Haja Yetu ya Imani

Haja Yetu ya Imani

Haja Yetu ya Imani

Marafiki wale walikutana kwa mujibu wa ahadi yao katika hoteli ya nyumba ya vijana, baada ya kuangalia ‘menyu’ Maiko na Rashidi wakaorodhesha oda yao, wakati ambapo Rajev alikuwa akiangalia menyu kwa umakini zaidi na akasema:

Hoteli nyingi hazijali kuweka vyakula vya mboga mboga, hata hivyo ninaweza kuagiza chakula chenye kunifaa.

Maiko: Kwa hiyo wewe ni miongoni mwa wala mboga mboga?

Rajev: Ndio inafikia asilimia arubaini (40%) ya wala mboga mboga nchini India.

Rashidi: Je, hilo ni kwa sababu ya dini au afya?

Rajev: Ukweli, katika dini ya Uhindu ambayo nilikuwa nikiamini, ulaji wa nyama ya ng’ombe ni haramu kabisa, India ulaji mboga mboga ni maarufu mno kwa wenye kufuata dini ya Uhindu, pamoja na kupungua idadi yao kwa sasa kutokana na ugumu wa kufuata mfumo huu na ukatili wake, ama mimi binafsi napendelea zaidi vyakula vya mboga mboga kwa ajili ya afya na mazingira..

Rashidi: (Akimuita mhudumu): kwa hisani oda yetu hii hapa.

Maiko: Lakini wewe Rajev umeacha dini yako kuelekea dini ipi?

Rajev: Si popote, masomo yangu nchini Ujerumani yamenipa fursa ya kusoma sana na kunifanya kuwa huru na kuangalia Uhindu kwa jicho la kukosoa na mashaka mengi, na hata hivyo sijakinaishwa na Ukristo, kwa ajili hiyo mimi niko karibu zaidi na upagani.

Maiko: Mimi nakukaribia wewe kwenye shaka hii, hata hivyo ninaamini kuwa mwanadamu ana haja ya kuwa na uhusiano na Mungu baadhi ya nyakati, lakini uhusiano huu usiwe kupetuka mpaka na kumtawala mwanadamu.

Rashidi: Mimi naamini kuwa maneno haya yanahitaji mjadala na umakini.

Maiko: Mazungumzo gani unayokusudia?

Rashidi: Hii fikra ya kumkana Mungu, na nafasi ya dini au Mungu katika maisha ya mwanadamu.

Rajev: Ninaamini ugunduzi wa mwanadamu katika elimu umemfungulia siri nyingi, umemfanya kutokuwa na haja ya tafsiri iliyojificha, tafsiri za kiroho, na naamini kuwa ulimwengu unaongozwa na kuhukumiwa na kanuni za kielimu (kisayansi) ambazo inaziongoza. Tunaweza kusema: Ulimwengu ni chombo cha kimakenika (kinachofanya kazi) ipo chini ya kanuni madhubuti na kila kinachotokea kina sababu ambayo hupelekea katika matokeo ya lazima yaliopangwa, na madamu kanuni hizi za kimakenika zinaendesha ulimwengu kulingana na sheria zake, basi hakuna haja ya kuwepo (fikra) ya Mungu ambaye atatawala ulimwengu.

Rashidi: Elimu (sayansi) ni chombo kizuri cha kufasiri yanayotuzunguka, lakini suala la (msingi) sio hili, hatuwezi kuzungumzia masuala makubwa kama haya, bali ni masuala makubwa yaliyowashughulisha wanadamu tokea mwanzo wa historia, huondoshwa kimoja hata ikiwa kuondoshwa huku hutuvutia au katika tunachokiamini, kuna mapana mengi katika maudhui, miongoni mwayo ni:

Je, elimu ina tafsiri ya yote yenye kutuzunguka? Bila shaka jibu ni hapana….Elimu haiwezi kufanya hilo, tukichukulia elimu ya nyota (astronomy) kwa mfano, tunaona nadharia za elimu hii kuwa yale yaliyovumbuliwa na elimu hii katika ulimwengu hadi leo hii huwakilisha asilimia tano tu (5%) na baki ya mambo mengi yako kwenye kiza, hatujui chochote kuhusiana nayo, na hii ni kulingana na uwezo wake wa sasa na walichokifikia, vinginevyo ingeweza kuwa yale wasioyafahamu ni makubwa zaidi.

Ikiwa hiyo ndio hali halisi ya ulimwengu wa (mambo yaliyo wazi) na kugusika, hali ikoje katika ulimwengu uliojificha?!

