NI UPI UJUMBE ULIOBAKIA?

NI UPI UJUMBE ULIOBAKIA?

NI UPI UJUMBE ULIOBAKIA?

Kujisalimisha kwake kwa Allah

$Thomas_Carlyle.jpg*

Thomas Carlyle

Mwandishi wa Mwanahistoria wa Scotland.
Mwenyezi Mungu hana Mshirika.
“Hakuna Mungu isipokuwa Allah peke yake hana mshirika. Yeye haki na kila asiyekuwa yeye ni batili, ametuumba na ameturuzuku. Uislamu ni kujisalimisha kwa Mungu, kumnyenyekea yeye, kutulia kwake na kumtegemea yeye tu–na kuwa nguvu yote iko katika (istiqama) kunyooka katika hekima yake, na kuridhika kwa mgawo wake kadiri itakayokuwa katika dunia hii na katika akhera. Na kwa kadiri yoyote Allah atakavyotupa mtihani (na hata ikiwa ni mauti) basi inatakiwa kupokea hayo nyuso kunjufu na nafsi zenye ghera, zenye kuridhia vile vile na kujua kuwa hayo ni kheri na kuwa hakuna kheri zaidi ya hayo, kwani ni upumbavu mtu kuweka ndani ya akili yake dhaifu mizani ya Ulimwengu na hali zake, bali ni juu yake kuamini kuwa Ulimwengu una sheria adilifu, na hata kama itapotea katika ufahamu wake, na ya kuwa kheri ndio msingi wa ulimwengu, na kutengeneza (Islahi) ni roho ya ulimwengu…ni juu yake kufahamu hayo na kuamini na kufuata katika utulivu na Ucha-Mungu.”

Dini zote zimejiita kwa jina la mwanzilishi wake au kwa jina la taifa alilotumwa, hivyo basi kunasibishwa jina “Zoroaster” kwa dini ya uzorosti (Zoroastianism) na “Budha” kwa ajili ya dini ya Ubudha, na kwa sababu Uyahudi ulitokeza kwa kabila la Yahudha (Jehova), ndio maana ukaitwa Uyahudi na Ukristo kutokana na Kristo, tofauti na Uislamu ambao haujafungamanishwa na mtu au taifa fulani, bali kila mwenye kujisalimisha kwa Allah Mtukufu, na kutekeleza maamrisho yake na kukatazika na makatazo yake, mwenye kunyenyekea kwake peke yake, basi mtu huyo atakuwa amejisalimisha nafsi yake kwa Allah Ta’ala.

Yule ambaye atamfuata Mtume wa mwisho Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) na akaelekea katika dini ya haki ambayo amekuja nayo, na kuamini na kumfuata; huyo ndie Muislamu wa kweli, vyovyote awavyo katika zama zozote au mahala popote, na katika rangi yoyote au jinsia yoyote ile.

Dini ya Ulimwengu wote

$Gustaf_Lubon.jpg*

Gustaf Lubon

Mwanahistoria wa Kifaransa.
Hakuna tofauti kati ya Muarabu na Muajemi.
“Waislamu, hawaonani wageni vyovyote vile watakavyotofautiana mataifa yao, vivyo hivyo katika miji ya Waislamu (Daarul Islam) hakuna tofauti kati ya Mchina Muislamu na Muarabu Muislamu katika kufaidi haki zao. Kwa sababu haki za Kiislamu zinatofautiana na haki za wazungu (Ulaya) na hii ni tofauti ya msingi kabisa.”

Uislamu ndio mwendo unaokwenda nao ulimwengu huu, Allah amesema: “Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumt’ii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa?” (3:83),

Kwa hiyo inafahamika kuwa kila kitu hapa ulimwenguni kinafuata kanuni maalumu, na mwendo maalumu thabiti; hivyo basi jua, mwezi, nyota, ardhi na sayari nyingine zipo chini ya kanuni za kudumu (zisizobadilika) haziwezi kujiondosha au kutembea nje ya mzunguko wake walau kwa kadiri ya unywele, hata mwanadamu kama utazingatia hali yake itakubainikia wewe kuwa ananyenyekea utaratibu wa Allah unyenyekevu kamili.

