Sifa za sheria

Sifa za sheria

Sifa za sheria

Chanzo chake ni Mwenyezi mungu

Chanzo cha dini ya Kiislamu ni Muumba Mtukufu Aliyemuumba mwanadamu na Ulimwengu na vilivyomo ndani yake, na kuwa kwake imetoka kwa Mwenyezi Mungu ina ipa hadhi nyingi, miongoni mwake ni kuwa Allah ndie Muumba na ndie mtoa riziki, yeye pekee ndiye mwenye kumiliki haki ya uwekaji sheria.

Mitume wote na wafuasi wao wakitegemea mwekaji sheria kutoka kwa Allah pekee, na hubatilisha kila sheria isiyotoka kwake, Allah akimuelezea Mtume wake wa mwisho kuhusu sheria yake na muelekeo wake: “Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.” (46:9)

Kwa hiyo Mtume wa Allah pamoja na utukufu wa hadhi yake na nafasi yake ya juu kwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) anafuata sheria ya Allah anayoshushiwa yeye wahyi, yeye sie mwanzilishi, bali hufuata mfumo wake na wala haendi kinyume nao, na kuwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ndie Muumba anajua aliowaumba: “Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” (67:14)

Yeye anajua maumbile ya waja wake na yanayowafaa na yanayowaharibu, anajua zaidi yanayowanufaisha na yanayowadhuru, hakuna mwingine anayewafahamu zaidi ya aliyewaumba, na hakuna zaidi ya mtengezaji anajua zaidi yake alichokitengeneza. Allah Mtukufu amesema: “…Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu?...” (2:140).

Na kwa sababu Allah ndie aliyeweka sheria, hii inaipa sheria yenyewe uadilifu na ukweli wake. Kamwe haiwezekani Allah ampendelee mja miongoni mwa waja wake kwa ajili ya hesabu ya mja mwingine, kama ambavyo adhabu ilivyo katika Uislamu basi Yule ambaye hakuchukua haki yake duniani kwa sababu yoyote au ambaye hajaadhibiwa duniani kwa ubaya wa matendo yake, basi atakuta malipo yake akhera.

Ya kimaadili

$Anatoly_Ondrboutc.jpg*

Anatoli Andrbush

Jenerali wa Kirusi
Dini ya Utulivu.
“Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimehisi amani na utulivu na kuwa ndani ya maisha yangu kuna thamani. Nimefahamu maana ya kuwa Mungu (Allah) ambae humuoni yeye anakuona popote uwapo na huangalia matendo yako na huyapima kwa vipimo vya uadilifu ili upate malipo yako ya haki Siku ya Kiama.”

Lengo la kanuni yoyote ni kuwa kanuni haifikiwi malengo yake kwa maumbile yake bali hutegemea mwitikio wa watu wa kutekeleza kanuni na sharia ile kwa ridhaa yao na kukinai kwao, kama vile ambapo lengo la kanuni husika halifikiwi kwa uzuri wa hukumu zake pekee, lakini hufikiwa pamoja nayo kwa utekelezaji wa wale waliowekewa sheria ile, kwa sharti ya kuwa utekelezaji huu uwe unatoka ndani ya Nafsi zao na mioyo yao.

Hisia hii hutokana na imani yao ya kuwa kanuni yenyewe ni ya uadilifu na kuiridhia kwao, na itikadi ya kulipwa na mtunga sheria nao wakiridhia sheria zake na hukumu zake mbali mbali. Sheria ya Kiislamu imesimama katika kuridhiwa na kukinai kwa watu wenyewe, Allah ameamrisha kufundishwa Uislamu: “…na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao.” (4:63), “Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. Wewe si mwenye kuwatawalia.” (87:21 – 22),

ndio maana Allah akaufunga Ujumbe wa Muhammad na kutumwa kwake kwa sababu hii; Amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam): “Kwa hakika nimetumwa kutimiza tabia njema.”

Huunganisha kati ya dunia na akhera

Miongoni mwa sifa zinazopambanua sharia ya Kiislamu dhidi ya sheria ziliotungwa na wanadamu ni kuwa (Sharia ya Kiislamu) humlipa mwanadamu katika maisha ya hapa duniani na katika akhera vile vile, malipo ya akhera ni makubwa kuliko ya dunia; kwa ajili hiyo daima muumini anahisi hili na kumsukuma ndani ya Nafsi yake katika ulazima wa kutekeleza hukumu zake, kufuata maamrisho na makatazo yake na kama atakwepa malipo katika maisha ya duniani hujua fika kuwa macho ya Allah hayaghafiliki wala kulala, na kuwa watu watachukuliwa kwa wayatendayo hapa duniani mbele ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) Allah Aliyetukuka amesema: “Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?” (90:5)

Na akasema vile vile: “Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?” (90:7)

Ya kijamii

Sheria ya Kiislamu haipendelei maslahi ya sehemu moja zaidi ya sehemu nyingine wala haimpendelei mtu mmoja dhidi ya mwingine, imeweza kutatua tatizo hilo kubwa ambalo jamii zingine mbali mbali linasumbuka nalo.