Hilo linatufanya tujiulize: Je, elimu ina mipaka inayoishia mbele yake? Yatupasa tufahamu kuwa uwezo wa elimu vyovyote itakavyokuwa ina mipaka yake katika kufasiri kila kitu; Ulimwengu ulojificha sio katika yanayojulikana kwa njia za elimu, kwa sababu elimu haiwezi kufasiri baadhi ya matukio ya Kifizikia ambayo tunaishi nayo sasa, vipi kwa elimu ya ulimwengu uliojificha ambao hauwezi kuwa chini ya maabara ya majaribio na vyombo vyenye hisia vya kudiriki?!

Tukiongezea hapo; Elimu yetu ya jambo fulani haipasi kutupeleka kwenye kumkana aliyeiumba wala kupunguza uzuri wa mgunduzi wake, kwa hiyo ikiwa mtu mshamba alipoona televisheni alishtuka na kushangaa, kisha baada ya hapo akajua nadharia na njia inayofanya televisheni kufanya kazi, hilo halitomfanya kudharau thamani ya kazi hii au kumkana aliyeitengeneza, vivyo hivyo mfano wake ikiwa tutaweza kupiga hatua katika elimu ya biolojia katika kufichua seli na kuvumbua DNA; na kuonekana maajabu yake, Je, ina maana kuwa katika hilo hakuna miujiza? Au kuwa maumbile yake hayana muumba wake? Kinyume kabisa, kwa hakika maajabu yote haya ambayo mwanadamu amesimama nyuma akiwa ameshindwa kufanya mfano wake kuanzisha kisichokuwepo au kutafsiri jinsi ya utendaji wake na hilo ni upeo mdogo linampelekea kwenye imani kuwa nyuma ya maumbile haya kuna muumba.

Chukua mfano mwingine: Anasema Profesor Syell Bays Hamkan nae ni mtaalamu wa Kimarekani katika biolojia:

“Kwa hakika ni tendo la ajabu katika kubadilika chakula na kuwa sehemu ya kiwiliwili kabla ya kunasibishwa na Mwenyezi Mungu, leo hii kwa uthibitisho mpya, limekuwa ni tendo la kikemia, Je, hili limebatilisha uwepo wa Mungu? Ni nguvu gani iliyozifanya elementi hizi kuwa chini ya elementi za kemikali zenye faida? Chakula baada ya kuingia kwenye kiwiliwili cha mwanadamu hupitia awamu nyingi katika mfumo wake binafsi, na ni jambo lisilowezekana kufanikisha uwepo wa mfumo huu wa ajabu kwa maafikiano barabara; imekuwa ni lazima baada ya kushuhudia huku kuamini kuwa Mungu anafanya kwa kanuni zake nyingi ambazo ameumba nazo uhai.

Maiko: Lakini nadharia ya Darwin ya Evolution (nadharia ya mageuko) imethibitisha mtazamo huu huu; ulazima wa elimu kuachana na uwepo wa Mungu Muumba, na imethibitisha (vile vile) kuwa viumbe hai vimekulia chini ya kanuni ya uteuzi wa mazingira na ukuzi, na wala sio kuumbwa.

Rashidi: Jambo hili linatupelekea kujiuliza maswali muhimu kulingana na nadharia hii au nyinginezo; Je, tafsiri ya elimu ni kamili katika hali zote? Wengi katika watunduwaji wamesahau kuendelea kwa elimu kuwa katika sifa za elimu ni kulimbikiza na kuleta mapinduzi, nazo hutengeneza au kuumba chombo cha maendeleo ya maarifa na sayansi, ambapo elimu inalimbikizwa na ugunduzi hadi kufikia kwenye kiwango ambacho kitaleta sheria mpya halisi katika kurejesha mtazamo katika maarifa ya zamani, ambayo yatabadilisha mtazamo wa mwanadamu kuhusu elimu.

Katika nadharia ya Darwin ambayo kwa vyovyote vile ni tokeo la kielimu, haijafikia kwenye kiwango cha ukweli wa kisayansi wala hata kufikia kiwango cha kuwa ni nadharia, bali ni fikra kuhusu mageuzi na ukuzi, fikra hizi zimegongana na ugunduzi wa elimu mpya ya embryolojia (elimu ya kiini tete) vile vile machimbo ambayo yamethibitisha kuibuka ghafla kwa makundi ya wanyama wakati mfupi ambayo yalijulikana kama zama za cambria (zama za mwanzo za jiolojia) na muda huu kujulikana kwa jina la Mlipuko wa Cambria hii ndiyo ilivyokuwa badala ya kukua mmoja, kuendelea na kukaa na kufuatana na mwingine, kama isemavyo nadhari ya ukuzi na mageuzi.

Rajev: Kama ni hivyo basi, Je, hakuna uwezekano wa kuwa mwanazuoni huyu aliibuka ghafla tu na bila ya kuwepo kwa muumba wake?

Rashidi: Niruhusu nikubainishie maana ya bahati nasibu kupitia matumizi ya misingi ya elimu ya hesabu na kanuni hizo za bahati nasibu; ili uweze kujua ni kiasi gani zinaweza kutokea.

