Mustakbali wa Dini Hii

Mustakbali wa Dini Hii

Mustakbali wa Dini Hii

Rajev alichelewa (katika hali isiyokuwa kawaida yake) katika kikao na rafiki zake, na alitokezea katika Skrini ya Laptop, Maiko akaanza kuzungumza nae.

Halo! Rajev, umezoea kufika kwa wakati katika miadi yetu tunataraji kuchelewa kwako kusiwe ni kwa tatizo lililokusibu.

Rajev: Samahani rafiki zangu, hakuna neno, lakini nilishughulishwa kumalizia utafiti wangu ambao nilitaka kuwaonesha.

Maiko: Vizuri sana, kama ni hivyo mjadala utakuwa na faida kubwa, utafiti wako unahusu nini?

Rajev: Kwa hakika mjadala wetu wa mara kwa mara umenivutia sana na umenipa maarifa mengi kuhusu Uislamu, hivyo basi nikataka kufanya utafiti kuhusu kuchambua katika harakati ya kuenea kwa dini hii na kupanuka kwake ulimwenguni.

Maiko: Jambo hilo hilo limenivuta kufanya utafiti vile vile, lakini katika nyanja nyingine zinazohusika na kupanua utafiti wa nyanja ambazo tutaziangalia kwa undani zaidi na kutokana na vyanzo vyake vya asili….hata hivyo nini ulichokipata katika utafiti wako? bwana Rashidi!! je upo nasi??!

Rashidi: Ndio, ndio, nipo nafuatilia pamoja nanyi.

Rajev: Nimekuta marejeo na elimu nyingi zinaashiria kuzidi kupanuka kwa Uislamu ulimwenguni, utafiti umegundua kuwa kuwepo kwa zaidi ya mila na desturi 4,200 ulimwenguni, na takwimu zinathibitisha kuwa dini ya Kiislamu ndio yenye kuenea zaidi kati ya itikadi zote ulimwenguni! Na kuwa leo hii inasambaa mabara yote uliwenguni kwa haraka, tutakapoangalia kiwango cha ukuaji wa Waislamu na kulinganisha na ukuaji wa wafuasi wa Ukristo mathalani, unapata takwimu ya Umoja wa Mataifa inayosema:Kiwango cha ukuaji cha Waislamu ulimwenguni ni asilimia 6.4% wakati ambao cha Wakisto haizidi asilimia moja 1%.

Utafiti wangu umeangalia Ulaya, nikakuta Uislamu kwa mfano: Ndio dini ya pili nchini Hispania, Ufaransa na Uingereza.

Huko Ujerumani Waislamu wanaongezeka, na kulingana na gazeti la Die Zeit la Ujerumani la kila siku ni kuwa: Uislamu husambaa Ujerumani na kuongezeka kila siku.

Utafiti uliofanywa na wizara ya ndani ya Ufaransa umethibitisha kuwa: Zaidi ya watu 3,600 wanasilimu kila mwaka kama ambavyo inaashiria kuwa kuna misikiti 2,300 na Waislamu milioni 7, na kuna matarajio kuwa ifikapo mwaka 2025. Waislamu watafikia robo ya wakazi wote wa Ufaransa, wakati ambapo utafiti huo huo unaashiria kuwa ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na Waislamu asilimia 20% Ulaya, kadhalika kuna takwimu nyingine zinaona kuwa ifikapo mwaka 2040 Waislamu ndio watakaokuwa wengi Ulaya.

Takwimu zinasema kuwa theluthi ya wananchi wote wa Holland watakuwa ni Waislamu baada ya miaka kumi, na moja katika tafiti hizo zinathibitisha kuwa idadi ya Waislamu inaongezeka kwa kustaajabisha kwa raia wa Sweden, ambapo takwimu rasmi zinaashiria kuwa idadi ya Waislamu inaongezeka kila siku kiasi cha kufikia leo hii Waislamu 120 elfu.

