Safari ya Milele

Safari ya Milele

Safari ya Milele

Maiko aliwasalimu rafiki zake pindi tu alipoingia katika chumba cha mazungumzo, Rajev alijibu maamkizi wakati ambapo Rashidi alisema;

Ni subirieni kidogo…. Na watayarishia onesho lenye kusisimua. Je, mmeona onesho la kuanguka kwa Piermario Morosini mchezaji wa timu ya Levono katika mchezo wake na timu ya Pescara katika ligi ya Italia….alikufa papo hapo kutokana na kusimama kwa moyo….ulikuwa ni mshtuko kwa watazamaji wakimuona anakata roho.

Maiko: Lakini la ajabu zaidi kuhusu tukio hilo: Ni tukio la kuanguka kwa mchezaji wa timu ya Bolton, Fabrice Ndala Muamba pindi timu yake ilipocheza na timu ya Tottenham katika kombe la F.A. Uingereza, mchezaji alianguka huku akipoteza fahamu huku moyo wake ukiwa umesimama, na watu wote walijua ameshakufa, katika hali isiyokuwa ya kawaida moyo wake ulirejea tena kufanya kazi baada ya kusimama kwa dakika sabini na nane na hili madaktari walilisema kuwa ilikuwa ni kifo cha dakika 78, kilichomfanya daktari wa timu Jonathan Tobin kuzungumza kwa kustaajabia hali hiyo kwa kusema: “Ni jambo ambalo mtu hawezi kuliamini, hatukuwa na matarajio ya kupona Muamba katika hali hii”, Muamba alikufa na akarejea tena katika maisha.

Rashidi: Mauti ni ukweli pekee ambao watu wote wanaukubali….lakini ni nini baada ya mauti? Je, ni mwisho, ama baada yake kuna mwanzo mwingine (siku ya mwisho) kama wanavyoamini watu wengi?

Rajev: Imani ya siku ya mwisho ni itikadi ya asili aliyoibeba mwanadamu tokea kuanza kwake kuishi ardhini, dalili nyingi na athari na kumbukumbu za kihistoria zimethibitisha kuwa itikadi hii ilikuwepo katika staarabu nyingi za zamani, Wamisri wa kale walijua hilo, kabila la Maya na Waroma na katika bonde la Ar-Rafidiyn na nyinginezo…ni itikadi ambazo hakuna dini yoyote ya mbinguni haikuacha kuiamini, hata dini zilizotungwa na wanadamu waliamini kama vile Brahma, Budha, Majusi, n.k.

Rashidi: Ulichosema ni sahihi, na itikadi hii imeita kuamini Mtume wa Uislamu, kama ambavyo mitume waliitangaza na kuonesha kwa watu, na imani hii ni sharti katika masharti ya mtu kuwa Muislamu katika zama na zama, kwani hakuna maana ya kumuamini Mwenyezi Mungu, vitabu vyake na Mitume yake bila ya itikadi hii.

Maiko: Hata hivyo mimi nimeona kuwa athari ya itikadi hii katika maisha ya watu yanatofautiana, kama ambavyo wachache miongoni mwao huichukua na kuiweka katika hisia na matendo yao.

Rashidi: Kweli kabisa, watu wote hilo wanalithibitisha katika kiwango cha itikadi ya nadharia, lakini wachache tu miongoni mwao ndio ambao wanaweka kwenye hisia zao itikadi ile ikiwa hai katika uhalisia….na ushahidi wa hilo: Tunapofikiria mlio wa filimbi ya hatari inayotokana na mashambulizi ya anga wakati wa vita…..ni katika hali ya kawaida ya tabia katika hali hiyo kutarajia barabara kuwa tupu kwa wapita njia na shughuli, kiasi cha kuwa asiyefanya hivyo itasemwa kuwa ni mpumbavu au mwendawazimu…. Ikiwa hilo ni kwa jambo dogo tu la duniani, itakuwaje hatari kubwa kuliko hiyo….hatari ambayo watu wanaamini kuwa lazima itatokea, na Mola wa ulimwengu huu ametahadharisha na kuitangaza kwa ndimi za Mitume wote, ilikuwa ni hali ya kimantiki kukubali kwao onyo hili kuwe ni kukubwa zaidi.

Maiko: Nadhani sababu katika hilo ni kuwa watu wanaona na wanasikia hatari inayopigwa na filimbi hiyo, hata kama hali hizo hawaja zijaribu basi watakuwa wameona katika hali zingine au katika nchi zingine na watakuwa wameona athari zake. Ama kuhusu siku ya mwisho ni jambo lililotenganishwa na ukuta wa kifo baina yetu na hiyo siku, na hilo halionekani kwa macho yetu leo na hili ndilo lillopelekea makundi ya yakini kati ya hali mbili.