Mwanadamu huyu hapumui wala hahisi haja yake ya maji, chakula, mwanga, joto ila kulingana na makadirio ya Allah yaliyopangilia maisha yake kwa utaratibu maalumu, na makadirio haya ndiyo yanayoongoza viungo vyake vyote; hivyo basi wadhifa na kazi mbali mbali zifanywazo na viungo hivi havisimami vyenyewe ila kulingana na alichokadiriwa yeye na Allah.

Makadirio hayo ya jumla yenye kukusanya ndio ambayo mwanadamu anajisalimisha kwake wala hakiondoki kitu katika utiifu wake katika ulimwengu huu, kuanzia sayari kuwa mbinguni hadi punje ndogo ya mchanga ardhini, yote ni katika makadirio yake Mwenyezi Mungu Mfalme Mtukufu mwenye kukadiria mambo; ikiwa vitu vyote mbinguni na ardhini na yaliyo baina yake huongozwa na makadirio haya, inatubainikia kuwa; Uislamu ni dini ya Ulimwengu wote; kwa sababu Uislamu una maana ya kufuata amri ya mwenye kuamrisha na kuacha makatazo yake bila ya kupinga. “Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.” (45:13).

Ama mwanadamu ambaye hamjui Mola wake na anakana uwepo wake pamoja na dalili zake, au kuabudu asiyekuwa Yeye na kumshirikisha na asiyekuwa Yeye, apende asipende mtu huyo anakuwa amejisalimisha kwake kwa maumbile yake aliyoumbiwa nayo.

Ama mwanadamu anashindana na mambo mawili:

Jambo la Kwanza:

Ni maumbile ambayo Allah amewaumbia nayo wanadamu kama vile kujisalimisha, kunyenyekea, na mapenzi ya kumuabudu Yeye Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na kujikurubisha kwake.

Kadhalika kupenda anavyopenda Allah kama vile haki, kheri, ukweli, kuchukia anachokichukia Allah ikiwemo batili, shari, jeuri, dhuluma na yanayofuata hayo katika nyenzo za maumbile ya mwanadamu kama kupenda mali, familia, watoto, hamu ya kula na kunywa, kuoa na yanayohitajiwa katika hayo ili viungo vya mwili kufanya kazi zake.

Jambo la Pili: Matakwa ya mwanadamu na Uchaguzi wake, wakati ambapo Allah amekwisha mtumia Mtume na kumteremsha vitabu; ili apambanue baina ya haki na batili, uongofu, upotevu, kheri na shari, na akampa akili na ufahamu ili awe na uoni katika uchaguzi wake; akipenda atafuata njia ya kheri ambayo itampeleka katika haki na uongofu, na akipenda kufuata njia ya shari ambayo itamwongoza katika shari na maangamizi: “Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae. Hakika Sisi tumewaandalia wenye kudhulumu Moto ambao utawazunguka kama khema. Na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyo tibuka. Yatayo wababua nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno!” (18:29).

Kwa hiyo ukimuangalia mwanadamu kwa mazingatio ya jambo la kwanza utaona kuwa ameumbwa juu ya kujisalimisha, umbile lake linampelekea katika kufuata na kulazimika, wala hawezi kwenda kinyume nayo hali yake ni kama hali za viumbe wengine.

Ukimuangalia kwa kupitia muono wa pili utamuona ni mwenye hiari; anachagua anayoyataka, kwa hali hii ni kuwa ima awe ni Muislamu au awe ni Kafiri, Allah Ta’ala amesema: “Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.” (76:3);

Kwa hiyo utakuta watu wanagawanyika sehemu mbili:

Mwanadamu mwenye kumjua Mola wake, anamuamini kuwa ni Mola wake, Mfalme wake na mola wake anayemuabudu Peke Yake, na anafuata sheria yake katika maisha yake ya uchaguzi, kama vile ambavyo yupo katika maumbile ya kujisalimisha kwa Mola wake, ambapo hawezi kwenda nayo kinyume, akifuata makadirio yake, na huyu ndie Muislamu aliyekamilika ambae ameukamilisha Uislamu wake, na hapo ndipo elimu yake ilipokuwa sahihi; kwani amemjua Mola na Muumba wake ambae amemtumia Mitume na kumpa uwezo elimu na kujifunza, na hivyo akili yake ikawa sahihi na rai yake kuwa nzuri, kwa sababu ameitumia fikra yake, kisha akaamua kutomuabudu yeyote ila Allah ambae amemkirimu kipawa cha ufahamu na rai katika mambo, hivyo basi ulimi wake ukawa sahihi wenye kutamka haki kwa sababu hakiri isipokuwa uwepo wa Mola mmoja tu ambaye ni Allah Ta’ala ambaye amemneemesha uwezo wa kuzungumza na kutamka.

