ya maisha, wanasema imetoka kwa Mungu.

Unakusudia nini kwa kauli yako “wanaona… wanasema?

Waislamu.

Umesema katika ujumbe wako wa mwisho wa email kuhusu Quran: “Inaelekea ni kutoka kwa Mungu”, ujumbe wako ulinishtua sana kwa hali zote zile.

Bali utafiti wangu juu ya swali lako kuhusu ukweli wa kuinasibisha Qur’an na Mungu ndilo ulionishitua, na bila ya shaka hichi wanachokisoma Waarabu ndicho alichokuja nacho Muhammad bila ya badiliko la aina yoyote, lakini bado swali lipo pale pale, je Muhammad ni mkweli au siyo?

Nilichofahamu katika ujumbe wako ulituonesha ni kuwa Muhammad ni mkweli na kwa hivyo ndio nikasema: Inaonekana ni kutoka kwa Mungu.

Hapana, sikuwa na kusudia hivyo, nilichokuwa na kusudia ni kwamba sio kama Agano la Kale na Jipya, kwani kuna nakala zenye kupingana tofauti tofauti.

Ijapokuwa mjadala ni mzuri, mimi nalazimika kuukatisha, nina kazi nyingi za kuandaa kabla ya safari, kwa mnasaba wako wapi watoto?

Wamekwenda ziara ya kishule, nilikufahamisha jana au umesahau! Nataraji wafike baada ya muda mchache na chakula kiwe tayari ijapokuwa kimechelewa sana.

Oh kwa hakika nimejisahau, na mimi nina njaa sana, asante mpenzi wangu, naomba ruhusa nikamilishe kazi yangu mpaka chakula kitakapokuwa tayari.

(3)

Joji alimuaga Katarina na watoto wake na kwenda uwanja wa ndege… alifika Cairo Saa kumi na mbili jioni, alimaliza kukaguliwa nakutoa mikoba yake na kuelekea katika ukumbi wa mapokezi na kumkuta mtu amebeba bango lililoandikwa jina lake: Joji Nesson, kwa maandishi makubwa, inaonesha mwenyeji wake hakifahamu Kiingereza vizuri, alimuelekea na kumuashiria, alitabasamu, na alimwita yule rafiki yake aliyekuja kumpokea Joji…

Karibu, karibu sana Misri, mimi ni ndugu wa Baasim (Jamali) na huyu ni ndugu wa Adam (Muhammad) hakifahamu Kiingereza vizuri, hata hivyo alijitahidi sana kukukaribisha.

Nakushukuruni sana.. na tuondoke kuelekea hoteli ya uwanja wa ndege, kwa sababu nimeshapanga chumba hapo.

Jambo linarudi kwako tu wewe, lakini hoteli ipo mbali na mji, na Cairo ina msongamano sana, kama ambavyo ni ghali sana.

Hamna neno tutabadilisha kesho, kwani nimekodi kwa siku moja tu ila nina mategemeo ya kuhamia katika hoteli nzuri iliyo karibu na katikati ya mji, na karibu na mashirika makubwa ya nchi.

Kuna hoteli nyingi katikati ya mji, na kesho utachagua hoteli unayoitaka.

Napendekeza unichagulie wewe kesho na uniwekee nafasi, ikinipendeza nitaendelea nayo, kwani nina kazi nyingi sana.

Kama utakavyo…mimi nitajitahidi kukuhudumia, kwani hujui thamani aliyokupa Baasim.

Jambo la kushangaza Baasim kunijali kiasi hiki!

Kuna sababu nyingi kwa hilo “Kwani wewe ni mgeni wetu, na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ametuamrisha kumkirimu mgeni, na wewe unafanya utafiti kuhusu Uislamu na sisi ni wajibu wetu kukufahamisha juu ya Uislamu na wewe ni rafiki wa ndugu yangu, na Mungu ametuamrisha kutekeleza ahadi.

Kwanza: Kwa nini kila mnaposema jambo, lazima mumtaje Muhammad? Pili: Nani kakueleza kwamba mimi natafiti kuhusu Uislamu?

Jibu la kwanza ni kwamba: Mtume ni kipenzi chetu na kiongozi wetu au kiigizo chetu. Pili: Baasim ameniambia kwamba wewe unatafuta furaha.

Ni kuhusu furaha na sio Uislamu

Sijui tofauti kati yao, kwani bila furaha hakuna Uislamu na kama sio hivyo basi nyinyi huko Magharibi mngekuwa na furaha zaidi, wala hakuna siri, kwa mfano: taifa la Sweden ambalo kuna wapinga dini na wasio kuwa na dini karibu asilimia 80% na ndio taifa kubwa linaongoza kwa kujiua duniani, ijapokuwa ni taifa linalosifika kwa maendeleo, je haikuwa mauaji ni kilele cha huzuni na kutaabika?

Je, kwani Waislamu hawajiui vile vile?

Kwa masikitiko ndio! Lakini wao ni wachache sana wanaojiua na kuna tofauti kubwa, katika utafiti kwa kisomi uliofanywa na Dr Gose Manuel na mtafiti Alesandar Felishman uliokusanya maeneo mbali mbali, ambapo walitegemea marejeo ya umoja wa mataifa kuhusu uhusiano wa dini ya mtu na kujiua wakakuta kuwa wasiokuwa na dini ndio watu wengi zaidi wanaojiua, na asilimia yao inakaribia 25% ya wenye kujiua, kisha wanafuatiwa na Mabudha halafu Wakristo, kisha Wahindu, mwisho wanafuatia Waislamu kwa asilimia ndogo kama moja hivi tu, halafu watafiti hao wakasema kwa sauti moja kwamba: Idadi ya wenye kujiua katika nchi za Kiislamu kulinganisha na mataifa mengine ni ndogo; inakaribia Sifuri, kwa sababu dini ya Uislamu imeharamisha na kukemea vikali kujiua.

Je Uislamu unaharimisha kujiua?

Bila shaka, bali unaharamisha kila kinacholeta madhara kwa binadamu, na kwa mshangao Mtume ametaja kupitia andiko lake zaidi ya asilimia 90% ya aina za kujiua kwa mujibu wa takwimu pale aliposema: “Mwenye kujiua mwenyewe kwa chombo cha chuma, basi chombo hicho cha chuma atakuwa nacho mkononi na kuchomwa katika tumbo lake na atakaa motoni muda mrefu sana, na mwenye kunywa sumu na kujiua atakaa motoni milele, na mwenye kujitupa juu ya jabali na akafa basi naye atatupwa katika moto wa Jahannamu na atakaa humo milele”.

Inaonesha kwamba umeathirika sana na taaluma yako, unapenda sana kutumia namba!

Asante kwa kunisifia, kweli taaluma yangu ni elimu ya hesabu kama alivyo kueleza ndugu yangu, na mahesabu ya akili yanaongeza katika mantiki ya akili bila shaka, lakini nimejifunza njia za elimu kupitia dini yangu kwanza.

