Ujumbe wa Mwisho

Ujumbe wa Mwisho

Ujumbe wa Mwisho

Marafiki watatu walikutana mbele ya lango kuu la mafikio yao kama walivyokubaliana baina yao, Rashidi aliwaongoza katika lile duka alipoona kitabu, “watukufu mia moja….mbora wao ni Muhammad”, pembeni ya nguzo za magazeti alisimama Maiko alikuwa anaangalia orodha: Ghafla alimuita Rashidi.

Rashidi…..Aliangalia maudhui iliyomvutia….ni maudhui kuhusu mjadala wetu leo hii: “Tangazo la kupatikana muswada wa kale wa Qur’an katika moja ya maduka ya vitabu Israil.”

Rashidi: Unakusudia kuniuliza ni vipi muswada huu umefika katika duka la vitabu Israel? Habari hii nimeisoma jana katika moja ya mtandao (website) baadhi ya wachambuzi wanaonyesha na kuashiria kuwa muswada huu uliibiwa Iraq katika vita vya washirika.

Maiko: Hapana, hapana sikusudii hivyo, nakusudia uhusiano na Qur’an ya asili mliyonayo, na uhusiano wa usahihi wa kuthibitisha Qur’an, kwani habari yenyewe inasema kuwa muswada wenyewe umeandikwa yapata kabla ya miaka 1200, yaani miaka 200 tu baada ya kuandikwa nakala ya kwanza ya Qur-an, hiyo ni habari ya kustaajabisha.

Rashidi: Kwanza: Hii sio nakala ya kale zaidi iliyovumbuliwa hadi sasa; Warusi wanasema kuwa nakala ya zamani ya Qur’an ipo katika mikono yao, hilo limethibitishwa na mtafiti wa kirusi, Yufim Ridhwan ya kuwa, X-ray ya carbon aliyofanya Holland imethibitisha kuwa muswada wa Qur’an ambayo ipo kwenye mikono yao inarejea katika karne mbili; karne ya nane na ya tisa.

Wakati ambapo Wamisri wanasema kuwa, nakala ya kale zaidi ya Qur’an imehifadhiwa katika Mash-had Hussein, Cairo, na inakaribia umri wake tangu miaka1400, na ni moja ya misahafu sita ambayo ilitolewa kopi na Khalifa wa tatu ‘Uthman bin Affan (Radhi ya Allah iwe juu yake) ili kuhifadhi Qur’an isipotee.

Huko Yemen nao wanasema kuwa, wamepata nakala ya Qur’an ilihifadhiwa wakati wa kukarabati msikiti mkuu wa Sana’a mwaka 1972, inarejea katika zama za ukhalifa wa kwanza wa Abu Bakr As-Swidiq.

Yote yanaweza kuwa sahihi; kwani nakala ile iliandikwa na kutumwa katika miji mingi.

Pili: Kauli ya kuwa Qur’an kuwepo mikononi mwa Waislamu katika zama za Mtume hii ni kauli iliyotulia kwa wanazuoni wa dini, na inaungwa mkono na wastashirikina, hata hivyo hawakubali kuwa imeteremshwa na Mwenyezi Mungu, wakati ambapo kitabu kitakatifu kwa agano zote mbili hakijathibitishwa asili yake.

Anasema Mustashriki mfafanuzi wa elimu ya Sosiolojia, Ernest Renan: “Qur’an haijapitiwa na upotofu au kubadilishwa.”

Anasema Mmarekani, Dr. Mike Hart, mwandishi wa kitabu ambacho tumekuja kukinunua sasa hivi: “Hakuna katika historia nzima ya ujumbe wa Mitume kitabu kilichobakia kwa herufi zake kamili bila ya kubadilishwa isipokuwa Qur’an ambayo imenukuliwa na Muhammad.” Ama mshairi wa Kijerumani Goethe yeye amefikia kusema: “Qur’an ni kitabu cha vitabu, nami naamini haya kama vile wanavyoamini Waislamu.” Bali alitangaza hadharani alipofikia umri wa miaka sabini, kuwa anaazimia kusherehekea kwa unyenyekevu usiku ule mtukufu ambao Qur’an ilianza kushuka kwa Nabii Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam).

Rajev: Na hii ndio maudhui yetu ya leo; ni kitu gani kinachothibitisha kweli kuwa Qur’an ni Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ya kuwa Uislamu ni dini ya Mwenyezi Mungu iliyoteremka kutoka mbinguni?

Rashidi: Sio kuwa tu ni dini ya Mwenyezi Mungu iliyoshuka, bali dini pekee iliyo sahihi hivi sasa.

Maiko: Hebu tusogee pembeni; ili tusiwakere wenye kuja kutembelea maktaba hii kwa sauti zetu.

