ALAMA ZA NJIA YA FURAHA

ALAMA ZA NJIA YA FURAHA

ALAMA ZA NJIA YA FURAHA

Ili kufahamu njia ya furaha katika hakika yake, ambayo ndio njia ya kumuamini Allah Aliyetukuka, ni vizuri kwetu tubainishe baadhi ya alama na Njia hii, ili tuwe watulivu na wenye hima za juu katika safari yetu hii.

Njia ya Allah Aliyetukuka

Allah amesema: “Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu.” (6:153),

$Carl_Jung.jpg*

Carl Jung

Mtaalamu maarufu wa tiba na Magonjwa ya akili Ulimwenguni.
Imani na Afya ya Nafsi
“Kwa muda wa miaka thelathini iliyopita nimewapa ushauri watu wa mataifa mbali mbali yaliyostaarabika ulimwenguni, nikatibu mamia ya wagonjwa. Sijapata tatizo moja katika matatizo ya wale wenye umri zaidi ya miaka thelathini na tano au mfano wake ila tatizo lao wote lilikuwa linarejea katika msingi wa kukosa kwao imani na kutoka katika mafundisho ya dini. Na ni sahihi kusema kuwa: Kila mgonjwa katika wagonjwa wale walikuwa ni mhanga wa maradhi: Kwa sababu wamenyimwa utulivu wa nafsi ambao unaletwa na dini. Hakupona hata mmoja miongoni mwao ila aliporejesha imani yake na kujisaidia kwa kufuata maamrisho ya dini na kuacha makatazo yake na kukabiliana na maisha yao.”

Hivyo basi njia ya furaha ni njia ya Allah na wasia wake aliousia waja wake kuufuata (naye ndie mjuzi wa yanayowafaa).

Hapana shaka yoyote kuwa mtu muovu ndie ambaye anaacha njia ya Allah na anatarajia furaha katika njia nyingi tofauti; hivyo hakuna furaha kwa hali yoyote ile bila ya kufuata njia yake, Allah Aliyetukuka amesema: “…basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” (20:123-124).

Furaha ni kwa aliyefuata njia na kufuata uongofu, na dhiki ni kwa yule aliyeupa mgongo na kukengeuka (kupotoka) hata idhihiri kuwa ni miongoni mwa watu maarufu au wenye nyota katika jamii.

Njia inayokusanya kati ya Furaha ya kiroho na furaha ya kiwiliwili

Kinachofahamika ni kuwa mwanadamu ni mkusanyiko wa roho na kiwiliwili, na kila kimoja kina chakula chake, na baadhi ya njia na falsafa dhaifu ambazo zimeshughulika na kujali upande wa kiroho tu na kukataa matakwa ya kiwiliwili ikawa ni tatizo ni kurejea tena, na wanaojali maada ya kisasa ni kinyume chake nao wamefuta na kuondoa mzizi wa mambo ya kiroho na kukipa kiwiliwili kila linachokitamani; hivyo kuondosha kundi kubwa la utu na ubinadamu kuelekea kwenye uhayawani wa ladha na matamanio! Au kuwafanya watu kuwa mashine zisizoweza kuzalisha.

Ama njia ya Uislamu roho yake imelishwa na mianga ya mbinguni na kuhifadhi kiwiliwili, na kushibisha hoja zake na matamanio yake kwa vitu vizuri vya halali: “Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe….” (28:77);

Mtume (Swala llahu ‘alayhi Wasallam) alithibitisha yale aliyoyasema Salman Al-Farisy (Radhiya Llahu ‘anhu):

“Kwa Mola wako una haki na nafsi yako ina haki na familia yako ina haki, mpe kila mwenye haki haki yake.” (Al-Bukhari).