Kila kitu ni kutoka kwenye dini yenu na Mtume wenu! Nyinyi mmezidi sana!

Huenda, ila huoni kuwa mfumo wa kisomi unataka uoneshe ninapozidisha, sio kunituhumu tu kuwa tunazidisha bila ya uthibitisho

Umenishinda! Vipi dini yenu inahimiza juu ya mfumo wa kisomi na kielimu katika kulishughulikia jambo?

Angalia baadhi ya misingi na dalili za Kiislamu zenye kufungamana na njia za kielimu, mfano Uislamu umetahadharisha kuiga bila kutumia akili. Allah anawaambia washirikina katika surat AlBaqarah ya kwamba: “…wao husema: Bali tutafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka? ” (2:170)

Na kufuata dhana bila ya kufuata mfumo wa kielimu;

“…Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu.” (6:116)

Na kufuata matamanio ambayo yamo kinyume na mfumo wa kielimu, mantiki, akili na utafiti;

“…Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao bila ya kuwa na ilimu….” (6:119)

Na bughudha na chuki ambayo inamuweka mtu mbali na uadilifu;

“…Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” (4:8)

Na kutumia maudhui ya kielimu bila kuegemea upande wowote katika elimu kama Allah alivyosema kuhusu Mayahudi;

“Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake, na husema: Tumesikia na tumeasi….” (4:46)

Na katika kutodhulumu na kutengana, ambapo tunasoma katika Surat Shuurah Ayah ya 42;

“Bali lawama ipo kwa wale wanao wadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika nchi bila ya haki.…. ” (42:42)

Na kuhusu uaminifu wa kielimu pamoja na uadilifu na watu, tunasoma katika Surat Nisaa:

“…Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu...” (4:58)

Na kuhusu uadilifu, unyoofu na ushahidi wa kweli katika Ayah ya 135 katika sura ya nne;

“Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu...” (4:135)

Na kuhusu umuhimu wa utafiti na kutumia hoja na matumizi ya dalili tunasoma katika Surat AnNamli Aya ya 64 na zingine pia:

“Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli. ” (27:64) na…

Nimetosheka, basi inatosha, je wewe ni mtu wa dini kama kaka yako?

Mimi na ndugu yangu sio masheikh kwa mtazamo wa kanisa, kaka yangu amebobea elimu ya Kiislamu na mimi mahesabu…kwa nyongeza, wewe umealikwa katika chakula cha usiku nyumbani kwa Muhammad ndugu yake Adam… anauliza je unapenda vyakula vya kimisri au vyakula vya haraka haraka (fast food)?

Vyakula vyepesi vya Kimisri.

Tuna chakula kiitwacho (Koshari) je utakula au hapana?

Koshari! Siijui hebu nijaribu.

Koshari ni mchanganyiko wa makaroni pamoja na wali na vitunguu na nyanya na vitu vingine, kwa ujumla ni chakula kizuri sana, na cha kimisri haswa, utakipenda, na hii ndio sehemu wauzayo Koshari maarufu na ya kipekee.

Muhammad hakupendezwa na chaguo la Jamali, alimwambia Jamali: Je inaingia akilini tumkaribishe mgeni wetu Koshari, haiendani na adabu za kumkaribisha mgeni.

Hapana ewe Muhammad, haya ndiyo matakwa yake…ewe Joji, Muhammad haridhiki wewe kula katika hoteli za bei rahisi, anataka ukale katika hoteli kubwa, nini rai yako?

Nashukuru sana, ila mwambie hayo ndio matakwa yangu na napenda sana hivyo.

Unaona kama nilivyo kueleza!

Ewe Jamali mwambie kuwa sisi tutafuata matakwa yake, lakini pamoja na masikitiko makubwa, sisi tumezoea kuwakirimu wageni wetu na hivi ndivyo tulivyozoea na ndivyo ilivyo dini yetu.

Kila kitu kwenu kinatokana na Uislamu na Muhammad, inaelekea kuwa nyinyi Waislamu ni wafuasi sana wa dini kuliko sisi Wakristo.

Ki vipi? Sijafahamu?

Sisi tunatosheka kusali siku moja katika wiki, yaani Jumapili tu, ninyi mnasali kila siku zaidi ya mara moja, nyinyi mnapendezwa na mnajali sana dini yenu na Mtume wenu. Sisi hatuwatukuzi hata Mitume wetu, nyinyi mnaiona dini kuwa ndio dira ya maisha yenu yote na sisi tuna muono kuwa ni mafungamano ya kiroho tu.

Je kusema huko ni kwa kutusifia au kutukosoa?

Haa haa, ni sifa tu, kwani nyinyi mnalipuka na kukasirika kwa hasira kali kwa yule anayedharau matukufu yenu, inatosha kwa mfano walioyafanya Waafaghanstani pale msahafu wao ulipo dharauliwa na kuchomwa na Wamerekani!

Na ambae hajali matukufu yake na kuwaheshimu Mitume, hastahiki kitu, je hamkuwa nyinyi mnawaheshimu Malkia wenu? Hawakuwa Wamarekani wanawasheshimu viongozi wao waasisi wa taifa lao? Je hawakuwa Warusi wanamuheshimu Marx na Lenin? Na Wajerumani Nazi kwa Hitler? Na wengineo wengi? Na sisi tunawaheshimu Mitume wote, bali tunamuheshimu Yesu sana kushinda hata Wakristo wanavyo muheshimu na tunampenda sana kuliko mumpendavyo, na wala hatumuweki zaidi ya ile daraja yake aliyopewa, kwani yeye ni mja wa Allah na Mtume wake.

Ndio, sahihi, ila nyinyi mnazidisha!

Kuzidisha ingekuwa ni sawa laiti tungesema Muhammad ni Mungu kama mlivyosema nyinyi!

Nakusudia mnazidisha kwa kule kufungamanisha maisha na dini.

Ama kwa mnasaba wa mahusiano ya dini na maisha, naamini mwenye muono wa mafungamano kati ya mja na Mola wake kuwa ni mafungamano tu ya kiroho ya muda kwenye swala tu, halafu maisha yote yanabakia bila Mola, mtu huyo atakuwa hajafahamu maana ya maisha wala dini wala Mungu, samahani mtu huyo atabaki kuwa katika huzuni, msongo wa mawazo kiasi cha kumfikisha mpaka kujiua kama tulivyozungumza hapo kabla, hakuna maisha wala dini au Mungu kama hakuna mafungamano endelevu kati ya vitu hivyo.

Walingia mgahawani na kuletewa koshari, walikaa katika meza ndogo na Joji akionesha mshangao kwa jinsi mgahawa ulivyo sheheni watu huku wahudumu wakifanya kazi kwa bidii na kujaribu kuitikia oda kwa haraka zaidi…waliagiza koshari tatu haikupita dakika mpaka mhudumu alipowasilisha maombi yao…..

Mtaje Allah ewe muheshimiwa, Koshari imefika.

Mhudumu anasema nini?

Ananikumbusha kumtaja Allah kabla ya kula.

Kwa nini?

