UJUMBE UNAOBAKIA

UJUMBE UNAOBAKIA

UJUMBE UNAOBAKIA

Upotofu wa dini za mbinguni

Kila mwanadamu anapokuwa mbali na uongofu wa mbinguni na ujumbe wa Mitume basi watu hao watagubikwa na kiza, ndio maana akawa anatuma Mtume baada ya Mtume: “Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (4:165);

Hivyo basi Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) hamuadhibu yoyote ambaye hajamtumia Mtume: “…Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume.” (17:15),

Na baada ya kutumwa kwa Issa (‘Alayhi salaam), kisha Allah akamnyanyua jamii mbali mbali ya wanadamu zilisumbuka kwa Ujahilia na upotevu, dhuluma na kiza; hivyo dini za Allah zilikumbwa na mabadiliko ya kuchafuliwa mafundisho yake na baadhi ya waovu wakabadilisha akida yake safi ya tawhidi kwa upagani na ushirikina, na kumfanyia Allah jeuri na kusema juu yake bila ya haki, na kwenda kinyume, na dhati yake, wakati huo hakukuwepo na tofauti yeyote baina ya wapagani na Ahlul Kitabu pamoja na waabudu masanamu katika ibada zao na maisha yao.

Nuru ya tawhidi ikawa imepotea katikati ya msongamano huu mkubwa wa ushirikina na upingaji na kubadilisha na kugeuza maneno ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), wale waliopewa kitabu wakatupa ahadi na makubaliano (agano), mikataba na maneno ya Allah nyuma ya migongo yao, na hawakuyajali wakaficha haki na kudhihirisha batili, na wakafanya ujasiri katika maharamisho ya Allah, kwa dharau haki za Allah na haki za viumbe, na wakanunua kwa hilo (kuficha kwao) thamani ndogo kwa baadhi tu ya vyeo na mali chache, kama ilivyotokea kwa viongozi wao wenye kufuata matamanio yao, wenye kutanguliza matamanio yao kuliko haki, hivyo basi vita vikaenea na udikteta ukadhihiri, wanadamu wakaishi maisha ya kiza juu ya kiza.

$George_Sarton.jpg*

George Sarton

Mhadhiri katika Vyuo Vikuu vya Washington na Havard.
Tukio tukufu.
“Tukio moja tu ni miongoni mwa matukio yenye faida zaidi katika historia ya mwanadamu nalo si jingine bali ni kudhihiri kwa Uislamu.”

Nyoyo zikapata kiza cha ukafiri na ujinga kutokana na hayo. Tabia zikachafuka, maadili, heshima za watu zikaharibiwa na haki mbali mbali ufisadi ukadhihiri katika nchi kavu na baharini, kiasi cha kuwa lau mtu akiangalia kwa akili yenye kufahamu ataona kuwa wanadamu (wakati ule) walikuwa katika hali ya mauti (Sakarati ya Mauti) na kuwa mwisho wao umekaribia, Allah hakuwataka kuleta maslahi makubwa ya utume ambayo itaondoa tatizo lililopo na kuwapelekea watu katika uongofu ili imuongoze mwanadamu njia yake na kumuongoza katika njia ya sawa…

Muokozi wa wanadamu

Hivyo basi Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) katikati ya janga hili lenye kiza katika maisha ya mwanadamu, Allah alimchagua Mtume wake Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) ili awe:

Na akamtuma pamoja naye nuru inayoongoza ambayo inamuokoa mwanadamu dhidi ya upotofu na mashaka yake, hadi Allah alipokamilisha dini hii kwa wanadamu na akatimiza neema yake kwa ukamilifu wake, na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) akafanya jihadi ili aweze kufikia kwenye haki kwa walimwengu wote: “Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote” (21:107),

$Lothrop_Stoddard.jpg*

Lothrop Stoddard

Mwandishi wa Kimarekani
Habari ya Ajabu Zaidi.
“Habari ya kuibuka kwa Uislamu lilikaribia kuwa habari ya ajabu zaidi ambayo historia ya mwanadamu imeandika, kudhihiri kwa Uislamu katika Ummah ambao kabla ya wakati huo ulikuwa hauna utulivu na nchi ilikuwa imeparaganyika. Haikupita muda wa miongo kumi ya kudhihiri kwake Uislamu ulikuwa umeshasambaa nusu ya Ulimwengu ikivunja falme kubwa na kuzitupilia mbali, na kubomoa dini za kale ambazo zimepita zama na vizazi, na hivyo kubadilisha nafsi za umma nyingi na kujenga Ulimwengu mpya wenye nguzo imara nayo ni Ulimwengu wa Uislamu.”

