Jua la Waislamu Linaangaza Kwa Wanadamu

Jua la Waislamu Linaangaza Kwa Wanadamu

Jua la Waislamu Linaangaza Kwa Wanadamu

Baada ya kusalimiana, Rajev na Rashidi waliona pupa ya Maiko ya kutaka kuanza kuzungumza, Rashidi akamtania kwa kumuambia:

Haya Maiko je, umeandaa mshale wenye kutoboa katika kikao hiki, nitajaribu kuwa mbali na skrini kwa kukwepa mshale wako!!!

Maiko: Hapana, hapana, tulia….mara hii unaweza kukodolea skirini yako bila wasiwasi…ukweli ni kwamba mjadala uliopita umenihamasisha kuchimba ndani zaidi na kujaribu kufahamu mchango wa Waislamu katika maendeleo ya wanadamu, nikaona filamu hii yenye anuani “Gunduzi elfu moja na moja za Maktaba za siri.” (1001 inventions and the Library of Secrets) Muda wa filamu hii ni mdogo sana inachukua dakika (13) kumi na tatu tu, lakini ni yenye kuvutia na nzuri katika maudhui haya…inaelezea jinsi gani ustaarabu wa Kiislamu ulivyochangia katika maendeleo ya leo hii ya mwanadamu, filamu hii imepata zaidi ya tuzo ishirini ulimwenguni.

Filamu imechukua staili ya kisa kifupi, ambapo mkutubi wa maktaba ile anawaelekeza baadhi ya wageni wa maktaba wakati wa ziara yao ya moja ya maktaba ya shule, na katika ziara hii wanagundua nyakati zilizokuwa zikiitwa zama za kiza (dark ages), mwandishi wa hekaya hizo ambaye anaonekana katika skrini ni ‘Sir Ben Kingsley ambaye amechukua nafasi ya Mkutubi, ambaye baadae alichukua haiba ya mwanazuoni wa Kiislamu Al-Jazary, ambaye huwatambulisha vijana na baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu ambao wameishi katika zama hizo, huwatambulisha na hazina kubwa ya uvumbuzi ulioshuhudiwa na ulimwengu wa Kiislamu katika zama kati ya karne ya saba na karne ya kumi na saba, ambayo imepitia historia yenye msisimko ambao haujapewa heshima yake stahiki.

Rashidi: Ni nini muhtasari wa filamu yenyewe na inalenga nini?

Maiko: Filamu inalenga kuthibitisha kuwa kipengele cha msingi na msukumo mkubwa wa kuzaliwa karne ya mwamko huko Ulaya ni lile lililoshuhudiwa na ulimwengu wa Kiislamu katika mafanikio ya kielimu na ya kitamaduni ambayo yamefungua mtazamo mpya, mpana katika mikono ya wanazuoni na wavumbuzi ambao ni viongozi waanzilishi kutoka dini mbali mbali, na filamu inaonesha kuwa mtazamo huu ni hakika za Kihistoria imesahaulika kwa kiasi kikubwa.

Rajev: Maiko umeniongezea shauku ya kufahamu zaidi ya ulioyasema.

Maiko: Pana maelezo mengi katika jambo hili, miongoni mwa hayo ni: Kuwa Al-Jazry, mmoja wa wahandisi, mkemia na mvumbuzi katika historia, alivumbua saa ya tembo, ambayo utajo wake umekuwa kama vile simulizi tu, kama ambavyo alivumbua vifaa vingi ambavyo hutumika kama vyombo au mashine ambazo tunazitumia katika maisha yetu ya kila siku, kila sehemu katika mgongo wa ardhi, vyombo vya kimekaniki vimetengenezwa kulingana na wasifu wa kizamani ambao unabainisha jinsi nguvu ya upepo inavyoweza kutumika na maji ili kuleta mapinduzi katika kilimo….vile vile: Daktari wa ki-Andalus, Az-Zahrawy ambae amevumbua mamia ya vifaa vya operesheni kabla ya miaka elfu moja, hadi leo hii uvumbuzi wa vifaa vyake unaokoa maisha ya wagonjwa katika hospitali za kisasa, pamoja na kuzingatiwa kuchunga taratibu za operesheni miongoni mwao ni: Al-Hasan bin Al-Haythami wa mwanzo aliyefafanua wadhifa wa jicho, na kupitia filamu hiyo tunaona mfano wa vyombo na vifaa vya uchukuaji picha kwa undani na umakini zaidi, ili tuweze kujua jinsi Ibn Al-Haythami alivyoweka msingi wa uchukuaji picha na utengenezaji wa filamu.

Rajev: Nimeongeza taarifa muhimu bwana Maiko, lakini sio wewe peke yako ambaye umeyapa umuhimu na kufuatilia haya na kuyagundua, nami pia nimetafiti haya, na nimeangukia juu ya kitabu chenye kusisimua cha mwandishi mwanamke wa Kijerumani jina lake Sigrid Honka, chenye anuani. “Jua la Mwenyezi Mungu linaangaza kutokea Magharibi” Sun rising from west.

