MATAMANIO NA MISIMAMO

MATAMANIO NA MISIMAMO

MATAMANIO NA MISIMAMO

(1)

Joji aliamka saa mbili unusu asubuhi, mwili wake ulikuwa ni mzito na uchovu, usiku ule homa ilipanda na hakuweza kulala na ikabidi aombe kishusha joto hapo hotelini. Alijivuta na kusimama, kisha akaoga na kujisikia aina fulani ya uchangamfu. Alishuka chini kwenye mgahawa hapo hotelini na kupata kifungua kinywa kisha alipata na kishusha joto kwa mara nyingine na hapo akahisi hali yake kuwa nzuri zaidi na uchangamfu kuongezeka.
Alipanda chumbani kwake mara nyingine ilipotimu saa tatu na dakika kumi hivi, alipofika tu simu ikawa inaita, alikuwa ni Levi kwa sauti yake nzuri.

Uko wapi? nimekuhofia, nimekupigia mara nyingi lakini hupokei…

Samahani, niliteremka kupata kifungua kinywa na nimesahau simu yangu chumbani.

Sio tabia yako kuchelewa katika ahadi.

Sikuweza kulala vizuri jana usiku, huenda nimepatwa na maradhi.

Mungu akuponye, je ungependa nikupeleke kwa daktari?

Hapana, asante, na samahani kwa kuchelewa. Najiona afadhali kwa sasa.

Joji aliteremka mapokezi na kumuona levi akiwa amevaa mavazi mazuri yenye heshima, lakini haufichi uzuri wake – akapeana nae mkono na kumkaribisha…Levi akamwambia kwa shauku:

Nasisitiza ukamwone daktari, haifai kunyamazia hali hii.

Asante Levi, hali yangu ni nzuri hivi sasa na kama tukienda kutembelea sehemu takatifu nitashukuru kwa hilo.

Kama utakavyo, la msingi ni kuwa katika hali ya furaha na starehe… leo tutatembelea sehemu mbili au tatu hivi, unaonaje?

Napendekeza tuanze na kilicho muhimu zaidi, hata tukiweza kumaliza ziara za sehemu mbili itakuwa inatosha. Kilicho muhimu zaidi ni kukaa na wewe na kuzungumza na sio ziara pekee.

Hata mimi kilicho muhimu ni hilo vile vile, tutaanza mwanzo katika ukuta wa kilio ‘Wailing wall’ na Mlima Yuria, kisha baada ya hapo tutatembelea kaburi la mfalme Daud katika Mlima Zayoni, na tukipata wasaa zaidi tutatembelea makaburi ya zamani ya Mlima Zaituni.

Sawa kabisa, nataraji ziara yetu iishe kabla sijaanza kujihisi vibaya na uchovu mwingi.

Vipi ilikuaje pamoja na Habib?

Uchaguzi mzuri kabisa kutoka kwako, inaelekea kuwa unanifahamu vizuri.

Macho yakakodoka na kung’ara na meno kuonekana na kutabasamu…

Mh mh… kiasi fulani, Habib amefunguka katika mambo mengi na ni msomi na anajua anachokifanya.

Umesema kweli, nimefaidika nae sana.

Naye anakusema hivyo hivyo.

Joji kwa mshangao:

Vipi na lini?

Alinipigia jana mara tu alipokuwacha hotelini, na akaniambia kuwa amejifunza mengi kutoka kwako…amekusifia sana na sikuwahi kumsikia kama alivyokusifu kwa mtu mwingine.

Huu ni katika ukarimu wake, ila muda wote tulikuwa kwenye mjadala wa nipe nikupe.

Ikiwa mfano wa mazungumzo yako pamoja nami, ni mazungumzo matamu yaliyoje!

Joji alijihisi akiwa na furaha akiwa anasikiliza maneno yake matamu kwa sauti yake nyororo…..na mwili wake wenye fitna na kwa roho yake iliyokuwa nzuri.

Ha ha ha, mnatofautiana kidogo, wewe ni mwema sana, mzuri, nae hayupo hivyo, hata hivyo nakushukuru kwa kunichagulia. Vile vile nakushukuru kwa kujali kwako na kutaabika nami, cha muhimu ni kuwa malengo ya safari yetu ya msingi yakamilike, nayo ni kuingia mkataba na kusaini na kutambua njia inayopelekea katika furaha.

Nakushukuru sana, bado unakumbuka mkataba? Mimi nilishasahau kabisa, kwa mnasaba huo kikao chako na Benjamin kimemchanganya.

Kwa vipi?

Sijui, lakini baada tu ya kuondoka aliniita na kuniambia: “Huyu ni katika watu wa ajabu ambao nimekutana nao katika maisha yangu.” Nikamuuliza kwa nini? Akaniambia: “Ima huyu ni mwendawazimu au ni mtawa”.

Ha ha ha, sina uchaguzi mwingine wa tatu! Sitaki kuwa mwenda wazimu, la kusikitisha siwezi kuwa mtawa na mimi ninampa rushwa.

Sijui kwa nini ameathirika na nilichomwambia, kila mara akikariri kuniambia kuwa sisi tunakosea tunadhani kuwa dunia ni mali tu, na hili lilikuwa jambo la kwanza katika maisha yangu kusikia haya kutoka kwa Benjamin.

Kwa kweli….pamoja na kutokuwa na raha nae, maneno yake hata mimi yameniathiri vile vile, Je, ni kweli starehe ya mwili ni adhabu ya roho? Je, hakuna njia ambayo nitakutana na raha, matamanio na kuondoka kwa maumivu?

Ni kiasi gani natamani kuipata njia hii.

Hivyo wewe ni kama alivyonieleza Habib unatafuta njia ya furaha?

Neno zuri sana (ulilolisema), lakini ni ipi njia ya kuelekea kwenye furaha kwa muono wako?

Ni ile njia ambayo ulikuwa ukiitafuta kabla ya muda kidogo na unatamani kuipata, nami ndio hiyo hiyo ninayoitafuta tokea muda mrefu.

Nami nina muda mrefu ninaitafuta vilevile … kisha nikatabasamu na kumuangalia machoni mwake, na akasema, ukaribu ulioje wa roho zetu?!

Habib aliniambia hivyo, kwa nini usiwe Mkatoliki?

Fikra niliyokuwa nayo ni kuukimbia Uyahudi na mazonge yake na upotofu wake, lakini lengo sio kutoka kwenye mafundisho ya Uyahudi na kuingia katika mafundisho mengine na kutoka kwenye upotofu huu kwenda kwenye upotofu mwingine, vinginevyo ni bora kubakia kwanye Uyahudi, dini ya zamani na yenye utukufu zaidi.