Ili kukamilisha maongezi yetu yaliyo tangulia, ni lazima Muislamu maisha yake yote yawe kwa ajili ya Allah, Muislamu anataja jina la Allah kabla ya kula, kwa maana ya kwamba naanza kitendo hiki kwa msaada wa Allah (Bismillah) kwa kutaka baraka kutoka kwake.

Vizuri !

Uislamu haujaacha mambo hivi hivi tu isipokuwa kuwa hukumu yake kama anavyosema Allah katika Surat An’aam aya ya 38; “Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa.” (6:38)

Kila kitu!

Haa haa, umenikumbusha kisa kilichotokea wakati wa Mtume alipomuijia asiekuwa Muislamu, na kuwaambia masahaba wake kwa dharau: Mtume wenu amekufundisheni mpaka kwenda haja kubwa! Wakamjibu ndio, hakika ametukataza kunawa kwa mkono wa kulia, na katukataza kutumia kinyesi na mifupa katika kuondoshea uchafu, na akatuambia: Mmoja wenu asiondoshe uchafu bila kuwa na mawe matatu.

Na je aliyoyasema swahaba wa Mtume wenu ni sahihi? Au ni hoja na mjadala tu kwa asiyekuwa Muislamu, je katika Uislamu kuna maelezo kuhusiana na adabu au tabia?

Ndio ni sahihi, na kuwa Allah amekamilisha dini kwa kusema katika Surat Maidah aya ya 3;

“Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini...” (5:3)

Na Mtume ameletwa ili kukamilisha matendo mema.

Kwa nini mnadhani kwamba nyinyi ndio mnamiliki tabia nzuri peke yenu?

Labda hujanielewa niliposema muda sio mrefu, pale aliposema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Hakika nimetumwa kukamilisha tabia nzuri.” Hiyo inamaanisha amekuja kukamilisha, maana yake ni kwamba: Tabia nzuri zipo kwa watu, na Mtume ndie atakae kamilisha na kutimiliza na hii ndio sehemu nzuri ya Uislamu pekee.

Unakusudia nini?

Ninakusudia kuwa Uislamu ndio utakamilisha na kuhitimisha tabia nzuri na dini na sheria, na Mtume ndio mkamilishaji wa ujumbe au utume tangu Adam, Musa, na Yesu amani ya Allah iwe juu yao. Na tabia katika Uislamu sio kitu kilichowekwa pembeni, bali ni kadhia ya msingi katika dini yetu.

Na je (Koshari) ina asili katika dini yenu?

Haa haa, ni chakula cha asili cha Misri, na sio katika Uislamu, ni chakula cha maskini na matajiri pia.

Koshari ni tamu.

Kwa pongezi na heshima zimuendee mwenyeji wetu mkimya; kwani Muhammad hajui Kiingereza vizuri.

Namshukuru sana Muhammad, na mweleze kuwa chakula nilichokula ni chakula bora zaidi.

Na imesalia Mahalabiya kwa maziwa ambayo nimekwishaiagiza.

Muhammad anakuambia kuwa bado Mahalabiya kwa maziwa nayo aina ya kitu kitamu cha kienyeji cha Kimisri.

Baada ya kumaliza kula waliondoka kwenda hoteli ya uwanja wa ndege na kuchukua chumba, na walipo maliza Jamali alimwambia Joji atamtembelea kesho asubuhi…
Joji aliingia ndani na kupanga mambo yake na kuoga haraka halafu akafungua email yake na kukuta marafiki wake wamemjibu…alizisoma nakuwarushia majibu…

“Kwa hakika majibu yenu yalikuwa ni yenye kushtukiza, lakini yalikuwa yenye faida kwangu mimi kama ifuatavyo: Habib: Siupendi Uislamu ijapokuwa mengi yaliyosemwa yana ushahidi wa kielimu, na kukusisitiza kulitembelea kanisa la Orthodoksi. Levi: Unapo ujadili Uislamu hapana budi kuujadili kwa kuzingatia unyama wao, siasa kali na ugaidi, ujinga, na ufisadi. Katarina: Sijui kuna siri gani kinachonivutia katika dini hii! Huenda ikawa ni vizuri kuhakikisha kama wao wanampenda Yesu pamoja na kumkirimu kwao mwanamke. Adam: Marejeo bora ni kitabu cha Allah (Qur’an) na napendekeza asiesoma Qur’an na kujifunza asiusemee Uislamu. John Luke: Uislamu ni mwepesi kiundani, na sijui kuna uchawi gani uliopo katika fikra hizi, ni vizuri kusoma vitabu vilivyosifiwa na Wamagharibi juu ya Uislamu. Na mimi Joji nitaongezea kwenu siri ngeni kuhusu Uislamu: Tawheed, upana wake, utulivu, mambo ya kiroho yaliyomo ndani yake, elimu, ugaidi, kuhusu mwanamke, marejeo, ukweli na Historia. Narataji pendekezo la barua ifuatayo ni kuchambua mambo hayo niliyo yataja, nani atakae kuwa wa mwanzo kutupa habari? Ni mimi Joji.”

Na baada ya kuituma … alipata ujumbe kutoka kwa Levi:

Mpendwa Joji: Ni matarajio yangu umefika salama Misri, na nahisi umeuelekea Uislamu kwa nguvu zote kuliko ulivyoudurusu Uyahudi na Ukristo mwanzo…kuwa makini na Waislamu, mimi na kuhofia kutokana na wao. Ni mimi Levi.”

Joji alimjibu kwa kumwambia:

Mpendwa Levi; Nakushukuru sana kwa kunikumbuka, nitakuwa na hadhari na nitakueleza moja baada ya jingine, ninaweza kuwa kama ulivyosema, lakini niamini sitaingia katika dini katu ila baada ya kujiridhisha kwa ukamilifu, na nitaomba ushauri wenu, nashukuru kwa pupa yako kwangu. Ni mimi Joji.”

Pia alikuta ujumbe wa Kakhi… na kufungua….

Mpendwa Joji, nimependezwa kuwa kwako mbali na Shirika, na kukubali kwako kazi usioijua kabla ya kukubaliana nayo, natarajia utafaulu; kwani nimekupangia kila kitu, na ukifeli utabeba matokeo ya kufeli kwako, nasubiri mafanikio yako. Ni mimi Kakhi .”

Saa moja asubuhi Joji alishuka kutoka chumbani mwake kwa ajili ya kupata chai hotelini, aliipenda hoteli kwa huduma zake mbali mbali kutokana na kuwepo kwa vyakula aina mbali mbali na vya kimisri, na akawa anaonja na kujua zaidi aina mbali mbali mpya za vyakula ambayo hajawahi kuvionja hapo kabla…
Mhudumu alimuuliza kwa Kiingereza dhaifu kama anahitaji kitu….!

Asante sana

Kutoka wapi ewe muheshimiwa.

Mimi natoka Uingereza.

Na wewe?

Mimi ni Mmisri… kutoka Alexandria.

Je unaweza kunihadithia kuhusu mji wa Alexandria?

