Sheria ya Mwenyezi Mungu

Sheria ya Mwenyezi Mungu

Sheria ya Mwenyezi Mungu

Baada ya kukutana kulingana na ahadi waliyowekeana Maiko alianza kuzungumza na kusema:

Leo hii nimesoma kitabu kilichonivutia cha mmoja wa wahusika wa masomo ya Mashariki, ametaja ndani yake mambo mengi kuhusu sheria za Kiislamu, ningependa kujadiliana pamoja nanyi.

Rajev: Ni maudhui yenye umuhimu mkubwa.

Rashidi: Kama utaweza kutaja masuala haya mara moja ili tuweze kuyajadili.

Maiko: Vizuri, nitataja mengi yaliyovutia akili yangu, na si vibaya lau swali litajitokeza kutoka kwa Rajev bila ya kufungwa na yaliyokuja kwenye kitabu.

Rashidi: Karibu.

Maiko: Kitabu kile kimetaja kuwa sharia ya Kiislamu imechukua sheria za Kirumi, na baadhi ya vipengele vinafanana.

Rashidi: Niruhusu nikuambieni kuwa maneno haya ni ya zamani hata leo hii mustashrikina wengi wakubwa hawasemi maneno haya, binafsi nimekutana na mmoja wa mustashriki wa Kirusi amesomea tahasusi ya kanuni na sheria ya Kiislamu, jina lake Leornard Sukanan, na akasema maneno haya: “Kwa sasa hivi hakuna katika watafiti wa Kimagharibi mwenye kushikilia fikra kuwa sheria ya Kiislamu imechukua sheria za Kirumi, hili lilikuwa katika karne ya kumi na tisa, fikra iliyokuwepo kwa baadhi ya watafiti wa Kimagharibi. Ama leo hii fikra ya kanuni ya Magharibi inakiri bila kizuizi vifungo vyovyote-wala sharti lolote ya kuwa uwekaji wa sheria au utungaji wa sheria ya Kiislamu ni mfumo wa kisheria unaojitegemea, hauathiriki na sheria za Kirumi.”

Hili ni mosi, ama la pili: Kwa hakika chanzo cha utungaji sheria ya Kiislamu kinatofautiana kwa ukamilifu na sheria nyinginezo, kama nilivyowatajia mara nyingi ni kuwa Uislamu ni mfumo ulio kamili, kulingana na utungaji wa sheria hilo lina mhusu Muumba kwa aliowaumba kuwapa jukumu ambalo litafanikisha lengo la kuumbwa kwao, na haki yake ni kuwa asitoke katika utiifu kwa kuwazingatia wao kwamba ni watumwa wa mamlaka yake, hivyo basi chanzo cha asili cha sheria katika Uislamu ni Wahyi unaowakilishwa na Qur’an na Sunna ya Mtume, na sote sisi tunafahamu kuwa Mtume wa Uislamu alikuwa hasomi wala haandiki, ni hali ya kawaida kutopata fursa ya kusoma kwa mtu wa namna hii (mbali na kuchukua) kutoka vyanzo vingine vikiwa ni vya kigeni nae.

Haya ndio wanayosema mustashrikina David Santillan: “Tunajaribu kupata chanzo kimoja kinachobeba sheria mbili, mashariki na magharibi (Uislamu na Uroma) kama ilivyothibitika rai juu ya hilo, kuwa sheria ya Kiislamu ina mipaka rasmi na msingi thabiti haiyumkiniki kuirejesha au kuinasibisha na sheria na kanuni zetu kwa kuwa ni sheria za dini zinabadilisha fikra zetu za asilia.”

Ama yanayoweza kutokezea katika kufanana kwa mifumo ya kisheria hii inatokana na kufanana kwa matatizo ya mwanadamu, kisha kufanana kwa mapana ya suluhisho lake ambalo linaweza kutokea kwa maafikiano ambayo msingi wake ni kukadiria maslahi na ufisadi katika mazingira yenye kufanana au katika maumbile ya mwanadamu, mfano kauli ya Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) “Ushahidi ni kwa mlalamikaji na kiapo ni kwa anayekataa.”

Maiko: Lakini inabakia uwezekano wa kuchukua sheria za Kiislamu kutoka sheria za Kiyahudi na kanuni za Kanisa, kwa mazingatio kuwa ni dini mbili za mbinguni zilizoutangulia Uislamu.