Kuwa mkweli kama ulivyonizoesha, je hii ndio sababu pekee? Au kuna sababu nyinginezo?!

Ukweli…... Kubadilisha dini sio jambo rahisi unadhani ni miamala gani anayofanya aliyebadilisha dini pamoja na wale wanaomzunguka, mfano mimi na Banjamin? Je, unadhani nitabaki na kazi yangu (baada ya kubadilishwa dini) walau siku moja?

Hivyo wewe unamuogopa yeye?

Nilikuambia bado sijakinaika, kwa ukweli nahofia kubadilisha dini yangu… uhuru una makato yake ya gharama….gharama za juu!

Lakini hatuna budi kulipa gharama hizo; Pili tupate uhuru wetu, hakuna kitu mfano wa uhuru wetu.

Bado naendelea kutafuta maamuzi sahihi, au njia ya furaha, na nitakapokinaishwa na hilo huenda nikachukuwa maamuzi kwa ujasiri, na huenda nikawa muongo kwa hilo, sijui itakuwaje…..sijui!

Je, unamuogopa Benjamin?

Bila shaka! Je unadhani maamuzi sahihi ya kijasiri, au kwa lugha nyingine kwa mazungumzo yako njia ya furaha ndiyo ambayo itakufikisha kwenye Ukristo?

Una uwezo usio wa kawaida kugeuza meza katika mazungumzo yako, sijui kwa nini?

Je, sijakuambia kuwa roho zetu zinaruka pamoja, leo huenda zikaungana pamoja.

Ehe umeshaanza kuwa mwanafalsafa! ewe mwanamke mzuri vipi roho zikutane?

Ha ha ha, sijui, ila ninavyofahamu ni kuwa kama inavyoungana miili basi na roho zinaungana vilevile, na ya kuwa roho yangu inaruka na yako.

Ni bora roho ziruke kwa furaha kuliko kuruka kwa shaka.

Swadakta, hata hivyo tuachane na hili….zimebaki dakika kadhaa kufika katika ukuta wa kilio (Wailing Wall), au kama wanavyouita Waislamu Ukuta wa AlBuraq nayo ni athari ya mwisho iliyobakia ya hekalu ya Mfalme Solomon kwa muono wa viongozi wa dini wa kiyahudi (Rabbi). Wayahudi walikatazwa kuingia katika msikiti wa Qudsi tokea hekalu lilipoharibika; hivyo basi ukuta ni sehemu ya karibu zaidi katika sehemu ya hekalu ambayo Wayahudi wanaweza kuswali ndani yake kulingana na Sheria za Kiyahudi za kisasa. Jina la ukuta unaolia limeitwa kwa kunasibishwa na ibada za kuomboleza ambazo zinafanywa hapo

Tokea lini (mambo haya)?.

Kabla ya karne ya kumi na sita Mayahudi walikuwa wakiswali na kutekeleza na ibada zao za misiba katika hekalu la Solomon katika sehemu tofauti panapozunguka sehemu tukufu ya Yerusalemu, kisha baada ya hapo wakawa wanakusanyika kila mwaka mbele ya jiwe karibu na ukuta fulani katika eneo tukufu Yerusalemu ndilo baadae likaitwa ukuta wa kilio (Wailing Wall) au kama wanavyouita Waislamu ukuta wa Buraq.

Ni nini ukuta wa Buraq?

Ni mtukufu vile vile kwa Waislamu, wanasema kuwa Mtume wao alipandishwa mbinguni kutokea pale, safari ya Mtume wao huyo ilianzia Makkah kwa njia ya nyumbu aitwae Buraq ambae safari hiyo iliishia hapo na kutoka hapo kwenda juu.

Je, mnawaachia Waabudie hapo?

Tumewaachia sehemu zote tukufu za Yerusalem na bado wanashindana nasi katika ukuta wetu! Kisha Waislamu hawana toba ya kuabudu athari wala hawapendi masanamu na hawaabudu vitu vyenye kuabudiwa.

Habib alikuwa ananikejeli na kuniambia kuwa sisi Protestant ni kama vile Waislamu hatupendi sanamu na picha.

Hili ndilo lililobakia katika hekalu zetu za kuabudia zilizo vunjwa, na tutatoka kuieleza dunia na kuonesha athari zenye kuthibitisha hilo.

Miaka yote hii hamjapata athari yoyote ile na bado mnataraji kupata?

Hahaha, hata kama hatukupata basi tutatengeneza!

Kama ni hivyo inaonesha hujakinaishwa bado?

Sijaridhishwa au bado, hiyo ni hali ya shaka, baadhi za tafiti zinaonesha kuwa, kwa mara ya kwanza watu waliswali kwenye ukuta ilikuwa ni wakati wa dola ya Ottoman, na sio kama nilivyokuambia kuwa ilikuwa kabla ya karne ya kumi na sita. Ama Waislamu wanasema kuwa huu ni uongo ulio wazi, kilicho muhimu ni kuwa hii ni sehemu tukufu kwetu, kisha alimgeukia Joji na akasema:Ni vigumu kuifurahisha roho yako na kuizoesha katika hilo. Je, ungependa tuishi bila ya kufanya ibada?

Leo unaonekana tofauti kabisa na jana.

Leo ni siku ya ibada na sisi tunaelekea katika ukuta wa kilio, na yatupasa tuteremke sasa hivi na tukamilishe safari yetu kwa kutembea.

Natamani tusitembee sana kwenye jua hili, athari za uchovu zimeanza kujitokeza kwangu.

Nataraji haitokutokea kwani wewe sio Myahudi.

Kwa vipi?

Vaa kofia hii.

Hamna sio neno, hahaha, usinichore ninapovaa kwani Katarina atakasirika.

Unaelekea unampenda sana Katarina!

Ndio, kwa sababu ni mwanamke mwenye dini, msomi na moyo wake mweupe kama wako.

Natamani kumpata mtu kama alivyo anayejali dini, usomi na fikra… tutapinda hapo kulia, kisha kulia tena na tutakutana na ukuta na tutawaona watu wakiwa wanalia.

Nimevaa kofia ya Kiyahudi lakini sijui kuigiza kulia kama wao.

Hilo sio muhimu, wengi mfano wake hawawezi kuigiza, utawaona wengine wengi wakilia au wanajua kuigiza kulia….wewe unaweza kuendelea; wanawake hawaruhusiwi kuingia.

