Tafadhali Niruhusu

Tafadhali Niruhusu

Tafadhali Niruhusu

Kabla ya muda wa kikao chao baina ya marafiki watatu Rashidi alikuwa tayari na kompyuta yake akimsubiri Rajev na Maiko, baada ya muda mdogo walikuja hali ya kuwa wanafuatana, baada ya kusalimiana tu, Rashidi akaanza kuzungumza:

-Katika kikao chetu kilichopita Rajev ulisema kuwa kuna maneno unataka kusema yanayohusiana na baadhi ya tabia za Waislamu kinyume na maudhui ya kutimiza miadi.

Rajev: Naam, kinachoonekana ni kuwa kukosekana kuchunga kwenu misingi ya kuamiliana na wengine haiishi tu katika kutimiza ahadi, bali linaendelea katika nyanja zingine katika fani ya kuishi na watu.

Rashidi: Vipi hilo? Je, umeona kwangu kukosa adabu au kupetuka katika muamala nanyi?

Rajev: Hapana, hapana, samahani, sikukukusudia wewe mwenyewe, lakini hii ni hali halisi inayoonekana kwa sifa ya jumla; kulingana na matembezi yangu katika moja ya hoteli nimeona bango limeandikwa juu yake; “Marufuku kuingia mbwa na Mwarabu!” “Nilipochukizwa na bango lile nilimuuliza mwenye hoteli sababu ya kuandika vile, akaniambia kuwa hoteli yake ni ya kifahari, ni ya hadhi ya juu ambayo wanaingia ndani yake mawaziri na watu wakubwa, na ilitokea wakawapokea vijana wa Kiarabu siku za nyuma, lakini matendo waliyofanya hayakuwa mazuri na yanayowachukiza wateja wa hoteli ile.

Mara moja kundi la vijana wa kiarabu likapangua meza kwa utashi wao na kuwalazimisha wafanyakazi; kilichosababisha fujo na usumbufu hotelini.

Wakati mwingine ugomvi ukazuka miongoni mwao na wakawa wanagombana kwa sauti ya juu kabisa.

Na baadhi yao wakawa wanaosha vidole vyao kwenye sahani katika namna yenye kuchukiza kitendo kilichowaingizia kinyaa watu wengine.

-Bali wengine walikuwa wakijikuna migongo yao kwa umma na kisu.

Na yule mwenye mgahawa akasema kuwa, amepoteza wateja wengi wakubwa kwa sababu ya tabia zao mbaya; akaamua kuweka mpaka wa jambo hili nalo ni kuwakataza Waarabu kuingia katika mgahawa wake.

Rashidi: Mengi uliyoyasema ni sahihi, lakini kama nilivyokuambieni hapo kabla: sisi tumezikosea nafsi zetu kwa matendo yetu na tumewapa wengine fikra mbaya kutuhusu…lakini kwa mara nyingine ninasahihisha kosa hili lisinasibishwe na Uislamu.

Maiko: Huenda kosa hili nalo ukalirejesha katika taathira ya mazingira?!

Rashidi: Bila shaka, siwezi kuacha fikra ya nafasi ya mazingira na malezi mabaya waliyokulia vijana hao.

Maiko: Mimi najua athari za malezi, lakini sifahamu athari za mazingira katika mambo kama haya!

Rashidi: Nitakupatia mfano upate kujua athari yake; Nyie mnaishi katika nchi zenye kufahamika kuwa ni sehemu zenye baridi kali ambapo mvua nyingi hunyesha na barafu kudondoka na kuvuma kwa upepo mkali wenye baridi, na katika hali ya namna hii ya hewa mtu hawezi kuishi bila ya kufanya mahesabu vizuri ya mazingira haya na kuyawekea mbadala wa kukabiliana nayo. Hivyo basi, hapana budi kupanga makazi vizuri, na miundo mbinu katika njia inayochunga mazingira haya, na wakati wa kutekeleza kwake unatakiwa uwe makini, mathalani ni lazima kutengeneza paa na madirisha kwa umakini mno ili maji yasipite na kuingia, hata upepo wa baridi vile vile, hapana budi kuchunga mazingira haya katika kutengeneza na kuweka mfumo wa kupasha joto nyumba unaofaa, na matayarisho ya kuweka mahitaji yote na vifaa ya kupasha joto nyumba… yote yanatengeneza tabia ya kuwa makini na kupangilia vizuri mambo.

