MABADILIKO

MABADILIKO

MABADILIKO

(1)

Joji alienda mgahawani kukutana na Adam lakini hajamkuta, alimuuliza mhudumu na kumjibu kwamba leo hajafika na yeye hajui chochote kuhusu Adam.

Nilionana nae jana na leo ilikuwa ni ahadi yetu kuonana.

Hatuna taarifa yoyote kutoka kwake na kutofika kwake ni jambo la kushangaza, kwa ujumla huenda akaja kesho

Joji alitoka pale mgahawani na kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa Adam na aligonga mlango bila majibu yoyote, alijaribu kumpigia simu lakini ilifungwa, alirudi nyumbani akiwa na wasiwasi.

Katarina, Adam haonekani sijamuona kazini wala nyumbani na simu yake imefungwa.

Na hii sio mara ya kwanza, je hukumbuki kuwa hili lishamtokea hapo kabla?

Ndio, nadhani alifungwa na wale ambao walituhumiwa kwa mlipuko wa ugaidi, ila mimi nilikuwa sijui kama yeye ni Muislamu.

Sijatangamana sana na Adam ila namheshimu sana, nimemuona ni mwenye huruma tena ni mwenye kujali pindi ulipokuwa mgonjwa, na nikaona muamala wake mwingine na Kakhi asiye na haya, mwenye uwezo wa kufanya chochote.

Na kile usichokijua kutokana na yeye, mimi namjua vizuri sana kuwa yeye ni mshauri mzuri wa watu na mwenye kunitakia kheri mimi, nimeliona hilo zaidi ya mara moja. Nikashangaa mbona kujali huku sana na mkweli kwangu kiasi hichi?

Lipi geni katika hilo?

Sikuona geni mpaka nilipojua kuwa yeye sio Mkristo.

Sijakufahamu, kwa nini?

Kwa sababu ni katika watu waliokuwa wakinihimiza kwenda Tel Aviv kuusoma Uyahudi, na ni yeye pia aliyenihimiza kusoma Ukristo na kwenda Roma, vipi afanye hivyo wakati yeye sio Mkristo?

Huenda hii ni dalili ya mtu kujiamini.

Au kuuamini mfumo na njia anayoifuata.

Huenda ikawa hivyo, kwa ujumla Qur’an ni kitabu chenye kushangaza sana, je hukukisoma kiasi cha wiki hivi kama ulivyogusia katika barua yako?

Kama nilivyokufahamisha hapo kabla nilitaka kukisoma, lakini suala la Kakhi lilinisumbua, kisha kupotea kwa Adam, je umeshamaliza kukisoma ili nichukuwe nikisome?

Ndio, nimekimaliza, lakini naona kuna haja ya kurejea tena baadhi ya maudhui na mambo fulani fulani, je unataka nikununulie nakala kwa ajili yako?

Ikiwa utakwenda duka la vitabu hivi karibuni ninunulie nakala, lakini je asili yake ni kwa lugha gani hasa?

Qur’an ni kwa lugha ya Kiarabu tu.

Sasa unakisoma vipi?

Mimi huwa nasoma tarjumi yake tu.

Sisi huwa tunasoma tarjumi la Agano la Kale na Jipya na tunasema kuwa tunasoma? Sasa kwa nini hapa utofautishe?

Kwa hoja ya swali lako katika barua, nimerejea maudhui na kusoma na kuitafiti, nikaona kuwa uhamishaji na unakili wa Qur’an katika zama mbali mbali ulikuwa wa umakini na wa kina kabisa ambayo historia ya mwanadamu umefahamu, watu wengi wamenukuu kutoka kwa Mtume wao Muhammad na kutoka kwao wengi wamenukuu na kupokea hadi leo hii tuzungumzapo, wala muda wote hakujatokea upotofu, ama tarjama ndizo zenye kutokea makosa na upotofu ndani yake.

Ki vipi?

Makasisi wengi walifanya tarjumi ya maana ya Qur’an, walitarjumi kama walivyotaka, na ndio maana kuna makosa katika baadhi za tarjumi.

Kama ni hivyo, Qur’an ni kwa Waarabu tu, na lugha zote kinyume na kiarabu itakuwa imebadilishwa na kutiwa makosa?

Huenda, ila mimi sijasema hivyo! Andiko la Qur’an halisemi kuwa ni la Waarabu tu katika maudhui zake nyingi: “Kwa watu wote” kama ambavyo tarjumi zake nyingi ni nzuri, lakini kunapotokea hitilafu hurejewa katika andiko la asili la Kiarabu, na cha kuchekesha ni kuwa andiko la asili sio tu kuwa limenakiliwa na kuhifadhiwa, bali Waislamu wamenukuu hata ile njia yao ya kusoma kwa sauti.

Ni kipi kipimo cha usahihi wa tarjumi?

Mwenye kufanya tarjumi hufanya tarjumi ya maana ya Qur’an tu na sio Qur’an yenyewe, Qur’an ni kwa lugha ya Kiarabu tu, kwa ujumla ni kuwa unapoisoma unahisi hilo.

Mimi nimechoka nataka kulala, na nina njaa nataka kula chakula cha usiku, na nina huzuni nataka kujua hali ya Adam, na mwenye hasira juu ya Kakhi, na mwenye ashiki anamtaka mpenzi wake, na wewe umeshughulishwa na tarjumi za Qur’an!

Katarina alitabasamu na kusema kwa kubembeleza:

Kwa hivyo tuanze na chakula, halafu mapenzi baadae, na mengine tutayaakhirisha.

Joji aliamka asubuhi na kujiandaa kwenda kazini, alitoka hali ya kuwa ni mzito na asiye na raha, hajui kama hisia zake ni kwa sababu ya Kakhi? Au ni kwa sababu ya babaiko lake ambalo bado hakulitatua jambo lake?
Aliingia ofisini kwake na kuwasiliana moja kwa moja na Adam, na kukuta simu yake imefungwa, alimtumia ujumbe akimtaka amtulize… dakika chache zilipita na Kakhi akampigia simu akimtaka afike ofisini kwake.

Kama kwamba umeibeba dunia kichwani mwako, una nini?

Hakuna kitu, nimechoka kidogo.

Na huzuni uliyo nayo!

Hapana kitu, kuna rafiki yangu mpenzi namtafuta sijampata na ninamhofia.

Je umemtafuta sehemu yake ya kazi, nyumbani na kwa marafiki zake?

Ndio, cha ajabu hata rafiki yake mhudumu wa mkahawa anashangazwa na kutotoa taarifa ya udhuru na sio kawaida yake.

Haa haa, rafiki yako kipenzi! Ni yule mhudumu niliyemkuta hospitali akiwa nawe?

Ndio.

Nilitaka kumfukuza hospitali, vipi unafuatana na mhudumu?

Bali Katarina alikaribia kukufukuza pale ulipomshambulia, Adam ni rafiki yangu mpendwa, na wala sipendi umseme hivyo.

Wewe umependekezwa kuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni, halafu unaniambia habari za rafiki mhudumu! Nina shaka juu yako ijapokuwa uwezo wako wa kazi ni mkubwa, lakini ufahamu wako kwa jamii ni mdogo sana, na kwa masikitiko ufahamu wa kijamii ni muhimu zaidi kuliko uwezo wako wa kazi ya kuajiriwa na haswa katika vyeo vya juu.

Kwani uwezo wa akili wa kijamii ni kuishi na watu katika hali ya mifarakano na jeuri?

Nina maana wewe una uwezo wa kutosha wa kuwa na watu wa maana ambao wanaweza kukuzidishia kipato na fursa ya kazi yako.

Je urafiki kwa mtazamo wako ni fursa ya kazi na kuingiza pesa?

Ndio, bali maisha yote yako hivyo, na wala sijui utaelewa lini hilo?

Wala sitaki kulijua hilo.

Rafiki yangu usiwe mkali, lini utasafiri?

Urafiki wako haunisaidii, urafiki wa Adam ndio bora kwangu.

Haa haa, ninachokijali ni kazi yako na sio urafiki wako, lini utasafiri kwenda Sweden?

Nitakujibu kesho, niruhusu niondoke.

Tumekuwekea tiketi, unaweza kuichukua kutoka kwa William ambaye ni mkurugenzi mkuu wa mahusiano. Haa haa tujulishe utakapomuona mhudumu.