Kwa vipi? siwezi kuingia kama hutoingia.

Ingia, mimi na kusubiri, unataka niingie kisha nifukuzwe kama mbwa, tafadhali ingia peke yako.

Joji alitembea safari iliyobakia peke yake, na akaanza kuhisi uchovu wa hali ya juu, hadi alipofika kwenye ukuta…. Idadi ya Mayahudi wengi waliokuwa wakilia ilikuwa ni kubwa na kuna wengine wengi ambao hawajui kulia vizuri (huenda hawakujifunza jinsi ya kulia vizuri)…. Alisimama pembeni yao akiwaangalia, hata hivyo alijihisi akiwa na dhiki, na akataka kuondoka haraka; na haswa zaidi kwa sababu uchovu uliongezeka, na joto lake la mwili likaongezeka, aliangalia pambizoni mote na hakumuona mwanamke yeyote, akajihisi vibaya na akachukizwa kukaa zaidi aliamua kurudi, lakini hatua zake zilikuwa nzito na athari za uchovu zilishaanza, alijivuta kwa kujibeba hadi alipofika kwa Levi, ambae alimkuta amekaa akimsubiri njiani.

Umerudi mara moja.

Nimechoka sana, Je tunaweza kurudi kwa gari mara moja?

Vizuri, kama utakavyo.

Au unaweza kuleta gari hapa?

Inaonesha umechoka sana… samahani haiwezekani kuja na gari, unaweza kuniegemea, haya twende.

Uchovu ulikuwa wazi sana kwa Joji, Levi aliweka mkono wa Joji shingoni mwake ili amuegemee, alijitahidi kuinua mkono wake wakati anatembea lakini uchovu ulimzidi uzito, aliinamisha kichwa chake mabegani kwa Levi, upepo unapovuma ulipeperusha nywele zake usoni mwa Joji, na harufu ya mwili wake puani mwake, nywele zake mkononi mwake, na wakati mwingine mashavu yake kukutana na ya kwake.

Samahani sana, nimekuchosha mara iliyopita na sasa hivi tena…inaelekea nadeka.

Usijali…cha muhimu ni kufika kwenye gari upesi….kuna hospitali ipo karibu hapa tutaelekea, baada ya hapo utakamilisha kudeka kwako na kupata tumaini.

(2)

Levi alimpeleka mbio Joji katika kitengo majeruhi hapo hospitalini, Joji alipigwa sindano ya kutuliza maumivu ambayo ilimpelekea kulala mara moja…Levi alikwenda kwa daktari kuulizia hali yake.

Ana nini?

Usiogope, nimempa dawa ya usingizi apumzike kidogo, baada ya saa moja hivi tutajua matokeo ya vipimo vyake, kisha akatabasamu na akasema: unaelekea kuogopa sana, Je, ni mume wako au mpenzi wako?

Ni rafiki yangu tu.

Kwa hali yoyote baada ya saa moja matokeo yatakuwa tayari na ninaamini ataamka kabla ya muda huo.

Levi alikaa pembeni ya Joji, na akaanza kumuangalia pale alipolala akawa anamfuta kipaji chake na kupapasa nywele zake, alikuwa akihisi hisia kali kwake… baada ya muda Joji alifungua macho yake, na mkono wa Levi ukiwa bado unapapasa nywele zake.

Nipo wapi?

Ashukuriwe Mungu kwa kuamka, tupo hospitali, nawe upo katika hali njema.

Yuko wapi daktari?

Atakuja baada ya muda, akiwa pamoja na matokeo ya vipimo, pumzika kidogo usijichoshe… Joji.

Joji alishika mkono wa Levi ambao ulikuwa una mpapasa usoni na kwenye nywele, kisha akampapasa kwa upole….

Nakushukuru sana Levi, sikutarajia kukuchosha hivi….

Usiseme hivyo, nipo kwa ajili yako.

Dakika kadhaa zilipita hawakuzungumza chochote mbali ya lugha ya ishara na ya kugusana ambayo ilikuwa ni kubwa kuliko lugha ya mantiki….hadi alipofika daktari kumuangalia Joji….

Umeamka Joji? mpenzi wako…samahani rafiki yako alikuhofia sana.

Ehe daktari kuna habari gani?.

Matokeo ya awali yanaonesha umeshambuliwa na virusi vikali, ama vipimo vingine vitatoka kesho.

Lini ninaweza kuondoka?

Baada ya saa moja au kesho ukipenda, muda utakavyojihisi vizuri, na utakapotoka nesi atakupatia dawa zako, haya nawaaga.

Samahani Joji kaa hapa hadi kesho; hii ni dhamana zaidi ya afya yako.

Joji aliuminya mkono wa Levi kwa nguvu, na kumuangalia kwa amani….

Asante sana Levi, nataraji kwenda hotelini, na naomba samahani kwa kutokamilisha msafara wetu.

Levi aliuondosha mkono wake na akaweka kifuani kwa Joji, kisha akaunyanyua na kuubusu..

Nakuomba msamaha

Levi alibabaika sana na uso wake kuonekana na haya pamoja na hisia ya furaha na uchangamfu aliokuwa nao Levi alitabasamu…..na akamuomba asifanye haraka; kwani leo ni Jumamosi na bado ni mchana na jua bado halijazama…

Unaomba msamaha kuhusu nini? Usiombe msamaha, muhimu uwe katika siha njema.

Levi alimaliza taratibu za kumtoa Joji hospitalini na akapokea majibu ya vipimo vilivyokwisha kuwa tayari na dawa na akaweka ahadi ya kesho saa 4 asubuhi.

Je, ni lazima aje mwenyewe au naweza kuja kumchukulia matokeo ya vipimo vyake?

Machovu yakimrudia njooni pamoja, vinginevyo inatosha kuja peke yako kesho kuchukua majibu yaliyobakia.

Kama ni hivyo nitakuja kuchukua majibu kesho, Je, ataondoka na gari la wagonjwa au gari langu?

Kwa gari lako, utaondoka akiwa anatembea kama utakavyoona… kisha akamgeukia Joji na kumwambia: tafadhali unaweza kwenda.

Basi subiri nitasogeza gari mlangoni.

Levi alirudi, akamshika Joji mkono na kumpeleka hadi kwenye gari, alimfungulia mlango na akabaki pembeni yake ili amsaidie…akamuangalia kwenye macho yake ya kibluu na yote yakiwa katika upole

Asante Levi, sijui nikushukuru vipi…..