Baada ya upanuzi wa misikiti ambacho ni kiashiria cha kusambaa kwa Waislamu, haswa wale walioshikamana na dini yao, tafiti hizo zinaonesha kuwepo kwa zaidi ya misikiti elfu 25 Ulaya pamoja na ongezeko la wenye kuswali katika misikiti hiyo miongoni mwa Waislamu.

Kwa mkabala tafiti zinathibitisha kupungua sana kwa wanaokwenda makanisani, utafiti uliofanywa na Dresdner Bank kuwa idadi ya wanaokwenda Makanisani huko Ujerumani imepungua katika miaka ya karibuni ambapo imetarajiwa kusimamisha misa za kidini katika makanisa 96 katika jumla ya makanisa 350 katika Essen Parish peke yake, na hivyo majengo ya kanisa kutumika katika malengo mengine, na hiyo ni kwa sababu ya kupungua wenye kwenda makanisani na kupungua kwa mapato ya kanisa.

Pengine kinachoonekana ni udhaifu mkubwa wa Wakristo kwenda makanisani mwao, kiasi cha hali hiyo kufikia katika kanisa moja katika nchi ya Ulaya lilifanya mashindano ya magari ili kuwavuta watu kwenye sala; kwa sababu ya uchache wa wenye kwenda kwenye makanisa.

Maiko: Hilo linaweza kufasiri tunachokiona katika zile hali ngumu za vyama vya mlengo wa kulia na baadhi ya wenye kasumba Ulaya kwa kuwabana Waislamu na kukebehi Uislamu Tuli zake na kuwafanyia uadui watu wake au nembo zao, bali kuwataka Waislamu wote waondoke Ulaya, Je, ni nini sababu za kuenea huku…haujakusudia bwana Rashidi kinyume cha mazoea yako?!

Rashidi: Bila shaka mimi ni mwenye kufurahi kwa ninayosikia, kwa hiyo nimechagua kunyamaza ili nizidi kusikiliza….kwa mtazamo wangu kuna sababu ndani ya Uislamu wenyewe, na kwa sababu ya jamii yenyewe ya Magharibi, na sababu zingine za mazingira: Na vipengele vingine vyenye kuchangia kusambaa kwa Uislamu…. Lakini nitaashiria kuwa hilo sio geni kwa dini kongwe, mizizi yake imesambaa na kunyooka tokea kuumbwa kwa mwanadamu, tokea Adam (‘Alayhi salaam), wala mzizi huu wa kihistoria hadi hivi sasa haujakatika.

Maiko: Hata hivyo bwana Rashidi sisi tunajua kuwa Uislamu haujadhihiri isipokuwa miaka elfu moja na mia nne tu iliyopita, na kama unavyojua kuwa kuna dini zingine za mbinguni, kama vile Ukristo na Uyahudi au utapinga hilo?!

Rashidi: Kuna ufahamu katika jambo hili unapaswa kusahihishwa, nao ni kuwa dini ya Mwenyezi Mungu ni moja na sio nyingi, moja kwa sababu inatoka katika chanzo kimoja, nacho ni kutoka kwa Allah (Mungu Mmoja) aliyeumba viumbe vyote, lakini kuna baadhi za hali ambazo huchungwa na dini hii moja inapelekea uwepo wa sheria mahsusi kwa hali hizi au katika umma mbali mbali, kama ambavyo inaweza kutokea upotofu wa dini hii kutokana na matokeo au umbali wa (wakati) kutoka kwenye chanzo cha ujumbe wenyewe, hivyo basi ikabidi kuhuisha dini kwa kutuma Mtume mpya ambae atathibitisha misingi ya dini hii, hili ndilo lililoashiriwa na hadithi ya Mtume wa Uislamu: “Manabii ni ndugu, dini yao ni moja, lakini mama zao ni wengi.” Yaani nyakati zao na sheria zao ni nyingi na zinatofauatiana, ama kilele chake kilikuwa wakati wa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na Ujumbe huu wa Mtume huyu ulikusanya vipengele vyenye kuhifadhi usalama wa dini hii na kuto kupotea, ambao umeihuisha na kurejesha katika usafi wake. Hivyo basi dini hii haitokatika na unyoofu huu wa kihistoria utaendelea hadi kuisha kwa wanadamu, kwa kuzingatia kuwa ni dini ya mwisho aliyoichagua Mwenyezi Mungu kwa wanadamu, hivyo katika hali ya kawaida ni yeye kuwaridhia wao yanaoafikiana na maumbile yao na kawaida kupata kuenea huku kukiachwa yatafanyika kwa njia ya kawaida.