Rashidi: Nitakujibu kwa jibu alilolitoa mmoja katika wanafikra wa Kimagharibi aliyehusika na jambo hili, anasema–mustrashrik wa Kijerumani Josef Shakhet: “Sharia ya Kiislamu inazingatiwa kuwa mfano wa maana yake haswa na ya kipekee katika kile kinachoitwa kanuni za dini, bali nikuwa sheria nyingine tukufu ambazo ni mfano wa kanuni za kidini zilizo karibu na sheria za Kiislamu kwa upande wa historia na jiografia (nazo ni sheria za Uyahudi na kanuni za Kikristo) zinatofautiana mno na sheria za Kiislamu na hilo ni kwa sababu sheria ya Kiislamu: ni pana mno na imebeba sura nyingi tofauti na sheria hizo zingine mbili, kwani zimekuja zikiwa natija za kuangalia na umakini zaidi kwa upande wa kidini katika maudhui za kanuni ambazo zimekuwa mbali kuliko kuchukua sura moja.”

Bali ni kuwa yeye anasema kinyume cha uwezekano unaomsukuma, anasema: “Upande mwingine wa bahari ya Mediteranian tunakuta sheria ya Kiislamu imeathiri sana matawi mengine yote ya kisheria…kuna athari ya sheria ya Kiislamu katika kanuni za dini nyingine zote kama Uyahudi na Ukristo ambazo “Rehema ya Uislamu ulizikumbatia na wakaishi katika dola ya Kiislamu…na hapana shaka kuwa matawi mawili makubwa ya Kanisa la Mashariki ambayo ni Wanestori na Wayakobo hawakusita katika kuchukua uhuru wa sheria za Kiislamu na kuzitumia, na uchukuaji huu ulikuwa katika maudhui yote ambayo mtu anaweza kusawiri kuwa yanaingia katika mtazamo wa kadhi Muislamu.

Rajev: Kama ni hivyo basi ni bora ukatuelezea kuhusu tofauti liyopo kati ya sheria za Kiislamu na sheria zingine.

Rashidi: Ni vigumu kukuelezea tofauti zilizopo, na haswa kwa sababu hukunibainishia sheria yoyote ya kulinganisha nayo, hata hivyo ninaweza kukutajia sifa ya sheria za Kiislamu, na wewe mwenyewe unaweza kulinganisha baina ya sifa hizi na nyingine. Sawa vizuri hamna neno.

Rajev: Hakuna neno

Rashidi: Sheria za Kiislamu husifika kwa:

1-Chanzo chake ni kutoka kwa Mungu – kama nilivyowatajia ni kuwa sheria hii hupokea mada zake kutoka vyanzo viwili vya msingi; Qur’an Tukufu na Sunnah za Nabii Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam). Ama nafasi ya mwanadamu ni kuchimbua kwenye sheria hiyo na kuzilinda na kuziweka katika matukio ya maisha ya kila siku, na kwa sababu chanzo chake ni kutoka kwa Mungu: Ni kuwa hukumu zake zinalenga kuunganisha watu na muumba wao.

2-Kukusanya baina ya tuli (thabiti) na zenye kubadilika, uthabiti wake upo katika: Asili yake, ujumla wake na sehemu zake, ambazo hazibadiliki wala hazibadilishwi, ambazo zinahifadhiwa na kupotea, tofauti na sheria nyinginezo, ama ulegevu wake (uwezekano wa kubadilika) upo katika matawi yake, na sehemu zake, kinachoipa uwezo wa kuzalisha sheria nyingi nazo kulinganisha na matukio na kuyafanya yafikie kila kinachojitokeza (mapya) katika zama husika.

3-Uenevu: (wakati, mahala, mwanadamu na hukumu). Zama kwa maana ya kuwa ni sheria ya karne na zama zote, mahala kwa maana inatekelezwa bila kujali mipaka ya Kijiografia, na mwanadamu kwa maana: Inazungumza na watu wote kwa hukumu zake na kwa maana ya kuwa: Imeenea sehemu zote za maisha ya mtu, kwani inamuhusu mwanadamu katika hatua za maisha yake na katika mambo yake yote, na kuishi nayo katika hatua zake zote: kichanga, mtoto, kijana na mtu mzima na kumheshimu akiwa amekufa na kuhukumu mahusiano yote ya mwanadamu na Mola wake, nafsi yake na wengineo.

4-Iko katika uhalisia, na hili linaonekana wazi pale inapochunga na kujali uhalisia wa waliokalifishwa pale sheria ilipowekwa kwao na kutangamana, kama ilivyochunga pande zote za mwili wa mwanadamu, kiroho, kiakili, mtu binafsi au kundi la watu, wala hakupuuzia nguvu ya mtu binafsi au kundi la watu katika utekelezaji wake.

