Nuru ya Mbinguni (Haja ya Watu na Utume)

Nuru ya Mbinguni  (Haja ya Watu na Utume)

Nuru ya Mbinguni
(Haja ya Watu na Utume)

Rashidi alipoingia Social Lounge katika nyumba ya vijana waliyokuwa wakikaa, alikuta Maiko amekaa katika moja ya meza akiwa anaangalia sakafuni kama vile anachunguza taa zilizoning’inizwa humo. Rashidi alimuelekea na kumsalimu… Maiko hakutanabahi kufika kwa Rashidi…alivuta kiti na akamuelekea, na akamsemesha:

Inaelekea umeshughulishwa na kitu muhimu….. naweza kushirikiana nawe kwenye jambo lako?

Maiko: Ooh….samahani, sikugundua kufika kwako.

Rajev hajafika bado?

Rashidi: Imebakia dakika tano kwa ahadi yetu….

Huyo anatujia…

Rajev: Salamu njema rafiki zangu.. Nimefurahi kukutana nanyi.

Rashidi: Na sisi hali kadhalika.

Maiko: Kwa hakika mimi ni mwenye furaha kwa kuingilia nukta hii, hivyo basi: Ni nini lengo ambalo Mungu ameumba ulimwengu na binadamu na akampa neema zake?

Rajev: Nilikuwa nafikiria nukta hii hii kabla sijafika hapa.

Rashidi: Maswali yenu ni mazuri sana, na katika sehemu yake..Hakika Mwenyezi Mungu aliyeumba wanadamu katika umbo bora, na akawadhalilishia yaliyomo ardhini na kuwateremshia kheri nyingi kutoka mbinguni, akili haiwezi kufikiri kuwa yote haya yameumbwa kwa mchezo tu na bila ya kuwepo kwa malengo.

Maiko: Vizuri sana kuzungumzia nukta hii, kama ni hivyo basi: Ni lipi ambalo Mwenyezi Mungu ameumba ulimwengu pamoja na watu na kuwapa neema?

Rajev: Nataraji hilo linaambatana na sifa za Mungu wa kweli ambazo imetangulia kutajwa katika mjadala uliopita, kwani Mungu alikuwepo kabla ya kuwepo viumbe hawa… hata hivyo siwezi kufupisha hilo kwa ukamilifu.

Rashidi: Sahihi kabisa ulichokitaja Rajev, nami najaribu kuainisha na kuleta karibu kwa mfano huu ambao naukusudia katika kulinganisha na sio kufananisha: Wewe unapopenda kitu basi utapenda uhakika wake halisi …. Au sivyo?

Rajev: Ndio, bila shaka.

Rashidi: Kama ni hivyo basi, nini kinachoweza kukuzuia kukitekeleza kiuhalisia?

Rajev: Sababu ambayo inaingia kichwani mwangu sasa hivi: Ni kutoweza kulitekeleza.

Rashidi: Utakapofanikisha uwezo huo basi utaupata….na hili ndilo jambo lenyewe.

Maiko: Mfano wako huo umezidi kunifumba na sio kunifumbulia.

Rashidi: Katika hilo una haki, lakini nitakamilisha, tulikubaliana katika mjadala wetu uliopita kuwa Mungu ana sifa nzuri, na miongoni mwa sifa hizi ni sifa zenye kupendwa; Mungu mtukufu na viumbe wake wanazipenda, na katika sifa hizi ni kuwa yeye Mungu mtukuka: Muumba ni Muweza, Mfalme na mwenye kupenda sifa hizi anahitaji kuzitekeleza.

Na kwa sababu Allah Ta’ala ni muweza, hakimzuii chochote katika kutekeleza matakwa yake, hivyo basi Mungu ameumba viumbe ili wawe ni athari katika athari za sifa zake zenye kupendwa; na kwa sababu yeye ni Muumba basi hupenda kuumba, na kwa sababu ananeemesha hupenda kuneemesha, na kwa sababu yeye ni Rahimu hupenda kurehemu, na kwa kuwa yeye ni Muweza basi hakuna kitu kinachoweza kumzuia katika kutekeleza kila ayatakayo.

Maiko: Kama ni hivyo: Ni nini sehemu yetu katika fomula hii?!

Rashidi: Nafasi yetu ni kuwa Mungu ametuumba ili tumtambue na tumtakase na mapungufu na aibu, na akatupa neema, sio tustarehe nazo tu, bali vile vile tumshukuru yeye juu ya hizo wala tusizipoteze, kwani yeye ni Mtukufu, anapenda kushukuriwa na kuhimidiwa, na hili linapelekea kumnyenyekea (ibada yake) peke yake, kwani yeye pekee ni mwenye kuneemesha na Muumba anayestahiki kufanyiwa ibada.

