Je, ni Njia ya Kumkana Mungu au Njia ya Dini?

Je, ni Njia ya Kumkana Mungu au Njia ya Dini?

Je, ni Njia ya Kumkana Mungu au Njia ya Dini?

Ni nani muumba?

$Lewis_Carroll.jpg*

Lewis Carroll

Mwana Hisabati
Njia zimekuwa nyingi Mungu ni mmoja
“Ikiwa hujui unakwenda wapi, basi njia zote zitakupeleka huko.”

Watu huanza kufikiria kujibu maswali yaliyotangulia, kuna njia mbili; Njia

ya kwanza ni ile ya kumkana Mungu, na ya kuwa ulimwengu ni maada.

Njia ya pili ni ile ya kumuamini Mungu kuwa ni Muumba wa kila kitu; na matokeo yake ni kujitokeza kwa maswali mengi miongoni mwake ni:-

-Je, inawezekana ulimwengu ukapatikana wenyewe tokea hapo mwanzo kutokana na maingiliano yaliyokuja ghafla bila kupangiwa muda.

-Je, inaingia akilini kuwa ghafla hii ya bahati nasibu isiyokuwa na mpangilio wowote ndio imeupata ulimwengu huu ulioratibiwa vizuri?!!

-Je, alichofikia mwanadamu tokea apatikane katika historia nzima ni zao la ukuzi au ndio huo ughafla wa bahati nasibu?!! Na ya kuwa sisi ni unyoya katika pepo yenye kuugeuza geuza kwa hali hiyo hiyo ya ghafla na fujo?!!

$Ralf _W_ Emerson.jpg*

Ralph Waldo Emerson

Mwanafalsafa wa Kimarekani
Ainisha Muelekeo wako
“Kwa hakika ulimwengu unakunjua njia kwa ajili ya mwenye kujua anakokwenda.”

-Je, mwanadamu ndio Mungu aliyepanga sheria, nae ni Muumba mbunifu, naye ni kila kitu, na nyuma yake hamna kitu kingine?

-Je, yaliyokuwa nyuma ya maumbile katika mambo ya ghaib. Je ni mazigazi ambayo yanapaswa kupotea mbele ya wasio kuwa na Dini na Ulimwengu wa maada?.

-Je, mwanadamu ni maada tu asiyekuwa na mazingatio yoyote, au ni kuwa asili yake ilikuwa ni nyani aliyeendelea kwa kupita muda?

Ni aina gani mada ya ambayo inaweza kumuumba mwanadamu mwenye sifa hizi za hali ya juu, na mengi bora matukufu, aliyeumbwa kwa mengi ya kushangaza?!

Na je asiyekuwa nacho anaweza kutoa?!

Siri ya kuwepo maisha

$Einstein.jpg*

Einstein

Mwanazuoni wa Fizikia
Elimu na Dini
“Mimi si amini ya kuwa elimu yapasa igongane na dini katika hali ya kawaida. Kwa hakika ninaona kuna uhusiano na fungamano baina yao. Hivyo basi mnasema kuwa elimu bila ya dini ni kama vile mtu aliyepooza mguu. Na dini bila ya elimu ni kipofu kila kimoja ni muhimu. Zinatakiwa zifanye kazi pamoja mkono kwa mkono. Inaelekea kwangu kuwa Yule ambae hatofurahishwa na ukweli katika elimu na dini ni kama mtu aliyekufa.”

-Je, dunia ndio lengo la mwanadamu na mwisho wa kimbilio lake, hakuna mazingatio kwa yaliyosemwa na dini mbali mbali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwepo nguvu nyingine zisizokuwa mwanadamu, au maisha mengine yasiokuwa maisha haya?

Allah Ta’ala amesema kuhusu kufikiri kwa watu hao. “Na walisema: Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipo kuwa dahari. Lakini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadhani tu.” (45:24),

$Newton.jpg*

Newton

Mwanafalsafa wa Uingereza
Ulahidi (Kumkana Mungu)… ni aina ya Upumbavu
“Kumkana Mungu ni aina ya Upumbavu: Ninapoangalia utaratibu wa jua ninaona kuwa ardhi imekaa sehemu inayostahiki kutoka kwenye jua, ambayo inayoiwezesha kupata kiasi cha kutosha cha joto na mwanga, na hii bila ya shaka halijatokea ghafla.”

Kuhusu wale waliokataa na kupinga Allah Ta’ala amesema, “Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa mafisadi!” (27:14).

Kwa hakika wapinga dini (walahidi) wanakiri udhaifu wao kamilifu kuhusu kujua siri ya uwepo wa uhai kwa kiumbe chochote; vyovyote awavyo, awe ni mdogo kwa umbile au mkubwa, na wanakiri kuwa hawawezi kurejesha roho kwa mtu kama imefika kooni, kama ni hivyo ipo wapi ile maada wanayoiona kuwa ndio iliyopata na kuwepo ndani ya ulimwengu huu?!

Ni maada gani iliyotumika katika kupatisha ulimwengu huu?!

