Kikombe cha Usahaulifu

Kikombe cha Usahaulifu

Kikombe cha Usahaulifu

Rashidi alikutana na rafiki yake Maiko mgahawani kulingana na ahadi yao, pindi tu walipokaa Maiko akamuwahi Rashidi kwa kusema:

Usiku huu napendekeza maudhui ambayo naamini utakubaliana na mtazamo wangu.

Rashidi: Subiri kidogo rafiki yangu, hebu tuagize kinywaji kwa heshima yako!!,

Maiko: Samahani kwa kuwa na pupa, una haki katika hilo.

Maiko alimuita mhudumu…nae mhudumu akaelekea kwao, akamuuliza Rashidi anachokitaka.

Rashidi: Chai

Mhudumu (kwa mshangao): Chai?!

Rashidi: Pamoja na ndimu.

Mhudumu (kwa mshangao zaidi): Chai pamoja na ndimu?!

Maiko (huku akicheka): Ndio, ni Muislamu huyo hanywi pombe…nami hali kadhalika chai na ndimu nikitanguliza samahani kwa kujipendelea ili nifanane na rafiki yangu.

Mhudumu aliondoka ili awaletee mahitaji yao wakati ambapo Rashidi alikuwa akiguna huku akiuliza: Sijui kinachoshangaza ni nini katika hilo?!

Maiko: Ewe rafiki yangu, kwa hakika unywaji pombe nchini mwetu ni kama vile unywaji wa maji, kuna aina nyingi na ladha nyingi na njia nyingi za unywaji; ndio maana mhudumu akashangazwa na ‘oda’ yako ambayo haina pombe, hanywi hivyo isipokuwa mtoto…samahani…samahani…

Rashidi: Hilo kwa hakika ni jambo la kushangaza!

Maiko: Nini la kushangaza? Hili si jambo jipya kwetu, na halipo nchini kwetu peke yake, bali nchi zote za Magharibi.

Rashidi: Hili haswa ndilo jambo la kushangaza.

Maiko: Ki vipi?!

Rashidi: Kwa sababu wengi wenu ni Wakristo, na inakuwa ni wajibu kwenu kuamini kitabu kitakatifu, na taurati imebainisha kuwa katika kunywa pombe kuna madhara makubwa na imeeleza kwa kutahadharisha, “Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo…”(Mithali 23:20) na imekataza kulewa: “Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao….” (Isaya 5:11).

Na katika maandiko ya injili imekuja katika Mambo ya Walawi (10:8). “Kisha BWANA akanena na Haruni, na kumwambia. Usinywe divai wala kileo chochote, wewe, wala wanao pamoja nawe…” na katika safari ya hukumu (13:14). “Asile kitu chochote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu chochote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze. Kisha Manoa akamwambia huyo Malaika wa BWANA….” Na mengineyo katika maandiko hayo mengi yenye kukataza unywaji pombe, na kukataza kukaa na walevi, bali huchukizwa hata kuwaangalia.

Maiko: Subiri ewe Rashid: Usidhani kuwa ni wewe peke yako tu ndie mwenye kujua vitabu vitakatifu, viongozi wengi wa dini huku kwetu wamehalalisha unywaji pombe, na wengine wamesema kuwa hata kwenye taurati kuna mtume mmoja amekunywa pombe hadi akalewa, nami nimewasikia baadhi yao wakisema kuwa kilicho haramishwa ni kulewa tu, na katika injili ni kuwa masihi alikunywa pombe, katika injili ya Luka tunasoma: (7:33) “Kwa kuwa Yohana mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, ana pepo. Mwana wa Adamu amekuja, anakula na anakunywa; nanyi mwasema, tazama mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi.”

Rashidi: Unachokisema ewe rafiki yangu kinatupelekea katika matatizo mawili makubwa yenye athari kwa mtu wa Magharibi na jamii za Magharibi:

Ya kwanza: Nasikitika kukuambia:Ukweli wa kitabu chenu kitukufu hivi sasa inathibitisha kuwa ndani yake kuna upotoshaji mwingi na kuwa mikono inayomhudumia ibilisi imekipotosha; kiasi cha kukifanya kinapingana katika itikadi nyingi miongoni mwazo ni: Kuharamisha pombe na kuihalalisha, na kunasibisha kunywa kwake na masihi (amani juu yake) kuwa ameinywa na wakati huo huo ikamkosha na hilo, imekuja katika Luka vile vile (1:15) ikitoa wasifu wa Masihi (juu yake amani) kwa ndimi ya Jibril (amani juu yake), kwani tunasoma: “Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za BWANA; hatokunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.” Angalia mgongano upo wazi.