Maiko: Nini kipya ulichopata?

Rajev: Nimeangazia vitu vingi ambavyo sikuvitarajia, unajua kuwa maneno mengi yaliyopo katika lugha nyingi za Ulaya ni maneno ya Kiarabu?

Maiko: Jambo la ajabu kabisa! una hakika na unachosema?

Rajev: Kweli sifanyi utani, mathalani: Neno (Coffee) katika lugha ya Kiingereza na mfano wake katika lugha zingine za Ulaya, imechukuliwa kutoka neno la Kiarabu’ kahawa’ na ndani yake kumetoholewa neno ambalo linaashiria sehemu ambayo ndani yake kunanywewa kinywaji hiki…..Neno Rice limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu ’Uruz’ na neno (sofa) kwa Kiarabu ni (sufa), ambayo ina maana ya kiti (kikalio) chenye mwavuli jirani na msikiti, bali kuna maneno mengine mengi yenye maana ya kisayansi moja kwa moja nimeyapata vile vile, yenye kulandana na neno la kiarabu; kama vile neno (Alcohol).

(Kitabu) kimenijuza hakika nyingi nilizokuwa sizijui, mwandishi alizifupisha kwa kauli yake: “Hakika Ulaya inadaiwa na waarabu na ustaarabu wa kiarabu, na deni lililo katika shingo za watu wa Ulaya na mabara mengine kwa Waarabu ni kubwa sana, na ilikuwa ni wajibu kwa watu wa Ulaya kukiri hili tokea muda mrefu, lakini kasumba na tofauti ya itikadi zilipofua macho yetu, na kuacha kiza juu yake (pazia)”.

Rashidi: Rajev amenitia shauku kufahamu zaidi kilichokuvutia katika hakika hizi ambazo hukuwa unazifahamu hapo kabla.

Rajev: Mathalani: “Mimi sikuwa nafahamu kuwa wa mwanzo kujua makosa ya Galinous na kumkosoa, kisha akaja na nadharia ya mzunguko wa damu hakuwa Sarvitous wa Hispania wala hakuwa Harvie wa Uingereza, bali alikuwa ni mwarabu katika karne ya kumi na tatu C.E. naye alikuwa ni Ibn Nafiis, ambae alifikia uvumbuzi huu mkubwa katika historia ya binadamu na historia ya tiba kabla ya Harvie kwa miaka mia nne na kabla Sarvitous kwa miaka mia tatu…Sikuwa nafahamu kuwa mwanazuoni wa Kiarabu Muislamu Ibn Al-Haytham ndie wa kwanza kusahihisha kosa la Iqlidis na Batlimous, walipodai kuwa macho matupu ndio yenye kupeleka mwanga kwenye vitu ambavyo yanataka kuviangalia, alipokuja Ibn Haytham alitangaza kuwa kudai hayo ni makosa; kwani hakuna mwanga unaotoka machoni ili mtu apate kuona, bali ni kuwa vitu vyenye kuonekana ndivyo ambavyo vinaakisi mwanga machoni na hivyo mtu kupata wasaa kuviona kupitia miale yake, Kama ambavyo nilikuwa sifahamu kuwa Muislamu Muarabu Al-Bayruni ndie aliyevumbua dunia kuzunguka jua na katika mhimili wake na sio Nicolaus Copernicus au mwingine kama inavyosambazwa..kama ambavyo mustashrikina huyu maarufu alivyotaja kuwa daktari wa Kiislamu Ar-Raziy ambaye anazingatiwa na wanahistoria kuwa mmoja wa madaktari wakubwa wa zama zote, ambae makala yake kuhusu ugonjwa wa majeraha mwilini na kujaa maji, na mapele yenye kujitokeza usoni na mwilini kuwa ni kazi ya mwanzo iliyofanikiwa sana kuhusu maradhi ya tumbo, ikielezea nguvu kubwa katika uchunguzi wa kimaradhi, hili lilikuwa maarufu huko Ulaya kiasi cha kuchapwa zaidi ya mara arubaini kwa lugha ya Kiingereza tokea mwaka 1489 hadi 1866. Kama ilivyotajwa kuwa waarabu katika zama hizi ambazo huko Ulaya ziliitwa zama za kiza walikuwa wakifahamu nusu kaputi (anaesthesia) katika tiba ambayo walidhania ni uvumbuzi wa hivi karibuni, wakati ambapo ukweli unasema, na historia inashuhudia kutumia sponji ya nusu kaputi ni fani ya waarabu pekee, haikuwa inajulikana hapo kabla….na kuna ufafanuzi mwingi ambao ni vigumu kuuelezea katika mjadala huu.

Rashidi: Kwa hakika hili linajibu madai ya baadhi ya watu ambao hawajui hakika za kihistoria au wanakana kuwa Waarabu na Waislamu hawakuchangia kitu kipya katika ustaarabu, haswa katika sayansi/elimu za majaribio ‘Experimental Science’ ambapo mwanadamu hakujua mfumo huu wa majaribio isipokuwa chini ya mikono ya Waislamu na Waarabu, niruhusuni ninukuu baadhi ya maneno ya wanazuoni wa Kimagharibi katika eneo hili.

