India… Nchi ya Maajabu

India… Nchi ya Maajabu

India… Nchi ya Maajabu

(1)

Akiwa uwanja wa ndege baada ya Joji kumaliza kukaguliwa pasipoti yake na kuingia alimkuta Maiko akimsubiri, aliweza kumfahamu pindi alipomuona kwani alishatuma picha yake katika barua pepe. Maiko alimkaribisha Joji kwa shauku na akamuuliza kama angependa kwenda hotelini, au amchukue katika matembezi ya kuona mji.

Nakushukuru, hata hivyo nipeleke hotelini, nimechoka safarini, suala la matembezi tulifanye kesho asubuhi kabla ya kwenda ofisini.

Joji alimuona Maiko kuwa ni mtu mtanashati mno na hutangamana na watu kwa hali ya juu kabisa. Joji alichukuliwa na gari la kifahari linalothibitisha kabisa kuwa mwenye gari hilo ni tajiri katika nchi yenye ufukara wa hali ya juu.
Katika siku iliyofuata, kwenye milango ya saa moja asubuhi, Joji alishuka toka chumbani kwake katika hali ya uchangamfu kabisa. Usiku uliopita alilala kwa muda wa kutosha, alimkuta Maiko akiwa mapokezi anamsubiri, ni kama vile alivyomuona jana, mtanashati ambao unamvuta mtu wa pili kumwangalia. Joji alimsalimu Maiko na wakaondoka pamoja kuelekea kwenye gari.

Unaonaje tufanye matembezi kwa muda wa saa moja, kisha baada ya hapo tutakuwa tumefika ofisini saa mbili na nusu?.

Vizuri, ningependa kuijua India.

Muda wote wakiwa njiani Maiko alikuwa akimuelezea Joji kuhusu majumba aliyoyaona na makanisa kwa kujifaharisha kuwa India ni nchi yenye historia kubwa, ila Joji aliona kuwa Maiko hapendi kuzungumzia baadhi ya majumba makubwa pamoja na Joji kumuuliza. Kadhalika alikuwa hapendi kuzungumzia masanamu ya budha yaliopo kila mahali. Maswali mfano wa hayo mara nyingi aliuliza na Maiko alikuwa akimhadaa katika majibu mara kwa mara, kana kwamba anataka kusema kuwa nchi ya India ni nchi ya Kikristu peke yake. Joji alitosheka kwa kuuona mji na hakuongeza chochote katika ziara hiyo, akakumbuka maelezo ya Kakhi kuwa Maiko ni mtu mkatoliki mwenye siasa kali.
Saa mbili na nusu Joji na Maiko waliwasili ofisini, walikaa hapo hadi saa tano wakizungumzia masuala ya kazi, miradi na mikataba, kwa hakika Maiko alihisi hali ya utulivu mkubwa kuwa na Joji, alinyanyua kichwa chake ghafla na akasema:

Wewe ni mkristo kama mimi, kwanini tunamwachia Kakhi Myahudi kucheza na mikataba ya wafanyakazi wote, unaonaje mchezo uwe katika mikataba ya wahindu, mabudha na waislamu tu, na tukashurutisha kuwa mikataba ya wakristo kuwa bora zaidi, sitaki myahudi huyu kutuibia!

Je, ni uadilifu kumuibia Mhindu, Mbudha na Muislamu?!

Maiko alifedheheka na kukaa kimya..na wakaendelea na kazi zao hadi saa moja, hapa Joji aliomba wapumzike kwani alishachoka.
Njiani wakielekea hotelini walirejea katika njia ile waliojia, na pindi Joji alipoona jumba kubwa alitaka kumuuliza Maiko kwa mara nyingine:

Ni nani aliyejenga jumba hili lenye kuvutia?

Waislamu …wabakaji.

Na hii ni nini?

Hekalu la Mabudha mataahira…wanaabudu mawe na watu mfano wetu.

Baada ya Joji kuhisi hali ya wasiwasi aliokuwa nao Maiko kwa maswali aliyomuuliza aliamua kunyamaza muda wote wakiwa njiani..

(2)

Joji aliafikiana na Maiko kuwa ampitie saa kumi; ili wapate kwenda kwenye chakula cha mchana pamoja, kwani alimuandalia hafla ndogo ya kumkaribisha, pindi alipotoka chumbani kwake kwenda chini na baada ya kupanda gari Maiko alimuuliza Joji:

Kuna ada na desturi anayoitaka Kakhi mara anapotujia, sikuona ukiulizia!

Ni lipi hilo?

Tuakhirishe jibu hadi tutakapofika hotelini, nadhani utafurahishwa na maandalizi yenyewe!

Walifika hoteli ya Taj India, hoteli ilikuwa inaonesha kila ufakhari katika kila kona yake. Joji alipendezwa na sehemu yenyewe na uzuri wake. Alivutiwa kwani ilikuwa ya kiasili kabisa na akavutiwa na udi uliokuwepo pamoja na kwamba hapendi harufu za udi. Maiko kuona vile alitabasamu akamwambia mbawa zake mahususi zitakuwa nzuri zaidi.
Katika mbawa moja maalum hapo hotelini, Joji aliwaona wasichana wawili wazuri na umri wao unakaribia miaka ishirini, walikuwa wakiwasubiri wao na pindi walipowaona walitabasamu, alipeana nao mikono huku wakitabasamu, Maiko akamkonyeza Joji na kumpiga piga mabegani:

Unaonaje mazingira haya?

Nzuri sana.

Kila mara anapokuja Kakhi namleta hapa kwa ajili ya chakula cha mchana, kisha anawachukua wasichana wote au mmoja wao anakwenda nao hotelini, na kumalizia usiku mwanana.

Joji hakuonesha furaha na alijibu kwa upole kabisa:

Kweli mazingira ya kuvutia, ama kwa upande wangu ni uzuri wa mahali hapa tu.

Ajabu, hukuvutikwa na hawa wasichana wawili?!

Kweli wao ni wazuri bila shaka, cha kushangaza ni wewe! Mimi sio Kakhi!

Una maana gani?

Unadhani anachokifanya Kakhi ni jambo zuri nifanye mfano wake?

