Je, Mke Mmoja Anatosha?!

Je, Mke Mmoja Anatosha?!

Je, Mke Mmoja Anatosha?!

Pamoja na Rashidi kufika kwenye ahadi waliyokubaliana kwa wakati alimkuta Maiko akimsubiri mezani, huku akiwa ameshachukuwa kinywaji cha maamkizi….Rashidi alimsalimia na kukaa kwenye kiti chake.

Maiko: Nimekuletea kinywaji chako ukipendacho, chai kwa ndimu…hivi ndivyo nilivyodhania kuwa utakunywa ukipendacho daima.

Rashidi: Maamkizi yaliyokubaliwa, pamoja na kuwa ndicho kinywaji nikipendecho, ila napendezwa zaidi kubadilisha hata kama hicho kingine kitakuwa ubora wake ni mdogo…nadhani hii ni tabia ya wanadamu wote.

Maiko: Huenda nikaafikiana nawe, lakini hebu tuachane na hili, tuanze maudhui yetu….Samahani Je, nikuagizie kinywaji kingine?

Rashidi: Hapana, hapana asante, inaelekea una hamasa sana na mjadala!

Maiko: Sio katika sura hii, lakini ili muda usituache katika kuzungumzia maudhui mengine kama ilivyopita katika kikao chetu kilichotangulia.

Rashidi: Kama ni hivyo na tuanze basi.

Maiko: Kama niliyokuambia katika kikao chetu kilichopita, maudhui ambayo nataka mjadala wake kuuzungumzia, naamini utaafikiana nami katika mtazamo wangu, pamoja na elimu niliyonayo kuwa imesambaa katika jamii yenu itikadi ya kinyume na mtazamo wangu huu.

Rashidi: Vizuri sana, mimi sipendi kutofautiana, na mjadala wangu pamoja nawe ili kufikia kwenye kushirikiana kutosheka, au kwa uchache ufahamu ulio sahihi kwa mtazamo wa kila mmoja wetu. Kama ni hivyo maudhui ni ipi basi?

Maiko: Kwa ufupi ni kuwa mimi naamini kuwa mahusiano ya ndoa yanapaswa kuwa ni ya mmoja katika pande zote mbili, kwa njia iliyo wazi zaidi. Ninadhani kuwa mfumo wa wake wengi ambao Uislamu umeuhalalisha ndani yake, kuna aina ya dhulma kwa mwanamke …je, huwafikiani nami katika hilo?!

Rashidi: Mwanamke gani unayemkusudia?

Maiko: (akiwa ni mwenye kushangazwa): Mwanamke! Nakusudia mke wa ndoa!....Je, kuna mwanamke mwengine katika mahusiano haya?!

Rashidi: Kama tulivyokubaliana huko nyuma, utafiti sahihi wa mambo unapaswa kuwa katika duara zima lililokamilika ambapo mambo yote huangaliwa kwa upana wake.

Maiko: Vizuri, lakini ni nini athari ya hilo katika maudhui yetu?

Rashidi: Athari yake ni kuwa tunapoyatafiti mas-ala haya inatupasa tuangalie maslahi ya mwanamke kwa kuzingatia jinsia yake, yaani wanawake wote, na kuangalia maslahi ya jamii kwa ujumla wake, bali maslahi ya mwanamume vile vile na kuzingatia tofauti iliyopo kati ya mwanamke na mwanamme.

Maiko (Akimkata): Hapa haswa ndipo tulipofika katika chanzo chenyewe cha dhulma kilichoko kwa wanawake huko kwenu, tofauti kati ya mwanamme na mwanamke!....Hakika tofauti hizi mnazolingania ni thamani ilizojiwekea mfumo dume wa jamii za Mashariki, lengo lake ni kumtawala mwanamke na kustarehe nae….ni tofauti gani hizi?! Kwa nini basi mwanamke nae asipewe haki ya kuolewa na mume zaidi ya mmoja?! Je, hiyo sio dalili yenye kuthibitisha matamanio ya mwanamke katika jamii hii?!

Rashidi: Pole pole rafiki yangu, umenitupia mabomu ya maswali ambayo hatuwezi kuyakabili mara moja…tutayajadili yote hayo, hata hivyo acha tutegue mabomu haya, na tuanze na lile lililokuathiri. Je, huamini kuwa kuna tofauti kati ya mwanamme na mwanamke?

Maiko: Tofauti gani?

Rashidi: Kwanza kabisa….ni tofauti za kibailojia, kati ya maumbile ya kiwiliwili ya mwanamke na ya mwanamme!

Maiko: Bila ya shaka yoyote kuna tofauti za kibailojia, lakini kuna uhusiano gani wa tofauti hizi na maudhui yetu?!