Na kwa nini wasiweze kuifikia ili kurejesha roho baada ya kiwiliwili kuwa mada isiyo na uhai wowote?.

Ikiwa kinachosemwa na hawa wanaopinga uwepo wa Mwenyezi Mungu ni sahihi iweje basi binadamu wote wakakubaliana kuheshimu dini kiasi hiki.

$Plato.jpg*

Plato

Mwanafalsafa wa Kigiriki (Kiyunani)
Ni nzuri yenye kufuata mfumo maalumu
“Kwa hakika Ulimwengu ni dalili katika uzuri na nidhamu wala hilo haliwezi kuwa ni matokeo ya sababu ya Itifaki, bali ni umbile la mwenye akili mwenye kukusudia kheri na kupanga kila kitu kwa makusudio na hekima.”

Kinachosemwa na hawa wapinzani wa Mwenyezi Mungu ya kuwa dini ni ndoto na mambo tu ya kufikirika?!

Kama ni hivyo kwa nini Mitume katika zama zao waliweza kubakisha mafundisho yao hai katika mioyo ya watu, wakati ambapo fikra mbali mbali za watu zimesahaulika, bali si hivyo tu, zimechuja baada ya kupita muda pamoja na njia mbali mbali za kuvutia zinazotumiwa na watu na ufasaha wao?!

Inawezekana vipi kutofautisha baina ya matendo ya kheri na yale ya shari? Bali ni kitu gani ambacho kinaweza kumkataza na kumzuia jambazi kuekeleza ujambazi wake? Na kitu gani kinaweza kufanya moyo wa tajiri kumhurumia fukara?

Na kipi kinaweza kumzuia mwizi na mtu mwenye kughushi, haini na mlevi wa mihadarati..wote hawa kipi kinachoweza kuwazuia kutekeleza matamanio yao?

$Lauren_Booth.jpg*

Lauren Booth

Mwanaharakati wa haki za binaadamu wa Uingereza
Furaha ya Kweli
“Hivi sasa ninaishi katika uhalisia na sio katika haiba ile ya udanganyifu ambayo tunaishi katika maisha yetu ya sasa. Maada, matumizi yetu, na maingiliano yetu na jinsia nyingine pamoja na matumizi ya mihadarati. kwa kudhania kuwa hivi ndivyo vinavyotupa furaha lakini kwa sasa nimeona Ulimwengu uliojaa furaha na uliojitosheleza kwa upendo, matarajio na amani.

Kwa hakika jamii za wakana Mungu zinaishi pamoja kama vile makundi ya mbwa mwitu yanayoishi kati ya wenye kudhulumu, wabinafsi, wenye kujipendelea, mapenzi ya matamanio yao na mengineyo; na hivyo basi ukanaji wa Mungu ni sababu kubwa ya tabu azipatazo mwanadamu, ufakiri, kuzidi kwa chuki, hofu na wasiwasi, amesema Allah Mtukufu: “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” (20:124).

Ukanaji Mungu ni fikra batili ambavyo akili, mantiki wala maumbile hayakubali, ni fikra batili inayopingana na elimu; na ndio maana wanazuoni wengi wamewapinga, kama ambavyo inakwenda kinyume na mantiki, kwani fikra yake imesimamia kuwa katika maisha haya hakuna mantiki, bali ni suala la ghafla na bahati nasibu tu ndio iliyouanzisha ulimwengu huu mzuri, wala hakuna maumbile maalum yaliyouanzisha; maumbile sahihi ni yale yanayomlingania mtu kuwa na dini hata kwa wale wanaojidai kuwa hawaamini: “Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa mafisadi!” (27:14).

KUNA MASWALI AMBAYO BADO YANAHITAJI MAJIBU

Bila elimu mwanadamu anakuwa si mwenye kufahamu majibu ya maswali haya, wala elimu za kisasa hazijaweza kujibu maswali haya; kwani kadhia hizi zinaingia katika mzunguko wa dini; na kwa ajili hiyo riwaya zimekuwa nyingi na ushirikina na simulizi zimekuwa nyingi katika maswali haya; jambo ambalo linazidisha babaiko kwa mwanadamu na kumtia hofu.

$Einstein.jpg*

Einstein

Mwanazuoni wa Fizikia
Ifanye furaha kuwa ni lengo lako
“Ukitaka kuwa mwenye furaha: Unganisha furaha na lengo na sio na mtu au na kitu.”

Wala mwanadamu hawezi kusimama kujibu majibu yenye kutosheleza kwa maswali hayo ila atakapoongozwa na Allah katika njia sahihi ambayo itamfikisha katika wema, amani na utulivu na kwenye furaha na raha.

