Mwanamke ni Malkia

Mwanamke ni Malkia

Mwanamke ni Malkia

Baada ya treni kuanza kuondoka, marafiki wawili, Rashidi na Maiko walikuwa tayari kuanza mazungumzo yao wakati wa safari.

Maiko: Tumezungumzia mambo mawili yanayohusu haki za mwanamke: wake wengi na hijabu… Nini rai yako tukamilishe mambo yaliyobakia kuhusu maudhui haya?

Rashidi: Fikra nzuri, huenda katika hilo tukafunga faili letu.

Maiko: Jambo la kwanza linalonijia akilini mwangu katika maudhui haya ni kwa nini Waislamu wameshikilia mwanamke kutoshiriki kama mwanamume katika nyanja za maisha?

Rashidi: Sisi ewe rafiki yangu tunaposema kuwa mwanadamu ana sehemu ya maada au ya uhayawani, haina maana kuwa wasifu wa sehemu hii na malengo yake au matunda yake katika uhayawani; kuna tofauti kubwa; sisi tunakuta kuwa kuna muelekeo mkubwa zaidi wa kijinsia kwa mwanadamu kuliko kwa mnyama, wakati ambapo nguvu ya kujaamiana ni dhaifu zaidi mara nyingi kuliko muelekeo huu, kinyume cha mnyama.

Tukichukua kwa mazingatio kilichowekwa katika maumbile ya mwanamke (mbali na matamanio ya kijinsia) kama vile haya, heshima, kujizuia, na unyoofu, bila shaka tunatohoa kutokana na hilo na yaliyotangulia kuwa makusudio ya kuwepo kwa nguvu ya mvutano wa kijinsia kwa mwanadamu ni kufanikisha mawasiliano ya kudumu baina ya wanandoa na sio kuishia kwenye kila matamanio ya kijinsia katika utendaji wa kijinsia, na hilo ndilo lililoelezwa ndani ya Qur’ani mara nyingine kwa “utulivu” na mara nyingine, “upendo na rehema”. Huu ni kwa upande wa nafsi… nataraji maneno yangu yako wazi.

Maiko: Takriban yapo wazi.

Rashidi: Kwa upande wa kibaolojia, utafiti umethibitisha kuwa mwanamke anatofautiana na mwanamume katika kila kitu. Katika umbile la nje, hadi maungo ya ndani, hadi katika seli za kiwiliwili chake; seli za mwanamke zimepigwa muhuri wa kike, na umbile lake linatofautiana na la mwanamume, mfumo wa kiwiliwili chake umewekwa na kuandaliwa kwa ajili ya kuzaa watoto na malezi yake, yaani ili uwiane na wadhifa wa mama, na pindi anapofikia baleghe humjia hedhi ambayo kwayo kila kiungo cha kiwiliwili chake kinaathirika nayo, hata hali yake ya kinafsi na ya kiakili inaathirika, hapo bado hatujazungumzia kuhusu hali ya mimba, nifasi na kunyonyesha.

Bali Homoni na hali ya kinafsi ya mwanamke inatofautiana na ya mwanamume, hivyo kwa mkabala wa maisha ya ujasiri ya mwanamume na kuthubutu kwake tunakuta haya ya mwanamke na kudeka kwake.

Na kwa upande mwingine: Mtoto wa mwanadamu anahitaji (tofauti na wanyama wengine) uchungaji na malezi ya wazazi wake kwa miaka mingi, kwani mtoto wa kibinadamu huchelewa kukamilika nguvu na uwezo wa kujitegemea katika maisha, na hili ndilo linalotakiwa mahusiano ya mwanamume na mwanamke yasiishie kwenye mahusiano ya kijinsia tu, bali kuvumilia kwake ndio matunda ya mshikamano wao na kushirikiana kwao katika maisha, na kwa ajili hii vile vile mwanadamu ameumbwa kuwa na fikra ya kuwapenda watoto wake mapenzi makubwa ambayo wanyama wote hawana.

Maiko: Baada ya hayo ni nini?

Rashidi: Kwa kifupi ni kuwa hili linathibitisha kuwa familia ndilo umbo la kijamii la kawaida kabisa la mwanadamu, na tunaweza kuweka wazi nafasi ya kila mtu na wadhifa wake katika umbo hili au umoja huu, nayo ni nafasi inayolingana na malengo ya umoja huu wa mshikamano na tabia yake (makazi, mapenzi na huruma), na yanalingana vile vile na uwezo wa kila mtu.

Maiko: Nimefahamu unachokusudia, kwa maana hiyo duru ya familia ni kueneza roho ya mapenzi ili kuhakikisha utulivu wa nafsi ya familia na kuwachunga kwa kuwalea mume na watoto.

