KUELEKEA NCHI YA MAKANISA

KUELEKEA NCHI YA MAKANISA

KUELEKEA NCHI YA MAKANISA

(1)

Afya ya Joji ilianza kuwa nzuri na kubadilika kidogo kidogo, na dalili zote za kufanikiwa kwa operesheni zilidhihiri, tokea siku ya pili aliweza kusimama kutoka kitandani mwake baada ya kuondolewa mashine, hata hivyo aliendelea kulishwa, wala hakuanza kupewa chakula…Katarina alikuja na watoto wamjulie hali, walifurahi sana walipomuona katika hali nzuri, akiwa anazungumza nao kwa furaha, na katika hali hiyo ya furaha Joji hakusahau kutuma barua ya kuwajulisha hali yake wale waliomjulia hali yake jana na akawaomba wamuombee dua, kwani huenda sababu ya kufanikiwa operesheni ile imetokana na dua ya mmoja wao..huenda ikawa hivyo!
Joji aliendelea kusoma na kujitayarisha na safari yake ya Roma akiwa na elimu kubwa kuhusu ukristo na madhehebu yake, na alishangazwa kwa nini akazaliwa kuwa ni Mprotestant, ila hajui elimu ya dini yake isipokuwa kidogo sana, mengi anayoyafahamu amejifunza kwa Katarina Mkatoliki, au kutoka kwa Habib ambaye ni Mkatoliki vilevile pindi alipokuwa Yerusalem, au kutokana na kusoma kwake hivi karibuni katika utafiti wake wa ‘Njia ya furaha,’ hakuweza kusoma dini yake hapo kabla, mfano huo ni sawa na wakristu wengi ambao hufuata dini ambayo hawaifahamu, bali utawaona wengi wao mfano wake yeye Joji hawajui zaidi ya jina tu.
Kwa hakika kusoma kuhusu Ukristo ilikuwa ni jambo lenye kusisimua, haswa alichokisoma kuhusu tofauti na mvutano mkubwa uliotokea baina ya madhehebu ya Kikristu: Tofauti kali za kiitikadi, mgongano wa kitabia na wa kiibada na kadhalika mgongano wa kijeshi na wa kivita. Alikuwa akifikiri kwa kina, kwa nini migongano hiyo? Je, Katarina ni mkweli alipomwambia kuwa tatizo lipo kwenye Protestant na sio kwenye Ukatoliki kwa kuwa Ukatoliki ndio uliotangulia, lakini alikumbuka kuwa Orthodoksi ilikuwa kabla ya Ukatoliki katika historia ya Ukristo, na kwa misingi ya ukaribu anaweza kuwa na haki kwa kuwa karibu zaidi na zama za Yesu. Hata hivyo kitabu kitakatifu hakikuandikwa wala kuhifadhiwa wakati wa maisha ya Yesu..hivyo basi ni madhehebu gani yaliyokuwa ni sahihi zaidi? Alitamani sana kuzungumza na mtu, akaamua kuwasiliana na Adam, hivyo akampigia..

Hallo Adam

Aha aha…tunamshukuru Mungu kwa kupona kwako.

Asante Adam, natamani tuonane hivi karibuni.

Nitakuja kwako kesho ikiwa ni sawa kwako?

Vizuri, lakini nina swali; je nimalize vikao vyangu na Tom au hapana?

Naona ukamilishe, lakini kwa nini swali hili? Na kwa nini sasa?

Sijui, wakati mwingine nahisi kuwa hakuna jipya!

Una maana gani kuwa hakuna jipya?

Sijui, ni hisia ngeni tu.

Hata mimi sijui kwanini vile vile, ninachokijua ni kuwa kwa asili ni kuendelea madamu hakutotokea jambo jipya, haswa kwa kuwa ipo wazi kuwa wewe mwenyewe unafaidika sana, kama ambavyo Tom amebadilika na kuwa katika hali nzuri zaidi kama usemavyo.

Umesema kweli, na sijui kwa nini nipo nae katika hali ya utulivu na raha na natengamana nae kama rafiki na sio kama daktari? Kwa ujumla haya ni mawazo yanipitayo, nitampigia nipate miadi nae, hata hivyo ningependa kujadiliana nawe kabla ya kikao hichokama itawezekanahuenda tukazungumza baadhi za kadhia.

Joji alimaliza mazungumzo, na akampigia simu Tom moja kwa moja, akimtaka apate nae kikao kabla ya safari yake ya Roma, na ikiwezekana kikao hicho kifanyike hospitali. Alimkubalia, kwani hakutaka kumchosha.

Basi ni bora iwe kesho kutwa asubuhi, kwani daktari amenijulisha kuwa nitaondoka baada ya siku tatu muda wa jioni.

Kama utakavyo Joji

Katarina alikuja pindi joji akiwa amezongwa na kusoma…alitanabahi kuingia kwake alipokuwa tayari chumbani na kutoa salamu kwa sauti kubwa yenye kushawishi, kisha akakaa pembeni yake akampiga busu shavuni..

Nimefurahi mno, hali yako ni nzuri kama alivyonijulisha daktari.

Naam, mimi nipo katika hali nzuri, vipi habari ya safari ya Roma?

Takriban kila kitu kipo tayari, nafasi ya ndege, ya hoteli na ahadi za kukutana na watu mbali mbali, pamoja na misafara ya kitalii ya pamoja.

Vizuri, unakusudia nini unaposema vikao pamoja na watu mbali mbali?

Ninajua ukitakacho, nimeratibu baadhi ya vikao pamoja na maaskofu na ziara ya Vatican.

Hili silo nilitakalo mimi, bali ulitakalo wewe.

Ndio, mimi nataka, ila sikuiratibu tu hivi hivi ila baada ya kujua kuwa wewe kadhalika unaitaka.

Swadakta, asante sana mpenzi wangu.

Je, utakaa pamoja na daktari Tom kabla ya safari yetu au baada ya safari yetu?

Kabla ya safari, kikao kesho kutwa hapa hospitalini…inaelekea unajali sana kikao?

Swadakta, sijui kwanini nahisi kuwa wewe umeanza kuwa na furaha tokea uwe na vikao vyako na Tom.

Hii tu ndio sababu?!

Naam, hii tu ndio sababu..au ni kwa sababu mimi ninahisia kuwa Tom ameanza kuwa ni bora kuliko hapo kabla, sijui kwa nini?

Nami kadhalika nina hisia hiyo hiyo, lakini nina hofia asiwe ananidanganya.

Yote yanawezekana, lakini mimi naelekea kuona kuwa amebadilika kikweli, pamoja na kuwa yote yanawezekana.

Lakini kama anatudanganya lengo lake ni nini hasa katika hilo?

Sidhani kama ana maslahi katika kutudanganya, hivyo naamini kuwa yeye ni mkweli katika mabadiliko yake.

Nami kadhalika, lau si yule mkuu wa ofisi yake Baraad.

Namchukia mtu yule, sijui kwa nini namuona kuwa ni mtu ambae hakuna mtu anaweza kukaa nae?

Hata Tom anamlalamikia!

Huenda, lakini hili halinikinaishi! Badala ya kumlalamikia, kwa nini asimfukuze na kustarehe nae.

Kweli, huenda kuna sababu nyingine, sijui! Kwa jumla nilikuwa nataka kusimamisha vikao vyangu na Tom.

Sidhani kama ni sawa, hata hivyo uamuzi ni wa kwako.

Rai yako ndio rai ya Adam vile vile, ananiambia: Umeianza njia na inavyotakiwa uikamilishe, na hili limemfanya Tom nae awe katika hali nzuri, na Adam akaendelea kuniambia kuwa umekuwa nae muda wote nae akiwa na tabia mbaya, na leo hii ameanza kubadilika na kuwa katika tabia nzuri unataka kumuacha.

Maneno yenye mantiki kabisa na hoja yenye nguvu.

Kukubaliana kwenu mara kwa mara kunanithibitishia kuwa Adam ni Mkatoliki na sio Mprotestant.

Ha ha ha, au huenda alikuwa ni muongo kwa kuwa Ukatoliki uko karibu kabisa na haki na ukweli kuliko Uprotestant.

Huenda ikawa hivyo, nimekusanya maswali mengi na vilinganishi huenda tukayajadili hayo huko Roma.

Fikra nzuri, kwani tutakuwa katika makao makuu ya Ukatoliki, bali kituo kikuu cha Ukristo duniani.

Huenda ukawa katika kituo kikuu cha Ukatoliki, lakini sio katika kituo kikuu cha Ukristo, kwani sisi hatuamini Upapa wenye mateso.

Usiseme hivi tena, masuala haya tutajadiliana tukiwa Roma kama tulivyokubaliana? Uhisi kuwa unaukosea Ukatoliki? Je, unataka na sisi tukueleze jinsi tunavyoukosoa Uprotestant uliotoroka?

Uliotoroka!! Wasifu mzuri wa Uprotestant! Huoni kuwa sijakasirika kama wewe pamoja na uliyosema!!

Ha ha ha, huenda hivyo kwa sababu unafahamu kuwa huu ndio wasifu sahihi wa Protestant, nyie ndio wale mnaotunga dini yenu mnavyotaka, na mnafahamu kitabu kitakatifu mnavyotaka, na huu ndio ukimbizi ambao ninaukusudia!

Huenda ikawa kama mlivyosema, au ni kwa sababu sisi tupo huru zaidi kuliko udhalimu wa kanisa la Roma na chuki za msamaha wa madhambi.

Tumekubaliana tuyajadili yote tukiwa Roma, je unataka tukatishe mjadala?

Ha ha ha, tumekubaliana, nataka uhakikishe na daktari kama tutahitaji kitu ili tusafiri kwa muda uliopangwa, kwani mimi nimehamasika sana na safari.

Makusudio yako ni kuwa umehamasika kukutana na maaskofu!!

Joji alikaa vizuri kisha akatabasamu na kusema:

Ndio; niwakinaishe mbele yako kwa makosa ya dini yake.

Pamoja na kujua dharau yako, mimi najitahidi sana kuwa kati na kati katika safari hii, Je unaweza kunisaidia mpenzi wangu?

Wewe unajua jinsi gani moyo wangu unavyomili mpenzi wangu, nikikushinda kwenye hoja, wewe unanishinda kwenye mapenzi, amini kuwa nitafanya jitahada kile ninachoweza.

Ninakupenda Joji, nitakwenda sasa hivi kwa daktari kuulizia hali yako pamoja na maudhui yetu ya safari.

Aliporejea Katarina baada ya saa moja alimkuta Joji amezama katika kusoma…

Aakh…je usomacho ni muhimu kiasi hiki?!

Ndio, nasoma kuhusu Martin Luther na John Cavin, wao ndio watu muhimu zaidi wenye athari kubwa katika Uprotestant.

Unakusudia ndio walioandika na kuitengeneza dini ya Uprotestant.

Swadakta kwa kiasi kikubwa, hata hivyo walifanya hivyo; ili wamalizane na maradhi ya Ukatoliki na tabia zake zinazochosha…

Wewe unaamini kuwa Uprotestant umetungwa?!

Kwa bahati mbaya ndio, ili iondokane na wimbi la ukanaji mungu ambalo limelinganiwa na Ukatoliki kwa siri zake na upapa wake, kiasi cha kuwa baadhi ya watu ambao wamekusanya baina ya dini na ujinga na upungufu wa akili! Je unataka tuzungumze hilo sasa hivi?

Ooh..mara moja maudhui yamekuwa kuhusu Ukatoliki, tutajadili tukiwa Roma, na hapo utakinaishwa kuwa Uprotestant ni dini iliyotungwa na upotoshaji wa dini ya Ukristo.

