Tabia ya Qur’an

Tabia ya Qur’an

Tabia ya Qur’an

Rajev: Alianza kuzungumza akielekeza maneno yake kwa Maiko na Rashidi akisema

Mazungumzo yetu yaliyotangulia kuhusu baadhi ya tabia za Waislamu zinatusukuma kuzungumzia maadili katika Uislamu, je, hamuoni kuwa maudhui haya ni muhimu kuzungumzia?

Maiko: Ndio, mimi ninashangazwa na baadhi ya Waislamu, kwa upande nawaona wakiwa katika kiwango cha juu cha maadili mema, na kwa upande mwingine watu hao hao nawaona wakiwa na maadili ambayo hayalingani na sura ya kwanza.

Rashidi: Hili linarejea katika vipengele viwili: Kwanza: Mtazamo wako kuhusu maadili. Pili, Namna wanaofuata utaratibu na kutekeleza maadili fulani, tabia ya mtu fulani hudhihiri, vile vile athari ya mazingira na malezi kwa uwazi, achilia mbali kipengele cha kurithi kwa dhati ya mtu mwenyewe…hili ndilo aliloashiria mwenyewe Mtume wa Uislamu na kuthibitishwa na majaribio na utafiti wa kielimu na kisayansi.

Rajev: Laiti ukalielezea zaidi

Rashidi: Ishara hii tunaipata kwenye hadithi mbili za Mtume (Swala LLahu ‘alayhi wasallam): Ya kwanza: Mtume anamwambia mmoja wa sahaba zake kwa kauli yake: “Hakika ndani yako kuna tabia mbili azipendazo Mwenyezi Mungu na Mtume wake “uvumilivu na upole.” Yule mfuasi wake akauliza, “ewe Mtume wa Mungu. Je, tabia hizo nimezitengeneza mimi au nimeumbwa nazo?” Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) akasema: “Bali Mwenyezi Mungu kakuumbia nazo?” Katika hadithi hii kuna uthibitisho kuwa uvumilivu na upole, anaweza kusifika nazo mtu kama tu ni vitu alivyoweza kuvirithi, yaani vipo katika jeni yake. Na katika Hadithi nyingine Mtume (Swala LLahu ‘alayhi wasallam) anasema: “Hakika elimu ni kwa kujifunza na uvumilivu ni kwa kuvumilia, mwenye kuchagua kheri atapewa na mwenye kukwepa shari ataiepuka.” Ndani yake kunathibitisha, kuwa yale maumbile ya uvumilivu (kwa yule mfuasi wa Mtume (Swala LLahu ‘alayhi wasallam) ni ya kurithi inaweza kupatikana katika mazingira anayoishi mtu na hii inatokana kupitia malezi ambayo huchangia katika makuzi ya jamii.

Maiko: Hili linatupelekea katika upambanuzi wa kina wa kifalsafa na maelezo mengi, lakini bila kujali matatizo hayo ya kifalsafa, ningependa kwanza kutoa ripoti kuwa hisia za kitabia kwa mwanadamu ni hisia za kimaumbile, anabeba katika kupenda baadhi ya sifa na kuchukizwa na nyingine katika kila zama, kwani ukweli, amana uadilifu na kutekeleza ahadi yote hayo ndio aliyoyahesabu kuwa ndio ubinadamu katika sifa za kimaadili sahihi kwa kusifiwa katika zama zote (nyanja zote), utu haupendelei hadi hivi sasa, uongo, dhuluma, hiana na hadaa, vivyo hivyo hali ya kuliwazana, kuhurumiana, upaji (ukarimu) ukunjufu wa moyo na kusameheana.

Je, tunaweza kusema kuwa Uislamu unatofuatiana katika hilo na watu wote, Je, anaweza yoyote kudai kuwa Uislamu unamiliki mfumo wa kimaadili unaojitegemea uliopambanukana na mifumo mingine?

Rashidi: Pamoja na kuhifadhi mawazo yangu katika kukiri ukweli uliotaja, na madhumuni ya tabia njema na mapungufu ya kimaadili uliyoyataja, na naongeza katika maneno yako: Pamoja na hayo ikaibuka mifumo mingine ya kimaadili, si katika Uislamu tu, bali katika dini zote na mifumo mingine ya kijamii iliyotungwa na mwanadamu; kwani imetofuatiana kuainisha viwango vya uzuri na ubaya katika maadili na njia za kielimu katika kujua kheri na shari, na kwa sababu hazijaafikiana katika nguvu inayofanyakazi nyuma ya kanuni na kudumu juu yake, na sababu ya tofuati hii ni tofauti katika taswira ya ulimwengu huu na nafasi yake katika mfumo wake mpana na lengo la maisha juu yake.