Joji alirudi ofisini akiwa ni mwenye kujilaumu, kwa nini hakumueleza haraka Kakhi kwamba hawezi kusafiri na kuvunja misimamo yake? Je aliogopea kupoteza kazi yake? Kama ni hivyo hana tofauti na Kakhi ambaye anajali mali tu, lakini anajificha katika maadili, tofauti na Kakhi ambae amekuwa ni muwazi kwake, yeye mwenyewe, na hata kwa watu, huenda akawa ni mkweli pindi aliposema kuwa sisi tunadumu katika maadili pale yanapokuwa katika maslahi yetu, lakini pale yanapokuwa hayatuhudumii tunajivua nayo. Alijihimu arudi kwa Kakhi ili amwambie juu ya uamuzi wake na liwe liwalo, lakini alirudi nyuma na kuamua kumuandikia ujumbe wa kuomba udhuru, na wakati huo huo aliingia Wiliam ambae ni mkurugenzi mkuu wa mahusiano.

Tafadhali, chukua hii tiketi imetoka kwa Kakhi.

Mimi nashangazwa na hamasa za Kakhi kwa safari yangu, ijapokuwa sina mapenzi nayo, kulingana na taarifa niliyonayo ni kuwa si wewe wala mkurugenzi wa masoko hamna neno nisiposafiri, na hii ni katika jumla ya kazi zenu na sio zangu!

Amelazimika kufanya hivyo, si katika uchaguzi wake.

Ki vipi sijakuelewa!

Katika kikao cha Idara wakati wa safari yako Tel Aviv palichukuliwa maamuzi ya wewe kupandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi Mkuu, na Kakhi kuhamishiwa kazi nyingine, na Kakhi hakupata njia ya kuahirisha maamuzi haya isipokuwa ila kuwajulisha kuwa kuna kazi ambayo hawezi kuifanya mwingine isipokuwa wewe, na kuwa maamuzi hayo yataakhirishwa hadi utakapotekeleza majukumu hayo.

Na kama sijasimamia majukumu hayo?

Sijui, nilitaka nisafiri lakini akakataa, pokea tiketi hii safari itakuwa ni siku ya tisa kuanzia leo.

Mambo yameanza kuwa wazi kwangu, sasa nimejua kwa nini anakazania, je unaweza kunitumia kwa anuani yangu simu na barua pepe ya wakala wetu huko Sweden?

Baada ya dakika tano utaipata kupitia barua pepe yako.

Kadhalika namba za simu na email za bodi ya wakurugenzi.

Nitakutumia.

Asante William.

Joji alirudi kuandika barua lakini alibadili uamuzi wa kumuandikia Kakhi na badala yake aliandika kwenye bodi ya wakurugenzi.

“Mabwana katika bodi ya wakurugenzi, Ni furaha kwangu kulitumikia shirika kwa karibu miaka 14, kama ambavyo nimefurahishwa na imani yenu kwangu, nataraji kuwa ni mwenye kustahiki sifa hiyo, mafanikio ya shirika letu ni jukumu letu sote, na napenda kuwashukuru kwa msaada wenu ulioniwezesha kutekeleza majukumu yangu katika shirika. Nasogeza kwenu kujiuzulu kwangu, na hiyo ni kwa sababu nilidhani kuwa mtathamini juhudi zangu, lakini nimeshtukizwa na vitisho vya kufukuzwa kazi kama sitokwenda kinyume na maadili yangu na misimamo yangu ya kazi yangu, nataraji kupata haki zangu, kujiuzulu kwangu ni bora kwangu na kwa shirika kuliko kufukuzwa, na kuliko kuuza maadili yangu. Nawashukuru wote kwa dhana njema nami. Ni mimi Joji Nesson”.

Alipomaliza barua yake, aliangalia barua pepe yake na kukuta anuani za bodi nzima ya wakurugenzi zimeshamfikia, alituma barua yake kwa wote akiwemo Kakhi, kisha alitoka nje ya shirika hadi nyumbani kwa Adam bila kumkuta mtu, hivyo alielekea mkahawani, ambapo hakumkuta vile vile, alimuuliza mhudumu mwenzake Adam nae akamjibu:

Wewe ndio uliokuja jana, na leo hajaja pia, lakini kuna mtu mmoja katupigia simu muda mfupi uliopita na kutuambia kuwa amepata ajali, na yupo hospitalini na afya yake inaendelea vizuri.

(2)

Joji aliulizia hospitali ilipo na kwenda moja kwa moja, na njiani alimpigia simu Katarina na kumfahamisha…

Kwa hakika alikuwa bega kwa bega na mimi nilipokuwa hospitalini, na hapana budi na mimi kumfanyia wema.

Unaonaje ukanipitia ili twende pamoja?

Mimi tayari nipo karibu na hospitali na kwenda sasa hivi, na wewe unaweza kumtembelea muda wa jioni.

Joji aliingia hospitalini na kuuliza chumba alipo Adam, na alipoingia alimkuta amelala juu ya kitanda na miguu yake imezungushiwa bandeji na huku amezungukwa na idadi ya watu.

Vipi Adam, kimekusibu nini?

Karibu Joji, samahani nimeiona sms yako katika simu kabla ya dakika tano hivi; na sikupata simu yangu isipokuwa muda mchache uliopita, vipi hali yako sasa?

Kimetokea nini?

Nimeanguka nilipokuwa nikishuka ngazi, na kuvunjika katika mguu wangu, na nimeletwa hospitali jana na nimefanyiwa operesheni ya kuunga mfupa, na mimi ni mzima.

Mbona hujanipigia simu?

Asante Joji wewe ni rafiki mkweli, kwa kweli sikuweza kuwasiliana na yeyote yule, rafiki yangu aliyenileta hospitali ndie aliyewasiliana na wale anao wajua katika marafiki zangu, nitakufahamisha kwao: Ahmad kutoka Syria ni Mhandisi Electronic, Adrian, Mfamasia Mwingereza, Ali kutoka Saudi Arabia, mwanafunzi Chuo Kikuu, na Sheikh Baasim wa Azhar kutoka Misri na ni Imam wa Kituo cha Kiislamu hapa London. Nami niwatambulishe; huyu ni rafiki yangu Joji, ni Mhandisi wa programu na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Advance Programming, aliyeniletea mkoba wa kifahari ambao mliupenda kupita kiasi.

Karibu, ndio mara ya kwanza kujuana na marafiki wa rafiki yangu.

Rafiki yangu Joji ni mwingi wa safari, na ni mtu mwenye kujua wajibu wake kijamii.

Kama alivyonitambulisha Adam, mimi nilikuwa Naibu Mkurugenzi wa shirika la Advance programming, kwa hakika nimefaidika sana na Adam.

Yaani umeacha? Tokea lini?

Kabla ya saa moja iliyopita hivi nimepeleka maombi ya kujiuzulu, na baada ya kukamilisha hilo nikaja hapa kwako.

Kwa nini?

Kisa cha kujiuzulu kwangu ni kirefu, achana na hili, vipi mguu wako sasa? Daktari anasema nini?

Alhamdulillah, maumivu yamepungua; ila nimelazimishwa kukaa hospitalini kwa muda wa siku tano, kisha nitapumzika nyumbani kiasi cha mwezi hivi, kisha mwezi tena, baada ya hapo nitatembelea magongo.

Baasim AlAzhari alitabasamu: Sipendi kukata maongezi yenu, lakini tunaomba radhi tusali adhuhuri, na tutarudi kwa mara nyingine.

Nakusubirini.

Sheikh Baasim ni mwalimu na Sheikh wangu tangu nikiwa mdogo.

Wameenda wapi?

Wameenda kusali adhuhuri.

Leo Jumanne ni swala gani hiyo?

Sisi Waislamu tunasali mara tano kwa siku, kila swala ina wakati wake.

Nilishtushwa nilipofahamu kuwa wewe ni Muislamu! Kwanini hukunijulisha tokea mwanzo?

Niliwahi kukueleza hapo kabla kuwa huwezi kuunganisha jina langu na mazungumzo yangu, bali sura yangu ni dalili ya wazi kuwa mimi ni muarabu Muislamu. Kwa ujumla sikutaka kukuficha chochote, lakini wewe uliniuliza ukinituhumu kuwa mimi ni Mkatoliki na wakati mwingine Mprotestanti, nareja tena kukuomba radhi kama utakuwa umehisi kukuficha kitu.

Je hamchoki kusali vipindi vitano kila siku?

Sala hutuondolea matatizo na tabu za dunia wala haituchoshi.

Nasi pia hali kadhalika, tuna starehe kwa sala ya kila wiki, ama mara tano kwa siku nadhani inachosha!

Sisi tunapata tabu kama hatusali sala tano kila siku, na sala yetu haihitaji kutoa juhudi au nguvu na hata kwenda msikitini.

Mnakwenda Msikitini?