Rajev: Maneno yako yanaelea katika nukta mbili; Ya Kwanza: Je, maana yake abaki mmoja wetu hekaluni ili afanikishe unachokisema kuhusu maana ya uja kwa Mungu?

Rashidi: Hapana, hapana, sijakusudia ulichokitaja katika uchunguzi wako, maana hii ya uja kwa Mungu ni maana finyu haikubaliwi na Uislamu ambayo ndio dini yangu, uja na Ibada kwa Mungu kwa maana yake pana inahusisha maisha yote ya mwanadamu, pamoja na kuendeleza dunia yake na kusimamisha ustaarabu wa mwanadamu na utu wake.

Maiko: Lakini sisi tunaimarisha (tunaendeleza) ardhi na tunasimamisha ustaarabu wetu bila kurejea kwenye dini.

Rashidi: Ndio maana tunaona mashaka makubwa ya wazi ayapatayo mwanadamu ni matokeo ya ustaarabu huu. Kama vile kuenea babaiko, hofu, woga na wasiwasi. Watu kujiua, mparaganyiko wa kijamii, mwanadamu kumdhulumu mwanadamu mwenzake, haswa anapojua hakuna wa kumchunga… na hilo linakuwa ikiwa watu wameelekea zaidi katika u-mamboleo (usasa), yaani mifumo ambayo inajali vitu na uvumbuzi na kuviendeleza, wakati ambapo ubinadamu unapotea; ikiwa tutazingatia suala hili la utu basi hapana budi kuchunguza yanayojenga ubinadamu na kilicho muhimu zaidi ni ile roho yake, na tunapounganisha ustaarabu na kuhusisha na nishati za mwanadamu kwa Muumba wa mwanadamu basi pande zake zote zitashikamana na utu wake, bali pamoja na ubinadamu wote, pamoja na ulimwengu wote, kwa uchache ni kuwa ambaye amemuumba mwanadamu huyu na ulimwengu huu ni mjuzi zaidi kwa yanayomfaa na yasiyomfaa.

Maiko: Je, ina maana kuwa Mhandisi Rajev kwa mfano ili awe mfanisi wa kazi yake ni vizuri arejee kwenye vitabu vya dini? Hilo litawezaje kuwa? Kisha tukikubaliana na maneno yako vipi tutaweza kufikia yale ayatakayo Mungu ili maisha yetu yanyooke?

Rashidi: Maneno yangu hayana maana kuwa dini isiingilie masuala ya kitaalamu katika sayansi, lakini inaweka kanuni na misingi ya kimaadili ya matendo na ni sharti zetu katika maisha yetu, na mfumo au utaratibu ambao tutaufuata katika maisha yetu, kama vile utaratibu wa mahusiano yetu na wengine katika wanadamu, pamoja na jamii yake, kati ya jamii zingine, ongezea kumfahamisha mwanadamu huyu nafasi yake hapa duniani, na uhusiano wake na Mola wake.

Nitawapigieni mifano miwili ili kuwawekea wazi: Mungu Mtukufu ametuumba na ameumba ardhi na yaliyo juu yake, na akatuoteshea chakula katika ardhi kutokana na maji aliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha akatuoteshea dawa na sumu zenye kuuwa na akatuzawadia uwezo katika akili zetu kuvitumia ili tujue yenye kudhuru na yenye kulisha, na akatupa uwezo kutumia uzoefu wetu katika kugundua mimea hii na kunufaika nayo na kutoa madawa ndani yake, kisha akatuwekea kanuni katika dini yake: “Kila chenye kutudhuru na kuwadhuru wengine ni haramu kwetu kufanya.’

Na mfano mwingine: Watu wote wanakubaliana na uzuri wa uadilifu na ubaya wa udhalimu, lakini tunapoingia kwa kina na kuangalia uadilifu huu, tunaona tofauti kubwa; kuwa akili zimetofautiana kwa malengo yake na makusudio yake, ongezea kugongana kwa maslahi katika kila kundi, hivyo basi: Sisi tuna haja ya kuwa chanzo cha uadilifu huu iwe ni kwa anayemiliki utawala wa juu kwa wanadamu wote, ambapo watu wote watakuwa sawa mbele yake, na upendeleo wa kundi au kuelemea au kunufaisha sehemu fulani utaondoka.

Ama namna ya kufikia katika maarifa ambayo Mungu anatutaka tuwe nayo; hilo limeunganishwa vile vile na sifa za Mungu Mtukuka, kwani Mungu Mtukuka ni mfalme na mwenye hekima… hili linaunganishwa na yale tuliyoyataja hapo kabla kwenye mjadala wetu kuwa Mungu ameumba ulimwengu huu kwa hekima na wala hakuumba kwa mchezo…Je, inafaa kuwa ni katika hekima kuwa na shirika ukaasisi na kujenga majengo yake na wafanyakazi wake kufanya kazi na kuzalisha na kutangaza bidhaa zake bila ya kuwepo utaratibu wa kazi na uongozi, na kanuni zinazowaongoza!!!