Swadakta, Uprotestant ni upotoshaji wa Ukatoliki, na ndio maana kila mmoja anamuona mwenzake kafiri, na huuwana vile vile…hata vikundi vya Kiprotestant vinakufurishana, je unajua kuna idadi ipi ya makanisa na madhehebu ya Kiprotestant?

Hapana, je zinafika makundi mia moja kwa mfano?

Huenda ikawa hivi, naona habari hii imekufurahisha. Ni kati ya ishirini na nane elfu hadi arubaini elfu katika makanisa na madhehebu.

Madhehebu na makanisa elfu arubaini!!

Joji alioneshwa kuchukizwa na maneno yale, kipaji chake cha uso kilijikunja, na akaamua kukaa vizuri, na akashusha pumzi na kusema:

Kwa bahati mbaya, ndio, na hili linanikumbusha vikundi mbali mbali vya dini zisizo za mbinguni, kama nilivyoona baadhi yake nchini India, na kwa bahati mbaya vile vile kuwa mkweli na nafsi ni ngumu sana!

Je sijakuambia kuwa Uprotestant ni tungo tu! Kisha akatabasamu na kusema: Hata hivyo tutajadili hayo huko Roma kama tulivyokubaliana.

Zaidi ya mara moja unasema uyatakayo, kisha unamalizia kuwa mjadala wetu utaendelea Roma, kisha akatabasamu na kusema: Hamna neno, kwa ajili yako tu, daktari anasema nini?

Nakupenda Joji…daktari anasema afya yako ni nzuri sana, na kuwa operesheni ilifanikiwa kwa asilimia mia moja, na utatoka hivi karibuni tu, inakutosha baada ya kutoka kukaa siku mbili au tatu hivi, kisha uendelee na maisha yako ya kawaida, na unaweza kusafiri bila matatizo yoyote yale.

Je kuna chochote cha kuchukua safarini kwa akiba?

Nimemuuliza hilo amesema: Hapana, hakuna chochote ila nasaha za jumla tu; mfano usijichoshe, au kujihatarisha na jambo, na hili halina uhusiano wowote na operesheni kama alivyosema.

Vizuri.

Itakuwa ni safari nzuri, na tutaijadidi ndoa yetu kama siku zile za mwanzo..

Ni uzuri ulioje wa mwanzo wa ndoa yetu! Tutaijadidi na tutafurahi kwenye safari yetu, lakini kutakuwa na mambo mapya..

Nini kipya?

Kuwepo kwa Maiko na Sali.

Pamoja na kuwa tutalazimika kubadilisha baadhi ya ratiba za safari yetu kwa ajili yao, lakini watazidisha furaha yetu, nawapenda sana.

Najua kuwa mimi nimekuwa na mapungufu kwa haki zao, na nahisi kuwa wamekuwa haraka kwa ghafla.

Tutawafidia wakati unaokuja, au sivyo?

Ndio, na nadhani zawadi bora zaidi ambayo nitawapa ni muongozo wa njia yao ya furaha.

Njia ya furaha kwa mara nyingine!

Na mara ya tatu na mara ya nne, sijui kwa nini nahisi kuwa nimeanza kuikaribia kufika?

Huenda tukaifikia pamoja tukiwa Roma.

Ha ha ha, unakusudia sote tuwe Wakatoliki kwa mara nyingine.

Huenda ikawa hivyo…au isiwe.

Na utauacha Ukatoliki?!

Au huenda wewe ukauacha Uprotestant.

Hebu tujaalie ndio itakavyokuwa, je una uwezo wa kuvumilia kuucha ukatoliki?

Maamuzi yalinichukuwa muda mrefu sana na migongano mingi…hata hivyo sasa hivi naweza kusema ndio, pamoja na kuwa maamuzi ni mazito.

Mimi najifakharisha kwako mpenzi wangu.

Bali mimi ndie nayepaswa kukushukuru Joji, hukuridhia kuishi bila ya kufafanua na kuainisha mipaka, malengo yako, na kuweka maana ya maisha yako, na kujibu maswali yako.

Ha ha ha, hongera kwako ewe Mprotestant.

Ha ha ha, bali hongera kwako kukinai na kurudi katika asili, kwangu Ukatoliki ewe mpingaji, Mprotestant.

(2)

Joji alizama katika kusoma baada ya kuondoka Katarina, na akakamilisha alichokuwa akisoma kuhusu Martin Luther na John Calvin na wengineo, na mabadiliko ya zama za sasa kuhusu Ukristo, wala hakutanabahi na muda hadi aliposikia sauti ya nesi ikisema:

Je una mtihani unaotaka kuufanya baada ya kutoka kwako hospitali?

Ndio, ni mtihani wa maisha yangu.

Katika kiwango gani cha masomo?

Sijui

Inaelekea hutaki kuzungumza, samahani kukatisha masomo yako, nimekuja kuondosha mashine ya kukulishia, na kuanzia kesho utaanza kula katika hali ya kawaida.

Samahani, sijakusudia ulivyofahamu, lakini ukweli nahisi nipo katika mtihani ingawaje sio wa masomo darasani.

Sijui chochote unachosema!

Dini yako ni ipi?

Mimi siamini dini zote, hata hivyo mimi ni Mprotestant..Mkalivini.

Yaani mimi ni katika wafuasi wa John Calvin

Ndio, ingawaje sijui alichokuja nacho kipya? Ninachokifahamu ni kuwa ipo karibu na akili zaidi na ni kongamano la wenye akili na sio kama Luther.

Umejuaje hili na wewe hujui kipya alichokuja nacho?

Mimi ni nesi na sio mtawa, inaelekea ni njia ya kusuluhisha migongano iliyopo kati ya Ukatoliki na Uprotestant.

Je inaingia akilini watu wa dini moja wakagongana?! Na je, inaingia kuja kwa mtu kama Calvin na akarudia upya kutengeneza dini?!

Ndio maana nikakuambia siamini Uprotestant wala Ukatoliki wala dini nyingine, na kama sio haja ya kuwa na dini nisingeamini Uprotestant.

Samahani unakusudia nini kusema haja ya dini?

Siwezi kuishi bila ya dini, maisha bila ya dini ni adhabu na masumbuko, mwanzo nilikuwa mkana Mungu, kisha nikahamia katika usekula, na nilikaribia kujiua kwa dhiki niliyokuwa nikiishi nayo, hata hivyo nilikuwa najua kosa langu ndani ya nafsi yangu, nikaamua kuwa Mprotestant, ambayo bila maelezo yoyote huwezi kufahamu kitu..mazungumzo nawe ni mazuri yenye kufurahisha lakini naomba ruhusa kwani nina kazi.

Je unaridhika na Uprotestant bila maelezo ya kutosha kama ulivyosema? Nadhani unaikimbia nafsi yako, lakini kwenda wapi?

Athari ya maneno yale yalionekana katika uso wa nesi, nae akificha huzuni yake katika moyo wake na roho yake ikiwa tupu:

Huenda ikawa hivyo, katika nisichokijua, mimi ni kama unyoya katika upepo upitao, lakini huenda nikafikia hilo siku moja, kwa heri.

Siku iliyofuata Joji aliamka mapema, alikula kwa hamu pindi alipoletewa istiftahi, alikuwa akihisi njaa kali na hamu kubwa ya kula, kisha akarejea kwenye utafiti wake, Yule nesi wa jana alikuja kumpima joto lake.

Vizuri, upo katika hali nzuri.

Samahani kwa kukukera jana.

Hakuna usumbufu wowote, asante kwa wema wako, nadhani maneno yako yalikuwa kweli uliponiambia kuwa naitoroka nafsi yangu bila lengo lolote. Lakini nifanye nini ikiwa ukanaji mungu na usekula ni adhabu na kuwa na dini ni kutoroka?

Kuwa na dini hakuna maana ya kutoroka, lakini wewe unaikimbia dini yako?

Lakini dini kama unavyosema hutungwa na hutengenezwa, na sio dini kutoka kwa Mungu, huenda akaja ambaye atakuwa ni mwadilifu katika dini ili iwe ni bora zaidi.

Lakini hii ni dini ya mbinguni kutoka kwa Mungu.

Wewe unajua zaidi kuliko mimi kuhusu dini, lakini itakuwaje ni dini ya mbinguni ambayo inabadilishwa na mtu kama Calvin na Luther na wengineo kama watakavyo? Na si hivyo bali Yesu aliuwawa kabla hata agano jipya halijaandikwa, ambayo waliiandika wanafunzi wa wanafunzi wake.

Inaelekea wewe ni mwanafalsafa wa dini mbali mbali!

Bali mimi nimeitoroka nafsi yangu kama ulivyoniambia.

Nini suluhisho kwa muono wako?

Suluhishi ni lile ulilonikosoa, kuikimbia nafsi.

Sidhani kukimbia matatizo kuna suluhisho lake.

Nini suluhisho kwa muono wako?

Tuingie na tufahamu vizuri kuhusu dini kwa uhakika wenyewe.

Ile tuwe maaskofu na watawa?! Na hata wao wana shaka nyingi kuhusu dini zao, na ndio mara kwa mara wanabadilisha dini zao.

Kujua njia haina maana kuwa maaskofu au watawa, mimi ninawaheshimu watawa na maaskofu, wala sitaki kuwa mingoni mwao, lakini shaka siku zote inapelekea tabu na mashaka, kama ilivyo yakini ya jambo hupelekea katika tumaini.

Unaelekea kuwa ni Mkatoliki, kwani wao ndio wanapenda sisi tujisalimishe kwa maaskofu na watawa bila ya mjadala, bali bila hata ya kuangalia na kurejea wenyewe katika kitabu kitakatifu.

Siwezi kuisalimisha akili yangu kwa mtu yeyote yule awe kati yangu na Mungu wangu, mimi ni Mprotestant.

Sasa nini unakosoa wakati wewe ni kama mimi?! Ila kama utakuwa ni Mlutheri

Ha ha ha, kwa kweli sijui ikiwa mimi ni katika wafuasi wa Luther au wa Calvin au mwingine yoyote, ninachokijua kuwa mimi ni Mprotestant, kwa sababu baba yangu na mama yangu walikuwa Waprotestant.

Kama hivyo hatuna tofauti, sasa kwa nini basi unanielezea kuwa mimi naikimbia nafsi yangu?!

Kwa sababu na mimi vile vile naikimbia nafsi yangu.

Unakimbilia wapi?

Kuelekea njia ya furaha.

Ha ha ha, njia hiyo iko wapi ewe mwanafalsafa?

Sijui, lakini nitaipata tu.

Inaelekea wewe ni yule bwana mafumbo wa kifalsafa, pamoja na kufurahia mazungumzo nawe lakini inabidi niondoke, kwa mnasaba ni kuwa nina hakika utaipata; kwa sababu ni mtu mwenye kudumu katika jambo, ukiipata tujuvye kwayo.

Nini hicho?!

Njia ya furaha!

Baada ya muda mdogo alipoondoka nesi alikuja daktari chumbani kwa Joji, na kujua hali yake ilivyo, na kumjulisha kuwa anaweza kutoka kesho jioni akipenda hilo, kwani hali ya afya yake ni nzuri.

Asante

Mke wako alinijulisha kuwa mtasafiri kwenda Roma, hongereni, ni nchi nzuri yenye mengi.

Ndio, nitakwenda naye pamoja na watoto wetu, je kuna usia wowote wa kiafya baada ya operesheni?

