MIONGONI MWA DALILI ZA UTUME WAKE (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam)

MIONGONI MWA DALILI   ZA UTUME WAKE (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam)

MIONGONI MWA DALILI ZA UTUME WAKE (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam)

Maafikiano yake pamoja na mitume katika dawah ya Tawhidi

$Hans_Kung.jpg*

Hans Kung

Mwanazuoni wa kidini wa Switzerland
Hamkanushi isipokuwa ni Mpingaji
“Muhammad ni Mtume wa kweli kwa maana halisi ya neno. Kamwe hatuwezi kukana kuwa Muhammad ndio kiongozi mwenye kuelekeza kwenye njia ya kuokoka.”

Kuwa amelingania kumuabudu Allah Ta’ala peke yake na kuacha kuabudu wasiokuwa yeye, akiafikiana katika hilo na Mitume wote, na atakayelinganisha baina ya aliyokuja nayo Musa, Issa (‘Alayhi salaam) na yale aliyokuja nayo Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) miongoni mwa akida sahihi na sheria na hukumu mbali mbali na elimu mbali mbali zenye manufaa atajua na kufahamu kuwa yote hayo yanatoka katika kijaruba kimoja nayo ni taa ya utume.

Miujiza

Kuwa alidhihirisha miujiza na alama mbali mbali ambazo hazidhihirishwi ila na Mitume ya Allah; kwani Sunnah ya Allah Ta’ala imepita katika mikono ya Manabii waliopita imevunja ada (mazoea) ili iwe ni miujiza kwao, na dalili ya ukweli wao, na nia ya kusimamisha hoja kwa kaumu yao, na miujiza ya kila Mitume ilikuja kwa jinsi ambayo kaumu ya mtume yule ilivyopiga maendeleo katika jambo fulani. Hivyo basi muujiza wa Musa (‘Alayhi salaam) ukanasibiana na jinsi kaumu yake ilivyopiga hatua katika fani maalumu; nayo ni fani ya uchawi, Allah kwa miujiza aliompa Musa akabatilisha uchawi wao, na wakashindwa kushindana na Musa katika hilo pamoja na werevu mkubwa na uhodari wa hali ya juu waliokuwa nao katika aina mbalimbali za uchawi. Kaumu ya Issa (‘Alahyi Salaam) waliiga maendeleo makubwa katika fani ya utabibu na madawa, Allah akawaponya katika mikono ya Issa (‘Alahyi Salaam) katika maradhi yaliyoshindikana kutibiwa kiasi cha kuwa Allah akawafufua wafu katika mikono ya Issa (‘Alahyi Salaam).

Miujiza yote hii ilikuwa ni ya kihisia (yaani yenye kuonekana), imefungamana na mahali na zama maalum, haina sifa ya kilimwengu na kudumu, miongoni mwa miujiza ya Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) ni kama miujiza ile ya kihisia; miongoni mwa miujiza hiyo ni:

$Deborah_Potter.jpg*

Deborah Potter

Mwandishi wa Kimarekani
Maneno ya Mwenyezi Mungu.
Nilipomaliza kusoma Qur-aan nikajawa na hisia kuwa hii ndio haki ambayo inakusanya majibu toshelevu kuhusu maumbile na mengineyo. Kadhalika hutupa matukio kwa njia ya mantiki ambayo tunaona yakigongana na vitabu vingine vya dini. Ama Qur-aan inayazungumzia kwa njia nzuri yenye kupendeza ambayo haiachi fursa ya mtu kutia shaka kuwa huu ndio ukweli, na ya kuwa maneno haya bila ya shaka ni ya Mwenyezi Mungu.

-Kububujika maji kutoka katika vidole vya Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam).

-Chakula kidogo kukifanya kingi kiasi cha kula yeye pamoja na Waislamu wengine walio nae, na kubakia.

-Kufanya maji kuwa mengi kiasi cha kunywa jeshi zima na kutawadha.

-Gogo kumlilia alipoacha kulitumia katika mimbari.

