Laura VecciaVaglieri.

quotes:
  • Tawhidi halisi.
  • “Mtume wa Waarabu Muhammad kwa sauti kutoka kwa Mola wake, amewaita waabudu masanamu, wafuasi wa Ukristo na Uyahudi yaliyopotoka kwenye dini safi ya Tawhidi, na hivyo kuridhia kuingia katika mgogoro mkubwa pamoja na makundi mengine ya watu ambayo yanampeleka mtu katika kumshirikisha Muumba na miungu mingine.”


  • Uislamu wa Kilimwengu.
  • Kwa hakika aya za Qur-aan ambazo zinaashiria kwenye Uislamu wa Ulimwengu kwa wasifu wake kuwa ni dini ambayo Mwenyezi Mungu amemteremshia Nabii wake kuwa (Rehema kwa Walimwengu): Huo ni mwito wa moja kwa moja kwa Ulimwengu wote. Hii ni dalili ya wazi kuwa Mtume alijua kwa yakini yote kuwa ujumbe wake umekadiriwa kuvuka mipaka ya Ummah wa Kiarabu, na kuwa ni juu yake kufikisha neno jipya kwa watu wanaonasibika na jinsi tofauti wenye kuzungumza lugha tofauti.”