Maiko: Bila shaka hapana.

Rashidi: Basi unafikiriaje kuhusu ulimwengu huu na viumbe hawa …ndio maana Mungu akateremsha vitabu vyake ambavyo ni mikataba, ili iwe ni muongozo wa watu na kiongozi chao katika manufaa yao ya kidini na dunia, na hilo ni kupitia mabalozi baina yake na waja wake, ambao ni Mitume yake walio miongoni mwa waja wa Mola. Akawabainishia maamrisho yake na makatazo yake ili wawafundishe watu kuhusu Mungu wao na kuwaelekeza kwenye alama za uadilifu na madhara ya dhuluma na udhalimu, kadhalika wawabainishie watu kinacho wanufaisha na kinacho wadhuru katika dunia na akhera yao.

Kwa hiyo mwanadamu ni mwenye haja kubwa ya ujumbe kwani yupo baina ya harakati mbili: Harakati moja inamvuta katika yanayomnufaisha, na harakati nyingine inamkinga na yenye kumdhuru, na Ujumbe huu ni kama mwangaza ambao utambainishia yenye kumnufaisha na yenye kumdhuru, nayo ni nuru ya Mungu katika ardhi yake na uadilifu wake baina ya waja wake.

Lengo la ujumbe sio kutofautisha kwa hisia kati ya chenye kunufaisha na chenye kudhuru, kwani hilo hutokea kwa wanyama wasio na akili; punda kwa mfano hutofautisha kati ya shairi na udongo. Kinachokusudiwa ni kutofautisha kati ya matendo ambayo humdhuru mtendaji katika dunia yake na akhera yake, na matendo ambayo yatamfaa hapa duniani na kesho akhera na kama sio ujumbe basi akili isingeongoka katika kujua yatakayomfaa na kumdhuru katika maisha yake.

Rajev: Ama nukta ya pili ni: Tunawaona watu wanatofautiana katika mtazamo wao kuhusu Mungu na namna ya kumnyenyekea na kumuabudu, sasa iweje wawe sawa sawa katika kustarehe kwa neema zake?!

Rashidi: Hii inatokana na hekima ya mitihani na uchaguzi ili kudhihirisha mtazamo wao kuhusu Mola wao, lakini kamwe hawawezi kuwa sawa katika malipo na marejeo yao, na malipo haya yatakuwa ndio msingi wa ujumbe wa Mitume ambao upo kwa sura ya sheria na mkataba ambao mtu anatakiwa kuurejea.

Maiko: Naongezea nukta ya tatu, nayo ni: Vipi watu wote wanaweza kufaidika na neema ya Mungu, wakati katika watu hao yupo muongo, tapeli na dhalimu, na wengineo wanaweza kukwepa adhabu zilizowekwa na jamii na sheria haiwezi kumfanya kitu?!

Rashidi: Hili pia ni katika hekima ya mtihani na majaribio, lakini watu hao wakikwepa adhabu na jamii kutekeleza adhabu juu yao, basi bila ya shaka hawataweza kukwepa uadilifu wa Mungu juu yao, na hili ni katika hukumu ya ufufuo na hesabu baada ya kifo katika Siku ya Kiama na malipo, yaani malipo kwa matendo mazuri na mabaya kwa Mungu, kwake binafsi na kwa watu wengine, katika siku hii yatakuwa malipo na hukumu ya haki kwa watesi.

Hata hivyo, hapana budi kuwepo kwa rejea watu wakihukumiana juu ya msingi huo na wawe wanalifahamu hilo na wanaweza kurejea…. hapa vile vile inakuja zamu ya ujumbe wa Mitume wa Mungu ambao watawaeleza watu msingi ambao watahesabiwa nao na ambao watawafahamisha ni nini kitakachotokea kwao kwa kwenda kinyume na msingi huu, na ambao watawajulisha watu maisha yajayo ya akhera yatakayo kuwa katika neema na adhabu chungu iumizayo, na nini kitakachotokea siku hiyo.

Rajev: Bwana Rashidi, je, unakumbuka kuwa tulizungumzia umuhimu wa mjadala kuhusu sifa au vigezo vya dini ya haki?

Rashidi: Sawa nakumbuka hilo.

Rajev: Nadhani umeshafikia muda wa kufungua faili hili.

Maiko: Ni kweli Rajev, nadhani tutenge mjadala wetu ujao kuhusu maudhui hayo.