JE, WATU WANA HAJA NA MITUME?

JE, WATU WANA HAJA NA MITUME?

JE, WATU WANA HAJA NA MITUME?

Uchovu wa akili

Mwenyezi Mungu ameumba viumbe wake katika umbile (fitra) sahihi, na akawawekea akili ili waweze kupambanua baina ya haki kwenye batili, na kwa sababu akili za wanadamu zina mapungufu na udhaifu, matamanio na maslahi, bali na migongano ndani yake.

Katika hali hiyo wanachokiona baadhi ya watu kuwa ni kizuri na wema wengine wanaweza kukiona kuwa kibovu, bali hata mtu mmoja anaweza kubadilika rai yake kwa kubadilika kwa zama na mahali, pamoja na kuwa akili hizo haziwezi kudiriki kilichojificha katika hali halisi katika elimu mbali mbali, kadhalika hawezi kudiriki muradi wa Muumba, maamrisho yake na makatazo yake, mbali na kuwa mwanadamu hawezi kupokea kutoka kwa Allah moja kwa moja, Allah amesema: “Na haikuwa kwa mwanaadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo), au kwa nyuma ya pazia, au kumtuma Mjumbe. Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hikima. ” (42:51)

Hivyo basi Allah akachagua viumbe vyake bora zaidi miongoni mwa Mitume na Manabii ili wawe mabalozi wazuri baina yake Yeye Allah na waja wake, Allah amesema: “Mwenyezi Mungu huteuwa Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (22:75),

Ili wawaongoze watu katika kumuabudu Yeye, na wawaondoshe kwenye dhuluma za kiza na kuwapeleka katika uongofu wa Nuru, ili watu wasiwe na hoja kwa Allah baada ya kupelekewa Mitume –Allah amesema: “Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. ” (4:165).

Neema tukufu

$Washington Irving.jpg*

Washington Irving

Mwanadiplomasia na mwanafasihi wa Kimarekani
Kuwa mtu Usio na Makuu
“Hata katika kilele cha utukufu wake Muhammad alidumu katika hali yake, alikuwa akichukia anapoingia sehemu yenye kundi la watu wakamsimamia au kupitiliza katika kumkaribisha.”

Hivyo basi suala la kutuma Mitume kwa watu likawa ni jambo kubwa la neema kwa watu kutoka kwa Allah; ili awafundishe kinachowafaa na kinachowatakasa, Allah amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwa Waumini vile alivyo waletea Mtume aliye miongoni mwao wenyewe, anaye wasomea Aya zake, na anawatakasa, na anawafunza Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya hapo walikuwa katika upotovu ulio wazi. ” (3:164).

Kwa hakika neema kubwa kutoka kwa Allah ni kuwatumia watu Mitume, na Mtume huyo kuwa “miongoni mwao”,

neema hii inaonekena dhahiri na wazi kuwa Mtume huyu ametumwa na Allah akizungumza na watu kwa maneno matukufu ya Allah Ta’ala, akizungumza na watu kuhusu dhati ya Allah na sifa zake na kuwaeleza ukweli wa Uungu na sifa zake, mbali mbali, kisha akawalingania katika yale yatakayofanya maisha yao yawe mazuri, na awaongoze katika kitakachofaa mioyo yao na hali zao mbali mbali, na kuwalingania na kuwaita katika Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, huu ni ukarimu mkubwa wa neema hii, fadhila hii na utoaji huu? Bali huwatoharisha na huwanyanyua na huwasafisha, husafisha mioyo yao na fikra zao na hisia zao, na husafisha nyumba zao, heshima zao na Swala zao, na hutoharisha maisha yao, jamii zao, na mifumo yao, na huwasafisha wao na uchafu wa ushirikina, upagani na upotofu na masimulizi potofu, na yale ambayo yanapatikana katika maisha haya katika minasaba mbali mbali na desturi mbovu zisizofaa kwa mwanadamu na maana ya utu wake.

Vivyo hivyo kuwasafisha na uchafu wa maisha ya kijaahiliya, na uchafu ulioenea katika hisia za watu, katika itikadi zao na ufahamu wao wa mambo mbali mbali.

David Parton

Mwandishi wa Kimarekani
Wanadamu ni Wanyama wanapokataa Dini
Katika takwimu katika moja ya vyuo vikuu nchini Marekani ambavyo yaliandikwa katika kitabu (Amerika ina swali au haiswali) ya David Parton kuwa: -Asilimia themanini 80% ya wanawake Marekani hubakwa mara moja katika maisha yao!! -Idadi ya wanawake wenye kubakwa kila siku ni zaidi ya wasichana 19000. Matokeo ya hilo ni kuwa kiasi cha asilimia thelathini 30% ya wasichana huko Marekani ima hupata mimba au hutoa mimba au kujifungua katika umri wa miaka kumi na nne. -Asilimia sitini na moja (61%) za ya hali ya kubakwa ilikuwa kwa wasichana chini ya miaka kumi na nane. -Asilimia 29% ya ubakaji ilikuwa kwa watoto chini ya miaka kumi na moja

Ujahilia ni Ujahilia, na kila ujahilia una uchafu wake, haijalishi huo ujahilia uko wapi kulingana na zama na mahali, pale ambapo nyoyo za watu zikaepuka na akida ya kiungu inayohukumu muono wao katika sharia ambayo inatokana na akida hii-ambayo ndio itakayohukumu maisha yao basi bila shaka kitakachokuwepo hapa kitakuwa ni Ujahilia katika sura zake mbali mbali, na hapana budi kumuokoa mwanadamu na Ujahilia huu iwe ujahilia huu ni wa zama hizi au wa zama za kale, Ujahiia ndio huo huo, Ujahilia uwe ni ule wa zamani au wa leo hii-sifa zote za Jaahiliya zitapatikana kwenye sifa zile za Ujahilia wa zamani katika upande wa tabia (Akhlaq) na wa kijamii, na utaweka malengo ya maisha ya mwanadamu na hali kadhalika upeo wake (mwisho wake)! Pamoja na kuwa ufunguzi wa elimu za maendeleo na makubwa ya kielimu na viwanda na teknolojia: “…ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.” (62:2)

Upotevu katika mtazamo na itikadi, na upotevu katika malengo ya maisha ni upotevu katika desturi na mifumo, na (tabia), ni upotofu katika nidhamu (mfumo) ni upotevu katika jamii na tabia.