Migongano

Migongano

Migongano

(1)

Sasa hivi ni saa mbili na nusu, je utaweza kuwahi ahadi na Gerges?

Tupate kifungua kinywa kwanza kisha twende tumuwahi, tukiwa njiani tumpigie simu tumjulishe kuwa tutachelewa kidogo atafahamu tu, Gerges ni mtu mwenye adabu na heshima zake tatizo ni ukali wake kwangu jana.

Ukali wake?!

Jana alinipigia simu na hakuacha chochote kinachowezwa kusemwa ila aliniambia na yote ilikuwa ni kwa ajili yako.

Nakariri masikitiko yangu kwa kila kilichotokea.

Inaelekea unataka kuvunja makubaliano yetu?

Hapana, asante sana Jamali, ni kiasi gani naweza kukushukuru.

Joji na Jamali walifika katika shirika la kimataifa la ajira na Joji alimuulizia Gerges, sekretari akamwambia kuwa anawasubiri, wakaingia ndani na Gerges akawakaribisha.

Nipe habari nzuri…je sahibu yako ameleta mkoba?!.

Tuache tukae kwanza, pili tusamehe kwa kuchelewa.

Nimeongea na sahibu yako anayeitwa Jamali jana kwa muda mrefu, ukweli ni mtu mwenye heshima zake na sidhani kama ameiba, hata hivyo nilimshinikiza sana.

Nasikitika kwa hilo, nimekusumbua sana, naomba unisamahe na nataraji utanisamehe, Jamali ni mtu mzuri na amenisamehe, mkoba wangu nimeupata bafuni hotelini!

Ah! Rehma zako ewe! Mungu, Mungu atusamehe, kwa kweli nimemkosea sana Jamali.

Nakutambulisha kwa rafiki yangu Jamali.

Samahani sana ndugu yangu kwa nilichokufanyia jana.

Mungu akusamehe, hamna neno…maudhui haya yamekwisha na tumekubaliana tuyafunge na tusiyazungumzie tena.

Wakati gani ulijua kuwa Joji alipata mkoba wake?

Nilijua saa mbili pindi nilipompa dhahabu za mke wangu kwa mkabala wa mkoba wake.

Tunaomba msamaha wako ewe Mola wangu, narudia samahani zangu; amesema kweli Allah:

“Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.” (49:6)

Ni andiko gani hili ulilolitoa?

Hili ni nukuu ya Qur’an Tukufu.

Je, Wakristo wanahifadhi Qur’an pia?

Je sijakuambia kuwa kesho nitakushtukiza kwa jambo na sijui kama litakufurahisha au hapana! Mimi nimesilimu kama miezi sita iliyopita tu.

Umesilimu na kuacha Ukristo?!

Ndio …kuna ajabu gani? Ni watu wengi wanaosilimu, bali Uislamu ndio dini inayoenea upesi zaidi ulimwenguni kote.

Sio jambo geni, lakini kwa mara ya kwanza namuona mtu ambae hakuwa Muislamu kisha akasilimu.

Jamali alishangaa na kuweka mkono wake juu ya kichwa chake na akasema:

Nilishangazwa sana na unapokuwa ukiniita ndugu yangu, nikawa najisemesha huenda anakusudia udugu wa ubinadamu tu, hongera ndugu yangu furaha ya dunia na akhera.

Furaha ya dunia na akhera! ama ya akhera: sijui, ama dunia: furaha yake tunayo sisi watu wa Magharibi.

Ikiwa unakusudia miundo mbinu na vyombo vya starehe ni kweli, ama ikiwa unakusudia furaha kwa maana yake basi utaona hali za huzuni na ajabu zinaongezeka. Ndio maana suala la kujinyonga, uendawazimu, maradhi mbali mbali ya nafsi katika nchi za Magharibi vinaongezeka siku hadi siku.

Je unanikusudia mimi Jamali?

Sifahamu! Wewe una uhusiano gani na niliyo yataja.

Mimi ni sehemu ya Magharibi ambayo unaizungumzia.

Suala lipo katika kulipa uhuru maana ya furaha ikiwa katika maisha ya raha au katika hisia za ndani ya mtu, nadhani watu katika maisha hayo ya kimada wamekosa hisia za kiroho ndio sababu ya kuchanganyikiwa katika ufahamu, na ndio sababu ya huzuni.

Alhamdulillah umepata mkoba wako, suala letu hapa sio furaha bali suala ni kuwa watu wanasubiri usaili na sisi tuna kazi.

Swadakta…Samahani, niwaacheni sasa.. nikufuate saa ngapi Joji?

Nataraji tutachelewa, napendekeza ukapumzike leo, tukimaliza nitamsindikiza hotelini mwenyewe.

Asante sana …Jamali je naweza kukuona kesho saa mbili?

Sawa, tumeafikiana, haya kwa herini, Asalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh!

Jamali ni mtu mzuri, umefahamiana nae vipi?

Kupitia ndugu yake Uingereza, vizuri nikujulishe lile ambalo hulifahamu ni kuwa kabla hatujafika alikuwa akisema kuwa wewe ni mwenye heshima sana, pamoja na kusema kuwa ulimkosea sana, hali kadhalika alikuwa akikudhania kuwa ni Mkristo.

Katika Uislamu tunatakiwa tuwafanyie uadilifu hata adui zetu, amesema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: “Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu.”(5:8). Tuliache hili sasa, tunahitaji kujadili mikataba kwanza, kisha tuwafanyie usaili, muda wako kadri nilivyofahamu ni mdogo sana.

Ndio, lakini ningependa kuzungumza nawe maudhui ya Uislamu wako baadaye.

Iwe wakati wa chakula au nitakapokusindikiza hotelini.

Saa kumi na mbili jioni Joji na Gerges waliondoka katika shirika la ajira na kurejea hotelini, baada ya siku nzito iliyojaa makabiliano na watu wengi na mikataba mbali mbali, Joji alipanda gari la Gerges.

Jitihada kubwa imefanywa kwa siku moja tu, umemaliza usaili kwa wote, nini rai yako kuhusu ulioonana nao?

Ukweli ni kuwa ni nzuri kuliko nilivyotarajia, na mbali na suala hili la kikazi na fani zao kilichonipendeza zaidi ni tabia zao za kijamii, hili hatukulizoea Uingereza, inaelekea majukumu yangu yatakuwa mepesi kwa sababu ya juhudi zenu….

Nini kinachofuata?

Sitaki kufanya haraka, nimebakiwa na usaili wa aina mbili kesho, na kesho kutwa katika ofisi zingine mbili, baada ya hapo ndipo ninaweza kuchukua maamuzi mnasaba.

Vizuri; haraka sio nzuri, au siyo?

Umenikumbusha tatizo haswa…ni kiasi gani nimefurahishwa na Jamali, ni mtu mzuri… lakini kwa sababu umesema haraka si nzuri; sasa kwa nini umefanya haraka kusilimu?!

Ha ha ha, usifanye haraka kuhukumu! Ni nani aliyekuambia kuwa nimefanya haraka? Bali ukweli nikuwa nimechelewa mno.

Ki vipi?

Nilichukua muda mrefu hadi nilipokinaika na Uislamu, na aliyenikinaisha ni huyu mwenye shirika, pamoja na kuwa hakunisukuma au kuniamrisha au kunitia dhiki nisilimu hadi muda huo sikuwa nimechelewa. Lakini baada ya kukinaishwa nimekaa miezi sita kabla ya kusilimu na hapo ndipo nilipochelewa.

Miezi sita ni michache mno kwa kuchukua maamuzi makubwa kama haya!

Je ningekufa ingekuwaje nikapata mateso duniani na akhera?

Nashangazwa sana nanyi kila mara mnaunganisha dunia na akhera, lakini niwekee wazi ni nini hizaya ya duniani na ya akhera?

Ama hizaya ya dunia ni; sikuwahi kuhisi utulivu, raha na furaha hadi niliposilimu! Huenda ukashangazwa na hilo lakini huo ndio ukweli wenyewe, hivyo basi maana ya kufanya Mungu kuwa ni mmoja na kumuabudu Yeye na kukimbilia kwake pekee bila kumshirikisha hupanua mioyo na kufurahisha nafsi za watu, hata kama ikiwa katika maisha yenyewe ya uhalisia kuna matatizo, kwani baada ya hapo baadhi ya jamaa zangu wamenihama na wakajaribu kunidhuru.

Kumpwekesha Mungu na ibada hupanua mioyo?!

Naam… kama ambavyo upagani, ushirikina na utatu unavyobana vifua. Ama hizaya ya akhera; mimi sipendi kutangulia kwa Mungu muda ambao ninamshirikisha Yeye na kingine au mwingine, kwani pamoja na ukarimu wake na huruma zake hamsamehi anayemshirikisha lakini husamehe yaliyo chini ya hapo, lakini Mungu wangu amenihurumia sijafa kabla ya kusilimu.

Maneno yako ni ya kushangaza!

Kuna nini cha kushangaza?

Kwa kuwa tumefika, tukamilishe mjadala wetu hotelini.

Nisamehe… nimechelewa nyumbani tutazungumza baadaye.

Hii ina maana kuwa nitakula peke yangu!

Likiwa hilo halitokutia dhiki.

Hamna neno, nakuruhusu.

(2)

Joji alipanda chumbani kwake na kuweka vifaa na begi lake, kisha akateremka kwenye mgahawa hapo hotelini, alikuwa akihisi njaa kali. Alipokuwa akila chakula chake cha usiku, pembeni yake alisimama mtu aliyekuwa amevaa mavazi ya ajabu.

Jina langu ni Rami, je utaniruhusu nizungumze nawe?

Karibu.

Wewe ndie uliyechukuliwa na gari la wagonjwa jana kwenda hospitali?

Ndio.

Chunga sana kuna wezi wengi hapa.

Ndio… jana niliibiwa.

Najua hili, ndio maana na kutahadharisha.

Umejuaje?

Mimi nafahamu mambo yote kwa njia ya kiroho.

Roho gani hizo?

Hii ni siri miongoni mwa siri zangu.

Je unajua kitakacho nitokea mimi kesho?

Ndio.

Huoni kuwa hili linagongana na akili ya mtu pamoja na dini?

Wewe unajua dini yetu kuliko sisi, kwani wewe ni Muislamu?

Hapana, lakini katika Qur’an yenu: “Hajui ghaibu isipokuwa Mungu.”

Hii ni elimu, hivyo achana na dini zote.

Mimi sio Muislamu, lakini naamini kuwa huo ni ushirikina na sio elimu, hivi ndivyo tunavyoamini sisi Wakristo, ama kwenu nyinyi Waislamu sijui!

Ha ha ha, Italia ni nchi ya Wakristo, je unajua kuwa idadi ya wapiga ramli waliopo huko ni zaidi ya wanazuoni wa dini waliopo Italia!