Rashidi: Sawa kabisa, na nafasi ya mwanamume ni kuhakikisha kuwa familia inapata mahitaji yake, na yote yanayohitajika katika kupambana na kukabiliana na hali ngumu na mashaka juu ya hayo.

Maiko: Lakini mtazamo huu unatufanya tupoteze nusu ya uwezo wa uzalishaji katika jamii.

Rashidi: Kinyume kabisa; mtazamo huu unatufanya tuipate jamii yote, lakini kila mmoja katika nyanja yake stahili; mwanamke anapopambana na maumbile yake na kutoka nje akisongamana na wanaume kazini kwa hilo anapata tabu kubwa kwa kazi yake mpya, na familia yake inapata shida na kutaabika; na hilo limepelekea jamii nzima kupata shida. Katika hali hiyo mwanamke amejaribu mno kusawazisha baina ya kazi yake na shughuli zake za nyumbani na kuwalea watoto wake lakini hakufanikiwa; kwani hilo litamfanya awe mke mtulivu na mama mwenye huruma lakini wakati huo huo awe mwanamke mchapa kazi kazini, yote hayo kwa pamoja atayapata wapi? Hivyo matokeo yakawa kuingia katika ncha nyingine, ili kujaza faragha ile ambayo mwanamke ameiacha, na sehemu hizi zilizojaza nafasi ambayo aliiacha, na ncha hizi hazikuwa matarajio au stahili kwa ajili ya majukumu haya, na kuongezea hilo: Wanawake kusongamana na wanaume kazini nje ya nyumba zao kumemfanya mwanamke kukumbwa na matatizo ya kushambuliwa na wanaume na kinachofuatia baada ya hapo miongoni mwa yanayoambatana na hayo, kama vile kumtongoza, kumbaka na mengine dhidi yake, na kazi anazochagua wakati wa kazi zake katika aina nyingi za kazi anazozifanya nje ya nyumba yake.

Maiko:Tunapozungumzia nafasi ya mwanamke katika maisha kama ni nafasi ya familia, basi hilo linatusukuma katika mazungumzo ya jambo lingine, ambalo naliona kuwa linambagua mwanamke au lipo dhidi ya mwanamke, jambo hilo ni usimamizi wa mwanamume kwa mwanamke.

Rashidi: Usimamizi wa mwanamume hauna maana kumbagua mwanamke, bali ni mfumo wa kitaasisi katika jamii ambao unaitwa familia, taasisi yoyote lazima iwe na mipaka yake ya kazi na mgawanyo wa kazi na wadhifa wa kila mmoja, pamoja na kujali uwezo wake wa kiutendaji, na kwa maana hiyo mkurugenzi kazini utu wake sio mkubwa kuliko muhasibu au mfanyakazi mwingine au anafaa zaidi kuliko wengine.

Katika maisha yetu ya kitendaji ya kila siku tunashuhudia kuwa taasisi au jamii inaweka baadhi ya mipaka iwe kwa kulazimisha juu ya watu kwa ajili ya wengine au kwa baraza la wadhamini peke yao, kwa mfano: Shirika linaweza kuweka aina fulani ya mipango, au kuweka aina fulani ya ulinzi, au kupitia mafunzo fulani, au kuwakataza kuacha kazi na kutoka nje ya shirika bila ya ruhusa, au kutoshughulika na shughuli nyingine zaidi ya kazi alizopangiwa, bali wakati mwingine shirika likiingia mkataba na mfanyakazi wake na kumwekea mipaka fulani baada ya kuacha kazi kwenye shirika lake….Yote haya yanafanyika na kukubalika, wala hakuna mwenye kuangalia katika mikataba hii kuwa ni ubaguzi au kuwadhulumu wafanyakazi wake. Yote haya yapo chini ya mfumo maarufu ulio wazi kama ambavyo hakuna taasisi wala kituo kilichofanikiwa bila kuwepo kwa mkuu wake aliyepata nafasi kubwa yenye kulingana na majukumu aliyowekewa shingoni mwake na maswala yatakayoweza kumtokea.

-Vivyo hivyo, taasisi ya familia ili iweze kufanikiwa haina budi kuwa na mfumo wanaopitia wote, na mfumo huu unaweza kuwa na baadhi ya vifungo na makatazo au wajibu (kujilazimu) ….Hapana budi kuwepo kiongozi mwenye nafasi inayolingana na majukumu yake, na hivyo kuwa na uwezo wa kutatua jambo pindi tofauti au mtafaruku unapojitokeza. Hata hivyo hapana budi vile vile kutekelezwa mfumo huu vile vile na kutumia nafasi hii katika kivuli cha msingi wa maisha ya kifamilia tuliyoyazungumza, nayo ni mapenzi na huruma na maisha ya masikilizano yenye kuhakikisha lengo la kuishi.