Kakhi hafungi mikataba ila kwa njia hii!

Hiyo ni rushwa kwangu ili nisaini mikataba!

Samahani, unataka nini?

Mimi ni mtu niliyeoa, sitaki kumsaliti mke wangu, je Maiko haya siyo mafundisho ya Ukristo?!

Ndiyo..ndiyo!

Alikuja mhudumu na menyu na akampa Maiko, akazungumza nao kihindi akaondoka pamoja na wale wasichana wawili, kisha akamgeukia Joji kwa tabasamu bandia:

Je nikuagizie au utaagiza mwenyewe?

Nichagulie, wewe unajua zaidi.

Joji alitaka kubadili hali ya kikao kile, akakumbuka kuwa Katarina alimtuma zawadi na alimkumbusha mara kwa mara, alisema zawadi ile inamkumbusha ushindi wa wakristo kuwashinda Waislamu washenzi huko India, kisha baada ya hapo India kugawika kwa Pakistani na Bangladeshi; na hivyo kumwambia Maiko:

Wewe unawajua watengenezaji wazuri wa msalaba, je unaweza kunielekeza sehemu nikanunue kwa ajili ya mke wangu?

Watakuletea chumbani kwako..kisha akakumbuka: nitakujulisha bei yake, sio rushwa!

Unajua, pamoja na kuwa mimi ni mkristo mprotestanti ila ni kuwa sijui ukristo, nadhani wewe ni muamini mzuri, je, unaweza kunikinaisha na dini yangu?

Ukristo ni dini ya mbinguni, imetoka kwa Mungu muumba, sio kama dini za ardhini walizotunga wanadamu.

Una maana dini gani hizo?

Dini kama vile Ubudha, Uhindu, Umajusi na nyinginezo, hapa India kuna mamia ya dini kama hizo.

Joji alikumbuka mazungumzo yake na Adam, akapendelea aendelee kumuuliza Maiko maswali, ili apate mtazamo wake kuhusu dini, na vipi anafasiri kuwepo kwake.

Ni nani anayethibitisha kuwa ukristo ni dini ya mbinguni na sio ya ardhini?

Historia inathibitisha hilo pamoja na mapokezi ya ushuhuda mbali mbali, ukimuuliza Mhindu atakuambia kuwa ukristo ni dini ya mbinguni na dini yake ni ya watu na inaendelezwa na watu…

Nadhani katika hali ya kawaida kabisa ni kuwa dini za mbinguni ni bora kuliko dini za ardhini.

Vizuri sana, neno kawaida, ni maelezo mazuri hayo! Ndio hilo ni sahihi zaidi, je kuna shaka katika jambo hilo?!

Haya ni maneno ya wakristu wote, hata hivyo katika hali ya kawaida ningependa kulihakikisha mwenyewe na ikiwezekana kuona.

Baada ya siku kupita, siku iliyokuwa na matukio mengi, Joji alielekea hotelini, na pindi alipojilaza kitandani, akawa anarejea yale yote yaliyopita, hakujihisi ila pale alipokuwa akilirejea jina la Adam: “Hakikisha kuwa unarahisisha mambo bila mafumbo, huku ukiwa na furaha bila huzuni”.
Alifungua Televisheni na akakuta kipindi kwa lugha ya Kihindi ikiwa na tarjumi kwa lugha ya kiingereza, kipindi kile kilikuwa kinazungumzia Uhindu, mafundisho yake na maadili yake mazuri. Kipindi kile kilikuwa kinahimiza kuwa dini ya Kihindu ni mchanganyiko wa dini ya Aryans ambayo inanasibishwa na kutukuza nguvu za maumbile ya asili, na dini ya Kihindu ya zamani, dini ambayo inahimiza vitu vilivyokuwa vikipendwa na watu wa India wa zamani, na baada ya kupita muda kuna maendeleo yaliyotokea na kukawepo aina ya muungano, wakaanza kuogopea kuondoka kwa maslahi ya baadhi ya tabakakatika kuandika baadhi ya fikra katika masuala haya, na fikra hizi baadae zikajulikana kama ni Fida na Veda. Veda ni kitabu kitukufu zaidi kwa Wahindu; maana yake ni:Kanuni au hekima, wakawa wanaandika kanuni na hukumu hizi, na muradi wake ni: kuwapa tabaka la Ari au waliokuwa weupe zaidi sifa ya ziada iliyokuwa kinyume na ile ya wale weusi, kanuni hizi zinawapa wachache sifa hizo zikaanzwa kuandikwa, sifa hizo sikazidi na kuwa nyingi, na ikawa ngumu kuzihifadhi kanuni hizi moyoni ni ngumu, hivyo wakasema: ‘Zinafaa kuandikwa, wakaanza kuandika, uandishi uliodumu kwa karne kumiyaani miaka mia moja (100)na ikawa ni hali ya kuendelea hadi hapo baraza kuu la makuhani wa Kihindu kuhitimisha kwa azimio kuwa haiwezekani kuongeza kitu katika kitabu hiki. Na kama si kuhitimisha kwa azimio hili basi uandishi wa kitabu ungeendelea na yangeongezwa mengi zaidi. Kitabu hiki ni kikubwa mno lina mijaladi mingi, kipindi kiliendelea kuelezea kuwa yenye kuashiria kuwa dini hii ya Kihindu haifai sehemu nyingine isipokuwa India tu, na kuwa Wahindi walipitisha azimio kuwa wanazuoni wao kuwa kuwa Uhindu ni dini maalum ya Wahindu, na kuwa uhindu ukitoka nje ya India sio Uhindu tena, Joji akacheka kwa dharau kuhusu dini hii yenye kasumba hata kwa sehemu, hata hivyo aliiizuia nafsi yake:

Kwa hali yoyote hii ni kadhia ya watu, na si kutoka kwa Mungu, hili ni kwa hali ya kawaida tu! kama kwamba naanza kuliona ninalolitafuta, hata hivyo bado halitoshi…

(3)

Saa mbili asubuhi Maiko alikuwa ameshafika katika ahadi yake akimsubiri Joji katika mapokezi. Pindi alipomuona Joji akija mbele yake alitabasamu, alimsalimia kwa lugha ya kusisitiza na kumwambia:

Leo hii tuna kazi ndefu, leo ni kama jana, Je, upo tayari?