Tatizo la mgongano kati ya maslahi ya mtu binafsi na maslahi ya Ummah katika jamii kama tuonavyo katika mfumo wa Kibepari wakati ambapo katika mfumo wa Kijamaa kupendelea masilahi ya jamii na kupuuza masilahi ya mtu binafsi na kupoteza na kuvunja haki ya mtu binafsi na hivyo kutupa haki ya mtu binafsi na uhuru wake na haki ya kumiliki, na hivyo basi vipaji vyake kutojitokeza na kupotea kwa utu wake na kupelekea kutotumika kwa uwezo wa mtu binafsi.

Lakini Uislamu umeweka haki kwa msingi wa usawa baina ya haki hizi za kijamii (haki) ambayo inaisimamisha; Uislamu umechunga maslahi ya jumla ya jamii ya Kiislamu, hata hivyo wakati huo huo haujaghafilika na matakwa ya Muislamu binafsi.

Katika upande wa kisiasa tunaona kuwa haki ya mtawala na kiongozi ni kupata kusikilizwa na raia zake na kutiiwa, lakini kwa sharti la kufuata sheria katika kuhukumu kwake huku akichunga maslahi ya Ummah.

Vinginevyo Uislamu unamnyang’anya haki hii; hivyo basi itapasa kumtii mtawala au kiongozi katika yasiyokuwa kumuasi Allah (Subhaanahu wa Ta’ala).

Uthabiti na kubadilika

Uislamu umesimama juu ya misingi thabiti isiyobadilika inachukuwa

vyanzo vyake kutoka katika misingi yake ya mwanzo:

Qur-aan iliyohifadhiwa na Allah: “Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.” (15:9),

Ambayo haingiliwi na batili yoyote: “Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa. ” (41:42).

Sunnah tukufu imerikodiwa nakuhifadhiwa kwa undani na umakini mkubwa na maandiko yake (nususi) mara nyingi hukusanya hukumu za uwekaji sheria bila ya kubainisha vipengele vinavyohusiana na utekelezaji wa

$Blasher.jpg*

Berisha Pennekmrt

Mwanataaluma wa Kithailand aliyetoka kwenye Ubudha na kuingia Uislamu.
Dini ya Utukufu na Ukarimu
“Uislamu ni dini ya amani, usawa, uhuru, udugu, ukarimu na utukufu, yote hayo yanaonekana wazi kwenye hukumu zake, misingi yake na taratibu zake, kwa mfano Saumu katika Uislamu si kama saumu katika dini nyingine, kwa sababu matatizo ya mwanadamu si (mtu) kukandamiza mahitaji ya mwili wake kama vile wafanyavyo watawa kiasi kwamba kiwiliwili cha mmoja wao kinakuwa kama vile hekalu la mifupa inayotembea. Uislamu umenyoosha matamanio ya kiwiliwili na haujayakandamiza; Saumu katika Uislamu unazoesha nafsi ya mfungaji kusubiri na Jihadi dhidi ya matamanio maovu yaliyoharamishwa, na kumchunga Allah katika siri na dhahiri na kujitambuza ladha ya kukosa na njaa, ili mfungaji awaonee huruma waliokosa, kama ambavyo Saumu ni fursa ya kuupa mwili raha dhidi ya kuvimbiwa. Saumu humfaidisha mtu afya yake, roho yake na akili, na katika yote kuna kujiburudisha kwake, na umoja wake.”

hukumu hizo; na hivyo kuacha uwezo mkubwa wa utawala na kukadiria kwa Mujtahidi akichunga tofauti za hali na mazingira, hata hivyo utekelezaji wa hukumu hizi bado umebaki katika kuangalia wasaa na kutokakamaa katika jambo.

Kwani lililo la msingi ni kutekeleza malengo haya bila ya kujali njia zitakazotumia au maumbo yaliyosimamia madamu hayaendi kinyume na andiko la kisheria au msingi miongoni mwa misingi ya kisheria ya Kiislamu, kwa hiyo utekelezaji wa makusudio ya jumla ya sheria ya Kiislamu kwa daraja ya juu ya wepesi na uwezekano wa kuendelea (kukua) kadhalika hakuna kizuizi katika kutokea kwa hukumu mpya ambayo haikujulikana hapo kabla kwa kuangalia kuzuka mazingira yanayoafikiana nayo.