H. G. Wells

quotes:
  • Mafunzo kutoka katika Hijja ya kuaga.
  • “Muhammad alihiji Hija ya kuaga kutoka Madina kwenda Makkah kabla ya kifo chake kwa mwaka mmoja. Wakati huo alitoa mawaidha makubwa kwa watu wake. Sentensi ya kwanza tu aliondosha mbele yake yote waliyokuwa nayo Waislamu kama vile unyang’anyi, uizi, kulipiza kisasi, na umwagaji wa damu, na paragrafu ya mwisho alisisitiza usawa kati ya muumini wa Kihebeshi na Khalifa wa Waislamu. Kwa hakika aliweka msingi mkubwa Ulimwenguni kwa ajili ya kuamiliana kwa uadilifu na ukarimu.”


  • Mwanga wa Uislamu
  • “Ni vizazi vingapi ambavyo vitapambana na hofu na tabu, kabla kuibuka tena kwa mwanga mpya wa Uislamu mtukufu ambao inadhihirika kuwa Historia nzima inaelekea upande wake. Wakati huo amani itafunika dunia na nyoyo za watu.”


  • Mfumo Bora
  • “Uislamu ulifanikiwa: Kwa sababu ulikuwa ni mfumo bora wa Kijamii na kisiasa ambao siku ziliweza kuutanguliza (mbele). Nao ulisambaa. Kwa sababu kila ulipokwenda ulikumbana na mataifa yaliyokuwa nyuma kisiasa. Mataifa ambayo yalikuwa yakinyang’anya raia zake, yakidhulumu na yakiwahofisha wala hayakusoma wala kuwa na utaratibu wowote, vile vile ulikuta serikali hizo zina ubinafsi na ugonjwa hazina uhusiano baina yake na watu wake. Hivyo Uislamu ukabaki ndio fikra safi zaidi ya kisiasa na utendaji mzuri ulimwenguni hadi muda ule ulikuwa ukiwatumikia watu kwa mfumo bora kuliko nidhamu yoyote nyingine. Ama mfumo wa Kibepari ulikuwa ukiwafanya watu kuwa ni watumwa katika ufalme wa Roma. Elimu, fasihi na taratibu na ada na kijamii huko Ulaya zilikwisha anguka kabla ya Uislamu kuibuka.”