Huzuni ya kuwa mbali na Njia ya Furaha

Huzuni ya kuwa mbali na Njia ya Furaha

Huzuni ya kuwa mbali na Njia ya Furaha:

Njia ya furaha ya duniani na akhera

Uislamu umekuja ukiwa ni wenye kufaa mahala na zama zote, unakwenda pamoja na maumbile ya mwanadamu, ukichunga mabadiliko ya maisha, ukienda pamoja na maendeleo na ustaarabu wa mwanadamu.

Uislamu huu ukijishughulisha na kutibu matatizo ya Ummah na mataifa na ukishughulikia uchumi, siasa, hali zao za kijamii na kivita na mengineyo; isipokuwa ni kwamba watu wengi wamepotea njia hii yenye mwanga, na wengine wakaupiga vita na wakaamua kuchafua sura yake ili wawaweke watu mbali nayo.

Hili ndilo ambalo limewasababishia watu wengi matatizo miongoni mwa watu na jamii mbali mbali ulimwenguni; Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) amemdhamini atakayefuata uongofu wake na kushikamana na sheria yake kupata furaha ya nyumba zote mbili na akawahukumia tabu na mashaka na udhalili na unyonge kwa atakayeupa mgongo na kuwa na kiburi.

Uislamu huu ndio ambao Allah amemkalifisha nayo mwanadamu ili mambo yake yanyooke, ili afurahi hapa duniani na huko akhera na asipate tabu na mashaka ya kuwepo duniani na kupata malipo mema akhera, hata hivyo nafsi ya mwanadamu (kwa tabia yake) haipendi majukumu na kufungwa kwa matamanio yake na vitu avipendavyo, hata kama majukumu haya ni kwa maslahi yake mwenyewe; na ndio maana Allah amewafaradhishia watu wa haki kulingania kheri na haki waliyoongozwa kwayo, na waibebe haki hiyo kwa walimwengu wote. Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alitumwa ili afurahi na awafurahishe kaumu yake na watu wote ulimwenguni, Allah Aliyetukuka amesema: “Hatukukuteremshia Qur’ani ili upate mashaka. ” (20:2)

Na akasema vile vile: “Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” (21:107),

Hivyo basi kumfuata Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na kushikamana na njia yake ni chanzo cha furaha na njia ya kuokoka, na ni njia ya maisha ambayo Allah ametuamrisha tuyaishi katika jumla ya kushikamana na maamrisho yake na kukatazika na makatazo yake hayo matunda yake ni furaha katika nyumba zote mbili (duniani na akhera), na kutoka katika mipaka hii matokeo yake ni tabu na mashaka duniani na akhera, amesema kweli Allah pindi aliposema: “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa. ” (20:124-126).

Vipi utaishi maisha mazuri yenye utulivu

$H._G._Wells.jpg*

H. G. Wells

Mwandishi na Mwanafasihi wa Kiingereza.
Mwanga wa Uislamu
“Ni vizazi vingapi ambavyo vitapambana na hofu na tabu, kabla kuibuka tena kwa mwanga mpya wa Uislamu mtukufu ambao inadhihirika kuwa Historia nzima inaelekea upande wake. Wakati huo amani itafunika dunia na nyoyo za watu.”

Tofauti kubwa iliyopo kati ya muumini ambaye Allah amesema juu yake: “…tutamhuisha maisha mema….” (16:97)

Na mwenye kuupa mgongo ukumbusho wa Allah ambae Allah amesema juu yake: “…basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki” (20:124),

Hivyo basi maisha mazuri yanakuwa kwa mtu kushikamana na maamrisho ya Allah na kukatazika na makatazo yake kwa siri na dhahiri, na moyo kutulia kwa hukumu za Allah; kwa sababu anaishi kwa stara yake Allah na uangalizi wake Allah Aliyetukuka amesema: “Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!” (13:28)

Na hivyo basi utulivu ule wa moyo ukaakisi katika matendo ya mwanadamu katika mambo yote yanayokwenda kinyume kabisa na yule anayeishi maisha ya dhiki na tabu kama ilivyo katika kauli yake Allah Aliyetukuka: “Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni. Namna hivi Mwenyezi Mungu anajaalia uchafu juu ya wasio amini.” (6:125),

