Maurice Bucaille

quotes:
  • Qur-aan na Sayansi bega kwa bega.
  • “Nilifanya utafiti kuhusu Qur-aan Tukufu bila ya kuwa na fikra yake yoyote hapo kabla, na bila upendeleo. Lengo ni kutafuta kiwango cha maafikiano kati ya Qur-aan na kinachopatikana katikaelimu leo hii. Nilichokipata ni kuwa Qur-aan haina aya au andiko linaloweza kukosolewa kwa upande wa elimu katika zama hizi.”


  • Qur-aan na Sayansi
  • “Qur-aan imekusanya ndani aya bainifu katika elimu ya mazingira (sayansi) zilizotolewa na Pro Yusuf Marwa katika kitabu chake, “Sayansi katika Qur-aan.” Na ikafikia aya mia saba na sabini na nne. Na maelezo yake ni kama ifuatavyo: Hesabu aya sitini na moja, Fizikia aya mia mbili na sitini na nne, atom aya tano, Kemia aya ishirini na tisa, Vipimo vya mwendo aya sitini na mbili. Hali ya hewa aya ishirini, maji aya kumi na nne, elimu ya anga aya kumi na moja, elimu ya wanyama aya kumi na mbili, kilimo aya ishirini na moja, elimu ya viumbe hai aya thelathini na sita, Jiografia aya sabini na tatu, elimu ya nasaba za watu aya kumi, elimu ya tabaka za ardhi aya ishirini na elimu kuhusu ulimwengu na historia ya matukio yake aya thelathini na sita.”