MAANA YA FURAHA NA HAKIKA ZAKE

MAANA YA FURAHA NA HAKIKA ZAKE

MAANA YA FURAHA NA HAKIKA ZAKE

Maana ya furaha

Neno furaha ni miongoni mwa maneno ambayo watu wametofautiana; kuna miongoni mwao wanaona kuwa ni mwenza wa neno ladha au raha au mali au cheo au umaarufu na kadhalika.

$Roger_Du_Pasquier.jpg*

Roger Du Pasquier

Mwanafikra na Mwandishi wa Kiswisi
Dini ya furaha na Utulivu
“Nilikuwa nikijiuliza: Kwa nini Waislamu wanahisi furaha imetawala katika maisha yao pamoja na ufukara wao na kukosa kwao maendeleo?! Na kwanini Wasweden wanahisi dhiki na huzuni pamoja na maisha mazuri, starehe na maendeleo makubwa wanayoishi nayo?! Hata nchini mwangu Uswisi nilikuwa nikipata hisia zile zile za Wasweden pamoja na kuwa ni nchi yenye maendeleo makubwa na kiwango cha juu cha maisha!! Mbele ya yote haya nimekuta kuwa nafsi yangu ina haja ya kusoma dini za Mashariki, na nikaanza kuusoma Uhindu, sikukinaishwa nayo sana, hadi nilipoanza kusoma Uislamu uliponivuta na kuona kuwa haugongani na dini zingine bali imebeba dini zote; nayo ni dini ya mwisho inayohitimisha, ukweli huu kwangu ukawa (umoja wa katiba ya wananchi) unapanuka kwa kupanuka kusoma kwangu hadi ikazama kwa ukamilifu akilini mwangu.”

Na kwa sababu hiyo watu wengi hupoteza maisha yao katika njia mbali mbali wakitafuta furaha, ndio…furaha ni hisia inayotoka ndani ya nafsi ya mwanadamu anapohisi hali ya kuridhika na utulivu, hata hivyo mtazamo wa watu kuhusu furaha umetofautiana na hii ni kutokana na tofauti tabia zao, mapenzi yao, na matarajio yao, na hata jamii zao, baadhi ya watu wanaiona ipo kwenye mali au makazi au cheo na afya, na wengine wanaiona ipo kwenye mke, au watoto au kazi au masomo na huenda wengine wakaiona ni kuwa ukaribu na mpenzi au katika kuondokana na mtu mwenye kero au katika hisia nzuri ya kiroho au kumsaidia masikini na fukara, ama jambo la kushangaza ni kuwa utakapo wauliza wengi miongoni mwa watu hawa: Je, wewe ni mwenye furaha? Jibu lake litakuwa ni kwa kukataa!!!

$Naseem_Sousa.jpg*

Naseem Souza

Mhadhiri wa Kiyahudi wa Iraqi
Furaha kwa Wanadamu.
“Inatupasa kupotea kwenye fikra kuwa maendeleo ya Magharibi kwa sasa yamefeli kwa sababu ya kuridhisha nafsi za watu na na kushindwa kushughulikia katika kuleta furaha ya kibinadamu kwa hiyo ikawatupa watu katika shimo la kuangamiza na kumaliza kila kitu. Ni mbali hali hii kusifika kwa ukamilifu, au iwe nyenzo ya kumtumikia mwanadamu kama ilivyokuwa katika zama za Uislamu.”

Kwa hiyo utaona kuwa taarifu zina tofautiana baina ya mtu na kwa mwingine na jamii moja hadi jamii nyingine, kiasi cha kufanya jumuia ya kimataifa kuweka daraja jina lake daraja la furaha miongoni mwa mataifa, walitaka kujua ni taifa gani lenye furaha zaidi, na hivyo basi kuzipa alama daraja hizi na wakasimamia ufuatiliaji na tafiti mbali mbali, Lakini matokeo yaliwa shangaza wote; hivyo Wamerekani wakawa ndio wenye matatizo zaidi na si furaha, na hawakupata isipokuwa alama za chini kabisa, pamoja na kuwa tunajua hali ya starehe na mas-ala ya anasa kwa watu wake.