Maiko: Ikiwa hali ndiyo ilivyo, kwanini usimamizi uwe kwa mwanamume? Kwa nini usiwe kwa mwanamke? Je huoni kuwa huo sio usawa?

Rashidi: Pamoja na kupendelea kwangu neno usawa, ambalo ni bora kuliko neno ‘uadilifu’ isipokuwa ninasema: Usawa au uadilifu unakuwa katika haki, ama haya tuliyomo ndani yake ni mgawanyo wa kazi na kuziba nyadhifa za kijamii zinayolingana na uwezo wa mtu na yaliyotayarishwa kwake.

Tulipokuwa tunazungumzia taasisi ya familia tumesema kuwa mwanamume na mwanamke kila mmoja ametayarishwa kwa umbile tofauti, na matayarisho haya yanalingana na nyadhifa mbali mbali za kijamii, wala usisahau kuwa katika mkabala wa usimamizi wa mwanamume kuna majukumu ambayo hakupewa mwanamke, na usimamizi wa mazingatio haya ni majukumu zaidi kuliko upendeleo, ni ubebaji wa majukumu na hili linahitajia uvumilivu zaidi na kutofanya haraka kuchukua maamuzi, na hii haina maana kumdharau mwanamke au utu wake.

Nyadhifa za kijamii hazimfai mwanamke vile vile; kwani wanawake ni kama vile alivyosema Mtume wetu Muhammad: “Wapungufu wa akili?

Maiko: “Wapungufu wa akili? Hakika mtazamo huu ni wa kumdunisha mwanamke, kama ambavyo mwanamke amethibitisha uwezo wake wa kielimu, na uwezo wake wa akili hautofautiani na wa mwanamume.

Rashidi: (Akicheka): Jambo la ajabu kabisa ewe rafiki yangu kuwa watu wengi niliozungumza nao kwa mazungumzo haya walifahamu ufahamu huu uliofahamu, jambo lililokusudiwa kuhusu akili sio akili hii ya maarifa bali ni uwezo wa kusimamia mambo kwa mizani ya sawa sawa, na kudhibiti nafsi na hisia mbali mbali, kinachomsaidia katika kuchukua maamuzi sahihi wakati wa matatizo na mazingira tata, yaani kwa maana nyingine; kinakabiliana na upole na kuelekea kwenye matamanio, wala mtu hawezi kupinga kuwa tabia ya mwanamke huelekea kwenye huruma zaidi na huathirika zaidi kuliko mwanamme hii ndio tabia ya hisia zake, na nafasi yake ya kijamii inapaswa kulingana na tabia yake hii, na huenda hekima hii vile vile hufunga nafasi ya mwanamke ili ayaendee majukumu yake ya kifamilia kwani yeye ndio mhimili wa familia.

Maiko: Tunapozungumzia dhulma ya mwanamke na mtazamo wa kumdunisha, ni vizuri kutajwa haki zake katika mirathi, kwanini inakuwa mirathi ya mwanamke ni nusu ya mwanamume?!

Rashidi: Kwanza kabisa: Sio katika hali zote fungu la mwanamke katika mirathi huwa ni nusu ya mwanamume.

Pili: Utukufu wa mwanaadamu haututaki tuwape watu haki tunazowapa wengine; uadilifu hauna maana ya usawa katika hali zote, lakini usawa ni wajibu pindi hali na mazingira yanapokuwa sawa, yaani: hapana budi kuzingatia tabia ya mwanamke na nafasi yake katika maisha, na haki zake ziwe sawa na majukumu yake.

-Katika masuala ya mirathi kwa mfano: Anachokipata mwanamke kinakuwa ni chake peke yake, wakati ambapo mwanamme mirathi yake atagawana na mkewe, watoto wake na ndugu zake, kama watakuwa bado hawajaolewa na wazazi wake kama bado wapo hai na hawana wa kuwahudumia, hapo litakuwa ni jukumu lake, mbali ya kuwa mwanamume ndie atoaye mahari kwa mwanamke na yeye ndie mwenye jukumu la kutayarisha nyumba baada ya kuoa na samani zake, na mwanamume ndie mwenye jukumu la kutoa matumizi ya nyumba, mke na watoto, wala haipasi mwanamume kumlazimisha mwanamke kufanya kazi, nae hana haki katika mali ya mke wake, mbali yakuwa mwanamke anajitegemea kwa mali yake kwa ukamilifu, jambo ambalo wanawake wengi wa nchi za Magharibi bado hawajalifikia, ambapo inadaiwa kuwa ndio wenye usawa zaidi.

-Je, kuna lililobakia katika maudhui haya ambalo tunapaswa kulijadili?

Maiko: Naam, imebakia suala la talaka, lakini nashauri tupumzike kwanza.