sababu za saada

sababu za kusuudika

sababu za kusuudika

Furaha katika maisha ambayo tunayaishi katika Uislamu yana vyanzo vingi na sababu mbali mbali, miongoni mwa hizo ni:-

Furaha kwa Tawhidi na imani kwa Allah

Hakuna furaha wala raha wala utulivu kama ilivyokuwa raha na utulivu wa Tawhidi, Allah Aliyetukuka amesema: “Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka.” (6:82)

$Nazmi_Luqa.jpg*

Nazm Luka

Mwanafalsafa na Mwanafikra wa Misri
Itikadi Nyepesi
“Itikadi ya Kiislamu ni itikadi moja ambayo ni nyepesi ambayo imani inakata nayo njia ya kila mwenye hofu na babaiko, na kufufua utulivu katika kila nafsi. Mlango wa akida hii upo wazi kwa mwanadamu yeyote. Haufungiwi dhidi ya yoyote (kuzuiwa kuingia) kwa sababu ya jinsia au rangi yake. Hivyo basi kila mtu hupata nafasi yake chini ya kivuli cha itikadi ya Mungu kwa misingi ya usawa na uadilifu ambao haimfadhilishi yoyote pamoja nayo ila kwa ucha-Mungu. Ucha-Mungu kwa Allah Mola wa Walimwengu.”

Hivyo basi hupimwa ukamilifu wa tawhidi na utimilifu wake kwa jinsi amani, utulivu, furaha inayopatikana duniani na akhera, ambapo Allah humuingizia mtu mwenyewe furaha ndani ya Nafsi yake.

Ama Shirki (Allah atulinde) ambao inamfanya mtu mwenyewe kuwa na dhiki, tabu na mashaka ndani ya kifua cha mtu mwenyewe kama kwamba anapaa mbinguni. Allah amesema: “Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni. Namna hivi Mwenyezi Mungu anajaalia uchafu juu ya wasio amini.” (6:125),

Hivyo bali hawalingani kati ya yule ambaye Allah amekunjua kifua chake kwa Uislamu; yeye yupo kwenye nuru ya Mola wake, na aliye katika kiza cha ushirikina kuwa mbali na dhikri ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) moyo wake umekuwa mgumu; naye yupo kwenye upotevu ulio wazi: Allah Aliyetukuka amesema: “Je! Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfungulia kifua chake kwa Uislamu, na akawa yuko kwenye nuru itokayo kwa Mola wake Mlezi (ni sawa na mwenye moyo mgumu?) Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisio mkumbuka Mwenyezi Mungu! Hao wamo katika upotofu wa dhaahiri.” (39:22)

$Lauren_Booth.jpg*

Lauren Booth

Mwana harakati wa kutetea haki za Binadamu wa Uingereza.
Amani ya Kweli.
“Ninapata hisia kama wapatavyo Waislamu wanaposwali; Hisia tamu inapochanganyika na furaha na hilo ndilo nililokuwa nikihisi na kushukuru kwa sababu yake. Kama ambavyo watoto wangu wapo katika amani. Kwa hakika sitaki zaidi ya hayo.”

Na hawi sawa yule aliyekuwa maiti katika kiza cha ushirikina kisha akaongozwa na Allah kwa fadhila zake na rehema zake kama yule aliyebakia katika kiza cha ushirikina hatoki humo, Allah Aliyetukuka amesema “Je, aliye kuwa maiti kisha tukamhuisha, na tukamjaalia nuru inakwenda naye mbele za watu, mfano wake ni kama aliyoko gizani akawa hata hawezi kutoka humo? Kama hivyo makafiri wamepambiwa waliyo kuwa wakiyafanya.” (6:122).

Kumtaja Allah Aliyetukuka na kumuomba na kuwa karibu nae

Vyovyote mwanadamu atakavyopewa katika mapambo ya dunia na maisha yake, na vyote atakavyomiliki na kupata sababu za furaha; hatoweza kupata furaha muda wa kuwa yupo mbali na njia ya Allah.