Rashidi: Maneno yako ni sahihi, lakini kinachotakiwa ni kuwa mwanadamu anatakiwa afikie kwenye ukweli ambao atakinaishwa nao mwenyewe kwa akili yake na sio tu kwa hisia zake. Sababu kuu ya udhaifu wa yakini kwa watu wale ni kwa sababu hawatumii jicho la akili yao, kwani wanapoangalia jambo kwa makini na kutumia fikra zao wangediriki kuwa wanachokiona kwa macho yao haishindi yakini ya kile ambacho kiko mbali katika mtazamo wao.

Kisha kuna mambo kusubiri kuyaona au kuyajaribu ni maangamizi kwake; kwa sababu hayavumiliki ila tu kupita mara moja tu; ikiwa mtu akishindana na mtu mwingine akamwambia kuwa anaweza kujitupa kwenye jengo refu bila kuumia na kupatwa na lolote, na huyu mtu mwingine akamwambia, basi tujaribu hilo! Kwa hakika hilo litakuwa jaribio la mwanzo na la mwisho la mtu huyu na utakuwa ndio mwisho wake, hivyo basi katika jaribio hili hatuwezi kuthibitisha usahihi wa madai hayo au makosa yake, lakini kuitumia akili na kuangalia yaliotangulia na lenye kufanana nayo yanatuwezesha kufikia kwenye matokeo yanayo tarajiwa ya uzoefu bila ya kuyaingia au bila ya kuyafanya.

Rajev: Hivyo basi, ni juu yetu ili tufikie yakini hii tuipe hoja imani hii kwa dalili za kiakili na mitazamo ya kisayansi.

Rashidi: Hamna neno katika hilo, lakini ninasema kuwa dalili kubwa katika hilo ni kuamini ukweli wa aliyetuambia hilo. Naye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ndimi za Mitume wake, na huu ndio muktadha wa imani hii ya kumuamini Mtukuka, kwani yeye ndie anayejua kuliko sisi na mwenye kujali zaidi kuliko sisi kwa yale yenye kutufaa na kutunufaisha.

Ama ulichokitaka katika dalili za kiakili na vithibitisho vya kisayansi, ni vingi sana… miongoni mwavyo ni:-

Hoja ya Kwanza: Hoja ya kufufuliwa: Ikiwa tumekiri kuwa Mwenyezi Mungu ndie aliyetuumba mara ya kwanza, basi yule aliyetuumba mara ya kwanza kutokana na kuwa hatukuwa kitu hashindwi kutufufua tena baada ya mauti, bali uwezekano wa kutokea maisha mengine ni wenye nguvu (kinadharia) kuliko uwezekano wa maisha ya mwanzo.

Hoja ya Pili: Kutoweza kupatikana kwa vitu kutoka hali moja kwenda nyingine na kutoka katika mazingira fulani kwenda mengine, Qur’an imetupigia mifano ambayo tunaweza kuijaribu kwa watu wote, nayo ni moto kutoka kwenye mti mibichi (kijani), ambaye anaweza kutoa kitu kwenye kinyume chake, na kunyenyekea kwake maada na viumbe hashindwi kuhuisha mifupa ikiwa ni majivu.

Hoja ya Tatu: Kubadilika viumbe, mauti kisha uhai, kisha mauti kisha uhai, kutoka katika punje lisilo na uhai ndani yake kunatoka mmea wa kijani unastawi na kuzaa, kisha mmea huu kutoa mmea ulio hai ambao nao hutoa punje za mbegu zisizo hai ambazo hazioti, na kutoka kwa ndege hai hutoa yai mfu, kutoka katika yai hili hutoka ndege hai mwenye kutembea kwa mara nyingine. Hivyo basi uhai umejificha katika ambacho tunadhania hakina roho na maiti… vivyo hivyo mwanadamu na wanyama wote.

Hoja ya Nne: Kushuhudia wazi kufufuliwa katika maisha ya mwanadamu, mnyama na mimea, mwili wa mwanadamu wa kawaida una seli zipatazo 260,000,000,000,000,000 zinabadilika kila sekunde, zinapungua kwa haraka, na upungufu huu unazibwa na chakula; hivyo mwili wa mwanadamu hubadilika wenyewe kwa wenyewe kama vile mto upitao, vivyo hivyo mwili wetu huwa chini ya mabadiliko ya mara kwa mara, kiasi cha kufikia muda ambao haitobakia ndani yake seli yoyote ya zamani katika kiwiliwili chake….tendo hili hukariri kwa vijana na watoto kwa haraka, wakati ambapo huenda pole pole kwa wazee.. mabadiliko haya hutokea mara moja kila baada ya miaka kumi.