Mathalani: Ubinafsi huchukuliwa ndio msingi wa nadharia nyingi za kimaadili huchukuliwa; katika karne ya mwamko (Renaissance) wa Ulaya Hobes na Spinoza walizungumza kwa nyakati tofauti kuwa hifadhi ya ya kubaki kwa dhati ndipo kheri inapolalia, kama ambavyo Freud kutokana na

maandishi yake ya mwanzo alitoa nadharia ambayo ndio inatengeneza tabia ya Wamagharibi wengi ambayo inatawaliw na mtazamo wa kuiridhia nafsi (self gratification). Mtazamo huu ambao umechukuliwa kuwa ni mtazamo wa msingi ukilinganisha na mitazamo mingine ya nafsi, ambapo uungwana na matendo mema huzingatiwa kuwa ni hali mbili zisizo za msingi zinapata taathira yake kwa kufungamanishwa na picha mbali mbali za kuiridhisha nafsi.

Kwa mkabala wa tabia hizi za mtu mmoja mmoja maadili ambayo yanachukuliwa kutokana na jamii kuwa ni msingi wake, na ndipo zinapojengeka aina za maadili ambayo yanaonesha umuhimu wa kundi kuliko ule wa mtu binafsi.

Maiko: Tukisema kuwa Uislamu una miliki mfumo wa kimaadili uliopambanuka na mwingine, Je ni kwa misingi gani mfumo ule unasimama? Ni nini tabia na sifa zake?

Rashidi: Kama nilivyotaja kwenye mijadala iliyotangulia: Uislamu ni mfumo wa maisha, maisha ya mwanadamu ni ya uhalisia kwa kila nguzo yake; kama ulivyo ni mfumo ambao unajumuisha taswira ile ya kiitikadi na kuipa sura halisi yenye kujiweka kwenye maisha ya mwanadamu; kama vile taratibu za kimaadili na chemchem zitokazo hapo, na msingi ambao zinatokea juu yake, na utawala unaotegemea, na mfumo wa kisiasa, umbo lake na sifa zake, na mfumo wa kijamii na misingi yake ya uchumi, na falsafa yake na maumbo yake na mfumo wa kimataifa na mahusiano yake na mafungamano yake.

Na hili ndilo ambalo Dr. M. H. Durrani aliyekuwa kasisi wa Kanisa la England amelielezea kutokana na uzoefu wa maisha yake, kwa kauli yake:

Uislamu una mfumo wote wa kimaadili, ibada mbali mbali zimefaradhishwa kwa watu wenye malengo ya kimaadili… ina lengo la kumwongoza mtu kimaadili na kiroho kwa njia inayokubalika, kama ambavyo ina lenga kuisafisha akili yake na kuing’arisha, hivyo kuipa nguvu ili iweze kutekeleza majukumu yake kuelekea kwa wengine ambao wanaishi pamoja nawe, kwani Uislamu ni dini pekee kwa kuwa kwake ni nadharia na utekelezaji, mtu hatakiwi kuamini misingi na siri zilizojificha kama ilivyo hali ya dini ya Ukristo, kwani Uislamu unakubali nyanja za maisha ya kiroho na ya kimaada kwa wakati huo huo, na huweka yote katika sehemu yake inayohusika nayo, na husimamisha falsafa yake kwa misingi ya kushughulikia pande zote za tabia za mwanadamu.

Rajev: Tukihesabu kuwa huu ndio msingi ambao msingi wa mfumo wa Kiislamu unausimamia, ni muhimu kutaja sifa za mfumo huu na kitu muhimu kinacho upambanua na mwingine.

Rashidi: Tunaweza kukusanya sifa hizi za mfumo wa kimaadli wa Kiislamu kwa:-

Msingi wa kiakida (Kiitikadi): ambao ni kwamba, mwanadamu ni kiumbe mwenye kulelewa, na ya kuwa Muumba wake hujua zaidi yanayomfaa, na ya kuwa hakumuacha hivi hivi tu, bali amemtumia Mtume wake kufikisha mafundisho yake na wakimfahamisha mfumo wake, na ya kuwa mwanadamu huyu atafufuliwa baada ya mauti katika maisha yajayo ambapo atahesabiwa kwayo kwa aliyotanguliza miongoni mwa mambo ya kheri au ya shari katika maisha yake hapo duniani, na hili ni tofauti na maadili ya kisasa ya kimagharibi ambayo yametengana na dini pamoja na utengano wa elimu na maisha kutoka kwenye kanisa.