Ikiwa inawezekana kwenda ni bora kwenda msikitini, na kama hali hairuhusu basi sehemu yoyote inafaa kusali, na mimi nitasali katika kiti changu muda sio mrefu.

Unasali ukiwa katika hali hii?

Ndio, kuwa katika hali hii ni bora zaidi kusali, kwani mimi namuhitajia Mola wangu kila wakati, na sasa hivi haja zangu kwake ni kubwa zaidi, vinginevyo mitihani ya maisha humfanya mtu akapoteza uwezo wake wa kuvumilia; na hivyo basi kupotea tabia na maadili yake.

Kwa hakika kushikamana na maadili kunachosha.

Hivyo basi swala na mawasiliano ya mtu na Mola wake ndio njia mojawapo katika njia za msaada, ili mwanadamu aweze kuongeza masurufu yake katika subira na kudumu katika jambo.

Nimekutumieni barua kuisoma Qur’an, lakini sijui nisome tarjumi ipi ya Qur’an.

Natamani ungejifunza Kiarabu; ili ufaidike na ladha ya Qur’an kama sisi tunavyofaidika nayo, hata hivyo nitakupa nakala ya tarjumi ya maana ya Qur’an, lakini ni baada ya kurudi Sheikh Baasim.

Je Uislamu ni kwa ajili ya Waarabu tu?

Idadi kubwa ya Waislamu ambao wapo nje ya mataifa ya Kiarabu inazidi mara nyingi ya idadi katika mataifa ya Kiarabu, na Uislamu ni kama Allah alivyosema katika Qur’an: “Rehema kwa walimwengu” (21:10).

Ni rehema!

Ndio ni rehema, laiti ungelisoma Qur’an na kuijua ungegundua ni mara ngapi rehema hiyo inapatikana kwa kila kiumbe!

Ni mfano wa maneno ya Katarina wakati anapozungumzia Ukatoliki.

Kama ulivyousoma ukatoliki, usome pia Uislamu, kisha urejeshe kama haujakuridhisha.

Ndio, nimeamua kuusoma na nitaanza na kusoma Qur’an, lakini kwa akili ya kuchambua na kukosoa.

Vizuri na haswa, Uislamu ni dini ya elimu, wala haukutaki uuamini kabla ya kuusoma, ndio maana maamrisho ya kwanza ya kushuka kwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) yanahusu: (kusoma).

Unajiamini sana kwa Uislamu, nilipokuwa Roma nilikutana na Muislamu kutoka Misri, alikuwa anasema na kuniambia kuwa anatamani kuwa kama sisi, na akaniusia nisijifunze Uislamu.

Na utakutana na Waislamu pia wakisema hivyo: Kwamba Uislamu ni dini ya wajinga, yenye kurudisha nyuma maendeleo, pia ni dini ya Ugaidi.

Alikuwa akisema hivyo pia.

Na utakutana na Waislamu wanaongelea kuwa Uislamu ni dini iliyomdhulumu mwanamke na Uislamu unalazimisha watu kusilimu.

Nafikiri yote hayo yamekusanyika kwa Muislamu huyu niliyekutana nae huko Roma.

Je huwezi kukutana na mtu mwingine anayatusi na kukosoa elimu ya hesabu, au uhandisi, au utabibu au kompyuta?

Wengi sana.

Je maneno hayo yanapunguza chochote katika hadhi ya elimu hizi? Au inapunguza uwezo wa elimu hizo katika kuhudumia haja zetu?

Katu hapana, lakini mambo ni tofauti hapa.

Mimi sioni tofauti yoyote; isipokuwa tu kuna mashambulizi yanayoelekezwa kuuhujumu Uislamu, wakati ambapo katika elimu hatuoni hayo.

Unakusudia nini kusema kuwa ni mashambulizi ya makusudi yaliyoelekezwa?

Je una kumbuka shambulizi la kigaidi lililotokea London ambalo lilifanywa na Waislamu?

Ndio, na baadae kuthibitika sio shambulizi la kigaidi.

Imethibitika hivyo baada ya vyombo vya habari kuzungumza kwa muda mrefu kuhusu ugaidi wa Waislamu, kisha kukanushwa na kunyamaziwa kama kawaida, je unajua kuwa mimi nilifungwa kwa sababu ya shambulio? Tuhuma ni kuwa mimi ni Muislamu; kwa maana mimi ni gaidi, je wajua kuwa dalili zote zilikuwa wazi kuwa Waislamu wako mbali na mlipuko huo, lakini vyombo vya habari tuhuma zao zipo tayari?

Je huoni kuwa hayo yote yanasababishwa na vitendo vya Waislamu vyenye kujirudia rudia?

Katika kila jamii na kila dini kuna wenye kupetuka mipaka, lakini tofauti ni kuwa kadhia inakuwa na makosa ya jinai inapokuwa hakuna uhusiano na Waislamu, na linakuwa la kigaidi kama linahusishwa na Waislamu! Je huoni kuwa hilo ni jambo la kuchekesha?

Inaelekea ni mwenye hamasa sana na Uislamu!

Niache niwe muwazi kwako, ni nini kinachokukataza usiwe Muislamu? Ili maisha yako yawe na furaha.

Swali limevuka mipaka, sikulitegemea, je kuingia katika Uislamu ni wepesi kiasi hiki?

Ndio, sidhani kama utahitaji shamrashamra za kanisa wala ugumu wa dini za watu, ni kitu chepesi lakini chenye kubeba ujumbe mkubwa.

Je unatarajia mimi kuingia katika Uislamu ewe Adam?

Ndio, bali nataraji hivi karibuni sana.

Samahani, inaonekana hunijui vizuri ewe Adam, mimi siwezi kukikumbatia kitu ambacho hakiendani na akili yangu, mawazo yangu, fikra na misingi yangu.

Samahani, bali wewe ndio ambaye huujui Uislamu!

Sijafahamu, unakusudia nini?

Kusilimu ni jambo jepesi sana, lakini haiwezekani kusilimu kabla ya kuridhika ndani ya nafsi yako kwa ukamilifu, na sio kusudio kutamka maneno ya shahada mbili, yaani Ashhadu anLailaha Illah Llah waana Muhammad Rasulullah kabla hilo hulijaingia ndani ya nafsi yako kwa ukamilifu, kilicho muhimu ni kile kilicho ndani ya moyo wako kwa hivyo la muhimu ni imani kuingia katika moyo wako na kuwa na itikadi na imani na sio maumbo.

Japokuwa sidhani kama nitasilimu siku moja, lakini nani anajua hilo?

Japo nina matumaini makubwa kuwa utasilimu, ila mlango wako utakuwa ni elimu; hivyo basi ni wajibu wako kuusoma Uislamu kwanza, na utaingia katika Uislamu baada ya hapo, wewe unapenda elimu, mantiki, fikra na maadili.

Sijajua kwa maneno hayo wewe unanisifia au unausifia Uislamu au unavisifia vyote viwili? Lakini unanikumbusha na yule Muislamu ambae nimekutana nae Roma na akamwambia Katarina maneno kama hayo, kabla ya kumzawadia kitabu chenye anuani: (Mapenzi yangu makubwa juu ya Masiya yamenifanya kuingia katika Uislamu).

Je hukuniambia muda mfupi uliopita kuwa Muislamu uliyekutana nae huko Roma alikuwa anaukataa na kujivua na Uislamu?

Tofauti iliyopo ni kwamba huyu wa mwisho alikuwa ni ndugu yake yule wa mwanzo niliokusimulia, na tulikuwa wote pamoja.

Ni yupi kati yao ni bora kwa mtazamo wako?

Sijui, ijapokuwa wa mwanzo ni mkubwa, ila huyu wa pili anaheshimika sana kwa mama yake na baba yake, na yeye anawaheshimu sana, na hakunishughulishi kuwafadhilisha kati yao.

Na je Katarina alisoma kitabu?

Ndio, na mimi nimekisoma mara mbili na najua kimemtikisa moyoni mwake.

Na je wewe umekisoma?

Ndio, nimekisoma, lakini wewe umeniambia nianze na Qur’an, na wewe utanipa tarjumi yake.

Sheikh Baasim atakuja sasa hivi amechelewa kidogo, nataraji wataingia sasa hivi tu, naomba nisali, na ukitaka kuuliza juu ya Uislamu; Sheikh Baasim ndio mwalimu na mjuzi, na mimi ni mwanafunzi wake tu, na nakala yako ya Qur’an zawadi yangu kwako kutoka kwa Sheikh Baasim.

Nitakusubiri mpaka utakapo maliza kusali, ikiwa watafika sawa na kama vipi nitaondoka.