Mustashrik wa Kifaransa Claude Cahen anasema: ikiwa wanazuoni wa Kiislamu (bila kujali muelekeo wao wa Kifikra) wana uwezo mdogo kuliko Wayunani katika kuzingatia na fikra tupu, lakini walifidia hayo kwa muelekeo wao katika elimu za majaribio, maendeleo ya elimu yaliyofuata yalibainisha umuhimu wa muelekeo huu hivyo basi elimu waliyoacha Waarabu ni elimu waliyoishi nayo na kuitumia katika kubaki, na Ar-Razy (mmoja katika wanazuoni wakubwa) alielezea na kufafanua vizuri kwa uwazi, uwezekano wa kuendelea kwa maendeleo ya kisayansi, nayo ni msingi wa ajabu kwa wanafikra wa zama za kati. Mtafiti mwanamke mtaliano Lora Fiche anajiuliza;

“Je, Waarabu hawakuwa ndio wa mwanzo ambao waliotutengenezea njia ya majaribio kabla ya Roger Becon kutangaza umuhimu wa jambo hilo kwa muda mrefu?! Na Kemia ikaendelea pamoja na elimu ya nujumi (astronomy) na kusambaa kwa elimu ya kigiriki, na kukua kwa elimu ya tiba na kuvumbuliwa kwa kanuni mbali mbali za fizikia, je, haya hayakuwa katika athari za Waarabu?!” Mwanafalsafa na mwanahistoria wa Kimarekani Will Durant anasema: “…Sayansi ya Kiarabu imekulia katika elimu ya kemia na njia za majaribio ya kisayansi, nazo ni nyenzo muhimu za kisasa za akili ndio fahari yake kubwa, na Roger Becon alipotangaza umuhimu wa kutumia njia hii huko Ulaya hilo lilikuja baada ya Jabir (Ibn Hayyan) kulitangaza kwa miaka mia tano, jambo ambalo lilimuongoza kwenye hilo ni nuru ambayo imeangaza njia kutokana na Waarabu wa Andalus na haukuwa mwanga huu wenyewe tu, isipokuwa ni mwanga wa nuru ya Waislamu wa Mashariki.”

Na hili ni sehemu ndogo inayoweza kusemwa kuhusu nyanja za uvumbuzi wa ustarabu wa uarabu wa Kiislamu ambao umeutoa kwa watu.

Maiko: Kwa hakika mtu hawezi kukana mafanikio haya, hata hivyo hatuwezi kusahau vile vile kuwa ustaarabu huu umefaidika vilevile na staarabu nyinginezo kama vile ustaarabu wa Kiyunani.

Rashidi: Rafiki yangu hii ndio hali na tabia ya maendeleo ya kisayansi: Ni mnyororo ulioungana katika mafanikio ya mwanadamu, na ndilo linalofahamika kwa jina ‘mnyororo wa mizunguko ya ustaarabu’ na ndilo analolihimiza mustashriki wa Kifaransa Aldo Mail; “…..Elimu hii ya Waarabu inaeneza mnyororo wa mawasiliano na kuendelea baina ya staarabu za kale na ulimwengu mpya wa leo hii, na kama sisi hatutapambana na elimu ile ya Waarabu wala kuifahamu tutajikuta tukiwa watupu tu, inashindwa kufasiri kati ya staarabu za kale na staarabu zetu leo hii.”

Dr. Toby E. Huff wa kitengo cha Historia ya elimu wa Chuo Kikuu cha Harvard mwenye kitabu: The Rise of Early Modern Science: Islam, China and the West.” kuwa kuhamisha maarifa ya kisayansi na ya kifalsafa ambayo yamepandana na kuhifadhika katika ustaarabu wa kiarabu na Kiislamu kwenda Magharibi kupitia juhudi kubwa ya tarjama ambayo imesimamiwa na watu wa Ulaya katika zama za kati, ilikuwa na athari kubwa katika maendeleo ya fikra za Magharibi.

Lakini niache niseme: Kwa hakika mafanikio ya ustaarabu wa Kiarabu wa Kiislamu ambao unasifika na sifa ambayo haijawahi kusifika nao ustaarabu mwingine, kama vile:

Elimu ya Kiislamu sio tu haijatengana na dini, bali dini ilikuwa nguzo na nguvu yenye msukumo mkubwa.

Kwa hakika elimu ya Waislamu haikuwa siri, bali walipupia kuueneza kwa watu kwa mafungamano yao tofauti, kwa hiyo vyuo vyao vikuu vilikuwa wazi kwa wanafunzi wa Ulaya ambao walihamia kutoka kwenye nchi zao kutafuta elimu.

Hakika mimi ni mwenye kujifakharisha na ustaarabu ule. Mwanadamu Anapotengwa