Tarekh ya mitume:Nuuh

Tarekh ya mitume:Nuuh

Tarekh ya mitume:Nuuh

Kaumu ya Nuhu

Watu wake hapo kabla walikuwa ni waumini, wakimuabudu Allah peke yake, wakiamini Siku ya Mwisho, na wakifanya mambo mema, watu wale akafa, watu wakahuzunika kwa wema wao na tabia zao njema wakatengeneza picha zao (Wakawapa majina yafuatayo: Wadda, Yaaghutha,Yaa’uqa, Nasra, watu wakavutika na picha zile na…) wakafanya ndio alama za wale watu wema waliokufa miongoni mwao, watu wa mjini wakatukuza picha zile, wakikusudia kuwatukuza wafu wale muda ukapita wale watu wazima wakafa na kubaki watoto na kuwa wakubwa, wakawa wanaongezea namna mbali mbali za kutukuza, na kunyenyekea mbele zao, picha na sura zile zikawa na nafasi kubwa katika mioyo ya watu wale, ama kizazi cha pili kilichofuatia wakawa wamejiwekea sheria ya kuabudu sura zile na kusema kuwa ile ni miungu inabidi wayasujudie na kunyenyekea mbele yake; wakawa wanayaabudu, wengi wakapotea kwa kufanya hivyo.

Baada ya hapo Allah akawatumia watu wale Mtume Nuhu (‘Alahyi Salaam); ili awaelekeze njia (iliyonyooka), na kuwakataza kuabudu masanamu, na kuwaelekeza kumuabudu Allah Ta’ala, Nuhu (‘Alahyi Salaam) akaenda kwa kaumu yake… “…Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu asiye kuwa Yeye…” (23:23)

Wakamkadhibisha, na hawakumkubali, akawaonya na kuwatahadharisha adhabu ya Allah Ta’ala. Akasema: “Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa.” (26:135),

Wakasema: “Wale watukufu katika kaumu yake wakasema: Hakika sisi tunakuona wewe umo katika upotofu ulio dhaahiri.” (7:60),

Nuhu akawajibu: “Akasema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika upotofu, lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. Nakufikishieni Ujumbe wa Mola Mlezi wangu, na ninakunasihini; na ninayajua kwa Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi.” (7:61-62)

Watu wakashangazwa na maneno ya Nuhu, wakawa wanasema. Wewe ni mtu kama sisi, utakuwaje Mtume kutoka kwa Allah? Na ambao wamekufuata ni kundi la watu dhaifu na watu wa chini, kisha hamna ubora kutushinda sisi, si katika mali wala katika vyeo, na sisi tunadhania kuwa mnadanganya katika madai yenu haya, baadhi ya kaumu wakawaambia wengine: “…Huyu si chochote ila ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu amependa basi yakini angeli teremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa zamani. Huyu si lolote ila ni mtu mwenye wazimu…” (23:24-25)

Baadhi yao wakahamasisha wengine kuabudu masanamu yao: “Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa’ wala Yaghutha, wala Yau’qa, wala Nasra. ” (71:23).

Nuhu (‘Alayhi salaam) akawaambia: “Je, mnastaajabu kukujieni mawaidha yanayotoka kwa Mola Mlezi wenu kwa njia ya mtu aliye ni mmoja katika nyinyi, ili akuonyeni…” (7:63)

Na baada ya hapo Nuhu akawachukulia kwa upole na ulaini, lakini watu waliendelea na inadi yao, na akawalingania wakati wote mpaka akasema: “Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana, Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia. Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno! ” (71:5-7)

Akawalingania katika kila njia iliyowezekana: “Tena niliwaita kwa uwazi, Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri.” (71: 9-10),

Wengine wakajiundia nyudhuru duni kwa kusema: “Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini?” (26:111)

$Wolf_Baron_Nazir.jpg*

Pro. Rolf Baron

Profesa wa Vyuo Vikuu vya Austria
Ujumbe wa Mwisho.
“Muhammad ni Mtume aliyeleta Uislamu; na hivyo kuwa kipengele cha mwisho katika mnyororo wa Mitume ambao wamebeba ujumbe mkubwa.”