Pole pole – kwa hisia asiyoikusudia – alimgeukia, na kukaribia mwili wake, akamkumbatia na kumbusu kwa muda mrefu; alibabaika sana pamoja na tabasamu lililojaa alijaribu kulificha..

Samahani leo ni siku ya ibada tu, huna haja ya kunishukuru; mimi nafanya kinachoniambia dhamira yangu.

Samahani sana labda nimekukera, sikujua jinsi ya kuonesha shukrani zangu kwako ndio maana nikakubusu.

Huu sio wakati wake …unaweza kupumzika kwa sasa… kisha akatabasamu tabasamu la mchawi: Kakhi alikuwa akinibusu sana (kumbatia) na hakuwa akiomba samahani: ni kiasi nilikuwa nikimchukia.

Samahani; sikukusudia kukuchukiza, sijui kwa nini nimefanya hivyo, huenda ulikuwa ni wakati wa dhoofu wangu, kwa sababu ya maradhi, au huenda kama alivyosema Habib: Kuvutiwa kwa roho nzuri kumechanganyika na kuvutiwa na mwili mzuri.

Au huenda ikawa ni kuchanganyika kwa roho ambayo tulikuwa tunaizungumzia, hata hivyo achana na maudhui haya, unajisikiaje sasa?

Najihisi kuwa na haya kwako na kwa nafsi yangu, matamanio yangu yameonesha udhaifu wangu, niamini sikuwa na nia ya kukukera au kukuaibisha bali nilitaka kuonesha na kutoa yaliyo moyoni mwangu.

Naomba funga maudhui haya, nimekwambia kuwa Kakhi alinikumbatia na si hivyo na kunibaka vile vile zaidi ya mara moja na wala hakuomba msamaha, bali baya zaidi ya hilo nilikuwa nikijihisi wakati mwingine naona raha pamoja na Kakhi mchafu fikiria nikiona raha pamoja na kulazimishwa kuachia misimamo yangu. Huenda ikawa Benjamin alikuwa mkweli ya kuwa sisi tunafurahisha viwiliwili vyetu huku tukidhulumu na zikiumia roho zetu.

Huenda hatukupata njia ambazo roho zetu zitanyooka pamoja na miili yetu, na hivyo basi roho zetu zikafurahisha miili yetu na miili yetu ikafurahisha roho zetu.

Huenda ikawa muradi wake ‘njia ya kuelekea kwenye furaha, usisahau kunijulisha ukiifikia, vinginevyo sitokusamahe.

Nitakapomaliza safari yangu, inaelekea kila ambaye nitakutana nae anasubiria matokeo, nina kariri kuomba radhi kwako na shukran nyingi kwako Levi.

Tutafika hotelini baada ya dakika chache, na ninakutaka upumzike chumbani kwako, na nitawaambia wakuletee chakula cha usiku –chumbani; kwani chakula cha mchana umeshachelewa, na ikifika asubuhi watakuletea kifungua kinywa….na mimi nitakwenda hospitali kuchukua matokeo ya vipimo, kisha nitakuletea. Lini unasafiri?

Nimeweka lijamu ulimi wangu, asante sana, safari yangu ni saa kumi na mbili jioni.

Walifika hotelini, Levi akapanda nae chumbani na kumlaza kitandani….

Napenda kukaa pamoja nawe, lakini naogopa kukuchosha kwa mazungumzo yetu na hivyo nitaondoka.

Huwezi kujua kiasi cha furaha yangu kwa mazungumzo nawe, lakini nakuruhusu uondoke ili upumzike, kwani nimekuchosha sana.

Jua limezama, na ninataka kufanya kitu lakini sijui, unaweza kufasiri unavyotaka.

Sijafahamu!

Levi alimsogelea Joji na kumkumbatia na akambusu kwa muda mrefu…. Joji alijihisi kama ule mmea uliopo jangwani inaponyeshwa na maji, pamoja na kuchoka kama angeendelea kukumbatiwa angeendelea ukaribu zaidi….

Jumamosi yetu imekwisha, nitakuachia tafsiri ya nilichokifanya; mimi sijui kwa nini nimefanya hivyo, kwa heri.

Tendo la Levi lilikuwa la ghafla sana kwa Joji, hakufahamu tafsiri ya tendo lake, kama alivyokuwa hajafahamu tafsiri ya tendo lake yeye mwenyewe alipomkumbatia je, ni kweli matendo yetu yanafanyika bila ya khiari! Au yakuwa udhaifu wa maradhi ndio sababu? Au ndio mchanganyiko wa kiroho ambao unaweza kufasiri hilo? Au ni matamanio ya kijinsi na makosa? Au ni mchanganyiko baina ya mchanganyiko wa kuvutiwa kwa roho na mwili kama alivyosema Habib?...Sababu yoyote ile iwayo lakini inabainisha udhaifu wa mwanadamu… au huenda ikabainisha haja zetu ya Yesu kusafisha madhambi yetu kisha baada ya hapo hisia zake zikaondoka akimfikiria Levi na akakumbuka alipokuwa nae na khofu yake, baina ya hali yake hiyo simu yake ikalia, upande wa pili alikuwa ni Katarina…

Mpenzi, vipi hali yako sasa hivi?

Hali nzuri, nimetoka hospitali sasa hivi na naendelea vizuri, nani aliyekuambia kuwa mimi ni mgonjwa?

Maradhi yako, maradhi gani? Ninachokifahamu ni kile alichoniambia Tom jana katika hafla kanisani kuwa ulimwambia umechoka sana.

Tom tena?

Mpenzi wangu bado unanishuku

Abadan, hali yangu ni njema na kesho narejea, ndege itaondoka saa kumi na mbili jioni.

Tutakusubiri na gari la wagonjwa.

Hakuna haja ya hilo, mimi ni mzima.

Usijali tunataka kutumaini hali yako… sitaki kurefusha jaribu kupumzika sasa, kwa heri kwa jina la Mungu

Kwa heri mpenzi wangu kwa jina la Mungu

Joji alimaliza mazungumzo akiwa anafikiria majaliwa ambayo yamemfanya Katarina kuwasiliana nae baada ya kumkumbatia Levi, ili amkumbushe Tom alipomkumbatia na ghadhabu yake kwa hilo, na akajiuliza: Je sisi ni unyoya katika mvumo wa upepo au ya kuwa majaliwa yanampelekea katika jambo asilolifahamu? Je raha ya kiwiliwili ina maana ya huzuni na tabu kwa roho na misingi yake! Jehaiwezekani kukusanya pamoja! Inaelekea kuwa siku za usoni pana matukio mengi ambayo hatuwezi kuyatabiri.
Katika hali hiyo alifika mfanyakazi na chakula cha usiku chumbani kwake, na akaingia mhudumu akiwa anatabasamu na akamsalimia Joji…

Inaelekea yule mwanamke anakupenda na kukujali sana, alihakikisha mwenyewe kuwa chakula ni kizuri, na akatupa maelekezo tukukumbushe kuhusu dawa zako, na hakuondoka hadi alipohakikisha kuwa tumepanda na chakula chako.