Alexandria ni katika miji mikubwa nchini Misri, ni mji mkongwe ulioasisiwa na Alexander The great Mmakdonia mwaka 332 B.C.

Joji alikumbuka kile alichokisoma kuhusiana na mji huu mkongwe wa Alexandria, ambapo Alexander alitaka uchukue jina lake, na uwe ni kituo cha biashara na utamaduni wakihelensia halafu zikafuatia zama na karne za ustaarabu mbali mbali na kuna kumbukumbu za kihistoria nyingi, kwa mfano minara ya Alexandria ambayo ni moja ya maajabu ya dunia ya zamani, na kuna Maktaba ya Alexandria iliyoingizwa na Ukristo kwa mkono wa Askofu Mtume Marcos, mwaka wa 45 (B.C.) na ilikuwa ni kituo cha kuendeleza Wakristo kielimu na ilikuwa na mchango pia wa falsafa, na ndio ilikuwa shule mashuhuri kwa falsafa, na ndipo palikpokuwa na shule ya Plato iliyoasisiwa, kama ambavyo kulikuwa na shule ya Alexandria ya kiungu ambayo ilijihusisha na maarifa na uungu wa Masiya duniani. Kisha akakumbuka mchango wake baada ya Uislamu ikawa ni ngome ya kielimu ya Alexandria na kwa hakika umekuwa ni kituo cha elimu ambayo wanapokea wanachuoni wa Kimagharibi na Andalusi elimu zao za dini kabla ya kurudi katika nchi zao…
Mhudumu alimkatisha:

Inaonesha fikra zako ziko mbali na mimi, naondoka…..

Joji alizinduka kutokana na mawazo yake kuwa mbali na kusema:

Nilikuwa katika mawazo ya kukumbuka historia ya mji wa Alexandria wenye historia kongwe.

Sijakamilisha utafiti wangu niliokuwa naandika, lakini naipenda Misri na hasa Alexandria, kwani ni mji wa zamani bila shaka, je umewahi kuutembelea ewe bwana wangu?

Umenivutia na kuniingizia hamu kuutembelea, je wewe ni Muislamu?

Hapana, mimi Mkristo…..

Vipi mahusiano kati ya Waislamu na Wakristo? Ni vipi Uislamu, uliingia Misri?

Vita vilitokea baina ya Waislamu na Byzantium na Wakoptic wa Misri walikuwa bega kwa bega na Waislamu kupigana.

Wakoptic Wakristo?

Wakoptic ndio wenye asili ya Misri na haimaanishi wote ni Wakristo…na walipoukomboa Waislamu mji wa Alexandria watu wake walistarehe kwa uhuru wa dini, na waliwalinda vizazi vya kiyahudi waliokuwepo humo na bila kudhuriwa katu na hata Makanisa yalisalimika.

Na kwa nini basi hujasilimu kama ulifurahishwa na Waislamu?

Mimi nimezaliwa hivi, na kwa nini nibadilishe dini yangu na dini ya baba zangu na babu zangu? Je wewe unaweza kubadili dini yako?

Huenda…nini kinazuia, kama itanikinaishi kwa dalili, na kukinai kwa dalili ndilo jambo la msingi.

Ama kwa upande wangu sipendi kubadili, na wala sipendi masharti magumu ya Uislamu.

Masharti ya Uislamu ni magumu?

Swala tano kila siku, zaka ya mali, kufunga saumu ya Ramadhani, kuhiji Makkah, usisema uongo; usiibe, usisengenye, usizini na mengineyo kama hayo.

Lakini wao wanastarehe kwa hilo, na wanahesabu ni katika kilele cha maisha bora na ya furaha.

Huenda wao wanastarehe, lakini mimi hapana, naomba samahani kwa kurefusha maongezi mimi na wewe.

Hapana mimi nimeshamaliza kula, nakushukuru kwa muda wako.

Joji alipanda chumbani na kukusanya begi lake; kujiandaa kwenda hoteli nyingine, alimuomba mbeba mabegi kushusha chini mabegi yake, kisha akateremka kumsubiri Jamali mapokezi, alipomaliza tu maandalizi ya kutoka, Jamali alifika kumsindikiza…

Unaonekana upo tayari na mwenye hamasa ya kazi.

Ndio…nina kazi nyingi leo na lazima nizifanye.

Tutaenda kuweka mizigo hotelini halafu nikupeleke unapotaka.

Ipo wapi hiyo hoteli mpya?

Hoteli ipo sehemu ya Maad pembeni mwa mto Nile.

Ni karibu na kazini kwangu?

Cairo ni kubwa kieneo, na sijajua hasa kazini kwako ni wapi, ila kwa mapenzi ya Allah itakufaa na itakuwa karibu na kazini kwako, na kama haikufai tuna uwezo wa kuibadilisha.

Walifika hoteli mpya na kumaliza utaratibu wa kukodi chumba…

Nitakusubiri upumzike na baada ya hapo tutatoka.

Hamna neno, nitapanda chumbani halafu nitarudi sasa hivi.

Joji alirudi haraka akiwa mwenye tabasamu ya furaha….

Samahani, nataka kwenda kwenye anuani hii…hili ni shirika la ajira nimeongea nalo.

Shirika lipo Giza, halipo mbali, pia lipo karibu na Mapiramidis.

Vizuri, natamani kuyaona Mapiramidis!

Kweli, haiwezekani ufike Misri halafu usiyaone Mapiramidis.

Je Mapiramids ni sababu ya dini yenu?

Mapiramids yalijengwa na Mafarao, na zama za Farao ni kabla ya utume wa Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na kabla ya Yesu (juu yake amani) kwa muda mrefu, mengi yalitokana na Tawheed na baadhi yake yalikuwa ya ukafiri, je hufahamu Firaun alivyomwambia Mtume Musa: Mimi ni Mola wenu mkuu, na aliwatesa wana wa Israeli mpaka alipoangamizwa na Allah?

Ni ajabu nimesoma kisa katika Agano la Kale (torati) na katika Qur’an.

Vizuri sana... na ukweli: Ni kipi kati ya viwili (vitabu) vinavyo mthamini zaidi Musa?

Kwa ukweli…Qur’an, japo ni Mtume wa Wayahudi, lakini……

Samahani, na kwa ukweli kabisa ni kipi kina mthamini Mtume wa Mungu Yesu zaidi, je ni Qur’an au Injili au kama unavyoita (Agano Jipya)?

Injili kwa upande wake na Qur’an kwa upande wake.

Ki vipi?

Qur’an kwa upande wake na kutaja tabia yake na haijampunguzia au kumbebesha mapungufu, na Agano Jipya imemkuza na kumfanya kuwa ni mungu.!

Unadhani kumfanya mtu mungu ni kumkirimu au kumzulia?!

Nafahamu vizuri unachokusudia, na utaniambia: Na katika baadhi ya nakala za Agano Jipya ni kuwa yeye ni mja na sio Mungu, na utaniambia mengi zaidi ya haya, na unayo haki kwa kile unachosema, lakini wewe umetaka mawazo yangu katika kitu maalum.