Vizuri

Adamu alianza kusali na Joji akimwangalia, muda huo huo Sheikh Baasim alifika na marafiki zake, Joji aliwageukia.

Adam ameniambia kuwa wewe ni mtu wa dini wa Kiislamu, na akanipa zawadi ya nakala ya tarjumi ya maana ya Qur’an, na akaniambia kuwa wewe ndie utakayenipatia.

Hakuna katika Uislamu wanaojiita watu wa dini, dini ni kwa watu wote, na nakala ya msahafu ipo katika gari nje, unaonaje tutoke pamoja nikupe?

Vizuri, nimechelewa sana na nataka kuondoka, ila tumsubiri Adam amalize swala labda arefushe.

Swala zetu ni kama dini yetu ni nyepesi na yenye furaha.

Furaha?

Ndio, furaha ya dunia na akhera, cha ajabu ni kuwa wewe ni rafiki wa Adam na asikuambie hilo, nitamlaumu Adamu kama hajakueleza dini hii kubwa ilivyo, wakati wewe ni rafiki yake, na hakuna atakae kuongoza vizuri kuliko kujifunza kwako Uislamu, je huoni kuwa watu wengi wanabadilika na kutoka katika njia za upotevu badala ya kufuata njia ambazo zitawaletea manufaa katika dini na dunia yao na wanaghafilika na dini ya mwisho ya Mitume na Manabii?

Huenda ni kwa sababu hiyo ndio maana amenizawadia tarjumi ya Qur’an kutoka kwako.

Adam alimaliza sala yake na kuwageukia upande wa Joji na Sheikh Baasim.

Ewe Sheikh Baasim usinilaumu; kwa hakika nimemueleza kwamba Uislamu ni furaha ya dunia na akhera.

Baasim alitabasamu na kusema:

Ewe Joji, sisi kila sala tunayosali tunakuwa na furaha ya dunia ya ajabu, kwani tunatupa mizigo ya dunia kwa Mola muweza, Rahiim, Karimu, Msikivu na Mjuzi, jifunze Uislamu kwani ndio njia bora ya furaha.

Joji nakutakia furaha ya dunia na akhera aliyokutajia Sheikh Baasim.

Haiwezekani kubadili dini yangu ila baada ya kusoma na kukinai, nitauingiza ndani ya fikra yangu, je sikufanya hivyo kwa dini zote ewe Adam?

Bila shaka, na haya ni maombi yangu kubaki katika njia ile ile, pamoja na mapenzi yangu ya kusilimu, lakini Uislamu hutufundisha elimu kwanza.

Hapana budi usome kwanza, kisha baada ya hapo huna udhuru wa kutosilimu ewe rafiki yangu, je unataka tushuke sasa hivi?

Sijajua chanzo cha kujiamini kwenu kuwa kama nitausoma Uislamu nitasilimu?

Imani yetu ipo kwenye Uislamu wenyewe kwani ni kutoka kwa Allah.

Nitaona!! Nakuahidini kuisoma Qur’an, na kusoma kuhusu Uislamu, na tuujadili, na baada ya haya nichukue maamuzi yangu.

Vizuri sana, na hili ndio bora.

Wala usisahau kusafiri kama ulivyosafiri kwa ajili ya dini zingine.

Tushuke sasa, nitakisoma kitabu chenu kitakatifu, halafu kila penye tukio kuna mazungumzo yake, na nitajaribu kukutembelea kesho, kwani kwa sasa mimi ni mtu ambaye sina kazi.

Kwa hakika nimeshtushwa kwa kuacha kazi yako, lakini unaonekana una haraka, na kama hutokuja kesho basi tuwasiliane kwa simu, Mungu awe pamoja na wewe.

Joji alirudi nyumbani kwake akiwa na nakala ya tarjumi ya Qur’an, hakumkuta Katarina nyumbani, aliwasiliana nae na kumwambia yupo njiani kwenda kumuona Adam hospitalini. Akaanza kusoma Qur’an, alishangazwa na wema wa Adam kwake, na kumtangulizia vitabu vingine vinavyo fundisha Uislamu na baada ya masaa mawili hivi, Katarina alirudi nyumbani.

Nimerudi kutoka kwa Adam.

Mimi najua hujamtembelea ila umefanya hivyo kwa kuwa yeye ni rafiki yangu na hiyo ni kuniridhisha mimi tu.

Ni mtu wa ajabu sana!

Ki vipi?

Sijui, lakini yeye pamoja na rafiki zake wote Waislamu ambao alikuwa nao hawapeani mikono na wanawake, na wakaomba radhi kwa upole na heshima ya hali ya juu, na je huu ni upambanuzi wao dhidi ya mwanamke kwa njia ya Wayahudi na Wakristo?

Huenda, sijui, mimi kabla ya masaa mawili nimeanza kusoma kuhusu Uislamu kwa kusoma kitabu chao kitakatifu Qur’an na kwa hakika kwa yale niliyoyasoma hadi sasa inamthamini mwanamke na kumuheshimu.

Ndio, nimesoma tarjumi ya Qur’an, ndivyo ilivyo lakini nimeshangazwa kwa namna walivyotangamana nami!.

Kwa nini? Je kulikuwa na aina yoyote ya udhalilishaji au dharau kwako?

Hapana, walikuwa wapole na heshima sana, lakini hawakunipa mkono na hawakuniangalia.

Hata hivyo umechelewa, je hawakuzungumza nawe?

Tumeongea sana, ila maongezi yao mengi yalikuwa kuhusu Uislamu, sijui kwanini wananikumbusha na baadhi ya makasisi.

Huenda ikawa hivyo kwa sababu sahibu yao Baasim ni mtu wa dini.

Hapana, Baasim sio mtu wa dini na amekataa wasifu huu, na akasema kuwa katika Uislamu hakuna watu maalumu wa dini kama vile mapapa kwenu, ila ni kuwa yeye ni mtaalamu wa dini.

Ndio, umesema kweli, aliniambia maneno hayo hayo, ni mtu mwenye maadili na mwenye tabasamu pana, na amenipa kadi yake ili niwasiliane nae, fikiria!! Ananitaka niingie katika Uislamu, nashangazwa sana na imani yao!

Katarina aliangalia chini ya sakafu, kama anafikiri jambo katika akili yake: Wote wana maadili mazuri, na wafanya ibada sana, japokuwa sio kama watawa, ni watu wanaotafuta maisha na sio kujitenga na ibada pekee, bali kizuri zaidi wanaona kuwa kazi zao na kusoma kwao ni sehemu ya ibada, na wao hawatenganishi maisha na ibada kama tulivyo sisi, fikiria Adam amesali juu ya kitanda chake! Na kuniambia: Sisi tunasali popote; na dini ni nyepesi.

Amesali nikiwepo, na akaniambia kuwa wao wanasali vipindi vitano kwa siku na kwamba sala zao zinawapa furaha, lakini mimi sijatosheka kwa yale waliyosema japokuwa wanasema kwa kukinaisha.

Ndio, kukinaishwa kwao kuko katika hali ya juu, na maneno yao yana athiri sana, mahusiano yao na tabasamu zao ni zenye athari kubwa.

Inaelekea umevutiwa nao mno!

Sio suala la kuvutiwa, suala ni kuwa Waislamu na Qur’an na Uislamu ni mfumo tofauti kabisa na ule tuliouzoea.

Pambanua zaidi, ni hisia hizo hizo nimezipata pindi nilipoanza kusoma kitabu chao kitukufu (Qur’an), sikuweza kuifahamu kwa ukamilifu wake, hisia ngeni kabisa za ndani mwangu, haswa katika maudhui kama: Kumpwekesha Allah na kumtukuza kwake, pamoja na majina na sifa zake, au visa vya Mitume na hasa Yesu na Bikira Maria, au maadili na tabia.

Ni kama hisia zangu hivyo hivyo, lakini nashauri tusifanye haraka kuhukumu, mambo mengi yatakuwa wazi kwetu kila tutakaposoma kuhusu dini hii, wakati huo tutajua udhaifu wake, mapungufu na migongano iliyopo, wala simaanishi kuwepo mfano wa mambo haya katika Uislamu, pamoja na hali yao ya kukosa maendeleo na udikteta wao.

Pamoja na kuvutiwa na Adam, lakini sina hamu ya kutaka kuujua Uislamu, ila nitajitahidi katika hilo, ingawa nimefurahishwa muda mfupi uliopita nilipokuwa nikisoma Qur’an.

Kwa hakika inashangaza unaposoma kitabu chao kitukufu!