Najimu Ramoni

Mhubiri wa Ghana
Kamwe Havipo pamoja
“Sikuwa na hiari katika kulinganisha kati ya msingi wa tawhidi ya Allah katika taswira ya Qur-aan pamoja na itikadi ya utatu kama Mkristo. Nikaona kuwa msingi huu wa pili upo duni sana kulinganisha na msingi wa Uislamu. Na kutokea hapo kwa dhati kubwa nikaanza kupoteza imani ya Ukristo kwa kuzingatia kuwa kumuamini kwangu Allah ndio mwanzo na muhimu zaidi katika dini yoyote: Kwa hiyo Ikiwa kumuamini kwangu Allah nimekosea katika ufahamu wa dini sahihi, maana yake ni kuwa kila kitu kinakuwa ni mchezo ambao hauna maana.”

Ni kama kwamba maisha yake yaliyobakia hayakubaki isipokuwa ukweli tu kwani anafuata sheria ya Allah katika mambo ambayo mwenyewe ana hiari nayo, na ukaenea baina yake na viumbe wengine ulimwenguni mtangamano wa kufahamiana na kuliwazana pamoja.

Kwa sababu hamuabudu isipokuwa Allah mwingi wa hekima, mjuzi, ambaye wanamuabudu na kunyenyekea na kufuata makaridio yake viumbe wake wote, na Allah amewadhalilisha kwa ajili yako ewe mwanadamu, Allah Ta’ala amesema: “Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa anafanya wema, basi huyo hakika amekwisha kamata fundo lilio madhubuti. Na mwisho wa mambo yote ni kwa Mwenyezi Mungu.” (31:22).

Dini ya manabii na mitume yote

Uislamu ni dini ambayo Allah ameiteremsha kwa wanadamu wote, Allah amesema: “…Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Jisalimishieni kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu” (22:34),

Nayo ni dini ya manabii na Mitume wote, Allah amesema: “Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.” (2:136)

Mitume wa Allah wameiamini, na kutangaza Uislamu wao kwa Allah, na kuulingania, Allah amesema kuhusu Nuhu: “Wasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Ikiwa kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu. Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula. Lakini mkigeuka, basi mimi sikukuombeni ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu.” (10:71-72),

Na kuhusu Ibrahim (‘Alayhi Salaam) amesema: “Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.” (2:131),

Bali Ibrahim aliwausia hayo wanawe baada yake, Allah amesema kuhusu hilo: “Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake. ” (2:132-133)

Na kuhusu Musa (‘Alayhi Salaam) Allah amesema: “Na Musa alisema: Enyi watu wangu! Ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni Yeye, ikiwa nyinyi ni Waislamu.” (10:84)

Na amesema katika habari za Masihi (‘Alayhi salaam): “Na nilipo wafunulia Wanafunzi kwamba waniamini Mimi na Mtume wangu, wakasema: Tumeamini na shuhudia kuwa sisi ni Waislamu.” (5:111).

Uislamu ni ujumbe wa mwisho kutoka mbinguni kwa ajili ya wanadamu ambao amemtuma nao Mtume wake Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kwa watu wote, ambao Allah ameukamilisha na kuuridhia kwa waja kuwa ndio dini yao. Allah Ta’ala amesema: “…Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini….” (5:3).

Katika aya hii tukufu Allah anaelezea kuwa amewaridhia wanadamu Uislamu kuwa ndio dini yao, na Allah akatangaza kuwa ndio dini ya haki, na ya kuwa hatokubali kwa yeyote dini isiyokuwa hiyo, Allah amesema: “Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu….” (3:19),

Na akasema vile vile: “Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.” (3:85).