Wakati katika nchi zetu hakuna mazingira haya magumu ya hali ya hewa, hivyo mwanadamu hahisi hoja ya tabia hizi ili abakie kuwa hai, na akiacha hivyo aathirike na mazingira yake basi fujo itaenea na itakuwa ndio sifa ya maisha ya watu wake, na usisahau kuwa mazingira yetu ambayo kwa ukubwa wake ni tabia za majangwani na kubeba tabia ya ukavu ambayo huenda ikahamia katika ukavu wa hisia za watu.

Rajev: Kama ni hivyo. Je, tutamuachia mtu huyu awe chini ya utawala wa mazingira yake, bila kurekebisha tabia yake wala kupangilia maisha yake, na aendelee kuishi maisha ya fujo na asiweze kuishi vizuri na watu?

Rashidi: Sivyo hivyo kabisa, nilitaka kuwaambia jambo hili na uchambuzi huu ili kujaribu kuwafahamisha sababu ya kweli ya hayo tuyaonayo.

Rajev: Tukipata tofauti kati ya mataifa ya Ki-magharibi na yale ya Mashariki au ya Kiislamu katika mazingira ya hali ya hewa, tutaona vile vile tofauti katika dini ambayo inatawala; kwa nini basi Uislamu vile vile usiwe ni sababu ya hali hii tunayoiona?!

Rashidi: Uislamu umepanga maisha ya Muislamu na wakati wake; ili ufanye amali yake yote kuwa ibada kwa Allah Mtukuka kwa mtazamo mpana wa ibada ambao nimeshawaelezea hapo kabla; na wengine wanaweza wasifahamu kuwa zile nadharia za kutangamana na watu wengine (Etiquette) nyingi zinathibitisha kuwa fani hii inarejea kwenye dini hii ya Uislamu ambapo zimefika katika nchi za Uhispania kupitia Waislamu, na baada ya kuanguka kwake elimu hii ilichukuliwa na nchi nyingi, miongoni mwazo ni Ufaransa, Hispania, Uingereza na wakaiendeleza na kuongezea vipengele vingine na wakavipanga, hadi ikatufikia sisi kwa sura yake ya sasa.

Maiko: (Huku akicheka) nyie Waislamu mna kasumba sana na dini yenu na mnapenda kunasibisha kila kitu kizuri na dini yenu… sitokuambia unithibitishie hili, kwa kuwa nina jua hilo linahitajia utafiti mwingi mrefu, hata hivyo nitataka unithibitishie kuwa misingi hiyo ipo kwenye Uislamu.

Rashidi: Uislamu umerekebisha tabia ya mtu na maadili yake katika nyanja zote za maisha, na kuna misingi mingi kwenye Qur’an na Sunnah Tukufu ambayo tunaweza kuipanga katika nyanja za fani ya matangamano na watu (Etiquette).

Maiko: Haya ni maneno ya jumla sana rafiki yangu nitolee mfano uthibitishe ukisemacho.

Rashidi: Nitakupigia mfano ili nibainishe maneno yangu; tuangalie muamala wa Mtume (Swala llahu ‘alayhi wasallam) pamoja na mke na watoto:

Tunapomuona mtu akimfungulia mtu mlango wa gari mke wake tunasema kuwa mtu yule amestaarabika, lakini Mtume (Swala LLahu ‘alayhi wasallam) alikuwa anakaa ardhini na anaweka mikono yake na kumtaka mkewe asimame kwa miguu yake na apande ngamia.

Na muamala wa Mtume pamoja na wake zake, watoto wake na wafanyakazi wake ulikuwa wa huruma, uvumilivu na kumsamehe mnyonge. Wakati fulani Mtume (Swala LLahu ‘alayhi wasallam) alikuwa amesujudu katika ardhi, na wakati huo akiwaongoza watu katika swala, akaja mmoja wa wajukuu zake wadogo na kumpandia mgongoni, Mtume hakutingishika hadi alipoteremka mgongoni mwake kwa kumchunga huyu mtoto.

