Uislamu na Ugaidi

Uislamu na Ugaidi

Uislamu na Ugaidi

Katika ahadi iliyoainishwa ya kuanza mazungumzo kwenye chumba cha mazungumzo walipoahidiana kukutana Maiko, Rashidi na Rajev– Maiko alianza kuzungumza baada ya kuwasalimu wenzake.

Maiko: Mimi naona mazungumzo ya Rashidi katika vikao vilivyopita ni maneno yaliyo kinyume na kinachofahamika kuhusu dini yake na kwa hakika tunahitaji kuchuja, Ustadh Rashidi amejitahidi kuonesha maeneo yenye kuvutia katika dini yake, lakini amepuuzia maeneo yenye kiza….Sisi tunaona kwa kutumia macho yetu kuwa ugaidi ambao unatikisa ulimwengu leo ni ugaidi wa Kiislamu.

Rajev: Naafikiana nawe katika sehemu ya mazungumzo yako, lakini ugaidi ni tabia ambayo haifungamani na dini au taifa na hili ndilo ambalo nimelifahamu India, nchini mwangu, ambapo matukio ya matumizi ya nguvu ni ya watu mbali mbali na yana sababu nyingi, Je, ni sababu zipi zinapelekea kuwepo kwa hali hii ambayo tunaweza kuijadili.

Maiko: Hili ndilo nililotaka kueleza, mimi dhana yangu ni kuwa ugaidi upo ndani ya Uislamu wenyewe, na inajulikana wazi kuwa Uislamu umeenea kwa upanga…Je, utapinga hilo bwana Rashidi?

Rashidi: Bila shaka nitalipinga hilo na uhalisia vile vile unalipinga.

Maiko: Ni uhalisia upi unaokusudia?

Rashidi: Hakika za kidini na ukweli wa kihistoria lakini niache niseme kwanza: Inabidi tuziepushe akili zetu na propaganda ambazo kwazo vyombo vya habari na wenye maslahi hukamata akili zetu.

Rajev: Mimi nadhani tunaishi katika jamii huru, na haiwezekani tukafanyiwa imla na shinikizo la kutengeneza akili zetu.

Rashidi: Ni kweli hatushurutishwi na hatulazimishwi, na sisi tu huru kwenye uchaguzi wetu, lakini mwisho wa siku tunachagua tunachopewa na wenye kutawala vyombo vya habari, wanasiasa wenye maslahi wanavyotuelekeza, bado maneno ya wana siasa na wanafikra wa Magharibi yametawala kuhusu ugaidi na kuufungamanisha na Uislamu, na madai ya vita vya wana msalaba chini ya kinachoitwa (kupiga vita ugaidi), na madai kuwa operesheni hii ni ya kulinda ustaarabu wa Magharibi wenye kusifika na kusamehe na kufunguka kama walivyotaja.

Maiko: Nakuahidi kuwa tutabaki kama tulivyokuwa tupe ukweli vyovyote iwavyo chanzo chake na vyovyote iwavyo tabia yake.

Rashidi: Ikiwa Uislamu ni dini ya uadui katika tabia na mazingira yake na kuwa imeenea kwa upanga, na Ukristo ambao wa Magharibi wanadai kuwa unajinasibisha na dini ya upole, Je, rafiki yangu unajua ni mara ngapi Qur’an imetaja neno ‘upanga’, na mara ngapi imetajwa katika kitabu kitakatifu?

Maiko: Sijui haswa, lakini bila shaka kwenye Qur’an imetajwa zaidi kuliko kwenye kitabu kitakatifu (Biblia)?

Rashidi: Haya pokeeni habari hizi zitakushangazeni Qur’an Tukufu ina sura 114, ina aya 6,236 na maneno 77,439. Neno ‘upanga’ au visawe vyake havikutajwa hata mara moja, pamoja na kuwa neno hili lina visawe vinavyofikia 60 katika lugha ya kiarabu, wakati ambapo neno ‘upanga’ limetajwa mara 200 katika kitabu kitukufu (Biblia).

Maiko: Aaah:…kweli ni jambo la kushtua….Je, hili ndilo ulilokusudia kuwa ndio ukweli wa kidini?

Rashidi: Bali huu ni ukweli mmoja tu ambao sitourefusha ili nitoe fursa nitaje mwingine.

Maiko: Ni upi huo ukweli mwingine?

Rashidi: Ukweli huu ni muhimu sana, hapana budi utakuwa unafahamu baadhi yake ewe rafiki yangu Rajev; nao ni kuwa sehemu zenye Waislamu wengi duniani, na kilele cha sehemu hizi ni Asia Mashariki na kusini mwake hakujawahi kufika jeshi la kiislamu hata mara moja na mfano wake vile vile ni sehemu kubwa katika Afrika.

Ukweli huu wa kihistoria unathibitishwa na wanahistoria waadilifu kuwa haujathibitika kwao hali za kulazimishwa kufuata Uislamu katika historia ya Uislamu.

