NJIA YA UTUKUFU

NJIA YA UTUKUFU

NJIA YA UTUKUFU

Mandhari ya Ikramu ya Mwenyezi mungu kwa mwanadamu

Allah alipomuumba Adamu aliwaamrisha (malaika) kumsujudia: “Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu.” (7:11),

Allah alimuumba mwanadamu na kumkirimu na kumfadhilisha juu ya viumbe vingine toka mwanzo; “Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.” (17:70),

Nae ni kiumbe aliyekirimiwa na kufadhilishwa tangu mwanzo kwa haya yafuatayo:-

1-Utukufu na ubora kwa kuumbwa kwake:

Allah amesema: “Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.” (95:4),

Kwa hiyo Akamuumba katika umbile ambalo ni umbile bora zaidi, kwa upande wa usawa wa kiwiliwili na kushikamana kwake, na kwa upande wa jinsi alivyompa akili na kufikiri, na akatamka na kusikia, na kumjaalia katika umbo lililo bora na umbile bora.

2-Utukufu na kufadhilishwa katika kudhalilishiwa bara na bahari kwa ajili ya mwanadamu:

Na hili linaingia kudhalilishwa kwa anga, nalo hili ni katika yanayohakikisha utukufu uliotajwa hapo mwanzo; kwa kuwa yeye Aliyetukuka amedhalilisha kila kitu kwa mwanadamu, na akafanya vitu hivyo kuwa ni vyake maalumu, tofauti na viumbe vingine; na hili linatoa dalili kuwa mwanadamu katika Ulimwengu huu ni kama vile Raisi mwenye kufuatwa au mfalme mwenye kutiiwa, na kila kisichokuwa hicho ni raia wake na mfuasi wake, Allah Ta’ala amesema: “Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini…” (17:70),

Bali Allah Aliyetakasika amefahamisha aliyoyadhalilisha kwa mwanadamu yaliyomo mbinguni na ardhini vyote: “Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.” (45:13).

3-Riziki ya vitu Vizuri

Allah amemfundisha mwanadamu kula anavyovitamani katika alivyoruzukiwa, na akajaalia katika chakula dalili za manufaa, na akafanya vyakula anavyokula mwanadamu ni vingi sana kuliko wanavyokula wanyama wengine, ambao hawali isipokuwa walichozoea, kama alivyomkirimu kwa kumdhalilishia yote hayo kwa fadhila zake na ukarimu wake yeye Subhaanahu: “(Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua.” (2:22).

4-Kufadhilisha kuliko viumbe wake wote Subhanahu wa Ta’ala aliyowaumba.

Hivyo basi mwanadamu katika njia hii anahisi utukufu, hadhi na umbo lake linalotokana na ukarimu wa Mwenyezi Mungu, hivyo basi mwanadamu hakuhesabika kuwa ni nukta ndogo tu katika Ulimwengu huu hai wa Mada… nukta ndogo isiyo na maana ukilinganisha na kiasi cha Mada ambayo ndio Ulimwengu mzima, ni nukta ndogo ambayo bomu moja tu la Nyuklia linaweza kufuta roho laki mbili kama ilivyotokea Hiroshima, ukubwa wa mwanadamu kwa mtazamo wa Uislamu unatokana na utukufu aliopewa na Allah ambaye ametayarishiwa mwanadamu tu, pale tunapoona katika maelezo ya Qur-aan kuhusu kuumbwa kwa mwanadamu na wote Ulimwenguni kumsujudia Adam, kisha Allah akamfukuza Ibilisi, kwa sababu ya kukataa kumsujudia Adam na sisi tunajua ni kiasi gani msingi huu muhimu katika kujenga na kumjenga mwanadamu wa Ulimwengu huu. Ni muhimu katika muda ambao mwanadamu hawezi kumaliza matatizo yake, kiasi cha kuvamia matakwa yake na nguvu ya mtu, ila kwa njia hii. Njia ya Qur-aan ambayo inampa mwanadamu uhuru wake, utukufu wake na rangi (aina) za uchaguzi wake wote.

Katika njia ya utukufu, ukarimu haifai kumdhalilisha mwanadamu au kumdharau, Allah Ta’ala amesema: “Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu.” (49:11).

Hakuna ubora katika kutukuzwa mwanadamu mweupe juu ya mweusi, au mwekundu juu ya manjano, au Muarabu juu ya Muajemi, au kabila fulani juu ya jingine au sehemu fulani juu ya nyingine, au tajiri juu ya masikini ila kwa ucha-Mungu, Allah Ta’ala amesema: “Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” (49:13),

Vipimo vya utukufu na ukarimu kwa mwanadamu

Na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Hakika Allah haangalii sura zenu wala mali zenu, lakini anangalia nyoyo zenu na matendo yenu” (Muslim).

Mwanadamu anapata utukufu na ukarimu kwa kadiri atakavyoshikamana na njia hii na kufuata: “Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu….” (36:10)

Na atadhalilika kwa kadiri ya kuwa mbali na njia hii ambayo wanakusanyika viumbe wote kumtii Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), Allah Ta’ala amesema: “Je! Huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu. Na anaye fedheheshwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumhishimu. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda apendayo.” (22:18).

Pamoja na kuwa Allah amemkirimu mwanadamu, isipokuwa watu wengi wamechagua njia ya udhalili. “Atakayedhalilishwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumtukuza”

$Berisha_Pennekmrt.jpg*

Berisha Pennekmrt

Mtaalamu wa Elimu Thailand aliyeingia Uislamu.
Kusingebakia Mwenye Njaa.
“Sijaona dini iliyoweka sheria timilifu kwa ajili ya Zaka kama Uislamu. Na Jamii ya Kiislamu inayopupia kutoa Zaka huepukana na ufukara, mtu kunyimwa mahitaji yake na watu kukimbia. Mimi ninasawirisha lau Ulimwengu wote huu ungeelekea kwenye Uislamu basi kusingebakia katika mgongo wa ardhi mwenye njaa yoyote mwenye kunyimwa.”

Na wakachagua kumuangalia mwanadamu kuwa ni wanyama au vyombo au kiasi cha mali alichonacho au mfano wa hayo katika mtazamo ambao inapingana na mantiki ya Allah kumkirimu mwanadamu huyu na kumfadhilisha. Utukufu wa mwanadamu ni kwa kuwa kwake mwanadamu, kwa hiyo Uislamu hautengenezi mgongano kati ya jinsia mbili, na huo si wa mwanaume dhidi ya mwanamke, au mwanamke dhidi ya mwanaume, watu wameumbwa, kwa Nafsi moja, Allah Ta’ala amesema: “Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.” (4:1),

Kwa hiyo Anayetaka ukarimu na utukufu basi na afuate njia ya karama na utukufu, Allah amesema: “…Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu...” (10:65).