Bila shaka nipo tayari, ndilo nililojia.

Wakiwa njiani Joji aliona sanamu la aina yake ambalo halifanani na la Budha, akageuza shingo yake na kuliangalia kwa kina, Maiko akamwambia huku akicheka:

Una nini? Huyu ni mungu miongoni mwa miungu, si nilikuambia kuwa dini za wanadamu kila siku zinatengeneza miungu wapya.

Nataka kukaa na mtu mwenye kuabudu dini hizi.

Hahaha, leo hii tutakula chakula cha mchana na mwanamke mkurugenzi wa uendeshaji katika shirika, naye ni Mbudha.

Walifika kwenye shirika wakashughulishwa na kazi walizoendea, Maiko aliona kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Joji na Kakhi, Joji alishughulishwa na mambo ya dini na akiulizia mara kwa mara, na ni mwenye kupenda kujua zaidi, ni mtu mwenye misimamo yake anayoiheshimu, tofauti kabisa na Kakhi mpenda mali na wanawake. Walipomaliza kazi zao mnamo saa sita mchana, Maiko alimsogelea Joji na akamwambia kwa sauti ya chini:

Tukimaliza nataka nikuambie kitu.

Hamna neno, niambie.

Wewe hufanani na Kakhi kabisa, pamoja na kuwa mnafanya kazi katika shirika moja.

Hahaha, unakusudia wale wasichana wa pale hotelini?

Ndio huyu ni mmoja tu, na kuna wengi mfano wake.

Vizuri, unadhani ni nini sababu ya tofauti hii kwa mtazamo wako?

Ni dini bila shaka.

Na wewe, je si mtu wa dini na unamwendekeza Kakhi?

Huenda ikawa, lakini si lazima ninachofanya kikawa sawa.

Maiko alisimama ili kuondoka, kisha akamgeukia Joji:

Je hupendi kukutana na Jiyotsana?

Ni nani huyo Jiyotsana?

Ndiye yule mkurugenzi mbudha..Je, unajua maana ya Jiyotsana?

Hapana, sijui.

Maana yake ni: mwanga wa mbalamwezi, kisha akatabasamu na kusema: Hahaha, umri wake hivi sasa unafikia miaka sitini, na sie mtu wa kutoa rushwa.

Bila shaka ningependa kukutana nae, je, anaweza kula pamoja nami hotelini saa kumi?

Inawezekana, na baada ya kukutana nae utaona neema ya ukristo..

Joji alipoteremka kutoka chumbani kwake kwa ajili ya ahadi ya chakula cha mchana, alimuona mwanamke mwenye umri mkubwa akimsubiri, alikuwa na mikato katika paji lake na anaonesha kuwa ni mwanamke aliyechanganya baina ya uchina na uhindi, au ndivyo alivyo kama alivyodhania, alimsogelea na kumsalimia:

Karibu, BiJiyostana.

Asante, nami nimefurahi kukutana nawe.

Alimwalika kula nae chakula Buffet (mgahawa ambao walaji hujihudumia wenyewe) pale hotelini, alimshukuru. Alionekana wazi kabisa kuwa ni mwanamke mwenye kujiheshimu na mwenye tabia njema.
Joji alichagua meza ya pembeni na akamkaribisha kwa kumwambia:

Maiko kanihadithia mengi kuhusu wewe.

Nami kadhalika, Maiko kanihadithia kuhusu wewe, aliniambia kuwa uliomba ule nami chakula cha mchana kwa kuwa ungependa kujua kuhusu Ubudha!

Ni kweli kabisa.

Kabla ya kuzungumza, katika hilo kuna kitu kimenivutia kwako, bali na wafanyakazi wote hulizungumzia katika shirika.

Ni nini hilo?

Kuwa wewe sio kama Kakhi.

Wamejuaje?

Habari imeenea kuwa umekataa kutofautisha baina ya mnaswara, mbudha, mhindu na muislamu kuhusu mikataba, kama ilivyoenea habari ya kuwakataa wasichana wale wawili! Na mfano wa hayo.

Je wamefurahishwa na hayo?

Kwa uchache mimi kama mbudha, ndio..sana.

Nafahamu kuhusu kutoichezea mikataba lakini vipi kuhusu hiana?

Sisi Mabudha tunachukia hiana na matamanio, bali tunaona kuwa mambo machafu yanatokana na sababu tatu zifuatazo: Kwanza: Kujisalimisha na matamanio; moja katika usia wa Budha ni: “Usipoteze uhai, usiibe wala kubaka, usidanganye, usinywe kilevi, usizini, usile chakula kilichoiva kabla ya wakati wake, usicheze wala usihudhurie ngoma na hafla za nyimbo, usiende kwa daktari, usilale katika kitanda chenye godoro na haswa laini, Usichukue dhahabu wala fedha.”

Ni usia mzuri kabisa, lakini nina baadhi ya maswali: Kwanini usiende kwa daktari, wala usichukue dhahabu wala fedha? Au usilale katika kitanda chenye godoro! Je, ni ukomunisti huo?

Kuipa nyongo dunia ni alama kuu za ubudha, nayo inajumuisha vile vile kuacha kuoa na utajiri, kuihama nafsi, na mfano wa mambo hayo kama ulivyosikia; ima ushikamane na dunia au uikimbie.

Nashangazwa na alama kubwa za ubudha ni kutokuishi maisha ya furaha hapa duniani, tabia ya mwanadamu ni kupenda mali, kutamani mwenza wa jinsia nyingine…, na huyo budha ni nani?

Nilikwambia ima dunia au kuikimbia, kuipa nyongo dunia ni mama wa mambo ya kheri. Ama kukujibu kuhusu nani Budha? Hilo ni swali gumu kulijibu!

Itakuaje jibu kuhusu Budha likawa gumu? Je, Yeye si Mungu wenu? Au Mtume wenu au Mkweli ambae nyote mnajinasibisha?!