Mwanadamu hatopata utulivu ila atakapokuwa karibu na Allah na katika kivuli chake cha harufu nzuri ya dhikri yake Allah amesema: “Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!” (13:28);

Na hiyo ni kwa sababu: “Ndani ya moyo wake mambo yameparaganyika ambavyo hayakusanyiki ila kwa kuwa karibu na Allah Ta’ala, na hiyo ni kwa sababu: “Ndani yake kuna ambayo haliondoshwi isipokuwa kwa kujiliwaza kwake katika faragha yake (kumkumbuka Allah) na kadhalika kuna huzuni ambayo haiondoki isipokuwa kufurahi kwa kumjua Allah na ukweli wa kuamiliana nae na ndani yake kuna babaiko ambalo halitulii isipokuwa kwa kukusanyika kwa ajili yake na kumkimbilia yeye tu.

Vivyo hivyo ndani ya moyo wa mtu kuna moyo wa majuto na wenye hasara hauzimwi isipokuwa kwa kuridhia maamrisho yake, makatazo yake na hukumu zake na kuikumbatia subira juu ya hayo, hadi mtu atakapokutana na Mola wake, na kuna kutafuta sana ambayo hakuna chenye kumzuia isipokuwa matakwa yake kwa Mola wake yawe peke yake, na ndani yake kuna balaa ambalo haliondolewi isipokuwa kwa mapenzi na kumtegemea yeye tu na kudumu katika dhikri yake na ukweli wa kumsafishia nia, hata kama mtu huyo atapewa dunia yote na vilivyomo basi hiyo haja yake haitozibwa milele.”

Matendo mema

Allah Aliyetukuka amesema: “Wale walio amini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri.” (13:29)

Walioamini kwa nyoyo zao–kuamini Mwenyezi Mungu, Malaika wake, vitabu vyake, Mitume yake na Siku ya Mwisho na imani hii ikasadikishwa na matendo mema–matendo ya nyoyo; kama vile kumpenda Allah, kumuogopa na kumtarajia, na matendo ya kiwiliwili, kama vile Swala na mfano wake wanakuwa katika hali nzuri ya ukamilifu wa raha na utulivu, na hiyo ni kwa sababu ya kupata kwao radhi za Allah na utukufu wake duniani na akhera, hivyo ni juu yetu matendo mema pamoja na imani, Allah Aliyetukuka amesema: “Hakika walio amini, na Mayahudi na Masabii na Wakristo, walio muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya mwisho, na wakatenda mema, basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.” (5:69),

Na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alikuwa akipata raha na ladha yake ndani ya Swala na utii na alikuwa akisema: “Ewe Bilal kimu swala, tufurahishe nayo.” (Abu Dawuud).

Ukarimu ni siri ya furaha

Hili ni jambo lililokwisha jaribiwa na kushuhudiwa, sisi tunawaona wale wenye kuwafanyia wema wengine kuwa ni watu wenye furaha zaidi na ni miongoni mwa watu wanaokubalika duniani, Allah Aliyetukuka amesema: “KABISA HAMTAFIKIA wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua.” (3:92),

Na utoaji una mifumo mingi sana; kwani Allah amefanya utoaji wa mali kuwa ni sehemu ya nguzo ya Uislamu; akafaradhisha na akawajibisha Zakkah kutoka kwa tajiri kwenda kwa masikini, na Allah akaamrisha kuwa utoaji huu unapasa kuwa uzuri wa Nafsi na (Ikhlas) kwa Allah kwa yale mazuri na ayapendayo mwanadamu na kutosimbulia watu, Allah amesema: “Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi…” (2:264),

Bali amepanua utoaji ili mali ifikie kila utoaji, ni sawa uwe ni mali au chakula au juhudi, au amali, Allah amesema: “Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.” (76:8-9),

Bali hata ikiwa utoaji huo ni kutabasamu kutupu, Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Tabasamu lako mbele ya ndugu yako ni sadaka” (Al-Tirmidh).

Akasema vile vile: “Mwenye kuwa na hoja ya nduguye basi Allah atakuwa kwenye haja yake, na atakayemuondolea Muislamu tatizo Allah atamwondolea matatizo yake Siku ya Kiama, na mwenye kumsitiri Muislamu Allah atamsitiri Siku ya Kiama.” (Abu Dawuud).

Bila shaka utoaji huu ndio ambao unapasisha furaha ya dunia, Ama utoaji ili mtu apate chumo lakidunia au masimbulizi au maudhi hatopata chochote katika furaha hata kama hilo likidhihirika (kinyume) vinginevyo.

