Watu wote wanatafuta furaha, njia iko wapi?!

Watu wote wanatafuta furaha, njia iko wapi?!

 

Watu wote wanatafuta furaha, njia iko wapi?!

Wameafikiana katika lengo moja

$Benjamin_Disraeli.jpg*

Benjamin Disraeli

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza.
Furaha kwa mkabala
“Huenda ukasimamia jambo lisilokuletea furaha lakini hakuna furaha bila ya kusimamia jambo.”

Watu wote wanatafuta furaha, hivyo basi njia iko wapi?! Kila mtu kwa njia yake nyepesi anatafuta furaha, pamoja na tofauti mbalimbali za watu kuhusu madhehebu yao, kabila zao, utaifa wao, misingi yao ya kimaadili, malengo yao, ila wote kwa pamoja wanaafikiana katika lengo moja; nayo ni; kutafuta furaha na utulivu.

Utakapomuuliza mtu yeyote: Kwa nini unafanya hivi? Na kwa nini umefanya vile? Atajibu: Nataka furaha!! Awe amesema hivyo moja kwa moja au kwa maana yake.

Ni nini furaha?

$Tolstoy.jpg*

Tolstoy

Mwanafasihi wa Urusi
Furaha ipo karibu sana na sisi
“Tunaitafuta furaha mara nyingi lakini ipo karibu yetu, kama vile tunavyotafuta miwani iliyopo machoni mwetu.”

Kama ni hivyo ni nini furaha, na tunawezaje kuifikia?!

Furaha ni hisia za utulivu inayoendelea, yenye raha, tumaini na shangwe, hisia hizi hutokea kwa matokeo ya hisia ya mambo matatu yenye kudumu, nayo ni; wema wa dhati ya mtu, wema wa maisha ya mtu, na wema wa mwisho wa mtu.

Kuhusu mambo haya matatu mtu huanza kujiuliza mwenyewe, na maswali yanaongezeka na kuwa makubwa kila akikua, wala mtu huyo hapati furaha hadi aweze kujibu maswali yake yanayomjia mara kwa mara akilini, miongoni mwa maswali hayo ni:-

-Nani mwenye kuumiliki ulimwengu huu na kuufanya atakavyo?

-Ni nani aliyeniumba na kuumba ulimwengu huu ulionizunguka?

-Mimi ni nani? Nimetoka wapi? Kwa nini nimeumbwa? Mwisho wangu uko wapi.

Pindi mwamko wa mwanadamu unapozidi katika nafsi yake na katika maisha yake, maswali haya huzidi kumsumbua akilini mara kwa mara, kwenye fikra zake na roho yake, wala hapati utulivu wowote na furaha hadi zipate majibu yake na kutuliza nafsi yake.