Umesimama katikati ya ugumu, sisi hatujaafikiana kama yeye ni Mtume, Mkweli, Mungu, Mtoto wa Mungu, au mwalimu au vyovyote vile..

Inaingia akilini?!

Kaskazini ya China inatofautiana na Kusini yake, na vivyo hivyo tofauti ya Burma (Myanmar) na Cylon katika kulielezea hilo. Kwa ujumla si hili, bali muhimu ni wewe mwenyewe kujiweka katika hali nzuri katika nafsi yako na roho yako ili uwe Budha.

Na kuitakasa Nafsi ni mtu asioe wala asikusanye mali, na kuvaa mavazi duni?

Ndiyo hasa, wala asiibe, wala asidanganye, kulewa wala kuua.

Joji hakushindwa kuona alipokuwa akizungumza na Jiyotsana mavazi yake aliyovaa yaliyovutia, alitamani kumuuliza kuhusu rai yake kuhusu mavazi yake na utanashati wake:

Je hilo linampasa kila anayefuata Budha?

Ndio..kisha akatabasamu: Kwa kiasi fulani, mazingira ya maisha yetu yanatushinda katika kufuata usia huu wenye hekima.

Kwa maana hiyo ni usia wa kimaadili tu, wala haufai kwa maisha ya watu wengi?!

Kwa kiasi fulani hata nyie hali kadhalika.

Una maana gani?

Kusema ukweli Maiko ni mtu wa dini sana. Hata hivyo anawapelekea wasichana Kakhi katika kila ziara aifanyayo huku! Na anacheza na mikataba ya wafanyakazi! Nawajua wakristu wengi wenye kunywa pombe, je, haya si makosa mliyonayo?

Umesema kweli, hata hivyo mimi nataka kujua dini yenyewe tu.

Hakuna tofauti kwangu mimi, nadhani tunafanana.

Baada ya hapo akawa anafuta mdomo wake akiashiria kuwa kamaliza kula, Joji alimuita mhudumu na akamtaka alete bakula la tamu tamu za kihindi, kisha akaendelea na mazungumzo yake:

Hamjaafikiana kuhusu Mungu wenu au ni mtume wenu au..au..je mmeafikiana kuhusu sheria na hukumu za dini yenu na wasia?

Kwa hakika wasia huu tunauongeza mara kwa mara.

Mnauongeza?!

Naam, Ubudha ni dini inayokuwa na nyakati; hii ni dini tuliyoitengeneza sisi na sio ya mbinguni kama mnavyodai dini yenu ya kikristu, pamoja na kuwa baadhi yetu wanadai kuwa ina asili ya kutoka mbinguni, hata hivyo mimi nashuku juu ya jambo hilo.

Je utaniruhusu nikuulize swali la moja kwa moja pamoja jepesi japokuwa linakera?

Sawa uliza, Mabudha wanapenda wepesi wa mambo.

Je, mnaamini kuwa dini iliyotoka mbinguni ni bora au ya ardhini (iliyotungwa na mwanadamu).

Jyostana alichukuwa muda kujibu, kisha akanyanyua kichwa chake:

Sitaki kudanganya..bila shaka kama ya mbinguni ni bora zaidi..hili ni kwa ajili misingi, hata hivyo waumini wengi wa dini za mbinguni ni watu wabaya zaidi…kisha akatabasamu: chukua mfano wa Kakhi Myahudi, na kwa uchache Maiko, ambao wanachezea mali za watu na kuiba.!

Umesema kweli..umesema kweli, kama ni hivyo kwa nini usiingie katika dini ya mbinguni ili uwe mwema zaidi?

Nimezaliwa na baba na mama Mabudha, na kwa ajili hiyo mimi ni Mbudha, lakini hatujui!! Huenda baada ya kufa kwangu nikawa Myahudi, Muislamu au Mkristo.

Baada ya kufa?!

Ndio..roho yangu itahamia kwa mtu mwingine baada ya kufa kwangu, na umri wangu sasa ni miaka sitini.

Je unaamini kuwa roho ya marehemu huingia katika mwili wa mtu mwingine.

Hapana, lakini ipo katika dini yetu.

Uchovu ulianza kujionesha wazi kwa Jyostana kutokana na maswali na majibu haswa ni kwa sababu ilikuwa ni baada ya muda wake wa kazi kumalizika, aliomba kikao chao kiishe, kwani mwili wake hauwezi kukaa zaidi.

Je kuna maswali mengine au jambo ninaloweza kukutumikia?

Hapana, asante, ulilolifanya ni kubwa sana, nimejifunza kwako mambo mengi.

Aliaga na kuondoka.
Maiko aliwasiliana na Joji jioni na kumwambia kuwa atakuta msalaba alioutaka katika mapokezi pale hotelini, na baada ya hapo akamtania: pana risiti hapo hotelini ili usidhanie kuwa ni rushwa!
Joji alimshukuru na akacheka bila kuona tatizo katika maneno ya Maiko.

Je umeona neema ya ukristo baada ya kukutana na Jiyostana?

Ndio.

Ungeendelea kukaa nae sana ungesikia mambo ya ajabu yanayoweza kukutia mvi, Je, amekuelezea kuhusu mambo yao ya kufikirika na falsafa ya dini yao?

Mambo yao ya kufikirika! Hapana.

Hahaha, hilo ni bora. Vinginevyo usingerudi tena India, hata hivyo ulichosikia kinatosha kukuonesha kuwa ukristu ni bora zaidi.

Una maana dini zote za mbinguni?

Hili ndilo nilionalo, tutaonana rafiki yangu.

Joji alimaliza usiku wake katika chumba hoteli, akipitia tovuti mbali mbali katika intaneti huku akiangalia Televisheni hadi usingizi ulipoanza kumchukua akajilaza kitandani. Ilikuwa ni siku yenye kuchosha kwa upande wake. Haukuwa uchovu wa kiwiliwili tu, lakini kichwa chake kilikuwa kizito kwa majukumu aliyonayo pamoja na majibu ya maswali yake binafsi ambayo ndio yalikuwa na msukumo wake wa kuja kwake India. Katika yote hayo usia aliopewa na rafiki yake Adam haukumuacha: “Hakikisha mambo yako unayachukuliwa kama yalivyo.” alihisi raha sana kwa hilo kwani leo imembainikia udhaifu mkubwa wa dini zilizotungwa na watu, na umbali wa dini hizi kutoafikiana na ubinadamu na hilo aliyakinisha yeye. Hivyo basi ni vipi mtu kama sisi atueleze sababu ya kuumbwa kwetu.?!

