HAJA YA JAMII MBALI MBALI KWA DINI

HAJA YA DINI KWA JAMII MBALI MBALI

Haja ya dini kwa jamii mbali mbali

Jamii ina haja ya kiasi gani na dini?

$Ernest_Renan.jpg*

Ernest Renan

Mwanahistoria wa Kifaransa
Hoja yenye kuzungumza
“Kwa hakika kuna uwezekano wa kudhoofika kila kitu tunachokipenda, na kubatilisha uhuru wa matumizi ya akili, elimu, na viwanda, lakini ni muhali kufutika dini, bali itabakia kuwa ni hoja yenye kuzungumza dhidi ya ubatili wa madhehebu ya kiyakinifu (yanayotanguliza dunia na anasa zake) ambayo yanataka kumdhibiti mwanadamu katika dhiki ya uduni katika maisha ya ardhini.”

Ikiwa mtu binafsi hana budi awe na dini, basi haja ya jamii mbali mbali kwenye dini ni kubwa zaidi, Dini ni ngao yenye kuikinga jamii; na hiyo ni kwa sababu maisha ya mwanadamu hayasimami isipokuwa kwa kushirikiana na watu wake katika mambo ya kheri: “…Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui...” (5:2),

$felip-hata.jpg*

Philip Hitti

Mwanahistoria wa Kilebanoni
Sheria ya kweli
“Sheria ya Kiislamu haitofautishi baina ya dini na baina ya ambacho ni dunia. Sheria hiyo inaonesha mahusiano ya mwanadamu na Mwenyezi Mungu na wajibu wake kwa Mungu na kuyapanga kama inavyofanya kwa hali ya mahusiano ya mtu kwa ndugu yake mwanadamu. Na amri zote za Allah na makatazo yake –katika yanayofungamana na mambo ya dini na dunia na mengine kwenye Qur-aan na ndani yake pana ayah elfu sita au ziada ya hapo, miongoni mwa hizo ayah elfu ni kuhusu sheria.”

Na ushirikiano huu hautimii ila kwa mfumo unaopangilia mahusiano yake, na kuainisha majukumu yake na kudhamini haki zao, mfumo huu hauna budi kutoka kwa yule mpole mwenye ujuzi na elimu kwa anayohitajia mwanadamu, “Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” (67:14)

Kila ambapo mwanadamu anapokwenda kinyume na dini, sheria yake na mfumo wake ndipo jinsi ambapo hupotea na kughibu na kudumbukia katika kiza cha shaka, upotevu, haya, taabu na mateso.

Athari ya nguvu ya dini na mshikamano wa jamii na utulivu wake

$Thomas_Arnold.jpg*

Thomas Arnold

Mustashrik (mtaalamu wa mambo ya nchi za mashariki) wa Kiingereza
Dini haina nafasi ya matamanio
“Tunaona katika sababu ya mapokezi ya kushangaza aliyokutana nayo Muhammad huko Madina, ni kuwa kuingia katika Uislamu kwa watu wa Madina ulianza kwa tabaka la viongozi na lengo ilikuwa ni kutibu fujo ile ambayo ilikumba jamii ya Madina na ikiteseka nayo. Sababu kubwa ni kile walichokipata ndani ya Uislamu, ambayo ni kuwepo kwa nidhamu madhubuti chini ya sheria zilizopangwa. Na matamanio ya watu kuwa chini ya utawala wa kisheria ambao umejitenga na matamanio yao.”

Hakuna katika ardhi yote hii nguvu ambayo ni sawa na nguvu ya dini au mtu kufuata dini katika kudhamini watu kuheshimu mfumo au utaratibu Fulani, na kadhalika kudhamini mshikamano wa jamii na utulivu kwa mfumo wake na sababu zote za usalama na siri katika hilo ni kuwa mwanadamu anatofautiana na viumbe vingine kwa kuwa harakati zake na matendo yake ya hiari yanayotawalia uongozi wake kitu ambacho hakitokei katika usikizi wake wala uoni wake, bali ni akida ya kiimani ambayo ina adabisha roho na kutakasa kiwili wili chake na kuifanya kuwa ni mwangalizi wa siri yake kama ambavyo inakuwa ni mwangalizi wa dhahiri yake, “Na ukinyanyua sauti kwa kusema...basi hakika Yeye anajua siri na duni kuliko siri.” (20:7).

Mwanadamu huongozwa na akida iwe ni sahihi au mbovu, akida yake ikitengemaa basi mambo yake yote yatatengemaa, na ikiharibika mambo yake yote yataharibika.

$Floter.jpg*

Voltaire

Mwanafalsafa wa Kifaransa
Ziko wapi akili zenu?!
“Kwa nini mna shaka ya kuwepo kwa Mungu?! Na lau si yeye basi mke wangu angenisaliti, na mtumishi wangu angeniibia.”

Kwa ajili hiyo dini ndio ikawa dhamana bora zaidi ya kusimamisha miamala baina ya watu katika misingi ya uadilifu na usawa, na hilo likawa ni jambo ambalo halina budi katika jamii, wala hatutokuwa tumekosea tukisema kuwa dini itachukua nafasi ya moyo katika kiwiliwili cha Umma mbali mbali.

Ikiwa dini kwa ujumla inachukua nafasi hii, na leo hii mtu akiangalia ataona dini nyingine na mila mbali mbali ulimwenguni, na kila jamii yenye dini fulani hufurahishwa nayo na hukamatana nayo. Kama hali ndivyo hivyo ilivyo ni dini gani basi ambayo ndio sahihi na ambayo itamthibitishia na kumkamilishia nafsi ya mwanadamu anachotaka kukifikia?! Na ni nini vidhibiti vya dini ya haki?!