Taifa lenye furaha zaidi ulimwenguni

Cha kushangaza mno ni kuwa watu wa Nigeria ndio waliopata alama kubwa zaidi na ndio walioonekana ni watu wenye furaha zaidi pamoja na ufukara wa watu hawa!!!

Hayo ndio yaliyokuwa matokeo ya mwisho ya utafiti huo uliofanywa na jarida la Newsweek la Marekani kuhusu taifa gani lenye furaha duniani, ambapo Nigeria nchi fukara yenye wakazi wengi Waislamu kuwa juu ya orodha miongoni mwa nchi sitini na tano, na kufuatiwa na nchi za Mexico, Venezuela, Salvador, wakati ambapo nchi zilizoendelea sana zimepata daraja za chini.

Katika majibu yao Waamerika wengi walikiri katika ripoti hii kuwa suala la furaha halihusiani na utajiri na mali , na hili ndilo linaloonekana kuwa jambo la kushangaza katika jamii inayofuata programu maalum ambayo imeasisiwa katika misingi ya Kibepari uliopetuka mipaka; jambo lililoisukuma jarida hilo hilo baada ya hapo kuangalia suala linaloenea kwa Wamarekani kurudi kwenye dini huko Marekani jambo ambalo linafanya maswali yarejee tena upya kuhusu hamu kubwa ya Wamarekani ya kutafuta furaha, kupitia njia za tafakuri za juu juu tu, ambayo mtu anapewa kama dozi ya tiba ya Nafsi kwa watu wenye matatizo hayo.

Matatizo haya yanaonekana katika maana ya furaha na jinsi ya kuipata kwa wengi wenye kuijua; Plato aliona furaha kuwa ni fadhila za Nafsi. (Hekima, ushujaa, kujitunza na uadilifu) na akazingatia kuwa mwanadamu hawezi kupata furaha iliyo kamili ila baada ya roho kurejea katika ulimwengu mwingine (akhera).

Ama Aristotle alizingatia kuwa furaha ni hiba kutoka kwa Allah, na akaigawa katika vipengele vitano; navyo ni: Afya ya kiwiliwili na usalama wa milango ya fahamu na kupata utajiri na namna nzuri ya kutumia, na kufanikiwa katika kazi na kufanikisha ndoto za mtu na usalama wa akili na usahihi wa itikadi ya mtu; sifa nzuri na kuwafanyia hisani watu.

Katika Saikolojia tunaweza kufahamu furaha kwa wasifu wa kuakisi kuridhia na maisha au kuakisi kurudia mara kwa mara kwa hisia za mambo yenye kufurahisha, hata hivyo Swali linalobakia katika tofauti hizi katika ufahamu wa furaha, Ni nini maana ya furaha? Na vipi naweza kuwa mwenye furaha? Na je furaha hufikiwa kwa kufanikiwa kwa kuthibitisha ladha fulani?

Ufahamu wenye makosa kuhusu maana ya Furaha

Mara nyingi watu huwa nyuma ya ladha mbalimbali, hawaachi ladha ila wataiendea na wataiendea na anadhani kama akipata ladha zote basi atakuwa amepata furaha, lakini hushtukizwa na kuwa mbali kabisa na mtu mwenye furaha, ladha zilizopo duniani ni nyingi sana na za kila namna na hubadilika maumbo, na wasifu lakini sio kila ladha ina furaha ndani yake, hivyo basi watu huchanganya maana ya furaha na maana ya ladha, kilichokuwa sahihi ni kuwa zinakutana upande mmoja mahali na kuachana upande mwingine, kukutana ambako kila kimoja humuingizia mtu furaha ndani ya nafsi yake, lakini huachana na kutengana, na tofauti baina yao ni kuwa ladha huchumwa na utamu wake huondoka mara moja baada ya kuondoka sababu zake, huenda baada ya hapo yakawepo majuto, na mashaka ambayo hakuna mfano wake, ama furaha huendelea kuwepo kwa mtu kwa muda mrefu.