Kiasi cha kuonja njia ya furaha, nae (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) katika jihadi yake yote hakuwa anataka chochote katika starehe za dunia, wala hakutaka ujira kwa watu, Allah amesema: “Sema (Ewe Mtume):Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu.” (38:86),

Bali Mola wake alimpa khiyari baina ya kuwa Mtume kwa sura ya malaika au Mtume kwa sura ya mwanadamu, Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) akachagua kuwa mja Rasuli. Ikawa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) ni mwanadamu anayeishi kama wanadamu wengine, anasikia njaa kama wanavyosikia maswahaba zake, anaumia na kupata majeraha kama wanavyojeruhiwa, na kufanyakazi pamoja nao, na anajifakharisha kuwa ni mja wa Allah, hivyo Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) anapotaka kumkirimu humsifu kwa uja, “Allah amesema: “Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo.” (18:1),

$Lamartine.jpg*

Lamartine

Mshairi wa Kifaransa.
Rehema kwa Walimwengu.
“Maisha ya mfano wa Muhammad. Na nguvu kama nguvu za kuchunguza na kufikiri kwake mambo, jihadi yake, na msimamo wake wa kuondosha upotofu uliokuwa katika Ummah wake na ujahilia wa watu wake na ukali wake wa kupambana na washirikina kunyanyua neno la Mola wake na kufungamana na ujasiri wake katika kuthibitisha nguzo za dini ya Kiislamu. Yote hayo ni dalili kuwa hakukusudia udanganyifu au kuishi katika batili; alikuwa ni mwanafalsafa, khatibu, Mtume, mweka sheria, mwenye kumuongoza binadamu kwenye akili, mwanzilishi wa dini isiyokuwa na udanganyifu. Yeye ni muanzilishi dola ishirini ulimwenguni, na mfunguzi wa nchi ya Kiroho mbinguni. Ni nani aliyepata ukubwa wa Uislamu kama alivyopata yeye!!

Bali alikuwa akitahadharisha watu kuvuka mipaka na kutoa zaidi ya haki yake, amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam): “Msinikweze kama Wakristo walivyomkweza Ibn Maryam, bali mimi ni mja, basi semeni mja wa Allah na Mtume wake.” (Bukhari).

Na kila mwenye kumuona na akamjua atajua ukweli wake na akasoma sira yake atashangazwa na tabia yake (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam), kwa nini isiwe hivyo wakati maadui zake walimshuhudia kabla ya marafiki, na makafiri kabla ya Waislamu! Inatosha uthibitisho wa Mola wake aliposema: “Na hakika wewe una tabia tukufu.” (68:4),

$Michael_Hart.jpg*

Michael Hart

Mwandishi wa Kimarekani.
Katika wakuu wa watu (Miongoni mwa watu mashuhuri).
“Muhammad alikuwa ni mtu wa pekee katika historia aliyefanikiwa kwa njia bora zaidi katika viwango vyote vya kidini na kidunia. Kwa hakika mkusanyiko (muunganiko) huu wa pekee ambao hauna mfano kwa ajili ya taathiri ya kidini na kidunia pamoja, linamfanya kuwa mtu mwenye haiba tukufu zaidi yenye taathira katika historia ya mwanadamu.”

Bali inatosha kuwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) alimchagua awe mwisho wa Mitume na manabii, na alipomaliza jukumu lake Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) alimfisha, lakini ujumbe wake ukaendelea kubaki hadi Siku ya Malipo.