Haki za Mwanadamu Katika Uislamu

Haki za Mwanadamu Katika Uislamu

Haki za Mwanadamu Katika Uislamu

Rashidi: Rashidi alipofungua laptop yake na kuingia katika chumba cha mazungumzo alipata barua kutoka kwa Maiko ikisema: “Jitayarishe kwa kikao kijacho kuna masuala muhimu tuyajadili: Muamala na watu wengine, uzimaji wa mfadhaiko, uhuru wa fikra…kwa heri.”

Rashidi: Aliwakuta rafiki zake chumbani, aliwasalimu kisha akaanza kuzungumza:

Masuala yanayohusiana na haki za binadamu ni mengi wala hayaishi: katika uliyoyataja peke yake rafiki yangu Maiko–na hili linanipelekea kuweka mipaka ya jumla ambayo kwayo tunaweza kufahamu masuala haya, vyovyote itakavyotofautiana au kuwa mbali.

Maiko: Si vibaya kupiga baadhi ya mifano; kama yale niliyokutajia katika barua yangu kwako; ili mazungumzo yetu yawe ya vitendo zaidi ambayo yanaweza kutekelezeka.

Rashidi: Sawa kabisa, hamna neno.

Rajev: Umetutajia katika kikao chetu kilichopita kanuni ambayo tunaweza kuanza nayo, nayo ni kuwa ikiwa kweli tutataka kurejea haki hizi na uhuru basi na tuchunguze maadili ambayo yamesimamishwa juu yake na sio utekelezaji na matendo ya wafuasi wake.

Rashidi: Sahihi….ufahamu wa maadili ya ’uhuru’ haki za binadamu zimepakwa uzoefu (background) na mawazo na fikra ambazo haki hizi zimetolewa, na kuwa chini ya mfumo wa kimaadii wa jumla wa kijamii ambao umekuwa kutokana nayo..na hapa namuuliza rafiki yangu Maiko Je, anaweza kutuwekea wazi uzoefu wa kifikra na mfumo wa kimaadili wa Ki-Magharibi ambao haki za kibinadamu hizi zimesimama juu yake?

Maiko: Tunaweza kusema: Wasifu na mipaka ya kifikra na kimaadili ambazo uhuru na haki za kibinadamu katika mangaribi zinatokana na;

1- Akili, ambayo ndio marejeo ya haki hizi na uhuru huu, hata kama akili hii itachukuwa baadhi ya maadili ya kidini–(kama vile walivyoathiriwa Waliberali (wenye kupenda mabadiliko) na Waprotestant) lakini akili ndio inayobaki kuwa hakimu wa maadili haya kwa kukubali au kukataa.

2- Usekula (kutenganisha dini na maisha na dola); huu ni mfumo ambao ndani yake kunapangika haki hizi na uhuru.

3- ‘Uhuru’ na ’Usawa’; ndio maadili ya juu kabisa ya jamii ambayo maadili mengine yoyote ya jamii yapo chini yake, nayo ni ‘tuli’ na ‘matukufu’ambayo hayawezi kuguswa.

4- Hadhi ya mtu na maslahi yake kuwa juu, pamoja na kutopuuza nafasi ya jamii na maslahi yake, yanayopelekea furaha na kuyapendezesha maisha ya mtu.

Rashidi: Maelezo mazuri kabisa, nakushukuru kwa hilo; kama ni hivyo: Ni wazi kuwa Rejea za Magharibi- (baada ya kutengana na Kanisa katika nyanja za maisha) ilielekea kwenye akili achilia mbali hisia za kimajaribio, na kutokana na rejea hizi kumechimbuka haki na uhuru, na ni wazi kuwa mfumo ambao ulianzisha haki hizi na uhuru huu ni Usekula.

Tunaweza kusema vile vile: Kuwa ‘uhuru’ na ‘usawa’ umekamata kileleni katika rejea hizi za Magharibi: Hivyo basi kufanikisha maadili haya (kulingana na mtazamo uliotulia wa Magharibi) yana kipaumbele halisi ambayo yanafaa kuwa chini yake, au kujifunga nayo, au unapangika juu yake maadili mengineyo ya jamii, kutokea hapa: ‘Uhuru’ na ‘usawa’ umekuwa ndio tuli na matukufu yaliyo kileleni kabisa ambayo hayawezi kuguswa kabisa, ambayo yanawezekana (vile vile) kutoa mhanga maadili mengine na haki zingine kwa ajili ya kuzihifadhi.

Na hii ndio tofauti ya msingi na ule uzoefu wa Uislamu na mfumo wake ambao umebeba maneno au istilahi kama hizo.

