Hakika za Kistaarabu

Hakika za Kistaarabu:

Hakika za Kistaarabu

Rajev: Alianza mazungumzo baada ya kukutana na rafiki zake kwa lengo la kuwaonesha picha alizozichukua hivi karibuni, akiweka wazi:

Picha hii nimepiga nikiwa Uturuki kwa mwaliko kutoka kwa mmoja wa rafiki zangu, nilishangazwa na niliyoyaona kutokana na athari za kistarabu katika nchi ile kongwe, rafiki yangu alinishtukiza kwa maarifa ya ustaarabu wa Kiislamu katika nchi yake, na kunifanya nirejee nilichokiona katika nchi yangu ya India.

Maiko: lakini mimi nina maarifa mengine kuhusu ustaarabu wa Kiislamu ambao unawakilisha upande mwingine wa ustaarabu wa Kiislamu.

Rashidi: Nadhani ni vizuri kwanza tuainishe mtazamo wa ustaarabu, kisha baada ya hapo tuangalie ustaarabu wa Kiislamu.

Maiko: Nadhani sisi tunaafikiana na mtazamo huu.

Rashidi: Hakuna neno, tuuainishe kwanza, na ikiwa kweli tumeafikiana basi tutaondokea hapo.

Maiko: Ustaarabu ni matokeo ya nishati ya mwanadamu iwe ni ya kimaada au ya kifikra ambayo jamii husika inaielezea kutokana na ubunifu wake na maendeleo yake kwa wakati maalumu.

Rajev: Nitaongezea maelezo machache katika maneno ya Maiko, nayo ni kuwa; ustaarabu ni mfumo wa kijamii ambao humsaidia mwanadamu katika nyongeza ya uzalishaji wake wa kitamaduni na kielimu na ustaarabu una vipengele vinne: Vyanzo vya kiuchumi, mfumo wa kisiasa, desturi za kimaadili na ufuatiliaji wa sayansi na fani nyinginezo.

Ustaarabu umejikita juu ya utafiti wa kielimu, na katika taswira ya fani kwa daraja la kwanza, upande wa kielimu unahusika na uvumbuzi wa kiteknolojia na elimu jamii, ama upande wa taswira ya kifani unahusika na fani mbali mbali za ujenzi, uchongaji na baadhi ya fani nyinginezo ambazo humpelekea mwanadamu katika maendeleo, hivyo basi fani na elimu ni vipengele viwili vinavyokamilisha (vinavyoongoza) ustaarabu wowote ule.

Rashidi: Ningependa kwanza kuchangia maneno ya rafiki yangu Maiko; tukitegemea ufahamu huu ulioutaja basi hapana budi kuangalia ustaarabu kuwa ni nishati ya mwanadamu katika daraja la kwanza, na matokeo ya mtazamo huu ni kuwa, hapana budi kuangalia katika maana zingine zote za mwanadamu bila kughafilika na chochote, vinginevyo ustaarabu huo utakuwa na mapungufu, au usipewe wasifu wa ustaarabu…hili ni moja.

Pili: Mandhari ya ustaarabu yanaweza kutofuatia baina ya jamii moja ya mwanadamu na nyingine, kwa wasifu wake kuwa yanaakisi msingi ambao juu yake jamii hii imeasisiwa na kuanzia hapo: inakuwa kuangalia usahihi wa maadili haya au makosa yake na kuafikiana kwake na utu wa mwanadamu na kiasi cha kulandana na mazingira yake anayoishi mwanadamu, ikiwa ni kipimo cha uzuri wa ustaarabu wowote, au uharibifu wake ….na hili ndilo ambalo litadhihiri kwetu masafa marefu baina ya staarabu mbali mbali na maafa anayoishi mwanadamu katika kivuli cha ustaarabu huu wa kileo wa Kimagharibi.

Maiko: Namuona bwana Rashidi akikimbia kujadili upande wa kiza katika ustaarabu wa Kiislamu, ambao tulikuwa tuuzungumzie.

Rajev: Huenda jambo hili likatutaka tumuombe Rashidi kututajia sifa za ustaarabu wa Kiislamu, na tofauti yake na staarabu zingine.

Rashidi: Vizuri, Ustaarabu wa Kiislamu umesimama katika taswira ya Uislamu kwa mwanadamu, ulimwengu na maisha, nitakutajieni sifa zake muhimu, lakini naomba niongezee vile vile mkabala na sifa hizi na sifa pambanuzi za ustaarabu wa Kimagharibi wa leo.

Sifa za msingi za ustaarabu wa Kiislamu ni:

Mwanadamu katika taswira ya Kiislamu: ambayo juu yake unasimamia ustaarabu huu, ni kiumbe kinacholelewa na Mwenyezi Mungu, amefanywa kuwa kiongozi katika ardhi hii, ameaminiwa juu ya mfumo wa Mwenyezi Mungu aliyetukuka, yu huru mwenye kuhiari, na ni juu yake yafuatayo: Kuwa mwenye kuamuriwa kufanya matendo mema yaliyojengewa juu ya mfumo huu, ni mwenye kuulizwa juu ya matendo ya utashi wake katika maisha haya duniani na huko akhera.