Kadhia hizi na maswali haya hayaelezwi na kufafanuliwa na mfano wake ila kwenye dini mbali mbali; kwa sababu kadhia hizi huchukuliwa na kuzingatiwa kuwa ni katika elimu za mambo ya ghaibu, na dini iliyokuwa sahihi ndio ambayo inajipwekesha na haki na kauli ya kweli; kwa sababu ni kutoka kwa Allah ambaye amewapelekea wahyi Mitume wake, amesema Allah Ta’ala: “…Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu…”(2:120)

Na kauli yake Allah: “…Sema: Hakika uwongofu ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu…” (3:73)

Hivyo basi imekuwa ni lazima kwa mwanadamu kuikusudia dini ya haki, kujifunza na kuiamini; ili babaiko hili na shaka limuondoke, na aelekee katika njia iliyonyooka, njia ya furaha na ya tumaini.

MAJIBU YAWE VIPI?!

Kwanini tumeumbwa? Na tunaelekea wapi?

Allah amesema: “Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo. Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji. Kisha hakika nyinyi baada ya hayo mtakufa. Kisha hakika nyinyi Siku ya Kiyama mtafufuliwa.” (23:12-16).

$Descartes.jpg*

Descartes

Mwanafalsafa wa Kifaransa
Muumba wa Kila Kitu
“Mimi nipo: Basi ni nani aliyenileta na ni aliyeniumba?, Mimi sijajiumba; hapana budi kuwepo na Muumba, na Muumba huyu hapana budi awe wajibu wa uwepo. Asiyehitaji uwepo wa mwingine aliyemleta, au mwenye kuhifadhi uwepo wake, Mungu huyu anapasa kusifika kwa sifa zote za uzuri Muumba huyu ni Allah mwanzilishi wa kila kitu.”

Hivyo basi mwisho wa kimbilio letu ni kufafanuliwa na kurudi kwetu kwa Allah Ta’ala, kwa maana hiyo maumbile haya hayakuwa ni mchezo (Mwenyezi Mungu Ametukuka dhidi ya kufanya mchezo) bali yalikuwa yenye hekima kubwa, Allah amesema: “Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?” (23:115).

Hiyo basi Allah hakuuumba mwanadamu na majini kwa mchezo, bali amewaumba kwa kumuabudu yeye peke yake tu bila kumshirikisha na yeyote, kumuabudu yeye tu kwa mtazamo mpana kwa kufanya yote ayapendayo Allah Ta’ala na kuridhika katika aliyoyafaradhisha, na swala, na dhikri na kuimarisha ardhi, na kuwanufaisha watu; Allah amesema: “Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” (51:56)

Watu wote wanarejea na kukimbilia kwake tu, pamoja na marejeo yote ni kwake; Allah amesema: “…Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu...” (3:28).

Yakini inaondosha mchezo katika maisha ya watu, na kuwapa maana ya maisha yao, na furaha katika mioyo na roho zao Allah amesema: “Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini. ” (52:35-36)

Mwanadamu anaposhindwa kujua siri ya Ulimwengu huu, na kuanza kufikiria viumbe wa Allah, ardhi, nyota, sayari mbali mbali, mfuatano wa usiku na mchana, uhai na mauti, na yote aliyoyaweka Allah katika Ulimwengu huu…. Mwanadamu akifanya hivyo anafahamu kwa yakini kwa maumbile yake ya asili (fitra) kuwa yupo mtukufu na mkubwa aliyeipata ulimwengu huu ambaye ndie mwenye nguvu zaidi kumshinda yeye, ambaye yeye binadamu anastahiki kunyenyekea kwake, kumuabudu, kutarajia thawabu zake na kuhofia adhabu zake.

$Cardinal_Koenig.jpg*

Cardinal Koenig

Raisi wa Maaskofu wa Austria.
Jibu lenye kutosheleza
“Historia ya dini kwa ujumla, na historia ya Tawhid haswa hutudhihirishia kuwa kumuamini Allah peke yake ni jibu tosha la kipekee la kila swali kuhusu ya Ulimwengu na ubinadamu na lengo la uwepo wao, haiwezekani maisha ya mwanadamu\yakawa na lengo ila Allah peke yake. Na kila ibada na dini kwa mwanadamu lengo lake ni asili ni iwe mtu anajua au hajui –humpelekea katika kumuamini Mungu mmoja.”

Vivyo hivyo tafakuri hii katika hayo humfanya mtu kumkubali Muumba Mtukufu Adhwimu, mwenye uwezo na mwenye hekima, na ya kuwa Maada haikuwa chochote isipokuwa kiumbe miongoni mwa viumbe wake vimetokea baada ya kuwa havikuwepo hapo kabla.

Mola huyu, mwenye hekima, mwenye uwezo ambaye amewajulisha waja wake na nafsi yake, na akawasimamishia alama na ishara za kuwepo kwake na dalili mbali mbali na fafanuzi mbali mbali, ambaye Yeye Allah anajitosha dhidi ya yote hayo (naye mwenyewe amejisifu kwa sifa kamilifu) sifa ambazo zinabainisha na kuthibitisha uwepo wake, Uungu wake, na Uola wake kwa sheria za mbinguni, na umuhimu wa kiakili na maumbile ya asili ya kitabia, na umma mbali mbali zikakubaliana katika hilo.