Hapana kabisa, hali yako ni nzuri.

Kabla ya chakula cha mchana alifika Adam..akimkuta Joji amezama katika utafiti wake akiwa mbali na yanayomzunguka, alimsogelea kisha akamtolea salamu:

Inaelekea kuwa unalosoma sasa hivi ni jambo muhimu mno, kiasi cha kushindwa kuwatambua waliokuzunguka!

Adam..Oho Karibu sana, umefika muda gani, nilikuwa nasoma historia ya ukristo ya zama za kale.

Vizuri, umepata nini?

Unaposoma Historia hii unakutana na mshituko wa ajabu kabisa na mambo ya ajabu kabisa!

Huoni kuwa unafanya haraka kuukosoa Ukatoliki hata kabla ya safari yako kwenda Roma.

Mimi siukosoi Ukatoliki.

Kama ni hivyo sijakufahamu, unakusudia nini.

Mimi ninaukosoa Ukatoliki na Uprotestant na madhehebu yote na makundi yote ya Kikristo.

Wewe unakwenda Roma, mambo mengi sana yatafunguka kwako baada ya kusafiri, usiwe na pupa, huenda yakakubainikia mambo ambayo wala hujayafikiria.

Hili ndilo ambalo nilitaka ushauri wako.

Sijafahamu, ni jambo gani ambalo unataka ushauri wangu?

Kulingana na rai yako, nimewasiliana na Tom na kuchukua ahadi ya kukutana nae kesho, lakini ninajua atakayoniambia.

Vizuri, kamilisha atakayokuambia?

Ataniambia: Fanya utafiti kuhusu Ukristo na uujue vizuri zaidi kabla ya safari yako ya Roma, na mimi nahisi kuwa najua kwa kiasi kikubwa, iwe kutokana na kusoma kwangu au kwa safari yangu ya Yerusalem au katika maisha yangu, mimi ni Mprotestant, na sihisi kuwa nitaongeza chochote kipya katika safari yangu.

Una umri gani Joji?

Thelathini na nane au tisa, kwa nini unauliza hilo?

Umesubiri kwa muda wa miaka thelathini na nane, wala huwezi kusubiri hadi utakapokwenda Roma, na kurejea ukiwa na hakika na maamuzi yako, huoni kuwa una haraka?

Huenda ikawa hivyo, kila ninaposoma kuhusu makundi ya Protestant ndio kila ninapozidisha kuwa na imani nayo zaidi.

Kwanini basi usihamie kwenye Ukatoliki au kwenye Orthodoksi.

Je sijakuambia kuwa wewe ni Mkatoliki? Lakini niamini, umbali wangu kuhusu upapa wa kikatoliki ni mkubwa zaidi kuliko umbali wangu na Uprotestant.

Huenda rai yako ikabadilika baada ya safari, ni vizuri kuamiliana na fikra mbali mbali kwa mawazo huru na sio kwa fikra zilizokwishakuathiri kabla.

Sina fikra tangulizi, nimesoma vitabu vingi vya kikatoliki na kiprotestant na historia zao na matokeo yao, lakini sijakinaishwa na chochote.

Vizuri, Jaribu kuwa huru zaidi na kufunguka zaidi, na kufikiria zaidi, wala usifanye haraka; na hivyo basi baada ya safari yako utakuwa ni mwenye hakika zaidi na mwenye utulivu na maamuzi yako.

Je akili iliyosalimika na elimu inaweza kukosea kuhusu dini?

Bila shaka hapana, haiwezekani ikawa hivyo kama dini ni ya kweli kutoka kwa Mungu.

Lakini kama dini itagongana na akili au hali halisi au elimu, je hii sio dalili ya kuwa sio dini ya haki?

Bila shaka ni kweli, lakini hata hivyo yatupasa tufahamu kuwa akili ina upungufu; kile ambacho hatuwezi kukidiriki haina maana kuwa kinakwenda kinyume na akili au elimu, bali ina maana udhaifu wetu kama wanadamu tu.

Vipi, nielezee kwa uwazi zaidi.

Kwa kuwa sisi hatujui asili ya mungu vizuri, wala hatuwezi kumdiriki kwa akili zetu; haina maana kuwa Mungu hayupo au sio sahihi, lakini ina maana kuwa haya ni mapungufu ya kawaida ya mwanadamu.

Pamoja na tabu na juhudi kubwa sikuweza kufahamu kuwa mungu mmoja ana nafsi tatu hadi leo hii, Je, hii ni siri ya Katoliki miongoni mwa siri za kanisa, unanitaka niamini hayo bila hata maelezo?

Kuna tofauti kubwa iliyo wazi ambayo sitaweza kujua hali yake, na kati yake kugongana na akili, ni lipi unalokusudia?

Nakusudia hili la pili, hili linagongana na akili yangu na siwezi kulifasiri.

Yanayogongana moja kwa moja na akili iliyo sahihi haiwezi kuwa ni dini sahihi, au dini ya haki.

Kwa maana hiyo basi itabidi tuachane na Uorthodoksi, Ukatoliki na Uprotestant.

Kwa nini usisubiri hadi urudi kutoka Roma?

Nikirudi na rai hii basi wakati huo nitakuwa ima ni mkana mungu au msekula.

Kwani ukanaji mungu na usekula haugongani na akili kwa upande wako?

Kwa msingi zinagongana, na kwa ajili hiyo nilitoraka nikaenda kwenye dini, kisha nikatoka kwenye dini za watu wa ardhini kuelekea kwenye dini ya mbinguni, baada ya hapo nikauchukia Uyahudi kama ilivyo hivi sasa, na nimeanza kuuchukia Ukristo, na hakuna kilichobakia sasa hivi ila niwe gaidi Muislamu.

Usichukue maamuzi yoyote hadi utakaporejea kutoka Roma, huenda ukafahamu na kukinai.

Kama sijakinaishwa?

Tafiti kuhusu Uislamu huenda ukapata njia ya furaha!

Kwa nini wewe usitafute kwenye Uislamu kwanza? Na uwe mpenda wanawake, gaidi na mtu asiye na maendeleo.

Sisi tupo kwenye hatua ya utafiti kuhusu Ukristo, nitakujulisha ukirejea Roma.

Sijui kwa nini wewe na Katarina mnazungumza kama kwamba Roma nitakinaishwa niende kinyume na akili yangu, na kuamini na kusadikisha yenye kupingana na mantiki.

Sijakuambia uende kinyume na akili yako, lakini nilikuambia usifanye haraka, wewe una akili, ukikinai sawa na lau kama hukukinai fanya unachotaka, kisha mimi nimekuja kulingana na matakwa yako, na sijakulazimisha ufanye kitu, sasa kwa nini unanishambulia mimi?

Samahani Adam, mimi ni mtu wa pupa kimaumbile, lakini niamini kuwa mimi nataka kufikia njia ya furaha kwa haraka iwezekanavyo, kitu kilichokuwa kinanitia hofu kabla ya operesheni ni kifo wakati ambapo sijaifahamu njia ya furaha.

Utaifikia Mungu akipenda, na bora kuchelewa kufika kuliko kutofika kabisa, pamoja na kuwa hujachelewa; bali unakwenda kwa mwendo wa kasi kubwa.

Narudia samahani zangu kwako Adam, huenda nikawa na pupa, na huenda ikawa nimechoshwa na maudhui haya.

Ikiwa ni mwenye pupa ili uweze kufika hili ni jambo moja ama uchovu ina maana ya kutokudumu katika jambo lenyewe, kisha je huoni kuwa hili linagongana na nafsi iliyokuja ikijali na kuvumilia jambo hili?

Balaa! huoni kuwa unazidisha?!

Bila ya kusisitiza, mtu hawezi kufika popote, wala kufikia mafanikio yoyote, na uchovu ina maana ya kutosisitiza, kisha huoni kuwa jambo hili linapingana na nafsi ya mwenye haraka katika kuvumulia kwa sababu ya kujali kwako?

Naafikiana nawe, lakini wewe unahamasika upesi, Je, hulioni hilo?

Huenda ikawa hivyo, lakini huoni kuwa unakusudia kunichokoza?

Ha ha ha, wakati mwingine…unahamanika mara moja.

Wakati huo aliingia Katarina akiwa pamoja na Maiko, Salli wakikimbilia kitandani kwa baba yao, akawakumbatia kwa shauku..akawa anazungumza nao na kumuacha Adam kidogo…Adam akasubiri dakika chache kisha akaamua kuondoka.

Nimefurahi kujua hali yako, je utaniruhusu niondoke?

Katarina alitabasamu kwa Adam akamwambia:

Samahani Adam, Sali na Maiko hawajamuona baba yao baada ya operesheni, na wala hawakukaa naye muda mrefu sana; kwani walikuwa safarini.

Kwa nini unaomba samahani?! Nimemaliza mazungumzo na kujua hali ya rafiki yangu, na nina kazi nataka kwenda kuzifanya.

Nakushukuru sana Adam, je tutaonana kabla ya safari yangu?

Nitafurahi tukionana, hata kama kwa bahati mbaya hatukuonana basi kwa uchache tutawasiliana, haya kwaherini.

Baada ya kuondoka Adam alimkumbatia Katarina:

Sijamuona rafiki yako huyu ila hospitalini, lakini ni mtu mzuri na mwenye adabu kabisa, na unaona raha kuwa nae sijui kwanini?

Huenda ikawa kwa sababu ni Mkatoliki kama wewe!

Wakatoliki wengi vivyo hivyo ni wenye heshima na wazuri, lakini hapo kabla uliniambia kuwa hujui dini yake.

Hadi sasa bado sijui, lakini kule kujali kwake na kunihamasisha niende Roma ili kuujua Ukatoliki na mara nyingi kuwa sawa nawe katika kufikiri inanihakikishia kuwa yeye ni Mkatoliki. Hebu fikiria leo hii alikuwa ananikinaisha kufunguka na fikra kuhusu Ukatoliki.

Ha ha ha, vizuri, huenda amejifunga katika kufikia katika Ukatoliki peke yake, na huenda ukafaidika na rafiki zako lile ambalo hukuweza kufaidika na mke wako..kwa mnasaba nimewajulisha watoto leo hii kuhusu uhakika wa safari ya Roma, hawa hapa mbele yako wasikilize wanachotaka.

Agizeni, Semeni..mnataka nini?

Baba je umesahau?

Nimesahau nini?

Nilitaka kuona ngome ya Saint Angelo, na Sali alitaka kuona Trevi Fountain.

Samahani, kwa kweli nilisahau.

Ninahofia safari hii isije ikawa ni safari ya kukaa hotelini tu na kusoma vitabu na kufanya kazi kwenye Kompyuta yako na kujadili muda wote.

Ninawaahidi kuwa tutakuwa na wakati maalum nanyi.

Hii ni ahadi baba?

Ni ahadi na kwa ushahidi wa mama yenu pia.

Na mimi ninawaahidi vile vile, kwa ushahidi wa baba yenu

Kikao kile cha familia kilikuwa cha upole na chenye furaha hadi ilipofika wakati wa kula chakula cha mchana, Katarina akawaambia wanawe:

Mnaonaje tukiondoka sasa na ninawaalika katika hoteli ya kitaliano?

Vizuri!

Haya twendeni.