Najua kuwa ushirikina katika nchi za Magharibi unaenea kwa kasi sana kwa sababu ya kuhangaika kwetu kutafuta mambo ya kiroho ambayo tunayakosa, lakini naamini kuwa yote ni ushirikina. Je unaweza kunikinaisha kuwa jambo hili ni la kielimu?

Ndio.

Jana niliibiwa mara mbili, je unajua walioniibia?

Je unaweza kunipa kiganja chako cha mkono niangalie?

Huu hapa.

Aliyekuibia mara mbili ni mtu wa karibu nawe sana.

Vizuri, inaelekea kweli unajua yasiyoonekana, ameniibia nini?

Umeibiwa vitu vyako muhimu sana.

Na ameviweka wapi?

Sehemu iliyopo karibu…mbali, nipe dola kumi ili niipe roho ambayo itanijulisha sehemu yake.

Ukinijulisha ulipo mkoba wangu ulioibiwa nitauchukua kisha nitakupatia dola mia moja.

Nipe kwanza dola kumi.

Sinayo kwa sasa.

Roho njema imeniambia kuwa utapata matatizo makubwa kama hukunipa hiyo hela sasa.

Ha ha ha, nimemaliza chakula changu, iambie roho njema uliyonayo kuwa ni muongo, na kuwa mkoba wangu ninao mwenyewe na haukuibiwa nilikuwa nacheza na wewe tu.

Joji alipanda chumbani kwake huku akishangazwa na tabia za mpiga ramli aliyekaa nae, na kushangazwa na wingi wa watu hawa huko Roma kuwashinda watu wa dini. Je dini, mantiki, akili na elimu zimefilisika na kuwaacha wapotoshaji hawa. Joji alifungua kompyuta yake kuangalia barua pepe ambazo hakuziona jana…aliona barua ya John Luke.

“Mpendwa Joji, Nimesoma barua yako na nimesikitishwa na yaliyokukuta hata hivyo hapana budi kuweka wazi mambo mawili: Kwanza: Inapasa tuweke kando dini, fikra madhehebu na matendo ya baadhi ya wafuasi wake madamu ya kuwa dini zao hazihamasishi kufanya hivyo. Pili: Mimi naishi na Waislamu hapa na kwa ujumla ni watu waliokuwa mbali sana na suala la wizi pamoja na ufakiri wao, na udhaifu wa serikali zao pamoja na tofauti zao za kikabila, na sababu kubwa ya kutofanya hivyo kwao ni dai kuwa wanajizuia kidini na sio hofu ya sheria, kwa sababu dini yao inawakataza kufanya hivyo. Ama sisi mara nyingi kinachotukataza ni serikali na sio tabia au dini, serikali zikivunjika au mfumo unaotawala ukiharibika mambo yanachafuka na kuharibika na wewe unajua zaidi uzoefu wa nchi za Magharibi kuliko mimi. Mwishowe napenda kukujulisha kuwa mimi pamoja na inadi yangu nilikaribia kusilimu lau kama si baadhi ya mambo fulani pamoja na khofu. John Luke.”

Joji akamjibu:

“Mpendwa John Luke. Nakushukuru kwa kuwa pamoja nami, sijui nikuambie nini lakini nilidhania kuwa nimeibiwa, na nikamtuhumu rafiki yangu Muislamu na kumdhulumu, kisha akadhihirisha tabia yake nzuri na jambo hilo likanifedhehesha, kwani ni mtu mwenye heshima na tabia njema. Sijui nitamuombaje msamaha kwa upumbavu niliofanya! Ama kuhusu Uislamu; sijajua bado ni kwa nini sijachukua hatua? Lakini nahisi kuwa haiwezekani kwa muda huu kwangu mimi kusilimu kwa uchache. Bado nina tatizo kubwa, kwa mfano nafasi na hadhi ya mwanamke katika Uislamu, haki za binadamu na kiwango cha ustaarabu wa dini hii, nataraji utanijulisha utakaopata majibu hayo. Joji.”

Kisha akapokea barua kutoka kwa Levi:

“Mpendwa Joji, Nimeumizwa kwa ulichokipata, nilikuonya na kukutahadharisha, huenda kilichotokea ni kheri kwako na kwa Habib ili mpunguze mbio zenu kuelekea kwenye Uislamu, je kuna kitu tunaweza kukusaidia, unaweza kuja Tel Aviv na utakuwa katika hali ya furaha kwetu sote na kuachana na hao Waislamu magaidi, nasubiri ujio wako. Levi.”

Joji akamjibu:

“Mpendwa Levi, Nimekutamani sana, na naendelea kuhitajia nasaha zako, lakini ukweli wa mambo ni kuwa hata sijui nikuambie nini… nilidhani kuwa nimeibiwa hadi nikamtuhumu rafiki yangu Muislamu na kumdhulumu kisha akadhihirisha tabia yake nzuri na kunifedhehesha kwa heshima na tabia yake njema aliyokuwa nayo. Nakariri kwako kuwa mimi sina pupa na Uislamu pamoja na kuwa hadi sasa nimevutiwa sana na hukumu zake, itikadi zake na katika mambo mengine bado sijakata shauri, na kupongeza kwa posa yako kutoka kwa Habib, niamini huwezi kumpata mfano wake katika akili yake, elimu yake na ufahamu wake, unapozungumza nae utamuona kuwa ana vitu ambavyo mwingine hana. Natamani kuja Tel Aviv, pamoja na kukuhakikishia kuwa hapa nimepata makaribisho mazuri ambayo nilipata kutoka kwako Tel Aviv, huenda hata hivyo nikawatembelea hivi karibuni. Joji.”

Kisha katika barua alizopata ni barua kutoka kwa Katarina:

“Mpendwa Joji Adam alinijulisha kuibiwa kwako na nduguye Baasim nilipomtembelea jana hospitalini. Jambo hili limenihuzunisha na kuniumiza, nataraji utakuwa thabiti; ufahamu wangu mdogo wa siku mbili kumtembelea Baasim wakati akinifahamisha kuhusu Uislamu sidhani kama ndugu yake kama atakuwa kama yeye anaweza kufanya hivyo, tujulishe maendeleo yako.”

Joji alimjibu:

“Mpenzi Katarina, Imethibiti kwa dalili isiyo na shaka ya kuwa hakuniibia; hivyo usijali, kilichotokea ni sintofahamu yangu, niombee msamaha kwa Baasim kwa niaba yangu. Kwa mnasaba: Je inaingia akilini kuwa Katarina Mkatoliki mwenye dini anataka kuujua Uislamu?! Au ya kuwa Qur’an au kitabu. “Mapenzi yangu makubwa kwa Yesu yamenipelekea kwenye Uislamu.” Kitabu ulichokuwa ukikiogopa kukisoma kimekuathiri?! Nimekutamani sana mpenzi wangu. Mpenzi wako,

Aliendelea kufungua barua mbali mbali kutoka kwa sahiba zake zikiwa na majibu ya maswali yake aliyowatumia, alifupisha na kuwatumia tena wote…

Kuhusu Ugaidi: Habiib: Ugaidi hauna dini kabisa. Levi: Kama Waislamu waliomuua baba yangu sio magaidi; basi sijui nini maana ya ugaidi! Hakuna ugaidi katika Uislamu. Adam: Gaidi ni yule anayekalia kwa mabavu nchi za watu na kuchukua kheri zao. Tom: Ugaidi ni mshumaa wanaoutumia magaidi kwa kutishia wasiyopenda. John Luke: Aina mbaya kubwa ya ugaidi ni ugaidi wa fikra; nayo ni kuwahofisha watu katika fikra tu, ama Uislamu unalingania watu kufikiri. Joji: Hadi hivi sasa sijaona uhusiano kati ya Uislamu na ugaidi ila tu kupitia vyombo vyetu vya habari. Ama kuhusu Mwanamke: Katarina: Mwanamke ametukuzwa sana kwenye Uislamu pamoja na kuwa hadi hivi sasa sijafahamu maana ya hijabu. Levi: Sio mbaya kama alivyo katika Uyahudi na katika Ukristo. Tom: Nahitaji kufanya utafiti zaidi katika maudhui haya, kwenye Qur’an wamendika: “Na mwanamume si sawa na mwanamke” (3:36) Habib: Hauja mdhulumu. John Luke: Katika utamaduni watu tunataka usawa baina ya mwanamme na mwanamke bali kutoyumkinika kwake. Ama Uislamu umemtendea mwanamke uadilifu na umempa haki yake. Adam: Hakuna dini iliyomtukuza mwanamke kama vile Uislamu ulivyomtukuza, mnaweza kuulinganisha na dini nyinginezo za mbinguni au ardhini…. Joji: Bado kuna mambo hayajakaa kwangu vizuri kama vile hijabu: kupeana mikono, mirathi na mengineyo, najaribu kuendelea kuyafahamu na kuyafanyia utafiti.” Kwa kuwa majibu yenu nyote kuhusu Uislamu ni chanya kwa ujumla wake, swali langu la moja kwa moja litakuwa: Kitu gani kinawazuia kuwa Waislamu? Nijibu kwa kina na kwa ukweli kabisa ndani ya siku mbili? Wenu Joji.”

Aliingia katika ukurasa wa face book wa Tom; hakuona kitu kipya, kisha akaingia wa Adam; akaona mfululizo mpya wa: “Mazingatio kutoka kwa rafiki yangu mtafuta furaha – 5.

“Niliwaambieni mara kwa mara kuwa rafiki yangu katika hatua zake za mwisho, naamini kuwa kwa kiasi kikubwa amekinaishwa na Uislamu kuwa ndio njia ya furaha yake, na hawezi kujibiwa maswali yake makubwa isipokuwa na Uislamu tu, lakini uongofu unaibukia kutoka kwa Mungu peke yake tu…mke wake alikuwa akilia jana, kilio kilikua kikubwa akiwa ameathiriwa na mapenzi ya Uislamu, na haijulikani kama alikwisha silimu au bado; kwani alikuwa amerejea nyumbani katika hali hiyo ya kulia, huenda Mwenyezi Mungu akamwongoza katika furaha ya duniani na akhera.’ Ama sahiba yangu kwa kadiri ya imani yangu kuhusu uwezo wa akili yake na ufahamu wake na kwa kadri ya hofu yangu juu yake kutoka kwa Waislamu, hivi sasa amesafiri kwenda Misri ili kuufahamu Uislamu, kwa masikitiko anasema kuwa Waislamu wamemuibia, na hakufahamu tofauti kati ya kuwa ni kosa au tatizo katika Uislamu au kwa Waislamu, pamoja na kuamini kuwa kuna ukweli ambao utamfanya apite katika mtihani huu na kuingia katika Uislamu, na nafupisha darsa hili kwa nukta hizi zifuatazo: Uislamu ni mkamilifu wa kila aibu, tofauti na Waislamu ambao wengi wao hawaepukiki na makosa. Kuchukua maamuzi ya kuingia katika Uislamu kunahitaji ujasiri mkubwa na kuufahamu kwa kina, huenda hilo akalihitajia sahiba yangu. Inatubidi tusifanye upesi kuwaingiza watu katika Uislamu na kuelekea katika njia ya furaha ila baada ya mtu kukinai kwa ukamilifu. Hatuna kitu cha kuficha katika njia ya furaha, ni mkamilifu kwa hali zote, yenye kukinaisha pande zake. Kwa kila aliyetukuzwa na Mungu kujua njia ya furaha awaelekeze watu kwa njia ya wema, na uongofu ubaki kwa Mwenyezi Mungu pekee. Namtamania sahibu yangu kheri pamoja na kuwa sijui kwa ukweli, kama Mwenyezi Mungu ataufungua moyo wake au hatoufungua? Subirini somo la sita; Adam.”