Nadhani umesoma au umepitia utafiti juu ya: “Je Masiya alikuwa ni Muislamu? Cha kiongozi wa kitengo cha dini na imani katika chuo kikuu cha Luther U.S.A. Profesa Robert Shidngar.

Ndio…. Nimekipitia kwa haraka haraka, nahisi amezidisha, vipi Masiya atakuwa Muislamu hali ya kuwa Uislamu umekuja baada yake?

Kila alichokisema sio mnachokiamini, Ima atakuwa amezidisha, au amepinga au ni kinyume na kanuni ya elimu, yeye ni kiongozi katika upande wa elimu ya Uungu na katika Chuo kikongwe na hajabadilisha kauli yake na chuo kinamuunga mkono, hivi huoni binadamu anahitaji kujiundia au kujitengenezea baadhi ya maamuzi kwa uhuru wa nafsi yake na ushujaa wa hali ya juu?

Huenda nikaungana na wewe katika sehemu ya nukta ulizosema.

Vizuri, tumefika, je unataka nipande na wewe? Au nikusubiri na uniambie utamaliza muda gani nije kukuchukua?

Sijajua… twende pamoja hadi mambo yatakapokaa sawa, kisha nitakujulisha baada ya hapo.

Waliingia katika shirika la ajira na waliomba kukutana na Mkurugenzi, na Sekretari aliwaambia kwamba Mkurugenzi wake Dr. Gerges ametoka na atarudi baada ya masaa mawili, hivyo wakakubaliana warudi baada ya masaa mawili.

Sisi tupo karibu na Mapiramids, je, utataka tuyatembelea mapiramids kwa muda huu wa masaa mawili au una miadi mengine?

Twende kwenye Piramids halafu turudi baada ya hapo.

Vizuri, kisha akasema: Kwa mnasaba Mkurugenzi wa shirika ni mkristo kama nyinyi, ila yeye ni Muodhodoksi na sio Mprostestanti.

Umejuaje? Je unamfahamu?

Simfahamu, ila jina lake kama alivyotuambia Sekretari ni Gerges na jina hilo kwetu linatumika na Wakristo ama kuwa yeye ni Muorthodoksi ni kwa sababu kila Mkristo kwetu ni Muorthodoksi na sio Protestanti..najua nyinyi mnapingana nyinyi kwa nyinyi.

Je katika Uislamu hakuna makundi yenye kupingana wenyewe kwa wenyewe?

Kwa masikitiko wapo.

Mfano nani?

Kuna waliopindukia wanaipinga Qur’an na kuwatukana maswahaba wa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na wake zake waliotwaharika na wanazua mambo yasiyofaa mengi tu.

Ni wepi hao?

Ni wachache sana katika Ulimwengu wa Kiislamu, na wanapatikana katika Iran, Iraq na katika mataifa mengine.

Unamaanisha ushia!

Nakusudia hasa Wapingaji ‘Rawaafidh’ ama wanaikataa Qur’an na hadithi, na wengineo wanaojinasibisha na Uislamu kama Bahai na Kadiyani na wengineo.

Kwa hivyo mmekuwa kama sisi, vikundi vya kuuana au kuchinjana na kukufurisha na wenyewe kwa wenyewe!

Hapana, sio kama nyinyi, wengi wa Waislamu wanayo Qur’an iliyoandikwa sahihi kwa ufahamu na matamshi yake sahihi tofauti na nyinyi, Waorthodoksi, Ukatoliki, protestanti na wengineo wanayo Injili isiyoharibiwa katu na mnafahamu vizuri hili.

Najua tofauti uliosema, ila naona kuna kufanana, la muhimu je mashia wapo Misri?

Kwa ufupi hawapo, ijapokuwa walitawala kipindi fulani Misri.

Je mliwaua baada ya hapo?

Sisi sio kama nyinyi, ulipoondoka utawala wao na wakabaki watu katika mwenendo wa Sunnah na katika maumbile sahihi, na wengine walirudi katika Sunnah na Uislamu.

Kitu gani unakusudia unaposema, “Sisi sio kama nyinyi?”

Nataraji usinielewe vibaya, ni kwa mfano tu, wako wapi wakazi wa asili wa Australia? Au wako wapi wa Amerika asilia?

Je unaweza kufafanua zaidi?

Unafahamu namna jamii zilivyodhulumiwa hasa! Na kwa bahati mbaya jamii ilifukuzwa ma kuangamizwa kabisa, ama Uislamu uliharamisha dhulma na ukaamrisha uadilifu..ooh angalia hizi mapiramids mbele yetu.

Ni makubwa sana!

Yataonekana wazi ukubwa wake na usanii wa majengo yake utakapo karibia, tutasimama hapa na tutashuka na kupanda mkokoteni wa farasi, lakini nakuzindua uwe makini sana na vitu vyako binafsi.

Una kusudia nini?

Sehemu zote za kitalii duniani kuna wezi na waporaji, na hili sio kwetu sisi tu, ijapokuwa kuna aina na mbinu mbali mbali za wezi.

Kwenu ingekuwa tofauti kama ulivyosema kuwa Waislamu hawaibi?

Muislamu sio kiumbe kama malaika, anayo makosa yake, udhaifu, upungufu na mengineyo ila dini yake inakataza hayo, japo kuna dini zingine zinamuhimiza mtu kufanya hivyo.

Ki vipi?

Baadhi ya dini. Hata kama asili yake ni sahihi kutokana na kuharibiwa –zinahimiza dhulma kwa wengine, kuuwa na kuiba, ama Uislamu unaharamisha kabisa hayo, lakini kwa kadri watu wanavyo kuwa mbali na dini zao ndivyo wanakuwa mbali na maadili ya Uislamu. Na ndio sababu ya kuwepo tabia na sifa nyingi mbaya ambazo sheria imekataza kama vile: wizi, zinaa, kuunywa pombe, uongo, kuvunja ahadi, ubinafsi na mengineyo, tafadhali shuka.

Inaonekana itakuwa ni safari nzuri yenye kustarehesha.

Jamali alikodi farasi wawili na kupanda ili wazunguke pyramids na wale walioshika farasi ni watu wasiojua Kiingereza vizuri, Joji alimuomba Jamali awaambie waendeshe farasi wale kwa haraka ili wamalize mzunguko kwa muda wa saa mbili. Na katika mwisho wa safari yao walienda kupanda gari ili wawahi miadi yao….

Nakushukuru sana Jamali kutoka kwenye moyo wangu kwa hakika safari ilikuwa ni nzuri, tunaweza kurudi ofisini tulipokuwa?

Sawa, na inawezekana ukitaka kumpigia simu ili akufuate hotelini, na sasa hivi ni saa saba.

Vizuri, niwasiliane nae.

Joji aliingiza mkono mfukoni mwake ili atoe simu na kukuta sehemu au kiasi cha pesa katika mfuko wake hazipo! Aliangalia vizuri hakuziona…

Inaonesha nimeibiwa!