Njia ya furaha na ujasiri

Atakayeonja utamu wa imani hatopenda kabisa kuachana nayo hata kama atawekewa upanga shingoni mwake, waangalie wachawi wa Firauni walipoamini na kufuata njia ya furaha, Firauni aliwatisha, na akawaambia kama ilivyo kuja katika Qur-aan Tukufu: “…Basi kwa yakini nitakukateni mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakutundikeni misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi aliye mkali wa kuadhibu na kuiendeleza adhabu yake.” (20:71)

Na jibu lao likawa la imara kabisa: “Wakasema: Hatutokukhiari wewe kuliko ishara waziwazi zilizo tujia, na kuliko yule aliye tuumba. Basi hukumu utavyo hukumu; kwani wewe unahukumu haya ya maisha ya duniani tu.” (20:72)

Na kilichothibitika kuhusu hilo baada ya muda mdogo tu kutokana na imani yao, na hiyo ni baada ya kuonja utamu wa imani hii ambayo imewafanya wakawa watulivu zaidi katika rai zao na maamuzi yao, bali hata katika hali ya kutishiwa kuuawa.

Furaha ni utulivu wa moyo

$Rosemary_Howe.jpg*

Rosemery Hawe

Mwanahabari wa Uingereza.
Majibu Toshelevu.
“Nimepata katika Uislamu majibu yenye kutosheleza kuhusu mas-ala tata ya roho na maada: Nikafahamu kuwa kiwiliwili kina haki kwetu kama ilivyo roho. Na kuwa mahitaji ya kiwiliwili katika mtazamo wa Uislamu ni silika asilia ambazo zinapaswa kushibishwa ili mwanadamu aishi akiwa ni mwenye nguvu na mwenye uwezo wa kuzalisha. Isipokuwa Uislamu umeweka kanuni za msingi ili kushibisha hoja hizi katika misingi ya amani ambayo itahakikisha ridhaa ya nafsi na kufuata maamrisho ya Allah. Kwa mfano ndoa katika Uislamu ni njia pekee ya kisheria ya kushibisha matamanio ya kijinsia. Na Swala, Saumu, kufanya ibada na kumuamini Allah ni njia nyingine ya kushibisha upande wa kiroho kwa mwanadamu, na kwa sababu hiyo hapo ndipo itakapothibitika mizani ya sawa ambayo hapana budi kwa maisha mema ya mwanadamu.”

Hakuna furaha isiyokuwa na utulivu, wala utulivu usiokuwa na imani, Allah Aliyetukuka amesema: “Yeye ndiye aliye teremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi Imani juu ya Imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ujuzi, Mwenye hikima” (48:4).

Imani humpa mtu furaha pande zote mbili:-

Kwanza: Inamzuia mtu kutumbukia katika shimo la uovu na jinai, nayo ni sababu hatari zaidi za tabu na mashaka, hakuna kitu kinachompa dhamana mwanadamu ili asivutwe na matamanio yake kufanya maovu yaliyokatazwa ila ni pale ambapo moyo wake unapokuwa ni mtupu wa imani kwa Mola wake.

Pili: Hiyo inatoa umuhimu mkubwa katika sharti miongoni mwa masharti ya furaha, nayo ni utulivu; katika wimbi la matatizo hakuna kitu kitakachoweza kumuokoa mtu zaidi ya imani bila ya imani khofu na wasi wasi humkumba mwanadamu.

Ama mtu akiwa na Imani hakuna chenye kustahiki kuhofiwa zaidi isipokuwa ni mtu kuwa mbele ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)

$William_James.jpg*

William James

Mwanafalsafa wa Kimarekani.
Imani na Babaiko Havikutani.
“Mawimbi makali ya bahari kamwe hayaathiri utulivu wa chini ya bahari. Wala kuathiri amani yake, vivyo hivyo mtu ambae imani yake imezama kwa Mungu kikweli ameepukana na babaiko na atahifadhi mizani yake, na atajiandaa wakati wote kupambana na matatizo yoyote yanayoweza kuletwa na masiku huko baadae.”

Katika Moyo wa muumini kila kigumu kinakuwa chepesi; kwa sababu humtegemea Allah na moyo mtupu usiokuwa na imani ni kama vile jani lililokatwa kutoka kwenye tawi lake, ambayo inachezewa hata na upepo mdogo upitao, Je! ni kitu gani kinachomtisha mwanadamu zaidi ya kifo na kuondoka katika ulimwengu huu?! Kwa muumini haswa sio jambo la kuhofia, bali ni jambo ambalo anatulizana nalo vile vile, mauti yana manufaa kwa yule ambaye moyo wake umejaa imani na ucha-Mungu!!