Ya Pili: Watu wenu wa dini wamekihodhi kitabu kitakatifu, baadhi yao wanadai kuwa wanaongea kwa jina la bwana, lakini wengi wao wanaona wana mamlaka ya kuharamisha na kuhalalisha, na nyie mnawafuata wao kwa hilo.

Maiko: Kweli kabisa, na kwa hili ninakuambia ukweli kuwa: Wengi wetu hawaamini ukweli wa kitabu kitakatifu wala hawaamini watu wa dini, kuna mabadiliko makubwa sana yametokea katika jamii zetu tokea zama za kunyanyuka kwa Ulaya.

Kwa hiyo basi tunapotaka kufuata kwa ukweli imani yetu hutupeleka kwenye akili na elimu za maada tu,…achana na vitabu vitakatifu na mambo ya dini, tuzungumze kwa kutumia akili na elimu.

Rashidi: Niruhusu nianze kuzungumza: Hili ni tatizo lenu nyinyi na dini, na haya ni matokeo ya tabu mlizopata na udhalimu wa kanisa na kupiga kwake vita elimu na sayansi, haswa katika karne ya kati, na kwa masikitiko mtazamo wenu wa dini ni mtazamo ule mliouona kwa Kanisa, na mnaonyesha kuwa dini inagongana na elimu na nafasi ya dini ipo kwenye kuabudu tu. Ama Uislamu hatusumbuki na tatizo hili, bali dini yetu inahimiza elimu, na ndani ya dini yetu hakuna siri takatifu ambazo zinahodhiwa na watu wa dini pekee.

Kwa ujumla tuzungumze katika lugha ambayo utatosheka nayo, lakini hilo haliendi kinyume na dini yangu, na nitakuthibitishia hilo.

Maiko: Haya tafadhali nieleze.

Rashid: Umezungumza kuwa unachoamini hivi sasa ni akili na elimu, kwa kuanza nakuuliza: Ikiwa akili ipo katika umuhimu mkubwa kiasi hiki, je, Pombe inailinda akili hiyo au inaipoteza?

Maiko: Huu ni mtego, sio swali.

Rashidi: Mwenyezi Mungu amemkirimu mwanadamu na kumfadhilisha juu ya viumbe wengi aliowaumba–na akamneemesha kwa neema ya akili, katika Uislamu Mwenyezi Mungu amemfanya asiyekuwa na akili hawajibishwi kisheria, Mwenyezi Mungu ametuamrisha tuilinde neema hiyo tukufu na kutoiga kitu kinachoweza kuiathiri, bali kuilinda ni moja ya mambo matano ya msingi katika Uislamu, kwa ajili hiyo ndio maana Uislamu umeharamisha pombe au kutumia mihadarati au mfano wa hayo katika vitu ambavyo vinaweza kupoteza akili ya mtu.

Maiko: Ni yepi hayo mambo matano ya msingi ambayo umeyataja?

Rashidi: Tukizamia hayo yatatuondoa katika maudhui yetu, hata hivyo kwa ujumla mambo hayo ya msingi ni matano: Dini, nafsi, akili, heshima na mali.

Maiko: Vizuri, endelea

Rashid: Kinachojulikana kielimu ni kuwa alkoholi (ambacho ndicho kinacholewesha) kinamezwa mara moja na utumbo mkubwa na mdogo, na haraka huingia katika mishipa ya damu, kisha baada ya hapo husambaa katika kila kimeng’enya cha kiwiliwili kwa wepesi sana, ikiwemo katika seli za ubongo.

Alkoholi huathiri (hata kama ni kidogo kiasi gani (0.03) katika mfumo wa akili (ubongo) na husababisha kupunguza umakini na utulivu katika harakati na kutoweza kutoa hukumu sahihi ya vitu, na ndio maana Qur-an yetu ikaharamisha kwa nguvu kwa kusema:

“Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet’ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.” (5:90).

Maiko: Hata hivyo tunaona kuwa katika pombe kuna baadhi ya faida, mfano kuchangamsha, kupasha joto, haswa katika nchi zetu zenye baridi.

Rashidi: Qur’an haikanushi kuwa katika pombe kuna baadhi ya faida, Allah Ta’ala amesema:

“Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri”(2:219), kwa sababu faida hizi hazilingani na madhara yake ndio maana Qur-an ikaharamisha, njoo tuzungumzie elimu ambayo unaiamini.