Rajev: Huu ni mtazamo mpya na wenye kunisisimua, kama ni hivyo turejee pale ilipokuwa ututajie sababu za kuenea kwa Uislamu.

Rashidi: Ndio; ama sababu za dhati za Uislamu tutafupisha kuwa sifa zake ndizo zinaifanya kuenea; nazo ni:-

Ni dini nyepesi katika jengo lake, yenye undani katika maana yake, wazi kwa mtazamo wake, imeenea katika mfumo wake, mafundisho yake ni mepesi, haihitaji uwezo mkubwa wa kiakili, haina talasimu, wala siri, wala ugumu wowote.

-Dini ya utu, huzungumza na maumbile ya mwanadamu na hutangamana nae katika mazingira yake, na kuitikia mahitajio yake, na kutibu kadhia zake, hujibu maswali yanayoelekezwa kwake na huunganisha katika jamii na kuthibitisha usawa uliotimia kati ya wanadamu kulingana na asili zao, juu ya tofauti walizonazo za rangi zao, ndimi zao, maarifa yao na viwango vyao vya kijamii.

Dini inayokwenda na mazingira, haiwi juu ya uhalisia wa mwanadamu wala haipotei, na kwa uhalisia huu ni dini inayokusanya baina ya dunia na akhera, wala haioni mgongano kati yake.

Dini inayoheshimu akili ya mwanadamu, na huithamini fikra ya mwanadamu na kuweka hoja za kiakili na njia za kimantiki juu ya kilele cha kufahamiana na kujadiliana katika mambo yanayofaa yenye faida.

Dini isiyopiga vita elimu na maendeleo, bali inaihamasisha, na hakika za kisayansi zilizothibitika walizofikia wanazuoni wa kisasa zinaafikiana na tafsiri ya mandiko ya Qur’an yaliyopokelewa katika nyanja zile kabla ya karne kumi na nne.

Dini inayokwenda pamoja na harakati za maendeleo, Uislamu umethibitishwa uwezo wake katika kuamiliana na mambo yenye kujitokeza na mabadliko ya kijamii ambayo yanajitokeza katika maisha kwa kutekeleza mabadiliko ya zama na mahala.

Dini yenye kumhakikishia mwanadamu uhuru wa kweli, ambao haufikiwi kwa ajili ya maana yake isipokuwa pindi mwanadamu anapompwekesha Mola wake kwa ibada ya kweli; kwa sababu ya hilo hawi mwanadamu ni mja kwa mwanadamu yeyote yule, au kwa kiumbe chochote, au mja wa kuyaabudu mazingira yake.

Dini iliyokuwepo na haitaacha kufunguka juu ya desturi zingine.

Maiko: Mimi nitakuambia sababu zilizojificha katika jamii ya Ki-magharibi.

Jamii zetu za Magharibi zinaishi katika janga la kifikra toka mwanzo wa karne iliyopita na kabla yake, na tatizo hili limejitokeza katika migongano mingi iliyoishi nayo jamii ya Magharibi, haswa baina ya kanisa na sayansi (elimu), kisha kati ya madhehebu mbali mbali ya kifalsafa na baina ya tabaka mbali mbali katika jamii tofauti, na hayo yameacha mpasuko mkubwa na babaiko, kukosekana kwa utambulisho.

Kisha baada ya hapo faragha ya kiroho ambayo inatoka kwa mwananchi wa Magharibi….faragha inayokaba roho ya mwanadamu na kuondoa hadhi yake na kushuka thamani ya mwanadamu…wakati ambapo vitu na maada vinakuwa juu ya hadhi ya mwanadamu na kufunika thamani zote za mwanadamu, kiasi cha kwenda kama vile mashine au sehemu ya mashine kubwa.