Vizuri, asante sana.

Joji alikula chakula upesi upesi… kisha akajilaza kitandani akifikiri siku hii ya leo, alitamani kuangalia barua zake hata hivyo aliona ni bora kuchelewesha hadi kesho.

(3)

Joji hakuamka ila saa tatu asubuhi, pale pindi mtumishi alipogonga mlango wa chumba chake akimletea kifungua kinywa.

Haya ni maelekezo ya mpenzi wako, kwani aliwasiliana nasi kabla ya nusu saa ahakikishe kuwa tumekutayarishia kifungua kinywa, kadhalika alitupigia jana saa nane usiku; ili ahakikishe kuwa tumewasiliana nawe ili uchukue dawa zako… wewe una bahati sana kumpata mwanamke mzuri kama yeye anayekupenda bali ni ashiki wako.

Asante Joji, hakumjibu akiwa anarejea maneno: Mwanamke mzuri, mwenye kupenda, kisha alipata istiftahi yake, na akawasha Kompyuta yake ili aangalie barua pepe na kujibu yale yanayopaswa kujibiwa kisha akamuandikia barua Tom na Adam kuwajulisha maradhi yake, na yakuwa atarudi leo hii London, na baada ya hapo akawauliza: Je, wanajua chochote kuhusu furaha za roho au ya kuwa roho haina isipokuwa mateso na ya kuwa starehe zote ni za kiwiliwili tu? Je, unaweza kuzifurahisha, au inapasa ili kuzifurahisha roho zetu basi viwiliwili na akili zetu ziteseke?
Levi alikwenda hospitalini, ili kupokea matokeo ya vipimo, daktari akamjulisha kuwa virusi vilivyompata Joji ni virusi ilivyokuwa nadra sana na kitaalamu kwa mara ya kwanza huingia kichwani, kwa maana hiyo wapo katika hali mpya. Daktari alipendekeza arudi tena hospitali baada ya wiki moja hadi siku kumi, kwani haiwezekani kutabiri kitakachotokea katika hali ya Joji, kwani virusi hivyo vinaweza kuibuka upya na kupata nguvu mpya na hivyo basi wakati wowote inaweza kutokea jambo ambalo itampasa kuwa karibu na daktari. Levi alilia sana akihofia hali ya Joji, na hakujua cha kufanya, akawasiliana na Habib ambaye alimfuata Levi hospitalini, alikuwa akijiuliza au akimuuliza Habib; kwa nini anajali sana hali ya Joji? Je anajali kwa sababu ya matamanio ya kiwiliwili kwa mtu aliyekataa kufanya nae mapenzi na hivyo kutaka kumhurumia kwa sababu ndizo huruma za kike? Au ni mshikamano wa kiroho kwa fikra yake, tabia yake na elimu yake? Au ni kwa sababu ya mchanganyiko wa kufanana katika utafiti wa njia itakayopelekea kwenye furaha? Alikuwa akimuuliza maswali hayo Habib naye….nae akijaribu kumuuliza, kisha wakaondoka pamoja kuelekea kwa Joji hotelini.
Simu ya chumbani kwa Joji ilipigwa akiwa anaendeea kusoma barua pepe zilizomfikia, akapokea huku upande wa pili Levi akisema:

Je utaturuhusu tuje chumbani kwako?

Karibu sana.

Aliingia Levi akiwa na tabasamu lililoficha huzuni ndani yake, Joji alimkaribisha na akampa mkono.

Nipo na mgeni, je utamruhusu?

Usiweke mipaka baina yetu, mgeni wako ni mgeni wangu, karibu.

Habib aliingia na Joji alimkaribisha kwa furaha, alifurahi kufika kwake.

Inaelekea ulipata ugonjwa kwa sababu yangu; maradhi yalikuanza ulipokuwa pamoja nami, na Levi yupo mbali na hilo.

Levi yupo mbali na kila aibu; Yeye ni tohara kuliko tohara yenyewe.

Lugha ya mapenzi katika hadhira yangu.

Ha ha ha, nimesahau kuwa wewe ni mlinzi wetu

kwa tabasamu la kichawi, akiwa anaona haya, akiwa ana muangalia Joji…

Sijafahamu uliposema kuwa Habib ni mlinzi wetu, mlinzi katika nini?

Usijali…. Joji anataka kutuharibia tu….kisha akamgeukia Joji: Na kumuuliza kuhusu afya yake sasa.

Katika hali nzuri kama unavyoona, nipo katika hali nzuri, Jana nilichoka sana na Levi nikamsumbua na kuchoka pamoja nami.

Hakunichosha kabisa, ila sikujua nifanye nini? Mara nyingi nababaika katika hali kama hizo katika mazingira magumu nataraji kuwa mimi ndie ambaye sijakuchosha, ilikuwa ni bora kufuta ile ziara yetu pindi uliponijulisha uchovu wako, huenda kwa kutokufahamu vizuri ndio sababu!

Hukukosea kabisa, na kilichotokea kwangu ni jambo la ghafla.

Daktari ameshauri kuwa ukae hospitali siku mbili au tatu, unaonaje?

Ndege inaondoka saa kumi na mbili kwa maana natakiwa kuondoka hapa baada ya masaa mawili na nusu kutoka sasa na wewe unaniambia siku mbili au tatu!

Joji nakuomba siku mbili au tatu tu ili tupate kutumai hali yako zaidi.

Hali yangu ni nzuri, nini ripoti ya mwisho ya daktari?

Mpe ripoti yake Levi, ripoti ni nzuri, na yeye anataka kupata tumaini tu.

Joji alichukuwa ripoti kutoka kwa Levi akiwa anamuangalia machoni, na akamuahidi kuwa ataiangalia nafsi yake na kwenda hospitalini mara tutakapofika London.

Itapasa kwenda kwa daktari mara tu utakapofika London ili tutumai hali yako Joji.