Imekuwa kheri Inshaalaah, huenda zimedondoka.

Hapana, nadhani yule muendeshaji wa farasi aliingiza mkono wake katika mfuko wangu ilipokuwa najiandaa kushuka juu ya farasi na kuzichukua, ila hajaingiza katika mfuko mwingine ambao ulikuwa na pochi na vitambulisho muhimu vya bima.

Sifa ni za Allah, je sijakutahadharisha kuwa makini na tahadhari!

Pesa hazikuwa nyingi, la muhimu acha niwasiliane na Gerges, mkurugenzi wa shirika lile la ajira.

Joji alikubaliana na mkurugenzi Gerges kukutana hotelini muda wa saa nane hivi, na kumweleza Jamali hilo, na walipofika hotelini, Joji alimuomba Jamali waende nae chumbali ili wakamalizie maongezi yao…

Sitaki kukusumbua na wewe una kikao cha kazi na Gerges.

Nataraji kikao kitakuwa kifupi; kwani ni maandalizi tu ya kikao kirefu kesho, na mimi nataka tujadiliane na wewe katika mambo muhimu, labda uwe na shughuli ya kukushughulisha.

Sina la kunishughulisha, karibu

Wote wawili walipanda kuelekea chumbani, na Joji aliandaa vikombe viwili vya chai katika meza iliyopo chumba cha wageni maalumu, walikaa huku wakiongea kwa dakika kadhaa mpaka ilipolia simu ya chumbani, mpokea wageni alimweleza Joji kwamba mkurugenzi wa shirika anamsubiri mapokezi.
Haraka Joji alibeba baadhi ya nyaraka, na alimuomba Jamali akaonane na Dr Gerges ambae Joji alimuona kuwa alikuwa ni mtu wa umri wa kati ya miaka hamsini, Joji aliharakisha kumsalimia na kumkaribisha…

Ikiwa utaona inafaa tukae tuongee kidogo kwa maandalizi ya kikao cha kesho.

Sawa kabisa

Kama nilivyo kutajia kupitia email, mimi nahitaji kuajiri idadi kadha ya wataalamu wa kiufundi katika shirika letu na wao watafanyia kazi hapa Cairo, lakini mimi nataka watu wenye uwezo maalumu.

Nimekuandalia idadi kadhaa ya watu unaweza kukutana nao kesho ukitaka.

Kitu gani unaweza kunifanyia kwa mapendekezo?

Utakao kutana nao ni hao tuliwapendekeza kwako, vinginevyo walioomba walikuwa ni wengi zaidi.

Kwa vigezo gani vilivyo tumika mpaka kuwachagua wao.

Kwa vigezo vya kazi! Sijakuelewa unacho kusudia nini?

Je haikuwa moja ya vigezo ni kuwa Wakristo kama sisi?

Hasira ilidhihiri katika uso wa Gerges….

Kwanza: Umejuaje kama mimi ni Mkristo? Pili: Mwenye shirika ni Muislamu na mimi ni mkurugenzi wake tu. Tatu: Waliopendekezwa ni watu kumi tu, mmoja wao ndio Mkristo, wengine waliosalia ni Waislamu, Nne….

Samahani, sijakusudia kitu, lakini nilifikiria mambo yana kushindana na kubaguana, kwa hiyo nilitaka mambo kuwa wazi tu.

Mambo kwetu sisi ni mazuri na sio kama mnavyofikiria au mnapenda yawe katika nchi zenu za Ulaya na ukweli ulivyo Wakristo wachache nchini Misri hawakupata himaya isipokuwa katika hukumu au utawala wa Kiislamu, na hata historia inaonesha Wakristo walisaidiana na Waislamu kupitia jeshi la Kiislamu kupigana katika vita.

Vizuri, nilitaka tu kujua kuwa vigezo vilivyotumika katika kuchagua sio vya kibaguzi.

Kuwa katika amani… uchaguzi ulitumia vigezo vya kazi, ijapokuwa idadi ya Wakristo walipendekezwa walikuwa wengi zaidi kuliko ilivyo.

Vipi?

Mmoja katika watu kumi ni nyingi kulingana na asilimia ya Wakristo hapa Misri, kesho nitakufafanulia vizuri maneno haya ya ziada.. sijui kama yatakupendeza au hapana?

Ok vizuri, mimi nalazimika kurudi chumbani, kwani kuna rafiki yangu mmoja yupo ananisubiri chumbani juu…na rafiki yangu huyu ni Mmisri tena Muislamu, kwa hiyo ahadi yetu ni kesho saa tatu katika shirika, na natarajia kukutana na idadi kubwa ili uchaguzi ufanyike kwa ukamilifu.

Sawa tumeafikiana nitakusubiri kesho, na utakuta kitachokupendeza na kukufurahisha, kwani Misri ni nchi iliyo na wajuzi wengi wenye viwango vya juu.

Joji alipanda juu chumbani na kumuomba samahani Jamali kwa kuchelewa… na akamuomba washuke kwa ajili ya chakula cha mchana hotelini…

Je ninaweza kukuuliza swali la moja kwa moja?

Karibu uliza.

Nisamehe kwa kweli: Ni maslahi gani utapata kutokana na kukaa na mimi na kunipeleka na kunisindikiza?

Maslahi ni makubwa sana na yako wazi.

Ni yepi hayo?

Kuwatumikia watu kwa dini yetu ni suala la muhimu sana, kwani ni katika vitu vya kujikurubisha kwa Allah.

Je haya ndio maslahi pekee kwako?

Hapana kuna maslahi mengine; mfano kumtumikia rafiki wa kaka yangu, na kuna muhimu zaidi ya hayo yote ni kukuvuta katika Uislamu.

Samahani; ama kwa maslahi ya mwisho sidhani, lakini maslahi yako kipesa yakoje na unataka shilingi ngapi kwa muamala huu?

Niamini sijafikiria pesa, weka wewe ni kiasi gani unataka kunipa, ila ondoa siku tatu za mwanzo ambazo ni haki yako kama mgeni kukukirimu.

Siku ya leo ilikuwa ni siku ndefu pamoja na kuwa bado ni mapema, ila nataka kumaliza baadhi ya kazi nikiwa chumbani na nilale mapema, na kushukuru sana wewe…ahadi yetu ni kesho saa mbili ili tuende shirikani, ahadi na Gerges ni saa tatu

Vizuri, tukijaaliwa na Mungu.

Joji aliingiza mkono mfukoni mwake ili atoe pochi ili alipe hesabu, hakuikuta…

Inaoyesha nimeacha pochi juu, ngoja nipande nikaichukue narudi nisubiri kidogo.

Unataka nini sasa hivi?

Nataka kumpa mhudumu ambae ametuhudumia japo pesa kidogo.

Chukua paundi mia hii, huna pesa za Kimisri, kesho Inshaallah utabadilisha na kunirudishia, ili upande mara moja tu na muda sasa hivi una karibia saa kumi na moja na wewe unataka kumalizia baadhi ya kazi.