Habari nzuri ni kuwa nimepeleka maombi ya kujiuzulu, ni kiasi gani namchukia Kakhi muongo na mwenye hila nyingi, nimekuja kufahamu kuwa yeye ndie aliyekataa nisipandishwe cheo na kunipa majukumu ya safari ya Sweden, nimeandika barua ya kujiuzulu kwa bodi ya wakurugenzi, wasiponijibu itakuwa ndio kujiuzulu kwangu moja kwa moja.

Kwa hivyo maadili yako yameshinda matakwa na maslahi yako?

Huenda, lakini kilichosukuma maamuzi hayo nilipojua maamuzi ya bodi ya wakurugenzi na majibu ya Kakhi, nina matumaini kutoka kwao, na kwa hali yoyote kama sijapata jibu la kuridhisha kutoka kwao, basi nitapeleka malalamiko yangu katika chama cha kutetea wafanyakazi.

Ama kwa upande wangu bado naendelea kupambana kati ya maadili na kazi yangu, nilikuwa najaribu kuficha shaka yangu, ila wewe umedhamiria kufungua kilichokuwa na sitara.

Tangu tumeoana sijawahi kukuona umebadilika kwa haraka kama mwezi huu wa mwisho na hasa baada ya kuwasili kutoka TelAviv!

Sio kila mabadiliko na mageuzi ni shari yote au ni kheri yote, na natamani mabadiliko yangu haya yawe ya kheri kama nilivyokuwa.

Haa, haa, je kuna kheri yoyote kwenye Ukatoliki?

Itikadi yangu kwa Masiya na Muokozi wetu ni kubwa sana na katika Ukatoliki pia, na wala sidhani kama kuna kheri zaidi ya hiyo, lakini ni nani anajua?

Haahaa, leo nataka kulala mapema, hata hivyo nitasoma barua pepe haraka haraka.

Joji alifungua email na kukuta baadhi ya majibu ya barua yake aliyouliza juu ya maadili, alifupisha na haraka kuwatumia wote, kwa kiasi kikubwa ilikuwa inawafikiana na maamuzi yake.

John Luke: Maadili yanakuwa kwanza kwa mtu mwenye ujasiri, lakini pamoja nayo kuna tabu na sononeko. Levi: Sahihi ni kuwa maadili ni kitu muhimu zaidi, lakini sio lazima tuwe na uwezo wa hilo, sisi tunakuwa ni dhaifu mbele ya mbinyo wa maisha. Habib: Ni lazima maadili yatangulie, vinginevyo tutakuwa kama wanyama porini. Katarina: Inavyotakiwa ni maadili kutangulizwa ingawaje ni uamuzi mgumu. Bado nasubiri majibu yenu juu ya barua yangu iliyotangulia kuhusiana na Qur’an. Joji.”

Aliendelea kupekua email yake na kuchukua ujumbe wa John Luke

“Rafiki yangu Joji, Japokuwa ni muda mfupi tu tokea tufahamiane, ila tumekuwa karibu na fikra zetu zinakaribiana, kwa hivyo naomba ushauri wako katika jambo huenda likawa geni kwako; Baada ya safari yenu, nimesoma kitabu alichopewa zawadi mke wako na Muislamu, nimesoma kupitia intaneti, halafu niiporudi nikakutana na mhandisi majengo Muislamu na tukajadiliana nae na akanitaka mimi nisome tarjumi ya Qur’an kwanza, nikasoma chote kwa ukamilifu zaidi ya mara moja, kisha tukakutana kwa mara nyingine na kujadiliana, sijui ni siri gani ya uchawi iliyopo katika kitabu hiki! Nikamuuliza ufafanuzi wa mambo katika Uislamu; alinijibu kuwa yeye hajui chochote zaidi ya kuwa yeye ni mhandisi tu. Nikamuuliza tena: Nani anaweza kunielezea vizuri juu ya Uislamu, alijibu kwamba hamjui yeyote hapa Italia kwani yeye ni mgeni, na ikiwa unataka kuujua vizuri Uislamu, kuna njia mbili mbele yako: Ima usome vitabu vilivyoandikwa juu ya Uislamu, navyo vipo vingi, ila baadhi yake vimeandikwa na maadui wa Uislamu, au njia ya pili: Umtafute mjuzi wa Uislamu hapa Italia au usafiri, nimeamua nichukue njia zote mbili, hivyo basi tokea msafiri nasoma kwa muda wa masaa matano kuhusu Uislamu, na nataka nisafiri kwenda Misri hivi karibuni, au Libya, je unanishauri nini? Salamu zangu kwako na kwa Katarina. Ni mimi John Luke.”

Alimjibu…Rafiki yangu John Luke.

“Nimesoma ujumbe wako na nimestaajabishwa na ushujaa wako, inavyoelekea mabadiliko ambayo yametokea kwako kwa muda mfupi tangu safari yetu ni makubwa sana na zaidi ya matarajio yetu, mimi nakuunga mkono kufuata njia zote mbili, na naomba unipe taarifa ya pale utakapofikia, kwa hakika nafaidika sana nawe na akili yako ya uchambuzi na utafiti, Salamu zangu kwako. Ni mimi Joji.”

(3)

Joji aliamka na kumkuta Katarina ameshaandaa chai, walikaa na kuanza kunywa chai.

Sina kazi leo na sijui nifanye nini?

Nenda kazini, kwani bado hujakubaliwa au kukataliwa kujiuzulu kwako, na kutokwenda kwako ni hoja dhidi yako katika chama cha watetezi wa wafanyakazi.

Sijakuwa na ufahamu huo akilini mwangu, unayo haki.

Ama kwa upande wako umekata shauri ya jambo lako, ama kwa upande wangu nitajaribu kulimaliza leo pia.

Unataka kulimaliza, vipi na kwa kitu gani?

Sijui, lakini nitakwenda na kujaribu kulimaliza suala langu.

Jana nilikutumia ufupisho wa yale yaliyokuja kati ya maadili na maslahi katika email yako, soma huenda ukafaidika nayo kabla ya kuchukua maamuzi.

Nitasoma kabla ya kuchukua uamuzi, nitakwenda sasa nisije nikachelewa.

Na mimi nitatoka sasa hivi.

Joji alienda kazini kwake na kuingia ofisini mwake, pindi alipokaa tu alijiwa na mkurugenzi mkuu wa mahusiano akiwa ni mwenye hasira:

Umefanya nini?

Sijafanya kitu, kwani nini kimetokea?

Baada ya kutoka wewe jana, Kakhi aliniita kwa hasira, na kwa mara ya kwanza nilimuona amekasirika hivi, na kuniuliza Joji amepata wapi anuani za wakurugenzi wa idara mbali mbali? Nilimjibu sijui.

Na kwa nini hukumweleza kuwa wewe ndie uliyenipa?

Huenda akanidhuru! Wewe unamjua kuwa yeye ni dhalimu hafikirii isipokuwa kwa maslahi yake tu.

Hivi ndivyo tunavyo ogopana wenyewe kwa wenyewe, jambo la kushangaza sana. Sitamueleza zimetoka kwako, kuwa na amani tu, lakini unajua kwa sababu zipi amekasirika?

Inavyoonekana wafanyakazi wa idara wamewasiliana nae na kutaka kukutana haraka ndani ya siku tatu, kwa mujibu wa barua yako.

Mkutano juu ya nini?

Sijui? Ninachofahamu ni maudhui kuhusiana nawe, ndio maana nikakuuliza ulichoandika katika barua?

Kama ni hivyo hali inahamasisha sana, sikutegemea kama itakuwa hivyo!

Inahamasisha! Kwa kitu gani inahamasisha?

Hakuna kitu, ila niliwatumia barua ya kujiuzulu kwangu, kwa hali hiyo niamini hakuna mtu mwingine atakayejua kwamba wewe umenipa email zao.

Nakushukuru, naomba ruhusa.