Rashidi: Sitozungumza nawe kwa mtazamo wa kidini ambao ninaamini kuwa ni muhimu kwa mtu aliyejisalimisha nao na kuridhika nao, lakini nitazungumza nawe kwa mtazamo wa akili na elimu ulioutangaza mwanzo kuwa ndio unaoamini….nisikilize bwana:

Tafiti nyingi zilizofanyika hivi karibuni zimethibitisha kuwa kemia ya upendo kwa mwanamme inatofautiana na mwanamke; kiasi kilichopelekea taasisi nyingi za kielimu kufanya utafiti kwa kina kuhusu hisia za mapenzi kati ya mwanamme na mwanamke, wanazuoni wakapata matokeo ya kushangaza kuwa jeni za mwanamme humsukuma katika mahusiano ya wanawake wengi, wakati ambapo jeni za kike zinamsukuma mwanamke katika utulivu katika uhusiano wa mtu mmoja, vivyo hivyo elimu leo hii imethibitisha kuwa mwanamme anaweza kumpenda zaidi ya mwanamke mmoja, bila ya mahusiano hayo kuathiri mapenzi kwa wengine.

Kadhalika mtandao wa CNN umemnasibisha Profesa wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Utah State huko Marekani, Liza Diamond, kuwa kuna dalili za kibaolojia kuwa mahusiano ya mwanamme kwa wanawake wengi kijinsia ni jambo linalotokana na maumbile yao ya kiwiliwili.

Kundi la watafiti katika Chuo Kikuu cha Oxford huko Uingereza katika utafiti wao wa mwaka 2007 umethibitisha kuwa wanawake wako kinyume na wanaume; muda wao mwingi huelekezwa kwenye viwiliwili vyao na kwa watoto wao kwa sababu ya Homoni Oxytocin ambayo inazidisha wao kuwa karibu zaidi katika uhusiano wao na watoto wao.

Utafiti mwingine mpya umeashiria kuwa sehemu maalumu katika akili ya mwanamme ni kubwa zaidi ya mara mbili ya mwanamke, na huenda tofauti kubwa kati ya ubongo wa mwanamme na mwanamke ni kuwa wanaume wana sehemu maalumu inayoshughulika na hamu ya kijinsia kubwa zaidi mara mbili na nusu kulinganisha na ile ya mwanamke.

Je, hudhani kuwa tofauti hizi hazina athari?!

Maiko: Ikiwa taarifa hizi ni za kweli, basi bila ya shaka zitakuwa na athari.

Rashidi: Hivyo basi unachokielezea kuwa ni matamanio ya kinyama ya mwanamme, na mahusiano yake na wanawake wengi ni jambo lisilokuwa na uhusiano pekee na Uislamu na jamii ya Mashariki…..Nami ninauliza swali naomba unijibu kwa ukweli na uwazi kama ulivyoahidi. Ni marafiki zako wangapi ambao hawana mahusiano na wanawake wengi? Sikusudii mahusiano yako peke yako.

Maiko: Hata kama unakusudia mahusiano yangu peke yangu, hili ni jambo linalojulikana huku kwetu na katika jamii zetu… lakini sio ndoa moja kwa moja.

Rashidi: Sawa, kinacholengwa katika jamii zetu kipo katika jamii yenu vile vile, pamoja na tofauti kubwa ambayo nitakutajia.

Hata hivyo nitakuzidishia juu ya hilo; Uislamu sio uliovumbua mfumo wa wake wengi, uhusiano na mfumo huu ulikuwepo tokea staarabu nyingi huko nyuma, na hakukuwa na kiwango maalum cha idadi kwa mwanamme, kama ambavyo ilikuwa ni ruhusa katika dini zote za mbinguni hali hii iliendelea kuruhusiwa katika dini ya Uyahudi hadi karne ya kati pindi ilipotangazwa na mwanazuoni Giorshom Eshkanaz (960-1040) uharamu wa zaidi ya mke mmoja, ama kanisa halikukataza hilo isipokuwa katika karne ya kumi na saba, lakini katika baadhi ya makanisa ni jambo lililoruhusiwa hadi sasa, kama ilivyo kwa madhehebu ya Mormon.

Maiko: Kama ni hivyo, hayo yalikuwa ni mambo ya zamani, ama sasa hivi mwanadamu ameendelea na kustaarabika zaidi.

Rashidi: Maendeleo na ustaarabu hauwi katika kupambana na maumbile ya mwanadamu na kutoitikia haja zao na kuvuka juu ya maslahi yao, haiingii akilini kusemwa: Kuwa mwanadamu katika zama za kale alikuwa akila nyama za wanyama (ng’ombe, mbuzi na kondoo) na kuvaa sufi za kondoo na ngozi ya mbuzi, na kukabaki kuwa kula nyama na kuvaa sufi au ngozi ni matendo ya kukosa maendeleo na ya kinyama….hata hivyo inaweza kusemwa: Kwa hakika maendeleo ya mwanadamu yanaweza kuyaendeleza matendo haya zaidi ili kuitikia zaidi haja zake na kudhamini zaidi maslahi yake na hili haswa ndilo lliloletwa na Uislamu.