$Gustaf_Lubon.jpg*

Gustaf Lubon

Mwanahistoria wa Ufaransa.
Uislamu ni Mwepesi.
“Hakika wepesi mkubwa wa Uislamu unatokana na tawhidi halisi. Katika wepesi huu ndio kuna siri ya nguvu ya Uislamu. Uislamu na ufahamu wake ni mwepesi umeepukana na yale tunayo yaona katika dini nyingine na akili iliyosalimika inakataa migongano na utata. Hakuna kitu kilicho wazi zaidi kuliko misingi ya Uislamu inayoeleza uwepo wa Mungu mmoja na usawa wa wanadamu wote mbele ya Allah.”

Katika aya ya kwanza anasisitiza kuwa dini anayoitambua ni Uislamu tu, na katika aya ya pili kuwa Allah hatokubali kwa yeyote dini isiyokuwa Uislamu, na kuwa watakaofaulu wakiwa na furaha baada ya mauti ni Waislamu peke yao, na ambao watakufa bila ya Uislamu watakuwa wamepata hasara katika akhera, na wataadhibiwa motoni; na kwa hili Mitume wote walitangaza Uislamu wao kwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na wakatangaza kuwa mbali na wale ambao hawakusilimu, atakayetaka kuongoka miongoni mwa Mayahudi na Manasara na kupata furaha basi asilimu na aingie katika Uislamu amfuate Mtume wa Uislamu Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ndipo awe mfuasi wa kweli wa Musa, Issa (‘Alayhima salaam); kwani Musa, Issa, Muhammad na Mitume wote ni Waislamu, wote walilingania Uislamu, kwani ndio dini ya Allah aliowatuma kuifikisha kwa wanadamu, hivyo haifai kwa yeyote aliyepatikana na kuzaliwa baada ya Muhammad hadi mwisho wa dunia kuwa yeye amejisalimisha kwa Allah, wala Allah hatokubali madai hayo ila tu baada ya kumuamini Muhammad kuwa ni Mtume kutoka kwa Allah, na amfuate, na atende kulingana na Qur-aan ambayo Allah ameiteremsha kwake, Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Naapa kwa ambae nafsi ya Muhammad ipo mikononi mwake, atayenisikia yoyote katika Ummah huu, awe Myahudi au Mnasara, kisha akafa na hakuniamini nilichoshushwa nacho, isipokuwa atakuwa katika watu wa motoni.” (Muslim).

Ujumbe uliokamilika

Uislamu huu ambao Allah amemtuma nao Mtume wake Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kwa watu wote ni Dini ya kumuamini Allah na

kumpwekesha, Allah Ta’ala amesema: “Yeye ndiye aliye Hai - hapana mungu isipo kuwa Yeye. Basi muabuduni Yeye mkimsafishia Dini Yeye. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Sema: Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, zilipo nijia hoja zilizo dhaahiri kutokana na Mola wangu Mlezi. Na nimeamrishwa nisilimu kwa Mola wa walimwengu wote.” (40:65-66).

Ni dini ambayo waja humsafishia ibada Yeye Peke yake, Allah Mtukufu amesema: “Je, mabwana wengi wanao farikiana wao kwa wao ni bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu? Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu.” (12:39-40),

Nayo ni dini ya akili zilizosalimika lau ingedhihirishwa ukweli na usafi

wake nafsi zingefuata kwa kutii na kujisalimisha, Allah Mtukufu amesema: “…Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui.” (12:40),

Ni dini ya dalili, hoja na uthibitisho: “…Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli.” (27:64),

Ni dini ya raha na furaha na utulivu: “Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema…” (16:97).

Ndani ya dini ya Uislamu ambayo Allah amemtuma nayo Mtume

Muhammad, Allah amehalalisha vizuri vyenye manufaa, na akaharamisha

machafu yenye kudhuru, na akaamrisha kila mema na akakataza kila maovu na munkari. Uislamu ni dini nyepesi, hakuna mashaka ndani yake, wala taklifu, wala mzigo ambao watu hawawezi kuubeba, Allah Mtukufu amesema: “Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.” (7:157).

$IbraheemKhaleel.jpg*

Ibrahim Khalil (Philobus)

Padri na Muhubiri wa Misri.
Hakuna kumuabudu asiyekuwa Allah.
“Navutika sana na Imani ya Uislamu ya Mungu mmoja. Hakuna kama Yeye. Imani hii ya Mungu Mmoja pekee inamuepusha mtu na kuwa mtumwa wa binadamu yeyote na huu ndio uhuru wa kweli. Ule uhusiano wa moja kwa moja kati ya Mungu na watumwa wake (waumini) ulinivutia vile vile.”