Rajev: Ili tuweze kulinganisha, tuwekee mipaka ya kifikra na maadili ambayo anga yake istilahi hizi zinaogelea (Haki za binadamu) katika Uislamu.

Rashidi: Katika Uislamu na (Jamii ya Kiislamu) kuna mfumo tofauti kabisa.

Kwanza: mkabala na (akili) na (hisia za majaribio) tunakuta katika Uislamu kuwa (wahyi) ni marejeo ya kwanza ya misingi na maadili ambayo huchimbuka kutoka humo ‘tuli’ na ‘matukufu’ yake, pamoja na kutopuuza umuhimu wa marejeo ya maarifa ya akili na hisia katika nyanja zake….

Pili: na mkabala wa (usekula) tunapata katika Uislamu (sheria) na kupangika dunia na dini pamoja nao kuna mifumo ambayo jamii hii inasimama.

Tatu: na mkabala wa ‘Uhuru’ na ’Usawa’ tunakuta katika Uislamu kuwa kuna ‘Uja’ wa Mwenyezi Mungu na ‘uadilifu’ kati ya wanadamu (na uadilifu hauna maana ya usawa kama wanavyofahamu baadhi ya watu). Na zinastawi juu ya kilele cha maadili ya jamii ya Kiislamu, na kuhakiki maadili haya na kutoyachezea ndio kipaumbele ambacho mtu anapaswa akinyenyekee au kujifunga nacho au kupangika maadili mengine ya jamii pamoja nacho pamoja na haki za uhuru ulionao.

Nne: na mkabala na ‘Ubinafsi’ tunapata katika Uislamu kupokezana majukumu kati ya mtu na jamii, na maingiliano baina yao bila ya dhuluma au mmoja kupetuka na kumdhulumu mwingine.

Rajev: Huenda tukaachana na taswira hizi mbili juu ya baadhi ya haki ambazo watu wanatofautiana ili sura hii iwe wazi zaidi.

Maiko: Tunaweza kuainisha maudhui ya uhuru wa kuabudu ili kulinganisha kati ya taswira mbili hizi, yaani ya Uislamu na ya Umagharibi, kulingana na uzoefu wa kimaadili wa kila mfumo, ambao ndani yake kunatoka haki za binadamu za kila mfumo katika mifumo hii miwili.

Rashidi: Uhuru wa kuabudu au (uhuru wa kushika dini) ni eneo pana kivitendo na kuoanisha, na hii ni maudhui yanayorejea kwenye kutofautiana na ufahamu wa chini na mafungamano yake na utukufu wa maadili katika mifumo miwili hii.

(Mathalani) katika nchi za Magharibi ni haki ya kila mtu kufuata dini au kuwa mpagani au kubadilisha dini yake; kwani hilo linaingia katika mipaka ya haki ya ‘Uhuru wa kuabudu’, nayo ni haki ‘binafsi ya mtu mmoja mmoja’ haipasi kumuingilia.

Lakini wakati huo huo tunamuona Muislamu katika nchi za Magharibi, (Kinadharia) kuwa anaweza ‘kuamini na kuabudu’ anachokitaka….isipokuwa hana haki ya kutumia uhuru wake kutekeleza anayoyaamini; yaani haruhusiwi na si haki ya Muislamu kutekeleza dini yake katika maisha yake; kwa mfano hukatazwa kuchinja kisheria (zaidi ya nchi moja amri hiyo ipo), kadhalika anakatazwa kuoa zaidi ya mke mmoja katika baadhi za nchi mwanamke hukatazwa kuvaa Hijab–nguo aliyoamrishwa kuvaa na dini yake, na matendo haya ni sehemu ya dini ya Muislamu….Je,unaweza kufasiri hilo?

Maiko: Kwa sababu matendo hayo yameondoka katika mipaka (mapenzi na dhamira ya mtu), ikiwa imetoka kwenye haki yake katika (uhuru wa kuabudu); na kwa hivyo hilo ni kuvunja sheria na mkataba wa jamii na mfumo ambao umeridhiwa na watu wengi, ambao umehukumu kutenganisha dini na mambo ya maisha.

Lakini kwa wakati huo huo ninakutuliza ya kuwa inaruhusiwa kwa Muislamu huyu kisheria kuishi na wanawake wengine nje ya mipaka ya taasisi ya ndoa, madamu hilo litatimia kwa ridhaa yao na sio katika kitanda cha wanandoa.

Rashidi: Lakini matendo haya yamehalalishwa kisheria kinyume na dini yake ambayo anaamini na kujinasibisha nayo!

Bila shaka ninafahamu kuwa nyie hamuhesabu vifungo hivi kuwa ni kuvunja haki na uhuru, kwa sababu hampati uhusiano kati ya matendo haya na dini, bali mnazingatia kuzuia na kubana himaya ya mapato yenu ya kimaendeleo ambayo yamekuwa ni tuli tukufu zinazodhibitiwa.