5-Usawa na Unyoofu, na hili linatimia katika kulazimiana na hukumu kwa ajili ya utaratibu wa kusawazisha kati ya matangamano yote (nayo ipo kati yao), hili ndilo linaipa nguvu na kudumu; kwa mfano: Sheria ya Kiislamu imeweka andiko la mtu binafsi kutamalaki chini ya udhibiti, na kupuuza kama vile ilivyo katika mfumo wa kijamaa, na kuuwacha wazi mno kama ilivyo katika mfumo wa kibepari, na ukahamasisha katika ushujaa nao upo katikati ya ujasiri na uoga, na ukaamrisha kutoa ambalo ni jambo lililo kati ya ubakhili na ubadhirifu kama hivi.

6-Kukusanya baina ya malipo ya kidunia na ya kiakhera, sheria hii inayoafikiana na sheria na mifumo mingine ya kisheria katika kuweka malipo ya mwenye kwenda kinyume na hukumu zake hapa duniani, na wakati ambao mkono wa kanuni iliyowekwa na mwanadamu haifiki katika kumuadhibu mwanadamu katika akhera yake, wakati ambapo sheria ya Kiislamu humkamia anayekwenda kinyume kwa kumuadhibu huko akhera, hilo linakusanya baina ya malipo mawili pamoja.

7-Kujali maslahi na kutogongana na elimu katika mambo ambayo yana uhusiano nayo.

Maiko: Wewe Rashidi daima unapenda kupamba dini yako kwa uzuri na umahiri.

Rashidi: Rafiki yangu sio suala la kasumba ya dini yangu, vinginevyo nini kauli yako katika maneno ya mshairi wa Kijerumani Goethe: “Sheria katika nchi za Magharibi ni pungufu ukilinganisha na mafundisho ya Uislamu, na sisi watu wa Ulaya kwa mitazamo yetu yote hatujafikia bado pale alipofikia Muhammad, hakuna atakayemtangulia.” Hili nalo alilizungumza Goethe kwa sababu nae alikuwa Muislamu?!

Rajev: Nukta ya mwisho katika sifa za sheria ya Kiislamu inataka ufafanuzi zaidi.

Rashidi: Nitakuletea mfano wa sheria kutogongana au kupingana na elimu: Katika mambo ambayo sheria ya Kiislamu inasifika nayo ni kusisitiza aina fulani ya uchinjaji wa wanyama ambao wanaliwa, mbali na idadi ya namna nyingi za wanyama hawa na kuongezea masharti mengine, hili tu ndilo nitakalojadili, yaani njia ya uchinjaji.

Njia ya Kiislamu inataka mnyama achinjwe akiwa hai kwenye mshipa wa shingo na kutong’oa au kutoa kabisa shingo yake, hili linahifadhi harakati za misuli baada ya kuchinjwa na humpa mnyama uhuru wa kutapatapa, kinachosaidia katika kuondosha kiasi kikubwa cha damu, ama katika njia zisizo za Kiislamu za uchinjaji mnyama huchinjwa bila kutajwa jina la Mwenyezi Mungu, na katika njia zenye makosa kama kunyonga kwa gesi au kwa umeme au kwa kupigwa risasi, njia zote hizi humkosesha mnyama uhuru wa kutapatapa na misuli yake kuwa huru; kiasi cha kusababisha mwili kubanwa na damu na hivyo damu kubaki katika kiwiliwili cha mnyama na unapelekea kusababisha bakteria wengi kuwepo na pindi damu hii inapotumbukia (mwilini) inazalisha sumu ndani ya mwili wa mwanadamu, na nyongeza ya hilo njia hizi zina mfanya mnyama kuumia kwa maumivu.

Lakini niachie nikuongezee nyongeza nyingine, sharti la kumtaja Mungu wakati wa kuchinja, pamoja haja ya hilo kwa mtazamo wa kimaada ambao haujali isipokuwa kumuua tu mnyama kwa ajili ya kumla, ama katika Uislamu kila kitu kimeunganishwa na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu na sheria imeunganishwa na mfumo kamili wa Dini kulingana na majibu ya maswali makubwa (Mungu, ulimwengu, mwanadamu na mwisho wake), Na katika hali hii mwanadamu kwa wasifu wake kuwa ni kiumbe katika viumbe vya Mwenyezi Mungu hana haja ya kuwafanyia uadui viumbe wengine na kutoa roho zao, isipokuwa kwa idhini ya Muumba wa kiumbe hiki, kwa lengo la kusimamisha maisha yake tu, hivyo basi kumtaja Mungu na jina lake ni kuomba ruhusa ya kutangaza mamlaka ya Mungu Mtukufu na kuwa tendo hili linalofanywa na Muislamu ni kwa ruhusa ya Mola wake aliyemhalalishia tendo hili, na ya kuwa Muislamu yupo katika unyenyekevu mkubwa kwake.

Maiko: Nikiri kwako kuwa ili kuweza kufahamu kwa kina sheria za Kiislamu na siri zake unahitaji ufanye utafiti wa kutosha.