Jack Rislow

quotes:
  • Qur-aan na Hadithi bega kwa bega
  • “Qur-aan ina kamilishwa na hadithi ambazo ni mtiririko wa maneno yanayofungamana matendo ya Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘Alayhi Wasallam) na maelekezo yake. Katika hadithi mtu anapata yale yote yaliyokuwa yakitokea kwa Mtume (Swala Llahu ‘Alayhi Wasallam). Ni kipengele cha msingi katika tabia zake mbele ya hakika zenye kubadilika katika maisha. Hivyo basi Sunnah ndio yenye kubainisha Qur-aan wala haijitoshi peke yake.”


  • Kukusanywa kwa Sunnah za Mtume
  • “Hadithi hizi ambazo mkusanyiko wake unatengeneza Sunnah zimeandikwa kutokana na yaliopokewa kutoka kwa Masahaba au kunakiliwa kutoka kwao kwa umakini mkubwa katika kuzichagua kwake; na kwa namna hii kiasi kikubwa cha Hadithi kilikusanywa.”


  • Kanuni za Pambanuzi Muhimu
  • “Qur-aan ina suluhisho la kadhia zote na kuunganisha kati ya sheria za kidini na zile za kimaadili. Huweka na kutengeneza mfumo mmoja wa kijamii na kupunguza kukata tamaa, nyoyo ngumu na uzushi. Kwa hakika unashughulikia kwenye kuunga mkono wanyonge, na kuamrisha watu kuhurumiana. Ama katika uwekaji wa sheria imeweka kanuni katika pambanuzi muhimu ili kusaidiana kila siku na ikaratibu mikataba na mirathi na miamala, ama katika uwanja wa familia umemuwekea kila mtu mfumo wa kuamiliana na watoto na watumwa, wanyama, afya na mavazi…..n.k.