-Jiwe kumsalimu alipokuwa Makkah.

-Mti kumnyenyekea yeye.

-Changarawe kusabahi katika kiganja chake.

Kuponya magonjwa kwa uwezo wa Allah, na mengineyo,

Qur-aan imerikodi moja katika miujuza ile muujiza wa Israa na Miiraji; Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) alipopelekwa Israa kutoka msikiti wa Masjid Al-Haram Makkah kuelekea Al-Masjidil Aqswaa, kisha akapaishwa Mii’raj kutoka katika msikiti wa Aqswa hadi mbingu ya saba, Allah Ta’ala amesema: “SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” (17:1).

$NassrySalhab.jpg*

Nassry Salhab

Mwanafasihi wa Kilebanoni.
Hazifanani.
“Hakuna mfano wa Uislamu, dini ambayo imetukuza Manabii na Mitume ambao walikuja kabla ya Mtume Mwarabu. Dini hii imewataka waumini wake kuwatukuza watu hawa na kuwaamini. Hakuna dini iliyo sawa na Uislamu katika kuheshimu dini zingine zilizoteremka ambazo zilitangulia katika kuteremka na Wahyi.”

Vivyo hivyo muujiza wa kupasuka kwa mwezi; ambapo Allah Ta’ala amesema: “Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!” (54:1),

Na hii ilitokea wakati Makafiri walipomtaka Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) athibitishe ukweli wake kwa muujiza uliokuwa wazi kabisa, na wakaainisha wazi awapasulie mwezi, na kuahidi kuwa baada ya hapo wataamini, siku hiyo ya tukio ilikuwa ni siku ya mwezi kamili (Badri), yaani: usiku wa siku ya kumi na nne ya mwezi; ambao mwezi unakuwa kwa ukamilifu wake na kwa uwazi zaidi..

Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) akamuomba Mola wake ampe walichokiomba; mwezi ukapasuka mara mbili: nusu ikawa juu ya mlima wa Saffa na nusu nyingine juu ya Jabali Qayqu’aan inayoelekeana nayo, baada ya kupatikana kwa muujiza huu mkubwa washirikina wa Kikureishi hawakuamini, bali waliuzingatia kuwa ni uchawi, na huu ndio mwendo wa wapingaji wa dini ya Allah.

$Blasher.jpg*

Régis Blachère

Mustashrik wa Kifaransa.
Kwa Ulimi Bainifu wa Kiarabu
“Aya ambazo Muhammad amerudia kuzitaja katika sura hizi tukufu zimeacha mbali nyuma yake kauli za wanadamu fasaha zaidi kama ambavyo inawezekana kuzileta kupitia maandiko yaliyowekwa ambayo yametufikia.”

Ni kawaida ya wapingaji pindi haki inapobomoa utawala wao na nuru ya Allah inapofunika upotofu wao, hapo hufanya vitimbi na kusimama mbele yake, ima kwa kupotosha misingi yake au kugeuza hakika zenyewe, kwa dhana ya kuwa hayo yatatosha kumaliza na kuangamiza ukweli wenyewe, Allah amesema: “Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea. Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.” (68:2-3).

Miujiza ya Qur-an itabakia hadi siku ya kiama

Qur-aan: Ni muujiza mkubwa zaidi, ni wenye kubaki katika karne zote na dahari, nao ni muujiza wa kimaana na kiakili na alama miongoni mwa alama za utume; kwa sababu ni kitabu fasaha zaidi, Allah amemteremshia (Mtume) Ummiyyi (asiyesoma yaliyoandikwa), ikawa ni changamoto kwa watu wenye ufasaha zaidi walete sura moja mfano wa Qur-aan.

Muujiza uliopo kwenye Qur-aan na changamoto yake na hakuna yoyote mwenye kukanusha hayo isipokuwa mwenye kiburi.

Kwa hiyo inashinda kwa ufasaha wake, balagha yake, umbuji, utaratibu na mpangilio wake, na yaliyomo ndani yake miongoni mwa habari zilizopita na zinazokuja, kadhalika sheria na hukumu mbali mbali na maadili ya juu zaidi uongofu, nuru na baraka.