Rajev: (Akimwambia Rashidi wakiwa wanaelekea pembeni wakazungumze): Iwe kama usemavyo, lakini kipi kinachothibitisha maneno yako?!

Rashidi: Nitawathibitishia, kwa kadiri muda utakavyoruhusu, kwa hakika Qur’an ni maneno ya Mwenyezi Mungu na sio maneno ya Muhammad, na nitakubainishieni baadhi ya miujiza yake ambayo inadhihirisha elimu pana iliyokusanya inayovuka mipaka ya mwanadamu.

Maiko: Tuambie yenye kutukinaisha na tulichoafikiana, tuambie kuhusu elimu na akili.

Rashidi: Wenye kufuata Kanisa wanakuta kitabu cha dini yao kuwa ni kitabu kitakatifu, na utakatifu unapinga kosa na migongano, kwa mgongano huo na sifa za Mungu wa kweli ambaye anatakiwa kuwa mkamilifu aliyetakasika dhidi ya upungufu; ili astahiki uungu huu..sitozungumzia msimamo wa kanisa kuhusu elimu na vita ambavyo imepigana kati yake na wanasayansi kwa sababu ya maandiko ya kitabu kitakatifu kugongana na elimu, hata hivyo tuangalie katika Qur’an na changamoto yake katika uwanja huu:

Mmoja wa wanazuoni wa Kiislamu katika zama hizi, Sheikh ‘Abdu Majid Az-Zindani pamoja na Profesa Guly Simpson mtaalamu katika magonjwa ya wanawake na mambo ya uzazi katika chuo kikuu cha Northwestern University huko Marekani, kuhusu maandiko ya Qur’an ambayo yanazungumzia hatua za mwanzo za maumbile ya kichanga anapokuwa manii, na namma ambavyo Qur’an inaonesha kuwa mwanadamu huumbwa baada ya kukusanywa kwa manii haya na baada ya hapo ndipo maumbile yanapokuwa, na baada ya hapo ndipo vipengele vya mwanadamu ambaye atazaliwa huanza kujengeka; rangi ya macho mawili, rangi yake ya ngozi, rangi ya nywele…., ambapo maelezo ya sayansi leo hii yamethibitisha kuwa urithi wa mwanadamu unakadiriwa katika hatua ya manii, na hili linaloafikiana na alichosema Mwenyezi Mungu:

“Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? Kwa kitu gani amemuumba? Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.” (Abbasa, 80:17-19). Na baada ya kusikia haya huyu Profesa alisimama katika moja ya mikutano akitoa rai yake kuhusu maudhui haya kwa kusema: “Qur’an imekuja kabla ya karne nyingi ikiunga mkono yale tunayoyaendea; kinachothibitisha kuwa Qur’an ni maneno ya Mungu….”

Niache nifungue laptop ili nisome baadhi ya ushahidi kwa kina….Na tunamuona Profesa Keth Moore mwandishi wa kitabu The Human Developing. Hatua za maumbile ya mwanadamu, nayo nirejea ya kisayansi ulimwenguni iliyofasiriwa katika lugha nane alisimama katika moja ya mikutano na kusema: “Wasifu wa kichanga cha mwanadamu katika Qur’an Tukufu haiyumkiniki kujengwa kwake juu ya maarifa ya elimu ya karne ya saba.”

Matokeo yenye kuingia akilini ni kuwa wasifu huu ulimteremkia Muhammad kama Wahyi; Hayumkiniki yeye kufahamu vipengele hivi; kwani alikuwa hajui kusoma yaliyoandikwa na kwa hiyo hakuwa amepata mafunzo ya kisayansi.” Dr. Keith Moore hakuishia hapo bali aliweka aya za Qur’an na Hadithi za Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) zinazozungumzia elimu ya kichanga (Embryology) katika kila kurasa ya kitabu chake.

Mwingine ni Profesa Yoshidi Kozani–Mkuu wa Anga-Tokyo, anasema: “Sipati ugumu wa kukubali kuwa Qur’an ni maneno ya Mungu; kwa hakika wasifu wa kichanga katika Qur’an haiyumkiniki kuujenga kwa maarifa ya kisayansi ya karne ya saba, tunachoweza kukitoa hapa ni kuwa wasifu huu ni Wahy kwa Muhammad kutoka kwa Mungu….” Je, mnataka nyongeza tena?!

Rajev: Je, ndani ya Qur’an kuna maelezo katika nyanja nyingine?!

