Minara ya Njia

Minara ya Njia

Minara ya Njia

Katika moja ya meza hapo Social Lounge, walikutana marafiki watatu; Rashidi, Maiko na Rajev, na kila mmoja kuagiza kinywaji akipendacho, kisha Rajev akaanza kuzungumza:

Katika kikao chetu kilichopita tulifikia kwenye mazungumzo kuhusu sifa ambazo anasifika nazo Mungu wa kweli, na jinsi ya kufahamu dini ya haki kwenye zingine.

Maiko: Niache nithibitishe uhakika na kuuliza swali: Bila shaka elimu katika matawi yote imepita hatua kubwa sana, kwa mfano elimu ya tiba leo hii imeitangulia iliyokuwepo kabla ya karne mbili, teknohama (Teknolojia ya habari na mawasiliano) imepaa mno, na kadhalika hakika nyingi zilizopo kwenye elimu ya Kemia…., na mara kwa mara mitaalaa huendelezwa kufundisha elimu hizo kwa haraka mno, kiasi cha kufikia vumbuzi mpya, hatupati katika elimu hizi za maada atakayesema leo hii miongoni mwa wanazuoni wa maada kuwa ardhi inafanana na mpira kwa mfano, wakati ambapo katika elimu za fikra bado ipo katika kujadili kadhia zile zile za miaka elfu iliyopita juu ya: Kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, dini ipi ni ya kweli, ni mfumo upi unamfaa mwanadamu katika maisha yake, na maana ya uadilifu…..na nyinginezo katika mitazamo na taswira mbali mbali, ukisema kuwa elimu inaendelea na kukua, kwa nini basi tusiseme vile vile kuwa nayo dini inakua na kuendelea?

Rashidi: Tokea maelfu ya miaka imani inagongana na taswira na fikra mbali mbali, na mgongano huo unaendelea hadi leo hii, kwa njia ya moja kwa moja au isiwe ya moja kwa moja, na hii Ina maana kuwa akili ya mwanadamu haijafikia katika elimu ya fikra kwenye maendeleo kama elimu za maada zilivyofikia maendeleo makubwa, na hii ni kwa sababu msingi wa uwepo wa mwanadamu haukubadiika, vivyo hivyo kadhia kubwa za msingi wa mwanadamu zinazoshughulisha fikra zake hazijabadilika vile vile.

Mwanadamu siku zote anatafuta tafsiri pana ya uwepo inayokusanya kila kitu, na huamiliana kwa msingi huu na uwepo huu..hutafuta tafsiri inayosogeza udiriki wake kwenye tabia ya hakika kubwa ambazo anaamiliana nazo, tabia ya mahusiano na hakika hizi, zinazotufanya kuwa ni watu tulioumbwa, yaani viumbe ambavyo vinaainisha mahusiano yao na Mungu pamoja na wengine, kwa hivyo basi tunaweza kufaidika na waliotutangulia katika kadhia hizi kama ambavyo tunaweza kufaidika na waliomo, hivyo basi maudhui ambayo imeshajadiliwa ndio maudhui hayo hayo yaliyoibuliwa, nayo ni maudhui yanayohusiana na ulimwengu, maisha na mwanadamu, ikiwa watu wameafikiana katika hakika nyingi za kielimu za kimaada wao hawakuafikiana katika hakika nyingi zinazohusiana na maudhui nyingi, taswira na mitazamo ya kifikra mbali mbali, na hali hii haitoisha ila kwa kuisha mwanadamu.

Maiko: Hivyo basi tunaweza kusema: Sisi hatuwezi kufikia kwenye hakika katika mfano wa maudhui haya.

Rashidi: Nani amesema hivyo? Vinginevyo nini faida ya mjadala?! Ninaamini kuwa tunaweza kupitia mjadala wetu wa kifikra pamoja na umuhimu wa kujitenga ili kufikia kwenye haki na kuacha matamanio na kasumba, kwa mwenye kutaka kufikia kwenye ukweli kwa nia safi na kufuata njia inayopelekea huko basi Mwenyezi Mungu atamuongoza kwenye njia hiyo, na dalili ya hilo ni kuwa pamoja na kuwepo kwa mgongano huu maendeleo yalishafikiwa chini ya Manabii na waja wema au watu wenye fikra, bali wakati mwingine kupitia dola mbali mbali, hata hivyo makusudio ni kuwa babaiko na migongano ni sifa inayosuhubiana na kadhia za kifikira au za kibinadamu nayo ni tatizo la zama zote za kale na za sasa.