Kama tukijaalia kuwa tuna sanduku kubwa lililojaa herufi za alfabeti, uwezekano “A” kuangukia jirani na “M” ili kutengeneza neno ‘AM’ huenda ikawa ni mkubwa kiasi fulani, ama uwezekano wa herufi hizi kujipanga (zenyewe) zikatengeneza nyimbo au shairi, bila shaka unakuwa finyu sana, iwapo itakuwa sio muhali (lisilowezekana).

Wanazuoni wamehesabu uwezekano wa kukutana atomi nyingi na uwezekano wa kutengeneza amino asidi (Amonium Acid) ambayo hutengeneza protein na nyama na wakakuta kuwa hilo linahitajia miaka bilioni nyingi na kuwepo na mada ambayo haitoshelezi kuwa nao, hii ilikutengeneza sehemu moja tu kwa udogo wake, sasa iweje kwa kutengeneza maumbo ya viumbe hai wote, miongoni mwa mimea na wanyama, sembuse kutengeneza maisha yenyewe na ulimwengu wenyewe… ni jambo ambalo haliingii akilini kuwa hili limetokea kwa bahati mbaya tu.

Hakika matawi yote ya elimu huthibitisha kuwa pana mfumo makini wa ajabu wenye kudhibiti na kuratibu uliotapakaa katika ulimwengu huu, msingi wake ni kanuni na nyendo za kilimwengu ambao haugeuki wala haubadiliki, ambao wanazuoni wanakesha kuufanyia kazi katika kuugundua na (kuujua) kuuzunguka, gunduzi nyingi za kisayansi zimefikia daraja la juu kabisa na umakini mkubwa kutuwezesha kutarajia kupatwa jua na mwezi na mengineyo katika mazingira yaliyo dhahiri kabla ya kutokea kwake kwa mamia ya miaka.

Basi ni nani aliyeweka kanuni hizi na kuwekea kila atom katika atom zilizopo, bali hata katika iliyo chini zaidi ya wizani wa atom kwenye ukuaji wake wa mwanzo?! Ni nani aliyeumba mfumo wote huu na maafikiano yale? Ni nani aliyesanifu akapendezesha usanifu ule na akakadiria na kufanya uzuri makadirio yale?! Je, vyote vimeumbwa bila ya uwepo wa muumba, au watu wenyewe ndio waumbaji? Hivi ndivyo Qur’an kitabu cha Waislamu kinavyosema:

“Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?” (52:35)

Kwa kweli kanuni na mfumo ambao unaendesha ulimwengu huu, na uzuri ule ambao tunauona popote pale macho yetu yatakapoelekea yanaonyesha kuwa kuna muumba muweza, mtambuzi ameanzisha huu ulimwengu.

Maiko: Lakini hapa linajitokeza swali pamoja na kutilia kwangu nguvu malengo yake nayo ni: Ni ipi haja yetu kwenye dini na kumuamini Mungu? Watu wengi wanaishi maisha yao bila ya kuamini kwao Mungu na bila ya wao kuwa na dini wanayoifuata.

Rashidi: Masomo ya Anthropolojia (elimu kuhusu mwanadamu) na elimu kuhusu dini yameunga mkono kuwa haja ya dini ipo kwa watu wote na zama zote na katika jamii zote, mwanadamu tokea hapo zama za kale alikuwa akitafuta Mungu anayeweza kumuabudu na kujikurubisha kwake, akiamini kuwa ni mwenye nguvu na mwenye kutawala ulimwengu, muumba wa kila kitu yu hai wala hafi.

Hakika maumbile ya mwanadamu yanashuhudia kuwa kila mwanadamu anapopata dhiki yoyote au anapotishwa na hatari au matarajio yake yakakaribia kupotea wakati huo mwanadamu huyo ana haja ya kibaolojia inayomsukuma kwenye kumuamini Mungu.

Kama ambavyo bila imani hii mwanadamu aghalabu anakuwa mnyama anayetawaliwa na matamanio wala hayarejeshwi na dhamira yake.

Rajev: Niruhusu ustaadh Rashidi, nimeishi katika nchi yenye dini nyingi mno, na nikahamia Ulaya na kufahamu dini zingine na wenye dini hizo, nimekuta kuwa, kila mwenye dini anatofautiana na mwingine katika taswira yao kuhusu Mungu, vipi tunaweza kutafsiri tofauti hii? Na vipi nitajua sifa anazosifika nazo mungu wa haki? Vivyo hivyo: Vipi nitajua dini ya haki dhidi ya nyinginezo?

Rashidi: Namuona mhudumu akija na chakula, na ninawaahidi kuyajadili masuala haya katika mijadala ijayo, lakini kwanza hebu tuafikiane katika kauli ya mwanafizikia Albert Einstein;

“Elimu bila dini ni kiguru, na dini bila ya elimu ni upofu.”