Kipengele kingine muhimu kina wakilishwa na shaka wanayoishi nayo Wamagharibi wengi kuhusu dini yao, na wanachokiona kuhusu kuwepo kwa migongano katika itikadi zao, pamoja na kasumba zilizo wazi kwao, achilia mbali yale yanayofanywa na Kanisa kwa kuzingatia kuwa ndio njia safi (tohara) na kusamehewa madhambi kwa njia ya utawa, wengi wetu wanaona kuwa ni kwenda kinyume na tabia na maumbile ya mwanadamu na kugongana nae katika mambo mengi ya maisha.

Hatuwezi kusahau kumomonyoka kwa maadili na kuparanganyika kwa familia na jamii ambayo imezikumba jamii nyingi za Magharibi.

Rashidi: Tukitaka kuzungumzia vipengele vya uhalisia, tunachokiona ni propaganda za kuupaka matope Uislamu, na kuwatesa wafuasi wake, hili linatupa kikwazo cha mtu kutaka kujua juu ya dini hii.

Kama ambavyo juhudi za wanaoita kwa Allah (wanaoutangaza Uislamu) na kuusambaza Uislamu, miongoni mwazo ni mijadala baina ya wanazuoni wa dini ya Kiislamu na dini zingine…hupelekea watu wa Magharibi kuujua Uislamu.

Usisahau athari za Waislamu wachache waliopo katika nchi za Magharibi, ambapo kuna fursa ile kwa Wamagharibi kujua kuwa ukaribu wa Uislamu kwa kuwaona Waislamu, jambo ambalo linatayarisha kuujua Uislamu na kuona namna wanavyoishi Waislamu wenyewe kiuhalisia.

Yote hayo yananipa hisia za hali nzuri ijayo inayothibitisha kuwa mustakbali ni wa dini hii.

Qur’an tukufu

Vitabu vya Sunna

Dr. Ibrahim Khalil:

Kwa nini rafiki yangu amesilimu? Na rai ya Vatican kuhusu changamoto ya Qur’an

Dr. Ibrahim Muhammad Ibrahim:

Dini za wanadamu katika vyanzo vyake vitukufu na mtazamo wa Kiislamu

Abu Al-A’ala Al-Maududi:

Uislamu kukabiliana na changamoto za kileo/kisasa

Uislamu na Mambo leo

Al-Hijab

Kuhusu utekelezaji wa shari’ah katika zama hizi

Misingi ya Uislamu

Sisi na Utamaduni wa Kimagharibi

Mfumo wa maisha katika Uislamu

Abu ‘Abdul Malik Walid bin Fahd Al-Wad’an:

Ujumbe kwa kila anayemuamini Yesu (Isa) amani iwe juu yake

Ahmad Deedat:

Dini inayokuwa haraka

Uchaguzi kati ya Uislamu na Ukristo

Suluhisho la Uislamu kuhusu Ubaguzi

Tofauti za kimsingi kati ya Uislamu na Ukristo

Mungu (Allah) katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu

Kati ya Injili na Qur’an

Tuhuma ya Upanga

Kwanini Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ndie mtukufu zaidi?

Kitabu kitakatifu kinasema nini kuhusu Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam)?

Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ndiye mtukufu zaidi ulimwenguni

Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ni khalifa baada ya masihi

Mtazamo wa Ibada katika Uislamu

Je, Masiya ndie Mungu? Jibu la injili kuhusu hayo.

Dr. Ahmad ‘AbduRahim As-Saayih:

Falsafa ya ustaarabu wa Kiislamu

Dr. Ismail Raji Al-Faruqi na Dr. Luis Limya Al-Faruqi:

Atlasi ya ustaarabu wa Kiislamu.