Katarina alipoondoka na wanawe, Joji alikula chakula chake cha mchana, kisha akarudia tena kusoma kwa mara nyingine..alianza kukumbuka alichosoma kwa umakini mkubwa tokea alipolazwa hospitalini, akaanza kuhisi hofu..kwani kila alipokuwa akisoma sana ndipo alipoona migongano kwa wingi zaidi, haswa kile alichokiita upagani wa ukristo na miungu kuwa mingi na kumfanya Papa na watu wa dini kuwa ni miungu! Je, inawazekana kuondosha haya yote kwa safari moja tu…! Ikawa haya yatatimia basi huenda upapa ukiwa ni sahihi na kisha yeye kuwa Mkatoliki kama alivyo Katarina na Adam…!

(3)

Joji aliamka mapema, baada ya kupata kifungua kinywa aliendelea na kusoma katika utafiti wake kama ada yake; alikuwa ana kitabu muhimu alikuwa anataka kukisoma nacho ni: ‘Hekaya zilizokatazwa katika Torati’ (Forbidden Tales of the Bible (Ballantine) and King David) mwandishi ni Jonathan Kirsch, alisoma maelezo ya jarida la Washington post kuhusu kitabu: “Mwandishi anatuambia katika kitabu hiki cha ajabu kuwa agano la kale limejaa baadhi ya visa vingi vyenye kutia hofu iliyo wazi katika fasihi ya magharibi ..vimefichwa kwa sababu ya urefu wa historia kwa sababu ni visa vyenye mshituko.” Je inawezekana maaskofu na watawa wanajua zaidi kuliko Mungu kwa yanayowafaa watu wayajue na yale ambayo hayawafai? Alikuwa akijiuliza ndani ya nafsi yake: Ni hekaya zipi ambazo hazifahamu za agano la kale (torati)? Na kwa nini zimefichwa? Na vipi? Je, inaweza ikawa ya kimapambano zaidi kama ilivyotokea na Levi huko nyuma? Aliamua kuanza kusoma kabla ya Tom kufika kwani ana ahadi nae leo hii.
Kitabu kilikuwa kimejaa uchezaji wa maneno ya tafsiri ili kuficha baadhi ya maudhui mbali mbali, bali katika kupunguza na kufuta nakala ambayo ipo katika lugha ya kiebrania; ili inasibiane na msomaji, kwa hoja ya kuwa itakuwaje tukawaruhusu watoto wetu wakasoma visa vya malaya, uchi na matumizi ya nguvu? Na wakati mwingine kwa madai kutoka kwa Khakhamat (wanazuoni wa kiyahudi) kuwa kitabu kitakatifu hakina maana ya kinachosema: Yote hayo yalikuwa ni majaribio yaliyofeli kuficha, kupotosha au kubadilisha andiko la asili, na swali lirudi katika akili yake: Je, hii ina maana kuwa wao wanajua zaidi kuliko Mungu? Au ina maana haitoki kwa Mungu? Au ni kuwa ilishaharibiwa na sio kutoka kwa Mungu?
Joji aliendelea kusoma katika hali ya mshangao na mshituko; ya kuwa kitabu hiki kitakatifu (agano la kale) inaaminiwa na dini zote za mbinguni (Uyahudi, Ukristo na Uislamu), na ukianza kukikosoa unakosoa dini zote za mbinguni; akasoma katika kitabu kisa cha Nuhu aliyelewa (aliyeleweshwa) akiwa uchi na akasoma kisa kichafu kuhusu jinsi baina ya Loti na binti zake, na jinsi binti zake walivyomlewesha baba yao Luti na wakakutana nae kimwili ili wahifadhi uzao wao bila baba yao kujua! au baina Reuben mtoto wa Yakubu na Bilha ambaye ni kijakazi wa baba yake…, nafsi ya Joji ilikuwa inajisikia kichefuchefu akisoma visa hivi vya kijinsia baina ya watu ambao hairuhusiwi kuoana, alishangazwa sana na visa hivi ambavyo vinasisimsha mwili wa mtu, iweje vifanywe na mitume ya mungu? Joji aliona uzito kukamilisha kusoma visa hivi..hadi alipofikia sehemu ambayo inazungumzia wasifu wa Mungu kuwa ni: “mungu mwenye hali yenye kubadilika badilika kama ilivyo zebaki, na mara nyingi anakuwa mvunjaji kuliko mhuishaji wa maisha”. Alikuwa akiona kuwa ni wasifu mgumu, na ya kuwa hawezi kumuabudu mungu wa aina hii! Je, wanathubutu kumfanyia hivi Mungu?! Ama kwa hakika wanaoabudu ng’ombe wanamtukuza mungu kuliko hata wenye vitabu vitakatifu wanavyomtukuza mungu wao.
Joji alicheka huku akijilaza, akiwa anasoma hekaya za Tamari kahaba aliyetukuzwa! Na jinsi gani uzinifu ulivyotukuzwa maadamu unafanyika hekaluni sehemu ya ibada? Bali wengine wakasema labda ni mchamungu mtawa, kisha ikaonekana kuwa huenda ni mke wa Yuda aliyezini nae, Joji alihisi kichefuchefu alipokuwa akisoma, na akahisi kuwa hawezi kuendelea kusoma hekaya na visa hivi, na akakumbuka fedheha za kijinsia za watawa na mapadri wa kikatoliki zilizoenea katika vyombo vya habari.
Alifunga kitabu na kufungua kompyuta yake, aliingia katika you tube na akaandika: Fedheha za jinsia za kanisa Katoliki”, zikamjia idadi kubwa ya fedheha hizo za jinsia kwa njia za kawaida na za picha hali kadhalika. Alikuwa akijiuliza: Je, nikamilishe safari yangu ya kwenda Roma ili nijue ubaya wa Ukatoliki, niendelee kama alivyonishauri Adam na Katarina Wakatoliki wawili? Au niende kwa ajili ya matembezi tu ya kawaida na nisahau kabisa maudhui ya njia ya furaha? Lakini alikumbuka kama ataacha njia hii ya furaha bila ya shaka atarejea katika njia ya mashaka ambayo alikuwa akiishi nayo, au aelekee katika ukanaji mungu, fikra ambayo inaangamiza nafsi ya mwanadamu sawa na nguvu inayoangamizi akili na elimu, aliona kuwa fikra zile zinagongana akilini mwake, bali ya kwamba kila fikra kabla ya kugongana na fikra nyingine inaigonga kabisa nafsi yake na roho yake, na kuanza upya kumrejeshea maswali yake, hakuna kilichomkatisha katika hili isipokuwa sauti ya daktari ikisema:

Joji..Joji hunisikiii?

Haah, naam karibu

Nazungumza nawe na wewe upo ulimwengu mwingine, ulikuwa unafikiria nini?!

Katika maudhui ninayoichukia ?!

Maudhui gani hayo?

Nachukia migongano, na kwenda kinyume na mantiki na akili.

Una maana gani?

Umesikia kuhusu fedheha za watawa na mapadri?!

Oooh, naam.

Itakuwaje mtu ajitenge kwa kumuabudu mungu, huku wakati huo huo anawalawiti watoto baada ya hapo.

Kama anavyokunywa pombe na kutumia madawa ya kulevya mtu kama daktari ambaye anajua hatari yake na madhara yake!

Lakini mnamuonaje daktari ambaye anatumia madawa ya kulevya kama heroin huko kwenu?

Huyu ni daktari aliyefeli, inafaa afukuzwe katika kazi yake na atangazwe!

Na je, ikiwa kuna taasisi husika ambayo ina majukumu hayo ya madaktari na ambayo inawapa vyeo na kuwapandisha daraja kisha inawanyamazia, bali ndio ambayo inafanya magendo hayo ya madawa ya kulevya, na kuwafundisha namna ya kufanya, na sio hivyo basi mfumo wake na katiba yake inaruhusu hivyo!

Hilo haliwezekani, lakini tukamilishe mazungumzo yetu, kama ni hivyo, basi hiyo ni taasisi ambayo inafumbia macho au kula njama, na hili ni jambo baya, je inapaswa watu walishwe kasumba hiyo miongoni mwa madaktari, au hospitali na fani yote ya tiba, unakusudia nini?

Huoni kuwa mafundisho matakatifu yanawafundisha watawa mambo ya jinsi, uzinifu na uchafu hata kubaka?! Huoni kuwa vitabu vitakatifu vimejaa mambo haya hata kwa manabii?! Kwanini tusitengamane nayo kama usemavyo?

Sijafahamu chochote, bali lililo sahihi sitaki kufahamu chochote kutoka kwako, Je, unataka tukane Mungu na dini? Katika ulimwengu wa tiba sisi tunafahamu kuwa wengi katika madaktari ni watu waliokana Mungu hata madaktari bingwa miongoni mwao wanakaribia kuwa ni wagonjwa wa nafsi, au niache niseme: Kwa uchache wao ni watu wasiokuwa na furaha katika maisha yao, ukitaka nasaha zangu kimbia na nafsi zako na fikra zako hizi hata kama umekinaishwa nazo, toroka kwa njia yoyote ile..kama utacheza na pombe au wanawake au jambo lolote lile.

Je inawezekana tukazikimbia nafsi zetu halafu tukapata hisia za furaha?!

Kwa bahati mbaya hilo haliwezekani kabisa, lakini tabu hizi huzingatiwa kuwa ni neema kulinganisha na tabu ya kumkana mungu na kuwa mbali nae…samahani kwa kukatisha mazungumzo matamu kama haya, lakini mimi nimekuja kukujibu swali au maelekezo ya kitiba tu kuhusu hali yako, na kwa kuwa utaondoka jioni hii, nakushauri ufuatilie sana joto lako kwa muda wa siku mbili hizi zijazo, je unalo swali lolote? Swali la kitiba tu?!

Hapana asante..je baada ya siku mbili hizo niendelee kuangali hali ya joto langu?

Hapana, siku mbili zijazo tu kwa akiba, na kama itakuwa imetulia, basi itakuwa ina maana kuwa utakuwa umerudisha afya yako kamili.

Tom aliingia na akatoa salamu kwa daktari na kwa Joji..daktari akaomba ruhusa ili aendelee na kazi zake, Joji akamuanza:

Kuna swali lisilokuwa la tiba je utaniruhusu?

Kwa sharti liwe la haraka, ehe.

Kwa kuwa unajua kuwa kukimbia hakutupi sisi furaha. sasa kwa nini tunakimbia?

Kuhofia ukanaji mungu, kwani huko ni kupata tabu kwa muono wangu kwa uchache.

Hivyo basi ima mtu akane mungu au atoroke? hakuna chaguo la tatu?!

Huenda ikawa kuna chaguo la tatu, lakini sijalijua, ukiifikia hilo nitafurahi na nitakushukuru sana, haya naomba ruhusa na kama una swali lolote la tiba kabla ya kutoka kwako unaweza kumuuliza nesi naye atanipigia, kwa heri.

Tom alimuangalia daktari akitoka, kisha akamgeukia Joji na kusema.

Joji sijui mlikuwa mkizungumza nini lakini mimi najua tabu na huzuni na humumi anayopata mkanaji mungu, nadhani kuliko mtu mwingine yoyote.

Kwanini ukanaji mungu una tabu kama msemavyo?

Katika jambo gumu sana ni kukosa wa kumtegemea, na kumuachia mambo yako, na kujua kutoka kwake njia yako.

Nitajuaje kwake njia yangu?

Kupitia mitume yake kwetu na vitabu vyake.

Je, unatarajia njia yangu ya maisha nielekezwe na mtawa kahaba na padri mbakaji?

Sifahamu?

Je, njia yangu ya maisha itaelekezwa na nabii mlevi mzinifu, au kitabu cha jinsi kitakatifu?

Una nini Joji? Kwa nini leo unazungumza hivi?