Habari aliyoandika Adam kuhusu Katarina ilimsumbua sana, alikuwa akijiuliza, “Je, inaingia akilini Katarina kuingia Uislamu? haiwezekani…huenda alimpendezesha tu Adam naye hakumfahamu vizuri, au huenda Adam akawa anaongopa na kujaribu kudhihirisha kwa wasomaji wa face book yake kuwa ameweza kuwaingiza Wakatoliki katika dini yake, kwani katika barua yake ya mwisho jana hakumwambia kuwa amesilimu…alirejea tarehe ya makala ya Adam na kuikuta kuwa imeandikwa kabla ya masaa mawili, wakati barua ya Katarina kwake ilikuwa katika tarehe ya jana asubuhi. Je inawezekana akawa amesilimu jioni? Kwani kama ni hivyo hakumwambia?
Barua zote za Katarina za mwisho zimebeba rai chanya kuhusu Uislamu, bali aliweza kutofautisha baina ya Uislamu na Waislamu katika tukio la wizi. Je haukuwa huu ni uthibitisho wake kuwa amesilimu? Lakini Katarina daima alikuwa ni mwenye hamasa na Ukatoliki, na kumpenda masiya mapenzi makubwa sana na kwa ajili hiyo maisha yake yote yalikuwa ni kuhudumia kanisa, anaweza kuacha vitu vyote hivi?
Usiku ule Joji alikesha katika mgongano mkubwa, kuna muda anaona kuwa ni haki kwa mke wake kufuata dini aitakayo, na wakati mwingine anajiona ndani ya nafsi yake akiwa anachukizwa na hilo, na wakati mwingine anakana habari ya Uislamu, alikuwa akijiuliza: Je yeye (Joji) angetaka kuingia katika Uislamu ingebidi amjulishe mke wake au ndio ubaguzi dhidi ya wanawake! Aliingiwa na hamu ya kumpigia zaidi ya mara moja, lakini alijizuia. Alikuwa na uwezo wa kuwasiliana nae na kumjulisha yeye mwenyewe, au kwa uchache kumtumia barua lakini inavyoonesha ni kuwa Katarina alikuwa bado hajachukua maamuzi mazito kiasi hiki.

(3)

Joji aliamka saa moja asubuhi akiwa ni mchovu, alikoga upesi na kuteremka katika mgahawa wa hapo hotelini ili apate kifungua kinywa, kisha akakaa kumsubiri Jamali watoke waende nae katika shirika la Ajira.
Walifika kwenye lile shirika na wakamuomba sekretari wamuone mkurugenzi wake.

Dakika chache tu mtaweza kuingia kwa AlUstadhi Mustafa.

Jamali, jina la mkuu ni Mustafa, lina maana gani?

Hilo ni katika majina ya Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam), yaani Mungu amemchagua, na Waislamu wanaitana majina hayo.

Yaani ni Muislamu!

Ndio, kwa asili hii.

Zilipita dakika mbili, kisha sekretari akawaambia kuwa Ustadh Mustafa anawasubiri.

Karibuni.

Nakuacha Joji, na nitakupitia saa sita mchana.

Sijui nitahitaji muda gani pamoja na Ustadh Mustafa.

Kulingana na barua pepe yako na matayarisho tuliyoyafanya, nataraji tutamalizia saa nane mchana au uje kesho kwa mara nyingine tena.

Kama ni hivyo nitakusubiri Jamali saa nane mchana.

Lakini ningependekeza tule pamoja chakula cha mchana; wewe ni mgeni wetu leo.

Mama yangu ameniomba nimpeleke Joji akale chakula cha mchana kwetu leo.

Kama ni hivyo basi chakula cha jioni pamoja nami.

Tumekubaliana, Jamali nitakusuiri saa nane.

Na saa moja nitakupitia hotelini kwa ajili ya chakula cha jioni.

Tumekubaliana, naombeni ruhusa.

Jamali alitoka, na Mustafa akamgeukia Joji.

Inaelekea nyinyi ni marafiki wawili mlioshibana.

Ndio pamoja na kuwa sikufahamiana nae ila hivi karibuni, lakini ni mtu kwa maana ya neno hilo.

Kwa kuwa wewe hukufahamiana nae ila muda wa hivi karibuni na kutahadharisha na hawa Waislamu siasa kali.

Ni kitu gani kinakujulisha kuwa ni Muislamu wa siasa kali.

Anaonekana hivyo.

Sasa unanitahadharisha na nini?

Nakutahadharisha wasije kukuuwa au kukuibia au kitu cha mfano wa hayo, wao wanakuona kuwa ni kafiri inapasa wakuchukie, bali inapasa wakuue.

Asante sana kwa nasaha zako, na wewe ni katika aina gani ya Waislamu?

Mimi ni Muislamu lakini ni mtu niliyefunguka, muda wangu mwingi nimeishi Marekani, na nimejifunza mambo mengi kuhusu ustaarabu ambao Waislamu wenye siasa kali wamekikosa.

Mfano nini?

Nimejifunza demokrasia, na kuwakubali watu kwa rai zao mbali mbali na dini zao tofauti na yasiyokuwa hayo unayoyafahamu zaidi kuliko mimi; kwa sababu wewe ni Mwingereza.

Huku ni kutojikweza kutoka kwako, lakini nashangazwa na maneno yako; kwa sababu hata sisi Wakristo tunawaona kuwa nyie ni makafiri ambao hamjaendelea!

Mustafa alibabaika, kisha akasema: Kweli sisi tuko nyuma mtazamo wako ni sahihi kwa upande huu.

Huenda, la msingi tuanze kazi yetu.

Vizuri, tuanze kazi yetu, lakini nakuhakikishia kuwa matangamano na watu waliofunguka na wenye tamaduni mbali mbali kuna dhamana zaidi ya kufanikiwa kwako, na wewe kuwa mbali na usiyoyataka.

Bila ya shaka na haswa zaidi ikiwa anaipenda nchi yake na jamii yake!

Asante sana, nimekutayarishia idadi ya wafanyakazi kwa sifa ulizotaja kwenye barua yako.

Vizuri, wako wangapi, unawatathmini vipi wao?

Idadi ya mwanzo wanane, na wengi wao wamefunguka kwa tamaduni mbali mbali.

Vizuri, vipi kuhusu fani na taaluma zao?

Sio mbaya, onana nao mwenyewe, je unataka tuanze usaili?

Sawa kabisa, nipatie CV zao kwa mpangilio kabla ya kuingia kwangu.

Hizi hapa, nitamjulisha sekretari waingie kwa mpangilio wa nyaraka ulizonazo kwenye chumba cha mikutano, karibu kwenye chumba cha mikutano nikusindikize kisha nitarejea utakapokuwa umemaliza.

Joji alikutana na wale wanane waliopendekezwa na Mustafa, hakumaliza usaili isipokuwa saa nane kasorobo.

Nakushukuru, nimemaliza usaili.

Umewaonaje?

Vizuri, nitachukua maamuzi baada ya kumaliza usaili mzima kesho, unaonaje tukamilishe mazungumzo yetu wakati wa chakula cha usiku leo, kwani Jamali atafika baada ya dakika chache.

Vizuri, nimekutayarishia kinachokupendeza na kukufurahisha, hadi atakapokuja Jamali, je umevutiwa na yeyote katika wale wanane uliokutana nao?

Nimewaangalia wengi na nimevutiwa na wengi.

Utakipata kile kitakacho kuridhisha leo.

Kivipi?

Tutamalizia mazungumzo yetu kwenye chakula cha usiku.

Joji alitoka kwenye shirika na kumkuta Jamali akimsubiri, akapanda kwenye gari kuelekea katika nyumba ya Jamali.

Vipi kikao chenu kilikwendaje?

Si mbaya.

Kama kwamba hukufurahishwa!

Sikufurahishwa kabisa!

Kwa nini?

Ameniletea watumishi ili wafanye kazi kwangu na mimi nahitaji wataalamu wa Programu.

Huenda hakukufahamu unachokitaka kwake?

Hapana, amefahamu vizuri kabisa, lakini amenidhania kuwa nataka kushibisha matamanio yangu, fikiria nimekutana na watu wanane, miongoni mwao wanawake watano, wawili tu ndio wenye fani za Programming, na wanaume watatu, wawili miongoni mwao ni watalaamu wa fani ya Kompyuta.

Sasa amewachagua kwa vigezo gani?

Nadhani kwa uzuri wao, utanashati wao na unafiki!

Nimefahamu unachokusudia, na nakuomba msamaha, lakini sisi Wamisri hatupo hivi!

Huenda, natamani nisikutane nae mara nyingine, pamoja na kuwa kuna kijana mmoja wa kiume na mmoja wa kike nimefurahishwa nao kwani wanasifa za kipekee.

Kwa sababu umeshamuahidi, kula nae pamoja leo jioni na uombe ukutane na uliovutiwa nao.

Hili ndilo litakalotokea baada ya kumaliza usaili wangu kesho.

Mara nyingi mambo hayawi mepesi, baada ya muda mdogo tutafika nyumbani na sasa hivi tutaanza kuingia katika mitaa yetu, samahani kwani sisi tunaishi kwenye mitaa ya msongamano na sio hoteli ya nyota tano au nne.

Mimi napendezwa na hili na narejea shukurani zangu kwako na mama yako.

Siwezi kuingia na gari zaidi ya hapa, kwani barabara ni kama unavyoziona ni nyembamba sana, tutateremka na kutembea kwa miguu, ni karibu sana na hapa.

Walifika katika nyumba ya Jamali iliyoko katika ghorofa ya tatu katika nyumba iliyoonekana ya kizamani, Jamali alimkaribisha Joji nyumbani kwake na kumuelekeza kwenye chumba kidogo kilichopangwa vizuri kwa ajili ya kukaribishia wageni.

Karibu, samahani dakika chache narudi.