Ama mtazamo wa kiistaarabu wa Kimagharibi leo hii kwa mwanadamu ni kuwa yeye ni bwana wa ulimwengu huu, ni mtu huru hakuna kinachomzuia isipokuwa kile anachokitaka mwenyewe chini ya ubwana wake hapa ulimwenguni, mambo yake ya msingi huzunguka kwenye matamanio na ladha zake, nao ni umuhimu ambao anashirikiana ndani yake na wanyama wengine pamoja nae. Ustaarabu wa kimagharibi unamwona mwanadamu kuwa ni kiumbe asiye na malengo wala hesabu isipokuwa kwa kile alichokiainisha mwenyewe, kama ambayo malengo yake mwanadamu ya kidunia ni duni.

Ulimwengu katika taswira ya Uislamu ni kiumbe aliyelelewa na Mungu kama alivyo mwanadamu isipokuwa amedhalilishwa kumuhudumia mwanadamu, hivyo basi mwanadamu anafurahia kufuata mfumo wa Mwenyezi Mungu pamoja na ulimwengu huu na anakamilika pamoja nao na anahisi amani pamoja nao.

Ama mtazamo wa kimagharibi kuhusu ulimwengu ni kuwa huzunguka baina ya kuwa kuna mgongano kati ya mwanadamu na ulimwengu, na sio furaha, kwa hivyo basi, vita ni vikali kati yao.

Maisha katika taswira ya Kiislamu ni miliki ya muumba wa mwanadamu na ulimwengu, nao ni kituo katika safari ndefu kuliko tuonavyo; kuna maisha ya dunia ambayo huisha kwa vifo vya watu, na kuna maisha yajayo husubiri baada ya vifo vyao. Mwanadamu ameamriwa kuimarisha ardhi katika anayoridhia Allah Mtukuka, Muumba wa wanadamu na ulimwengu. Na maisha ni shamba la akhera, na kuna hesabu na malipo katika matendo yake ya kila siku duniani.

Ama ustaarabu wa Magharibi unayaona maisha kuwa ni ya kidunia tu, hauamini akhera wala hesabu na malipo, hivyo basi: Nafasi aliyonayo mwanadamu ni ya maisha haya ya dunia pekee.

Yote hayo tunapata matokeo kuwa ni muhali ustaarabu wa Kimagharibi kukutana na ustaarabu wa Kiislamu katika taswira, ni staarabu mbili kinzani.

Maiko: Bwana Rashidi niruhusu nikuambie nilichokifahamu kutokana na maneno yako:

Kwanza: Umesahau kitu muhimu katika nukta za ustaarabu wa Kimagharibi nazo ni dini za Ukristo na Uyahudi vile vile, kwa mfano wewe unasema kuwa mtazamo wa ustaarabu wa Kimagharibi hauamini akhera, hesabu wala malipo, na hili si sahihi, dini hizo mbili zinaamini akhera pamoja na kuwa vipengele vya imani hii inatofautiana kutoka dini moja kwenda dini nyingine.

Pili: Maneno yako hayo yanafaa kuwa ndio msingi uliosimamia ustaarabu wa Kiislamu ukiulinganisha na wa Kimagharibi, lakini sifa ambazo zinasimamia ustaarabu wa kiislamu hukuzizungumzia kama alivyokuomba rafiki yetu Rajev.

Rashidi: Rai yako ya mwanzo au uchunguzi wako wa mwanzo ninatofuatiana nawe; kuna tofauti kati ya misingi inayosimamia ustaarabu na yaliyomo katika jamii ile ambayo ustaarabu ule umeanzia, hapana shaka kuwa kuna taathira ya Ukristo na Uyahudi katika ustaarabu wa Kimagharibi, lakini hauwezi kudai kuwa ustaarabu wa Kimagharibi umesimama katika misingi ya dini hizi mbili, bali tunaweza kuthibitisha kinyume chake kabisa, nayo ni kuwa umesimama katika kupinga dini kwa ujumla na utawala mahususi wa Kanisa, yaani kwa matumizi ya akili tupu na mambo matupu ya kidunia tu, na hilo ndilo ambalo lipo kwa uwazi katika usekula, ambalo maana yake ni kutenganisha dini na maisha, nadhani mnakubaliana nami katika hilo.

Ama ugunduzi wako wa pili naafikiana nawe kabisa, lakini naongezea kuwa misingi hii ambayo inafupisha sifa za ustaarabu wa Kiislamu ni hii ifuatayo:

Ama (sanaa nzito) katika ustaarabu wa Kiislamu ni kumjenga mwanadamu kwenye: Kuchunga yaliyomo ndani yake, kushibisha utu wake, kufanikisha uhusiano wake na ulimwengu wake, na kufikia lengo la kuumbwa kwake.