$Maurice_Bucaille.jpg*

Maurice Bucaille

Qur-aan na Sayansi bega kwa bega.
“Nilifanya utafiti kuhusu Qur-aan Tukufu bila ya kuwa na fikra yake yoyote hapo kabla, na bila upendeleo. Lengo ni kutafuta kiwango cha maafikiano kati ya Qur-aan na kinachopatikana katikaelimu leo hii. Nilichokipata ni kuwa Qur-aan haina aya au andiko linaloweza kukosolewa kwa upande wa elimu katika zama hizi.”

Kama ambavyo miujiza ya kisayansi inayovumbuliwa kila siku inakubaliana na habari za wahyi madamu ni hakika za kisayansi ulimwenguni, ambazo hazikuwa zikifahamika hapo kabla zote hizo ni uthibitisho bayana wa ukweli wa utume wa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam), kama ambavyo sayansi leo hii ilivyovumbua hatua mbali mbali (tofauti) anazopitia kichanga anapokuwa tumboni kwa mama yake na kuwepo kwa kizuizi cha maji baina ya maji tamu na maji chumvi baharini na mifano mingine kama hiyo.

Hata hivyo uthibitisho mkubwa zaidi za kuwa kwake kutoka kwa Allah ni kubakia kwake ikiwa imehifadhiwa zaidi ya karne kumi na nne bila ya kupotoshwa, au kubadilishwa, wala hachoki msomaji wake hata akikariri mara nyingi kwa kuisoma, Allah amesema: “Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.” (15:9).

Bali Qur-aan yenyewe imehifadhi akida (itikadi) sahihi ikiwa na sheria kamili ndani yake, na ikasimamisha Umma bora kabisa, hapa inatudhihirikia sisi kuwa muujiza wa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) umekuwa bora tofauti na miujiza ya ndugu zake manabii na Mitume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) waliotangulia kwa kulinganisha ukubwa wa miujiza ile, pia miujiza ya Mtume Muhammad ni ya watu wote ulimwenguni na wa zama zote na ni muujiza utakao dumu milele.

Changamoto inaendelea kusimama dhidi ya wote wataendelea kushindwa kuleta mfano wa Qur-aan hii, Allah amesema: “Sema: Wangeli kusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur’ani basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao.” (17:88).

Kujulishwa habari zilizopita na zijazo

$Fisay.jpg*

F. Motague

Mwanafikra na Mvumbuzi wa Kifaransa.
Hayo ni Maneno ya Mwenyezi Mungu.
“Mimi sina shaka japo mara moja katika ujumbe wa Muhammad na ninaamini kuwa yeye ni Mtume wa mwisho. Ametumwa kwa watu wote na ujumbe wake umekuja kuhitimisha Wahyi uliokuja katika Torati na Injili. Dalili nzuri kabisa katika hilo ni Qur-aan yenye miujiza. Mimi napinga fikra za Pascal mwanazuoni wa Ulaya mwenye chuki kubwa ya Uislamu na Waislamu isipokuwa fikra moja tu: nayo ni kauli yake: Qur-aan sio katika utunzi wa Muhammad kama ambavyo sio katika utunzi wa Mathayo.”

Kuwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) alitabiri matukio mbalimbali ulimwenguni na yalitokea kama alivyosema; kama vile Fathi (ufunguzi) ya Shaam, Iraq na Constantinople (uturuki). Hali kadhalika ameelezea kuhusu Ummah mbali mbali zilizopita na hali zao pamoja na manabii na mitume wao, kuanzia Adam (‘Alayhi salaam), Nuuh, Ibrahim, Musa na Issa (‘Alayhi salaam), kama ambavyo alitabiri matukio ya siku za usoni; na yakatokea kama alivyotabiri na miongoni mwa hayo ni pale Wafursi walipowashinda Warumi, Allah akaeleza kuwa baada ya miaka michache Warumi watawashinda Wafursi, Allah amesema: “Alif Lam Mim (A.L.M.) Warumi wameshindwa, Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini watu wengi hawajui. Wanajua hali ya dhaahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera.” (30:1-7),

Na tukio hilo likatokea kama alivyolielezea Allah (Subhaanahu wa Ta’ala).

