Nafsi ya Mwanadamu Baina ya Mifumo Miwili

Nafsi ya Mwanadamu Baina ya Mifumo Miwili

Nafsi ya Mwanadamu Baina ya Mifumo Miwili

Sehemu waliyofikia Rashidi na Maiko ilikuwa sehemu nzuri kwao, nyongeza ya urahisi wa gharama ya makazi, ndani yake kuna kiwanja cha michezo na sehemu za kujisomea na kupumzika, na uwezekano wa mawasiliano, na muhimu zaidi ya hilo ni kuwepo wageni wenye umri unaolingana nao na viwango vyao vya elimu.

Maiko na Rashidi walipumzika katika moja ya meza katika ukumbi wa kijamii (mkutano) na kila mmoja akaagiza kinywaji akipendacho, kisha Maiko akaanza kuzungumza:

Katika mazungumzo yetu yaliyopita tuliishia kwenye yale aliyoyasema mwanazuoni huyu kuhusu dini yenu ambayo umezungumzia, na je, alichokisema kinaafikia na au kinapingana?

Rashidi: Sio masuala ya kuafikiana au kugongana, Uislamu ni mfumo kamili unaojitegemea kikamilifu, na umesimama katika misingi ya wazi, hata hivyo sitorefusha kuuelezea…Mwanazuoni huyu jina lake ni Ibnu Qayyim, amezungumza katika vitabu vyake kuhusu uhusiano kati ya moyo, nafsi na akili, lakini nitapenda kwanza kuashiria kuwa alichokisema kilikuwa ni kwa mujibu wa ufahamu ambao unaambatana pamoja na misingi ambayo ustaarabu wa Kiislamu umesimama, hivyo basi napenda kuunganisha mazungumzo yangu yaliyotangulia kwa kufafanua tofauti kati ya mfumo huu na madai ya nadharia ya Freud ambayo yametengeneza sehemu kubwa ya hali halisi ya jamii ya magharibi na maadili yake.

Maiko: Ili tuweze kutumia wakati wetu vizuri, niachie niweke bayana sehemu ya mwisho ya maneno yako, pamoja na kuwa yapo kinyume na unachoamini, natarajia utanisahihisha.

Rashidi: Karibu.

Maiko: Tunachokipata kutoka katika nadharia ya Freud ni aina nyingi za haiba ya mtu, zinawakilishwa na yafuatayo:

Pindi silika na matamanio ya kijima au ya kihayawani yakitawala (yaani: Id) kwa mtu, basi (Ego) ya mtu itaonekana kuwa ni mtu mbinafsi au muovu mwenye kufanyia uadui haki za wengine, yeye atakuwa anatafuta kushibisha matamanio yake na kuitikia haja zake za kihayawani, na kusaga saga maadili mema na desturi njema na yaliyo matukufu (Super Ego).

Na ikiwa maadili mema, desturi njema na matukufu yatatawala (Super Ego) juu ya (Ego), basi utadhihirika kwa mtu huyo upole na utawa lakini asiyeishi katika uhalisia wake na wakati huo akisaga saga katika njia yake hiyo silika na matamanio ya kijima.

Haiba itakuwa ni sahihi na tulivu atakapoweza kulinganisha na kuweka sawa baina ya matamanio na silika kwa upande mmoja, na maadili na vifungo vya nje kwa upande mwingine, na hilo hutokea kwa kuficha na kufukia baadhi ya silika hizi katika baadhi ya hali au kuondokana na vifungo na maadili katika baadhi ya nyakati zingine kwa kadri ya makadirio ya kila hali.

Rashidi: Vizuri sana, tumefikia kujua tofauti kati ya nadharia hii na ustaarabu wa Kimagharibi ambao tumeuangalia kijamii na kuulinganisha na mfumo wa Kiislamu… na tofauti hii huonekana katika kumaliza hali ya uadui na mgongano kati ya (Ego) na (Super Ego) bila ya kimojawapo kuacha haki zake na hilo ni kupitia ulingani makini na ukamilifu unaoenea sehemu zote za mipaka ya wanadamu katika nyanja za maisha yake, na siri katika hilo hujificha kwa ninachokiita tahadhari ya kupetuka haki.

Maiko: Kwa mara ya kwanza ndio nasikia hili la kupetuka haki, na utanieleza ni vipi haki zinapetukwa, hata hivyo niache kwanza nikuambie kuwa maneno yako yanathibitisha fikra ya uumbwaji wa mfumo wa nafsi.