Dr. Ikram Lam’i:

Talaka katika Ukristo (Mtazamo wa Biblia)

Andrew Newton na wenzake:

Misingi ya Upagani katika Ukristo

Anwar Mahmuud Zanatiy:

Kamusi ya upotoshaji wa magharibi juu ya Uislamu

Bernad Louis:

Istanbul na Ustaarabu wa Dola ya Ukhalifa

Ja’ad Al-Karim Jaba’i:

Haki za wanadamu katika Fikra ya Kiarabu leo hii

Jamil bin Subaih:

Utekelezaji wa ukhalifa wa mwanadamu ardhini

Dr. Godfrey Conzelin:

Balaa lililoikumba ukristo na usekula ulaya (ushuhuda wa Ujerumani)

Dr. Hussein Mu’unis:

Ustarabu-Utafiti na misingi yake

Muhtasari wa katiba ya Umma wa Kiislamu

Khalid ‘Abu Al-Futuuh:

Uislamu na uliberali-Ukweli wa muelekeo wa Marekani na uwezekano wa makutano ya kifikra (makala)

Matumizi ya wakati na kuiongoza nafsi (makala)

Ustaarabu na istilahi zake (makala)

Kwa nini tunaichukia Marekani? (makala)

Yaliyojitenga na changamoto zake (makala)

Dr. Dawud Darwesh Hals:

Haki za kitamaduni za mwanadamu kati ya sheria za kiislamu na mikataba ya kimataifa

Roger Garuddy:

Wachimba makaburi-Ustarabu unaochimba utu kaburi lake.

Zigrid Honka:

Sun rising in the west: athari ya ustaarabu wa kiarabu ulaya

Sami ‘Amiriy:

Je, Qur’an imechukua kutoka katika vitabu vya mayahudi na manasara?

Su’d bin ‘Abdul ‘Aziz bin Muhammad Al-‘Arifi:

Dalili za kiakili na za kunukuu juu misingi ya itikadi

Sayyid Qutb:

Uislamu na matatizo ya ustaarabu

Mustakbali wa dini hii

Taswira za Kiislamu na nguzo zake

Dini hii

Dr. Sayyid Muhammad Badawiy:

Akhlaq kati ya Falsafa na Elimu Jamii

Dr. ‘Adil Swadiq:

Talaka sio suluhisho

Dr ‘Adil ‘Ali Shadi na Dr. ‘AbduRazaq Ma’ash:

Haja ya mwanadamu ya Ujumbe wa Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam)

‘Abass Al-‘Aqaad:

Athari ya waarabu katika ustaarabu wa watu wa Ulaya

‘Abdu Ad-Daim Kahiil:

Miujiza ya tiba ndani ya Qur’an na Sunna

Insaiklopidia ya miujiza ya nambari katika Qur’an tukufu

‘Abdur-Rahman Hassan Habanakah:

Udhibiti wa maarifa na misingi kutoa hoja na mijadala

‘Abdur-Rahman Al-Juzairy:

Dalili za yakini za kujibu ukosoaji wa wamishionari

Dr. ‘Abdul’Aziz Swaqr:

Dini na Dola katika mazingira ya magharibi..utafiti kuhusu nafasi ya dini katika nchi yenye kulingania uzalendo

Dr. ‘Abdul’Aziz bin ‘Uthman At-Tuwaijry:

Haki za mwanadamu katika mafundisho ya Uislamu

Dr. ‘Abdullah bin ‘Abdul Muhsin At-Turkiy:

Haki za mwanadamu katika Uislamu

‘Abullah Nasih ‘Ulwaan:

Vielelezo vya Ustaarabu katika Uislamu na athari yake katika kunyanyuka kwa Ulaya

Dr. ‘Abdul Muhsin bin Zain Al-Mutwairy:

Dalili za wazi kuhusu ukweli wa Utume wa mbora wa viumbe Swalla Llahu ‘alayhi wasallam

‘Ali Ezzet Bigovich:

Uislamu kati ya mashariki na magharibi

Dr. ‘Ali Muhyyiddin Al-Qurra Daghi:

Sisi na wengine

‘Ali bin Nayf Ash-Shuhud:

Kipambanuzi katika kujibu kuhusu ustaarabu wa magharibi

Dr. ‘Imaduddin Khaliil:

Walivyosema kuhusu Uislamu

Dr. Fahd bin ‘Abdu Rahman bin Sulaiman Ar-Rumiy:

Sifa za Qur’an tukufu

Dr. Mazin Al-‘Armouty, Numeir ‘Abass Madh-har, Kayyid Hashim

Uislamu na Umagharibi na Haki za binadamu

Michael Hart:

Watukufu mia moja mbora wao ni Muhammad

Mujahid Mahmud Ahmad Nasir:

Mfumo wa Qur’an katika kusimamisha hoja na dalili

Muhammad bin Ibrahim Al-Hamd:

Uislamu ni njia ya furaha ya milele

Muhammad Abu Zahra:

Jamii ya mwanadamu katika kivuli cha Uislamu

Muhammad Abul Qasim Hajj Hamd:

Mjadala juu ya yasiyoonekana (Ghaib) na mwanadamu

Dr. Muhammad Bashariy:

Uhuru wa kidini katika sheria ya Kiislamu

Muhammad Taqiddin Hilaal Al-Maghribiy:

Dalili ndani ya Biblia kuwa Issa ni mja na sio Mungu

Muhammad Rashid Al-‘Uwaidy:

Wao wanaangalia inavyoporwa

Dr. Muhammad Az-Zuhaily:

Haki za binadamu kiini cha makusudio ya sheria

Dr. Muhammad Dwiyaa Rahman Al-Aadhwami:

Tafiti katika Uyahudi, Ukristo na dini za India

Muhammad bin Twahir At-Tanyar Al-Bairuti:

Itikadi za kipagani katika dini ya ukristo

Muhammad Twahir bin ‘Ashuur:

Muhtasari wa msingi wa mfumo wa kijamii katika Uislamu

Dr. Muhammad bin ‘Abdullah bin Swalih As-Suhaim:

Uislamu-Misingi yake

Dr. Muhammad ‘Ammarah:

Uislamu na haki za binadamu…mambo ya msingi na sio haki peke yake

Baina ya Kusamehewa madhambi na maendeleo..manabii katika Qur’an na kitabu kitakatifu (makala)

Muhammad Al-Ghazali:

Haki za mwanadamu

Muhammad Qutb:

Shubuhaat (utata) dhidi ya Uislamu

Muhammad Mutawalli Ash-Sha’arawiy:

Dalili za Kimaada za kuwepo Mungu

Muhammad Yasin:

Majibu ya wanazuoni wa Kiislamu kuhusu tuhuma za wayakinifu na mustashrikina

Kituo cha mabadilishano ya Utamaduni, kwa kushirikiana na Unesco:

Athari ya Waarabu na Waislamu katika kunyanyuka kwa ulaya

Dr. Marwan Ibrahim Al-Qaisiy:

Insaiklopidia ya haki za mwanadamu katika Uislamu

Nasir bin Dakhilillah bin Falih As-Su’aydiy:

Hoja za kiakili na maana za kibalagha

Harun Yahya:

Hadaa ya maendeleo

Ufahamu wa haraka wa imani

Qur’an ni muujiza wa miujiza

Miujiza ya Qur’an

Hanz Henry. H. Shebder:

Roho ya Ustaarabu wa kiarabu

Dr. Hiba Rauf Ezet:

Matatizo ya maana ya haki za binadamu (makala)

Wahiddudin Khan:

Changamoto ya Qur’an

Kadhia kubwa

Dr. Yahya bin Muhammad Hassan Zamzami:

Haki za mwanadamu-maana na utekelezaji wake katika Qur’an tukufu

Yusri Muhammad Sa’id Mubyadh:

Siku ya mwisho katika dini za mbinguni na dini za kale

Dr.Ya’aqub bin ‘AbdulWahab Al-Bahusein:

Njia za kutolea dalili na nguzo zake kwa watu wa mantiki na watu wa usuli