Uislamu umelingania tabia ya kunyenyekea viumbe na upole, na Mtume (Swala LLahu ‘alayhi wasallam) amesifika kwa hilo pamoja na kuwa Muhammad alikuwa ni Mtume mwenye kutukuzwa na wafuasi wake na alikuwa kiongozi wa dola, isipokuwa alikuwa mwenye sifa ya unyenyekevu mno, na miongoni mwa unyenyekevu wake alikuwa akiwasaidia wafanyakazi wake kufua nguo zake mwenyewe, na alikuwa hawabebeshi wafanyakazi wake yale wasiyoyaweza, na anawasaidia wakitaka chochote, pia alikuwa na tabia kama hiyo hata kwa wasio Waislamu, wakati fulani jeneza la Myahudi lilipita na yeye akasimama, waliposhangazwa waliokuwa pembezoni mwake aliwabainishia kuwa heshima ya maiti haitofuatishi kati ya watu.

Bali Uislamu umefungamanisha baina ya mwendo wa mtu na tabia zake, Qur’an imeweka misingi ya tabia njema hata katika kutembea, nayo ni kuwa mtu asinyanyue kichwa chake sana wakati anapotembea na kujikweza mbele za watu, wala asiiname chini kiasi cha kuonekana dhalili Mwenyezi Mungu amesema: {Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna na kujifakhirisha. Na ushike mwendo wa katikati,...}
[31: 18-19].

Rajev: Je, ukionana na yule bwana mwenye mgahawa unaweza kumpa sura hii kuliko ile aliyoiona kwa vijana wale?

Rashidi: Nitakutajia baadhi ya adabu za Kiislamu ambazo zinahusiana na niliyoyataja katika matendo mabaya ya vijana wale na wengineo katika sehemu hii au nyigineyo.

Miongoni mwa maadili haya: Uislamu umeamrisha kutoa salamu kwa wengine, na umetaka hilo lifanyike sana katika jamii, na ukaonesha kuwa ni sababu ya watu kupendana, na kujibu salamu ni jambo la wajibu kidini na sio tu jamii, kama ambavyo Uislamu umekataza kwa mwenye kula ikiwa chakula kipo kinywani kutoa au kujibu salamu, vivyo hivyo kumsalimu aliyeanza kulala na kupunguza sauti kama watu wamelala.

Uislamu umechukizwa na mtu kupaza sauti bila ulazima: {…na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya kuliko zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda} [31:19], umemuita yule mtu anayemuita mwenzie kwa sauti kubwa nje ya nyumba yake kuwa hana akili; {Hakika hao wanao kuita nawe uko nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili} [49:4] Na Mtume (Swala LLahu ‘alayhi wasallam) hakuwahi kumfokea mtu wala kupaza sauti yake.

Uislamu umelingania usafi wa kudumu na kila sehemu: kwenye kikao, kwenye chakula, nyumbani, nje, na kuweka adabu ya kula na kunywa; na wakati huo watu walikuwa bado hawafahamu vifaa vya kulia kama vile vijiko na uma wala hakukuwa na sahani nyingi. Mtume (Swala LLahu ‘alayhi wasallam) amekataza kula kwa kutumia vidole zaidi ya vitatu na amekataza kuzungusha mkono wa mlaji katika sahani, na kumuelekeza mtu kula kilichokuwa karibu nae, na asinywe maji kwa mkupuo mmoja bali mara tatu na kupumua baina yake wala asijaze tumbo lake kwa chakula na kunywa kupita kiasi….na ukachunga mipaka ya kijamii na ya kihisia ambayo yanaweza kutokea wakati wa kula, na hivyo ukafanya suala la kula kuwa ni mlango wa watu kuingiiana na kupendana kati yao, na ukapendelea mazungumzo wakati wa kula pamoja na mgeni wake ili asijihisi mpweke au kuona haya wakati wa kula. Mtume (Swala LLahu ‘alayhi wasallam) alikuwa akimlisha mkewe kwa mikono yake mweyewe, na alikuwa akisema: “Sadaka bora ni tonge analoliweka mtu kwenye mdomo wa mke wake.” Na Mtume alikuwa akinywa sehemu ile aliyoweka mdomo mke wake Aisha (Radhiya Llahu ‘anha) na Uislamu umefungamanisha kati ya kula na ibada kwa Allah, na ukaamrisha kutajwa Allah wakati wa kula na kushukuru baada yake.

Maiko: Niache nikuambie Rashidi, kuna tofauti kubwa kati ya dini yenu na matendo yenu, na sisi tupo karibu ya mafunzo ya dini yenu katika nyanja hii kuliko nyie wenyewe.

Rashidi: Kwa masikitiko makubwa, maneno yako ni sahihi.