Bishara ya mtume kwake na mwisho wa utume

Manabii (‘Alayhi salaam) wametabiri kuja kwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) kabla ya kuja kwake kwa dahari nyingi wakatoa wasifu wa kutumwa kwake, mji na umma na mataifa mbali mbali na wafalme kumnyenyekea yeye na umma wake na wakataja kuenea kwa dini yake.

Kuwa yeye ni mwisho wa Mitume, na kama asingetumwa basi utabiri wao ungekuwa batili.

Ushuhuda wa Ahlul Kitaab na ukweli wake

$Aldo_Mieli.jpg*

Aldo Mieli

Mustashrik wa Kifaransa.
Ni tengenezo la Mwenyezi Mungu.
“Katika zama ambazo nchi nyingi zilianguka, nchi ambazo hapo kabla zilikuwa sehemu ya utawala wa –Ufalme wa kale wa Diocletian. Ghafla katika moyo wa majangwa ya Arabia aliibuka mtesi (utesi). Ufalme ule uliochoka ukawa unafuatilia mtesi Yule kama kwamba ni ufalme mpya ambao ulikuwa unaibukia Magharibi. Uadui huu ulikuwa unapanuka siku hadi siku machoni mwa watu. Na ulinzi wa Mwenyezi Mungu ndio ambao daima ulikuwa ukiwaongoza askari wale wakweli na waaminifu kuelekea kwenye jihadi na ushindi mkubwa. Ushindi ule ulipelekea kufunguliwa kwa Syria na Misri, na baada ya hapo ufalme wa Wasasani wakaingia katika mazungumzo na Wakonstantini wakitishiwa na muelekeo ule (wa ushindi wa Waislamu).”

Ukweli wa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na kuthibiti jambo lake katika Taurati na Injili, na baadhi ya watu katika Ahlul kitabu wakati wa kutumwa kwake ambao kasumba haikuwapofusha (kufanya hivyo); kama vile mtawa Bahira, bwana Waraqa bin Nawfal, sahaba Salman Al-Faarisy, aliyekuwa mwanazuoni wa kiyahudi kabla hajasilimu Abdallah bin Salaam na Zaid bin Sa’atah.

Nusura ya Allah kwake na sifa na maadili yake

Ushindi wake kwa Ummah mbali mbali aliopigana nao ni dalili na alama miongoni mwa alama za utume wake; kwani ni muhali kwa mtu kujidai kuwa ametumwa na Mwenyezi Mungu (nae ni muongo) kisha baada ya hapo Allah ampe ushindi na kumuwezesha kuwashinda maadui, da’wah yake kuenea na kuongezeka kwa wafuasi wake, hilo halitokei ila katika mikono ya Mtume Mkweli.

Ibada yake Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam), ukweli wake, historia yake nzuri, mwendo wake, sheria yake na tabia yake njema, kwani aliyemtengeneza katika adabu hizo ni Mola wake: “Na hakika wewe una tabia tukufu.” (68:4),

Kwani sifa hizi tukufu hazikusanyiki isipokuwa kwa Nabii wa kweli.

Tawatur iliyonakiliwa uthibitisho wake na miujiza yake na kutojua kwake kusoma yaliyoandikwa

Njia ya upokeaji wa habari ya Tawaatur ambayo utume wa Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) umenukuliwa pamoja na miujiza yake, mwenye kuangalia kwa makini hali za manabii mbali mbali na kusoma historia zao; atafahamu ufahamu wa yakini kuwa hakuna njia iliyothibitisha utume wa Nabii yoyote ila njia hiyo vile vile imethibitisha utume wa Nabii Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam).