Joji alikaa huku akiangalia samani katika chumba kidogo, pamoja na kuwa ana mapenzi na sehemu za kawaida kama hizi hata hivyo alishaingiwa na hisia ya hofu tokea aanze kuingia katika mtaa huo hadi alipofika kwa Jamali, je hii ni nyumba yake kweli? Au amemleta hapa kwa malengo yake? Alikumbuka mazungumzo ya Mustafa kuwa Waislamu hawa wa siasa kali ni wauaji na wezi na wana hisia za kulipa kisasi tu. Alizicheka fikra zake ngeni na akakumbuka msimamo wa Jamali pindi alipomtuhumu kumuibia mkoba wake, akiwa katika fikra zile, mara Jamali akaingia akiwa na sahani kubwa ikiwa na vyombo vyenye vyakula mbali mbali, aliweka sahani ile mbele ya Joji.

Samahani kama nimechelewa, karibu.

Akiwa anaangalia chakula, asante sana, umejikalifisha sana.

Hapana sijajikalifisha, chakula hiki si changu bali kutoka kwa mama, kwani yeye ndie aliyekualika chakula na atafika baada ya muda mdogo akusalimie.

Ajabu mualikaji hayupo wanapoingia wageni.

Mwanamke katika Uislamu ametukuzwa kuliko mnavyofikiria, yeye ni Malkia anayehudumiwa, mimi nipo tayari kufanya chochote akitakacho mama yangu kwa hali yoyote ile.

Kwa hali yoyote ile?!

Ndio, kadri ya uwezo wangu, Mungu amefananisha utiifu wake ni kama kuwatii wazazi wawili na haswa zaidi mama.

Mama Baasim alifika na kusimama mlangoni, aligonga mlango pole pole, kisha akazungumza kwa lahaja ya Kimisri.

Asalaam Alaykum mwanangu, umetutukuza, umetuletea nuru na kututukuza kwa kufika kwako, Baasim anakusalimu na anatuusia kwako.

Mama yangu anakusalimia Joji na kukukaribisha, na anakuambia: Ewe mwanangu umetupa utukufu na kuingiza mwanga na umetukirimu kwa kuhudhuria kwako, na Baasim anakusalimu na anatuusia kwako.

Mpe shukurani, sijui la kusema, kwa nini hakai pamoja nasi..njoo pamoja nasi.

Mama amekuja kukukaribisha na kukujulisha kuwa sote tupo chini ya huduma yako, kwani wewe ni mgeni wetu.

Mmenifehedhesha kwa ukarimu wenu samahani, lakini kwa nini hakai na sisi? Kwa nini hatoi mkono?

Wanawake huku kwetu hawakai na wanaume bila ya haja maalum, wala hawapeani mikono na wanaume ila kama ni katika maharim (ndugu wa karibu).

Kama nilivyokujulisha leo hii nimekutana na wanawake watano, wanne miongoni mwao nimepeana nao mikono, na nilishangazwa na mmoja wao aliyekataa kunipa mkono, na wote walikaa pamoja nami.

Nini alichokuambia yule aliyekataa?

Aliomba samahani kuwa hapendi kuwapa mikono wanaume.

Nini rai yako kwake?

Nimeheshimu matakwa yake, na nikizingatia wale wasichana niliopeana nao mikono na ule uangaliaji wao, ulikuwa wa ukosefu wa adabu.

Je mimi ninaweza kwenda Uingereza nikampa mkono malkia?

Kuna uhusiano gani na hilo! Kamwe kuna aina saba ya watu ambao wanaruhusiwa na sheria kumpa mkono malkia.

Kwani sijakuambia kuwa katika dini yetu mwanamke ametukuzwa kama vile malkia aliyetukuzwa. Uislamu hauruhusu kumpa mkono mwanamke ila aina saba ya watu waliotajwa ambao ni: Baba, babu, mume, na baba yake mume na mtoto wa ndugu, baba mdogo, mjomba na mtoto wa kaka na mtoto wa kiume wa dada na mjukuu wa kiume. Ni kama mfanyavyo nyie kwa malkia wenu kama ni kumheshimu na kumtukuza, na sisi vivyo hivyo tunawafanyia kama ni heshima kwa malkia wetu ili kumweka mbali na uharibifu.

Ha ha ha, malkia aliyetukuzwa! Kama ni hivyo kwa nini basi wale wanawake kwenye usaili walinipa mikono?

Kwa masikitiko ni kuwa Waislamu wengi wamepetuka mipaka kwenye dini yao, lakini dini ipo mbali nao.

Adam hakuwahi kumpa mkono Katarina walau mara moja! Sasa nimefahamu! Je inakutia dhiki na kukerwa kumzungumzia mwanamke katika Uislamu?

Je unatarajia nikerwe na wewe unamzungumzia malkia!

Niache nikuulize swali la moja kwa moja, kwanini mmempa mirathi nusu mnayompa mwanamme, kisha mnamwona eti ni malkia, mpeni sawa tu na mwanamme wala msimfanye kuwa malkia.

Kwani wafanyakazi wote ambao mtawaajiri mnawapa mshahara sawa?

Inaelekea kuwa unataka kutoka kwenye maudhui!

Hapana mimi nipo kwenye maudhui yenyewe.

Bila shaka hapana, je unatarajia nimpe mkurugenzi sawa na mtumishi?!

Je unamdhulumu mtumishi unapompa kidogo ya Mkurugenzi?

Hapana, mimi nafanya uadilifu.

Na Uislamu hivyo hivyo umekuja kuweka uadilifu baina ya wanaume na wanawake, na baina ya watu wote kwa usawa, na ndio maana mwanamke akapata katika mirathi nusu ya mwanamme, na huenda ikawa ni kinyume chake. Ni juu ya mwanamme kumhudumia mwanamke na yeye mwanamke hatoi chochote, na yote hayo ndio uadilifu.

Kwa nini mke wako asitoe nusu ya matumizi ya nyumbani?

Matumizi ya nyumbani ni majukumu ya mwanamme, na yeye anapaswa kuhudumiwa.

Samahani, kama ni hivyo hakuna haja ya mwanamke kusoma au kufanya kazi.

Nani kasema hivyo?! Inabidi asome kama mwanamme, na ni haki yake kufanya kazi.

Na kuhusu mshahara wake?

Ni haki yake peke yake, na si juu yake kutoa matumizi.

Ha ha ha, kama ni hivyo kiuchumi wanawake hali zao ni nzuri kuliko wanaume.

Hapana, hawawazidi wanaume bali wapo sawa sawa, kama ambavyo maumbile yake yanatofuatiana na mwanamme, basi hali kadhalika hukumu zake ni tofauti kwa kiasi cha maumbile yake na kazi zake vile vile.

Wasifu mzuri wa uadilifu, lakini kwa upande mwingine huoni kuwa hijabu imemdhulumu mwanamke kijamii?!

Bali umemkirimu na kumtukuza.

Kwa vipi, kufungwa fungwa na mavazi ambayo yanaficha uzuri wake na uke wake?!

Vipi hali ilivyokuwa ya malkia na wana wa kike wa wafalme huko kwenu miaka hamsini iliyopita?!

Unakusudia nini?!

Jibu swali langu.

Walikuwa na haki zao kamili.

Mavazi yao yalikuaje?

Nakusudia kuwa walikuwa wakivaa kama wavaavyo wanawake wa Kiislamu leo hii?

Ndio, bila shaka katika hilo, kisha hata mavazi haya huvaliwa vile vile na watawa.

Lakini tumepata maendeleo na mavazi ya mwanamke yakabadilika.

Mavazi ya watawa hayajabadilika kwenu na nakariri hili kwa masikitiko kuwa hadhi ya kanisa imeanguka, na mavazi ya mwanamke kwenu hayajapata maendeleo bali yamerudi nyuma, tizama mashambulizi ya kijinsia, uzinifu, utoaji mimba na mfano wa hayo.

Na ninyi hali kadhalika!

Sisi ni wanadamu na tuna makosa yetu, lakini yaliyokuwa kwetu hayafikii walau asilimia ndogo kabisa ya mlionayo, na mengi yao kwa masikitiko ni ya kuwaiga.

Ki vipi?

Je utaniruhusu nitumie lugha za takwimu na tafiti mbali mbali; kwa hakika ni mpenzi wa takwimu?

Lugha za takwimu ni zenye kushawishi zaidi, vizuri kwangu.

Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa asilimia tisini (90%) ya wanawake ambao hawajaolewa hufanya uzinifu mara nyingi huko Ulaya na Marekani. Ama Marekani wanafunzi wadogo wa kike asilimia 48% hupata mimba katika shule za sekondari. Asilimia 88.8% katika wanafunzi wa kike katika shule za sekondari Marekani walishafanya tendo la ngono katika maisha yao. Miongoni mwao asilimia 22% kabla ya umri wa miaka kumi na miwili, si hivyo tu bali asilimia 60% ya watoto wanaozaliwa Sweden ni watoto wa zinaa tu.

Inatosha, hili na zaidi yake nalijua katika jamii yetu ya Magharibi, lakini hali hii ipo ulimwenguni kote! Hata nyie ni kama sisi!

Kama nilivyotaja kwa masikitiko wengi kwetu tunaelekea njia hiyo, kila mtu anavyokuwa mbali na dini basi mtu huyo anakaribia hali hii, isipokuwa tofauti ni kubwa, tena ni kubwa sana.

Unataka kuniambia kuwa watu wa dini kwenu hawaoi na kuwa watawa kama vile makasisi na mapapa?

Nimekuambia mara nyingi kuwa hatuna watu wa dini katika Uislamu, bali hata Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alioa.

Ndio, nimeshangazwa na kuoa kwa Mtume wenu! Samahani, mke wako yuko wapi?! Wewe si umeoa?!

Yupo shuleni; yeye ni mwalimu wa somo la fizikia katika shule ya sekondari, anamaliza kazi zake jioni saa kumi na mbili, muda wowote anaweza kufika.

Hebu niambie ukweli, je umemlazimisha kuvaa hijabu?!

Bila shaka hapana.

Kwa nini mnawalazimisha wanawake wa watu kuvaa hijabu wakati wa kwenu hawavai? Ni matumizi mabaya haya ya dini kuwaingilia watu katika mambo yao!

Mimi sijamlazimisha; amevaa kwa mapenzi yake mwenyewe, na nakubaliana nawe kuhusu matumizi mabaya ya dini katika mambo binafsi, hata Mtume wetu (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amekataza hilo.

Una maana kuwa amevaa hijabu bila ya wewe kumlazimisha!

Ndio.

Kitu gani kinamfanya avae hijabu?!

Dini yake na amri ya Mungu wake, kisha anajilinda mwenyewe.

Anajilinda na nini?

Ili asiwe ni mhanga wa zile takwimu zilizopita! Ha ha ha, isipokuwa kama utahitaji takwimu nyingine, kwani ninazo nyingi.

Hapana… inatosha, nami ninazo nyingi, samahani lakini kwetu Uingereza tunasikia wanawake wengi wa Misri wachezaji na waimbaji?!

Ndio, nimekuambia kuwa kila tukiwa mbali na dini kwa masikitiko tunawaiga.