Maiko: Mbali na hayo uliyoyataja ya maneno ya baadhi ya Wanahistoria; ambao na mimi naweza kuleta maneno ya wanahistoria wengine wanaoona kinyume na hivyo; ni kipi kinachothibitisha madai haya?

Rashidi: Kuna zaidi ya dalili zenye kuthibitisha nilichosema:

Kwanza: Sehemu nyingi zilizofunguliwa na Waislamu kijeshi watu wake walibaki katika dini zao za kale chini ya utawala wa Waislamu, na wengine wamebaki katika dini zao hadi sasa, na hili ndilo lililotokea huko Misri, Palestine, Lebanon, Ugiriki na India……kwa mkabala wa sura nyingine kinyume chake pindi Wakristo walio tawala kijeshi huko Andalus (Hispania) Quds, na Ufilipino… kulikuwa na mauaji yaliyoenea (ya halaiki) au kulazimishwa kuingia Ukristo au kuhama, hayo ndio malipo (hisa) ya waliotofautiana nao katika dini.

Pili: Pindi utawala wa kijeshi wa Kiislamu katika nchi ilizozifungua ulipoondoka na kutokuwepo kwa sura yoyote ya shinikizo kutoka kwa Waislamu au wengineo, hatujaona watu au mataifa haya yakiacha Uislamu, bali tumeona watu Waislamu wa Soviet Union hapo kabla wakihifadhi Uislamu wao kwa siri chini ya ukandamizaji wa Ukomunisti wakisubiria fursa ya kuondoka kwa utawala huu kandamizi ili warejee kwa nguvu katika Uislamu wao.

Tatu: Historia inataja visa vya mataifa ambayo yalishambulia nchi za Kiislamu na kushinda nguvu zake za kijeshi na kuteka sehemu zake kubwa zilibadilika na kuufuata Uislamu kama vile Tatari na Waturuki.

Maiko: Nitakubaliana nawe kuwa Uislamu haukusambaa kwa upanga, lakini tuachane na historia, tuzungume hali tuliyonayo hivi sasa. Je, hutokubaliana nami nilichokisema: Kwa hakika ugaidi unaousumbua ulimwengu hivi sasa ni ugaidi wa Kiislamu mia kwa mia?

Rashidi: Tuainishe kwanza: Ni nini maana ya ugaidi? Kisha tuangalie ulimwengu ili tuone ni nani anauongoza ugaidi katika zama hizi, nani anautengeneza?.

Rajev: Dola za ulimwengu wala taasisi zake za kimataifa hazijaafikiana/ hazijakubaliana juu ya maana ya ugaidi, hata hivyo sisi tunaweza kuafikiana juu ya maana yake, “Kuwatisha watu waliokuwa katika hali ya amani kwa sura yoyote ile juu ya kuathiri utashi wao au kupata mapato ya kisiasa au ya kiuchumi kwa upande unaoshambuliwa.”

Rashidi: Bila ya shaka kutokuainisha makusudio haya katika baadhi ya nchi, ili ufahamu uwe kama mpira ambao unaweza kuuchezea, hata hivyo naongezea katika maana yako (taarifa): “Vyovyote awavyo huyu adui (anayeshambulia) ni mtu binafsi kundi au nchi.”

Maiko: Sina tatizo na nyongeza hiyo, na kulijenga hilo: Tukiangalia matukio yanayoendelea ulimwenguni tunaona ulipuaji wa kituo cha biashara huko New York miaka 2001 na yaliyofuatia kama vile ulipuaji wa treni Madrid, Bahi-Indonesia dhidi ya watalii wa nchi za Magharibi na matendo wayafanyayo Wapalestina dhidi ya Mayahudi yote hayo ni matendo ya kigaidi yaliyofanywa na Waislamu.

Rashidi: Kidogo kidogo rafiki yangu, matendo wayafanyayo Wapalestina ni mapambano ya kujilinda dhidi ya waliowakalia kwa mabavu katika historia nyeusi ya ugaidi, je, inawezekana kufumbia macho ukaliaji ardhi ya taifa kamili kuwafukuza na kuwatisha kwa njia mbali mbali, miongoni mwazo ni:-

Mauaji ya Baldat As-Shaykh (al-Shaikh village) yaliyotokea tarehe 31/12/1947, ambapo waliuawa watu 600 wananchi wasio na hatia ndani ya nyumba zao.

Mauaji ya kijiji cha Deir Yassin, yaliyotokea 10/4/1984, ambapo zaidi ya nusu ya wakazi wa kijiji hicho waliuawa.

Mauaji ya Lydda yaliyotokea tarehe 11/7/1948 ambapo wananchi 426 waliokuwa wamekusanyika msikitini waliuawa, Mayahudi walivamia na wakaua waliomo ndani.