Katarina mke wangu ameshajua hali yangu na kuwa atanisubiri kwa gari la wagonjwa Uwanja wa ndege, nimeshawasiliana nae asifanye hivyo lakini amesisitiza hilo, ana inadi mfano ewe Levi.

Vizuri alivyofanya hivyo Katarina, ili apate kutumai hali yako, mbele yetu tuna masaa mawili takriban, kwa hivyo inanipasa kula chakula cha mchana, kisha tayarisha mkoba wako wa safari.

Chakula cha mchana baada ya saa moja hivi kwa pamoja tutakwenda kula hapo katika mgahawa wa hoteli, nawaalikeni wala msinirudishe, na wala sihitaji zaidi ya robo saa baada ya chakula cha mchana ili nikoge na kutayarisha mikoba yangu.

Tumewafiki ili mradi iwe chumbani kwako na sio katika mgahawa hapo hotelini; ili tusikuchoshe.

Oh oh ewe Levi…. ningependa kutembea kidogo, wala hainichoshi kula mgahawani.

Habib, akiwa anajaribu kuondosha upweke uliojificha baina yao….

Ili tutumie muda uliobakia, lete habari za njia ya furaha?

Hii ni mara ya pili nasafiri kwa ajili hiyo ewe Habiib katika kutafuta njia ya furaha, mbali ya vikao mbalimbali na majadiliano na mikutano mbalimbali, maudhui haya yamenikamata. Wakati wangu na juhudi yangu yote nimeipotezea hapo, na nataraji kupunguza juhudi kwa mafanikio.

Levi: Mafanikio yako ni mafanikio yetu sote, tunasubiri matokeo ambayo yatafikia hapo.

Habib: Safari yako ya kwanza ilikuwa wapi?

Nitawaambieni katika mpangilio kama asemavyo Katarina: Nchi ya ajabu, kisha nchi ya vita na mauaji, kisha nchi za Makanisa.

Habib Nchi ya maajabu tunaifahamu kuwa ni India, na nchi ya vita na mauaji ni hii uliopo sasa, nchi ya Makanisa ni ipi?

Rome na Vatican, ndio safari ijayo inayonisubiri.

Habiib: Ziara yako ya Yerusalem inaweza kuwa imekusaidia; kwa kuwa ni uzawa wa dini na rejea zake katika migogoro yake, na Vatican unaweza kusawiri maana ya ziara yako; kwani ni sehemu muhimu kwa Wakristo pamoja na tofauti za dini zao, ama India kwanini ulikwenda na ikawa safari yako ya mwanzo?

Kwa sababu swali langu la mwanzo lilikuwa Je, dini za mbinguni ni bora kuliko dini za ardhini? Ndio maana nikaenda India, kisha swali lililofuata….

Levi: Samahani kwa kukukata ulitarajiwa swali la kwanza liwe: Je, ni bora kuwa na dini au kupinga dini ni bora.

Swadakta, lakini nilikuwa naona na bado ninaona kuwa kumkana Mungu na dini ni maradhi ya nafsi baada yake inafuatia Falsafa ya kusadikisha hata hivyo ndani ya nasfi zao wanaamini kuwepo kwa Mungu, na huwezi kupata maradhi yaliyokuwa makubwa zaidi na mabaya zaidi kuliko kumkana Mungu.

Habib alitabasamu akiwa anamuangalia Levi, kisha akasema:

Swadakta, lakini ulipaswa kutafuta hili kwa njia ya kielimu zaidi.

Nimetafuta ukweli, nimetafuta! Lakini unanitaka nisafari ili nione hilo?

Habib; Ha ha ha, safiri ndani ya maisha ya mkana Mungu yoyote, na utahakikisha unachokisema!! Sijui wanawezaje kustahmili!!

Levi: Ndio maana wengi wao ni wenye huzuni na wenye kujua mara kwa mara.

Niache nikamilishe, suali la pili limekuja baada ya kujua kuwa dini za ardhini ni za uongo, yaani dini za mbinguni ni bora? Hivyo basi safari ya nchi takatifu ilikuwa ni kuuangalia Uyahudi kwa karibu kisha akamgeukia Levi na kusema; Na baada ya kufika hapa nimefurahishwa na usuhiba wako.

Hivyo basi mazungumzo yetu juzi kuhusu Ukristo na madhehebu yake mbalimbali na vita iliopo baina ya madhehebu hayo tumeharakisha kabla ya safari yako ya tatu?

Ndio, lakini ni haraka ya mahali pake, safari ya tatu itakuwa Vatican; ili kujua vilivyo dini ya Ukristo.

Imebaki kujua dini ya Uislamu vilivyo.

Ghadhabu ilikuwa wazi katika uso wa Levi, na akasema: Dini ya Wanyama, nenda Makka ili uifahamu, hawatokuruhusu kuingia kadiri utakavyofanya.

Ha ha ha, punguza ghadhabu zako, ukweli ni likuwa natamani kukutana na Waislamu hapa Yerusalem (Qudsi), usisahau kuwa wakazi wengi hapa ni Waislamu, lakini sikuweza kwa sababu ya upungufu wa muda wa safari, kisha haya maradhi, kwa ujumla huenda nisihitaji safari ya kwenda nchi za Kiislamu.

Habib alimwangalia Levi machoni.

Ama suala la wasiokuwa Waislamu kukatazwa kuingia Makkah ni sawa na Wayahudi kuwakataza Waislamu kuingia katika ukuta wa kulilia au ni kama wanavyozuiwa wanawake kuiingia. Au mfano wake kukatazwa kwa vijana kuswali katika msikiti wa Aqswa siku ya Ijumaa, au…..

Joji, polepole sijakuambia kuwa wewe ni Muislamu uliyejificha katika Ukatoliki!

Levi: Ha ha ha, huyo ndivyo alivyo siku zote, nasasa hivi nina mtu wa mfano wa dini yangu dhidi yako ewe daktari.

Usitake msaada wa Joji dhidi yangu; yeye anaondoka leo hii, na sisi tutaendelea na mjadala wetu, hata hivyo kwa ajili ya uadilifu ni kufanya utafiti kama anavyofanya Joji kuhusu Uyahudi, Ukristo vivyo hivyo ufanye kuhusu Uislamu. Je, sikukutaka ewe Joji ufanye utafiti kuhusu ukanaji Mungu? Je ukanaji Mungu kwenu nyinyi ni bora kuliko Uislamu?

Ha ha ha, huenda ikawa hivyo.

Tumechelewa, Je, tukutangulie mgahawani au tuteremke pamoja?