Kwa nini kwa masikitiko?

Samahani, sikusudii kuwaudhi, lakini nadhani kuwa hadhi ya mwanamke kwenu inakuwa mbaya sana kiasi cha kuwafanya wengi wenye akili miongoni mwenu wananadi umuhimu wa kuangalia balaa hili linaloendelea katika jamii.

Balaa gani unalokusudia?!

Kwa nini mwanamme aoe madamu anapata ayatakayo bila kuoa? Jambo ambalo linafuta na kuharibu hadhi ya familia, na kuvunja jamii yenye nguvu zaidi duniani na kuifuta.

Nibainishie zaidi.

Je si ukweli kuwa kumlea mbwa ni gharama ndogo zaidi kuliko kumlea mtoto kwa watu wengi, je hawara gharama yake si ndogo kuliko mke wa ndoa?

Wakati huo huo maumbile yao huharibika.

Swadakta, na hili ndilo lililofikia baadhi ya jamii nyingi, je unajua kuwa kiwango cha uwezo wa kuzaa katika baadhi ya jamii imefikia chini ya mtoto mmoja kwa kila mwanamke. Jamii hizi zitakwisha na kupotea iwe ni sasa au baadaye.

Ha ha ha, na ndio maana mmezidi kwa idadi hata zaidi ya Ulaya.

Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Oeni wanawake wazuri wenye mapenzi wanaozaa.”

Hata katika maelezo kama haya Uislamu unaingilia!

Uislamu ni dini kamili katika mambo yote ya maisha; na ndio maana nafsi ya mwanadamu ikapata utulivu na kufurahi, wala upande mmoja haudhulumu upande mwingine ukapata tabu.

Maelezo ya kina kiasi gani kuhusu Uislamu! Lakini hii ni aibu na fedheha na sio sifa nzuri kuhusu Uislamu?!

Kwa vipi?!

Maelezo, haya ya kina yanamchosha mtu kufuatilia, hiki ni kifungo kingine cha maisha!

Lipi bora: Nchi inayofuata sheria kama vile Uingereza au nchi yenye kuongozwa na fujo tu?

Nimefahamu unachokusudia, lakini kanuni bora ni ile inayotoa nafasi kubwa ya uvumbuzi na jitihada.

Kama vile unatoa wasifu wa Uislamu! Kwani umetufungulia upeo mkubwa wa uvumbuzi, kutaamali na kufikiria, na mara nyingi Qur’an huwataka watu wafikiri na kuangalia mbali zaidi, historia na mienendo mbali mbali na mfano wa hayo.

Hamhofii kuwa kama watu watafikiria kwa kina watafahamu upungufu na udhaifu wa dini yenu?

Hilo ni sawa kwa dini za ardhini zilizotungwa na wanadamu na dini zilizopotoshwa tu. Ama Waislamu ni kuwa kila wanapozidisha kufikiri wanazidisha imani na yakini na kuabudu kwao kunazidi, kwa bahati mbaya kila kunapopungua kufikiri na dini hupungua.

Inanishangaza imani yenu na kujiamini kwenu na dini yenu.

Je naweza kukuuliza?

Uliza!

Kitu gani kinakuzuia usiingie katika Uislamu?! Mimi nahisi kama umeshakinaika na Uislamu!

Joji alibabaishwa na swali la Jamali na akashikamanisha vidole vyake kwa nguvu, alikumbuka alichoandika Adam kuhusu kilio cha Katarina, na haja yake ya ujasiri ili achukue maamuzi, vivyo hivyo alikumbuka aliyoyaandika John Luke katika barua yake ya mwisho. Joji alipumua kwa nguvu, kwani swali hili hili ndilo alilowaandikia rafiki zake akiwauliza, sasa kama ni hivyo anahofia nini kulijibu, je ni udhaifu au kubabaika au ni ujinga au ni kutofanya mambo kwa pupa! Sababu yoyote iwayo ni kuwa hapana budi ajijibu kabla Jamali hajamjibia. Alimgeukia Jamali:

Je utaniruhusu nisikujibu sasa hivi?

Hili ni la kwako tu, nimekuambia hivyo nikikutakia kheri tu.

Asante sana, nitakujibu siku mbili au tatu zijazo.

Huna haja na sio muhimu kunijibu, la msingi na muhimu na kujibu roho yako maswali yake, kwa bahati mbaya maisha haya ya maada yametufanya kuwa ni mashine ambayo ukifikiri unachoka, na ndio maana binadamu wanaishi kwa tabu kubwa.

Joji alishusha pumzi alipoisikia ile jumla “Utakapoijibu roho yako.” Na akakumbuka maneno ya kikongwe aliyekutana nae, kisha akasema:

Kama kwamba unanielezea nilivyo:

Samahani sijakusudia kukukera, lakini hii ndio hali ya wanadamu wanapomwacha Mwenyezi Mungu, Allah amewasema: “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” (20:124) na “Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni.” (6:125).

Maneno gani mabaya uyasemayo?

Samahani sikukusudia ubaya lakini hii ni sifa tu, bali ubaya zaidi upo kumpa mgongo Mwenyezi Mungu, na hiyo sio hali ya sasa hivi tu bali ya maisha yote!

Una maana gani?

Watu wengi huyakimbia maisha yao kwa njia nyingi mbali mbali; kuna wengine wanayakimbia kwa kunywa pombe na starehe, na watu wengine wanayakimbia kwa kufuata ushabiki wa kidini kwa sababu hushibisha kiasi cha njaa yao ya kiroho, na wengine wanayakimbia kwa falsafa kavu, na wengine hukimbilia pasipo julikana; ili wakwepe kufikiria maudhui hayo, kwa mara ya mwisho ninakuambia: Kitu gani kinachokuzuia na mapenzi ya duniani na akhera?

Nimekuambia nitakujibu baada ya siku mbili au tatu.

Walipokuwa wakijadiliana mara wakasikia sauti ya mlango unafunguliwa, Jamali aliomba ruhusa kwa Joji.

Samahani, mke wangu Aisha amefika.

Je utaniruhusu nizungumze nae kidogo?

Inabidi nimshauri na kuchukua rai yake.

Katika nini?

Najua hapendi kuzungumza na wanaume, sipendi kumlazimisha kitu ambacho hakipendi.

Jamali alitoka chumbani, alimuacha Joji katika hali ya mshangao, kilichotokea leo hii ilikuwa ni mtetemo wa nguvu, alihisi nafsi yake ikiwa imepotea na hajui afanye nini, alijiuliza siku nzima, nini kilichomfanya aende Misri? Na maswali yangu yamenifanya kujiuliza: Ninataka nini? Kwa nini ninaishi? Kwa nini tabu yote hii, Ah aah. Jamali alitoka chumbani, alimuacha Joji katika hali ya mshangao, kilichotokea leo hii ilikuwa ni mtetemo wa nguvu, alihisi nafsi yake ikiwa imepotea na hajui afanye nini, alijiuliza siku nzima, nini kilichomfanya aende Misri? Na maswali yangu yamenifanya kujiuliza: Ninataka nini? Kwa nini ninaishi? Kwa nini tabu yote hii, Ah aah.
Alipokuwa mbali kuyafikiria maswali yake, Jamali aliingia akiwa na mke wake, aliponyanyua uso wake akamuona kuwa ni mwenye Hijabu hakikudhihiri kitu kwenye uso wake ila sehemu ndogo tu.

Huyu ni mke wangu, unataka nini?

Jamali ameniambia kuwa unataka kuingia katika Uislamu, na ya kuwa una maswali kuhusu hadhi ya mwanamke katika Uislamu.

Sikusema kuwa nataka kusilimu kabisa, bali nataka kufahamu tu hadhi ya mwanamke katika Uislamu?!!!

Kama hutaki kusilimu; kwanini basi unataka kufahamu hadhi ya mwanamke katika Uislamu?!!

Kufahamu tu.

Maarifa yasiyomsaidia mtu hayana thamani, na elimu ambayo haimnyanyui mtu mwenyewe ni upotevu, elimu inapelekea katika kumwogopa Mungu ndio maana Mungu akasema:

“Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni.” (36:28)

Nakusudia kuwa nilikuwa nataka kuujua tu, je maarifa na elimu hivi hivi tu ni kosa kwenu?!

Kwetu sisi elimu ambayo hailingani na matendo haina thamani, na nadhani kuwa kufanya upuuzi tu na kukosa malengo ni maradhi ya akili na dini, mnajua vizuri.

Unakusudia nini unaposema, ‘Kwetu sisi?!’

Nina maana kwetu sisi Waislamu, niache niingie pale utakapo kwani mimi nina hakika huulizi tu isipokuwa kwa lengo la kutaka kuwa Muislamu.

Una hakika gani kusema hivyo?!

Nataraji lisikukere, Mwenyezi mungu anasema: “HUENDA ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu.” (15:2). Hakuna mtu mwenye akili ambae hajampwekesha Mwenyezi Mungu na kujisalimisha kwake ila katika nafasi yake atapata kitu chenye kumkereketa kutokana na migongano ya matamanio yake na dini nyingi zilizopotoka.

Unakusudia nini kusema: Mwerevu?!

Mtu mnyonge, dhaifu wa kufikiri anaweza kuruka juu na akaacha migongano ya maisha yake na dini yake na maswali mbali mbali kutoka moyoni mwake akaelekea kwenye mambo ya pembeni yasiyokuwa ya msingi, lakini…

Lakini nini?!

Lakini Jamali ameniambia kuwa wewe ni mwerevu mno, kama alivyoambiwa na nduguye Baasim na kama alivyoona yeye mwenyewe.

Ahsante.

Tuingie katika maudhui yetu, “Mwanamke katika Uislamu.” Unataka tuanzie wapi?

Anza popote unapotaka, nami nitakuuliza maswali muda ninaotaka.

Uislamu ulipokuja Waarabu walikuwa wanazika watoto wao wa kike hai na kuwaua.

Mwisho wa ujinga na unyama!

Swadakta, lakini hali hii ambayo ilikuwa inatia kichefuchefu haikuwa ya Waarabu peke yake, kwani kulikuwepo na mabaraza ya wanafalsafa yakifanya vikao ili wajadili mambo muhimu sana! Je mwanamke alikuwa na roho kama mwanamme? Je ana roho ya kibinadamu au roho ya mnyama?! Walikuwa wanahitimisha mijadala yao ya kuwa mwanamke anayo roho lakini ipo daraja ya chini zaidi kuliko roho ya mwanamme. Ama Waroma mwanamme alikuwa na madaraka kwa mwanamke ima amuuze mke wake au ampe talaka, amkubali mwanae au amkatae, na mwanamke kwa Wagiriki alikuwa hana haki ya kurithi kamwe.

Kwa masikitiko kabisa, umesema kweli, historia chafu kabisa!