Huku kuchanganya baina ya maana ya furaha na mtazamo wa ladha mara nyingi humuweka mtu katika utata kutoka kwa mtu mwenyewe na hivyo kudhania kuwa kila starehe ni furaha.

Umaarufu ni ladha isiyo na mfano wake, mtu kuwa mashuhuri na maarufu mbele za watu, watu humtanguliza mabarazani na humsifu –yote hayo ni aina za ladha, lakini ni watu hao hao maarufu na mashuhuri au wenye mali au vyeo au uzuri, pamoja na hayo lakini ni wenye huzuni, wenye kutibiwa na tabibu nafsi, au maisha yake yakaishia kujiua na hivyo basi kero, huzuni na tabu!!! Yakamuondoka.

Mara ngapi tumewasikitia watu mashuhuri maarufu ambao maisha yao yaliishia katika kujiua ili amalize maisha ya shida na tabu aliyokuwa akiishi na hivyo kuamua kuyaondoa kwa kujiua!!

Mara nyingi tunamuona mtu aliyeizamisha nafsi yake katika starehe za jinsia na kubadilisha mwanamke mmoja hadi mwingine na baada ya muda utakapomuulizia baada ya hapo utakuta ni mhanga wa maradhi ya AIDS!!

Mahusiano yaliyoharamishwa ni matamu lakini yanavunja familia, nyumba na kuangamiza jamii na kuchanganya nasaba za watu, na kuangalia filamu za jinsia kuna aina ya ladha na raha lakini kunavunja nafsi ya mtu mwenyewe, na kuvunja mahusiano matukufu, na kuifanyia uadui staha ya jamii, na katika aina zingine za ladha ni chakula; tunawaona walio na mapenzi ya kula kuliko vile yalivyo mapenzi yao ya ibada au zaidi ya hapo, na huenda akavimbiwa kwa kula kwake nyama kwa wingi au kula kwake vyakula vyenye sukari, lakini muda si mrefu mtu huyo tuna muona hospitalini kwa madaktari.

Wakati mwingine hii inakuwa ni kuingiliana kwa maana ya furaha na maana ya ladha, iliokusudiwa kutoka pande fulani hivyo basi pande nyingi zinajaribu kutangaza ladha mbali mbali kuwa ndio furaha yenyewe na kiini cha furaha, na malengo yao katika hilo ni kutawala akili za watu na kuzipeleka katika mielekeo tofauti, kwa mfano kijana mwenye kutumia madawa ya kulevya, mwanzoni hutumia ili apate ladha iliyokuwemo ndani yake, lakini baada ya hapo hubadilika kuwa ni mdoli katika mikono ya mwenye kumpa au kumuuzia!!

Matangazo mbali mbali ya biashara huwahadaa watu kwa bidhaa zake zinazotangazwa; utawaona sokoni wakitafuta bidhaa mpya au nguo mpya.

Furaha si kwa mwanadamu kupata kila akitakacho! Na kama ingekuwa hivyo basi matajiri wote pamoja na maraisi wangekuwa ni watu wenye furaha, ila tunachokiona katika tafiti mbali mbali za kisomi pamoja na hali halisi linapinga hilo, na huenda hilo ni kutokana na ukamilifu wa uadilifu wa Allah katika ulimwengu huu, Je, huoni furaha kwa fukara wengi pamoja na kuwa hawafahamiki! Basi kwani huoni furaha kwa matajri kutamani mambo mengi yalio kwa fukara ambayo yeye hana! Huenda basi furaha ikawemo kwenye raha!!