Tuli: Maadili ya Kiislamu yanaelezwa na misingi ya maadili thabiti na yanatokana na misingi na taswira thabiti ya mwanadamu na maisha na ulimwengu, nayo inaelekezwa kwa mwanadamu ambae ukweli wake haubadiliki, wala kiini chake kwa miaka mingi, hata kama itabadilika mazingira yanayoizunguka ya maisha na matukio,hivyo ukweli, uaminifu, uvumilivu utabakia kuwa ni matendo mema milele, na uongo, kusengenya, kuteta itabakia kuwa vitendo vibaya dahari yote, na matendo machafu yatabakia vivyo hivyo hayabadiliki hata kama yataenea kwa watu au yakaruhusiwa na baadhi ya mifumo, hata kama tabia na maisha ya watu yatabadilika.

Vya kupigiwa mfano pamoja na hali halisi: Ikiwa baadhi ya watu wanaona kuwa maadili ya Kiislamu ni ya kufikirika, isipokuwa ukweli wake wa kufikirika ni vya uhalisia ambao yanachunga hali halisi ya mwanadamu na nguvu zake, na hivyo kila mtu ana uwezo wa kuitekeleza na kwenda nao pamoja, haya ni maadili ambayo yanahifadhi maisha ya mtu kwa kuzingatia kuwa ni kiumbe kitukufu, na kufanya maisha yake yaendelee bila ya kupambana na vikwazo. Maadili hayagongani na tabia ya mwanadamu wala hayapingani, bali yatakamilika na kuishi pamoja; hivyo basi taswira ya Kiislamu ambayo ndani yake kuna sehemu ya uwekaji sheria ya maisha ambao Uyahudi umeujali sana na kuna upande wa kiroho ambao Ukristo umeuhimiza na hili ameliashiria mwandishi wa Kihindi Peggy Raderik kwa kauli yake:

“Kwa hakika mafundisho ya Uislamu ya kitabia yana hakikisha mchanganyiko timulifu baina ya kufikirika na uhalisia, na hivyo mwanadamu kuweza kwa maadili yake kumjua Mungu, na kuwa mtu wa Mungu wakati ambapo atakuwa ameshughulishwa na mambo ya maisha yake ya kila siku.”

Kujilazimisha (na kudumu katika hili): maana yake, mwanadamu kulinda na kushikamana na maadili haya katika kupambana na wanadamu wote, na hii ni kwa kuwa mwanadamu ni mwenye kuwajibishwa na maisha haya ya dunia, ana ujumbe, na anabeba majukumu, ana utashi ambao unahukumu matendo yake na ndio sababu ya malipo yake, hivyo basi suala la kushikamana na maadili ni alama kubwa ya majukumu ya mtu binafsi.

Majukumu: Haiwezekani mtu mwenye tabia njema bila kuwa na hisia za uwajibikaji, na hapa uwajibikaji una maana ya: mtu kukiri matendo yake, na yupo tayari kuwajibika kwa matokeo yanayotokana na kushikamana kwake na maamuzi yake; yawe ni hasi au chanya, mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya dhamira yake na jamii yake.

Na inahusiana na uwajibikaji (mipaka ya uwajibikaji), nayo katika Uislamu ni majukumu ya mtu binafsi yanayohusika na vyanzo vya maamuzi au matendo, nayo ni majukumu ya kijamii atakaposhiriki katika matendo au maamuzi zaidi ya mtu mmoja kama ambavyo kuna uwajibikaji wa kubadilishana kati ya mtu na jamii yake, lakini kuna kanuni isemayo “Mtu hawajibiki kwa matendo na maamuzi ya mtu mwingine.”

Kukuza uzindushi wa ndani wa nafsi (kilinzi cha ndani ya mtu) pamoja na kufungamanisha maadili mema na mfumo mzima wa kijamii: Mwanadamu ndie anayeupamba ulimwengu wake wa ndani, katika ulimwengu huu huzalika mawaidha ya kweli ya kujilazimisha na maadili, Uislamu umejihusisha na kujenga mawaidha haya kupitia mkazo katika kila hali ndani yake juu ya kile chenye kufahamika kama ni kuleta nia nayo ni kuhudhurisha makusudio ya ndani yaliyoainishwa na matendo mema ambayo mwanadamu anafanya, lakini Uislamu unajua kuwa mwanadamu sio mkamilifu wala aliyehifadhiwa na makosa, na kuwa mwanadamu huyo wakati mwingine anapatwa na muda wa kudhoofika na kuwaathiri walio mzunguka, hivyo basi: Mwanadamu hakuacha dhamira yake ndani yake, bali imemsaidia mtu kufuata misingi ya kimaadili aliyoiainisha kupitia maamuzi yake kwa mkusanyiko wa makosa, na adhabu za kijamii na za kisheria, na za akhera kwa atakayetoka katika misingi hii.

Rajev: Kwa kweli, ni mfumo unaostahiki kuutafakari na kuuheshimu.