Katika hili tunajifunza kuwa miili yetu ya kimaada hubadilika mara kwa mara, ama mwanadamu kwa ndani habadiliki: Elimu yake, desturi zake, kumbukumbu zake, matarajio yake, fikra zake…. Vyote hubakia kama vilivyokuwa. Lau ingekuwa mwanadamu anakwisha na kubadilika (kama seli) basi kwa uchache mabadiliko yangekuwa ni makubwa zaidi….na hili linathibitisha kuwa maisha ya mwanadamu ni mengine na sio kiwiliwili peke yake, nayo ni yenye kubaki pamoja na kiwiliwili kubadilika mara kwa mara kwa kubadilika kwa seli zake.

Hoja ya Tano: Elimu leo hii inaashiria kuwa vyombo vya ulimwengu vinasajili matendo yote ya mwanadamu, katika malengo muhimu ya akhera ni: Kulipwa watu kwa matendo yao hapa duniani yakiwa ni kheri au yakiwa ya shari, kulingana na matendo ya mwanadamu yalivyosajiliwa na matendo hayo yanakusanya nia ya mtu, maneno yake na matendo….na ushahidi wa kisayansi unathibitisha kwamba hayapotei bure; bali kuna uwezekano wa kuyajua na kuyarejea baada ya kwisha kwake.

Hivyo basi fikra au nia ambazo zinapita akilini mwetu na kuzisahau…tunayaona usingizini au tunayazungumza katika hali ya Historia au wendawazimu bila ya kujua, na hili linathibitisha kuwa akili au kinachohifadhi sio yale ambayo tunayahisia peke yake, bali kuna pande zingine katika hifadhi hii ambayo hatuihisi nazo zipo zikiwa zinajitegemea, na sayansi imethibitisha kuwa sisi hatuna uwezo wa kuzifuta.

Ama kauli kuwa sayansi ya leo hii imethibitisha kuwa sauti ambazo tunazisikia ni mawimbi katika hewa na imethibitika kuwa kipande cha mawimbi haya hubakia baada ya kutokea kwake kwa mara ya kwanza, na kuna uwezekano wa kuisikia tena kwa mara nyingine baada ya kupita karne na karne, hata kama wanazuoni hawakuweza kutekeleza kivitendo hadi sasa, na hili linathibitisha kuwa kila anachozungumza mwanadamu kinarekodiwa.

Ama suala la kufanya kazi, utasadiki katika hali inayoshangaza uwezekano wa kutokea akhera, sayansi leo hii inathibitisha kuwa harakati zetu zote na matendo yetu yapo katika mwanga au kiza na yote yapo katika anga katika hali ya picha, na inawezekana wakati wowote kukusanya picha hizi, kwa hiyo miili isiyo na uhai inayotembea hutoa joto muda wote, na hivyo kwa upande wake huakisi mambo ya kiwiliwili na pande zake, na kuna chombo makini kimevumbuliwa chenye kuchukua picha ya mawimbi ya joto yanayotoka kwa kila kiumbe, lakini vitu hivi haviwezi kupiga picha mawimbi ya joto ila baada ya masaa machache ya tukio lenyewe.

Maiko: Kama tutakubaliana kwa hitimisho la kutokea siku ya mwisho, na tukajua nafasi yake katika Uislamu, sasa ni alama zipi muhimu za itikadi hii?

Rashidi: Vipengele vya itikadi hii katika Uislamu vinatofuatiana sana na yaliyokuja katika dini nyingine, hata hivyo tunaweza kufupisha kwa haya yafuatayo:-

Kwamba Mwenyezi Mungu atafuta ulimwengu huu, na vyote vilivyomo katika viumbe, katika siku inayofahamika kama siku ya kiama.

Kisha yeye Mtukuka atawafufua kwa mara nyingine, na atawakusanya mbele yake, na huko ndio kukusanywa na kufufuliwa.

Kisha atawaweka katika mahakama ya Kiungu kila mtu atakachokuwa amekipata kama vile kheri au shari katika maisha yao duniani, bila ya upungufu au nyongeza.

Mwenyezi Mungu anapima kila tendo la mtu katika matendo mema au maovu, ambae matendo yake mema yamezidi basi atasamehewa, na ambae makosa yake yatazidi basi ataadhibiwa.

Wale watakao samehewa wataingia peponi na wale watakaoadhibiwa wataingizwa motoni.

Rajev: Kweli, jambo hili ni zito mno.