Joji alitafakari kwa kina hatua inayofuata ambayo anatakiwa kuifanya kwa sasa, kwa sababu anajua hila na uongo wa Kakhi, na inawezekana akaitumia njia hii katika kikao cha idara kwa urahisi na yeye hataki kuliachia shirika, je atatakiwa kuhudhuria katika kikao cha baraza, au awape taarifa ya kina kilichotokea? Au afanye nini? Cha ajabu ni kuwa hadi sasa hajajibiwa na mtu yoyote kutoka kwa wajumbe wa idara kwa njia ya barua pepe! Kitu ambacho kinajulisha kabisa kuwa watamsikiliza Kakhi peke yake, na hili ndilo asilolitaka, alifikiri sana, halafu akaamua kutuma barua ya pili kwa idara kwa kuandika:

“Wajumbe baraza la idara: “Ni furaha kwangu kulitumikia shirika kwa karibu miaka 14, kama ambavyo nimefurahishwa na imani yenu kwangu, nataraji kuwa ni mwenye kustahiki sifa hiyo, mafanikio ya shirika letu ni jukumu letu sote, na napenda kuwashukuru kwa msaada wenu ulioniwezesha kutekeleza majukumu yangu katika shirika. Nimekuleteeni nyinyi dhulma zangu na naomba kujiuzulu, na sijapata jibu lenu, kwa maana hiyo ni kuendelea kudhulumiwa na kukubaliwa kujiuzulu kwangu, au ndio utakaso kwangu na kutaka kuendelea na kazi, nina matarajio kuwa mnijadili moja kwa moja katika kikao cha Baraza la Idara. Nakushururuni nyote kwa ushirikiano wenu mzuri. Ni mimi Joji.”

Kwa barua hii Joji alitaka aitwe kuhudhuria katika baraza; ili awaonyesha kila karatasi wajumbe hao, lakini haikuchukua muda baada ya kutuma barua ile ilipigwa simu ofisini kwake, na Kakhi akiwa upande wa pili.

Yote hayo ni kwa ajili ya maadili ewe mwenye maadili! Je unaweza kuja sasa hivi ofisini kwangu?

Ndio ni kwa ajili ya maadili na sitobadilisha maadili yangu.

Je unaweza kuja kwangu?

Nakuja sasa hivi.

Joji aliingia kwa Kakhi na kumuona ameghadhibika, na haraka alimsemesha.

Joji unataka nini?

Nataka kutokwenda kinyume na misingi yangu.

Kama kwamba unakwenda mbio uwe rais wa shirika.

Hilo sijaliendea mbio, likinijia na hali ya kuwa nastahiki si tatizo.

Kwa hiyo masuala siyo maadili bali ni vyeo.

Elewa kama unavyotaka, ila mimi sibadili maadili yangu, na sijaja kwako ila ni baada ya kuniomba na kunijulisha kuwa tutaafikiana, amini Kakhi kuwa sitaachana na maadili yangu.

Ikiwa masuala ni kama unavyosema; masuala ya maadili na sio masuala ya vyeo, basi nina ombi lingine kwako.

Ni lipi hilo?

Mimi nitasafiri kwenda Sweden, kwa sharti wewe utoke London.

Kwa nini?

Maudhui yananihusu mimi mwenyewe, mimi sitaki kutoka katika shirika kwa sasa hivi, baraza la idara likikutana kwa sasa na wewe upo London watachukua uamuzi wa kunitoa katika shirika, kwa hivyo nimewakinaisha umuhimu wa safari yako Sweden, kisha akatabasamu na kusema: Kwa kuchunga maadili yako mimi ndie nitakwenda Sweden, lakini ni lazima wewe uwe nje ya London kwa wakati huo ili maamuzi yachelewe kutolewa.

Nisafiri wapi?

Sehemu gani unapenda, tuna kazi Ujerumani, Ukraine na Misri.

Na ikiwa nitakataa?

Itakuwa wazi kadhia ni vyeo au maslahi na sio maadili! Na wakati huo kila tukio lina mazungumzo yake.

Nitatafakari na kesho nitakupa jibu.

Utanijibu mimi na sio kwa wajumbe wote wa baraza.

Nakuahidi hilo.

Joji alitoka katika shirika, njiani akiwa kwenye gari lake alimpigia Tom.

Je unao muda nikutembelee?

Karibu sana.

Baada ya nusu saa nitakuwa kwako, nipo njiani.

Joji alifika kumtembelea Tom na kuingia tu akamkuta mpokea wageni mpya, nae alimkaribisha Joji;

Dr. Tom anakusubiri karibu.

Karibu Joji, mgonjwa wa kwanza baada ya kufungua kliniki, haijafunguliwa ila leo, na sijaweka ahadi isipokuwa kuanzia kesho.

Habari njema, samahani sijafuatilia maudhui ya Baraad je imeisha.

Ameondoka bila kurudi.

Amekwenda wapi?

Jela, amekamatwa akiuza madawa ya kulevya.

Baraad ni mtu ninayemchukia sana!

Kwa nini unamchukia?

Ni mtu asiyekuwa na maadili na mtu anapokosa maadili anakuwa karibu na wanyama wa porini.

Mitihani migumu iliyoje! Nilikuwa na chaguzi mbili mbele yangu kuyaacha maadili yangu na kumaliza matatizo yangu yote kwa haraka, au niendelee na maadili yangu na niingie kwenye mtihani mgumu, kwa hiyo nimeamua kubaki katika maadili yangu na nilikaribia kupoteza kila kitu, lakini nimekinai kuwa kushika maadili mwisho wake kuna wema na hili ndilo lilivyotimia.

Kana kwamba unafahamu lile ulilokuja nalo!

Ni lipi?

Joji alimuhadithia Tom kirefu tatizo lake pamoja na Kakhi mpaka kafika katika maudhui ya safari na kusita sita kwake.

Nilitaka kukushauri wewe: Je unadhani kuwa safari yangu pasina masharti ni jambo lisilokuwa la kimaadili na kuachana na maadili yangu?

Sijakufahamu! Vipi inawezekana kujiondoa katika maadili yako? Wewe utasafari kwa kazi nyingine.

Lakini mimi nina hakikisha malengo mabaya ya Kakhi.

Na huenda ukamfedhehesha sana Kakhi mbele ya Baraza la Idara.

Kwa hiyo rai yako mimi nisafiri?

Ndio, nenda Misri.

Kwa nini?

Hukumbuki kuwa katika kikao chetu kilichopita majadiliano yetu yalikutaka usome Uislamu, na hii ni fursa imekuja kwako, na laiti kama sio kufungua kliniki leo tungesafiri pamoja.

Sitaki kusafiri, kwa sababu nimesafiri sana kipindi kilichopita, na kama kusafiri basi ningependa kwenda Ujerumani.

Uamuzi upo kwako, ila mimi naona safari ni muhimu, utajua Waislamu walivyo na kujua aibu na makosa yao.

Nitafikiri, na kwa hali hiyo wewe ndie mtu wa mwanzo nakutaka ushauri, nitafikiri zaidi kisha nitakuomba tena ushauri, kisha nitakujulisha maamuzi yangu, naomba ruhusa yako; leo wewe umeshughulishwa na kliniki yako, na wewe unastahiki hivyo kudumu katika maadili yako, naomba niondoke.

Akiwa njiani aliwasiliana na Adam na kumweleza kuwa anataka kumtembelea, alimuomba udhuru kwa sababu daktari atachukuwa baadhi ya vipimo sasa hivi, hivyo atamsubiria kwa ziara ya jioni, Joji alielekea nyumbani na aliamua autumie wakati wake kwa kusoma kitabu kitakatifu cha Adam ambacho ni Qur’an.
Pindi alipokuwa akisoma mara watoto wake Maiko na Sali wakaingia

Baba, leo umerudi mapema?

Ndio, kuna mambo yametokea kazini ndiyo yaliyonifanya kurudi mapema.

Unasoma nini baba, upo kwenye mawazo na wewe unasoma?

Nilikuwa nasoma kitabu kinachoelezwa kwamba ndio cha Waislamu.

Waislamu ambao wanaitwa magaidi?

Ndio.

Shuleni kwetu kuna mwanafunzi Muislamu kutoka India, ni mvivu darasani ila ni mzuri na sio gaidi.

Ugaidi hauna dini, achana na yale wanayosema, na unaweza kuingiliana na watu kwa mujibu wa tabia zao.

Japokuwa ni mwema ila nahisi yeye anajitenga kidogo na sisi.

Kwa nini?

Sijui! Labda ni kutokana na wanavyosema sana kuwa yeye ni gaidi, au ni kutokana na baadhi ya wanafunzi kudharau umbo lake lilivyo.

Ni nani anayesema hivyo?

Mimi sipendi hivyo, lakini baadhi ya wanafunzi wanafanya hivyo.

Mwanangu maadili na tabia za watu ndio vitu vinavyotakiwa kunyanyuliwa au sivyo watu watapotea.

Ni mfano wa maneno ya Iqbaal.

Ni nani Iqbaal?

Ni rafiki yangu Muislamu Muhindi niliyekueleza.

Ndio katika Qur’an: “Hakika ya mbora wenu mbele ya Allah ni MchaMungu” (49:13); hakuna mtu mbora wa rangi yake, au jinsia yake isipokuwa kwa UchaMungu tu?

