NI DINI IPI TUNAYOHITAJIA?!

NI DINI IPI TUNAYOHITAJIA?!

NI DINI IPI TUNAYOHITAJIA?!

Dini ya maadili

$Albert_Camus.jpg*

Albert Camus

Mwanafalsafa wa Kifaransa
Mtu na tabia zake
“Mtu asiye na tabia njema ni mnyama amaeachwa huru katika ulimwengu huu.”

Dini hiyo ilingane na tabia nyema na matendo mema, Allah amesema: “Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini. Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka. Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu.” (6:151-153)

$Youl.jpg*

Jul

Mustashrik wa Kidenimaki
Kuwa Mwanahalisi
“Mtazamo halisi katika maisha na ushauri wa kweli na kulingania kwenye hisani, huruma na mguso wa kheri wa kibinadamu, haya na mengineyo ni katika dondoo ambazo kwangu zilikuwa ni dalili kubwa za ukweli wa dini ya Uislamu.”

Na Allah akasema, “Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka.” (16:90)

Haisihi dini ambayo italingania uongo au mauaji au dhulma au wizi au kuhaka na kupora na kufanya uasi au mfano wa hayo.

Dini yenye nidhamu

Itengeneze mahusiano kati ya Mwanadamu na Muumba wake, na mahusiano ya viumbe kwa viumbe, Allah amesema, “Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui. ” (12:40)

$Ernest_Hemingway.jpg*

Ernest Hemingway

Mwandishi wa Kimarekani
Tabia njema zinakupa raha
“Ninachokifahamu kuwa tendo zuri ulifanyalo linalotokana na tabia njema ni lile linalokufanya baada ya hapo uhisi raha, na tabia mbaya baada ya kulifanya unapojisikia vibaya”

Hivyo basi inapasa dini hiyo kutengeneza majukumu ya mwanadamu kwa Mola wake, kadhalika itengeneze mahusiano ya viumbe na watu, Allah amesema: “Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia….” (4:36).

Dini yenye kumkirimu mwanadamu

Dini hiyo imuheshimu mwanadamu na imkirimu wala isitofautishe baina ya wafuasi wake kwa tofauti zozote zile ziwe za kijinsia, rangi au kabila; kigezo cha kufadhilishwa na ubora ni kile anachokipata mwanadamu kutoka katika kazi yake, elimu na ucha-Mungu, Allah amesema: “Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini…” (17:70)

Na akasema vile vile, “Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” (49:13).

$Joseph_Schacht.jpg*

Joseph Sachacht

Mustashrik wa Kijerumani
Urithi bora
“Miongoni mwa mambo muhimu ambayo Uislamu umeyarithisha Ulimwengu huu ulioendelea ni kanuni zake za dini ambazo zinaitwa Sheria. Kwa hakika sheria ya Kiislamu ni kitu cha pekee katika mlango wake, ni jumla za amri za kiungu ambazo zinaratibu maisha ya kila Muislamu katika Nyanja zote, nazo zinakusanya hukumu maalumu kuhusu ibada na mambo mengine ya kidini, kama ambayo inakusanya misingi ya kisiasa na kanuni zake mbali mbali.”

Nane: Dini hiyo imuelekeze mwanadamu katika njia sahihi isiyokuwa na kombo, na njia hiyo iwe ni tiba kwa mwanadamu na iwe nuru na muongozo wao, Allah amesema akielezea kuhusu majini baada ya kusikiliza kwao Qur-aan wakiambizana, “Wakasema: Enyi kaumu yetu! Sisi tumesikia Kitabu kilicho teremshwa baada ya Musa, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake, na kinacho ongoza kwenye Haki na kwenye Njia Iliyo Nyooka.”(46: 30),

$Aristotle.jpg*

Aristotle

Mwanafasafa wa Kigiriki
Hakuna Usawa
“Aina mbaya zaidi ya kukosekana usawa ni kujaribu kusawazisha kati ya vitu visivyo sawa.”

Na akasema Allah, “Na tunateremsha katika Qur’ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhaalimu ila khasara. ” (17:82)

Nayo ni nuru na muongozo wa watu ambao unawaongoza watu kutoka kwenye dhuluma za ujinga (ujahili) na upotevu kwenda kwenye Nuru ya utiifu na furaha katika nyumba zote mbili, Allah amesema: “Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anaye samehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha.” (5:15)

$Dale_Carnegie.jpg*

Dale Carnegie

Mwandishi wa Kimarekani
Mtake Msaada Mwenyezi Mungu
“Pengine ingewezekana kuokoa maelfu ya wanaoadhibika kwa kupiga makelele katika hospitali za wendawazimu, lau wao wangeomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu badala ya wao wenyewe kuingia kwenye mapigano na Nafsi zao bila ya msaada wala muokozi.”

Na Akasema Allah tena, “Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet’ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet’ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu. ” (2:256-257).