Yatupasa tumsaidie kushuka kwani yeye bado amechoka.

Asante Levi, tangulieni nitakuja sasa hivi kwani nitaingia maliwatoni.

Habib na Levi walitangulia mgahawani, wakachagua meza nzuri, wakakaa wakimsubiri Joji, na wakati huo huo Habib akaanza kuzungumza…

Nina wasiwasi kuwa umevutiwa sana nae kuliko inavyotakiwa.

Kwa nini?

Samahani kukuingilia lakini jinsi mnavyoangaliana inatia shaka na jinsi mnavyoangaliana ni kama vile wapenzi wawili.

Sijui kwanini tumefikia hapo! Pamoja na kwamba nilikwambia kuwa tokea mwanzo amekataa maingiliano yoyote ya kimapenzi, na aliniambia kuwa anampenda mke wake na analiona jambo hilo ni kama vile kufanya hiana.

Nilikuambia kuwa usichanganye baina ya kuvutia kwa roho na tabia na kuvutiana matamanio yanayotokana na silika ya jinsia.

Jana lilitokea jambo la ajabu sana, nilimbeba baada ya kuanguka, kisha akanibusu kwa mara ya kwanza, baada ya kumuweka kitandani chumbani kwake nami nikambusu.

Busu kwa bahati mbaya ni jambo la kawaida kabisa katika jamii zenu wote, lakini kilichokuwa si cha kawaida ni kuachana na misimamo yenu.

Sina tafsiri ya kilichotokea, nadhani ni kama unavyosema, au ni udhaifu wa mwanadamu.

Mara akafika Joji akakaa mezani pamoja nao.

Mgahawa wa buffet umefunguliwa, je mngependa tusimame tuchukue chakula chetu?

Walipokaa mezani kwa mara nyingine baada ya kuchukua chakula chao. Habib alipendekeza kuwa Levi na Joji waendeleze mjadala, kwani hiyo ni fursa nzuri na wamekutana wote watatu pamoja…

Tuendelee tuliposhia, mimi nashauri usafiri haswa kwa ajili ya kuwajua Waislamu.

Pamoja na kuwa natofautiana nae daima, ila kwa hili nawafikiana nae kwa sasa, kwani kautetea ukanaji Mungu kama alivyoutetea Uislamu.

Ha ha ha, siwezi kuutetea ukanaji Mungu wala Uislamu, mimi nazungumia suala la mfumo wa Kielimu ili kufikia kwenye ukweli.

Mara nyingi ninaposafiri ninakutana na mijadala ya namna hii, kadhalika inabidi niwe na tabia ya kusoma kwingi. na kufikiri kwa kina na kushauriana na watu baada ya kurudi kwangu, ila mara hii nimepambana na maarifa mengi na elimu nyingi kuliko wakati wa kuyafikiria, huenda kazi hiyo ya kufikiri nikaifanya baada ya kurejea kwangu na haswa ya kuwa safari yangu ilikuwa na utajiri mwingi na faida lukuki

Levi akiwa anaangalia macho ya Joji kutafuta dalili.

Je naweza kuuliza swali ambalo nataraji lisikukere?

Karibu, uliza.

Je utakapokinaishwa kuwa Uyahudi au Ukatoliki, Orthodoksi au hata Uislamu au Uprotestant kuwa ndio njia ya furaha.Je, utahamia moja kwa moja huko, au utaanza kufikiria faida na hasara zake?.

Mimi nadhani kuwa mahesabu yote ya faida na hasara yataishia pindi nikipata njia hiyo ya furaha; kwani hiyo ni faida halisi, Je, kuna faida iliyo na furaha kuliko njia hii …cha msingi ni kupata.

Habib alimuangalia Joji kwa kumkazia na kumwambia:

Utaipata, mwishowe utaipata, lakini naingiwa na mashaka na unachokisema…

Unashuku katika nini?

Ninashuku kwa wepesi wa hilo, na kutokuwepo mahesabu ya faida na hasara, baadhi ya maamuzi ni magumu…!!

Vipi?

Niachie niikaribishe fikra yangu kwako, wagonjwa wote wa sukari wanajua kuwa kula sukari kwao inawadhuru hata hivyo bado wanatumia! Na kila mnene anafahamu kuwa kula chakula kwa wingi si katika siha na ni madhara kwao lakini hata hivyo wanakula.

Ni nini uhusiano wa hilo?

Kubadilisha dini ni kugumu kuliko kubadilisha ada ya chakula, bali ni kubatilisha maana ya maisha na sababu zake na ndio zenye kuiharakisha na kuisukuma, kisha akamgeukia Levi akasema: Nadhani Levi analifahamu hili vizuri, kwa hali yoyote mwishowe utaipata hiyo njia.

Kwa nini una hakika namna hii? Si nyote mnatafuta na hamjaipata hadi sasa hivi?

Huwezi ukashikilia namna hii kisha usiipate, kisha anakuwa mbali na ukarimu wa Mungu Je, hawezi kumsaidia anayetafuta ukweli?

Unanikumbusha kikongwe niliyekutana nae aliyekuwa akisema hivyo hivyo.

Kikongwe alisema nini?

Mtashangazwa nitakachokisema, niliamua kwenda kujinyonga, nikakutana nae akielekea kuwa ni mtu mwenye furaha, nikamuuliza je wewe ni mtu mwenye furaha? Akanijibu ndio, nikamuuliza tena nitaifikiaje njia hii ya furaha? Kwa ujumla yeye ndie wa mwanzo aliyeniambia na kulitaja neno hili “Njia ya furaha.”

Alikujibu nini?

Hakunijibu kitu bali aliniambia: Ukiwa unaloshikilia hilo na kuazimia utalipata.

Hukuwasiliana nae baada ya hapo?

Kwa bahati mbaya sikuchukua namba yake wala anauani yake yeye ndie aliyechukua namba yangu na anuani yangu, hata hivyo hakunipigia.

Samahani, muda wako Joji unakwenda upesi, inabidi umalize chakula chako na kutayarisha mikoba yako upesi.

Sitochelewa …robo saa nitakuwa tayari… kisha huyo akapanda chumbani.

Nimevutiwa na ujasiri wa Joji na wepesi wake wa mambo.

Hata mimi.

Kwangu mimi naweza kuvutiwa nae itakavyo, kwa kuwa mimi ni mwanamme, ama wewe jichunge.

Nyie Waarabu mnatofuatisha baina ya mwanamme na mwanamke!