(4)

Asubuhi siku pili, Joji aliamkia katika soko kubwa la kompyuta hapo Delhi, alipanda hadi ghorofa ya tano, katika ofisi ya Mutwi ambaye anamiliki maduka mengi ya Kompyuta na programu zake.
Joji alikutana na ofisi ya kawaida kabisa, hata hivyo ilikuwa ni ya kawaida lakini ya kifahari kwa wakati mmoja, harufu ya udi wa kihindi ilijaa kila sehemu, Joji aliingia na kukutana na mtu wa mapokezi na kuulizia ofisi ya Mutwi, naye akamjibu:

Sheikh Mutwi, upande wa kulia, mlango wa mwisho kulia, utakutana na ofisi ya sekretari wake.

Joji aliondoka akiwa analitaja lile jina mara kwa mara huku akishangazwa: Sheikh Mutwi!! Sheikh! Ina maana gani?! Alimsalimia sekretari, ambaye alikuwa yupo kwenye kompyuta anafanya kazi, ambapo alijieleza na kutoa kitambulisho chake cha kazi, na kumjulisha kuwepo kwa ahadi na Mutwi.

Karibu sana, Sheikh anakusuburi takriban tokea dakika tano zilizopita.

Joji aliangalia saa yake, kweli ilionesha kuwa ni saa mbili na nusu na dakika tano. Hadi alipoingia katika ofisi ambayo pamoja na kuonesha ukubwa wake ila ilikuwa haina mpangilio, Mutwi alisimama na kumkaribisha, akamshukuru kwa wema wake na wakaanza mazungumzo yao ya kazi.

Je unaweza kunielezea upana wa mashirikiano tunayoweza kuyafanya pamoja?

Kwa ujumla ni chochote kinachoweza kuleta mapato kwangu na faida kati yetu.

Joji alifurahia hali hii ya kawaida (ya Mutwi kutokuwa na makuu), alimpa mkono na akafuatia kwa kicheko:

Tumeafikiana..haya ni makubaliano ya haraka zaidi katika historia, lakini yatupasa kufahamu: Ni njia gani itakayotupatia faida sote?

Nadhani majibu hayo yanaweza kutolewa na ndugu yangu Karimullah, ni mjuzi zaidi yangu katika kipengele hiki, unaweza kujadiliana nae, hata hivyo kwa sasa hayupo. Kutaneni kesho saa tatu asubuhi, na muandikiane vipengele vya makubaliano yetu.

Je umeshatembelea Delhi na pembezoni mwake? Kama sivyo ni haki yetu kukutembezakama mgeninaweza kukutayarishia matembezi haya.

Nimetembea mwendo mfupi kwa muda wa saa moja na nusu.

Kama ni hivyo hukuona kitu chochote cha maana; India ni nchi kubwa sana na ina mengi..je utanikubalia kuwa mwenyeji wako?

Nitafurahi kwa hilo.

Kama ni hivyo twende, tukimtegemea Mungu.

Mpaka wapi?

Matembezi, tutaaanzia Taj Mahal.

Joji akiwa na Mutwi walishuka chini na kuliona gari zuri la Mutwi likiwa na dereva wake akiwasubiri, Mutwi alikaa nyuma pembeni ya Joji.

Njia kuelekea Taj Mahal inachukua muda wa saa nzima na nusu, njia haikuwa na msongamano wakati huu, njia yenyewe kuelekea Taj ilikuwa ni sehemu ya matembezi vile vile, ama Taj yenyewe ni katika maajabu ya dunia, sitokuelezea kuhusu Taj bali utaiona mwenyewe.

Nani aliyeijenga?

Mfalme Shah Jihan, nayo ni mfano wa majengo ya Kiislamu India.

Kiislamu?!

Ndio.

Samahani, hawa waislamu si ndio wale waliopora ardhi ya India, nao ni watu wakatili?!

Kusikia hivyo Mutwi alitabasamu..

Naam..naam tumeiba India, na tukawauwa watu wake, na tukaipokonya kheri zake!

Nasikitika sana, kumbe wewe ni Muislamu?

Naam, nilikuwa nakudhania unajua hilo.

Samahani kwa swali langu, lakini hivyo ndivyo tunavyosikia kuhusu waislamu.

Usijali, Mimi wala wenzangu hatukuja toka nje ya India na tukaingia India kupoka kheri zake…mimi ni mzawa wa India mtoto wa mzawa wa India na .., na ukitaka kujua nani aliibia India utaona utakapofika Taj Mahal, ni nani aliyekata johari zake?

Ni nani?

Muulize muongozaji watalii tutakapofika..na natarajia hilo halitakushitua, mimi najua propaganda dhidi ya Waislamu wala sishughuliki kujibu, na nadhani historia ndogo ya India utakayosoma itakubainishia hilo.

Vipi?

Unaweza kuandika historia ya India kwa kuangalia katika Intaneti, na utaweza kujua ni nani aliiteka India na kuiba, je ni waislamu ambao ni wakazi wake wa asili, au waliokuja..kisha baada ya hapo angalia maisha waliyokuwa nayo watu wengine katika hukumu ya dola ya Kiislamu..kisha akakumbuka na kucheka: pamoja na kuwepo makosa mengi, moja wapo ni katika Taj Mahal tunayoiendea sasa hivi, alijenga kaburi la mke wa Shah Jaan.

Wewe unazungumza kwa hali ya kawaida kabisa!

Kawaida katika mtazamo wa maisha ni moja katika anuani za maisha ya furaha na kuridhika.

