Stanley Lane-Poole

quotes:
  • Msikiti…Chuo Kikuu
  • “Ndivyo misikiti ilivyokuwa hapo kabla (hata leo hii baadhi yake) imekuwa ni vyuo vikuu vya Kiislamu: Ni mshangao mkubwa kwa wanafunzi waliojawa na katika elimu. Wanafunzi ambao wamekuja kusikiliza mihadhara ya wanazuoni katika elimu za dini, sheria, falsafa, tiba na hesabu. Na kwa hakika wanazuoni wenyewe wamekuja kutoka pande zote za Ulimwengu ambao walikuwa wakizungumza lugha ya Kiarabu, nao walikuwa wakimkaribisha kila mwanafunzi bila kujali utaifa wake.”


  • Mapenzi ya kuelimika
  • “Haikuwahi kutokea katika Historia ya maendeleo Ulimwenguni harakati yenye kufurahisha kuliko mapenzi ya ghafla ya utamaduni. Kama ilivyotokea katika sehemu zote za ulimwengu wa Kiislamu: Ikawa kila Muislamu kwa khalifa kuwa ni msanii (mtengenezaji) kama kwamba ghafla tu amekumbwa na shauku ya elimu na kiu ya safari (kutafuta elimu). Haya yakawa ni mambo ya kheri Uislamu ulioyaleta kutoka pande zote. Wanafunzi walisongamana katika vituo kama vile Baghdad. Na baada ya hapo katika vituo vingine ambavyo vilikuwa ni mbeleko ya adabu na elimu, mfano wake ni harakati mpya za wanazuoni wa ulaya ambao walifurika katika vyuo vikuu kuchukua elimu mpya. Bali kwa hakika lilikuwa ni jambo zuri.”