Jamali nakushukuru sana.

(4)

Joji alienda chumbani kwake na kufungua kompyuta yake ili amalizie kazi zake, halafu akakumbuka mkoba wake, aliutafuta bila kuuona, alipekuwa chumbani vizuri bila mafanikio! Na kubaini haupo, baada ya hapo alikuwa ni mwenye dukuduku sana kwani kulikuwa na vitambulisho muhimu sana na pesa nyingi, alifikiri sana halafu akawasiliana na Jamali…

Mkoba wangu uko wapi?

Wewe umesema umeuacha chumbani.

Naomba uwe muwazi zaidi, mimi nimeuacha chumbani na pia nilikuacha chumbani, nimerudi sijaukuta.

Unakusudia nini?

Usinihadae kwa paundi yako mia uliolipa, rudisha mkoba wangu sasa hivi.

Samahani, sijauchukua mimi.

Ulikuwa peke yako chumbani na mkoba ulikuwa huko nani kauchukua?

Narudia kusema kuwa mimi sijauchukua kabisa.

Na unaniambia, malipo utapata kwa Allah ninamtumikia rafiki wa kaka yangu, sasa mambo yamedhihirika kwamba dini yenu ni dini ya wizi, kwa siku naibiwa mara mbili!

Tafadhali usiushambulie Uislamu, mimi sijachukua.

Kwa hiyo umeenda wapi? Je umeruka?

Kwa nini unaniambia hivi?

Kama hutaniletea mkoba wangu kabla ya saa tatu asubuhi nitakutumia polisi, kisha unaniambia mimi eti! kuwatumikia watu ni katika dini, inaonesha dini kwenu nyinyi ni kuwaibia watu kwa jina la dini, nisirefushe maneno ahadi yetu ni saa mbili uje na mkoba wangu, haya ndio maneno yangu ya mwisho kwako.

Joji alikata maongezi na kujitupa kitandani akiwa na hasira, hana la kufanya…

Inaelekea Kakhi atapata ushindi kwangu! Kitu gani kimenileta katika nchi hii, ni kwa ajili ya kuujua Uislamu, dini ya wezi? Leo hii nimeibiwa mara mbili… halafu Jamali anakuja na maneno yake nisilimu!!! Ujinga ulioje huu??!

Joji aliendelea kutafakari karibu ya saa, akiwa ni mwenye wasiwasi na mwenye hasira sana, na alikuwa anajua wasiwasi wake sio kwa ajili ya pesa na vitambulisho vilivyokuwepo humo japo vilikuwa na umuhimu wake ila anahisi kuwa amefanywa kama mtoto mdogo anayechezewa na wengine kwa jina la dini, alifikiri kupeleka ujumbe wa kufungia kadi zake za bima kwa ajili ya kitambulisho chake, lakini alifikiria tena anakihitaji kukitumia, alitarajia Jamali kukirudisha kesho ili kumaliza mchezo huu mchafu wa kuigiza… alikumbuka ahadi yake ya kesho na kusitasita…

Itakuwa vizuri ahadi yangu kesho ni kukutana na Mkristo na sio Muislamu na hii itanifanya yeye kunipa ushauri zaidi…kwa hiyo aliamua kuwasiliana nae na kumpa habari kwa yaliyotokea, alimpigia.

Hallo je ahadi imebadilika?

Hapana, lakini nimeibiwa na rafiki yangu Muislamu aliyekuwa chumbani kwangu wakati nikiwa nawe na naomba ushauri nifanye nini?

Una uhakika amekuibia?

Kwa huzuni ndio, kwani nimemuacha yeye pamoja na mkoba wangu ulikuwa humo na baada ya kurudi sijaukuta.

Huenda unatakiwa kutafuta vizuri humo chumbani au huenda umekudondoka hotelini.

Mimi nina uhakika, ni mara ngapi alinifanya mjinga alipokuwa akinicheka kwa kutumia mwamvuli wa dini nimemtisha kama hatauleta kesho asubuhi nitalifikisha polisi.

Nategemea aulete, ama kulifikisha polisi halitokusadia kitu; kwani hakuna ushahidi wowote kwa jinsi nilivyokufahamu kwa maneno yako.

Ndio, hakuna ushahidi lakini ni lipi suluhisho?

Ni lini, kesho ndio una miadi nae?

Saa mbili.

Vizuri, je unaweza kunipa namba yake ya simu ili nijaribu kuongea nae?

Haya, chukua namba yake hii….

Naomba upumzike, na kesho tutaangalia nini cha kufanya, na kwa hali yoyote nategemea atakuja na mkoba.

Joji alimaliza maongezi na huku akihisi utulivu kidogo… akafungua email yake na kukuta ujumbe kutoka kwa John Luke:

Mpendwa Joji, Nataraji upo salama na katika furaha huko Misri kama ambavyo mimi nilivyo hapa Libya, raia wa hapa wanamapenzi sana, tabia nzuri na wenye dini sana, labda tu kuna tofauti kati ya tabia za Ulaya na hawa Waarabu. Tabia walizonazo ni sehemu ya dini yao, si kwa ajili ya kujinufaisha na kusubiri manufaa kutoka kwa watu kama ilivyo tabia yetu sisi Wamagharibi. Tupe habari za afya yako na hali yako. “Ni mimi John Luke.”

Joji alimjibu John Luke:

“Kwako Mpendwa John Luke, Nimefurahishwa na uzima wako hapo Libya, lakini nakuomba uwe makini na tahadhari na Waislamu, kwa upande wangu mimi nimeibiwa mara mbili mpaka sasa na Wamisri Waislamu, mmojawao ni mtu aliyekuwa akinilingania mimi Uislamu, na hakuwa na mimi bega kwa bega nilipopatwa na mtihani isipokuwa Mkristo mwenzangu, ni kiasi gani natamani nimalize shughuli zangu mapema hapa ili nirudi Uingereza. Ni mimi Joji.”

Kisha Joji alimuandikia barua Levi akimjibu barua yake ya tahadhari kutokana na Waislamu:

“Mpendwa Levi Kwa masikitiko yamenipata yale uliyonitahadharisha nayo, nimeibiwa hapa Misri, japokuwa uliniambia mwanzo lakini kutokana na ile pupa yangu ya kuujua Uislamu ndio ikatokea hili, hata hivyo sasa nina yakini kuwa ni dini isiyokuwa na adabu au maadili, huenda ikawa Uyahudi na Ukristo umeshachafuliwa na mafundisho yake yameharibiwa ila ni kuwa Uislamu usiokuwa na maadili kabisa, nitakujulisha maendeleo yangu hivi karibuni, lakini sasa nimekumbuka tahadhari zako na uzembe nilioufanya. Ni mimi Joji.”