Dini zote za mbinguni zimeleta uadilifu kwa mwanamke, lakini Mayahudi wamepotosha kitabu chao, kikawa kitabu chao kilichopotoka kimejaa mambo ya kufikirika kuhusu ngono na dhulma yenye kuchukiza na chungu kwa mwanamke.

Levi amenielezea haya yote, na nimesoma mambo mengi kama haya.

Levi ni nani huyo?!

Mwanamke wa Kiyahudi mwenye heshima sana.

Ni kiasi gani napenda afurahi na akirimiwe na Uislamu.

Hapana, sidhani, hata hivyo endelea.

Funguo za mioyo ipo katika mikono ya Mungu, tukamilishe na Ukristo ukapotoshwa vile vile, na kwa masikitiko Ukristo nao umejaa dharau kwa mwanamke.

Mfuatano mzuri.

Baada ya hapo Uislamu ukaja; ukamkirimu mwanamke ambapo hakuna dini iliyomtukuza mfano wake, hakikupotoka chochote chake; Mwenyezi Mungu pekee ndie aliyetoa dhamana ya kukihifadhi.

Inakinaisha na kushawishi kuwa Uislamu haujapotoshwa, na nina maswali, lakini ningependa ukamilishe kwanza.

Mwanamke ulimwenguni hakuhisi utukufu kama alivyokuja kuhisi pindi Uislamu ulipokuja. Ulaya ilipoingiliana na Waislamu ikajifunza kitu katika kumtukuza mwanamke, walijifunza uadilifu na elimu mbali mbali, lakini ikapambana na upotofu uliopo kwenye vitabu vyao vitakatifu na mafundisho ya Kanisa. Kwa bahati mbaya hawakusilimu, na hivyo basi kutafuta mfumo wa kumtukuza mwanamke ambapo akili zao ziliwaelekeza kudai usawa.

Kwa maana hiyo akili ya mwanadamu imekuwa juu kuliko akili za dini nyingi?

Bila shaka hawakuweza kubadilisha maumbile yake na tabia yake na majukumu yake ili yalingane na usawa huo wanaodhania, hivyo basi wakaamua kumpa majukumu ya kazi kama ya mwanamme pamoja na kazi zake kama mwanamke! Cha kushangaza na ajabu ni kuwa anafanya kazi kama mwanamme pamoja na kazi zake kama mwanamke kwa mshahara nusu au robo! Laiti wanaume wangeacha kupunguza ujira wake na kumkalifisha asiyoyaweza. Hayakuwa hayo tu bali walimtumia na kuchukua kutoka kwake bila ya ndoa, na hivyo kubadilika kutoka kuwa ni mke anayeheshimiwa na kulindwa na kuwa ni hawara mwenye kutumiwa hovyo na hizo taasisi za usawa na haki za binadamu zikapeperushwa na zikaja karibu kubadilisha hali hii mbaya. Katika hali hiyo zikataka na kudai usawa katika malipo na mishahara, juu juu wakaonekana wamefanikiwa lakini ukweli hawakuwa wamefanikiwa, na waliweka masharti ili mume asiweze kuchukua haki za mke wake, wakagundua kuwa ambae anachukua haki zake sasa amekuwa ni hawara bila hata mafungamano yoyote ya kisheria.

Unachokisema hakifanyiki nchi zote za Magharibi.

Ndio, hutekelezwa sehemu kubwa tu, ingawa bado kuna wengine ambao maadili yao yanawakataza katika mambo kama haya, lakini balaa zaidi ni kuwa yanamtetea kwa jina la usawa, wakati mwingine kwa jina la starehe na kwa jina la uhuru kutokana na utawala wa mwanamme ili awe huru zaidi kiasi cha kumfanya kufikia kiwango ambacho mnyama atastahi wala hatoridhia kwa nafsi yake.

Unakusudia nini?!

Samahani kama maneno yangu makali au kuonekana kama nimewadhalilisha, lakini ninachomaanisha ni kuwa mwanamke kwa masikitiko amekuwa kama ni chombo cha kuchezea tu na kukiharibu kwa jina la usawa na kuchukua haki zake, vinginevyo utawezaji kufasiri kuwepo kwa chaneli mbali mbali za ngono na filamu chafu na biashara ya ngono?

Inaweza kufasiriwa kuwa ni aina ya kushangazwa na kiumbe huyu mzuri!

Hivyo unakiri kuwa kiumbe huyu mzuri anatofautiana na mwanamme, na usawa baina yao ni kumdhulumu mwanamke na kumdhulumu mwanamme. Ama mimi nafasiri kuwa mwanamke katika jamii hizi baada ya kunyang’anywa haki zake za kiuchumi, na baada ya kuanza kufanyakazi zake anazotakiwa kama mwanamke na zile anazolipwa katika kufanyakazi akaibiwa tena haki zake za kibinadamu na kufanywa kama ni bidhaa ya kuchezea, vinginevyo tutafasiri vipi kuachwa uchi au nusu uchi katika uso wa maduka mengi katika nchi nyingi, kama vile ziwekwavyo bidhaa, samani au magari!

Matendo haya ni mabaya sana lakini hayawakilishi jamii zetu kamwe.

Kwa uchache ni matendo ambayo yamewekewa sheria na taasisi, na hijabu kwa wanaoamini lakini inakatazwa kisheria vile vile hivyo basi serikali au sheria ndio ambayo inaruhusu mwanamke kuwa ni bidhaa ya kuuzwa na kununuliwa na haimruhusu mwanamke wa Kiislamu kuvaa hijabu.

Mimi vile vile sikubaliani na matendo hayo ya dhulma yanayofanywa na baadhi ya nchi za Ulaya.

Kwa maana hiyo wewe ni gaidi kwa vigezo vyao, nisameheni nimerefusha lau kama sio mume wangu kutaka hivyo ili huenda nikawa ni sababu ya kusilimu kwako basi vinginevyo nisingefika huku.

Nina baadhi ya maswali ya haraka haraka, nimewauliza watu wengine lakini ningependa nijibiwe na mwanamke.

Karibu, uliza.

Wewe ni mtaalamu wa fizikia, yaani elimu ya kisasa ambayo imewajia kutoka kwetu na ikanyanyua viwango vyenu, pamoja na hayo unavaa hijabu, kwani umelazimishwa kufanya hivyo?! Au ni kama vile hijabu ya watawa kwetu ambao uvaaji wao hauna maana ya kujihifadhi lakini ni mavazi tu kwa desturi zao?! Au ni kwa sababu mnaishi katika jamii yenye matamanio ambayo huna budi kuvaa mavazi ya aina hii vinginevyo utakuwa ni muhanga wa kushambuliwa na wanaume?! Au nini?!

Ha ha ha, kwanza “Elimu au sayansi ni urithi wa wanadamu; kabla ya elimu hizi za kisasa kuja kutoka kwenu ziliwajia kutoka kwetu mlipokuwa kwenye kiza kinene. Ama kuchukuliwa, kunyang’anywa na kushambuliwa na wanaume wewe unajua kuwa kuna mahusiano ya moja kwa moja na suala la kwenda uchi, ukitaka takwimu ambazo zinaunga mkono hilo tutazungumzia, ama kwangu mimi ninavaa hijabu kwa ajili ya kufuata dini na kwa elimu niliyo nayo ni kuwa hiyo ni katika furaha ya dunia na akhera. Hapa duniani utapata furaha na utulivu na akhera fadhila na utukufu kutoka kwa Mtukufu Aliyetukuka.

Daima mnarudia rudia maneno, furaha ya duniani na akhera.

Ndio, furaha haijui ila yule aliyeijaribu.

Huenda ikawa hivyo, lakini je utaridhika kama Jamali atakuolea mke mwingine kama alivyofanya Mtume wenu?!

Aisha alimuangalia Jamali aliyesimama pembeni yake kimya, kisha akaendelea:

Sidhani kama Jamali atafanya hivyo, na natamani asiniolee.

Lakini Mtume wenu alioa wake wengi?

Ndio ameoa wake wengi, na mmoja wa wake zake ni Mama wa Waumini jina lake kama langu Aisha.

Kama ni hivyo kwa nini hutaki Jamali amuige Mtume wenu na kukuolea?!

Uislamu haukunitaka mimi ila niwe mwanamke, na haki yangu ni kuona wivu, wala haukunitaka kuwa dhalili siwezi kujieleza na mahitajio yangu na ninayopenda, lakini nina yakini kuwa kuoa wake wengi ni bora kuliko kuwa na hawara wengi.

Na kutooa mke zaidi ya mmoja ni bora zaidi.

Naamini kuwa kuna haja kama ni sehemu ya maumbile ya baadhi ya wanaume kuoa zaidi ya mke mmoja. Kuoa wake wengi hakupo kwa Waislamu peke yao tu, bali katika dini zote takriban, tofauti kubwa iliopo ni kuwa katika dini zilizotangulia hakuna idadi maalumu. Nabii Sulaiman alioa wake elfu moja, Adam alioa wake kumi na tatu, Dawud alioa wake tisini na tisa, katika Uislamu kuna idadi maalum, yaani wasizidi wake wanne tu.

Sisi kwa sasa hatukubali wake wengi na mifumo yote, sheria na serikali imekataza.

Kitabu chenu kitakatifu kina mifano mingi ya wake wengi, watu wa dini wamechoshwa na tafsiri hiyo, baadhi yao wamesema: Haya ni makosa ya wanadamu na wakazungumza juu ya manabii. Wengine wakasema: Ilikuwa ni haja tu ya kihistoria kwani kulikuwepo na vita vingi sana na wanawake walikuwa ni wengi sana na wanaume ni wachache, wameacha ukweli ulivyo sasa kuwa vita ni vingi hivi sasa. Wakatokezea wengine wakasema: Bali Mwenyezi Mungu amelirudi hilo (Mungu atusamehe kwa hilo) Na hivyo kumfanya Mungu mpungufu hajui haki ametakasika kwa wanayo yasema.

La msingi ni kuwa sisi tumeiendeleza dini yetu na kanuni zetu; ili kukataza watu kuoa wake wengi.

Nzuri “Tumeendeleza dini yetu.” Kwa asili ni kuwa dini ya kweli inafaa kwa zama na mahala pote wala haihitaji kuendelezwa ila kitu kilichokuwa na upungufu tu;

“Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.” (5:3) Sisi hatuiendelezi dini yetu; kwa sababu dini yetu imekamilika.

La msingi tu ni kuwa tumeendeleza mifumo yetu, kanuni zetu ili tusiruhusu wake wengi kwa dhulma.

Ndio katika nchi nyingi za Ulaya na Amerika mmekataza wake wengi katazo zuri lililokuwa wazi, na mkaruhusu mahawara ruhusa pana.

La msingi sisi tumekataa wake wengi.