Na muradi wa hilo ni taswira ya (Itikadi au dini) imekuja ikiwa imelandana pamoja na mtazamo wa Kimagharibi (Kisekula) wa dini, ambao unajitenga na maisha; hivyo basi dini kulingana na mfumo huu haina uhusiano na utaratibu wa jamii, lakini mapenzi au dhamira anayoihifadhi ndani ya nafsi yake, naye kwa hilo atengane moja kwa moja na matendo ya maisha, kama ulivyotangulia kuelezea.

Rajev: Sasa nimeanza kufahamu mtazamo wa Kiislamu.

Rashidi: Katika taswira ya Kiislamu ‘uhuru wa kuabudu’ umedhaminiwa ‘katika mipaka’ ya kuchunga ‘tuli’ za juu za jamii hii (uja na dunia ni kwa ajili ya Mungu Mtukuka), na kwa hilo: Jamii ya Kiislamu inakubali kumuingiza chini ya mwavuli wake kila mwenye kutangaza kukubali kwake utawala wa Mungu juu yake kwa ujumla, na kutengwa kila mwenye kutangaza uasi na kutoka katika utawala huu, na hapa ndipo jamii ya Kiislamu ilipopanuka kwa kuingiza matangamano na wafuasi wa dini nyingi ndani yake, pale ulipokubali kuishi pamoja na wenye kufuata Uyahudi, Ukristo na kuwaachia uhuru wa kuratibu mambo yao binafsi, wakati ambapo hilo halikutokea kwenye dini zingine za kipagani na hilo ni kwa sababu Uyahudi na Ukristo ni dini mbili zenye asili ya mbinguni na wao wanatangaza kuwa chini ya mwavuli ule wa uja ule kwa ujumla.

Lakini upotofu uliojitokeza kwa dini zile mbili kulingana na Uislamu (ni mgongano wa ukweli wa na uja wa Allah) ambao unafanya mzunguko ‘uhuru wa kujieleza’ kuwa mdogo zaidi kuliko unafanya mzunguko ‘uhuru wa kujieleza’ kuwa mdogo zaidi kuliko mzunguko wa ‘uhuru wa itikadi’, hivyo basi si halali kwao kulingania dini zao, wala kudhihirisha alama za dini zao (zinazoelezea upotofu wao) nje ya mzunguko wa wafuasi wao; hivyo ‘uhuru wa kuabudu’ kutoka katika mzunguko huu huvunja utaratibu wa jamii na huvunja tuli za msingi na matukufu ya mwanzo katika kilele cha maadili ya kijamii.

Maiko: Na vipi kuhusu Uislamu kuwakataza watu kubadilisha dini?

Rashidi: Hili nalo linahusiana vile vile na nililolitaja; suala la murtadi (aliyeacha Uislamu) linahusiana na taswira kuhusu ‘uhuru wa kuabudu’ kulingana na taswira ya Uislamu; wakati ambapo Uislamu haumuadhibu ambaye hajaingia kabisa, wala haumlazimishi yeyote kuingia ndani ya imani yake: “Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet’ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” (2:265), “Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae….”(18:29), “Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu. ” (109:6) tunaona kuwa wakati huo huo unamkataza na kumuadhibu mwenye kuhama kwenda kwenye dini nyingine.

Tunaweza kufahamu msimamo wa Uislamu kwa murtadi, katika mazingira ambayo kuhama kule huzingatiwa kuwa ni kukosoa maadili ya juu zaidi ya msingi ambayo jamii imesimamishwa juu yake, au kwa lugha nyingine: Hilo huchukuliwa kuukosoa ukweli wa dini hii, au mwanadamu kutokuwa na haja nayo, na hilo halikubaliwi katika jamiii ambayo inategemea sheria yake na marejeo yake katika kuamini ukweli wa dini hii na haja ya mwanadamu kwa dini hii.

Mfano huu ni kutokea mtu katika nchi za Magharibi akataka kubomoa tuli za uhuru na matukufu na kuyaangusha, kidogo kidogo majibu yake atayapata mara moja kwa wafuasi wa uhuru huu, nao ni kunyanyua kauli mbiu: Hakuna uhuru kwa uadui wa uhuru; na hiyo ni kwa sababu matakwa haya yatatumia uhuru kuwa uhuru, yaani kuangamiza maadili ya juu na ya msingi ambayo jamii hiyo imesimamishwa.

Maiko: Nakushukuru Rashidi kwa ufafanuzi huu...nimefurahishwa na mijadala hii, ninatamani iendelee.