Kumtegemea Allah ni ufunguo wa furaha

Mara nyingi mtu hujihisi mnyonge na kutokuwa na uwezo wa kufanya kitu; na hurudi kwa mwenye nguvu akaomba msaada wake na kumtegemea ili afikie analotaka, sasa ni nani aliye na nguvu kuliko Allah?!

Kwa hakika ufunguo wa furaha ni kumtegemea Allah, mwenye nguvu na muweza ambaye anamiliki falme (Malakuti) za mbingu na ardhi, ambaye akitaka kitu husema: ‘kuwa na kikawa’, Allah amesema: “Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.” (36:82);

Hivyo Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ameamrisha kumtegemea Yeye peke yake, Allah amesema: “…Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini.” (5:23);

Basi ni toshelezo gani analolipata mtu baada ya hilo, atatosheka na Allah Aliyetukuka kuwa ndie wakili wake, Allah amesema: “…na umtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.” (4:81),

Bila ya shaka hilo litampa utulivu, raha, furaha na kutosheka na kutekeleza mambo ambayo mtu hafahamu isipokuwa yule aliye yajaribu, Allah amesema: “…Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea. Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” (65:2-3),

Mbali na ulinzi wake Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) anaowapa wanaomtegemea dhidi ya shetani, Allah Aliyetukuka amesema: “Hakika yeye hana madaraka juu ya walio amini na wakamtegemea Mola wao Mlezi.” (16:99),

Na maadui vile vile, Allah amesema: “Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa. Basi wakarudi na neema na fadhila za Mwenyezi Mungu. Hapana baya lilio wagusa, na wakafuata yanayo mridhi Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu. Hakika huyo ni Shet’ani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.” (3:173-175)

Na siri ya kumtegemea Allah na ukweli wake ni moyo wa mtu kumtegemea Allah peke yake, na hakutomdhuru kuvaana na sababu wakati ambapo moyo wa mtu humtegemea yeye, kama ambavyo kauli ya kusema kwake kuwa nimemtegemea Allah wakati ambapo anamtegemea asiyekuwa yeye, hivyo basi kutegemea kwa ulimi ni sehemu moja na kutegemea kwa moyo ni sehemu nyingine.

Furaha katika yakini na kumwamini Allah Aliyetukuka

Kwa hakika imani inampa muumini yakini na kumtegemea Allah kwa ukamilifu, jambo linalompa mtu kujiamini; hivyo haogopi lolote katika maisha haya, kwa hiyo atajua wakati wake kuwa mambo yote ni ya Allah Aliyetukuka, Allah amesema: “Na ikiwa Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea hayo ila Yeye. Na ikiwa akikugusisha kheri, basi Yeye ndiye Mwenye uweza wa kila kitu.” (6:17),

%%

“Kuna utafiti unaothibitisha kuwa mtu kuwasaidia wengine ni tiba ya babaiko la nafsi, wataalamu katika saikolojia wanathibitisha kwamba kuwasaidia wengine hupunguza wasiwasi na msongo wa mawazo ambapo kushughulika kwa hima katika kuwasaidia wengine huhamasisha kutoa Homoni aina ya hormone endorphins nayo ni homoni yenye kumsaidia mtu kuhisi raha ya kinafsi na hisia za juu za furaha, Alan Leeks Mkuu wa zamani wa chuo cha “Kukuza Afya” (institute for health promotion) huko Marekani anathibitisha kwamba kuwasaidia wengine husaidia katika kupunguza msongo wa mawazo ambapo mtu kuwasaidia wengine hupunguza mawazo yake yeye mwenyewe binafsi na matatizo yanayomkabili mwenyewe: Na mwisho hupata mwenyewe hisia za raha na utulivu wa nafsi.”

Kama ambavyo ana yakini kuwa riziki yake ni kutoka kwa Allah peke yake, Allah amesema: “Hakika nyinyi mnaabudu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, na mnazua uzushi. Hakika hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawakumilikiini riziki yoyote. Takeni riziki kwa Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na mumshukuru Yeye. Kwake Yeye ndio mtarudishwa.” (29:17),

Na ya kuwa hakuna mnyama aliyepo ardhini ila Allah anadhamini riziki yake, amesema Aliyetukuka: “NA HAKUNA mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote yamo katika Kitabu chenye kubainisha.” (11:6),

Hata kama hatoweza kuleta riziki yake Allah amesema: “Na wanyama wangapi hawawezi kujimilikia riziki zao! Mwenyezi Mungu anawaruzuku hao na nyinyi pia. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.” (29:60),