Tom nimechoka, ninafikiri kwa kina nisisafiri kwenda Roma, au nisafiri kwa ajili ya matembezi na utalii tu.

Kwa nini, kuna mpya gani?

Hakuna mpya, lakini nimesoma na nimeona mambo ya jinsi na matumizi ya nguvu katika torati na biblia.

Kwani hili ni jambo la kipekee kwa Katoliki?!

Una maana gani?

Je matumizi ya nguvu yaliyomo kwenye Uprotestant si kama hayo na zaidi ya hayo?! Unajua ni nani aliyeuwa watu huko Ujerumani na sehemu zinginezo katika mauaji makubwa ya kihistoria?

Ndio, Uprotestant, lakini nimechoka, huenda hata Uprotestant haufai!

Joji kuwa ni mwenye nguvu kama ulivyotuzoesha, ole wako na udhaifu, ukisubiri na kushikilia ulitakalo utafikia njia ya furaha, na ukishindwa na ukidhoofika utakuwa kwenye tabu, na huzuni mbali mbali.

Nifanye nini?

Sijui, ninachokifahamu ni kuwa Mungu hawezi kuficha njia ya kumfikia.

Njia hii iko wapi? Je si kwamba wakristu na waislamu wanaamini agano la kale? Kitabu kile chenye mambo mengi ya jinsi na matumizi ya nguvu, nilikuwa simuamini Levi alipokuwa akizungumza katika hili, lakini nimekinaika sasa na alichokuwa akikisema, je unataka nikupe dalili katika agano la kale?!

Sihitajii hilo, lakini ukitaka nikupe dalili katika agano jipya naweza.

Kwa nini basi unataabisha nafsi yako kwa kuutafuta Ukristo na Uislamu wakati zote zipo katika njia moja?

Tulikubaliana tokea mwanzo kuwa twende katika njia ili tupate ukweli, wala sijui kwa nini nahisi kuwa tumekaribia kufikia kwenye njia, usikate tamaa au ukasalimu amri mwisho wa mashindano..Joji wewe hutafuti au kwenda kwenye njia hiyo kwa ajili ya nafsi yako tu, mimi nipo pamoja nawe, kwani masomo yangu na utafiti wangu sasa ni huo huo, naamini hakika tutafika, lakini usiniulize vipi?

Nami nina hisia kama hizo, lakini mara nyingi nina hisi kuwa labda naichezea nafsi na roho yangu, vinginevyo dalili zote zinathibitisha kuwa nimepotea njia, pamoja na kuwa ndani ya nafsi yangu nahisi kuwa nimekaribia.

Safiri kwenda Roma uujue Ukatoliki na Uprotestant kwa karibu, kisha angalia na ufanye mazungumzo katika ulichosoma, wala usichukue maamuzi yoyote hadi umesoma dini zote za mbinguni.

Na ufanye utafiti katika Uislamu hali kadhalika?!

Ndio bila ya shaka, kutafiti kitu si kwamba umeamini, je, si umefanya utafiti na kusoma kuhusu Ubudha, Uhindu na Uyahudi? Kuna mpya gani basi? Je hatukukubaliana hapo mwanzo kuwa tuwache kuhukumu jambo hadi baada ya kujua na kutambua dini zote za mbinguni?!

Nitakamilisha, ingawaje sioni mbele yangu sasa ila ni kikwazo cha ushirikina, matumizi ya nguvu na jinsi na upotoshaji katika fikra na dini mbali mbali zilizoondoka na kubaki, pamoja na imani iliyomo ndani ya nafsi yangu kuwa nitafika katika njia ya furaha.

Weka fikra yako zaidi kuwa utafika katika njia ya furaha, kama kufika kwenyewe kuko wazi na kwepesi tusingehitaji kukutafuta!

Nitafika, na huenda nikashtushwa kuwa suluhisho lililo jirani yangu ni jepesi na lipo wazi, lakini sikuweza kuliona.

Huenda njia hiyo ikawa Ukatoliki au Uprotestant ….au Uislamu.

Pamoja na kukinai kwangu kuwa njia zote hizi zimejaa ushirikina, udajali, na dini kunyonya watu mali zao, jinsi, lakini tutakamilisha, unaniusia nini?

Je umesoma vingi?

Ndio, sikuchoshwa ila kwa kusoma kwangu kwingi, kwa munasaba: Ukatoliki haututaki tusome hata kitabu kitakatifu ila kwa maelezo ya Papa, kilicho katika kitabu kitakatifu ni lazima tukifahamu kama anavyofahamu Papa?! Na wanataka tuhamishe akili zetu.

Swadakta, lakini Waprotestant wanataka kutunga dini watakavyo, na kufahamu kama wanavyotaka na ndio maana ikagawanyika sana.

Bali asili ya agano jipya imejaa upotofu mwingi, iwe ni sawa tumeifahamu kama atakavyo Papa au kama tunavyotaka sisi nayo bado imepotoka, je sikukuambia kuwa dini zote hizi hazifai na kuwa zote ni ushirikina tu?

Vizuri, soma sana, jifunze sana, jadiliana sana, funguka zaidi, baada ya hapo utaiona njia.

Lakini Ukatoliki imesimama juu ya siri mbali mbali ambazo hazipasi mtu kuzijadili, siri za kanisa saba ambazo hazifahamu ila mtawa tu!! Na kuzijadili na kufikiria au kuzipinga ni kufanya kufuru, pamoja na kuwa zinakwenda kinyume na akili au mantiki!

Hata Waprotestant wanaamini siri mbili miongoni mwa hizo saba.

Je, huoni kuwa kila nikikuambia kitu unaniambia: Hata Protestant ni hivyo hivyo? Je, umeshakuwa ni Katoliki baada ya kufuatana na Katarina kwenda kanisani? Ninafahamu vizuri usemavyo, lakini mimi nazungumzia Ukatoliki.

Sitaki uelemee upande mmoja na kupendelea dini bila ya elimu wala kutumia akili, ikiwa ni kwa akili na kwa elimu sema utakayo bila kupendelea upande mmoja na kuwabebesha wengine mzigo.

Ninayosema ni kutokana na elimu na kutumia akili.

Na hata ninayosema mimi ni vivyo hivyo kadhalika, nilitaka uwe unaweka mizani ya mambo vizuri zaidi.

Ah ah..swadakta, huenda nikaegemea zaidi kwa Ukatoliki, pamoja na kuwa mengi nisemayo kuhusu wao yapo katika Uyahudi na Uprotestant; bali nadhania hata kwenye Uislamu kadhalika.

Kama ni hivyo tuache tukamilishe safari yetu ya uvumbuzi kwa utulivu kama tulivyoanza, hadi hapo mambo yatakapotubainikia zaidi..si wewe uliyeniambia: ‘Kwa wepesi bila ugumu’?

Ndio, hii ni katika sentensi za Adam zilizokuwa mashuhuri.

Kama ni hivyo basi ni kuwa, kila mtu anapokuwa mtulivu kila anapokuwa mizani yake ni nzuri na akaweza kuitumia akili yake vizuri zaidi. Kama ambavyo mimi tokea mwanzo nilikuwa ninakulingania kuwa na ufahamu wala usichukue maamuzi yoyote kwanza hadi mambo yote yatakapokuwa wazi kwako, kwani huenda ukachukua maamuzi ikawa njia hiyo ni Uyahudi kwa mfano, kwanini haraka basi?

Kwa wepesi siwezi kuamini kuwa ikawa ni Uyahudi kwa hali yoyote ile, mimi nachukia sana matumizi ya nguvu, na Torati imejaa matumizi ya nguvu, hebu fikiria kuwa katika agano la kale: (Maluuni anayeinyima panga lake damu) na (Amesema Mola Mungu wa Israel: Kila mmoja wenu na abebe upanga wake na azunguke mitaani mlango kwa mlango, na amuue ndugu yake, rafiki yake na jirani yake), ugaidi gani namna hii?!

Je, Wakristo na Waislamu nao si wanaamini agano la kale?! Kuwa mpole zaidi, wala usihukumu hadi mambo yote yatakapokuwa wazi kwako, nami nina hakika kuwa utafika kwenye njia ya furaha.

Hili ni tatizo kubwa katika dhana yangu, Wakristo wanaona kuwa agano jipya ndilo lililokamilisha agano la kale, na Waislamu kadhalika, zote kwa hakika ni dini za mabavu na kigaidi.

Hapa kuna nukta mbili: Ya kwanza haifai kuwa na dhana katika mambo haya, bali rai yako inabidi ijengwe kwa elimu, Pili: Natamani uwe makini zaidi na ufanye uchunguzi wa kina, ina maana gani kuwa agano jipya linakamilisha agano la kale? Je ina maana wao wanaamini au hawaamini?

Naafikiana nawe katika uliyosema, dhana sio elimu, kama ilivyo kuhariri jambo na kulifanyia uchunguzi wa kina ni muhimu sana, lakini kwa bahati mbaya Wakristo hawakuliweka vizuri istilahi ‘Linakamilisha’ kwa uwazi, na si mimi ndie ambaye sijalihariri, Kwa mfano Ukatoliki unawakataza wafuasi wao katika kulifahamu hata hili agano jipya, na wanaona kuwa ni haki ya watawa kuifahamu tu, na wanawaelezea watu wengine kama mimi na wewe, kwa mfano kama unavyofahamu andiko la agano jipya katika Mathayo Mtakatifu 10:34: ( Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! sikuja kuleta amani, bali upanga), au (ama maadui zangu ni wale ambao hawakutaka niwamiliki, nileteeni mbele yangu na muwachinje).

Na wewe unajua kuwa Wakristo wana maelezo ya kauli kama hizi.

Ndio tuna maelezo na tuna maandiko yaliyo kinyume yake ambayo yanalingania huruma na mapenzi, pamoja na hizi tafsiri kutotumia mantiki ila ni kuwa yatabakia kuwa ni maelezo yake, hata hivyo tafsiri hizi hazilingani na imani yetu ya agano la kale yaliyojaa mambo hayo, na matendo yetu kwa bahati mbaya yanathibitisha hayo, sin a wengine tu, bali hata baina yetu sisi, je, unataka nikutajie hayo kwa mfano katika mambo ya unyama wetu?!

Haya sio maudhui yetu sasa, acha tuweke kila kitu sehemu yake, na tuangalie kwa mtazamo wa jumla, kusoma dini yoyote ile ni vizuri mtu akaangalia misingi ya dini kama vile: Mungu wao, Mtume wao, kitabu chao, itikadi yao, hukumu zao mbali mbali, historia yao, hali yao halisi, na katika kusoma hayo ni vizuri umuhimu zaidi ukaupa katika kusoma mambo kwa ujumla wake na sio mambo madogo madogo.

Vizuri, vipi hivyo?

Badala ya kuiangalia sana kwa makini kauli fulani iliyopo kwenye agano la kale au jipya na tafsiri zake mbali mbali, tuangalie kitabu kitakatifu muono wa jumla kulingana na usahihi wa kutufikia, na mwandishi wake na kinacholingania, itikadi zake kuhusu mungu na manabii wake, na baada ya hapo nukuu za maelezo ya ndani yatabaki kuwa ni ushahidi wa kuthibitisha asili yake.

Vizuri sana, pamoja na kuwa nimesoma sana kuhusu hayo, lakini hata hivyo naweza kuangalia upya hayo ili nisome zaidi na kujadili zaidi.

Ili uweke wazi hili tujaalie kuwa umemaliza maudhui kuhusu Uyahudi kama usemavyo, hivyo ni kuhusu vitabu vya agano la kale? Ni nini kinalingania? Na nini mtazamo wake kuhusu Mitume ya Allah?