Joji alifurahishwa sana na matembezi yale na suala la wizi wa johari ulifanywa wakati wa utawala wa Waingereza, Mutwi hakupenda kuumiza hisia za mgeni wake, Joji alipenda tabasamu la Mutwi na usafi wa nafsi yake, lakini alihisi kitu kimoja kwake, Mutwi kwani alimuacha Joji mara tatu peke yake katika matembezi yale na kila wakati akimwambia: Nisubiri nakwenda kuswali kisha narudi, kama kwamba hakuwa ni mtu mwenye nidhamu na mpangilio mzuri katika matendo yake.
Matembezi yalimalizika, Joji alifika hotelini kwake saa mbili usiku akiwa amechoka, alikoga na kwenda kitandani kulala, hata hivyo kabla ya kulala akakumbuka jambo na kumpigia Maiko kutaka ushauri wake kuhusu mazingira ya maafikiano atakayofanya na Mutwi.

Halo..ndio, nataka ushauri wa haraka, inaonesha Mutwi mwepesi kuingia katika makubaliano, je ni wepesi wenye hadaa?

Pamoja na kuwa sina raha na Mutwi ila namuona kuwa ni mkweli, lakini vile vile ni mtu asiyekuwa na nidhamu katika kazi yake, na lau angeweza kuwa na nidhamu nzuri katika kazi yake angekuwa na matokeo tofauti sana.

Kakhi alikuwa akiniambia kuwa Mutwi ni mtu mgumu lakini nimemuona kinyume chake.

Ndio, ni mgumu katika dini yake, lakini ni mpole na mwepesi katika mikataba yake, kisha akacheka na kuendelea: ni mgumu kwa sababu hakumuunga mkono Kakhi katika tamaa yake na wanawake wake, ndio maana hakukubaliana na Kakhi pamoja na vikao vyao vingi pamoja, na sasa unajua sababu ya mtu mwenye dini kama mimi kumletea Kakhi wanawake wazuri!

Kesho nitakaa nae ili kuingia nae katika mkataba, je una nasaha zozote za kunipa?

Abadan..sina kitu kingine, roho mtakatifu atakulinda, je utapenda nikuchukue matembezini kesho?

Asante..nikihitaji kitu nitawasiliana nawe.

Kwa heri.

(5)

Asubuhi, pindi Joji alipokuwa akipata kifungua kinywa katika sehemu ya kulia hapo hotelini, alikuwa anaongea na mhudumu aliyekuwa akizungumza kiingereza kibovu:

Jina lako nani?

Naitwa Kapoor.

Inasemekana kuwa India ni nchi ya dini mbali mbali, dini yako ni ipi?

Uhindu

Vizuri, dini yenye maadili mazuri.

Ndio, kweli kabisa.

Je ni kweli hawezi mtu mwingine wa nje kuingia katika dini yenu isipokuwa tu mtu anayekaa India, na ndio maana inaitwa Hindus?

Ndio, dini hii tumeitengeneze iwiane na mtu anayekaa India tu.

Mmetengeneza dini?!!

Ndio, tumeitengeneze itufae!

Ni yupi Mungu wenu mnayemuabudu?

Sisi ni matajiri dunia nzima kwa kuwa na miungu mingi!! Tuna idadi kubwa sana ya miungu, na huenda pengine tukahitaji vitabu vingi zaidi kuorodhesha majina ya miungu yetu, kiasi cha kumfanya mwandishi Will Durant (aliyeandika kitabu Historia ya Ustaarabu) kusema: Kuhesabu na kuorodhesha miungi itahitaji pengine vitabu mia moja.

Ajabu kabisa.

Sisi tunaabudu vitu katika anga, na tunavifanya kuwa miungu kama vile jua, nusu ya baadhi ya miungu yetu zina wasifu wa Malaika na nusu nyingine zina wasifu wa shetani.

Mungu yuko karibu zaidi na shetani!

Baadhi za hirizi ni miungu, kuna aina ya ndege ambayo ni miungu na kadhalika baadhi ya wanyama.

Mnyama Mungu!

Kwa mfano Tembo ni mungu (Janisha), ndani yake kuna mchanganyiko wa tabia za kibinadamu na mnyama, na nyoka anayeua kwa kugonga mara moja tu ni mungu (Naja), na sisi tunawapa nyoka hawa maziwa, lozi na tunawafanyia sherehe za ibada.

Mnawaabudu vipi miungu yote hii?!

Kwa wingi wa miungu tulionao tumewaweka katika makundi matatu au moja katika sehemu tatu.

Moja katika sehemu tatu..kama vile wakristo!.

Huenda tukawa tumechukua haya kwa wakristo, sisi tunaiendeleza dini yetu wenyewe, au huenda nyie mmechukuwa kwetu.

Mhmh, malizia…

La muhimu ni kuwa miungu watatu au mmoja katika sehemu tatu nao ni: Brahmanae ndiye muumba, Vishnu huyu ndie mwenye kuhifadhi na kuuokoa ulimwengu na Shiva nae ni Mungu wa maangamizi.

Dini ya maajabu kabisa! lakini hukuzungumza kuhusu ng’ombe?! Nimesikia kuwa nyie…

Hahaha, nitakuambia kama anavyosema Ghandi: Ng’ombe ni mungu wetu na tunampenda kuliko tunavyowapenda mama zetu, mama yangu ananinyonyesha mwaka mmoja au miwili na ninamtumikia umri wangu wote, wakati ng’ombe ananihudumia miaka yote na hataki kwangu isipokuwa chakula chake tu. Mama yangu anapokufa ninagharamikia maziko yake, wakati ng’ombe anapokufa tunafaidika na vitu vyake vyote hadi mifupa yake.

Je ibada zenu hizi zinawapeleka peponi baada ya kufa?

Kwetu sisi hatuna pepo wala moto.

Kama ni hivyo aliyetenda mema atalipwaje na aliyefanya ubaya ataadhibiwaje? Au wote wako sawa?

Mtu mzuri atalipwa baada ya kifo chake kwa roho yake kuhamia kwa mtu mwema, na huenda akaungana na Mungu Brahma katika safari yao, ama aliyefanya uovu ni kuwa roho yake itahamia kwa mtu muovu atakayepata mateso hapa duniani.

Je mnaweza kutofautisha hapa duniani baina ya mtu mwema mtiifu na mkosaji?