Hivyo basi dhiki na tabu yake ya maisha yake sio kwa sababu ya ufukara na sio kwa sababu ya maradhi, lakini hali ya wasiwasi katika matendo yake au katika maamrisho yoyote yanatokana na kupupia kwake dunia kwa mtu aliye na huzuni au kuupa kwake mgongo hakumuondoshi katika duara lake la mashaka na tabu zake, na sio sababu za mashaka aliyonayo, bali sababu yenyewe ni namna anavyofikiri na njia ya kufikiri kwake, hivyo basi ziada ya mali yake au upungufu wake na siha yake au maradhi yake huenda ikawa ni sababu ya kuongezeka kwa mashaka yake Allah Aliyetukuka amesema: “Yasikufurahishe mali yao wala wana wao. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwayo hapa duniani, na zitoke roho zao na hali wao ni makafiri.” (9:55),

Na akasema vile vile: “Wala zisikushitue mali zao na watoto wao. Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwa hayo katika dunia; na zitoke roho zao na hali wao ni makafiri.” (9:85).

Tabu na mashaka ayapatayo mwanadamu hayahusiani na utajiri au umasikini, wala maradhi au mitihani, bali tabu na mashaka ni mtu kuwa mbali na Allah na kupotoka na njia yake, na mja kukata kabisa mahusiano yake na Allah, Zakaria (‘Alayhi Salaam) alipomuomba Mola wake alisema: “…sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.” (19:4)

Hapo kabla alinikirimu kwa kuitikia dua yangu na kunifanya ni mwenye furaha kwa kunijibu.

Jambo hili halimuhusu Zakaria (‘Alayhi Salaam) pekee bali Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ametujulisha aliposema Subhaaanahu: “Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.” (2:186).

Madamu kuna kamba inayomuunganisha mja na Mola wake moja kwa moja, basi furaha ataipata na kufanikiwa, na mashaka na tabu atapata pindi akikata kamba hii, na kwa kadiri mwanadamu atakapokuwa na mapungufu katika kuihukumu nafsi yake kwa dini hii ndio kadiri inapoangukia tatizo na wasiwasi katika nafsi na maisha yake. Kwa hili ndio maana Allah anaambatanisha baina ya Uongofu na rehema, upotofu na tabu, ya kwanza ni kauli yake: “Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa. ” (2:5).

Na kauli yake : “Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.” (2:157)

Na kauli yake: “….Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.” (20:123),

Na uongofu: kumkataza na upotofu, na Rahma: kumkataza au kumuepusha mashaka na tabu, na hili ndilo alilolitaja Allah mwanzoni mwa Surat Twaha katika kauli yake Allah: “T’AHA! Hatukukuteremshia Qur’ani ili upate mashaka.” (20:1-2).

Hivyo akakusanya kati ya kumteremshia Qur-aan na kuondosha mashaka kwake, kama alivyosema mwisho wa sura kuhusu wafuasi wake: “…hatapotea wala hatataabika.” (20:123),

Hivyo basi uongofu na ubora na neema na rehema ni yenye kulandana hazitengani, kama ambayo upotofu, mashaka ni yenye kulandana na hayatengani, Allah amesema: “Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu.” (54:47),

$Bernard_Shaw.jpg*

Sir George Bernard Shaw

Mwandishi wa Kiingereza.
Mwokozi wa Binadamu
“Kwa hakika ni katika Uadilifu Muhammad kuitwa, “Mwokozi wa Wanadamu”. Naamini kuwa mtu mfano wake lau angetawala ulimwengu huu leo hii angefanikiwa kutatua matatizo yake na hivyo furaha na amani ingechukua nafasi yake.”

Na su’ur ni wingi wa sa’iyr; nayo ni adhabu ambayo ni kilele cha tabu na mashaka na kwa mkabala wake ni mwisho mbaya wa waovu Allah amesema kuhusu marejea ya wacha-Mungu katika sura hiyo hiyo: “Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito. Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.” (54:54-55)

Hii ndio njia ya furaha ikiwa utataka kuifuata na kujipamba nayo, ni njia ambayo haisimami kwa upotofu na uzushi katika dini, kiroho au fikra tupu, ni njia ya Furaha, nayo ni njia vile vile ya elimu na ustaarabu.