Tujaalie kuwa inatoka kwa Mungu.

Kwani Mungu ndiye aliyeandika? Je aliandika Mtume Musa? Je aliandika Harun? Je unamjua aliyeandika?

Ninadhani mfano wa haya utasema kwa agano jipya?

Bila ya shaka, vinginevyo utaelemea upande mmoja, njia hii ya kufikiria ipo karibu katika kutufikisha katika njia ya furaha, vinginevyo tutashughulika na vitu vidogo vidogo ambavyo kuna kuchukua na kurudisha.

Fikra nzuri, nakubaliana nawe kuhusu hilo.

Na baada ya kurudi kwako kutoka Roma tutakuwa tumeshatathmini dini mbili muhimu katika dini za mbinguni, itabakia moja na sura itakuwa wazi zaidi kwetu, na hivyo basi safari yetu ya uchunguzi kutafuta njia ya furaha itakuwa imekwisha.

Ikitubainikia kuwa zote hazifai?!

Kama ningekuwa kama nilivyo hapo kabla ningekuambia turejee kwenye ukanaji Mungu, na mimi sikukutaka uchukue njia hii kisha tena urudi kwenye ukanaji Mungu, lakini sasa ninasema kuwa lau ikitubainikia hivyo kuwa zote hazifai tutarudi na tutapanga kazi zetu kwa ukamilifu tokea mwanzo, na tutaanza tena tokea mwanzoni na kujiuliza swali: Je, dini ni jambo la msingi? Kisha tutawezaje kuchagua dini? Na hivyo hadi tufikie tulipofikia sasa, wakati huo mambo mengi yatakuwa wazi kwetu.

Safari ni ndefu sana.

Sitarajii kama tutarudi tena, natamani hilo, lakini swala hilo linaungana na elimu, kwa maana kila tutakapoongeza elimu tutaongeza uoni, na kinyume chake kila tutakapokuwa vipofu wa baadhi ya maeneo ndio ujinga utazidi na kutuweka mbali na kufikia majibu ya maswali yetu, na hivyo basi kuwa mbali na njia ya furaha, mimi nina hakika kuwa utafika, lakini subiri kidogo.

Nitafika sina ujanja katika hilo, kisha akatabasamu na kusema: Kikubwa ambacho kinanichosha ni kuwa sioni njia ya kuelekea.

Njia ya kuelekea njia tunayoikusudia iko wazi, lakini tunachokiona ni njia, na watu wengi wanadhani kuwa njia ya kuelekea njia ni sehemu ya njia ambayo wanaitafuta na hawajaiona.

Falsafa nzuri, lakini nibainishie mimi uwazi wa njia ya kuelekea njia.

Je, hujui kuwa tokea mwanzo ulifuata njia ya ukanaji mungu na usekula? Kisha ukaachana na njia ya dini za ardhini (za wanadamu)? Kisha ukafadhilisha dini za mbinguni? Je, haikuwa hivyo?

Nakubaliana nawe kabisa, lakini ambacho hakipo wazi kwangu ni vipi tutaweza kukifikia?

Hili ndilo nililokuambia, kilichokuwa sicho wazi kwako ndio njia, na sio njia ya kuelekea njia.

Hahaha, vizuri lakini hebu tulivuke hilo, unaninasihi nini katika safari yangu?

Nakuusia Kwanza: Jisikie furaha kwenye safari yako, na watembeze wanao, unahitaji upumzishe akili yako, na upange maarifa uliyokusanya yapate kukusanyika vizuri pamoja na mijadala yako. Pili: Endelea kusoma na kufanya mijadala, lakini kwa akili iliyofunguka na jali mambo muhimu na ya msingi.Tatu: Zidisha kutaamali katika mambo ambayo yatakusaidia katika kushusha na kupanga maarifa yako, na kukusaidia katika kumakinika katika mambo ya msingi.

Vizuri, naamini kuwa ni wasia muhimu sana na nitajitahidi sana kuufuata, pamoja na raha niipatayo katika kutafuta majibu ya maswali yangu, ila sasa nimekuwa mtu makini zaidi.

Umakini sababu yake inatokana na msukumo wa kila mara katika akili yako, msukumo wa maarifa mbali mbali, msukumo wa wanaokuzunguka, hivyo basi mizigo yako imekuwa ni kubwa, hivyo punguza mizigo yako kwa wasia niliokupatia.

Ndio, nitafanya hivyo, hata watoto wangu nimewaahidi hivyo.

Safari njema, tutaonana utakaporudi, ukiwa mchache wa mizigo uliyonayo, na mwenye maarifa mengi zaidi, na kufunguka zaidi.

Vipi Tom kuna habari gani kuhusu Baraad?

Inaelekea kuwa maudhui yale yanasonga mbele, ameanza kunitishia sasa bila kujali picha alizonazo pamoja na aliyoyarekodi.

Kukutishia!

Ndio, anazo picha za zamani ambazo si nzuri za baadhi ya wagonjwa wangu, na amerekodi baadhi ya vikao vyangu, na ameanza kunitishia kwa hayo, vinginevyo atavifikisha katika tume ya tiba na chama cha madaktari.

Itakudhuru nini kama atapeleka katika taasisi husika ?

Leseni yangu ya fani ya udaktari itafutwa, mbali na fedheha.

Anataka kuingia katika makubaliano ya nini?

Nifanye naye kazi.

Katika nini?

Hahaha, katika kuuza mihadarati, na kutekeleza anayotaka mimi nifanye.

Kufika katika vyama ni bora kuliko kuwa muuza mihadarati.

Swadakta..lakini nikifukuzwa kwenye kazi yangu itakuwa ni balaa kubwa vile vile.

Utafanya nini?

Sijui, lakini nitapanga mambo yangu, naomba ruhusa, kwaheri.

Joji alirejea kusoma akifurahia kikao chake na Tom alihisi kuwa amepata tumaini na kutulia baada ya kukutana nae, moyo wake ulifunguka baada ya mazungumzo nae, na akaamua kufanya aliyomuusia kadiri awezavyo. Hata hivyo akili yake ikaanza kushughulishwa jinsi gani atamsaidia Tom kwa tatizo la Baraad baada ya kuamini kubadilika kwa Tom hakutaka kumuacha peke yake, lakini anaweza kufanya nini?
Alipokuwa akifikiria tatizo la Tom..alifungua barua pepe yake, na kukuta barua mbili kutoka kwa Habiib na Levi wakitaka kujua afya yake, akawajibu:

“Mpenzi Habib Nilifanya operesheni yenye mafanikio, nakupa bishara kuwa hali yangu ni nzuri wa afya, baada ya siku mbili nitasafiri kuelekea Roma, ni kiasi gani nilitamani lau ungekuwa kule; ukanifasiria kwa elimu uliyokuwa nayo na akili yako iliyofunguka baadhi ya yanayonitatiza katika Ukatoliki. Wako: Joji.” “Rafiki yangu Levi, nilifanya operesheni yenye mafanikio, nakupa bishara kuwa hali yangu ni nzuri wa afya, baada ya siku mbili nitasafiri kuelekea Roma, ni kiasi gani nilitamani lau ungekuwa kule; ukanifasiria kwa elimu uliyokuwa nayo na akili yako iliyofunguka baadhi ya yanayonitatiza katika Torati na katika Uyahudi. Wako: Joji”

Wakati alipokuwa akimalizia kuangalia barua pepe mara akaingia Katarina..

Tumeanza taratibu za kutoka kwako, baada ya muda mfupi Mungu akipenda.

Natamani nyumbani, kuwaona watu na gari.

Muda wa kutokuwepo kwako ulikuwa mzito kwangu na kwa watoto. Ama wewe ulikuwa umeshughulishwa na kusoma kwako na mjadala wako, je Tom alikuja?

Ndio, kilikuwa ni kikao kizuri.

Je sikukuambia hilo?

Nasaha zako daima ni zenye faida, la msingi ni kuwa muda gani tutatoka?

Baada ya muda mfupi tu, namalizia baadhi ya karatasi, nitakwenda kukamilisha sasa kisha nitarudi ili tuondoke na huko njiani niambie kilichotokea baina yako na Tom leo?

(4)

Kabla ya muda wa safari kwenda Roma kwa masaa mawili familia iliondoka kwenda Uwanja wa Ndege, walipanda ndege kwa wakati muwafaka kabisa uliopangwa. Katarina aliipangilia safari hii ya Roma kwa uangalifu, aliweka nafasi Raphael Hotel ambayo umbali wake na Piazza Navona n barabara moja tu, inayosifika kwa kuonyesha mandhari yote ya mji wa Roma, kanisa la Saint Peters hadi hekalu la Pantheon, vile vile inaangaliana na njia za usafiri wa mabasi na sehemu takriban zote zenye kuvutia za historia katika mji wa Roma kwa masafa madogo sana kiasi cha kuweza kutembea kwa miguu..

Katarina uchaguzi wako ni mzuri sana.

Mama asante sana, chunguza ipo jirani na ngome ambayo tunataka kuiangalia.

Wala haipo mbali na Trevi Fountain ambayo unaitaka vile vile kuiangalia Sali.

Sasa ni saa moja usiku, mnaonaji tufurahishwe na mandhari ya hoteli kwanza, kisha tule chakula cha usiku, halafu tupumzike; tuanze na ratiba yetu kesho asubuhi tukiwa tumechangamka.

Sawa baba..

Familia iliamka mapema na kula chakula cha asubuhi hotelini, kisha wakaondoka pamoja na muelekezaji watalii hadi katika uwanda mpana uliopo karibu na hapo sehemu iliyojaa sehemu za kihistoria za kitalii, familia ilikuwa katika hali ya furaha sana wakiwa wanaangalia majengo ya Kiroma ya zamani, pamoja na sanamu mbali mbali, makanisa yenye majengo yenye kupendeza, ambayo unapata hisia za heshima na maana kamili ya historia.
Ilifika wakati wa chakula cha mchana; walikwenda kwenye mgahawa mpya wa kitaliano ambao upo katika staili ya kiroma..…

Baba sikujua kabisa kuwa ustaarabu wa kiroma upo katika uzuri na nguvu kiasi hiki!

Ustaarabu wa kiroma ni wazamani sana ewe Maiko, ni katika staarabu kubwa kabisa Ulaya baada ya ustaarabu wa kigiriki, ilikuwa inatawala kisiwa chote cha Italia mwaka 275 BC, na kwa karne mbili zilizofuatia Roma iliweza kujenga na kusimamisha dola iliyotawala ulaya nzima na kaskazini ya Afrika vile vile, na kadhalika utamaduni wa kigiriki pia ulimezwa

Kikubwa kinachotowa wasifu wa Roma ni hii Pizza, na sio masanamu yaliyopo nje.

Je, Maiko unayapenda masanamu haya?

Ni majengo mazuri sana.

Katarina kwa tabasamu zuri:

Ni uzuri ulioje wa sanamu la Yesu na bikira Maria!

Sijui kwa nini sanamu hizi na sanamu za Yesu zinanikumbusha sanamu za Budha na wengineo katika sanamu mbali mbali huko India? Na nahisi kuwa zote ni moja.

Achana na hili kwanza, tukimaliza kula tutakwenda upande wa pili wa Uwanda huu.