Na akawa na yakini kuwa riziki yake itamjia bila ya shida na hilo ni jambo la haki lisilokuwa na shaka ndani yake, Allah amesema: “Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa. Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema.” (51:22-23)

Na ya kuwa Yeye Subhaanahu Aliyetukuka amegawa riziki yake kwa watu na akamkadiria, Allah amesema: “Sema: Hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki na humdhikisha amtakaye. Lakini watu wengi hawajui.” (34:36)

Na ataamini imani ya kweli yenye kukata kuwa Allah anampa mtihani daima katika kheri na katika shari, Allah amesema: “Kila nafsi itaonja mauti; na tunakujaribuni kwa mtihani wa shari na kheri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa.” (21:35)

Na kama sio upole wa Allah Subhaanahu basi angeangamia maangamivu makubwa.

Kama ambavyo anajua kuwa yeye ni mgeni katika dunia hii vyovyote umri utakavyokuwa urefu au ufupi, bila shaka yeye atahamia katika ulimwengu mwingine; hivyo basi yeye anatembea katika dunia hii kwa msingi huu, haogopi misiba ya dahari, wala hamuogopi yoyote isipokuwa Allah, hata kama adui yake atakuwa karibu kiasi cha ncha mbili za upinde au zaidi;

Allah amesema: “Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana! (Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa! Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa. Na tukawajongeza hapo wale wengine. Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote. Kisha tukawazamisha hao wengine. Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini.” (26:61-67).

Hapa tunamuona bwana wa wenye yakini Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam), lau adui yake angeangalia chini ya miguu angemuona, lakini kwa imani na yakini ya Mola wake na wakati huo washirikina wakimuandama ili wamuue - anamwambia sahibu yake Abu Bakr (Radhiya Llahu ‘anhu) akiwa nae pangoni: “…Usihuzunike. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake, na akamuunga mkono kwa majeshi msiyo yaona, na akalifanya neno la walio kufuru kuwa chini, na Neno la Mwenyezi Mungu kuwa ndilo juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima.” (9:40).

Kama ambavyo ameyakinisha kuwa Allah ndie ambae amemkadiria mauti hivyo hayaogopi mauti, Allah amesema: “MWENYEZI MUNGU huzipokea roho zinapo kufa. Na zile zisio kufa wakati wa kulala kwake, huzishika zilizo hukumiwa kufa, na huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.” (39:42),

$Ernest_Renan.jpg*

Ernest Renan

Mwanahistoria wa Kifaransa
Imani na Maisha.
“Imani ni nguvu ambayo hapana budi ipatikane ili iweze kumsaidia mtu maishani. Kukosa kwake ni ilani ya kushindwa kukabiliana na maisha na changamoto zake.”

Bali ameyakinisha kuwa huo ndio ukweli halisi ambao hakuna kukimbilia, Allah amesema: “Sema: Hayo mauti mnayo yakimbia, bila ya shaka yatakukuteni. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda.” (62:8),

Na kuwa mauti hayaji isipokuwa wakati ule ulioandikwa, Allah amesema: “Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wachukulia watu kwa mujibu wa dhulma zao, basi asingeli mwacha hapa hata mnyama mmoja. Lakini anawaakhirisha mpaka muda ulio wekwa. Na unapo fika muda wao hawatakawilia hata saa moja wala hawatatangulia.”(16:61).

Kuridhika ni mlango wa njia ya furaha

$Roger_Du_Pasquier.jpg*

Roger Du Pasquier

Mwanafikra na Mwanahabari wa Kiswisi.
Basi Zianguke Staarabu za Vitu
“Imekwisha bainika kuwa Uislamu na misingi yake humletea mtu utulivu katika nafsi yake. Ama ustaarabu wa Maada (vitu) humpelekea mtu kukata tamaa: Kwa sababu wao hawaamini chochote, kama ambavyo imebainika kuwa watu wa Ulaya hawakufahamu Uislamu: Kwani wanapima kwa vipimo vyao vya kimaada.”