Ndio, na baadhi yetu wana nafasi ya uungu hapa duniani.

Vipi hilo?

Brahma ameumba watu katika makundi mbali mbali kutokana na sehemu za kiwili wili chake, wale Brahmins aliwaumba kutokana na uso wake, na ndio maana wanakuwa ni watu wa kufikiri sana na kutumia hekima, ama Kshathriyas wameumbwa kutokana na mikono yake; na hivyo basi hao ni watu wa kutumia nguvu, watu wa kupigana na mambo ya jeshi, Vaishyas wameumbwa kutokana na mapaja yake; na hao mara nyingi kazi zao ni kuhudumia jamii katika mambo ya biashara, viwanda na kusimamia chakula, na Shudhras wameumbwa kutokana na miguu yake; nao ni wafanyakazi na watumwa na wana kazi zao. Ama ibada za Shudhras na kuhudumia tabaka tatu kubwa zilizotangulia, ama waliokuwa hawaingii katika tabaka hizo nne hawaingiii katika sehemu ya dini ya Uhindu.

Je, nikiwa katika tabaka la Shudhras je naweza kupanda cheo nikaingia katika Brahmins, au kama wewe ni katika kundi la waliotengwa unaweza kuingia katika dini ya Uhindu?

Muhali kabisa..ibada ya Shudhra ni kuhudumia tabaka tatu za juu, na waliotengwa (maluuni) hawapo katika sehemu ya mpangilio wetu.

Joji alishikwa na mshangao, na akahisi kichefuchefu kwa ubaya wa dini hii, lakini alitengeneza tabasamu na kumuachia Kapoor na kutoa hela kidogo na kumpa, akasimama aondoke kwa ahadi ya kukutana na Karimullah, kwani asije akachelewa ahadi yake pamoja nae.
Njiani, alikumbuka maneno ya Maiko alipomwambia ubaya wa dini zilizotungwa na mwanadamu (dini za ardhini) na lau angeendelea kukaa zaidi na Jiyostana basi angeichukia India yote na asingependa tena kurudi. Kwa kweli dini zote hizi zipo kinyume kabisa na mantiki ya akili na maumbile halisi aliyoumbwa nayo mwanadamu. Hata hivyo ubaya huu ni kwa dini hizi za ardhini au ni dini zote kama alivyosema Dr. Tom: “Utarudi ukiwa umechukia dini zote” hali ya Maiko mwenye dini haitofautiani na ya Kakhi, na wote hawamshindi Mutwi pamoja na vurugu yake! Alikuwa na hakika kuwa dini ya haki haikinzani na akili wala maumbile halisi wala mantiki, je dini ya namna hii ipo au la..?

(6)

Saa tatu kamili Joji alifika katika ofisi ya Sekretari wa Mutwi, aliomba kuonana na Karimullah, akaambiwa kuwa anamsubiri katika ofisi ya Sheikh, alipoingia akakutana na ndugu wawili Karimullah pamoja na Mutwi wanazungumza, walimsimamia na kumkaribisha. Alimuangalia usoni Karimullah lakini hakumfurahia, hata hivyo hakujua kwanini!

Karibu ofisini kwangu, mimi nipo tayari kuandaa na kutengeneza mkataba.

Mutwi akawakatisha:

Baada ya kumaliza ningeomba kukuona wewe Joji kabla ya kuondoka.

Na mimi kadhalika kabla sijaondoka nataka kukuaga.

Joji alikwenda akifuata na Karim katika ofisi yake, ilikuwa ni ofisi kubwa lakini ya kawaida kabisa.

Ndugu yangu amekuambia kuwa tupo tayari kwa maafikiano yatakayopelekea faida kwa pande mbili.

Ndio..wewe unafanana na mtu..!

Nafanana na Usamah bin Laden! Hahaha, wewe si mtu wa kwanza kuniambia hivyo.

Natamani usiwe mfano wake.

Mimi ni kama yeye Muislamu, lakini natofautiana nae kwa kuwa mimi ni Mhindi na yeye ni Muarabu.

Yaani sio kama yeye muuwaji gaidi.

Wachana na hayo; yeye ni gaidi kwa sababu hawawapendezi wala haafikini nanyi.

Vipi? Si yeye na wafuasi wake wanalipua mabomu katika treni, nyumba nakadhalika huko kwetu?!

Maraisi wenu wameua mara nyingi zaidi kuliko alivyofanya bin Laden lakini hamuwaiti kuwa ni magaidi, bali nchi nyingi za magharibi zimeuwa watu wengi sana katika nchi walizotawala na hamuwaoni kuwa ni magaidi, kisha akatabasamu na kusema: na wakati alipokuwa akipigana na adui yenu Mrusi mlimuita shujaa sio gaidi…hebu tuingie katika kazi yetu.

Joji alihisi kuwepo na ombwe kubwa baina yake na Karimullah, akaazima mazungumzo yoyote ya nje, amalize kazi yake tu, na kwa haraka sana akajizungumzisha kuwa huenda Tom akawa mkweli, hawa waislamu wanamtetea gaidi mkubwa katika historia ya mwanadamu!

Vizuri, haya sio maudhui yetu.

Je una muswada wa mapendekezo ya mkataba wetu, au nikupe mapendekezo kutoka kwetu?

Ninao mswada wetu lakini nipe wa kwako niusome.

Tafadhali pokea.

Naomba dakika chache niusome.

Joji alianza kusoma mswada ule, akaona kuwa vipengele ni vyepesi na vinafahamika, vimedhibitiwa kiasi, na ni bora kuliko mswada wake uliomtesa kuutayarisha, lakini unaotoa uhuru mkubwa kwa washirika wake; alimgeukia Karimullah aliyeshughulishwa na kusoma kitabu.

Nimeuona kuwa ni mzuri kabisa, ila nina maoni machache.

Ruhusa ni yapi hayo.

Je huoni kuwa kuna uhuru mkubwa wa shirika lenu, na ucheleweshaji wa fedha kutoka kwetu!