Waarabu au Wayahudi? Mimi nadhani tumefunga mjadala wetu, lakini vimebaki baadhi ya vitu tofauti huwezi kuvifuta.

Mfano wa nini?

Ha ha ha, mfano wa kuwa mimi sio mzuri kama wewe, nami si mwanamke, na wewe sio mwanamme, unataka kubadilisha tabia tufanye nini, na itabakia kuwa kila mmoja ana nafasi yake tofauti, na utaendelea kubakia ni binti mzuri unayeweza kufanya mjadala na mimi mwanamume ninayeweza kujadiliana. Ama kuwafanya wanawake kama mbwa au uchafu au najisi…hili haliwezi kutoka kwa mtu au kwa dini ambayo inawaheshimu waamini wake.

Ninakifahamu unachokusudia vizuri, na ninaomba uache kunikosoa.

Samahani, lakini cha muhimu ni kubakiwa na kuvutiwa na fikra zake na kukishikilia na tabia na roho yake na sio kiwiliwili chake, na ulishamwambia hilo, na hii ndio maana ya mimi kuwa mlinzi wenu.

Aah, nimefahamu maana ya mlinzi, nitaingalia nafsi yangu, inatosha kilichotokea jana.

Joji aliteremka upesi, na kumaliza taratibu za kuondoka hapo hotelini, na akaelekea hadi kwa Levi na Habib ambao walikuwa wakimsubiri.

Inaelekea kuwa wakati unatutupa mkono, je tuondoke?

Ndio, naogopea foleni au vituo vya ukaguzi njiani.

Mungu akuhifadhi, Levi atakusindikiza, Ama mimi unanisamehe nina ahadi sehemu, hata hivyo usiache kutujulisha maendeleo yako na “Njia ya Furaha.”

Je, hutokamilisha ulinzi?

Ha ha ha, hakuna wa kuwalinda isipokuwa Mungu, wala hakatazi mtu kitu mfano wa misimamo yake.

Nitasogeza gari mlangoni ili kubeba mikoba.

Nakushukuru Joji, umetufurahisha, nasubiri kusikia habari zako. Mungu akulinde usisahau kwenda hospitali ya karibu pindi ufikapo London, kadhalika usisahau kuchukua sindano ambayo anayo Levi.

Sindano gani?

Sindano ambayo unaweza kuitumia ndani ya ndege ikitokezea umepatwa na uchovu, ni sindano uliyopewa na daktari.

Asante sana.

(4)

Joji alitoka na kumkuta Levi akimsubiri kwenye gari, na mikoba ipo tayari garini, akapanda wakaondoka kuelekea uwanja wa ndege.

Tutakukosa Joji, hujakaa nasi isipokuwa siku chache tu, ila ni kuwa umetuachia kumbukumbu kubwa isiyosahaulika.

Bali tabasamu linalong’ara na elimu yako na fikra zako hazisahauliki, nimefaidika nawe sana, na nimekuchosha sana, asante sana.

Macho ya Levi yalijaa machozi…

Nami nitakosa mijadala yako na mazungumzo yako na mtazamo wako, nitarejea katika mateso ninayoishi nayo.

Hastahiki mfano wa Benjamin machozi haya.

Si tatizo iwe ni Benjamin au ni Mayahudi wote, la kweli lipo ndani, mimi sijui njia ya furaha, na nilikuwa nahisi furaha nyingi katika mjadala wetu.

Mjadala wetu utaendelea pamoja, kadhalika mjadala wetu utaendelea pamoja na Habib vile vile. Unajua! Wewe ni mkweli kwani mimi tokea nilipoanza kupita katika njia ya furaha sikupatwa na humwona ambaye ilikuwa hainiachi.

Nachukulia hii kuwa ni ahadi kutoka kwako ya kunijulisha utakapofikia katika safari yako ya njia ya furaha, nami nitakujulisha tulipofikia na Habib.

Ahadi lakini kwa sharti.

Sharti lipi?

Kufuta machozi yako na kutabasamu, ningependa kuuona uso wako ukiwa na tabasamu.

Tumewafikiana, na naomba msamaha wako kwa yaliyojitokeza jana nilipokuwa nakuaga, niamini sikujua kwa nini nimefanya hayo.

Nimekufahamu vizuri, nami kama wewe sikujua kwa nini nimefanya mfano wake tulipokwenda katika ukuta wa kulilia. Ha ha ha, huenda kwa sababu sikuweza kulia pale ukuta wa kulilia.

Kwa nini hukulia?

Kwa nini nilie? Nilie katika hekalu ambalo hawakupata bado leo hii dalili ya (ukweli wake) pamoja na yote waliyofanya!

Huoni kuwa unavuka mpaka wa kupetuka mstari mwekundu unapozungumzia dini yangu?

Ha ha ha, samahani, unisamehe niliyoyafanya nami nipetuke mipaka kuhusu Protestant, kwani wao ni majambazi wameua mamilioni ya Wakatoliki huko Ulaya. Je umeridhia na kunisamahe ewe bibie?

Nimekusamehe bwana wangu, lakini kwa sharti.

Rudia tena, sharti gani hilo?

Nipate tumaini kuhusu hali yako kesho, walau kwa barua.

Tumekubaliana.

Tumeshafika, huu ndio uwanja wa ndege wa Ben Gurion umechukua jina la waziri mkuu wa kwanza wa Israel, na kwa taarifa uwanja huu uliwahi kushinda tuzo la uwanja wa ndege bora Mashariki ya Kati.

Joji alimaliza taratibu za safari na Levi akawa ana msubiri, alipotaka kuingia mlango wa kuondokea, Levi alimpa mkono ukiwa na sindano na kumwambia: Hii ni kutoka kwa daktari, utakapohisi joto ghafla limepanda juu au utakapohisi uchovu tumia, itakupa utulivu hadi utakapofika London.

Asante sana.

Macho ya Levi yalijaa machozi, na akatoa mkono kumpa Joji kisha akasema: Asante sana kutoka moyoni mwangu kwa muda wote tuliokaa pamoja, Joji alimpa mkono na mkono wake mwingine kuweka juu ya mkono wake, na akahisi kuwa atampoza mpenzi wake wa miaka mingi anayefahamiana nae, lakini pamoja na hayo yote alikuwa juu ya matamanio yake kama alivyokuwa Levi juu ya matamanio yake.

Nakuaga na Yesu akuhifadhi.

Nakuaga na Mungu akuhifadhi.

Kisha akageuka nyuma na moyo wake ukimkata kwa kuachana na Joji.