Furaha ni ile hali ya Nafsi ya mtu kuishi kwa kuridhika; kwa hiyo chuki, inda humkaba mtu maisha yake, roho yake na hisia zake, ama kuridhia ni mlango wa furaha, utulivu, ghera na furaha. Kwa hiyo utulivu katika moyo hadi kwenye uchaguzi wa Allah kwa mtu. Kwa hiyo utulivu huu unamfanya mtu kila kinachotokea katika maisha yake kuwa ni kheri kwa mwanadamu, furaha na raha, hivyo hamuangalii mwingine isipokuwa Mola wake tu, wala haoni hasara kwa chochote cha duniani, humfanya mja kufanya kazi kwa bidii na kumuomba Mola wake, kisha huridhika kwa yale Mola wake aliyomgawia; ili aishi maisha ya hali ya kuridhika na mwenye furaha. Kuridhika kuna aina nyingi; miongoni mwa hizo ni:-

1-Kuridhia kuwa Allah ni Mola na Uislamu ndio dini na Muhammad ni Nabii na Mtume, na ambae hatoridhia kwa hilo basi ataishi katika babaiko daima na maswali tata kila mara, amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Ameonja utamu wa imani atakayemridhia Allah kuwa ni Mola wake na Uislamu kuwa ni dini yake na Muhammad kuwa ni Mtume.” (Al-Bukhari).

Na yule ambae hakuonja utamu wa imani basi hajaonja utamu wa furaha, bali ataendelea kuwa katika babaiko na wasiwasi na tabu na kumridhia Allah ina maana kuamini uwepo kwa Allah na kuhisi ukubwa wake, hekima yake, uwezo wake, elimu yake na majina yake mazuri, na imani na kuridhia ibada yake, vinginevyo itakuwa ni shaka, wasiwasi, maradhi na huzuni na sononeko Mwenyezi Mungu utulinde na hayo.

2-Kuridhia hukumu za Allah na sheria zake, Allah amesema: “La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenyekee kabisa.” (4:65),

Na binadamu amejaribu njia za mashaka mengi, tabu na dhiki nyingi katika maisha yake hapa duniani kwa kutegemea sheria na hukumu na mifumo yenye dhuluma yenye mapungufu; kwa sababu ni katika matengenezo ya mwanadamu na sio katika sheria za Muumba wa watu, mwenye kujua yenye kumfaa mtu, Allah amesema: “Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” (67:14).

3-Kuridhia hukumu za Allah na Kudura zake Subhaanahu: kwani ana yakinisha kuwa haiwezekani kupata msiba isipokuwa kwa matakwa ya Allah Aliyetukuka, na ya kuwa Allah Aliyetukuka atauongoza moyo wake, Allah amesema: “Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.” (64:11),

Kuwa yeye anaridhika na hukumu ya Allah na kudura zake; kwa sababu anajua (kwa elimu ya yakini) kuwa yoyote haondoshi madhara isipokuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Allah Ta’ala amesema: “Na Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea ila Yeye. Na akikutakia kheri, basi hapana awezaye kurudisha fadhila yake. Huifikisha kwa amtakaye katika waja wake, na Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” (10:107).

Hakika miongoni mwa ajabu ya mambo ya imani ni kuwa muumini anachuma radhi kwa yale Allah aliyomgawia, na hivyo kusubiri juu ya misiba na matatizo, na kushukuru neema na anavyopata, na hili linamungizia ndani mwake kuridhika yale Allah aliyomgawia na hili halipati mwingine asiyekuwa muumini.

$Rex_Ingram.jpg*

Rex Ingram

Muandaaji Sinema maarufu Ulimwenguni.
Roho ya Uislamu.
“Mimi naamini kuwa Uislamu ni dini ambayo huingiza amani na utulivu ndani ya nafsi. Na humfundisha mwanadamu utulivu, kupumzisha akili katika maisha haya. Roho ya Uislamu imetambaa kwenye nafsi yangu: Nikahisi neema ya kuamini hukumu ya mungu na kutokujali athari za Ki-Maada kama vile utamu na uchungu.”

Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Ni ajabu jambo la muumini, hakika mambo yake yote ni kheri na hilo haliwi kwa yoyote isipokuwa muumini, akipata yenye kufurahisha anashukuru na hivyo kuwa ni kheri kwake, na akipata lenye kudhuru anasubiri na hivyo kuwa ni kheri kwake.” (Muslim).

Bali Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ametufundisha namna ya kuridhika hata kama tumemuona aliye juu yetu katika kupata neema na starehe za hapa duniani, amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Waangalieni walio chini yenu na wala msiwaangalie walio juu yenu, kwani hilo litawafanya msidharau neema ya Allah kwenu.” (Bukhari na Muslim).