Kufungamanisha na kuchanganya baina ya dini na dunia kwa upande mmoja na kati ya dini, akili na elimu kwa upande mwingine, na ukuzi wa mfumo na nishati ya ustaarabu juu ya msingi huu.

Ulinganisho na kuoanisha kati ya vyanzo ya maarifa ya ubinadamu, kwa hiyo; kweli yote, yenye kuhusiana na maada na zaidi ya hapo, ziko katika matumizi ya mwanadamu; anaweza kuyafikia kwa njia zake nyingi zilizopangwa kwa hatua, zenye kutegemeana, kwa hiyo vyenye kuweza kupatikana kisilika nyuma yake vinapatikana kihisia, kisha kufahamika kiakili na hizo za kiakili hupelekea kwenye vitangulizi vya kuweza kupokea mambo ya ghaibu kwa njia ya WAHYI na kujisalimisha kwake.

Kufunguka kwa staarabu na tamaduni zingine, yaani ustaarabu wa Kiislamu ni wenye kuathiri na kuathiriwa, ikiwa na maana ya kupokea na kutumia yanayowafikiana na ustaarabu wa Kiislamu kutoka katika yaliyozalishwa na umma zingine, na kufungua milango ili umma zingine ziweze kufaidika na uzalishaji na matukufu ya ustaarabu wa Kiislamu.

Rajev: Samahani bwana Rashidi, Maiko amesema ana maelezo kuhusu eneo ambalo ustaarabu wa Kiislamu umeboronga, naomba umpe fursa azungumzie ili picha yetu ikamilike.

Maiko: Jambo muhimu hapa ni kuwa dola iliyooanisha ustaarabu huu imesimama kwa ncha ya upanga, na imehusishwa na matumizi ya nguvu na ukatili.

Rashidi: Rafiki yangu upanga hausimamishi ustaarabu, kwani moja katika shuruti muhimu ya ustaarabu ni utulivu na amani, nayo ni kinyume na hali ya vita, kama ambavyo ushindi wa kiaskari hauna maana kuwa ushindi katika uwanja wa fikra, utamaduni na ustaarabu ni juu yako kutafakari historia ya watatari, wamangoli na umma zingine zilizo kuwa na nguvu kubwa ya kiaskari lakini kwa nguvu zao hizo hawakutengeneza ustaarabu.

Lakini ikiwa unakusudia madai ya Uislamu kuenea kwa jihadi, mimi naashiria kwamba Uislamu ulienea na kusimamisha ustaarabu eneo kubwa ulimwenguni ambalo halijafikiwa na jeshi la Kiislamu, na maudhui haya yana fafanuzi nyingi, lakini nitakupelekea katika ushahidi na uthibitisho wa Wanafikra wengi wa Kimagharibi, katika hili, anasema mwandishi wa Kimarekani T. Lothrop Stoddard katika kitabu The New World of Islam “Ulimwengu mpya wa Kiislamu” Waarabu kamwe hawakuwa ummah uliopenda kumwaga damu na kupenda kunyang’anya na kuangamiza, bali walikuwa, kinyume na hayo, umma uliozawadiwa tabia njema, wakipenda kusoma, wenye kutumia vizuri neema, neema zile zilizomaliza staarabu zilizopita, pamoja na kuenea kuoana baina ya washindi na wenye kushindwa na kubadilishana fikra, maingiliano haya yalizaa ustaarabu mpya: ustaarabu wa Kiarabu.”

Anasema Luteni wa jeshi la Kifaransa Conte Henry De Castry; “Sisi tunaamini kuwa kuangalia dini hii katika karne hii sasa hakubakisha athari yoyote kwa walicho dai kuwa imeenea kwa ncha ya upanga, lau dini ya Muhammad ingeenea kwa matumizi ya nguvu na kulazimisha basi isingekoma kuendelea kwake baada tu ya kuisha kombozi za Waislamu, wakati ambapo sisi tunaona kuwa Qur’an inakunjua mbawa zake kwenye sehemu zote zilizokaliwa.”

Sipati neno lenye kuweza kuelezea athari za ustaarabu wa Kiislamu katika historia ya mwanadamu yenye ukweli kuliko maneno ya mwanahistoria wa Kifaransa Gustav Lubon:

“Hatuoni katika historia Umma wenye athari iliyo wazi kama Waarabu; Umma zingine zote zilizokuwa na uhusiano na Waarabu walichukua ustaarabu wao hata kama ulikuwa ni muda mdogo tu….”

Mwishowe: Ni juu yenu kuangalia maisha yanaonekana vipi yakitishiwa kuwaangamiza wanadamu kwa njia ya kuangamiza sifa zake za utu wa mwanadamu, katika kivuli cha ustaarabu uliopo hivi sasa, jambo ambalo kusimama kwa jamii ya Kiislamu ni la lazima kwa kulinda utu wa mwanadamu na ni hatima ya maumbile yake.