Joji alifahamu kuwa Katarina hapendi mjadala huu mbele ya watoto na hivyo akaheshimu rai yake, lakini ndani ya akili yake, hakuweza kuacha kutofautisha kati ya sanamu la Yesu na sanamu la Budha, bali itikadi za kishirikina na za kipagani na itikadi za kikatoliki.
Familia ilimaliza matembezi yake ya kitalii, na wakarejea hotelini baada ya kuzama kwa jua kwa muda mdogo tu, walikula chakula chao cha usiku wakiwa hotelini, na mwisho walipanda vyumbani kulala. Joji alifungua barua pepe yake akiangalia barua mbali mbali, akakuta barua ya Habib:

“Joji nakuandikia barua hii nikiwa pamoja na Levi, tumesoma barua yako tukiwa na furaha kwa kufanikiwa kwa operesheni yako, tutasherehekea baada ya muda mdogo tu, ama kuhusu kile kinachokutatiza kuhusu Ukatoliki au Uyahudi sisi tutafurahi kama tutajadiliana kuhusu hilo, bali tutafurahi hata kujadiliana kuhusu Uprotestant na Uislamu, tunasubiri tuanze mazungumzo hayo pamoja nawe. Habib na Levi.” Tanbihi kutoka kwa Habib: Usisahau kumtembelea Papa katika misa ya Jumamosi.

Joji akawajibu:

“Hallo Habib na Levi Mimi nipo Roma sasa, nchi ya Wakatoliki, na karibu na Vatican ya Wakatoliki, nimefurahi kwa furaha yenu, kuhusu tatizo nililonalo nitatoshelezwa kwa kuwatumia andiko, na nitasubiri maoni yenu juu yake kwa ufupi sana..kadhalika nitawatumia paragrafu kuhusu kitabu “Hekaya zilizoharamishwa katika Torati” iliyoandikwa na Jonathan .., na paragrafu inazungumzia kuhusu torati au agano la kale na andiko lenyewe ni hili: Tokea mwanzo hadi mwisho kitabu kinaelezea kuhusu tabia mbaya zenye kutisha na kuharibu maadili kulingana na alichokiandika Michelle Fintora (mwandishi wa habari) ambaye alichanganyikiwa pindi alipoona katika torati “Wanawake wanaolewa na nyoka, ndugu wanauana wenyewe kwa wenyewe, mataifa yanachinja bila msamaha wowote, makabila yanaimba nyimbo za kubembeleza juu ya vichwa vyao majangwani, watoto wanaonyonya wanahama, mauaji yanayofuata utabiri, na utabiri unafuatia mauaji, wachezaji dansi wanadai vichwa vya manabii.” Fintura anafikia katika hitimisho na kusema: Kwa hakika jamii yoyote inayoipa hadhi Torati kama ni kitabu kitakatifu jamii hiyo itajiweka katika wazimu, kinachochekesha katika alichoongeza: “Ukitarajia ustaarabu ambao utategemea kitabu hiki, jamii hiyo haitokuwa isipokuwa ni jamii ya wanyama na ya waharibifu” Je, mnakubaliana na Fintora au hapana? Pamoja na tanbihi kuwa dini zote za mbinguni zinaamini kitabu hiki kitakatifu?! Wasallam, wenu Joji”

Aliamua vile vile kutuma maandiko haya kwa Adam na Tom katika barua moja, kisha akakaa akifikiri: Je anakubaliana na Fintora kuhusu alichosema? Ili ajadiliane kuhusu fikra hii kwa atakayekutana nae kesho kulingana na jeduali alilopanga Katarina..
Baada ya chakula cha asubuhi, Katarina aliondoka na watoto kuelekea sokoni wakati ambapo Joji alimsubiri John Luke Franco, kulingana na ahadi aliyoweka Katarina. John Luke alikuwa ni mwandishi wa kitaliano, alikuwa anafanya uchunguzi kuhusu Ukatoliki na Uprotestant kwa kadiri Katarina ajuavyo. Katika ahadi iliyopangwa saa tano asubuhi John luke alikuwa ameshafika hotelini, Joji alimkaribisha na akajibu kwa salamu yenye uchangamfu kabisa na kuanza kuzungumza nae:

Kulingana na kilichonifikia kutoka kwa askofu mmoja wa marafiki zangu ni kuwa wewe unatafuta majibu ya maswali makubwa? Na ya kuwa mke wako kasisi aliwasiliana na rafiki yangu padri Luogi Stefano na akamjulisha hilo, niache nijitambulishe.

Mke wangu sio kasisi, atakuja muda si mrefu, nimefurahi kukutambua, karibu.

Mimi ni mwandishi wa habari hapa Italia, nimesoma falsafa chuo kikuu na nimeipenda mno, kutokana na maswali muhimu ya wanafalsafa, kisha akatabasamu na kuendelea kusema: Kwa wenye akili bila shaka, ni maswali makubwa kuhusu maisha; nimefanya juhudi kubwa kutafuta majibu ya maswali haya.

Kwa hivyo basi umeongea na Padri aliyeongea na Katarina.

Ndio

Nini matokeo ya utafiti wako wa miaka mingi?

Ha ha ha..nimefikia katika matokeo muhimu sana na nukta fulani maalum.

Vizuri sana, ni zipi hizo?!

Rahisi, hamna kitu! Kwa sababu nilichokuwa nacho ni kukosoa ukweli unaosikitisha wa dini mbali mbali, lakini haukujengwa kwa fikra iliyokamilika.

Unaweza kunisaidiaje na hujapata chochote katika matokeo ya utafiti wako?!

Kwa hakika mimi nina uzoefu wenye faida kubwa sana ninaweza kukusaidia, kama ilivyo ninaweza kufaidika vile vile na uzoefu wako, lakini matokeo ya utafiti wangu wa kujibu maswali kwa masikitiko hamna kitu!

Je unaamini kuwa inawezekana majibu yakawa hamna?

Wewe ni mtu unayeangalia vitu kwa kina na kwa wepesi kabisa kwa wakati mmoja, vizuri kabisa kamilisha.

Nikamilishe nini? Mimi nakuuliza unijibu.

Majibu yako wazi, ndio maana sikujibu, hakika kabisa ni kuwa majibu hayawezi kuwa hamna kitu, hivyo kamilisha (utafiti wako)

Kwa maana hiyo kuna majibu na wewe hujayafikia?

Sehemu moja ya akili inasema kuwa kuna uwezekano wa kupata majibu na kuna uwezekano vile vile majibu yasiwepo.

Sidhani kuwa akili inaweza isipate majibu, kwani huu ni muktadha wa kuwa wanadamu wanaogelea katika upotofu, na ambayo inapelekea kuzaa nadharia za kizembe na zisizokuwepo na za hovyo.

Wewe ni mwanafalsa mzuri kabisa, hii ndio rai yangu vile vile, lakini nimesema nilichosema nione utasema nini, lakini kwa rai yako nitapata wapi majibu ya maswali yangu kama hali ni hiyo?

Mimi nimetafuta na hadi sasa sijapata, nini rai yako wewe?

Baadhi ya marafiki zangu wakanao dini na Mungu walijaribu kunishawishi na kunikinaisha kuwa maisha hayana uhusiano wowote na Mungu, na kuwa majibu ya maswali yanaweza kuwa kwa njia ya kielimu yenye kupimika, au kwa bahati tu.

Vizuri. Je walijibu maswali yako?

Ukanaji Mungu ni falsafa iliyopotea au isiyo na mashiko, haiko mbali na kufanana visa, ngano, ushirikina, hata ikivaa mavazi ya kisomi na kutumia fikra, niamini ukanaji Mungu naufahamu vizuri kabisa na nimejadiliana na watu wengi miongoni mwao.

Inaelekea umeegemea upande mmoja na kuwapa lawama wakanaji Mungu na masekula.

Nahofia usije kuwa mkanaji Mungu; na ndio maana unawatetea, lakini nitazungumza nawe kwa uwazi, nipe fursa hiyo. Kila mkanaji Mungu anajua ndani ya nafsi yake kuwa ana makosa, mimi nilikuwa miongoni mwao, na nimeishi muda wa umri wangu katika ukanaji Mungu, hali hii ya ukanaji Mungu ni aina fulani ya kutoroka matatizo ya dini mbali mbali wala hawana falsafa ya kuwatetea au nadharia au hata dalili za kiakili au kielimu. Ama usekula wao wanaamini dini, lakini kazi yako kubwa ni kuwa iwe mbali na maisha kwa sababu ile ile waonayo wakanaji Mungu.

Vipi, sijafahamu?

Tatizo la ugomvi na mvutano baina ya dini na elimu ni tatizo kubwa tokea zamani, zinapogongana dini na elimu, watu wanaipa elimu nafasi kubwa na kuisadiki kuliko dini.

Je elimu zetu zinaweza kuwa ni bora kuliko elimu aliyoleta Mwenyezi Mungu?

Bila shaka hapana, je Mungu anaweza kuleta kitu au kikashuka kutoka kwake kitu chenye makosa au kisichowezekana?

Unakusudia nini?

Kwa yale wanayosoma watu au kusikiliza katika wasia wa kitabu kitakatifu kuwaamrisha wao kuuwa au kuzini au kunywa pombe, nao wakiwa na hakika kabisa ya madhara ya vitu hivi kiakili, kimaadili na kielimu, unataka wafanye nini?

Kama ni hivyo wewe umefika katika usekula ili uitulize nafsi yako na majibu ya maswali makubwa.

Kwa masikitiko…Usekula hautulizi chochote kabisa, lakini nazungumza na wale ambao wameamini usekula, unatoa suluhu tu ya mgongano wa dini na elimu, na kutatua tatizo la kihistoria tu, ama ukitaka ukweli ni kuwa Usekula unanasibiana sana na dini ya Ukristo.

Vizuri, nibainishie hii nukta ya mwisho.

Njia ya Upapa au mfumo wake ni njia ambayo inaweza ukafanya chochote kile; inaweza kukuuzia cheki ya msamaha na hivyo matatizo yako yakaisha; na hivyo basi unaweza kufanya chochote ukitakacho mbali kabisa na dini, kisha baada ya hapo ukanunua tena cheki ya msamaha.

Lakini Uprotestant hauamini hivyo, au siyo?!

Ndio, huenda ikawa hivyo kwa sababu hawaamini sana, na sio kwa sababu hawatenganishi dini na maisha, bali wao ndio wanatenganisha rasmi kabisa, hivyo basi linganio kubwa la Usekula bali hata la ukanaji Mungu linatoka Kanisani!

Wewe unalingania nini?! Katika dini gani?! Mara unatetea ukanaji Mungu, mara nyingine unautetea usekula na wakati mwingine Ukatoliki!

Mimi sipo popote pale, sijakuambia kuwa sijapata matokeo yoyote? Na wewe je?

Mimi ni Mprotestant, kwa sababu baba yangu na mama yangu walikuwa hivyo, kisha baada ya hapo hamna kitu!

Ha ha ha…kwa maana hiyo sisi tunafanana.

Je umeridhika kuwa hujafikia matokeo yoyote? Au unahisi kutofikia chochote ndio umeshafika?

Hakuna kitu hakifikiwi! Na huenda haya yakawa ndio sababu ya kuanza na kukuwa kwa madhehebu ya kijinga na ya kipuuzi huku kwetu nchi za magharibi.

Mielekeo ya kipuuzi!

Ha ha ha, ndio makundi na madhehebu ambayo yanajenga dini yake pasina kitu au katika upuuzi mbali kabisa na dini.

Kama ni hivyo hili ni balaa la hakuna kitu.

Bali balaa ni kuwa maswali kuhusu maisha hayajajibiwa bado.

Kwa nini usiyasahau na kuyakimbia?