Lakini niache nikutanabahishe katika nukta mbili muhimu katika suala hilo, nazo ni:

Kwanza: Kutangulia katika elimu ya maada haina maana kuwa yatakuwepo maendeleo ya kifikra, taswira na ufahamu, kwani hakuna mafungamano baina ya maudhui mbili na dalili ya hilo kwa mfano ni ukaribu wa kimaada wa Marekani na Japan pamoja na tofauti zilizopo za taswira na ufahamu na fikra ya mwanadamu na ya kidini, na hii ina maana kuwa kuendelea kwa baadhi ya jamii katika baadhi ya elimu za kimaada haina maana kuwa ni lazima ziendelee katika elimu na fikra.

Pili: Ni kuwa, hakika haipati usahihi wake na kutiwa nguvu na kundi la watu au kupinga kwao kwa sababu jamii ya mwanadamu mara nyingi huangukia kwenye batili, bali historia ya mwanadamu imesajili mjumuiko wa watu wengi wapo katika taswira zenye makosa au matendo yasiyokuwa ya kimaadili au hata ujambazi wenye kutisha.

Rajev: Naafikiana nawe katika hilo, lakini naona kuwa sisi tupo katika vyanzo tofauti vya staarabu, na kadhalika sote tunabeba itikadi na taswira mbali mbali, hivyo hapana budi tuafikiane kwanza katika misingi au hoja ambazo tunathibitishia ukweli wa jambo au kutosihi kwake.

Maiko: Naona kuwa hakuna njia ya hilo isipokuwa kupitia njia mbili: Akili, au elimu.. hili ndilo tunaafikiana wote.

Kimsingi nakubaliana nawe, lakini ni akili gani unayoikusudia? Kwani akili yangu sio akili yako, kadhalika elimu gani?, Je, unakusudia elimu ya majaribio peke yake?

Nakusudia matumizi ya akili ya kuzaliwa ambayo watu wawili wowote hawatofautiani au hoja za kiakili ambazo tunakubaliana nazo, na nadhani sisi hatutofautiani juu ya hakika za kisayansi zilizothibitishwa kisayansi, na bila shaka hii ni tofauti na zile fikra za kielimu au nadharia au majaribio ambayo hayajafikia kwenye kiwango cha ukweli, je, huafikiana nami katika hilo.

Rashidi: Nakubaliana nawe katika hilo, lakini naashiria katika hoja nyingine ambayo umuhimu wake haupo mbali na hoja hizi: Nayo ni hoja ya mazingira katika maumbile. Ambapo nataka kuleta hoja nyingine inayohusu mamlaka ya matumizi ya akili na sayansi. Kwamba kuna tofauti kati ya kinachothibitishwa ana akili kuwa ni kosa au hakiwezekani au kile ambacho akili inakiona kuwa ni kigumu kukifahamu.

Rajev: Unakusudia nini kwa hoja ya maumbile?

Rashidi: Nakusudia: Hisia au muelekeo wa mwanzo wa ndani ya mwanadamu ambao wanashirikiana watu wote, kuna tabia na sifa ambazo zimewekwa kwenye vitu vilivyopo, iwe ni kwa vitu, mimea, au mwanadamu na mnyama, kwa mfano: Tunasema kuwa katika maji kuna sifa ya kuchemka itakapofikia daraja mia moja, au mwili wa mwanadamu unahitajia uwe na joto kati ya asilimia 34-42 ili mtu abakie kuwa hai, mambo haya yapo katika vitu hivi ila vimekuwa bila ya mwenyewe au chenyewe kutokuwa na matakwa yake katika hilo.

Maiko: Unakusudia silika iliyopo kwa mwanadamu na mnyama?

Rashidi: Silika zilizopo kwa mwanadamu na mnyama, nayo ni maelezo kuhusu sifa mahususi za ndani inazozitoa katika maisha yake, kama vile silika ya kushambulia na kuwinda kwa wanyama wakali, hakuna mtu ambaye anaingiza uelekeo kwa wanyama, au kuelekea na kurudi katika nchi zao za asili kwa ndege, na kuhamahama kwa samaki, na silika ya umama kwa wanawake, na mwenye silika ile anaweza kulifahamu hilo lakini asitanabahi siri ya silika yake.