Joji alikuta majibu ya maswali yake yaliyotangulia kutoka kwa marafiki zake katika email yake, lakini hakuwa na hamu ya kusoma barua yoyote ile, aliamua kufunga kompyuta yake… na kujilaza juu ya kitanda akijaribu kulala lakini hapati usingizi, aliamka kitandani na kufungua T.V. katika chaneli ya B.B.C na kuangalia habari kidogo, halafu akawa anatafuta kila chaneli mpaka alikuta chaneli ya Kiislamu kwa lugha ya Kiingereza.
Kipindi kilikuwa kikiongelea sifa nzuri katika Uislamu na kwamba Mtume aliletwa kukamilisha tabia nzuri….alijiuliza mwenyewe:

Huenda jamii hii ya Kiislamu ina matatizo katika haiba yake na kutenganisha baina ya mafundisho na tabia…ni mara ngapi naichukia dini hii ambayo inapimika kwa vipimo viwili au kwa mitazamo miwili!

Hakuweza kukamilisha ratiba kutokana na hasira aliyokuwa nayo, alijaribu kulala tena kwa mara nyingine, na akawa anagaragara kitandani mpaka alipopata usingizi… na katika muda ya saa tisa alfajiri aliamka usingizini ghafla, alienda chooni, na alipotoka macho yake yaliangukia kutazama mkoba wake uliokuwa karibu na sehemu ya kufulia! Na alikumbuka alitumia bafu kabla ya kushuka na kwenda kuonana na Dr. Gerges adhuhuri na kwa haraka yake alichukua nyaraka maalumu au muhimu na bila kuzinduka kuwa amesahau mkoba wake mpaka alipoukosa yakatokea yaliyotokea!
Alikaa juu ya kitanda chake mwenye kuchanganyikiwa, na alianza kuhisi kizunguzungu… vipi ataweza kumuomba msamaha Jamali kwa yale yaliyotokea? Kwani amemkosea kwa kumtuhumu wizi kabla hajahakikisha hilo, na baya zaidi amemtuhumu bila ya ushahidi na Adam alimtahadharisha na kumuonya sana kutokufanya haraka katika maamuzi yake, nini anaweza kufanya kwa sasa?

(5)

Asubuhi ya saa mbili.. Jamali alifika hotelini na kumuomba mpokea wageni awasiliane na Joji ili kumueleza kufika kwake, lakini alijibiwa na mhudumu huyo:

Joji Mwingereza?

Ndio.

Leo asubuhi amepelekwa na gari la wagonjwa hospitalini kwa sababu ya presha.

Na je amerudi?

Ndio amerudi kama masaa mawili hivi, na sijui kama amelala au bado?

Naomba mpigie sasa hivi na mweleze kuwa mtu mmoja anaitwa Jamali anataka kupanda kukuona.

Yule mhudumu alimpigia Joji na kumweleza kwamba Jamali kafika na alimtaka apande juu chumbani… Jamali alipanda kwenda chumbani na Joji alimfungulia mlango kwa shida na uchovu ukidhihiri usoni mwake…

Samahani Joji, sijakusudia kukufanyia ubaya naomba niamini na huu ni mkoba wa dhahabu wa mke wangu, nauweka dhamana kwako mpaka benki zifunguliwe ili nikachukua pesa nikuletee, na mimi sikuweza kuleta mkoba wako na wala sijui kuna kiasi gani!

Yote hayo ni kwa ajili ya hofu ya Polisi?

Mimi nasikitika kwa yaliyotokea, ila polisi hawawezi kufanya chochote.

Kama ni hivyo, ni kwa nini umeleta dhahabu ya mkeo?

Wewe ni mgeni na ni haki yako kukirimiwa, na wewe ni msafiri na umekatikiwa na safari ni haki yetu kukusaidia, pia sitaki nichafue sura au picha ya Uislamu machoni mwako.

Bado nasita kwamba wewe sio uliochukua mkoba?

Bila shaka sio mimi, ila sitaki tulijadili hilo sasa hivi usije ukajichosha zaidi.

Laiti ungelikuwa nafasi yangu ungelifanya nini?

Hakika sijui na hii inategemea na kiasi cha umuhimu wa mkoba na mahitajio yake kwangu mimi, na utulivu wa nafsi, huenda labda ni kwa sababu ya kusoma elimu za hesabu–labda ndio inanifanya kila kitu nikiangalie kwa muono huo.

Na laiti ungefanya kama nilivyofanya mimi, unatarajia ningefanya nini ningekuwa sehemu yako.

Samahani hilo siwezi kujibu.

Je unategemea nifanye kama ulivyo fanya wewe sasa hivi?

Kwa hakika hapana, lakini wewe unastahiki hilo.

Na baada ya kufanya ulivyofanya na kupata mkoba wako, ni kitu gani ungesema au kumwambia rafiki yako?

Je umeupata mkoba wako?

Ni katika kudhania tu, jaribu kuwa nami katika hisia zangu hizo.

Hapana budi kumuomba msamaha rafiki yangu, nahisi masuala ni magumu sana kwangu, kwa hakika itanifanya niishiwe na nguvu.

Na hata kama nimemuomba msamaha na amekataa msamaha wako, na hatosahau ulicho mfanyia?

Anayo haki, lakini bora asamehe kwani Allah ni msamehevu na anapenda kusamehe.

Kwa hivyo naomba unisamehe; kwani nimeupata mkoba wangu..na kwa sababu hiyo ndio maana nimepata shinikizo la damu na kupelekwa hospitali na sikujua nifanye nini: Narudia kusema nisamehe na Allah kama ulivyosema anapenda kusamehe.

Jamali alifuta machozi yaliyokuwa yakimlenga lenga machoni mwake bila kujitambua…

Nimekusamehe, ninachoweza kukwambia ni kuwa sijapata usingizi jana na mpaka muda huu, sio mimi, wala mke wagu, wala kaka yangu Basimu na Adam Uingereza.

Kwani umewaambia?

Naam, nilibanwa sana na mimi nilikuwa nataka ushauri au ufumbuzi na Gerges alinipigia simu akiniwaidhi na kunijulisha maadili ya Kiislamu, wala sikutaka niwe ni mtihani kwako, kama Allah anavyosema katika Surat Mumtahina Aya ya 5;

“Mola wetu Mlezi! Usitufanyie mtihani kwa walio kufuru. Na tusamehe, Mola wetu Mlezi. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (60:5)

Samahani sana.

Japokuwa nina jeraha lakini mambo yameisha, na zingatia kama vile hakujatokea kitu, vipi afya yako kwa sasa hivi?

Mimi ni mzima, lakini nimekukosea sana kukuvunjia heshima yako.

Mimi nimekusamehe, lakini nina sharti.

Ni lipi hilo?

Sahau yaliotokea na angalia afya yako, vinginevyo sitakusamehe.

Mimi naungana na sharti lako kwa sharti na wewe usahau mabaya yangu kwako.

Tumeafikiana kwa hilo, je umeshapata kifungua kinywa?

Hapana.

Mimi nakualika kupata staftahi na fanya haraka ili usichelewe ahadi yako na Gerges, mimi natangulia hotelini utanikuta chini nakusubiri.

Nipe dakika tano tu nashuka chini.