Na hata maisha yaende vizuri kwa kufuata tabia ya mwanadamu na ya kijamii kufuata haja ya baadhi ya wanaume zaidi ya mke mmoja mkaruhusu hawara zaidi ya mmoja, bali lililo la hatari zaidi ni kuwa baadhi za nchi zimeruhusu waume wengi badala ya wake wengi na kuruhusu ndoa nyingi na kukataza wake wengi. Bila ya shaka umemtukuza mwanamke awe na waume wengi na sio kuwa na hawara.

Vizuri, lakini elimu hii ya kisasa ambayo umesoma na kufundisha huenda ikawa inapingana sana na dini yenu!

Elimu ipo kinyume na dini yetu! Wewe hujui dini yetu au hujui chochote kuhusu sayansi! Kwa hali yoyote ile Jamali anajua zaidi yangu kwa uhusiano wa dini na sayansi. Mimi nimeombwa nizungumze kuhusu mwanamke tu, na sikutaka kufanya hivyo ila aliponiambia kuwa kufanya huku utakuwa umefanyia kazi dini; naombeni ruhusa nataka kufuatilia masomo ya mwanangu.

Aisha alitoka, Joji akamgeukia Jamali huku akitabasamu.

Nakupongeza kwa mke ulie nae, ila anafaa kuwa mwanamme na sio mwanamke.

Ha ha ha.

Una nini? Mbona unacheka?!

Kumbe unajua mwanamke sio mwanamme sasa kwa nini mnalingania usawa?! Niamini hakuna aliyekuwa mpole kuliko yeye wala zaidi mwenye huruma kuliko yeye, yeye ni mtu wa dini; na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amemuusia anitii.

Kwani Mtume wenu hakuwausia umfanyie wema?

Bali ameusia kwa kusema: “Mbora wenu ni mbora wenu kwa familia yake na mimi ni mbora wenu kwa familia yangu.” Bali ametaja kuwa yeye ni mbora wa watu wa familia yake, nimefurahishwa na mjadala wako, lakini nataka kwenda kuswali alasiri.

Sasa hivi ni saa kumi na nusu, ikiwa ni sawa kwako tutoke pamoja usali, nami nitembee Cairo kwa muda wa saa moja hivi, kisha twende kwa Mustafa kwani amenialika chakula cha usiku na sijui kwanini.

(4)

Joji alibaki garini akimsubiri Jamali amalize kusali, baada ya kumaliza sala akawa anawaangalia watu mbali mbali waliosali nje ya msikiti, alimuona mtu mmoja mwenye sura ya Kizungu na akamuashiria, na akamfuata, akamjibu kwa kiingereza kibovu:

Karibu, mimi ni William, wewe unatokea wapi?

Mimi ni Joji kutoka Uingereza.

Na mimi ni kutoka Ujerumani.

Lakini ulikuwa ukisali pamoja na Waislamu!

Ndio mimi ni Muislamu wa Ujerumani.

Kutoka Ujerumani au ni Mmisri unayeishi Ujerumani?

Nusu ya Waislamu Ulaya ni wenyeji wa huko na mimi ni mmoja wao, idadi ya Waislamu Ujerumani ni milioni nne, yaani ni karibu ya asilimia tano ya wakazi wote.

Najua hilo, waislamu kwetu Uingereza ni zaidi ya milioni mbili, yaani asilimia tatu, lakini swali langu ni je wewe ulikuwa ni Mkristo?

Baba yangu na mama yangu walikuwa Wakristo, ama mimi nilikuwa mkana dini, namshukuru Mwenyezi Mungu kisha nikasilimu, nikawa mwenye furaha na mimi nipo hapa kuusoma Uislamu.

Nini kilicho kufanya ukawa Muislamu?!

Ni swali nililokuwa nikijiuliza mara kwa mara, ninaweza kufupisha mvuto wangu kwa Uislamu katika utafiti wa maneno matatu, nayo ni: Ukweli (hakika), furaha na uadilifu.

Je umeupata katika Uislamu?! Kwa vipi?!

Ndio nimeupata, ukitaka maelezo zaidi unaweza kunitembelea baadae, kwa sasa naomba radhi kwani nina ahadi pamoja na mmoja wa marafiki zangu, na hii ni kadi yangu, kuna maelezo yote kuhusiana nami.

Asante sana, samahani kukusumbua.

Joji alirejea kwenye gari na kumkuta Jamali akimsubiri.

Umerudi muda gani?

Nimekuona ukiongea na mtu, sikupenda nikukate, la msingi ni kuwa hivi sasa ni saa kumi na moja unusu, je tumebaki na muda gani kabla ya ahadi yako na Mustafa?

Saa nzima takriban, ukweli ni kuwa nimechoka sana na ningependa kwenda hotelini kupumzika, lakini Mustafa aliipa umuhimu sana kwa sababu ambayo siifahamu; na nikampa ahadi ambayo sitaki kwenda kinyume nayo.

Vizuri sana, Qur’an pamoja na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) wamehimiza sana kutekeleza ahadi, huenda katika hilo kuna kheri, nashauri muda wa saa moja iliyobakia tukapumzike katika matembezi ya boti kwenye mto Nile, kwani miadi yenyewe ni karibu na mto Nile.

Fikra nzuri.

Walikwenda Nile, wakakodisha boti kwa muda wa saa nzima hivi, wakaanza matembezi yenye utulivu ambapo Joji alihisi kupumzika na kupata utulivu, kadhalika akahisi kuwa maarifa mengi aliyoyapata kwa ghafla tu yameanza kujipanga yenyewe kichwani mwake, kisha walipomaliza wakaelekea kwenye miadi ya Mustafa.

Nakushukuru, matembezi haya yalikuwa ni mazuri sana na kwa wakati wake.

Inshallah utakuwa umepumzika kidogo.

Ndio, isipokuwa tabu na msukumo wa maswali unaniandama kila ninapopumzika.

Maswali gani?

Je naweza kukuuliza swali?

Karibu, uliza.

Je wewe huwa unajiuliza kwa nini umeumbwa?

Bila shaka … mara nyingi…

Utaijibu vipi nafsi yako? Au utalitoroka vipi swali hili?

Kwa nini nilitoroke na mimi nina majibu yaliyo wazi?

Ni jibu gani hilo?

Anasema Mungu Aliyetukuka: “Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” (56:51)

Unakusudia kuwa mimi ni kiumbe kwa kusali na kufunga tu!

Hapana, wewe ni kiumbe wa kufanya ibada kwa maana yake pana, na haikuwa swala na kufunga ila ni mafungu muhimu tu ya ibada.

Vipi?

Ibada inakusanya kila kitu katika maisha yetu; haifanyiki katika siku maalumu tu au katika sehemu fulani tu au katika umri fulani, bali Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ametufundisha kuwa hata kama mume atamwingilia mke wake na kustarehe nae, basi mtu huyu atapata malipo.

Ehe, vipi?

Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ametubainisha hilo kwa kusema: “Je, ingekuwa anafanya hivyo kwa njia ya haramu angepata madhambi, vivyo hivyo akiweka katika halali atapata ujira pamoja na kumsafishia nia Allah (Subhaanhu wa Ta’ala). Hivyo basi maisha yote ya mwanadamu yamekuwa ni kwa ajili ya Allah (Subhaanhu wa Ta’ala): Swala na ibada zangu, bali uhai na umauti; kama alivyosema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala); “Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.” (6:162).

Kwa nini tunaishi?

Ninaweza kukujibu kwa jibu lililotangulia na ni kuwa mkweli, ninaweza kukuambia: Kwa ajili ya kuimarisha ardhi na maisha na kuyastawisha, na uhakika ni kuwa kuimarisha ardhi na maisha na kuyastawisha ni katika ibada zilizo muhimu sana, Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) amesema: “Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo.” (11:61)

Kwa masikitiko tumeshafika, ila mjadala wetu tuukamilishe kesho, nitakusubiri saa nne asubuhi; mimi ninataka kupumzika kidogo na ahadi yangu ni saa tano pamoja na shirika la mwisho.

Sawa, tumekubaliana.

Joji aliingia kwa Mustafa, ambae alimkaribisha.

Kila kitu kiko tayari, chakula cha usiku kitakuwa katika moja ya hoteli, na wote wanatusubiri huko.

Vizuri.

Inaelekea umechoka, tumekutayarishia kitakacho kuchangamsha na kukuburudisha na kukurejeshea uhai wako, uchangamfu wako, kwa masikitiko ni kuwa sisi Wamisri tunasahau pindi tunapotembelewa na marafiki zetu kutoka Ulaya kuwa maisha ya Wamisri hayawafai watu wa Ulaya.

Vipi?

Mimi nimesoma Chuo Kikuu Marekani nayajua maisha yenu vizuri sana, utaona leo hii kitakachokufurahisha.

Katika moja ya hoteli Mustafa alisimamisha gari lake, na akatembea katika maingilio ambayo taa za rangi rangi zinawaka, kulikuwa kuna muziki ukienea kila sehemu, Mustafa aliweka mkono wake katika bega la Joji na akamkaribia ili aweze kumsikia.

Tuna jukwaa letu maalum lenye kututosheleza.

Walifika sehemu hiyo waliyotayarishiwa akakutana na wanawake wanne alioonana nao asubuhi kwenye usaili wakimsubiri.

Nadhani umeshafahamiana nao asubuhi, nimewaleta hapa ufahamiane nao kwa ukaribu zaidi, huyu ni Samira na huyu ni Manal na Aisha na Diana.

Samira alimpa mkono huku akitabasamu, Joji nae akampa mkono na kutabasamu, kisha akawapa mikono wengine waliobakia na kukaa.

Nakukumbusha, mimi ni Manal na umri wangu ni miaka ishirini na nne, nimekuja kukuhudumia.

Vizuri kila mmoja ajitambulishe kama Manal alivyofanya.

Mimi ni Samira Nudhmi umri wangu ni miaka ishirini na tatu, nimekuja kukufurahisha.

Mimi ni Aisha Khalid umri wangu ni miaka ishirini na tano, nimekuja kwa ajili yako.

Na mimi ni Diana Saamih umri wangu ni miaka ishirini na tano.

Vizuri karibuni, na mimi ni Joji na umri wangu unakaribia miaka arobaini.

Mustafa aliamka kutoka kwenye kiti chake.

Nawaombeni ruhusa nitakuja baada ya muda kidogo, Joji furahia muda wako.

Kikao hiki kwangu ni cha ghafla, sijajua kuwa kama tutaonana hapa.

Mustafa ametuambia atatutoa sisi kama ni zawadi kwako.

Sijafahamu.

Wewe uko peke yako, na sisi tumekuja kwa ajili yako.

Aha, nimefahamu, na kwa kiasi gani nyie mmejitayarisha kunihudumia na kunifurahisha?

Ha ha ha, kwa kiasi kikubwa.

Taka utakacho na utaona mipaka ya utumishi.

Joji alinyamaza akiangalia nyuso za wale wasichana wanne, ni wazuri kabisa na tabasamu zao zilimfitinisha katika kiasi kikubwa na kumvutia, lakini alikuwa akihisi kichefuchefu, akaamua kuvunja ukimya na kuzungumza nao.