Mauaji ya Kafr Qasem yaliyotokea mwezi wa kumi 1965 amapo wananchi 94 waliuawa wakiwemo watoto na wanawake.

Mauaji ya Sabra na Shatila yalitokea tarehe18/9/1982 huko Lebanon na yalifanywa na jambazi la kivita, Ariel Sharon akishirikiana na jeshi la Kikristo la Lebanon ambapo mauaji yaliendelea kwa masaa 72 na kuuawa Wapalestina 3,500 na Mlebanoni mmoja wengi wao wakiwa ni wanawake, watoto na wazee, hawakuwa na kosa lolote zaidi ya kuwa walishambuliwa kwa kuwa ni Waislamu.

Mauaji ya msikiti wa Al-Ibrahimi yaliotokea tarehe 25/4/1994 yaliofanywa na mmoja wa askari wa jeshi la Israel akishirikiana na makundi mengine ya jeshi hili na masetla wa Kiyahudi, katika mauaji haya waliuawa watu 29 waliokuwa wakiswali msikitini na wengine 50 waliokuwa nje, na kujeruhiwa zaidi ya watu 350 waliokuwa wakiswali.

Lakini ili mtazamo wako uwe mpana, nitaongeza matukio mawili tena: Ulipuaji wa jengo la Federal la Oklahoma mwaka 1995 ambapo walikufa watu wapatao 168 na kujeruhiwa watu wengine 500, na mauaji ya Oslo na kisiwa cha Uto ya mwezi wa saba mwaka 2011 ambapo watu 92 walikufa na wengine 90 kujeruhiwa, matukio yaliyofanywa na Wakristo wenye siasa kali wenye kushikilia ugaidi na ubaguzi wa hali ya juu.

Kama ambavyo sisi ikiwa tunafuata uhusiano kati ya dini au ustaarabu fulani na ugaidi hatuwezi kusahau ukweli uliopo katika karne hii sasa:-

Haijawahi kutokea nchi yoyote ya Kiislamu kuvamia nchi ya Ki-Magharibi (yoyote), lakini kinyume chake kabisa historia imeshuhudia kuwa ulimwengu wa kale na ulimwengu mpya umekuwa ni lengo la kushambuliwa na nchi za Magharibi.

Wahindi wa Kimarekani waliuwawa katika mauaji ya Kimbari na waliokuwa wakibeba bendera ya ustaarabu wa Kimagharibi; ili kupunguza idadi yao kutoka milioni 10 kufikia laki mbili (200,000) pamoja na kuwanyang’anya bara lao.

Watu wa Magharibi ndio ambao wamesababisha ulimwengu maafa ya vita viwili vikubwa ambayo vimeitwa (Vita vikuu viwili vya dunia), lakini ukweli wenyewe na haswa vya kwanza (vya Ulaya mbili) ambapo wahanga wake (vya kwanza) ni milioni ishirini na majeruhi na vilema mfano wa idadi hiyo, na vya pili wahanga wake walifikia milioni 55, na majeruhi milioni 53, na wengine milioni 3 hawajulikani walipokuwa, wengi katika wahanga hawa ni watoto katika koloni zao na miongoni mwa raia, kwani kilichokuwa ni katika tabia maarufu ya wapiganaji ni kuwalenga raia wasio na hatia ili kuvunja utashi wa adui.

Kama ambavyo (hata kama tumeafikiana kimsingi uharamu wa kuwafanyia uadui raia wasio na hatia) hatuwezi kupuuzia malengo ya waliofanya matukio haya kwa lengo la kuilinda na kuizuia Marekani na Magharibi na muendelezo wa uadui na ugaidi wa Waislamu, haswa Iraq na msaada wao wa mauaji ya Wazayuni kwa Wapalestina.

Rajev: Kwa hivyo basi, muhtasari wa kauli tunaoweza kutoka nalo ni kuwa: Ugaidi hauna dini wala ustaarabu.

Rashidi: Ninaweza kukubaliana nawe kuwa hauna dini, lakini kuna haja ya kuangalia muelekeo wa ustaarabu wa Kimagharibi ambao umesimama katika msingi wa magomvi na kutukuza nguvu na uhusiano wake na matumizi yao ya kiuadui; hivyo basi ustaarabu huu wa leo wa Kimagharibi msingi wake fikra yake umetegemea na kuathiriwa na urithi (staarabu mbili) wa Kiyunani na Kiroma, na ndani ya staarabu hizo ilikuwa ni maarufu kutoka kwao fikra kama: fundo la kuwa juu, kutukuza nguvu na ulazima wa mgogoro…fikra hizi zimerithiwa na ustaarabu wa kisasa na mamboleo, na mafundisho ya Kikristo haukuweza kuzuia matendo hayo mabaya yenye kutisha na ugaidi ulioenea Ulaya na ulimwenguni kote.

Maiko: Kwaheri tutaonana katika mjadala mwingine.