Maiko: Kivipi?

Rashidi: Wewe unasema kuwa mahusiano ya mapenzi na kijinsia mengi yako nje ya duara la ndoa lililoenea katika jamii zenu za Magharibi, nayo ni dhulma yenyewe kwa mwanamke na ufisadi kwa jamii yenyewe, ni mahusiano ambayo hayapelekei katika utulivu wa nafsi wala hayathamini haki mbali mbali, wala kusimamisha jamii iliyosalimika, na ikiwa suala hili la wake wengi lipo katika staarabu za kale bila ya mipaka, Uislamu umekuja ukamfanyia uadilifu mwanamke pindi ulipoitikia haja zake na kumfanya mshirika wa kisheria katika ndoa, na ukaiwekea udhibiti na vifungo vya ndoa hii ili kudhamini kiasi kikubwa cha mafanikio ya taasisi hii ya familia.

Uislamu unachunga maslahi ya kila mwanamke, na umeweka mizani sawa sawa kati ya matamanio ya mwanamme na kuyaacha huru, na yote hayo kwa misingi ya taasisi ya kijamii ya kwanza ambayo imevunjika kwa kiasi kikubwa katika nchi zenu… familia.

Maiko: Lakini sensa ya kisomi inasema kuwa kiasi cha uzazi wa watoto wa kike ni sawa na wa kiume takriban, na ukitekeleza misingi ya wake wengi basi watabakia baadhi ya wanaume bila ya wake, na hili vile vile litakuwa ni jambo la hatari.

Rashidi: Ikiwa takwimu za kisomi zinathibitisha hilo, na huthibitisha kuwa wastani wa umri wa wanawake ni mkubwa kuliko wastani wa umri wa wanaume, katika ulimwengu wa Magharibi huishi wanaume kwa wastani wa umri wa miaka saba kwa upungufu wa wanawake, na tofauti hii inazidi kila mara kwa karne iliyopita, kwa mfano: Huko Ujerumani hufikia umri wa mwanamke miaka themanini, ama mwanamme hufikia wastani wa umri wa miaka sabini, wakati ambapo tofauti hii ilikuwa ni ya miaka miwili tu katika mwaka 1900.

Mwanazuoni Daniel Kroger kutoka chuo kikuu cha Michigan huko Marekani anasema: Katika nchi nyingi ulimwenguni mwanamme anaishi katika umri pungufu kwa mwanamke na anaongeza ‘Kroger’ moja katika sababu ya tofauti hii, ni tofauti ya homoni kati ya mwanamke na mwanamme; kwani homoni za mwanamme hurutubisha jeni ambazo husababisha maradhi ya moyo na mzunguko wa damu.

Naongezea hilo: Uwezekano wa vifo vya wanaume vinavyotokana na vita katika nchi zenye migogoro ni mkubwa, pia mara kwa mara wanaume hufariki kutokana na kazi ngumu na za hatari wazifanyazo, mbali na matukio mengine mbali mbali ambayo wahanga wake wengi ni wanaume.

Yaani, idadi ya wanawake katika jamii mbali mbali inazidi idadi ya wanaume, na hii ni hali halisi inayoshuhudiwa na takwimu za nchi nyingi ulimwenguni, kuongezea tatizo la wanaoachwa wajane.

Je, wanawake hawa ambao hawakuolewa wataachwa wakiendelea kupata matatizo haya ya kinafsi na ya kijamii na ya kitabia, au wasukumwe kuomba haki zao na kushibisha matamanio yao ya kimaumbile kwa kificho, jambo ambalo linawaathiri wao na kuiathiri jamii kwa ujumla, au waendelee kufuata mfumo wa kijamii ambao utaitikia haja za jamii katika mipaka ya udhibiti wa kisheria ambayo huchunga uwezo wa mazingira ya mwanadamu, na kudhamini hilo litimie kwa njia ya uadilifu, bila ya kuwepo dhuluma au msukumo kutoka upande wowote ule?.

Hilo lilijibiwa na mwanazuoni wa mambo ya jamii Mfaransa Dr. Gustav Lubon, aliposema: “Ama kwa hakika mfumo wa wake wengi wa Mashariki (akikusudia Uislamu) ni mfumo mzuri unaonyanyua kiwango cha tabia za mataifa, na familia huzidi kushikamana na humpa mwanamke heshima na furaha ambayo haipatikani Ulaya.”

Tafadhali nipatie glasi ya juisi ya ndimu na kikombe cha chai.