Je haukuwa Uislamu ni kwa Waarabu tu? Mimi nimeshangazwa nilipo jua kwamba Iqbaal ni Muislamu!

Idadi ya Waislamu wanakaribia bilioni na nusu, na wameenea China mpaka Marekani na cha ajabu ni kwamba asilimia 80% ya Waislamu wapo nje ya ulimwengu wa kiarabu.

Ni mara ngapi natamani usawa huu kwetu sisi!

Nini?

Baadhi ya wanafunzi wananihesabu mimi ni Muhindi na sio Muingereza, na hiyo ni kwa sababu ya umbo langu, na kwa sababu ya mama yangu.

Hili limetakatazwa mwanangu, na unaweza kumuambia mwalimu.

Nitamwambia, lakini najua kuwa hawataacha kusema ila mbele ya mwalimu tu.

Joji alipata kigugumizi moyoni mwake pale walipotoka watoto wake:

Hata Sali anajua tofauti kati ya utaratibu wa kimaadili na kati ya maadili peke yake!

Joji aliendelea kusoma Qur’an hadi alipoingia Katarina.

Ilikuwa ni siku ndefu ilioje!

Samahani, dakika tu.

Kitu gani unasoma?

Nasoma kitabu cha Waislamu, Je unaweza kunisubiria muda mimi nina kazi.

Umefika wapi kusoma?

Sijamaliza.

Unaonekana umezama.

Sikia, nini anasema Mola katika kitabu cha Waislamu: “Alif Lam Ra. (A.L.R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur’ani inayo bainisha. HUENDA ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu. Waache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua. ” (15: 13)

Kwa nini umechagua ayah hizi au kipande hiki hasa?

Sijui hasa, ni kwa nini baadhi ya maeneo ya kitabu hiki yananiongelea mimi kwa dhati? Miongoni mwayo ni kipande hiki.

Ni nini ambayo kinakuongelea katika kipande hiki?

Kitabu kinachobainisha…makafiri wanatamani Uislamu..Hawa makafiri wanadanganyika kwa kula na kustarehe, sijui kwa nini! nahisi aya hizo zinanisemesha mimi?

Je zinakulenga wewe, yaani wewe unatamani kuwa Muislamu?

Fikiria, haiwezekani …lakini natamani nipate majibu ya maswali yangu, na nipate njia ya furaha, na nisishughulishwe na kula, kunywa, na kustarehe, sijajua ni kwa nini nahisi baadhi ya aya zinanisemesha mimi mwenyewe hasa?

Je haiwezekani kwamba njia ya furaha ikawa Uislamu?

Haa haaa –ni kama maneno ya Adam, ijapokuwa mimi sidhani hivyo, lakini nitaurudi Uislamu kwa elimu kama nilivyozijibu dini zingine na sio kuishia katika dhana tu.

Kwa mnasaba kwanza vipi habari ya Adam?

Wewe umemuona baada yangu, na mimi sijamuona leo hii, kuna mambo mengi sana yametokea kazini leo.

Nipe habari nzuri, kuna jipya?

Kakhi amenipa ofa mpya ya kusafiri kwenda Ujerumani, pasi na kuacha maadili yangu.

Je umewafiki na kumaliza tatizo?

Hapana, nimemwambia kuwa nitatafakari, kwani mimi sitaki kusafiri kwa sasa.

Kwa hiyo masuala sio maadili, kadhia kwa sasa ni rai.

Hivi ndivyo Kakhi alivyonieleza..kwa hakika zimejitokeza sababu zingine, hakika nimemshauri Tom na yeye ana rai nyingine.

Ni ipi rai ya Tom?

Ananitaka nienda Misri.

Uliniambia Ujerumani?

Kakhi amenipa uchaguzi: Ujerumani au Misri au Ukraine, na mimi napendelea Ujerumani na Tom ananihimiza Misri.

Ni kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa maswali yako?

Ndio, lakini sipendi kwenda katika nchi zisizo za maendeleo za Afrika, badala ya nchi yenye nguvu na maendeleo kama Ujerumani.

Lakini Misri pamoja na kujua Uislamu na waislamu pia ni nchi ya Wakoptiki na ni nchi yenye Piramidi na mto Nile.

Unaelekea wewe kuijua Misri vizuri!

Ndio, ni nchi ya kanisa la Orthodoksi wa Kikoptic, na nchi yenye moja ya maajabu ya dunia, piramidi, ni nchi yenye mto mrefu duniani. Mto Nile, nilikuwa namjua mkoptik wakiothodoksi na mara nyingi alikuwa akiwakosoa sana Wakatoliki…ananikosoa kwamba mimi ni mwenye kurahisisha sana mambo ya dini kama sisi tunavyowakosoa nyinyi Waprotestanti.

Kwa sababu nyinyi mmejigawa kutokana na wao kama walivyojigawa Waprostanti kutokana nanyi. Je nielewe kutokana na maneno yako kwamba wewe ni kama Tom unaunga mkono Misri kuliko Ujerumani?

Huenda, ila uamuzi unao wewe, mimi napenda nchi zenye historia za kale, na huenda wewe unapenda nchi zilizoendelea, zilizozuka sasa hivi, japokuwa umestarehe sana ukiwa India.

Nitaangalia, lakini unaonekana unaunga mkono mimi nisafiri.

Japo mimi natamani tukae pamoja na tustarehe baada ya safari zako zilizofululiza, lakini kujivua na misingi au maadili inamfanya mtu kupata hasara mwenyewe, na laiti ungethibiti katika maadili yako huenda ungepata hasira katika kazi yako, na huenda kwa hatua hii ni bora kuhusiana na maudhui yako.

Ndio, huenda hii ndio njia bora ya kujikomboa, kwa hali yoyote bado ninayo fursa mpaka kesho kutafakari zaidi juu ya maudhui, na wewe je unalo jipya katika maudhui yako?

Ndio, natamini huenda likawa limeisha.

Limeisha, nini lililoisha?

Nadhani huu ndio mwezi wa mwisho kufanya kazi kwao.

Na baada ya hapo?

Nimeanza mpango wa kutafuta kazi nyingine, usijisumbue nafsi yako nitakueleza hatua kwa hatua, nataka kuwaandalia chakula cha mchana Sali na Maiko.

(4)

Wakati wa ziara ya jioni Joji alielekea hospitalini kumtembelea Adam, aliingia ndani na kumkuta akiongea na Sheikh Baasim huku wakicheka.

Karibu, inaonyesha leo mna furaha.

Namshukuru Allah, mimi nina furaha siku zote, na leo furaha ni zaidi kwako na kwa kaka yangu Adam, habari yako?

Ni nzuri, vipi hali yako ewe Adam?

Mimi ni mwenye afya nzuri, namshukuru Allah mwenye fadhila.

Nimekuja ili kukujulia hali yako na kukuomba ushauri wa jambo!

Karibu.

Sitarefusha muda wako, mimi nimeingia katika mtihani baina ya maadili yangu na kazi zangu, na baada ya mvutano huo nimechagua maadili yangu, na mambo yangu yamekuwa mepesi, lakini kwa safari ya ghafla.

Kila mwenye kuthibiti katika maadili hata kama itaonekana kupata hasara lakini atafaidika mwishoni.

Sheikh Baasim alitabasamu na kusema:

Samahani naomba kuongezea, Je hujaisoma Qur’an namna gani Mitume walishinda kwa subira zao na maadili yao?

Enyi Waislamu mnayo katika Qur’an kwamba kila Mtume alinusurika bali hata Issa alinusurika na hakuuwawa, ama kwa upande wetu sisi ni kwamba Issa alijitoa muhanga kwa ajili ya wanadamu ili kuwakomboa.

Sheikh Baasim akiwa mwenye tabasamu:

Haa haa kwa hivyo Uislamu unamthamini Yesu na kumpenda zaidi kuliko nyinyi.

Lakini haumpi sifa na maajabu na kuwatetea wanadamu kama sisi.

Bali unampa sana, inaonyesha hukusoma Qur’an, je hukusoma kisa cha Yesu katika Qur’an na maudhui zaidi?

Mimi sijachukua tarjumi kutoka kwake ila jana tu, lakini nimesoma vitu takriban vyote, na nimesoma kisa cha Yesu mfalme wa amani.

Ikiwa umesoma chote, basi nataraji kuwa umesoma tarjumi ya kauli yake Mwenyezi Mungu katika sura ya maryam kwa ndimi ya Yesu (Juu yake amani): “Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai” (19:31)

Na kauli yake Mwenyezi Mungu:

“Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.” (19:33)

Na tarjumi ya kauli yake katika surat AlImraan:

“Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini.” (3:49)

Ndio, nimesoma zote ulizozitaja, lakini ajabu yenu ni jinsi mlivyompokea Yesu!