Ni dini kamilifu, iliokusanya yenye kufaa kwa zama na mahali pote hadi pale Allah atakapoirithi ardhi na vilivyomo. Imekuja na mahitaji yote ayahitajiayo mwanadamu katika dini na dunia yao.

Uislamu ni njia ya furaha na utulivu, njia ya elimu na ustaarabu, njia ya uadilifu na wema, ni njia ya karama na uhuru, njia ya kheri zote na wema.

Ni utukufu wa dini hii na ukamilifu wake!! Na ni dini ipi ni bora kuliko ile ambayo mja amejisalimisha kwa Allah Mtukufu? Allah amesema: “Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule aliye usilimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa mwema, na anafuata mila ya Ibrahim mwongofu?...” (4:125).

$Michael_Hart.jpg*

Michael Hart

Mwandishi wa Kimarekani
Dini na Dunia Viko Pamoja
“Umoja huu wa kipekee ambao hauna mfano wake kwa taathira ya kidini na ya kidunia kwa pamoja, inamfanya Muhammad aonekane kuwa ni mtu mwenye haiba kubwa ya pekee yenye taathira katika historia ya wanadamu.”

Huu wito kutoka kwa Mola wako ambaye yeye ni Mwenye kukuhurumia wewe zaidi kuliko hata nafsi yako uliyo nayo. Anakulingania, kutoka kwenye kiza kwenda kwenye Mwanga, Allah Mtukufu amesema: “Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.” (3:64).

Katika mkabala wa hilo mja ambae amejisalimisha kwa Allah kuna mtu Mwingine amekataa na kufunika umbile lake la Uislamu ambalo Allah amemuumba nalo kwa pazia la kupinga na kukanusha pamoja na mfululizo

$Goethe.jpg*

Goethe

Mwanafasihi wa Kijerumani
Kwanini Isiwe Hivyo
“Ikiwa huu ndio Uislamu. Kwa nini basi sote tusiwe Waislamu.”

wa dalili na miujiza inayoonesha usahihi wa dini hii.

Hivyo mtu huyu akajichagulia nafsi yake ushirikina kinyume na Tawhidi, kiza cha dhana, uzushi badala ya mwanga wa haki, yakini na uongofu, na kuridhia nafasi yake kuwa ni mtumwa wa waja mfano wake, kama vile watawa na wanazuoni wa kiyahudi, bali na Mitume badala ya kuwa ni waja wa Allah mmoja Peke yake; na hivyo basi fitra yake ikapotea na akili kupotea na kunyenyekea katika matamanio na utata huku akiacha fitra ya Allah ambayo Allah amemuumba nayo, hakuzaliwa mtoto yoyote ila katika fitra ya Uislamu: “Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui.” (30:30).

$b-w_nehru.jpg*

Jawaharlal Nehru

Waziri Mkuu wa Kwanza India.
Imani ya Muhammad juu ya Ujumbe Wake.
“Huenda wale wafalme na watawala ambao walipokea barua waliingiwa na mshangao kutokana na mtu huyu asiye na makuu ambae aliwaita kwenye utii. Kutuma barua hizi kunatupa picha ya kiasi cha kujiamini kwa Muhammad mwenyewe na ujumbe wake. Aliuandalia Umma wake kwa kujiamini huku na imani hii ni nguvu, utukufu na ulinzi, pembezoni mwake ni wakazi wa majangwani kubadilika kuwa mabwana waliofungua nusu ya Ulimwengu uliokuwa ukijulikana katika zama zao. Muhammad alifariki baada ya kuyafanya makabila yote ya Kiarabu yaliyotawanyika kuwa Ummah mmoja wenye ghera na hamasa.”

Sasa ni juu yako kukadiria ndani ya nafsi yako kilichomtumbukiza kafiri kwenye upotevu wa wazi: “Yeye ndiye aliye kufanyeni manaibu katika ardhi. Na anaye kufuru, basi kufuru yake ni juu yake; na kufuru za makafiri haziwazidishii kwa Mola wao Mlezi ila kuchukiwa. Wala kufuru za makafiri haziwazidishii ila khasara.” (36:39)

Ni ipi misingi na rejea na sifa za Ujumbe huu?