Jeffrey Lang

quotes:
  • Ananijua Kuliko Ninavyoijua Nafsi Yangu
  • “Qur-aan, kitabu hiki kitukufu kimeniteka kwa nguvu na kumiliki moyo wangu na kunifanya nijisalimishe kwa Allah, na Qur-aan humsukuma msomaji wake kwenye upeo wa mbali ambapo humtanguliza (kujiona) anasimama peke yake mbele ya Muumba wake. Ukiichukulia Qur-aan kwa umakini zaidi basi huwezi kusoma kwa urahisi, kwani hukubeba kama kwamba ina haki juu yako! Nayo inajadiliana nawe, kukukosoa na kushindana nawe. Nilikuwa katika kipande cha mwisho ikadhihirika wazi kuwa aliyeshusha Qur-aan ananijua kuliko ninavyojijua mwenyewe. Kwa hakika Qur-aan siku zote inanitangulia katika kufikiri kwangu, ilikuwa inajibu maswali yangu na kila usiku nilikuwa ninaweka maswali yangu na pingamizi zangu, hata hivyo nilikuwa napata majibu siku inayofuatia. Nimekabiliana na nafsi yangu uso kwa uso katika kurasa za Qur-aan.”


  • Kuijaza Roho Tupu
  • “Katika kipindi fulani cha maisha yangu, Mwenyezi Mungu amenipa elimu kubwa na rehema nyingi baada ya adhabu na maumivu yaliyonipata baada ya kuwepo na matayarisho makubwa kwangu na kujaza roho tupu ndani ya nafsi yangu. Hivyo nikasilimu, na kabla ya kuwa Muislamu sikuwa ninajua ndani ya maisha yangu maana ya mapenzi lakini mimi baada ya kusoma Qur-aan nilihisi rehema nyingi pana na mapenzi yakinifunika. Nikaanza kuhisi mapenzi yaliyodumu ndani ya moyo wangu. Kilichoniongoza kwenye Uislamu ni mapenzi ya Mungu ambayo hayazuiwi.”