Rashidi: Fikra ya uumbwaji wa mfumo wa nafsi ndiyo ambayo nimekutajia hapo mwanzo kuwa, mmoja wa wanazuoni wa Kiislamu bali baadhi yao wamesema yanayofanana nayo kabla ya mamia ya miaka, angalia alichokisema mwanazuoni huyu anayeitwa Ibnu Qayyim katika moja ya vitabu vyake, hapo Rashidi akatoa kitabu, kisha akasoma: “Hivyo basi mambo ni manne: Yanayochukiza yanapelekea katika kuchukiza, na yenye kuchukiza, yanapelekea katika yenye kupendwa, na yenye kupendwa yanayopelekea katika yenye kupendwa, na yenye kupendwa yanayopelekea katika yenye kuchukiza. Kwa hiyo yenye kupendwa yenye kufikisha katika yenye kupendwa hukusanyika ndani yake muitaji wa kutenda katika sura mbili, na yenye kuchukiza yenye kupelekea katika yenye kuchukiza hukusanyika ndani yake muitaji katika kuacha katika sura mbili.

Kumebakia sehemu mbili zinazovutana na waitaji wawili; Mwenye kuita katika kutenda na kuacha (vita katika balaa na mtihani). Katika hali hii nafsi huathiri kilicho karibu nae zaidi, na hilo ni lile lenye haraka zaidi, na akili na imani huathiri chenye kunufaisha na kubakia zaidi, ama moyo upo katika miito miwili, wakati mwingine upo kwa huyu na wakati mwingine kwa huyu, wanazuoni wa Kiislamu wanataja huku wakidhukuru maandiko ya Qur’an na hadithi za Mtume Muhammad kuwa pindi akili inapoghafilika (Super ego) basi wakati huo matamanio yanakuwa katika nishati (Id) bila ya mlinzi au msimamizi.

Je, huoni mfanano katika wadhifa (kazi) za nafsi na (Id) kwa Freud, na kati ya akili na imani na (Super ego) na moyo na (Id).

Maiko: Kama ni hivyo basi kuna mfanano mkubwa.

Rashidi: Kuna tofauti ya msingi kati ya maneno haya na yale, tofauti inayopambanua mfumo huu na ule, tofauti hii inajificha katika kauli ya Ibnu Qayyim (nayo ni vita kati ya balaa na mitihani), wakati ambapo Freud anaona kuwa uzima wa mtu (Ego) ambayo ni moyo kwa Ibn Al-Qayyim) ipo katika kuitikia silika (Id/Nafsi) na matamanio yake. Ama katika mfumo wa Kiislamu unaona kuwa mwitikio wa silika hizi na matamanio ndani ya nafsi na msukumo wake katika uhalisia huchukuliwa kuwa ni mitihani kutoka kwa Allah, wala haifai kuitikia mwito moja kwa moja ili kuiridhisha (Id/Nafsi), vile vile haitakiwi kuiangamiza moja kwa moja na kuipeleka kwenye hesabu ya (Super Ego) au akili na imani kama ilivyo kwenye utawa.

Na huu ndio wastani na kulinganisha mizani ambayo hatuyapati katika isiyokuwa Uislamu; kudhibiti matamanio na silika, na kushibisha haja za silika za mwanadamu bila ya kugongana na akili na imani na bila ya kupetuka haki zingine.

Maiko: Sasa ni nini makusudio ya kupetuka haki?

Rashidi: Makusudio yake ni kuwa maadili na tabia njema zina haki zake, na kwa upande mwingine matamanio na silika zina haki zake vile vile, na Uislamu unahadharisha kutopituka moja wapo ya maadili na matukufu ya tabia au hata matamanio au hata silika kushambulia haki nyinginezo, kwa maana ya kwamba haya ni maadili matukufu na hizi ni haja chafu, na ili kuyaelezea vizuri nakutajia hadithi ya Mtume wa Uislamu, “Makundi matatu ya watu yalikwenda katika nyumba ya Mtume Muhammad na wakauliza ibada zake na walipoambiwa walizihesabu kama kwamba ni kidogo, wakadhania kuwa hilo ni kwa sababu Mtume Muhammad ana sifa tofauti nao, na wao kwa sababu wana madhambi mengi zaidi hivyo basi nao wanatakiwa wafanye ibada nyingi zaidi kiasi cha kukata hoja zao za kimaumbile, katika hilo mmoja wao akasema: Ama mimi nitaswali usiku umri wangu wote wala sitolala, mwingine akasema: Mimi nitafunga (sitokula asubuhi hadi jioni) kila siku na wa mwisho akasema: Mimi sitooa daima. Mtume Muhammad akawaendea na kuwaambia: “Nyie ndio mliosema hivi na vile, ama Wallahi mimi ndie mcha Mungu wenu zaidi, lakini ninafunga na nakula, na ninaswali usiku na kulala na ninaoa wanawake, mtu ambae ataacha sunnah (mwenendo) yangu si katika mimi.” …watu wale waliongeza kitu katika dini (Super ego) ambayo kiuhalisia ni vitu vya ziada kufanya na vyenye kupendeza na kutakiwa, lakini yalikuwa yamevunja haki zingine hata kama haki hizi zitahusu nafsi ya mtu (Id), imekuja katika hadithi nyingine yenye kubainisha vizuri zaidi msingi huu: “Hakika Mola wako ana haki juu yako, na nafsi yako ina haki juu yako, na familia yako ina haki juu yako, hivyo kila mwenye haki mpe haki yake.” Katika Qur’an Tukufu zipo aya nyingi zenye kuthibitisha hilo, miongoni mwa aya hizo ni:

{Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi} [28:77]

{Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi} [17:29]

Na bila shaka rafiki yangu unafahamu kuwa Uislamu umekataza utawa..

Katika Uislamu mtu anairidhisha akili yake, dhamira yake, kutekeleza dini yake na kushibisha haja zake za kimaumbile…bila kupingana.

Wakati Rashidi na Maiko wamezama katika mjadala wao, alisogea karibu yao kijana aliyekuwa amekaa kwenye meza pembeni yao, alisimama mbele yao na kuanza kuzungumza:

Je mtaniruihusu nikae pamoja nanyi?

Maiko na Rashidi kwa furaha… karibu.

Kijana: Kwa hakika nimefurahishwa na kuvutiwa na mazungumzo yenu, nitafurahi kama tutafahamiana na kunishirikisha kwenye mjadala wenu.

Maiko: Mimi sina tatizo.

Rashidi: Karibu, karibu, nikutambulishe kwa rafiki yangu Maiko kutoka Uingereza, yeye ni mwalimu, na mimi ni Rashidi kutoka Misri, ni mwandishi wa habari na mtunzi wa vitabu.

Kijana: Karibuni sana, na asanteni kunikaribisha kujiunga nanyi, nijitambulishe kwenu, mimi ni Rajev, kutoka India, nasoma uhandisi Ujerumani, nipo hapa Paris kuwatembelea baadhi ya rafiki zangu.

Maiko na Rashidi: Fursa nzuri kufahamiana nawe Rajev.

Rashidi: Kama tunaona kuwa wanazuoni wa nafsi wa Magharibi hawaangalii nafsi isipokuwa kupitia aibu, maradhi, na maafa ya nafsi..ama katika Uislamu nafsi imebeba ndani yake kheri na shari, na kuna uwezekano wa kubadilisha hali ya nafsi na kuigeuza na kuitoa kwenye dhuluma ya uhayawani na kuifikisha nafsi ile kwenye kilele cha ukamilifu bila kugongana na umbile la mwanadamu au kutia kasoro haja zake.

Rajev: Najifunza kutoka katika mjadala wenu kuwa matamanio yaliyofichwa daima yanatafuta kushibishwa kwa haja zake kwa njia ya moja kwa moja au kwa kuzunguka, basi hilo litapelekea kuzingatia ustaarabu unaosimama katika misingi ya maadili mema kuwa ni ustaarabu uliozaliwa kwa kuficha mahitaji na matamanio ya mwanadamu kulingana na mtazamo wa Freud.

Rashidi: Kwa hakika ustaarabu wa Kimagharibi unapozalisha maadili mema huzalisha kupitia kushinda mtazamo wa ulimwengu juu yake, na humpa mwanadamu kipaumbele kwa kumzingatia kuwa ni bwana wa ulimwengu huu, yote hayo yamejitokeza kwa kuondoa fikra ya Mungu katika ustaraabu. Ama mtazamo wa ustaarabu katika Uislamu ni kuwa Mungu ndie yuko juu, hata hivyo mtazamo huu haufuti mwanadamu kutamalaki ulimwengu.

Rashidi: Huu ni ushahidi madhubuti kuwa maadili katika jamii za wanadamu ni lazima chanzo chake kiwe kutoka katika ufunuo (wahyi) na sio akili, kwani akili peke yake inapotea, ama akili ikiwa katika mipaka ya wahyi basi maadili yatakayozalishwa yatakuwa ndio yenye kutakiwa.

Maiko: Uwepo wako ewe Rajev utakuwa na athari njema katika mjadala wetu, naona tuweke ahadi ya kuonana kesho katika sehemu hii hii tuanze mjadala wetu mpya, mnaonaje?

Rajev: Ndio, sawa kwangu.

Rashidi: Nitafurahi kama mkikubali kupokea mwaliko wangu wa chakula cha mchana katika kikao chetu nayo ni kwa heshima ya rafiki yetu mpya Rajev.

Maiko na Rajev: Kwa furaha kabisa.