Hivi ni vipengele viwili: kwanza uhuru; ili niweze kushughulikia eneo pana la ugavi na kwa bahati mbaya mpangilio wetu si mzuri. Ama suala la ucheleweshaji wa fedha ni kwa sababu hatutaki kuahidi uongo katika mkataba wetu pamoja nanyi.

Hutaki kusema uongo, una maana gani?

Kwa kukuahidi ninakwenda kinyume na ahadi, na kama siko huru, nitahitaji kila mara kuomba samahani kwa sababu zisizo za msingi za uongo na hili ni jambo nisilolitaka, si mimi wala nyinyi. Hata hivyo masharti haya yanafanya soko lenu kuwa kubwa zaidi; na hivyo basi mtapata faida kubwa zaidi na katika mkataba kwa ulipaji wa benki kuna dhamana kamili.

Je tunaweza kutoa malipo ya kila miezi mitatu, tumekubaliana?

Tumekubaliana, nami napenda kuwa sawa pamoja nawe, ili asitujie tena Kakhi mara nyingine.

Kwanini hamumtaki Kakhi?

Nitaomba samahani kutokujibu ili isikukere.

Hutonikera kabisa, niambie kwa nini?

Hafikirii kabisa ila faida ya mali tu, na kwa njia ambayo si nzuri sote na yeye tunapata hasara, nadhani kuwa misingi mizuri inawafanya wote kupata faida, kama ilivyo tabia yake nyingine ya kutaja wanawake ambayo sisi hatuikubali, samahani sisi watu wa mashariki tuna jihifadhi zaidi.

Si neno, naafikiana nawe kwa mengi unayosema, tumeafikiana na ninasubiri mikataba ipigwe mihuri na ubalozi wa Uingereza, nami yangu nikirejea nitaipiga mihuri katika ubalozi wa India huko kwetu.

Nakushukuru, na nisamehe nilichosema kuhusu mkuu wako wa kazi.

Usijali, nataka kumuaga Mutwi Rahman kabla sijaondoka.

Haya twende.

Joji aliingia na Karimullah waliingia kwa Mutwi Rahman, alimkaribisha Joji na kumchangamkia, kisha akamuuliza:

Je mmemaliza mkataba?

Ndio.

Je ilikuwa nyepesi na kawaida kabisa kama nilivyokuambia?

Kawaida kabisa.

Kila jambo jepesi ndilo lenye kufanikiwa, na kila lililo gumu linakuwa kinyume na akili, maumbile halisi aliyoumbwa nayo mwanadamu na dini hali kadhalika…kisha akaendelea kusema: Kwa sababu mmemaliza, Joji unapenda nini India nikupeleke uone? Kutalii India nchi yenye maajabu ni vizuri.

Asante sana..ningependa kurudi hotelini mapema leo hii; nina kazi katika intaneti nataka kufanya.

Kama upendavyo, kisha akafungua droo akatoa vikasha viwili vya kifahari vyenye mafuta ya aliudi, na akasema: Hii ni zawadi yangu kwako, kisha akamuwekea katika mfuko wa kifahari, na akamwambia: Dereva anakusubiri akupeleke hotelini kwako.

Ukarimu huu wa nadra ni wa watu wa mashariki tu, nakushukuru sana, kisha akachukua mfuko na kuondoka zake.

(7)

Joji alimkuta dereva akimsubiri, pindi alipomuona akija akamfuata na kumuelekeza kwenye gari, na kumfungulia mlango:

Karibu mheshimiwa.

Asante sana. Jina lako nani?

Steven.

Oh, jina la kizungu.

Mimi ni Mkristo, ndio maana jina langu kama la kizungu.

Ukristo uliingia lini India?

Miaka mingi sana.

Je ukoloni na misafara ya kimishonari ina nafasi katika hilo?

Bila shaka, vinginevyo India yote ingekuwa ya Waislamu.

Waislamu! Unakusudia wangeichukua India yote kwa ugaidi wao?

Hapana, wewe hujui ujinga wa dini za ardhi (zilizotungwa na watu), ni dini mbovu na zenye vichekesho, kama sio misafari ya kimishonari, watu wote wangekuwa Waislamu kwa mapenzi yao.

Nimefahamu baadhi yake, lakini dini za mbinguni hazitofautiani nazo!

Ajabu! Utakuwaje mkristo kisha ukasema hivyo? Hii ni lugha ya waliokufuru!

Nachukia ukafiri na najua inavyojikinza yenyewe kwa yenyewe, hata hivyo hizi dini zinazodai zimetoka kwa Mungu hazitofautiani na hizi za watu walizojitungia wenyewe.

Ama sisi wakristo tunataka kuwatoa watu katika shaqawa yao, na tunawahakikishia usafi, na tabia njema, na sikubali mtu kutuhumu dini yangu katika hali yoyote ile, wala sikubali hilo kutoka kwa mtu kama Mutwi Rahman ambaye ni Muislamu pamoja na kuwa mimi ni dereva wake, pamoja na kuwa hajawahi kunifanyia hivyo hata mara moja, sembuse kutoka kwa mkristo kama wewe?! Lakini huenda ikawa hivyo kwa sababu wewe ni mprotestanti! Hata ikiwa hivyo sikubali!.

Sikukusudia kuutuhumu ukristo! Kwanini niutuhumu nami ni mmoja wao! Ninachokusudia ni matendo ya watu wenye dini hizi zinafanana na watu wenye kuabudu dini walizotunga wenyewe, na wanaboronga katika mambo mengi mfano wa dini walizojitungia watu..

Sijafahamu!

Je tunaweza kubadilisha maudhui haya, na kumalizia sehemu ya safari yetu kujua historia ya India?

Tumekaribia kufika, kwa ufupi Pakistan na Bangladesh na India zilikuwa nchi moja, kisha Pakistani na Bangladesh zikajitenga na India.

Kwa nini zilijitenga?

Kwa dhulma waliyokuwa wakiona waislamu wakifanyiwa na Wahindu, kisha kidogo kidogo wakajitoa kutoka India, vinginevyo India ingekuwa ni nchi ya Kiislamu.

Wewe unawatetea sana Waislamu pamoja na kuwa wewe si katika wao! ..je ni kwa sababu unafanya kazi kwao au unawaogopa?

Hahaha, pengine!