Nuhu akawajibu kwa upole na ulaini na kuwakumbusha: “Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?” (26:112)

Kisha akawaambia: “Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!” (26:113)

Kisha Nuhu akasema tena: “Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini.” (26:114),

Na, “na mimi sitawafukuza walio amini” (11:29).

Vipi nitawafukuza watu ambao wameniamini, wamenihami na wamenisaidia kutangaza da’wah?! Kisha akawaambia: “Na enyi watu wangu! Ni nani atakaye nisaidia kwa Mwenyezi Mungu nikiwafukuza hawa? Basi je, hamfikiri?” (11:30), “Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri.” (26:115).

Ninawaonya watu sawa kwa sawa, bila kutofautisha kati ya mtukufu na mnyonge, tajiri na fukara, mkubwa na mdogo na mweupe na mweusi…, watu walipokatikiwa na hoja na kushindwa kujibu dalili za Nuhu, wakawa wanamtisha kumpiga mawe: “Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe.” (26:116).

Safina ya Nuhu

Nuhu alipokuwa na yakini kuwa hawakubali maelezo yoyote (mantiki), wala hawaongoki, alinyenyekea kwa Allah amuokoe dhidi ya watu wale wenye inadi, “Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha.” (26:117)

“Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini.” (26:118)

Pamoja na kuwa Nuhu alikuwa akihofisha kaumu yake na adhabu ya Allah, pindi watakapong’ang’ania ukafiri, baadhi yao walimjibu kwa kejeli: “…Basi tuletee hayo unayo tuahidi, ukiwa miongoni mwa wasemao kweli.” (11:32),

Nuhu akawajibu: “Jambo hili halipo katika mikono yangu”: “Akasema: Mwenyezi Mungu atakuleteeni akipenda…” (11:33), “Wala nasaha yangu haikufaini kitu nikitaka kukunasihini…” (11:34).

Allah akamteremshia Wahyi: “…Hataamini yeyote katika watu wako ila wale walio kwisha amini. Basi usisikitike kwa waliyo kuwa wakiyatenda.” (11:36),

Hoja ikakamilika, udhuru ukakatika, na da’wah ikaendelea takriban karne kumi, Nuhu alikata tamaa, akamuomba Mola wake, kwa kusema: “Na Nuh’u akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri! Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.” (71:26-27).

%%

Kiburi na uharibifu wa Historia.
“Katika karne ya kati Wakristo katika maandishi yao walianza kugawa watu kwa misingi ya kikabila na kitaifa kama ilivyotajwa katika agano la kale (Mwanzo) na kuongeza ugawaji wa tabaka jipya: Ikawa ni itikadi iliyoenea kuwa watu wa dini na makasisi wanatokana na kizazi cha Shemu. Wapiganaji wanatokana na kizazi cha Yafith. Mafukara wanatokana na kizazi cha Hamu watoto wa Nuhu (‘Alayhi Salaam). Ilifikia kuwa katika mwaka 1964 kumpeleka Senata wa Marekani Robert Byrd kutoka mji wa Virginia ya Magharibi kutumia kisa cha Nuhu kama sababu ya kubaki sera ya ubaguzi katika Marekani.

Allah akamteremshia Wahyi wa kutengeneza Meli (Safina): “Tukampa wahyi: Unda jahazi mbele ya macho yetu na uwongozi wetu!...” (23:27)

Akaanza kutengeneza: “Na akawa anaunda jahazi, na kila wakipita wakuu wa kaumu yake wakimkejeli….” (11:38)

Nuhu akawa anawajibu kwa adabu na upole: “…Yeye akasema: Ikiwa nyinyi mnatukejeli na sisi tunakukejelini kama mnavyo tukejeli.” (11:38)

Kisha akiwaonya kwa adhabu ya Allah: “Nanyi mtakuja jua ni nani itakaye mfikia adhabu ya kumhizi, na itakaye mteremkia adhabu ya kudumu.” (11:39)

Na akafanya kazi kwa bidii, hadi alikamilisha kutengeneza Safina.