Ama maumbile na mambo ya kimaumbile, hayo yanapatikana kwa mwanadamu tu, nayo vile vile ni mambo ya kiasili kwake na sio anayoyapata kutoka nje, naye anayajua na kuyadiriki, lakini tofauti kati ya maumbile na silika, ni kuwa silika huwa katika mambo ya kimaada, wakati ambapo maumbile ya asili (Fitrah) huhusiana na mambo ya kibinadamu, kwa mfano: Kupenda elimu na maarifa, kutafuta ukweli, hamu ya uvumbuzi, kuelekea kupenda kheri na fadhila, kuelekea kupenda uzuri…. Mwanadamu hupenda vitu hivi na kuvitafuta na kuvutika navyo bila kuingilia mazingira yenye kumzunguka wala bila ya kuyapata kutoka kwenye malezi anayolelewa au makuzi yake ya kijamii, kwa hivyo mambo ya fitra yamepandwa kwa mwanadamu na huota katika dhati yake, mfano wake ni mfano wa silika za kihayawani, lakini ni mambo maalumu kwa mwanadamu, na fitra hii kwa mwanadamu ndio ambayo humfanya mwanadamu kukubali mazuri na kuchukia mabaya, hivyo huwezi kumpata mwanadamu mwenye maumbile sahihi anayechukia mafuta mazuri na mandhari nzuri na kuvutika na harufu mbaya na mandhari mbaya.

Rajev: Tutawezaje kuainisha mambo haya ya kimaumbile, ili tuweze kuhukumu kuwa jambo hili ni la kimaumbile au sio?

Rashidi: Mambo ya kimaumbile kwa mwanadamu yanajulikana kwa sifa nyingi miongoni mwazo ni:

- Pana, yanayokusanya mengi, na yanayoenea kwa watu wote.

- Ni ya zama zote, hayawezi kukidhi jambo katika zama moja na yasikidhi jambo jingine katika zama zingine.

- Yanayotokea ndani ya mwanadamu mwenyewe na dhati yake, wala hayapatikani kwa mtu kusoma au kwenye mazingira, pamoja na kuwa elimu ndio itakayoyakuza na kuyaendeleza.

- Hayawi chini ya utawala wa mazingira yenye kumzunguka, hata hivyo yanaweza kuathirika na baadhi ya hali, mambo ya maumbile yanaweza kubadilika usafi wake na kuharibika kwa tabia yake, hali hiyo ni kama hali ya milango ya fahamu ya mwanadamu kama vile kusikia, kuona, kuonja akipata maradhi, hata hivyo kwa ujumla hayafutiki, bali yanaweza kudhoofika au kufifia bila kuondoshwa kwenye misingi yake.

Maiko: Naona kuwa sisi tumeafikiana juu ya yaliyoelezwa, lakini kwa sababu ya nukta hii ya mwisho nina mashaka katika baadhi ya mambo, kuwa maumbile ni moja ya nyenzo za kuthibitisha katika maudhui yetu.

Rajev: Tunaweza kujadili masuala yanayohusiana na maumbile wakati wake, tukikubaliana sote basi tutaafikiana juu yake, na na tusipokubaliana tutatafuta hoja nyingine.

Rashidi: Kwa mnasaba huu napenda kutanabahisha baada ya kuafikiana nyenzo hizi kuwa huenda baadhi ambao hawafahamu wakadhania kuwa kuwafikiana kwetu katika nyenzo hizi hakuafikiani na dini ya Uislamu, na hili ni kosa.

Maiko: Ninachokijua ni kuwa dini iliyosimama katika imani kwa maandiko matakatifu na kujisalimisha kwa ukweli wa kadhia zake haikubali mjadala au kusitasita, kwa ajili hii kumetokea vita vingi katika historia ya Ulaya baada ya uvumbuzi wa kielimu, ambapo Kanisa ilikuwa likipiga vita uvumbuzi na fikra ya akili inayojitenga na kitabu kitakatifu.

Rashidi: Maneno yako ni sahihi pamoja na kuzuia baadhi za rai zangu, hata hivyo hilo halihusu Uislamu, ni kweli dini inasimamia imani kwa maandiko matakatifu, na kukubaliana na usahihi wa kadhia zake ni usahihi kabisa, lakini Uislamu umeifanya akili, kufikiri, elimu inayotokana na mazingatio, kuangalia kwa kina, uzoefu katika nafsi na katika matarajio ni njia ya kumuamini Mwenyezi Mungu na Qur’an, kitabu kitakatifu cha Waislamu na Mtume wake… Historia ya Uislamu haijashuhudia mgongano huu na mgogoro unaozungumzia kati ya dini, elimu na akili.

Rajev: Jambo la kushangaza kabisa, kitabu chenu kuhimiza na kuheshimu akili, tafakuri na elimu!

Maiko: Namuona muhusika wa ukumbi anatuashiria kuwa muda wa kufunga umekaribia, tusimame katika nukta hii na tukamilishe kesho.

Rajev: Mimi nitakuwa mwenye shughuli kesho, nitafurahia kama mtakubali mualiko wangu kesho kutwa katika safari ya pembezoni mwa mto Seine.

Maiko na Rashidi: vizuri sana, bila shaka tutafurahi.