Nitawaomba baadhi ya vitu, nitaanza na Aisha.

Mimi ni rehani kwa ishara yako.

Nina Swali: Je jina lako silo jina la mke wa Mtume wenu?

Ndio, kwa nini unauliza?

Hivyo basi sina shaka kuwa unamuiga kwa metendo yako yote?!

Kwa nini swali hili? Omba utakacho nami nitaitikia wito wako.

Ombi langu ni unijibu…

Nigeukie mimi, mimi ni Samira Mkristo, unataka nini kwa maswali haya ambayo yana mjeruhi rafiki yetu?

Unamtetea?

Ndio, rafiki yangu, na ni haki yangu kunyanyua maswali yako yanayojeruhi.

Unamtetea ili umuondoshe na hali hii, na wewe unamuona kuwa yeye ni kafiri wa motoni katika Jahannamu, kwani Masiya hakumkomboa na madhambi yake!

Mimi ni Mkristo lakini kwa hakika ni Msekula sijali isipokuwa ni elimu na matokeo yake.

Kwa sababu unapenda elimu kama unavyosema; hukukamilisha masomo yako ya sekondari achilia mbali ya chuo kikuu, na uwezo wako wa kipekee (fani yako) ni uzuri tu!

Je unataka kuujaribu uzuri huu? Au kuonja au kuufurahia?!

Huenda, lakini nina ombi, sio hicho ufanyacho kinagongana na Ukristo?

Nimekuambia kuwa mimi ni Msekula.

Unakusudia mpinga Mungu na dini?.

Si neno, sijui tofauti zake.

Lakini kuuonja uzuri wako si kunapingana na sheria na mfumo wenu na tabia njema?

Sisi tunajua kuhusu sheria za hapa kuliko wewe, na suala la tabia ni la kiwango tu.

Ki vipi?

Linaloonekana kuwa ni kinyume cha maadili kwa mtu fulani, kwa mtu mwingine ni maadili ya hali ya juu.

Wala hakuna misingi kamwe?

Msimamo wangu pekee ni maslahi yangu tu.

Huu ndio msingi wangu, wengi katika wakanao dini ni watu wa maslahi tu.

Na je sasa unataka kujua furaha ili uonje uzuri?

Swali langu sasa ni kwa Manal.

Sihitaji maswali yako, tunalolifanya sasa ni fedheha na kilichotusukuma ni haja zetu na Mustafa mtu mbaya sana, Aisha simama tuondoke.

Sasa kwa nini mnasimama?

Aisha aliondoka na Manal, na ukimya ukaenea na sauti ya muziki iliyokuwa juu ikaenea sehemu ile, ukimya ule ulivunjwa pindi alipofika mhudumu.

Mustafa ametaka niwaletee vinywaji vya kupasua roho, lakini ameniambia kuwa mnipe uchaguzi, sasa mnataka nini?

Samahani, mimi sinywi.

Hunywi! sasa kwa nini umekuja na hawa watoto wazuri, kwa kila hali ni kuwa hafla ya kucheza itaanza baada ya nusu saa, na Mustafa ameniambia kuwa nikujulishe kuwa yeye amewaacha ili upate muda wa kustarehe kwa wakati wenu. Yeye atakuja saa mbili unusu ili aone umahiri wako katika kucheza, ukibadilisha rai yako na ukataka kinywaji basi niashirie nitakuja.

Hunywi! Wewe sio Mkristo wala sio Mzungu! Nilikuwa nataraji uwe laini katika kuutumia uzuri huu baada ya kunywa!

Kwa nini? Kwani ni lazima Mkristo kunywa?!

Kwa kiasi fulani hata maaskofu hunywa kwa ajili ya ibada na wanaamini kuwa ni kinywaji kitakatifu.

Je na kwa Mzungu kuna ulazima gani?

Kwa ujumla ndio, Wazungu hawafanani na Waislamu siasa kali, Mustafa alipata shida kumkinaisha Aisha na Manal waje, na sasa majibu yako haya yamewavunja sana na huenda yakawafanya wawe Waislamu wa siasa kali.

Ooh, yaani mimi ndio nimekuwa nautangaza Uislamu wa siasa kali?!

Diana pekee ndie aliyekuwa kimya na hakuzungumza hata herufi moja muda wote wa kikao. Joji alimgeukia huku akishangazwa na hali yake, kwani yeye pekee ndie aliyevutiwa nae asubuhi, pekee ndie mtaalamu wa fani ya kompyuta.

Na vipi kuhusiana nawe? Wewe uko peke yako!.

Kwa nini mimi tofauti na wao?

Msomi na mkimya!

Lakini mimi ni sawa na wao tu, ni bidhaa tu na zawadi tunayokupa.

Kwa nini nawe umekubali kuwa ni bidhaa?

Ili kuikimbia nafsi yangu.

Kwa vipi?

Mimi nimechoka sana na ni mgonjwa, usia wa mjomba wangu kwa Mustafa ni kunitoa kwenye msongo na fundo la nafsi kwa kufurahi na kustarehe.

Na wewe nini rai yako?

Ningekuwa najua maana ya maisha ningekuwa na rai! Lakini ni kama vile Pia katika upepo wa maisha yananigeuza bila ya maana, na huenda tabia ya mjomba wangu ya kuratibu jambo hili pamoja na Mustafa ni bora kwangu!

Ni bora ukayakimbia maisha yako na kupoteza umri wako na kugeuka kuwa bidhaa?!!

Huenda ukawa hujui maana ya kupotea na kupoteza malengo, vinginevyo msingeniambia hivyo, bora kujinyonga kuliko hali niliyo nayo.

Lakini ninyi kwa dini yenu mnajua ni kwa nini mnaishi? Na kwa nini mmeumbwa?

Mimi sijui na nitashukuru kama utaniambia.

Rafiki yangu Muislamu leo hii ameniambia kuwa mmeumbwa kumuabudu Allah, na kwa maana ya kifalsafa ni vizuri kuabudu.

Lakini mimi ni Mkristo Muorthodoksi na sio Muislamu.

Waislamu wawili wameondoka, na sasa inawezekana ukafurahi zaidi; muda wa kuanza kwa hafla umekaribia.

Kwa sababu nyie ni Wakristo wawili kama mimi, nakubaliana nanyi tufurahi usiku huu lakini kwa sharti la Diana kunikinaisha.

Kukukinaisha na nini?

Unanikinaisha kuwa furaha ni katika kufurahia uzuri wako, na kunywa pombe na kusahau dunia na kuyakimbia maisha ya uovu kuelekea neema ya kusahau.

Samira anaweza kukukinaisha zaidi kuliko mimi.

Sharti langu ni kuwa wewe Diana unikinaishe.

Samira ni katika wasichana wazuri hapa Misri, nae ni mchezaji mahiri atakusahaulisha dunia yote, haswa akinywa, je umekinai?!

Nimeanza kikinai, lakini kwa nini useme Samira, unaonaje kama nikitaka kunywa pamoja nawe kwanza kisha nicheze nawe?

Pamoja na kuwa sijawahi kunywa maishani lakini nimekubali, mimi nahisi dhiki kubwa sana, napenda kuondokana na maswali haya yanayoangamiza maisha yangu.

Maswali gani hayo?

Maswali mengi ya kila mara tokea muda mrefu kuhusu sababu ya kuwepo, na kuumbwa, na maana ya maisha, na mfano wa hayo.

Je unaamini kuwa kunywa kwako, kucheza kwako au hata matendo yako ya kijinsia yanaweza kukusahaulisha maswali yako?

Kwa uchache na kwa muda mfupi, mimi nipo tayari kwa uyatakayo; hivyo siongezi au kurefusha maswali yako yenye kuchosha.

Mimi ni kama wewe nimechoshwa na maswali, lakini nimekinaishwa kuwa kuyakimbia ni mfumo wa wapumbavu, na kilicho sahihi zaidi ni kukabiliana nao na kujibu maswali hayo.

Nami hali kadhalika.Nimechoka.

Wewe ni mzuri, mwenye adabu na msomi na akili yako inafanya kazi, usiharibu uzuri wa mambo yote haya kwa uzuri tu wa kiwiliwili chako.

Mimi nitaondoka sasa hivi, asante sana kwa nasaha zako na udhalilishaji ulionizawadia, kisha akasimama na kuondoka.

Nimebaki mimi na wewe tu, na mimi nipo tayari je unapenda tucheze na tustarehe hapa au hotelini kwako?

Yuko wapi Mustafa?

Mustafa ametuacha ili tustarehe pamoja, haya.

Haya twende.

Joji alisimama pamoja na Samira, pindi Samira alipokuwa anaelekea jukwaani kucheza Joji aligeuka na kuelekea mlangoni ili atoke, alipotaka kutoka mara alimwona Mustafa akiwa amesimama huku amemshika msichana, alimtupia macho haraka haraka na akageuka akitoka nje.

Joji nisubiri, una nini rafiki yangu?

Hamna kitu, nimechoka na ningependa kwenda hotelini kupumzika.

Njoo panda ili nikupeleke.

Vizuri, haraka ikiwezekana.

Nini rai yako kuhusu wale wasichana?!

Ni wazuri mno.

Nimekuacha ili upate wasaa wa kufurahi nao.

Nimefurahishwa nao kiasi cha kutosha.

Ni nani aliyekufurahisha zaidi?

Wote, je wewe ni Muislamu?

Ndio, na jina langu ni jina la Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam).

Ni fedheha kwa Waislamu!

Unasema nini?

Hamna kitu, wewe ni Muislamu kama rafiki yangu Jamali lakini unatofuatiana nae sana.

Nimekuambia kuwa yeye ni siasa kali na mimi nimesoma nje na nimefunguka zaidi.

Naomba ufanye haraka kwani najihisi kuchoka sana na ninataka nifike hotelini haraka.

Ahadi yetu kesho saa ngapi?

Hatuna ahadi kesho; nina shughuli nyingine, nitakupigia simu.

Joji alifika hotelini nae akipiga mikono yake makofi akishangazwa, siku ilikuwa ndefu kwake, siku iliyojaa migongano na mambo ya kushtukiza. Alijihisi mzito, alipofika tu alijitupa kitandani, hisia ya woga wa maswali yake ilimjia kwa nguvu, alimkumbuka Diana msomi aliyevamiwa na shaka kama yake, akakimbilia starehe (ili ajisahaulishe) kisha, akakumbuka swali alilowatumia rafiki zake, na swali hilo hilo aliulizwa na Jamali leo hii: “Nini kinachokuzuia kuingia katika Uislamu?
Aliendelea katika kufikiri na hakuhisi chochote ila ilipotimu saa mbili unusu asubuhi, alipoamka kutoka usingizini na kujikuta kuwa alilala pamoja na nguo zake akiwa katika hali ya kusikitisha.