Mbali na athari zake za kitabia na madhara ya kinafsi na ya kijamii na matumizi ambayo hayazingatii hisia ambazo zinaweza kupelekea kwenye kufanya jinai na kutumbukia kwenye hasara ya mali na kuwaudhi wengine, elimu imethibitisha kuwa unywaji pombe na haswa kufikia kiwango cha ulevi na uraibu wake unasababisha madhara mengi ya kiafya:-

1-Huathiri katika tezi za mwili na husababisha mapigo ya moyo.

2-Husababisha kubanana kwa mfumo wa mkojo.

3-Husababisha vidonda vya tumbo na matatizo katika mfumo wa chakula.

4-Huleta matatizo makubwa na maambukizo ya moja kwa moja katika mdomo, koo, utumbo na ubongo na tezi ya endocrine.

5-Kuharibika kwa maini, kiasi cha kuyafanya maini yavimbe kama vile yanatokota motoni kiwango ambacho mtu hawezi kupona na ambayo yanapelekea katika kansa ya ini.

6-Madhara ya pombe kwa mfumo wa pumzi ni vigumu kuyahesabu.

Ama ulisemalo kuhusu kujipa joto kwa kutumia pombe, hilo hutokea kutokana na athari ya damu ya mnywaji pombe juu ya ngozi yake, ambayo hutokea kwa kupanuka kwa mishipa midogo ya damu kwa njia zote mbili za mshipa mkubwa upelekao damu moyoni na mirija ya damu, na ndio tunaona juu ya ngozi kumejaa damu yenye uvuguvugu ambayo hutoka katika maeneo mbali mbali mwilini ikibeba harara na joto; na ndipo hapo mnywa pombe anapojihisi kuwa ni mwenye joto lakini joto lenyewe sio la kweli, na ndio maana tunamuona mnywa pombe ngozi yake imekuwa nyekundu na hudhani kuwa hasikii baridi, na damu huendelea kuzunguka katika kiwiliwili katika mzunguko wake wa kawaida; kiasi cha kiwiliwili kukosa harara ya ndani na joto lenye kuhitajika katika matendo ya Fisiolojia ya kila siku katika maisha ya mtu.

Kuna njia zingine za kupata joto tofauti ya unywaji pombe, kinachofahamika ni kuwa Waislamu ambao wanaishi katika sehemu za baridi hawaingii kwenye kupata joto kwa kunywa pombe.

Maiko: Lakini angalia Ustadh Rashid maneno yako yanahusika tu katika hali ya mtu kulewa, na juu ya hilo nadhani kuwa unywaji pombe kidogo haudhuru.

Rashidi: Tatizo linajificha katika kuwa mtu anapoanza kunywa pombe huhisi uchangamfu kisha kiwiliwili kutaka nyongeza ya alkoholi; kinachofanya mnywa pombe kutaka ziada ya hilo, na kila anapozidisha kiwango cha alkoholi kiwiliwili kinahitaji nyongeza zaidi na hivyo hivyo kadhalika hali inaendelea.

Niache nikutajie ufupisho wa utafiti wa tiba huko New Zealand; imeashiria kuwa madhara yanayotokana na unywaji wa pombe (hata kwa kiwango cha chini au cha kati) kinazidi faida yoyote inayotarajiwa. Utafiti huu unapingana na ufahamu ulioenea katika nchi za Magharibi kuwa, kikombe kimoja tu cha pombe kila siku kinaweza kuzuia maradhi ya moyo, katika makala iliyotolewa na jarida la Lancet Medical. Profesa wa elimu ya magonjwa ambukizi wa Chuo Kikuu cha Auckland New Zealand, Dr. Rud Jackson anaona kuwa uwezekano wa kuzuia maambikizi yoyote ya ugonjwa wa moyo kwa ulevi mdogo au wa wastani wa pombe, ni mdogo sana kulinganisha na madhara yanayopatikana kutokana na unywaji pombe.

Hapa kunafichuka muujiza wa kisayansi na wa kisheria katika hadithi tukufu ya Mtume (Swala Llahu ‘alayhi Wasallam) inayosema: “Kila kinacholewesha ni haramu, kinacholewesha kingi chake basi kichache chake ni haramu.”

Maiko: Oouh, ulikuwa ni mjadala moto moto, nadhani mimi nina haja ya kupata glasi ya ndimu baridi (Juisi), ili tuhitimishe nayo kikao chetu.

Rashidi (Akicheka): Ndimu bila ya chai?! Isipokuwa hukutaja maudhui ambayo mimi nitaafikiana nawe.

Maiko: Basi na iwe ndio mjadala wetu ujao.

Rashidi: In sha Allah Ta’ala.