Rashidi: Kuna ayah nyingi katika nyanja nyingi–Kwa mfano kuna ayah zinazozungumzia kuhusu hakika za kihistoria ambazo zimethibitishwa na elimu hivi sasa, kwa mfano kisa cha Musa na Firauni, Qur’an imezungumzia kifo cha Firauni na kuzama kwake, na kuokolewa kwa kiwiliwili (maiti) chake ili kiwe mazingatio ya vizazi kuangalia kisa hiki na kukumbuka mazingatio haya, na hilo ni kwa kauli yake Mungu: “Leo, basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa ajili ya walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu.”(Yunus, 10:92) na hapa kuna ishara tatu:

1. Namna alivyokufa Firaun, kwa gharika.

2. Kukiokoa kiwiliwili chake kutoka kwenye maji.

3. Kuhifadhiwa kiwiliwili chake katika sura ambayo inaweza kuonekana na watu (kutiwa dawa maiti).

Na hili haswa ndilo lililothibitishwa na elimu ya zama zetu, lakini kuhusu kiwiliwili (kilichotiwa dawa) hakijavumbuliwa isipokuwa mwaka 1898 C.E. yaani baada ya kifo cha Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kwa miaka elfu moja na mia mbili (1,200), na wakati huo bado haikujulikana sababu ya kifo chake ambacho kilikuwa ni kwa gharika, isipokuwa ni katika mwaka 1981 kupitia vyombo vya utaalamu wa hali ya juu na majaribio magumu yaliyofanywa na kundi la wana sayansi wa Kifaransa wakiongozwa na Profesa Maurice Buccaile ambaye hakujua kabla ya hapo kuwa Qur’an ya Waislamu imethibitisha hivyo, kitu kilichompelekea kutangaza Uislamu wake kisha baada ya hapo akaandika kitabu chake muhimu. “Qur’an, Taurati, Biblia na Sayansi…aliitia vitabu vitakatifu na kuvilinganisha katika elimu za sasa.

Katika Qur’an kuna ayah zenye miujiza mingi katika zaidi ya nyanja moja katika wakati huo huo; katika Surat Ruum Mwenyezi Mungu anasema: “Alif Lam Mim (A.L.M.) Warumi wameshindwa, Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda” (Ruum 30:1-3). Hapa kuna sehemu mbili za muujiza wake; Kwanza: Qur’an inazungumzia kuhusu ushindi wa Warumi kwa Wafursi baada ya kushindwa kwao, yaani baada ya miaka michache: yaani katika muda wa miaka tisa na hili lilitokea kilichoahidiwa na Qur’an Tukufu baada ya miaka saba, ambapo kulitokea vita vingine kati ya Wafursi na Warumi mwaka 627 C.E. ambapo Warumi walishinda.

Sehemu ya pili ya muujiza wa ayah: Imeelezea hali ya kijiografia ambayo haikuwa ikifahamika kwa wakati ule, nayo ni kuwa vita vilipiganwa sehemu ya chini (adna) ya ardhi, na neno chini kwa Kiarabu una maana mbili: sehemu ya karibu zaidi, msemo wa sehemu ya chini, kwa maana hiyo upande mmoja inakusudia sehemu ya karibu zaidi na Bara Arabu na kwa upande wa pili ni sehemu ya chini ya ardhi, yaani ipo chini zaidi ya kina cha bahari kwa futi 1312 yaani mita mia nne, yaani ni sehemu ya chini zaidi ambayo Satellite imesajili katika ardhi kavu, kama ilivyotajwa na encyclopaedia ya Uingireza, ukweli wa kihistoria kuwa vita vimepiganwa sehemu nyingi ardhini zilizo chini katika hodhi ya bahari maiti (Dead Sea) ambayo haikuwezekana kupimwa kwa kukosekana teknolojia ya zama zetu.

Maiko: Nadhani haya yanatosha Rashidi.

Rajev: Ni muhimu mimi kujua, je, Qur’an imezungumzia nyanja zingine kama vile elimu za nyota (astronomy), elimu kuhusu mambo ya ardhi, bahari na mengineyo?

Rashidi: Ndio, katika Qur’an kuna ishara za miujiza katika nyanja hizi na nyinginezo, kama vile mwanzo wa ulimwengu, mwanzo wa mwanadamu, elimu za tiba, elimu za mimea, elimu za wanyama, fizikia, historia na mambo ya hesabu..nyongeza ya miujiza ya Qur’an yenyewe na sheria zake na mengine mengi.

Maiko: Maudhui ambayo yatupasa kuzungumzia ni mengi, lakini kwa bahati mbaya tutamkosa rafiki yetu Rajev; kwani safari yetu ni kesho.

Rajev: Hili linanihuzunisha sana, nimefurahi kufahamiana nanyi na nimefaidika sana na mjadala wenu, tunaweza kuendelea kuwasiliana kupitia njia mbali mbali katika intaneti.

Rashidi: Fikra nzuri, nina fikra nyingine, mnaonaje tukasherehekea mnasaba huu ili tuuhitimishe kwa kumbukumbu nzuri?

Maiko na Rajev: Fikra nzuri.