Kwa hakika imani inasukuma hisia ya utulivu kwa mtu; mtu aliyekuwa muumini hupita katika njia ya Allah kwa amani na utulivu; kwa sababu imani yake ya kweli daima humpa matarajio mema na kusubiria msaada wa Allah na ulinzi wake katika nyakati zote, nae huhisi mara zote kuwa Allah Aliyetukuka yupo nae kila wakati, Allah amesema: “…Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini. “ (8:19).

Muda wowote muumini atakapokabiliana na matatizo, na wakati wowote muumini matatizo yatakapomuelekea, na wakati wowote atakapopambana na mitihani basi Allah na maneno yake yanayong’aa kwa mwangaza wa Nuru ya uongofu hutosha kumuondoshea yote aliyonayo ndani ya Nafsi yake, kama vile wasi wasi na maumivu katika kiwiliwili chake na ugonjwa hivyo khofu yake kubadilika kuwa amani na salama kwake, na tabu zake, mashaka na huzuni kuwa furaha na uchangamfu, na hivyo basi huongozwa katika kufanikisha utulivu wa nafsi na furaha ya kiroho ambayo haikabiliani na furaha yoyote nyingine hata kama mtu huyo atamiliki hazina za dunia na vilivyomo.

Safari ya furaha kutoka duniani kwenda katika pepo yenye neema

$Cassius_Clay.jpg*

Casius Clay

Bondia wa Zamani wa Marekani.
Wema wa Amani
“Kila Muislamu anaposoma Qur-aan kwa undani zaidi na akasimamisha kutekeleza alama za Uislamu kwa ukweli, basi mtu huyu atakuwa amepanda wema wa amani katika msafara wa Uislamu. Na hivyo atakuwa amepanda vile vile treni ya utulivu na kuwa mbali na uchafu wa shetani.”

Kuwa maisha ya mwanadamu yapo katika hatua tatu: Ya kwanza ni hapa duniani, na ya pili ni Kaburini baada ya kifo na ya tatu ni Siku ya Kiama.

Njia ya furaha hupita katika hatua zote hizi tatu; hapa duniani Allah amesema: “Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.” (16:97) ;

Yaani tutamhuisha hapa duniani maisha ya furaha yenye utulivu na amani hata kama atakuwa na mali kidogo; na hiyo ni kwa kuridhisha nafsi na hali yake ya kiroho na ya kinafsi na hivyo kupata utulivu, na yakini yake kwa Allah Aliyetukuka na utulivu wake kwake (Allah).

Ama suala la furaha ya mwanadamu kaburini kwake; tunaliona katika aliyopokea Abu Hurairah (Radhiya Llahu ‘anhu) kuwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Hakika muumini ndani ya kaburi lake yupo katika bustani ya kijani, na kaburi lake hupanuka kwa dhiraa sabini na huingizwa mwanga kama vile usiku wa Badri.” (Al-Albany amesema kuwa ni Hadithi Hassan).

Ama kuhusu furaha yake Akhera Allah amesema: “Na ama wale walio bahatika, wao watakuwamo Peponi wakidumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hicho ni kipawa kisio na ukomo.” (11:108)

Na hapo atakuwa amefaulu kupata furaha duniani na neema zisizokwisha Akhera.

$Bernard_Shaw.jpg*

Sir George Bernard Shaw

Mwandishi wa Kiingereza
Dini ya Dunia na Akhera
“Mwanadamu msomi anaelekea kwa tabia yake katika Uislamu. Kwa sababu ni dini pekee ambayo inaangalia mambo ya duniani na akhera kwa usawa.”

Kwa hivyo Uislamu umeleta furaha ya milele; furaha ya mwanadamu katika maisha anayoishi sasa, na furaha katika nyumba ya akhera na kilicho kwa Allah ni kheri na ndicho kinachobakia zaidi na Allah amefanya furaha hii ya mwanadamu na furaha yake akhera ni vitu viwili vilivyo pamoja, bila ya mvutano kati yake wala mgongano.

Maisha haya ya dunia si chochote bali ni njia ya kuelekea akhera na kwenye furaha kuu zaidi Siku ya Kiama, zote ni njia moja, ni njia ya furaha milele duniani na akhera, Allah Aliyetukuka amesema: “Anaye taka malipo ya dunia, basi kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo ya dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” (4:134).