Kisha Allah akamuamrisha Nuhu kubeba katika safina ile wale walioamini pamoja nae, na kila chenye roho jozi mbili: “Hata ilipo kuja amri yetu, na tanuri ikafoka maji, tulisema: Pakia humo wawili wawili, dume na jike, kutoka kila aina, na ahali zako, isipo kuwa wale ambao imekwisha wapitia hukumu; na watu walio amini. Na hawakuamini pamoja naye ila wachache tu.” (11:40)

Akawabeba wote walioamini pamoja nae jozi mbili mbili, “Na akasema: Pandeni humo kwa Bismillahi, Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.” (11:41).

Kuangamia kwa kuzama

Nuhu alipopanda na walioamini kwenye Safina pamoja nae, na akachukuwa wanyama, kila mmoja katika mahali pake, mbingu ikaanza kunyesha mvua kubwa, chemchem za ardhi zikaanza kububuja maji mengi: “Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika. Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa. Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba .Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa.” (54:11-14)

Nuhu akamuona mwanae ambae hakuamini pamoja nae akiwa anataka kukimbia ili asizame akamuita: “…Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi, wala usiwe pamoja na makafiri” (11:42)

Lakini mtoto alikataa imani, na akakataa nasaha za baba yake, alimjibu Nuhu kwa kusema: “Akasema: Nitakimbilia mlimani unilinde na maji….” (11:43)

Nuhu akamuonea huruma mtoto wake huku akisema: “(Nuhu) akasema: Leo hapana wa kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu ila aliye mrehemu mwenyewe...” (11:43),

Hapo hapo: “…Na wimbi likawatenganisha, akawa katika walio zama” (11:43)

Nuhu akamsikitikia mwanae, na kunyenyekea kwa Allah amuokoe mwanae. Allah alimuahidi kuwaokoa watu wake, Nuhu (‘Alayhi salaam) akasema: “…Ee Mola Mlezi wangu! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ni haki. Na Wewe ni Mwenye haki kuliko mahakimu wote.” (11:45).

Allah ambae alimuahidi kuwaokoa watu wake (familia yake) waliokuwa wema, alisema: “Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Mwendo wake si mwema….” (11:46),

Katika dini hakuna kuwepo mtu wa kati, huyo si katika watu wako, haitamnufaisha kuwa ni mwanao madamu hakumuamini Allah wala kumpwekesha.

Baada ya maji kufurika kila sehemu, na kila kafiri kuangamia: “Na ikasemwa: Ewe ardhi! Meza maji yako…” (11:44)

%%

Mitume kudharauliwa.
Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema, Na alaaniwe Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisakwa ndugu zake.” (Mwanzo: 9:20-25) na hivyo akawabariki Shemu na Yafethi. Katika tafsiri ya andiko hili Talmud Baabli imetaja. Kitabu Sanhadrin uk. 70 kuwa Kanaani au Hamu aligombana na Nuhu na kumfanyia maovu!! Kamwe haiwezekani kwa Nabii Mtukufu kufanya hivyo.

Na maji yalioyotoka chini ya ardhi kusita. Allah aliteremshaWahyi, “…Na Ewe mbingu! Jizuie...” (11:44)

na simama kunyesha mvua; mvua ikasimama: “…Basi maji yakadidimia chini…” (11:44)

Hilo ni jabali ambalo safina ilitia nanga juu yake, na Wahyi ukateremka kwa Nuhu (‘Alayhi salaam): “…Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya watu walio pamoja nawe…” (11:48)

Nuhu akateremka kutoka katika Safina, na wakataremka waumini waliokuwa pamoja nae, wakajenga mji, na kupanda miti na wakawaacha wanyama waliokuwa nao, na ardhi ikaanza kuimarishwa na watu kuzaana na kuenea.