Ukiangalia namna utume wa Musa na Issa (‘Alayhima salaam) ulivyonukuliwa, utafahamu kuwa imenukuliwa kwa njia ya Tawaatur, na ndio Tawaatur iliyonukuu utume wa Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) ni tukufu zaidi na yenye kuaminiwa zaidi, kadhalika Tawaatur iliyotumika kunukuu miujiza na alama mbali mbali ni zenye kufanana, bali ya Muhammad ni kubwa zaidi na ni zama za karibuni zaidi; kwa sababu miujiza yake ilikuwa ni mingi zaidi, bali muujiza ulio mkubwa zaidi ni hii Qur-aan ambayo inaendelea kunukuliwa na kupokewa kwa njia za tawaatur kwa njia ya sauti na maandiko.

Kutosoma kwake kilichoandikwa na kutoandika kwake ni dalili ya miujiza yake, Allah alimtumia Mtume wake Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) akiwa hasomi na kuandika na huu ni uthibitisho kuwa Qur-aan tukufu imeshushwa kwake na Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na ni dalili kubwa sana na haswa kwa kuwa yeye ameishi pamoja na watu wake miaka mingi sana na lau angekuwa anajua kusoma yaliyoandikwa washirikina wangedai kuwa alichokuja nacho ni katika uvumbuzi wake na katika fikra zake. Allah amesema: “Na namna hivi tumekuteremshia Kitabu (cha Qur’ani). Basi wale tulio wapa Kitabu (cha Biblia) wataiamini (Qur’ani), na miongoni mwa hawa (washirikina) wapo watakao iamini. Na hawazikatai Ishara zetu isipo kuwa makafiri. Na wewe hukuwa kabla yake unasoma kitabu chochote, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kulia. Ingeli kuwa hivyo wangeli fanya shaka wavunjifu.”(29:47-48), Kama inavyothibitisha kuwa aliyokuja nayo Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) ni kutoka kwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na sio kutoka kwake mwenyewe (yeye Muhammad), Allah amesema: “Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.” (62:2)

$Thomas_Carlyle.jpg*

Thomas Carlyle

Mwandishi na Mwanahistoria wa Scotland.
Tabia za Utume.
“Kwa hakika mimi nampenda Muhammad: Sababu ni ile tabia yake safi aliyonayo na mawazo na fikra zake. Kwa hakika mtoto huyu wa majangwani alikuwa ni mwanamme mwenye rai huru: Hujitegemea mwenyewe tu wala hajidai yasiyokuwepo, hakuwa mwenye kiburi!! Hata hivyo hakuwa dhalili, akisimama na nguo zake zenye viraka kama vile alivyompatia Mola wake na kama alivyotaka mwenyewe. Huzungumza na wafalme wa Kirumi na wa Kiajemi kwa maneno yake yenye kutetemesha anawaelekeza maisha haya na maisha ya akhera. Alikuwa anajua uwezo wa Nafsi yake, alikuwa ni mtu mwenye kupitisha azma yake, hacheleweshi kazi ya leo hadi kesho.”

Katika wasifu wa Mtume Umiyyi ambaye anawasomea wasiojua kusoma aya za Allah, yaani Wahyi wake, na kuwatakasa na kuwafundisha kitabu, yaani anawakaririsha hicho, kama ambavyo Mitume walivyokuwa wanawatamkisha Ummah kitabu kwa kuandika na kuwaelimisha hekima ambayo Mitume iliyotangulia imefundisha Ummah zao. Katika wasifu wote huu kuna changamoto kwa muujiza wa Ummiyyi (kutosoma yaliyoandikwa) katika Mtume huyu (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam), pamoja na kuwa kwake Ummiyyi ameletea Ummah wake faida nyingi ambayo Mitume iliyosoma imewapelekea Ummah zao, hakuna upungufu wowote, hivyo Ummiyyi wenyewe umeibuka kuwa ni muujiza umempatisha sahibu yake yaliyo bora zaidi kuliko waliyoyapa mitume wenye kuandika kama vile Musa (‘Alayhi salaam).