Sikuweza, na sidhani kuwa mtu mwenye akili anaweza kufanya hivyo.

Je unakusudia kuwa watu walio wengi ni wenda wazimu au wapumbavu?

Bali ninakusudia kuwa watu walio wengi hawawezi kusahau na wanachukizwa sana na maisha yao na kuondoka kwa furaha zao.

Wewe ni mwanafalsafa, lakini wakati huo huo ni msorajua, na hukuweza kufikia bali umefikia matokea ya hakuna kitu, sasa suluhisho ni lipi basi?

Suluhisho nililonalo ni kuwa tuendelee, hadi tupate majibu ya maswali..na wewe una suluhisho gani?

Ndilo hilo nililolisema tu, lakini natofautiana nawe kwa kuwa ninahisi kuwa hivi karibuni nitapata majibu.

Kuwa na matarajio ni neema kutoka kwa Mungu, na nataraji matarajio yapo sehemu yake, lakini matarajio yako inabidi yawe na dalili yake.

Dalili yake ni kuwa twende katika njia tukiwa na rajua na bila ya kubabaika wala kuwa na shaka.

Vizuri sana, ubunifu mzuri, ehe na ulifikia wapi kwenye njia hiyo.

Nimemaliza kujua kuhusu ukanaji Mungu na dini zote za ardhini, na zote hazina maana wala hazina manufaa kama ulivyotaja, kisha nikaanza kushughulika na dini za mbinguni, na mimi sasa nipo kwenye utafiti kuhusu Ukristo.

Mimi ni Mkatoliki kulingana na makuzi yangu, lakini ninakwambia kuwa siamini chochote kuhusu Ukatoliki, kwani ni makundi ya mzaha na siri mbali mbali na migongano tu.

Kama ni hivyo basi kwa nini usiwe Mprotestant?

Samahani sana ewe Mprotestant; nimeanza na dini yangu kwanza, Uprotestant nao ni majaribio ya kukimbia dhihaka ya Kikatoliki, ni jitihada iliyofeli na aliyeanzisha hana dini hivyo, kwa hivyo basi walichokifanya wao wamechukua kiasi cha dhihaka ya Katoliki na siri zake mbali mbali pamoja na uchache wa imani ya dini yao.

Nibainishie zaidi, wakati mwingine mgumu kufahamika.

Je, hawakuwa wao pamoja (Ukatoliki na Uprotestant) wakitegemea Biblia? Na yaliyomo ndani yake katika agano jipya na la kale ambayo haswa ndio vyanzo vya dhihaka hiyo na ushirikina.

Kwa nini unasema hivyo kuhusu kitabu kitakatifu kilichoteremshwa na Mwenyezi Mungu?

Kana kwamba na wewe ni Padri, nitakujibu kama nilivyojibu, nijibu kwa ujasiri, je, unaweza kunithibitishia kuwa kilichopo mikononi mwetu sasa hivi kimeteremshwa na Mwenyezi Mungu? Mimi ninaweza kukuthibitishia kuwa baadhi ya yaliyomo kwa uchache sio kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Utawezaje kunithibitishia hayo?

Kwa dalili nyingi, miongoni mwayo: soma ukipenda historia ya kuandikwa kwa kitabu kitakatifu, hata anayesema kuwa ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu utashtushwa na hakika ya kihistoria, angalia migongano bali hata zinavyotofautiana nakala na matoleo mbali mbali na tafsiri au tarjama zake mbali mbali, bali utashangazwa na tofauti iliyopo katika toleo moja! Soma baadhi ya matukio ambayo yanakataa kabisa kuitwa kuwa yametoka kwa Mungu, au ya kuwa Mungu huyo ni mwenye shari na mbaya, je unataka dalili nyinginezo? Je unataka maelezo ya kina kuhusu dalili yoyote?

Nakubaliana nawe kwa mengi uliyosema, pamoja na kuwa nataka kujadiliana na kasisi katika hili na mengineyo; ili nimsikie yeye.

Wewe ni mtu wa ajabu, kwa nini basi unajadiliana nami katika hili

Ikiwa hali ndio hiyo uliyosema, suluhisho ni lipi?

Nimekuambia kuwa matokeo yangu hayakuwa na kitu.

Samahani, kutokuwa na kitu maana yake kutokuwa na maarifa nayo, na mimi ninamtaka mwenye elimu na maarifa hayo.

Unachosema ni sahihi, lakini mimi sikimiliki.

Kwa rai yako ni nani mwenye majibu?

Ningekuwa namjua basi tabu zangu za siku nyingi zingekwisha.

Nataka kukutana na mmoja katika maaskofu kama inawezekana; kwani nataka kusikia majibu yao katika hoja hizi na nyinginezo.

Nina marafiki zangu wengi maaskofu, je unawataka wenye kasumba miongoni mwao au waliofunguka? Au unawataka wanazuoni wao au wanaojifanya kuwa na elimu?

Ikiwa nina uwezo wa kuchagua, aliyefunguka ni bora kuliko wenye kasumba, lakini la msingi zaidi ni kuwa na elimu, namtaka mwenye elimu zaidi yoyote awaye awe ni mwenye kasumba au aliyefunguka zaidi.

Kama ni hivyo basi pata tumaini, kila elimu ya mtu inapozidi kuwa kubwa ndipo anapofunguka zaidi, nitaweka miadi na rafiki yangu Padri Lougi Stefano ambaye alizungumza na mke wako, kwani yeye ni katika maaskofu wenye elimu kubwa kati ya niliowaona, na aliyefunguka zaidi. Kesho au kesho kutwa nitakupa ratiba ya miadi.

Nakushukuru sana.

Nafahamu unachosema, ni mwenye furaha kukusaidia.

Joji akitabasamu:

Nahisi kuwa nimekuchosha lakini nina swali, Je, ulishafanya utafiti kuhusu Uislamu?

Hapana…nimesoma juu juu tu, na mahojiano ya hapa na pale tu.

Kwanini?

Uislamu ni dini ya matumizi ya nguvu, Jihadi, kumdhulumu mwanamke na kuwa nyuma, na mifano mingi ya namna hiyo.

Umejuaje hayo yote na wewe hukufanya utafiti wowote kuhusu Uislamu?

Mwenye kumiliki hoteli jirani na nyumba yetu ni Muislamu kutoka Misri, wakati mwingine ninajadiliana nae.

Naye anakuambia hivyo mwenyewe?

Hakuna anayeweza kusema hivyo mwenyewe, lakini ananiambia kuwa yeye ni Muislamu aliyestaarabika, na sio kama waislamu wengine ambao hawakuendelea, na pindi nilipomuuliza sababu ambazo zinawafanya Waislamu wasiendelee, aliniambia: sababu ni dini yao, kwani ni dini inayolingania kasumba na kuwauwa wenye kwenda kinyume nao, na kumfungia mwanamke, bali na kumpiga.

Jambo la ajabu kabisa. Je ninaweza kuonana nae?

Wewe ni mtu wa ajabu, unataka nini kwake? Katika hali yoyote tunaweza kula pamoja hotelini kwake na kuonana nae siku yoyote ile.

Vizuri, lakini nina swali lingine kama ukiniruhusu?

Uliza.

Kwanini Padri anakutuma kwangu na yeye dhahiri anafahamu rai yako kuhusu Ukatoliki?

Je, sijakuambia kuwa yeye amefunguka? Mara nyingi nahisi kuwa anakinaishwa na ninayoyasema, lakini hajui uchaguzi unaofaa!

Rai ya maana kabisa, ikiwa haikutubainikia njia za majibu ya maswali yetu basi tuliyokuwa nayo sasa hivi ni bora kuliko kupotea kabisa.

Swadakta, na natamani isiwe niliyokuwa nayo sasa hivi ni upotevu, lakini bado naendelea kufanya utafiti.

Samahani, sikutaka kukukosea hata kidogo.

Nafahamu hilo.

Katarina alirejea pamoja na Maiko na Sali, wakakutana na John Luke, Katarina akampa mkono na kumkaribisha..

Ashukuriwe Bwana, nimefika baada tu ya kuondoka, wewe umekuja kwa njia ya Padri Lougi Stefano?!

Ndio, wewe ni mke wa Joji, Padri anasema wewe ni katika Wakatoliki wenye dini zaidi Uingereza, pamoja na kuwa hujawa mtawa.

Nakushukuru pamoja na Lougi, yeye ni mwalimu wangu, kwani nimesikia mawaidha yake mengi sana pamoja na mihadhara yake.

Nitaratibu miadi naye pamoja nanyi kesho au kesho kutwa.

Vizuri sana…kama Joji atakubali.

Joji ndie aliyetaka hili, na tutakula chakula katika Grand Hotel.

Vizuri, nitakutana na mwalimu wangu…lakini kwa nini Hoteli hiyo uliyosema?

John Luke mjulishe..

Kuonana na mmoja katika Waislamu hapo.

Kwa nini?

Sijui, lakini anataka kusikia kutoka kwake kuhusu Uislamu kuwa nyuma pamoja na ushenzi wao na ukatili wao.

Na kama Muislamu huyu hajakujibu hilo mimi ninaweza kukujibu, inatosha tu kuangalia nchi zao zilivyo ili kujua kwa nini wako nyuma hata kwenye dini yao.

Kwa ujumla hii ni kadi yangu, nitafurahi kwa mawasiliano nanyi na kwa maelezo yoyote yale kuhusu dini au utalii, na nitawapigia kuwahakikishia miadi pamoja na rafiki yangu Padri Luogi Stefano. Kwaherini.

John Luke alitoka, Katarina alitabasamu akimgeukia Joji huku akisema:

Ehe kikao kilikuwaje? Nilitamani sana kurudi mapema ili nikutane nae.

Nzuri sana, asante.

Bila ya shaka Padri hawezi kumtuma mtu ila mtu huyo awe ni msomi na mwenye dini zaidi na Mkatoliki..

Ndio..yeye ni mwanafalsafa na mwanazuoni. Lakini si mwenye dini Mkatoliki kama usemavyo.

Ajabu! Lakini umesema kuwa ni rafiki yake.

Ndio ni rafiki yake

Inawezekana vipi Padri akasuhubiana na mtu asiyekuwa na dini?! Kwa ujumla, ni muhimu atupangie ahadi ya kukutana nae; huenda tukafaidika nae.

Vizuri kufaidika na kila mtu, na vipi mtu huyo akiwa ni Padri, ehe nijulishe habari za sokoni?

Matembezi yalikuwa mazuri sana, watoto walicheza sehemu zao, kisha tukanunua baadhi ya vitu…hatukuchelewa isipokuwa njiani tu.

Leo tutatembelea wapi katika sehemu za athari mjini?

Leo tutatembelea ngome ya Saint Angelo kwa ajili ya maombi ya Maiko, ni husuni nzuri sana na ipo karibu tu na itamaliza siku yetu ya leo hii pamoja na kutembelea pembizoni mwake.

Twendeni sasa hivi, yuko wapi Maiko na Sali?

Chumbani mwao, wanavaa viatu vyao vipya; twendeni sasa hivi.

Familia iliondoka kuelekea ngome ya Saint Angelo, joji alijali sana kutekeleza usia wa Tom wa kupunguza huzuni na wasiwasi wake na mizigo aliyojibebesha, na kuwa ashughulishwe na matembezi na furaha na wanawe tu, alijaribu kutofikiria mambo mengi kuhusu njia ya furaha, vinginevyo ataingiwa na wasiwasi na kulalamikia katika njia ya kufikia majibu ya maswali yake, bali ni juu yake kutafuta kwa njia ya utulivu mno.