Je unapenda ukweli.

Haa haa, bila shaka.

Nyinyi hamumpokei Yesu kama sisi.

Ki vipi?

Nyinyi mnamuona kama amesulubiwa, na sisi tunaamini Allah alimpaisha, je, hujaisoma ayah katika Sura ya AnNisaai: “Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.” (4:157)

Ndio.

Nyinyi au kwa uchache baadhi yenu, mnaamini kuwa Bi Maryam mwenye kutakasika kwamba amezini.

Na katika nyinyi wapo wanaoamini ni baba wa Yesu.

Hana baba, ni kama alivyomuumba Adam bila ya baba wala mama, kadhalika Yesu ameumbwa kutokana na mama bila baba, na yeye aliongea akiwa mchanga, ili amtetee mama yake mtoharifu.

Bali heshima yetu ni kwa dini zote tangu kwa baba wa binadamu Adam juu yake amani, Mitume wote walikuwa wakilingania kitu kimoja ambae ni Mungu mmoja, na kila Mtume aliyeletwa alikuwa anabashiri kwa Mtume baada yake, je hukusoma tarjumi: “Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri! ” (61:6) Je siyo hivyo katika kitabu chenu?

Hapana, sijasoma ulichotaja, huenda ikawa kwenye zile zingine zilizosalia ambazo sijazisoma, ni hivyo katika baadhi ya vitabu vyetu tu.

Tatizo la injili ni kwamba imebadilishwa mara nyingi sana na katika uandishi tofauti tofauti, na hasa kipindi ambacho Wayahudi waliwabana Wakristo.

Nahisi hili ni tatizo la vitabu vyote vitakatifu, niletee kitabu ambacho hakijabadilishwa.

Qur’an haijabadilishwa katu, kwa mujibu wa maafikiano ya Waislamu wao kwa wao na hata wasiokuwa Waislamu bali hakuna kitu kilichodhibitiwa kwa kunakiliwa kwa kiwango cha wanadamu kama Qur’an na hili limethibitishwa na hata wasiokuwa Waislamu, wamenakili maelfu ya watu kutoka kwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na kutoka kwake wakanakili maelfu, na wala hakuna tofauti kati ya mtu na mtu mwingine katika kunakili na hata herufi moja kutofautiana, sio herufi tu bali hata chini ya herufu.

Ni nini hicho chini ya herufi?

Katika lugha ya Kiarabu kuna kitu kinaitwa udhibiti, nayo ni sauti ya herufi, na kitu walichokubaliana katika Qur’an, bali wamekubaliana hata katika namna ya usomaji wake na uvutaji wake.

Je hakuna tofauti kati ya nakala zake?

Katu, ila kuna tofauti ya visomo vilivyo pokelewa na wapokezi tofauti tofauti lakini hakuna tofauti ila katika lahaja tu.

Kwa maneno yako, inawezekana kuwa Yesu katika kisomo kingine ameuliwa, na kisomo kingine amejitoa mhanga?

Haiwezekani, kwani Qur’an ni moja na haitofautiani, ninachomaanisha ni tofauti ya utamshi tu, na mara nyingi ni maana hiyo hiyo au maneno hayo hayo tu, tofauti ipo katika matamshi tu.

Kwa kiwango hiki nadhani unazidisha!

Unaweza kusoma yale yaliyosemwa na wanahistoria wenu na utakuta yanalingana na niliyosema mimi.

Lakini…je huoni wewe unazidisha au mwenye hamasa kupita kiasi?

Huenda, lakini Adam ameniambia ulikuwa unatafuta majibu ya maswali yako kwa muda mrefu na umepitia dini zote kutaka kujua, na sasa umefikia kuufahamu Uislamu, na amenieleza wewe unataka majibu ya kielimu yanayo endana na uhakika.

Adam alijiweka sawa katika kikao chake na akaingilia mazungumzo yale:

Mjadala ni mzuri, samahani kwa kuwakata, niambie ulikuwa unataka kuniomba ushauri gani Joji?

Kwa kweli umenisahaulisha maudhui yangu ewe Baasim.

Samahani Joji.

La muhimu ni kuwa baada ya kushikilia maadili yangu nimefika katika njia panda; ima nisafiri safari ya kikazi isiyopingana na maadili yangu au niache kazi yangu, na mimi nina hamu ya safari, na wakati mwingine najihisi kuchoka na safari nyingi.

Wewe umetoka katika safari na kwenda safari!

Umesema kweli, ukweli sina hamu ya safari, lakini inaonekana ndio sehemu bora zaidi ya kutokea kutokana na tatizo langu kazini.

Uchovu wa mwilini rahisi kuliko mtu kayaacha maadili yake, na ikiwa utajivua nayo; kwa hakika roho yake itachoka, na wapi unakusudia kusafiri?

Kwenda Ujerumani au Ukraine au sehemu nyingine ile.

Nilikuwa natamani usafiri kwenda katika nchi ya Waislamu, kama ulivyosafiri kujifunza dini za wanadamu (za ardhini), kisha kujifunza Uyahudi, kisha Ukristo, nilikuwa natamani usafiri; ili uujue Uislamu zaidi.

Ujerumani au Ukraine au Misri.

Adam aliangalia chini na kuachia mikono yake: Oh, natamani sana Misri, mimi na Sheikh Baasim tumetokea Misri, natarajia wewe utaujua Uislamu vizuri kama utakwenda Misri.

Je wewe ni Mmisri?

Ndio, na nadhani nilikujulisha hapa kabla.

Huenda, lakini sikumbuki.

Ikiwa utakwenda Misri, nitaongea na baadhi ya rafiki zangu wakupokee huko, na wakupeleke sehemu za kitalii.

Sheikh Baasim kwa sauti ya furaha:

Ndugu yangu ni mwalimu wa hesabu Cairo, huenda akakutayarishia kila unachohitaji.

Pamoja na kuwa nilikuwa na hamu ya kuelekea Ujerumani, ila ni kuwa kila ninayemtaka ushauri ananiambia niende Misri, huenda kama ni hivyo nikamjibu Kakhi kesho kuwa nitasafiri kwenda Misri.

Na mimi nitasubiria jibu lako ili nimwambie ndugu yangu.

Laiti ningesafiri pamoja nawe, nimetamani sana Misri, nimewakumbuka jamaa, ni takriban miaka miwili sijarudi huko.

Kwa nini hatuendi pamoja na mimi?

Kesho kutwa nitapewa ruhusa ya kutoka hospitali Inshaalah, na mitihani ya Chuoni ni baada ya wiki tatu.

Kwa kuwa unaendelea vizuri hili linatosha, unataka zawadi gani nikuletee kutoka Misri wewe na Baasim?

Haa haa, niletee Misri yote.

Haa haa.

Usiku ulipoingia Joji alifungua email yake na kukuta majibu ya rafiki zake yamefuatana kuhusiana na swali lake juu ya Qur’an, na kuwarudishia tena baada ya kuifupisha.

Levi: Sina jibu la wazi, nimesoma baadhi tu, muda haukutosha. Habib: Kimeandikwa kwa umakini zaidi kuliko vitabu vingine vya mbinguni. Tom: Samahani, nilishughulishwa na kliniki, sijasoma kitabu cha Waislamu ila kidogo tu, lakini nitakisoma. Katarina: Kinaonekana kweli kimetoka kwa Mungu. John Luke: Kielimu Qur’an ni thabiti, imenukuliwa kutoka kwa Muhammad bila kubadilishwa, hivyo basi mwenye kumuamini Muhammad ni wajibu kwake kuamini kuwa Qur’an imetoka kwa Mungu.

Na kilicho mshangaza Joji ni kwamba John Luke baada ya barua yake chini yake ameandika jina lake, kisha TripoliLibya, kisha akatuma email mpya kwa wote:

“Barua ya nane: Ninataka muujue Uislamu zaidi, na nategemea kusafiri kwenda Misri; kwa kadhia iliyojitokeza, na mwenye: “Marejeo na anijulishe; ili kuujua Uislamu au kuijua Misri. Mambo yanayotakiwa kujadiliwa au kuchambuliwa. Majibu yanayo takiwa kuwasilishwa. Nasubiri majibu yenu kwa muda wa siku mbili au tatu hivi, kisha nitachambua na kutuma kwenu muhtasari wake kama ilivyo ada yetu. Ni mimi Joji.”